Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

    Report Post
    Page 4 of 10 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 191
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,506
      Rep Power : 46711
      Likes Received
      16373
      Likes Given
      8453

      Default Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema "Wazanzibari hatuutaki Muungano" na wakati mwingine kudai "Wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki Muungano.

      Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano. Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa bara au serikali ya Muungano.

      Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya katiba ya Zanzibar. Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba Yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.

      Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la? Kwa vile hoja ya kupinga MUungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.

      Swali liwe rahisi tu:

      Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania?

      a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014
      b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa ifikapo Julai 1, 2014

      Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie" manake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014

      Na ikisemwa Hapana isibakie manae ni kuwa mazungumzo ya kuvunja Muungano yataanza na ifikapo Julai 1, 2014 Zanzibar itajitoa kwenye Muungano.

      Wazanzibar waandae kura hiyo ya maoni wao wenyewe kama walivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya Katiba na lolote watakaloamua Tanzania Bara WATAHESHIMU uamuzi huo.

      Ni rahisi sana kumaliza hoja ya Muungano au kutokuwepo Muungano. Yote YAMO MIKONONI MWA WAZANZIBARI. Hawahitaji kutuambia hawautaki Muungano, hatuhitaji watuambie tunawakandamiza kama wanataka kutoka kweli na siyo mikwara mbuzi njia nyeupeeeee!!! Andikeni sheria, itisheni kura ya maoni, pigeni kuchagua 'b' and then mambo yatakua yameiva ifikapo 2014 tutawasaidia kufunga mizigo.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    2. FemaTV & Radio

    3. #61
      mawazotu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th April 2010
      Posts : 57
      Rep Power : 472
      Likes Received
      4
      Likes Given
      10

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      two years ago nilikua naongea na mzee mmoja kuhusu kero za muungano , akanipa mtihani nimtajie faida kumi za muungano trust me i took me ages kufikisha ata tano . kuna umuhimu wa kuuangalia huu muungano upya . wote wazanzibari na wabara

    4. #62
      nderingosha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th March 2011
      Posts : 817
      Rep Power : 1448
      Likes Received
      440
      Likes Given
      119

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By kombo1
      Nyinyi Watanganyika ndio msioruhusu kuitishwa kwa kura hiyo kwani huyu Raisi wenu Kikwete hata anapinga Muungano usijadiliwe katika katiba hiyo mpya. Vingine hawa viongozi wetu wa Zanzibar wote wanaogopa kuitisha kura hiyo ya maoni kwani wote ni vibaraka wa vyama vyao ambavyo vyote viko mikononi kwa Watanganyika. Usidanganyike kura hile ya maoni ilifanyika kwa ruhusa ya CCM na mataifa makubwa ya nje waliotaka Zanzibar kuwe na usalama. Hapo awali Rais Aboud Jumbe alipoonesha tuu kwamba anataka kuwe na serikali tatu, mara moja aliitwa Dodoma na kufukuzwa kazi. Zanzibar tunataka uhuru wetu na hii katiba mpya tutaikubali iwapo muungano utakuwa kama hule wa mfumo wa nchi za ulaya magharibi vinginevyo sote wazanzibari tutaukataa mpaka milele. Angalia watu waliojitokeza kupinga muungano, wengi wao ni vijana hii inaonyesha tatizo hili litaendelea kwa muda mrefu sana mpaka zanzibar iwe huru.
      mi naona nyie wazanzibari mkikomaa (kwa amani lakini)mtaweza kuwashinikiza watawala wakakubali hoja yenu...itasaidia mengi...nyie muwe na zanzibar yenu nasi tuwe na Tanganyika yetu...sasa sijui mtakuwa na zenj ya namna gani...maana nasikia hata wapemba nao unguja hawatakiwi...anyway..i think its time for you guys to re-claim your zanzibar...and for us to have back our long lost Tanganyika. Nachoshindwa kuelewa kila siku ni kwanini watawala wa nchi hii wanakuwa so hesitant kuruhusu mijadala ya muungano???...maana hili nalo linachangia matatizo haya....Hainiingii akilini..kwani ni watawala hawa hawa ambao wamewahi kushiriki kuvunja mambo ya msingi kama azimio la arusha etc.....
      Mzee Mwanakijiji likes this.
      ....real change begins with PEOPLE.......

    5. #63
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,145
      Rep Power : 41574
      Likes Received
      6044
      Likes Given
      1056

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By kombo1
      Nyinyi Watanganyika ndio msioruhusu kuitishwa kwa kura hiyo kwani huyu Raisi wenu Kikwete hata anapinga Muungano usijadiliwe katika katiba hiyo mpya. Vingine hawa viongozi wetu wa Zanzibar wote wanaogopa kuitisha kura hiyo ya maoni kwani wote ni vibaraka wa vyama vyao ambavyo vyote viko mikononi kwa Watanganyika. Usidanganyike kura hile ya maoni ilifanyika kwa ruhusa ya CCM na mataifa makubwa ya nje waliotaka Zanzibar kuwe na usalama. Hapo awali Rais Aboud Jumbe alipoonesha tuu kwamba anataka kuwe na serikali tatu, mara moja aliitwa Dodoma na kufukuzwa kazi. Zanzibar tunataka uhuru wetu na hii katiba mpya tutaikubali iwapo muungano utakuwa kama hule wa mfumo wa nchi za ulaya magharibi vinginevyo sote wazanzibari tutaukataa mpaka milele. Angalia watu waliojitokeza kupinga muungano, wengi wao ni vijana hii inaonyesha tatizo hili litaendelea kwa muda mrefu sana mpaka zanzibar iwe huru.
      Kama viongozi wa Zanzibar wote ni vibaraka wa Watanganyika, na Rais Kikwete Mtanganyika anakataa uhuru wa majadiliano kuhusu muungano, kwa nini unafikiri mfumo wa muungano wa Ulaya Magharibi utaleta mabadiliko yoyote? Kwa nini unafikiri kwamba Zanzibar haitamezwa na kuburuzwa na Tanganyika?

      Kwa nini usitake Zanzibar ijitoe kabisa kwenye muungano na kujiendea zake kama nchi huru ili kusiwe na utata wowote kuhusu ubeberu wa Watanganyika?
      Mzee Mwanakijiji likes this.
      Allow others to say their say, but always say your piece, it's only right.

    6. #64
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,429
      Rep Power : 2885
      Likes Received
      4784
      Likes Given
      2852

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Kiranga
      Kama viongozi wa Zanzibar wote ni vibaraka wa Watanganyika, na Rais Kikwete Mtanganyika anakataa uhuru wa majadiliano kuhusu muungano, kwa nini unafikiri mfumo wa muungano wa Ulaya Magharibi utaleta mabadiliko yoyote? Kwa nini unafikiri kwamba Zanzibar haitamezwa na kuburuzwa na Tanganyika?

      Kwa nini usitake Zanzibar ijitoe kabisa kwenye muungano na kujiendea zake kama nchi huru ili kusiwe na utata wowote kuhusu ubeberu wa Watanganyika?
      Kiranga hicho ndicho kitu kinawasumbua sana Wazanzibar.
      Walianza na serikali tatu tukawauliza ihudumiweje?
      Wakaja na mkataba wa muungano, tukawauliza uhusu nini ambacho pande zote zitafaidika?
      Sasa wamekuja na muundo wa ulaya (EU), tunawauliza kwanini muundo huo usiwe wa EAC kila mmoja akiwa kivyake?

      Wanajua nini wanafaidika ndani ya muungano, wanajua nini kitatokea baada ya kuvunja. Hawatamki vunja wanazunguka zunguka. Sisi tunasema, hewala tunawatakia kila la kheri ondokeni ndani ya muungano. Uwezo mnao mnasita nini?

    7. #65
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,506
      Rep Power : 46711
      Likes Received
      16373
      Likes Given
      8453

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Wazanzibar itabidi tuwape ultimatum ya kuamua kujitoa kwenye Muungano ama sivyo tutawatoa kiaina - pushing for one country, one government...
      Mwalimu, FJM and SnowBall like this.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    8. Miaka 50

    9. #66
      MILKYWAY GALAXY's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 12th December 2008
      Posts : 149
      Rep Power : 569
      Likes Received
      33
      Likes Given
      1

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Wazanzibar itabidi tuwape ultimatum ya kuamua kujitoa kwenye Muungano ama sivyo tutawatoa kiaina - pushing for one country, one government...
      Mzee naona umeniwahi, nilitaka kusema hili hili !

      Nina marafiki na jamaa zangu weengi wenye asili au kutoka ZNZ wako huku bara, hawafikirii kurudi na wala hawajisikii tofauti

      Hizi pirika za nataka sitaki ni kwa wachache wenye kunufaika nazo, wenyewe walaa !

    10. #67
      Negotiator's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 9th August 2010
      Posts : 301
      Rep Power : 510
      Likes Received
      36
      Likes Given
      35

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Gonga gonga humaliza gogo. Haya hima na tumalizie.

    11. #68
      Uswe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 1,783
      Rep Power : 794
      Likes Received
      440
      Likes Given
      437

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      sina cha kuongeza, MODS sticky this!
      mbona sioni umeme, maji wala barabara, 30% PAYE na Kodi nyingine katika bidhaa, zinaenda wapi?

    12. FJM
      #69
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,174
      Rep Power : 2568
      Likes Received
      5323
      Likes Given
      4587

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By nderingosha
      mi naona nyie wazanzibari mkikomaa (kwa amani lakini)mtaweza kuwashinikiza watawala wakakubali hoja yenu...itasaidia mengi...nyie muwe na zanzibar yenu nasi tuwe na Tanganyika yetu...sasa sijui mtakuwa na zenj ya namna gani...maana nasikia hata wapemba nao unguja hawatakiwi...anyway..i think its time for you guys to re-claim your zanzibar...and for us to have back our long lost Tanganyika. Nachoshindwa kuelewa kila siku ni kwanini watawala wa nchi hii wanakuwa so hesitant kuruhusu mijadala ya muungano???...maana hili nalo linachangia matatizo haya....Hainiingii akilini..kwani ni watawala hawa hawa ambao wamewahi kushiriki kuvunja mambo ya msingi kama azimio la arusha etc.....

      nderingosha, kitu ambacho bado hakijawa very clear ni Zanzibar wanataka kujitenga kabisa and have nothing to do with Tanganyika, au wanataka uwepo wa serikali ya Tanganyika na hivyo kufanya muungano uwe wa serikali tatu?

      Kwangu mimi, option ya serikali tatu upo uwezekano mkubwa sana wa mzigo mzito ukabakia kwa 'mnyamwezi' - Tanganyika. Hata ilivyo sasa Tanganyika ndio wanabeba mzito zaidi ya Zanzibar.

    13. #70
      Rohombaya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2011
      Posts : 346
      Rep Power : 468
      Likes Received
      52
      Likes Given
      40

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Kiranga
      Kwa nini unafikiri swala la muungano na Zanzibar linatakiwa kupigiwa kura na Wazanzibari tu?

      Hufikiri kwamba kuna uwezekanao Wazanzibari wengi wakasema wanataka kuwa katika muungano, ila watu wa bara wakawa hawataki muungano?

      Ili kura ya maoni iwe na maana, inafaa ipigwe nchi nzima. Usichukulie for granted kwamba wabara wanautaka muungano.

      Unaweza kumaliza kura ya maoni Zanzibar bila ya kuwashirikisha watu wa bara, ukapata kura za kukubali muungano nyingi sana, only to find out kuna malalamiko kutoka kwa watu wa bara kwamba hawakushirikishwa.
      Kwahili hata mimi nakuunga mkono, Inaonekana kama Muungano huu ni tatizo kwa wazanzibari tuu wabara hawana tatizo nao kwa sababu hiii nadhani inawezekana labda kweli wazanzibari wanaonewa ndani ya muungano
      Lakum diinukum waliyadiin!!!!

    14. #71
      MrFroasty's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd June 2009
      Posts : 544
      Rep Power : 613
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Mwanakijiji,

      Naona uzee umeanza kukurubia kwa kasi, kwani madai ya wazanzibari na hio kura ya maoni si kila siku wanapigwa mabomu wakienda pale barazani ?

      Hivyo uamsho is the only way out, karibu tutaanza na kuchinja wamasai wote kule Nungwi....Nyie mnaweza pia fanya kama hivyo, kwa kuanzia na Mwinyi, Jumbe, Mapuri n.k.

      Wasalaam,
      mrfroasty
      MZALENDO.NET-Zanzibar na Zama za ukweli na uwazi...

    15. #72
      Dawa ya Mjinga's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 12th June 2009
      Location : Magubike
      Posts : 160
      Rep Power : 538
      Likes Received
      34
      Likes Given
      76

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By KIDUNDULIMA
      Mwanakijiji kwa idadi ya watu umepotosha kidogo. Kama Zanzibar inawatu 1.5 million wenye haki ya kupiga kura ni wangapi? unataka kuniambia kuwa wote hao 1.5 million ni wapiga kura? Kama sio wote wapiga kura, sahihi za watu 500,000 ni asilimia ngapi ya wapiga kura wote. Na ukishapata % ndipo utuambia kuwa ni wachache au ni wengi
      Mkuu majibu yako yanazua maswali mengine. Kwanza kuna uhakika gani kuwa hao watu laki tano waliotia saini zao ni watu tofauti au ni saini laki tano za watu fulani? Pili, haijaelezwa umri wa watia saini hao na hivyo kulinganisha na idadi halali ya wapiga kura itakuwa vigumu kweli.
      Zaidi ningependa kugusia suala (ambalo kwa maoni yangu limepitwa na wakati) la kuwa na serikali tatu. Za nini? Zitasaidia nini Muungano? Upendwe Zanzibar na ukipendwa ili iwe nini? Ni gharama ambazo siamini kama Zanzibar au Tanganyika itakuwa tayari kuzibeba (kwa uchumi upi?). Kwa Tanganyika ni bora fedha hizi zikatumiwa kupunguza umasikini uliokithiri nchini badala ya kuendelea kupoteza rasilimali kwa mradi ambao umeshindSasa hivi (Waziri mkuu alisema Bungeni kuwa) Tanganyika ndiyo inayobeba gharama zote za kuendesha serikali ya Muungano (pamoja na kulipia gharma za umeme). Ikumbukwe kuwa fedha hizi ni pamoja na zile za gesi na madini (halafu Wazanzibar wanasema hawanufaiki na Fedha za madini - ajabu). Sasa ni sababu ipi ambayo itaifanya Tanganyika iendelee kugharimia Zanzibar katika muundo huo mpya? Wao wanataka usawa (equal partnership), sawa, lakini ilishasemwa wakati uliopita kuwa haki bila wajibu si haki! Waeleze ni wajibu gani ambao hawautekelezi sasa ambao watakuwa tayari kuubeba sio kudai upande mmoja tu wa shilingi. Shilingi halali ina pande mbili tofauti - haki na wajibu. Hii shilingi yenye upande mmoja tu wa haki (bila wajibu) - ni feki.
      Kweli jamaa wamedhamiria kuuvunja Muungano - acha uvunjike, maana hakuna atakayekubali kubeba mzigo wao katika mfumo wanaoulazimisha. Kwa vyovyote vile Muungano huu unavunjika - dawa ni kuharakisha kabla hawajabadili mawazo. Tukubali tu ukweli kwamba duniani si vitu vyote vinawezekana wakati wote. Tumeshakuwa na mradi huu wa Muungano kwa miaka 50 inatosha na kwa wapenzi wa historia wanaweza kuandika vitabu kwa kumbukumbu. Tufungue ukurasa mpya. Uvunjwe kwa amani ili ushirikiano uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar uendelee kama nchi jirani. Hakuna sababu ya kuweka uadui - kisa Muungano. Mbona majirani wengine tunahusiana vema na hatuna muungano nao?
      SnowBall likes this.

    16. #73
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,429
      Rep Power : 2885
      Likes Received
      4784
      Likes Given
      2852

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Rohombaya
      Kwahili hata mimi nakuunga mkono, Inaonekana kama Muungano huu ni tatizo kwa wazanzibari tuu wabara hawana tatizo nao kwa sababu hiii nadhani inawezekana labda kweli wazanzibari wanaonewa ndani ya muungano
      Ni kwa malalamiko hayo ndiyo maana tumewafungulia 'vitabu' vya kujikomboa

      Chapata 1:
      1:Wana Rais wa Zanzibar
      2: Makamu wawili wa Rais
      3; Baraza la mawaziri
      4: Baraza la wawakilishi lenye uwezo wa kutengua hata mambo ya muungano
      5: Bank ya Zanzibar
      6: Idara ya mapato ZRA
      7: Chama chao cha michezo ikiwemo Soka
      8: Baraza lao la mitihani
      9: Wizara ya elimu, kilimo, afya, ardhi, maliasili na utalii
      10: Wimbo wa Taifa
      11: Bendera ya taifa
      12:Mufti

      Chapta 2:
      1.Baraza la Wawakilishi lifanye yafuatayo
      a) Kupitisha azimio la kutomtambua Rais wa JMT
      b)Kumtaka makamu wa Rais aliyepata wadhifa kwa uzanzibar ajiuzulu mapema na arudi nyumbani
      c)BLW limtangaze IGP wa Zanzibar kwa mswada kama ulioondoa cheo cha waziri kiongozi na kukiacha katika katiba JMT
      d) BLW liweke visa kwa Watanganyika kuingia kama lilivyozuia ajira
      e) Kurudisha pesa(currency) iwe Dirham

      2) Wafantakazi wote wa taasisi za umma walioko bara warejeshwa SMZ haraka
      3) Wanafunzi wote warejee kusomea chuo kikuu cha Zanzibar ili kupata maadili ya utamaduni wa Zanzibar

      Haya yanawezekana kwasababu mengi yamefanywa na hakuna athari. Ikiwa yatafanyika katika kikao cha bajeti ni wazi kuwa July 1 2012 kutakuwepo na Zanzibar huru yenye neema.
      FairPlayer likes this.

    17. #74
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,239
      Rep Power : 31388
      Likes Received
      9613
      Likes Given
      683

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Hivi vijitu nishavichoka mimi.
      Mwalimu likes this.
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    18. #75
      Mtu wa Pwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2006
      Posts : 4,250
      Rep Power : 1491
      Likes Received
      159
      Likes Given
      147

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By nyani ngabu
      hivi vijitu nishavichoka mimi.
      hata bado unalo hili
      Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

    19. #76
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,239
      Rep Power : 31388
      Likes Received
      9613
      Likes Given
      683

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Mtu wa Pwani
      hata bado unalo hili
      Vimejazana Gerezani na kila pembe ya Dar vinafanya biashara pasipo bugudha. It's gonna get ugly.
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    20. #77
      Mtu wa Pwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2006
      Posts : 4,250
      Rep Power : 1491
      Likes Received
      159
      Likes Given
      147

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Nyani Ngabu
      Vimejazana Gerezani na kila pembe ya Dar vinafanya biashara pasipo bugudha. It's gonna get ugly.
      mbona wachina wamejazana pia? au mumeungana nao ? acha chuki babu zitakuuua. saidia tupate zanzibar yetu watarudi hao na watakuachieni nchi yenu
      Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

    21. #78
      Mtu wa Pwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2006
      Posts : 4,250
      Rep Power : 1491
      Likes Received
      159
      Likes Given
      147

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By MILKYWAY GALAXY
      Mzee naona umeniwahi, nilitaka kusema hili hili !

      Nina marafiki na jamaa zangu weengi wenye asili au kutoka ZNZ wako huku bara, hawafikirii kurudi na wala hawajisikii tofauti

      Hizi pirika za nataka sitaki ni kwa wachache wenye kunufaika nazo, wenyewe walaa !

      mbona na kule wako watanganyika hawana mawazo kabisa ya kurudi tanganyika hata ukivunjika muungano. suali si kutishana wazanzibari wameweka hoja zao mezani na wanataka nchi yao

      watanganyika walikuwepo zanzibar kabla ya muungano na wako wazanzibari walikuwepo tanganyika kabla ya muungano. na hata ukivunjika wako wataaamua kubakia walipo na hilo sio tatizo kabisa

      tusimiminiwe chuki za bure cha msingi zanzibar hawataki tena muungano na ni haki yao waachiwe wapumuwe
      Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

    22. #79
      Nyani Ngabu's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 15th May 2006
      Location : Ikungulyabashashi
      Posts : 39,239
      Rep Power : 31388
      Likes Received
      9613
      Likes Given
      683

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Mtu wa Pwani
      mbona wachina wamejazana pia? au mumeungana nao ? acha chuki babu zitakuuua. saidia tupate zanzibar yetu watarudi hao na watakuachieni nchi yenu
      Wachina wanaleta vurugu na kuchoma nyumba za ibada na mali za watu? Au na sisi Wabara tuanze kuwapiga, kuwaua, na kuwachomea Wazanzibari mali zao?
      Miafrika Ndivyo Tulivyo.

    23. #80
      Mtu wa Pwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2006
      Posts : 4,250
      Rep Power : 1491
      Likes Received
      159
      Likes Given
      147

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Nyani Ngabu
      Wachina wanaleta vurugu na kuchoma nyumba za ibada na mali za watu? Au na sisi Wabara tuanze kuwapiga, kuwaua, na kuwachomea Wazanzibari mali zao?
      ndugu yangu ngabu mm na ww ni marafiki hapa tokea 2006, ni wanaforum wa muda mrefu na kwa hakika bado nnaamini ni muelewa wa kutosha kaka yangu.

      kuchomwa makanisa bado hujaona kuwa ni janja wa usalama wa Taifa kutaka kubadilisha motion ya mjadala ?

      zanzibar uamsho wamefanya mikutano zaidi ya mia unguja na pemba na hakujachomwa kanisa hata moja, hujiulizi jeee iweje juzi baada ya kukamatwa sheikh wao kihuni ?

      kama ww swahiba wangu na mkomavu wa siasa kitendo cha polisi kumkamata sheikh mbele ya wafuasi wake kama muhuni pasipo kufata sheria ww uliliona liko sawa ?

      nnaomba uwe mtu wa haki na kusukumwa na justice kuliko chuki, wazanzibar waliungana na tanganyika kama nchi na sasa wanaidai nchi yao kuanzia serikali yao na wananchi kwa ujumla na nnamini unajua hilo

      NNAKUOMBA TENA SIMAMA KWENYE HAKI TUSAIDIE ILI HAKI ITENDEKE, MAKANISA SS HATUNA MATATIZO NAYO TUNAYO MDA MREFU KULIKO HATA TANGANYIKA. NA HATA RAIS WETU KAZUNGUMZA HILO
      Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

    Page 4 of 10 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...