Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

    Report Post
    Page 26 of 27 FirstFirst ... 1624252627 LastLast
    Results 501 to 520 of 537
    1. #1
      kilewo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th February 2010
      Posts : 514
      Rep Power : 578
      Likes Received
      622
      Likes Given
      40

      Default Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      IKULU ILIINGILIA KESI YA UCHAGUZI. – GODBLESS LEMA.

      Ndugu Wananchi;

      Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo . ( J.K . KIKWETE.)

      “Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge”.

      Mh Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha .

      Mh Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa dhidi ya haki , utu na ukweli.

      Mh Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni "Afadhali Vita Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu" umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama chako. Hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi ya kebehi na hadaa, Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea Zanzibar, mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .

      Mh Rais, Mama Theresa, Nelson Mandela, Martin Luther Jr na Malcom X hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao. Sihitaji Ubunge kupigania ukweli, haki na utu, nahitaji dhamira safi, nia njema na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini, nitakapomaliza mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini nilifanya. Ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta, magorofa, magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki, Usawa na utu vikiwa kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo. Pengine sitaishi miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi, Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe, hata hivyo siogopi kufa kwani nisipokufa kesho, nitakufa siku moja ambayo siijui, napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama itawezekana, lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora ishindakane kwa kuthamini haki. Kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana, unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako, niko tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu watu wa Arusha Mbunge wao.

      Mh Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli katika Jimbo langu na Nchi yangu.

      Mh Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na haki na ukweli .

      Mh Rais “Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri” Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .

      ONLY TIME WILL TELL”.

      GODBLESS .J. LEMA.

    2. Miaka 50

    3. #501
      matawi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th March 2010
      Posts : 1,464
      Rep Power : 757
      Likes Received
      125
      Likes Given
      67

      Default

      Quote By TIMING
      Lema may not be the best politician, but surely is one of the best man for Arusha and M4C team

      It seems They wanted Lema to be their man, and he has slipped out of their system
      Kama ni kweli Lema alifanya mkutano na Kikwete na hakukubaliana naye sasa nimefunguka!!!! Kuuumbeee. Kama babu seya kafungwa maisha yule godbless sijui itakuwaje

    4. #502
      Shine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2011
      Posts : 9,197
      Rep Power : 2431
      Likes Received
      948
      Likes Given
      378

      Default

      Quote By Rejao
      Jamani CDM msaidieni huyu mtu wenu. Naona kama hayuko sawa!
      Mtu kusema ukweli hayuko sawa!?

    5. #503
      Shine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2011
      Posts : 9,197
      Rep Power : 2431
      Likes Received
      948
      Likes Given
      378

      Default

      Quote By DALLAI LAMA
      Lema napenda unavyojiamini
      Ndiyo dhamira ya kuvaa gwanda

    6. #504
      Shine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2011
      Posts : 9,197
      Rep Power : 2431
      Likes Received
      948
      Likes Given
      378

      Default

      Quote By Bajabiri
      Dah,,,,hahahahahha..........na baki naasama mdomo tu hapa....wanasiasa bhana,,,,,,leo yote yapo wazi,,,kumbe mlikaa Oysterbay?????shabassssh...... ..
      ukiona hivyo walimtangazia dau ili awaachie ccm jimbo akakataa!

    7. #505
      Jackbauer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : CTU
      Posts : 4,876
      Rep Power : 1692
      Likes Received
      1348
      Likes Given
      277

      Default

      Quote By Kasheshe
      Hahahaha Jackbauer, naomba nimalize mjadala wangu na wewe kusema yafuatayo... yupo kiongozi ninayemkubali sana ambaye viongozi wengi duniani wawe in politics are in corporate wana-mu-admire... naye si mwingine lakini ni yule ambaye hakuwa popular.... a.k.a kwenye kundi ya (normal distribution curve) si mwingine bali na Rais mstaafu wa Marekani anaitwa Abraham Lincolin... Mandela mwenyewe anasema al-mu-admire sana mpaka akawa anafuata alivyokuwa anaongoza... this guy was among un-popular presidents of U.S. Soma biography yake utajifunza mengi.... Asante na nakupenda na nakutakia baraka tele na ufahamu wa mengi... please do not caught up by these cheap politics... taking advantage of ignorance population if not community.

      For those future leaders jifunzeni kusoma ya Abraham Lincolin kuna mengi ya kujifunza kutoka kwake....
      sijasoma sana juu ya lincolin lakini ninachojua kuwa he was humble!
      Kasheshe likes this.

    8. RukaaJuu Final

    9. #506
      mhalisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2011
      Posts : 565
      Rep Power : 601
      Likes Received
      140
      Likes Given
      121

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By matawi
      Kama ni kweli Lema alifanya mkutano na Kikwete na hakukubaliana naye sasa nimefunguka!!!! Kuuumbeee. Kama babu seya kafungwa maisha yule godbless sijui itakuwaje
      ilisemwa sana kwamba Bwana mkubwa alihusika kwenye hukumu ya Babu Seya na wanawe.

    10. #507
      GABE100's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th March 2012
      Posts : 50
      Rep Power : 371
      Likes Received
      2
      Likes Given
      2

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      lema unakosea unapomwita kikwete mheshimiwa.

    11. #508
      Baba V's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2010
      Location : Buguruni Mnyamani
      Posts : 10,962
      Rep Power : 30234
      Likes Received
      4725
      Likes Given
      3477

      Default

      Quote By mhalisi
      ilisemwa sana kwamba Bwana mkubwa alihusika kwenye hukumu ya Babu Seya na wanawe.
      Inji hii bana!

    12. #509
      sir.JAPHET's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th May 2012
      Posts : 609
      Rep Power : 475
      Likes Received
      90
      Likes Given
      45

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      mungu yuko upande wetu wapenda haki, lema usjal lazima tushinde hii vita..

    13. #510
      Mwanamayu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th May 2010
      Location : Manzese
      Posts : 3,049
      Rep Power : 1069
      Likes Received
      240
      Likes Given
      112

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By kilewo
      IKULU ILIINGILIA KESI YA UCHAGUZI. – GODBLESS LEMA.

      Ndugu Wananchi;

      Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo . ( J.K . KIKWETE.)

      “Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge”.

      Mh Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha .

      Mh Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa dhidi ya haki , utu na ukweli.

      Mh Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni "Afadhali Vita Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu" umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama chako. Hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi ya kebehi na hadaa, Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea Zanzibar, mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .

      Mh Rais, Mama Theresa, Nelson Mandela, Martin Luther Jr na Malcom X hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao. Sihitaji Ubunge kupigania ukweli, haki na utu, nahitaji dhamira safi, nia njema na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini, nitakapomaliza mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini nilifanya. Ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta, magorofa, magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki, Usawa na utu vikiwa kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo. Pengine sitaishi miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi, Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe, hata hivyo siogopi kufa kwani nisipokufa kesho, nitakufa siku moja ambayo siijui, napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama itawezekana, lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora ishindakane kwa kuthamini haki. Kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana, unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako, niko tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu watu wa Arusha Mbunge wao.

      Mh Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli katika Jimbo langu na Nchi yangu.

      Mh Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na haki na ukweli .

      Mh Rais “Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri” Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .

      ONLY TIME WILL TELL”.

      GODBLESS .J. LEMA.

      Ingekuwa busara aidha kukaa kimya au kuwataarifu wananchi pale ulipokutana na JK Oysterbay. Na ulitakiwa kukutana na JK ukiwa na baadhi ya viongozi wa CDM without his notice. This is hypocrisy; you are now behaving like Maige!

    14. #511
      Pendael laizer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2012
      Posts : 945
      Rep Power : 561
      Likes Received
      90
      Likes Given
      5

      Default

      Quote By mhalisi
      ilisemwa sana kwamba Bwana mkubwa alihusika kwenye hukumu ya Babu Seya na wanawe.
      Kwa sababu gani?je hiyo ni haki?ipo siku nayeye atakuwa hukohuko maana malipo ni hapahapa.

    15. #512
      Mnama's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th October 2010
      Posts : 737
      Rep Power : 1163
      Likes Received
      174
      Likes Given
      108

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By Rejao
      Jamani CDM msaidieni huyu mtu wenu. Naona kama hayuko sawa!
      kweli we gamba gumu haswa.

    16. #513
      ThinkPad's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2008
      Posts : 1,449
      Rep Power : 857
      Likes Received
      89
      Likes Given
      83

      Default

      Eeeeh nilikuwa sijaona hii kitu.

    17. #514
      Maganiko's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 20th February 2011
      Posts : 131
      Rep Power : 444
      Likes Received
      58
      Likes Given
      986

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By Kasheshe
      Siku zote ukiona hoja zako zinakubalika sana na watu wengi wakawaida... ask yourself whats wrong...!!!!
      Kasheshe,

      You of all the people inakuja na hoja dhaifu namna hii? watu wengi wa kawaida ni kina nani? JK anaongoza watu gani? Tu-assume kuwa hivi ndivyo hoja yako ilivyo, historia ina mifano mingi tu jinsi ambavyo watu wengi wa kawaida walivyoleta mapinduzi ya kimfumo ndani ya jamii. Ni watu wa kawaida tu waliokuwa wakida mkate ambao ndio walisababisha au kuleta mapinduzi ya Ufaransa, kwa mfano rahisi tu.

      Ni kweli watu wengi wa kawaida wanahitaji uwakilishi wa viongozi wa kawaida kama Lema ili kubadili mfumo uliopo. Nyie msio wa kawaida, ndo mmetufikisha hapa tulipo, the likes of you, Rwekaza Mukandala, Ben Bana etc, kwa kupika na kuandaa takwimu za ujanja ujanja tu kuhusu watawala kwa malengo yenu.

      Kasheshe, jua limeshachanua na watu wengi wa kawaida wanazidi kuuona mwanga, sisi watu wengi wa kawaida tunahitaji viongozi wa kawaida kuleta mabadiliko ya kimfumo na kiutawala katika maisha yetu, as simple as that, period!
      Kasheshe likes this.

    18. #515
      Maganiko's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 20th February 2011
      Posts : 131
      Rep Power : 444
      Likes Received
      58
      Likes Given
      986

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By Kasheshe
      Hahahaha Jackbauer, naomba nimalize mjadala wangu na wewe kusema yafuatayo... yupo kiongozi ninayemkubali sana ambaye viongozi wengi duniani wawe in politics are in corporate wana-mu-admire... naye si mwingine lakini ni yule ambaye hakuwa popular.... a.k.a kwenye kundi ya (normal distribution curve) si mwingine bali na Rais mstaafu wa Marekani anaitwa Abraham Lincolin... Mandela mwenyewe anasema al-mu-admire sana mpaka akawa anafuata alivyokuwa anaongoza... this guy was among un-popular presidents of U.S. Soma biography yake utajifunza mengi.... Asante na nakupenda na nakutakia baraka tele na ufahamu wa mengi... please do not caught up by these cheap politics... taking advantage of ignorance population if not community.

      For those future leaders jifunzeni kusoma ya Abraham Lincolin kuna mengi ya kujifunza kutoka kwake....
      Na JK je? Anamuiga au yuko inspired na nani?
      Kasheshe likes this.

    19. #516
      KABALE's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 91
      Rep Power : 600
      Likes Received
      14
      Likes Given
      4

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By Kasheshe
      The challenge is LEMA is and individual while Rais ni Taasiss... sasa pima mwenyewe!
      Kila mtu anajua LEMA is an individual LAKINI..Hiyo taasisi ambayo unazungumzia isiyo shughulikia mafisadi wa UCHUMI wa mama yetu Tanzania na watu wake iko wapi...ni mbwa mzee aliyengolewa meno. Taasisi ambayo vyombo vyke vinadokoa raslimali za nchi... ni taasisi tena hiyo...

      Yo better keep quite.. ..Lema is one indivudual but behind him there thousand more than him. je hao mtawafanya nini.. this is new generation wake up

    20. #517
      mpenda's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 21st July 2010
      Posts : 172
      Rep Power : 483
      Likes Received
      5
      Likes Given
      100

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By kitila mkumbo
      why? Because he is daring to speak his mind? What lema is saying is what is going on in the minds of millions of tanzanians. The only difference is that lema can dare to speak it in public while many of us can only speak in corridors and in our bed rooms. We should therefore be congratulating and encouraging lema instead of ridiculing him!
      great thinkers dare to talk openly.
      Maganiko likes this.

    21. #518
      kichomiz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 4,053
      Rep Power : 1232
      Likes Received
      652
      Likes Given
      80

      Default

      Quote By raider
      chadema iko na kichaa mingi ngoma ikivumaa sana inapasuka sasa hii ni kama babu wa loliondo
      Akiwemo na baba yako pia.

    22. #519
      IKHOIKHOI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th January 2012
      Location : Bustani ya Eden
      Posts : 345
      Rep Power : 438
      Likes Received
      35
      Likes Given
      34

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Ni ukweli peke yake utamweka Lema huru
      ora et labora

    23. MTK
      #520
      MTK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th April 2012
      Posts : 939
      Rep Power : 4497
      Likes Received
      303
      Likes Given
      333

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By kilewo
      IKULU ILIINGILIA KESI YA UCHAGUZI. – GODBLESS LEMA.

      Ndugu Wananchi;

      Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo . ( J.K . KIKWETE.)

      “Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge”.

      Mh Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha .

      Mh Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa dhidi ya haki , utu na ukweli.

      Mh Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni "Afadhali Vita Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu" umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama chako. Hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi ya kebehi na hadaa, Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea Zanzibar, mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .

      Mh Rais, Mama Theresa, Nelson Mandela, Martin Luther Jr na Malcom X hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao. Sihitaji Ubunge kupigania ukweli, haki na utu, nahitaji dhamira safi, nia njema na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini, nitakapomaliza mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini nilifanya. Ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta, magorofa, magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki, Usawa na utu vikiwa kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo. Pengine sitaishi miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi, Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe, hata hivyo siogopi kufa kwani nisipokufa kesho, nitakufa siku moja ambayo siijui, napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama itawezekana, lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora ishindakane kwa kuthamini haki. Kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana, unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako, niko tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu watu wa Arusha Mbunge wao.

      Mh Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli katika Jimbo langu na Nchi yangu.

      Mh Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na haki na ukweli .

      Mh Rais “Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri” Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .

      ONLY TIME WILL TELL”.

      GODBLESS .J. LEMA.

      RIGHT WILL PREVAIL AGAINST MIGHT; Godbless Lema the voice of the people is a voice of God; and if GOD is with you no one can be against you, stay firm, focused and vigilant, God will see you through.

    Page 26 of 27 FirstFirst ... 1624252627 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...