Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

    Report Post
    Page 12 of 27 FirstFirst ... 2101112131422 ... LastLast
    Results 221 to 240 of 537
    1. #1
      kilewo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th February 2010
      Posts : 514
      Rep Power : 578
      Likes Received
      622
      Likes Given
      40

      Default Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      IKULU ILIINGILIA KESI YA UCHAGUZI. – GODBLESS LEMA.

      Ndugu Wananchi;


      Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo . ( J.K . KIKWETE.)

      “Narudia tena , IKULU iliingilia kesi yangu ya Ubunge”.

      Mh Rais nimekusikiliza kwa makini sana ila nakupa pole kwani bado unafikiri unaongea na Tanzania ya mwaka 1961 , umesema sasa Arusha ni shwari tofauti na miaka miwili iliyopita kwani sasa kuna amani na utulivu wa kutosha ndio maana hata mkutano wa AFDB umefanyika Arusha .

      Mh Rais , najua IKULU iliingilia kesi yangu kama ilivyoonekana na ndio sababu hata Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati anaapisha Wakuu wa Wilaya alimpongeza Jaji kwa hukumu nzuri aliyowafurahisha wakati kesi hiyo iko mahakama ya Rufaa , lakini jambo moja la msingi ambalo huwezi kulitambua kwa sasa ni kuwa Haki na Ukweli haviwezi kushindwa na dhuluma, ubaya wala mamlaka , natambua wewe ni Rais na unayo mamalaka makubwa katika Taifa hili lakini vile vile nataka utambue kuwa huna mamlaka makubwa dhidi ya haki , utu na ukweli.

      Mh Rais hakuna Amani Duniani inayozidi Haki na usawa ,utu na ukweli , haipo na wala haitakuwepo , ndio maana kila siku nasema ni "Afadhali Vita Inayotafuta Haki na usawa kuliko Amani inayopumbaza na kudhalilisha utu wa Mwanadamu" umefurahia sana mkutano uliokupa fursa ya kutoa maneno ya kebehi na kudhihirisha ila chafu iliyofanywa na Serikali yako na kujaribu kuhadaa Umma kama ilivyo kawaida ya Serikali yako na Chama chako. Hata hivyo wakati huu kuna mambo ya msingi yakushughulikia zaidi ya kebehi na hadaa, Uchumi wa Nchi umeyumba, huduma za msingi za jamii zimepuuzwa, Mpasuko katika suala la Muungano na vururugu zinazoendelea Zanzibar, mfumuko wa bei hizi ni sababu chache ambazo haziwezi kuruhusu wakati huu kuwa wakati wa kebehi na mizaha isipokuwa kazi .

      Mh Rais, Mama Theresa, Nelson Mandela, Martin Luther Jr na Malcom X hawakuwa Wabunge kupigania haki za Nchi yao na watu wao. Sihitaji Ubunge kupigania ukweli, haki na utu, nahitaji dhamira safi, nia njema na huu utakuwa wajibu wangu mpaka nakwenda kaburini, nitakapomaliza mbio hizi najua nitapata fursa ya kutazama nyuma yangu nione nini nilifanya. Ukweli nisingependa kuona vituo vya mafuta, magorofa, magari na viwanja vingi kila kona ya Nchi bali Haki, Usawa na utu vikiwa kama nguzo ya imani ya watawala wetu watakaokuwepo. Pengine sitaishi miaka mingi sana kama utachukizwa sana na waraka wangu huu kwani Polisi, Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi wanakutii wewe, hata hivyo siogopi kufa kwani nisipokufa kesho, nitakufa siku moja ambayo siijui, napenda kuishi maisha marefu nimwone mke wa mtoto wangu kama itawezekana, lakini kuliko iwezekane kwa kuishi kwa hofu ni bora ishindakane kwa kuthamini haki. Kwa hiyo kama utakuwa umekasirika sana, unaweza kufanya jambo lolote baya kwa kutumia mamlaka yako, niko tiyari sio kesho wala leo isipokuwa sasa hivi, najua IKULU imewazulumu watu wa Arusha Mbunge wao.

      Mh Rais ninajua wazi njama zote na hasira hizi zinaweza kuwa zimetokana hasa na mkutano tuliokaa Osterbay Dar mimi na wewe kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 hata hivyo sikupuuza maongezi yetu isipokuwa nilichagua kufuata dhamira yangu na wito wangu wa utumishi wa kweli katika Jimbo langu na Nchi yangu.

      Mh Rais nimekuelewa na Wananchi wamekuelewa kila mahali , wewe ni Rais unayo mamlaka makubwa na mimi ni mwananchi mamlaka yangu makubwa ni kwa mke wangu tu , sina Polisi wala Usalama wa Taifa lakini nitawaomba wanyonge wafunge na kusali tuone kama mamlaka yako inaweza kushindana na haki na ukweli .

      Mh Rais “Mtu anaweza kuzini kwa siri lakini hawezi kuugua ukimwi kwa siri” Serikali na Chama cha Mapinduzi kimepuuza watu na haki zao kwa muda mrefu , lakini wakati umefika ambapo hawatapuuzwa tena hata hivyo kwa kauli yako hii naamnini haiwezi kuwafundisha kazi majaji wa mahakama ya rufaa .

      ONLY TIME WILL TELL”.


      GODBLESS .J. LEMA.


    2. FemaTV & Radio

    3. #221
      legendary's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th September 2011
      Posts : 22
      Rep Power : 392
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      Wana JF kwa hili tuongee ukweli.

      Lema sio mwanasiasa wa level ya Tz kwa 7bu ktk maongez yake ukweli umezidi wakat ni waz kabisa siasa zaTz zimejaa uongo mwingi.

      Inauma kuona watu wa muhimu wengine wanawakejeli ingali wakijua kabisa Anachoongea Lema ni ukweli ulitukuka na hawa watu ni wauaji kwa sababu wanafanya kazi ya kuchelewesha haki za watz wote wanaoteseka na kufaa kwa njaa na matatzo mengne kwa serikali mbovu hawa watu ni bora wakajitambua na wakaacha mchezo wao wenye laana kwa maslah yao wenyewe

    4. #222
      Apollnary's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th March 2011
      Posts : 112
      Rep Power : 438
      Likes Received
      27
      Likes Given
      55

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By RockSpider
      Ndugu Wananchi;
      Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa ndugu zetu wa Arusha kwa kuwapokea vizuri na kuwakarimu vyema wageni wetu hao. Nawaomba waendelee na moyo huo mpaka watakapoondoka wote. Naomba kuwepo kwa mkutano huu kuwakumbushe umuhimu wa mji wenu kuwa tulivu. Miaka miwili iliyopita isingekuwa rahisi kwa watu au shirika kubwa la kimataifa kama Benki hii kuamua kufanya mkutano wake Arusha. Isitoshe hata sisi wenyewe tusingeshawishika kuomba au kukubali maombi ya namna hiyo. Lakini sasa imewezekana. Naomba kila mmoja wetu aweke azimio moyoni mwake la kuhakikisha kuwa hali ile haijirudii tena. Nyota ya Geneva ya Afrika lazima iendelee kuangaza. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo . ( J.K . KIKWETE.)

      If you can read btw the line Rais anawaambia watu wa Arusha kuwa Jimbo likiwa upande wa upinzani kamwe mikutano mikubwa ya kimataifa haitafanyika Arusha! Wrong move! wananchi wanahitaji ushawishi zaidi na si vitisho vya kitoto ...Kana kwamba haitoshi, je ni wananchi wangapi wa arusha wanaofaidika na mikutano hiyo? sana sana ni delegates zitokazo Dar ndiyo ambao hufaidi Per Diem zitokanazo na kodi zetu ... ANYWAY wasiwasi wangu uko pale pale kuwa wasaidizi wa Raisi hawamsaidii ama hawafanyi kazi zao inavyotakikana...

      Dah...Yani ninashindwa kabisa kuelewa kama watanzania hivi sasa tunajadili masuala kutokana na jinsi mambo yalivyo,ama kutokana na jinsi "ghadhabu" zetu zinavyotutuma.

      Ninaelewa kwamba Watu wengi Nchini wana ghadhabu za ajabu hasa dhidi ya Uongozi uliopo Madarakani.

      Jambo hilo linapelekea kwamba chochote kitakachosemwa ama kufanywa na Uongozi huo kuonekana ni baya.

      Nimejitahidi kusoma tena na tena jinsi Mheshimiwa Rais alichosema na Lugha aliyoitumia,sioni ni kwa namna gani watu wanaweza kumrukia kama walivyomrukia kwenye respond zinavyoonyesha hapa.

      Sioni mahala ambapo inaonyesha alikuwa akimsema mtu,zaidi ya kuona kwamba anaongelea "general condition" ya Arusha

      Sielewi na sishawishiki kwa nini hasa Lema ameweza ku react kwa namna hiyo kutokana na hiyo hotuba.....Ingawa Ninaweza kuelewa kidogo kwamba yeye ni muhanga mkubwa wa kuvuliwa Ubunge,ambapo ki taalamu yupo kwenye Post traumatic period,ambayo ni stress kubwa....hivyo anaweza kuongea hayo yote kwa sababu tu ana hasira,hivyo anaweza kushindwa kuunganisha vema kinachoongelewa na kuhusisha moja kwa moja na matatizo yake.(sisemi kwamba siamini ama ninaamini kwamba alionewa ana alitendewa haki respectively----yawezekana alionewa,ama alitendewa haki)

      Ninachojua mimi na pia hata nyie ndugu zangu kama kweli mtataka kuchambua kipengele hicho cha hotuba ya Mheshimiwa Rais kwa kutumia mioyo na akili zenu huru (zisizojazwa chuki ama kumshabikia mtu tunayempenda ili kumpa moyo), Lugha aliyoitumia Mheshimiwa rais ni ya Kinyenyekevu sana na yenye wingi wa shukrani kwa wananchi wa arusha kwamba wameweza kufanikisha Mkutano huo kwa kuwa katika hali ya Utulivu.

      Sisi sote hapa tutakubaliana kwamba Events kubwa kama za Michezo ya Kimataifa,Mikutano ya Kimataifa,Utalii wa Nje ni vitu ambavyo huingiza pesa nyingi na kutoa ajira kwa Watu sehemu yeyote ile Duniani,hivyo kila Nchi na serikali hujitahidi sana ku lobby ili waweze kuwa wenyeji wa kuandaa Events kama hizo zinapotokea na wao wakawa Kisheria wana uwezo wa Kuandaa.....Na Mara nyingi Nchi hutakiwa zianze kushindana kuweza kuonyesha kwamba zinaweza kuandaa Events kama hizo....na katika Vigezo vingi vilivyopo,kati ya vingi kinachoweza kuwaangusha kwa mara moja katika kupewa nafasi hizo ni kushindwa kuhakikisha kwamba "Usalama wa Uhakika utakuwepo kwa participants" na wageni wengineo watakaohudhuria mikutano ama event kama hizo...

      Nchi ka Africa ya Kusini,wakati wa kuomba kuandaa Kombe la Dunia lililopita,mnaweza msiamini kwa jinsi walivyopata shida ya kuwa convise wale watu wa Kamati ya FIFA kwamba Nchi yao ni safe kwa ajili ya kuhost Mashindano hayo (ambacho kingewaangusha ni crime rate na fujo za kila siku south africa,Shida yao kubwa ilikuwa about guaranteing safety, licha ya kwamba kwa upande wa mambo mengine walikuwa fit)...Sasa Kiongozi gani atakosa fadhila ya kuwashukuru Watu kutoka kwenye Mji ambao ulikuwa katika pilika pilika za "mshike mshike" wa hapa na pale kila mara katika kipindi kilichopita?

      Nani anayedhani kwamba ile kipindi cha miezi ya february wakati wa vurugu za Arusha kuna Institution ingeweza kukubali ku host mkutano ama event kubwa sehemu kama hiyo?Ama tutoe mfano rahisi,angalieni hii juzi tu hapa mambo ya vurugu za Zanzibar siku 3 tu,tayari Wakenya washatangaza kwamba kwetu Zanzibar sio kuzuri kwa Utalii sio safe....Sasa hebu niambieni ni kwa sababu gani zitatufanya tuchukie ikiwa rais atakuja kuwashukuru Wazanzibar kama mambo yakienda safi huko Zanzibar wakatulia na nchi ikaendelea na shughuli za kawaida ...Nani anayedhani kwamba kuna Kiongozi anayefurahi kuona vurugu zinaendelea sehemu fulani ya Nchi yake?(hapa achana sitaki kuongelea kwamba watulie wakiwa wamepata wanachotaka,who knows wanachotaka ndio right?,who knows na wasiotaka wanachodai hao jamaa ni wengi pia?)

      Just kumbukeni jinsi Rais wa Ivory coast alivyokuwa aki lobby na kuomba Makao makuu ya Benki ya Maendeleo ya Afrika yarudi nchini kwake(kwa sababu yalihamishwa kipindi ivory coast hakuna Usalama----ingawa level ya hatarisho la Usalama wa kule ilikuwa kuna "vita" wakati arusha kulikuwa na "restlessness" ya kisiasa na shughuli za kijamii)

      Ninajua wengi hapa mnaweza kusema kwamba ni bora "vurugu inayotaka kuleta haki kuliko salama inayoonea", hapo siwezi kusema sana,kwa sababu kwangu mimi sakata la Arusha sielewi vema nani hasa ni mkweli kati ya Upinzani na Chama tawala (ninachojua mimi mambo ya Siasa kila Chama kinataka kutawala, hivyo kila fitna zinatumika, Chama tawala kitafanya fitna ili kiendelee kutawala, na Vya Upinzani vitafanya fitna ili vipate ridhaa ya kutawala----hivyo kama mwananchi ambaye huwa napenda kuona ukweli zaidi ya kufuata "ushabiki", huwa nabaki kila siku nashangaa story zinavyobadilika tu na kuona mambo yako Ndivyo sivyo siku zote---hivyo siwezi bisha ama siwezi kubali upande upi ndio unasema kweli kwa suala la Arusha).

      Ila ninachoweza kusema ni kwamba tujitahidi mara nyingine kuweza kuona kwamba tunatulia na ku analyze na kuelewa kitu kwa namna kilivyoongelwa na si jinsi tunavyodhania kwamba ndivyo huyo mtu anavyomaani....huwa nakuwa msomaji tu humu,lakini kwa jambo kama hili nimeshangaa kwamba hivi mbona kipengele hicho kimetafsiriwa vingine kabisa na wachangiaji humu.

    5. #223
      Lole Gwakisa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2008
      Posts : 2,959
      Rep Power : 1132
      Likes Received
      462
      Likes Given
      330

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By FortJeasus
      Ukweli ni kuwa, mnaopinga kauli ya Ndugu Lema na ambao kila siku hamtaki kuona mazuri ya CHADEMA, mpo, mlikuwepo na kwa hakika lazima mtaendelea kuwepo. Mnajijua, mnafahamiana, yawezekana mnajua mnachofanya, isipokuwa haiwezekani, hata mara moja, kupata matokeo mnayopigania!Hicho ndicho hamtaki kukubali!

      Katika kuzalisha mawazo /fikra mpya ,tofauti za mawazo/mitizamo ni moja ya necessary pre-conditions.Bahati mbaya enyi wapinzani wa CDM hamjapata kuonyesha kama mnaongozwa na ukweli, uhalisia, hekima, busara achilia mbali nia safi.

      Katika mazingira kama hayo haiyumkiniki kuzalisha mawazo mapya! Haiwezekani!

      Kwa kuwa mawazo mapya ni muhimu,wana CDM wenyewe watashindanisha fikra na mawazo na hakika wataednelea kupata mawazo mapya from within maana tunabaini enyi wana wa upotevu hamna nia njema na chama chetu, watu wake na hata kwa taifa!

      Hata hivyo, kwa kuwa chama chetu kinaamini katika dhana ya demokrasia,tunawahakikishia jambo moja: Tutaendelea kuwaheshimu kama wanadamu wenzetu, kadiri ya katiba ya Jamuhuri. Kimantiki, na hata mawazo yenu tumekuwa tukiyaheshimu, tunayaheshimu na tutaendelea kuyheshimu kwa kuwa tunathamini na kuheshimu uhuru wa mawazo. Isipokuwa hayatafanyiwa kazi.
      Mkuu unafaa kwendma kufundisha chuo cha makada wa Chadema kama kipo.

      Filosofia uliyoimwaga sidhani kama vichwa kama vya kina Lema au Nassari wanaweza kuelewa.
      Yours faithfully!

    6. #224
      Activist p's Avatar
      Member Array
      Join Date : 20th May 2012
      Posts : 40
      Rep Power : 361
      Likes Received
      2
      Likes Given
      2

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Namuunga mkono na mguu kwa vyote watetezi wa haki watashinda tuuuu!

    7. #225
      Naytsory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2011
      Posts : 721
      Rep Power : 759
      Likes Received
      127
      Likes Given
      2

      Default Re: Habari ya mhe. Godbless lema kwenye gazeti la tanzania daima la leo

      Hivi uonevu uliofanywa kwa Mh. Lema unafikiri ni wa kwanza Ikulu kuhusika? Yawezekana wako wengi waliotendewa hivi hasa pale wanapotetea haki za raia. Aibu na iwe juu ya Ikulu ya nchi yangu Tanzania. Inachowatendea watanzania Mwenyezi Mungu atalipiza kisasi.

    8. Miaka 50

    9. #226
      Raia Fulani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2009
      Posts : 9,253
      Rep Power : 2622
      Likes Received
      1291
      Likes Given
      834

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Tunahitaji part 2 ya hii stori. Pale ostabei palizungumzwa nini mnamo 2010?
      Beware of a sucker punch

    10. #227
      Unstoppable's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th January 2011
      Posts : 940
      Rep Power : 612
      Likes Received
      330
      Likes Given
      2041

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By Kasheshe
      Huu ni upuuzi... kwani Mh. Rais amezungumzia ni tatizo jimbo kuwa chini ya CDM au amezungumzia utulivu wa mji wa Arusha... why don't you guys read.
      Hapa ninachoona ni Raisi kuzungumza kwa mafumbo/mipasho lakini wengi wamemuelewa; Lema amezungumza direct na hivyo kufanya waliolala waamke. What next- I do not know. But ningependa kujua hicho kikao cha Oysterbay kabla ya uchaguzi kilikua nicha nini? Je kuna mtu alitaka kununuliwa ikashindikana sasa ndio mambo ya kulipa visasi? Mmh taratibu tutaelewa I guess. Navuta subira.

    11. #228
      Honolulu's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 19th January 2012
      Posts : 720
      Rep Power : 0
      Likes Received
      284
      Likes Given
      0

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By Rejao
      Jamani CDM msaidieni huyu mtu wenu. Naona kama hayuko sawa!
      Nadhani wewe ndio hauko sawa! Unasikitisha sana!

    12. #229
      Mnyonge Namba1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2012
      Posts : 402
      Rep Power : 449
      Likes Received
      78
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By masopakyindi
      Nakama Ikulu iliingilia, so what?
      CDM msaidieni huyu mbux3 kucheza boli na saizi yake.

      Sana sana inathibitisha kuwa Lema is not so smart as he is tring to prop himself up.
      Kama ni mjanja mbona tayari yuko nje ya Bunge, wenziwe kama Dr Slaa wanaweza kufikiri 24x7 njia zote za kujikwamua katika matope, yeye inaelekea anafikiri anacheza na watoto wenziwe.

      Cha kushangaza ni kuwa kiti cha Arusha kiko wazi na wanachadema wengi tu wanakitaka. Mshaurini Lema kuwa kama anafikiri ana akili basi si wengi walioiona akili yake kwa kutupwa nje ya bunge kirahisi rahisi.
      Unafikiria kwa kutumia ma*ak* ww na nyinyiemu nzima

    13. #230
      Unstoppable's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th January 2011
      Posts : 940
      Rep Power : 612
      Likes Received
      330
      Likes Given
      2041

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By Likwanda
      Tatizo la wana cdm wengi ni kuwa na mtazamo wa kishabiki kwa kila suala hata kama wamekosea. Binafsi sijasikia JK akisema kuondoka kwa Lema ndio kumesababisha Arusha kuwa shwari bali nilivyoelewa ni kuwa kama mkutano huu ungefanyika ktk kipindi kile cha vurugu isingekuwa rahisi kufanyika huko, sasa kuna ubaya gani kukumbuka historia.
      Mimi sio CDM lakini naamini kabisa JK alikuwa anarusha vijembe fulani hivi purposely. Hatujamfahamu JK leo kwa mipasho; ameanza zamani e.g. Alipozungumza na madaktari akaja kivingine kuwapa mipasho through wazee wa DSM. Alipowaahidi waislamu mahakama ya kadhi akaja kivingine (siku ya baraza la Iddi i believe) akawageuka kwa mipasho na mafumbo, alipokosolewa na maaskofu; akawajibu siku ya sherehe yao kwamba ni wauza unga (talk about finding the major events to spill nonsense). Hakuna asiyejua JK ni mtu wa mafumbo na mipasho hivyo; sidhani kama anaonewa hapa. Hii ni tabia yake ameionyesha mara kwa mara. Nafikiri hata wana CCM wenyewe wanamfahamu kwa hilo. Huwa sikubaliani na mambo kadhaa anayofanya Lema, lakini kwa hili amenifurahisha. Viongozi lazima wasimamie kile wanachokiamini bila woga. Ameongea straight bila kuuma uma maneno. CCM ingekuwa na watu kama Lema 10 hivi (straight talkers), wasio waoga, wanaosimamia ukweli at any cost, CCM isingeyumba kama ilivyo sasa. Mafisadi wangekuwa na wakati mgumu sana.

    14. #231
      mahoza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th March 2012
      Posts : 264
      Rep Power : 415
      Likes Received
      36
      Likes Given
      309

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Yatasemwa yote tujipe siku moja hivi. Kwani tungejua kuna ya osterbay? Hapana. Ukweli ukidhihiri uongo utajitenga. Rais jiandae kujibu ya osterbay. Siri imefichuka.

    15. #232
      Naytsory's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2011
      Posts : 721
      Rep Power : 759
      Likes Received
      127
      Likes Given
      2

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Aibu kwa kurugenzi ya Ikulu waliokanusha kipindi kile kuwa Ikulu ilihusika kumvua ubunge Mh. G. Lema. Watanzania tutaendelea kumwomba Mungu awashughulikie watawala na vizazi vyenu vyote mnaotumia madaraka yenu vibaya. Hasa Mh. Rais tupo watu wengi tunadhulumiwa haki zetu, tunanyanyaswa na kuonewa sana hata tunapolalamika hatusikilizwi kumbe Ikulu siyo MAHALA PATAKATIFU TENA. Ee Mungu sikia kilio cha Watanzania Amen.

    16. #233
      Mnyonge Namba1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2012
      Posts : 402
      Rep Power : 449
      Likes Received
      78
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Rejao
      Jamani CDM msaidieni huyu mtu wenu. Naona kama hayuko sawa!
      Inakuuma jinsi kilivyoanikwa wazi hicho kipurezidaa chenu na hila zake

    17. #234
      palalisote's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th August 2010
      Location : WA HAPAHAPA
      Posts : 2,064
      Rep Power : 2038
      Likes Received
      929
      Likes Given
      3827

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By Mnyonge Namba1
      Chama dhalimu,Uongozi dhalimu
      Mimibaba likes this.

    18. #235
      Tume ya Katiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Location : Chumbuni-Zanzibar
      Posts : 2,677
      Rep Power : 0
      Likes Received
      538
      Likes Given
      273

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By ritz
      Ndivyo anavyowadanganya kwa taarifa yako Wassira alimpa Lema, milioni 10.
      Ritz, umefunguka mkuu! kumbe kala fungu?

    19. #236
      Tume ya Katiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Location : Chumbuni-Zanzibar
      Posts : 2,677
      Rep Power : 0
      Likes Received
      538
      Likes Given
      273

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By Raia Fulani
      Tunahitaji part 2 ya hii stori. Pale ostabei palizungumzwa nini mnamo 2010?
      Nimemnukuu ritz moja ya mambo yaliyofanyika oryesterbay
      Quote By ritz
      Ndivyo anavyowadanganya kwa taarifa yako Wassira alimpa Lema, milioni 10.
      kutomuunga mkono mchungaji au padre mnafiki, mpika majungu, mfitini, anaendesha kanisa kwa maono ya hawara yake, mkabila, ndumilakuwili haimanishi kwamba nimelihasi kanisa-mwampamba

    20. #237
      Domowazi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st February 2012
      Posts : 79
      Rep Power : 383
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By kenethedmund
      wewe madhani utujui watu wa arusha vizuri tutapiga kura za hasira, ushindi utakuwa asilimia 98% Chadema na 2%ccm.
      hahhahahaaa keneth cyo ccm 2% no ni nccr 0.5%,ccm 0.1%,tlp 0.4% na CDM 99%...dats R Chuga

    21. #238
      Mnyonge Namba1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2012
      Posts : 402
      Rep Power : 449
      Likes Received
      78
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By KIM KARDASH
      Leo ndio nimeamini huyu mwizi wa magari mstaafu needs a rehab,anachanganya sana mambo,rais kaonge kitu kingine yeye anaongea kitu kingine kabisa na kujaribu kutaka ionekane wanaongea kitu kimoja,hivi arusha ile na hii kweli ni sawa???
      Tatizo uelewa wako finyu kama wa Y.Makamba

    22. #239
      Gerald's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2007
      Posts : 264
      Rep Power : 640
      Likes Received
      38
      Likes Given
      29

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      ritz
      yaani unatudhihirisha kuwa hata mahali patakatifu rushwa nje nje? Wapi pcb, uwt? Kama mkuu wa nchi anatoa rushwa kwa lema kwa nini yeye asishitakiwe? Aina sababu ya hizi kesi za uchaguzi basi.

      Hapa umetufungua macho ni mengi yanayofanyika pale magogoni Aisee 10m hongo ndani ya ikulu?

      Lema kuchukua pesa ni sawa kabisa ila nafsi yake kaitendea haki hakukubali kununuliwa kajali utuwake zaidi kuliko kuzalilishwa kwa pesa.

    23. #240
      KIM KARDASH's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 4,252
      Rep Power : 0
      Likes Received
      564
      Likes Given
      55

      Default Re: Lema amjibu Kikwete, asema yupo tayari kwa lolote kuanzia sasa

      Quote By Mnyonge Namba1
      Tatizo uelewa wako finyu kama wa Y.Makamba
      wewe uelewa wako mkubwa kama huyo mwizi wenu wa magari lema ambae sijui kule mahabusu walimfanya nini sijui,maana toka atoke mahabusu amebadilika sana kimuenendo na kimatendo.Anatia shaka kwa kweli.

    Page 12 of 27 FirstFirst ... 2101112131422 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...