Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 38 of 38
    1. #1
      ngoshwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st March 2009
      Location : everywhere
      Posts : 3,691
      Rep Power : 1357
      Likes Received
      570
      Likes Given
      770

      Lightbulb Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Hii ndio Kauli ya Mhe. Ezekiel Maige katika Ukurasa wake wa Face Book:






      ".......Ndugu zangu na rafiki zangu. Kwanza niwape pole kwa mshituko mlioupata kwa haya yaliyojitokeza. Naomba msisikitike sana. Kila jambo alilopanga Mola hutokea kadiri ya mapenzi yake. Route ya maisha ya mwanadamu hupangwa na Mola mara tu anapompulizia pumzi ya uhai. Hili lilipangwa hata kabla sijatokea duniani miaka 42 iliyopita!

      Mungu hakushindwa kumwokoa mwanawe Yesu asisulubiwe, tena kwa kuonewa! Hasha, tungeupataje ukombozi bila hilo kutokea? Wakati mwingine Mungu hutoa nafasi kwa mambomagumu kuwafika waja wake, si kwamba hawapendi,bali ili unabii utimie. Ilifika wakati hata Yesu akaona kama Mungu kamuacha! Hasa sisi kwa hili tunaweza kudhani Mungu katuacha! Hasha, ni njia ya kuufikia ukombozi wa kweli.

      Pili, kwa kifupi sana, niwafahamishe kuwa, yaliyotokea ni ushahidi kwamba maliasili ni ngumu. Kukabiliala na wabaya ni kazi ngumu. Wapo waliojipanga ukiwavamia ovyoovyo unaondoka wewe. Ndivyo ilivyotokea.

      Niwahakikishie, wazalendo wamepoteza mpambanaji. Nimepambana na wahalifu angani, majini, porini, mijini na vijijini ndani na nje ya nchi. Nilitumia kila aina ya uwezo wangu kulizawadia taifa langu utumishi uliotukuka. Sikubakisha chembe ya energy.

      Waziri gani aliyesimamia sheria na kuwapa vitalu watanzania maskini wenye sifa na kuwaacha wazungu kama sheria ilivyoelekeza?

      Waziri gani aliyewafikisha mahakamni watorosha twiga akina Kamrani na wenzake? Watu wametumia records za matukio ya 2009/10 kuficha matendo na maamuzi ya kishujaa ya maige ya 2011. Yawezekana hawakutaka nipate sifa, lakini ipo siku nitaipata. Tena si siku nyingi. Niliwaomba wenzangu wamwogope Mungu. Bado nasisisitza hivyo, si Mungu wangu kama ilivyodhaniwa, bali Mungu wetu wa haki.

      Waziri gani aliyefunga biashara ya wanyamahai?

      Waziri gani aliyeonyesha mfano wa kuchukua hatua kwa watumishi pale alipoona hawatendi sawa? Maige hakusita kuchukua hatua.

      Maamuzi haya ni magumu na yamegusa watu wenye nguvu na ushawishi mkubwa. Nilitegemea vita hii, na ninaamini tutashinda. Nilisema Bungeni, watanzania wapenda haki wanisikilize kwa makini. Muda haukuruhusu, ila nitarudi Bungeni na nitasema.

      Imesemwa issue ya nyumba. Nimefafanua na kutoa vielelezo. Kila mbunge aliyetaka amekopeshwa shs 290m, wengine wameanzisha biashara na wengine wamenununua magari na wengine majumba. Wapo walioficha, na tupo tuliojiweka wazi! Mkopo wangu huo umekuwa my contribution na balance kulipwa na benki na nyumba kuimortgage. Nimetoa nyaraka zote kwa wanahabari na vyombo vyote husika. Nimesema mwenye mashaka aende kwa Msajili wa hati wizara ya ardhi, au kwa kamishna wa maadili, au CRDB Azikiwe na Dodoma nilikokopa au amtafute muuzaji. Kote huko utapata rekodi ya bei na mode of payment. Wapo wahuni, kwa maslahi ya kisiasa na chuki binafsi wametangaza bei tofauti na niliyonunulia. Manasheria wangu anashughulikia hilo.

      Niwahakikishie, vita nimepigana, imani na dhamana nimeilinda, muda wa kutuzwa na mwenye kumbukumbu sahihi, Mungu utafika. Naamini nimejiwekea akiba isyooza Mbiguni.

      Yapo mengi yasiyo sahihi yaliyosemwa. Nitakuwa nafafanua kila nipatapo fursa na muda utazidi kutufunua. Kwa kifupi, kwa suala la vitalu, hakuna kampuni hata moja iliyopewa kitalu cha uwindaji bila kuomba, kukaguliwa na kamati ya ushauri na hatimaye kupewa alama. Kampuni zisizokuwa na sifa ni zile zilizopata chini ya alama 50. Na kwa kampuni zilizokuwa kwenye biashara, passmark ni alama 40 kwa mujibu wa kanuni ya 16(5) ya kanuni za uwindaji wa kitalii za mwaka 2010. Hakuna kampuni iliyopata chini ya alama 50 iliyopata kitalu. Hakuna kampuni ya kizalendo iliyopendekezwa na kamati ya ushauri ambayo haikupewa kitalu.

      Kwa upande wa report ya CAG, haikunigusa binafsi kwani ilikuwa inaishia juni 2010 wakati mimi ilishika dhamana Novemba 2010.

      Ka upande wa biasharaya wanyamahai, hakuna wanyama waliosafirishwa kinyume cha sheria wakati wangu (2011), na matukio ya utoroshaji tulipoyabaini, tulifungua mashitaka kwa watuhumiwa nakufnug biashara hiyo.

      Naanza kazi ya kuwawakilisha wananchi wa Msalala. Nitawawakilisha kwa mujibu wa katiba na ahadi zangu kwao hadi 2015 watakapopata fursa ya kuamua vinginevyo.

      Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana. Ka wakristo, naomba msome Mwanzo 4:1-15.

      Wasalaam..... "


      https://www.facebook.com/permalink.php?story_fbid=29215 1247542210&id=100002420106482
      Last edited by ngoshwe; 3rd June 2012 at 18:44.
      Ndusty likes this.
      "Mnataka kujua nini? Sikuzaliwa ili nipate nishani... "Please don't make it an issue, acheni suala hilo ni uchonganishi, acheni," - Malecela.

    2. Miaka 50

    3. #21
      Kigogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2007
      Location : Calabash
      Posts : 8,208
      Rep Power : 2097
      Likes Received
      1234
      Likes Given
      313

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      yaani huyu maige imemuuma kweli kweli kupokwa uwaziri..mbona aalalamika sana?kwa nini..khaaa ni uwaziri tu au kuna lingine?
      ______________________________ _
      Niko tayari kufa huku nimesimama kuliko kuishi huku nimepiga magoti....

    4. #22
      King Kong III's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Enaboishu-Umenyeni
      Posts : 11,932
      Rep Power : 5065
      Likes Received
      3204
      Likes Given
      2665

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Mbona analalamika tu mda wote?? Endeleea na Ubunge tu maige,the world is not fair jipange!!

    5. #23
      Tango73's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2008
      Posts : 1,041
      Rep Power : 741
      Likes Received
      290
      Likes Given
      2

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Quote By Losambo
      Maige anatafuta pa kufia, hana jipya.
      mbona hasemi kuhusu samaki wa mionzi ya nuklia waliotoka japani alivyowaruhusu kuja TZ?
      ngoshwe likes this.

    6. #24
      ngoshwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st March 2009
      Location : everywhere
      Posts : 3,691
      Rep Power : 1357
      Likes Received
      570
      Likes Given
      770

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Quote By Tango73
      mbona hasemi kuhusu samaki wa mionzi ya nuklia waliotoka japani alivyowaruhusu kuja TZ?
      NI yeye?
      "Mnataka kujua nini? Sikuzaliwa ili nipate nishani... "Please don't make it an issue, acheni suala hilo ni uchonganishi, acheni," - Malecela.

    7. #25
      petrol's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 140
      Rep Power : 439
      Likes Received
      45
      Likes Given
      0

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      maige ajivue gamba aende wapi - udp, tlp au nccr? labda aende kanisani maana anatoa mahubiri mazito


    8. #26
      Nicholas's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2006
      Posts : 5,265
      Rep Power : 3671
      Likes Received
      1325
      Likes Given
      2214

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Bado analilia nini?kwnye picture kashindwa hata na mzungu?Mzungu kavaa tai ya rangi za TZ yeye kavaa asichokijua huku akijiita mzalendo.
      SIMPLY THE RADICAL: I can`t wait to see the criminalization of CCM,UWT,Bunch of Policemen/women,and all wanafiki na wachumia tumbo.

    9. #27
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,103
      Rep Power : 12256
      Likes Received
      6016
      Likes Given
      6866

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Quote By Nicholas
      Bado analilia nini?kwnye picture kashindwa hata na mzungu?Mzungu kavaa tai ya rangi za TZ yeye kavaa asichokijua huku akijiita mzalendo.
      sasa anaboa
      .....Ana sifa zote, nzuri na mbaya!!!

    10. #28
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,672
      Rep Power : 977
      Likes Received
      584
      Likes Given
      10

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Kwa mchambuzi makini,Maige ni mtu muhimu ktk kipindi hiki kuchukuliwa na CDM. Inaonyesha anafahamu mengi,na kama kawaida ametumiwa na mfumo,na ametupwa,ana hasira. Nawaomba mabingwa wa mikakati wa CDM msipoteze fursa muhimu kama hizi zinapojitokeza!

    11. #29
      MwalimuZawadi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st September 2007
      Posts : 623
      Rep Power : 724
      Likes Received
      50
      Likes Given
      3

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Huyu jamaa ningeweza hata kupata pumzi ya kumwamini kama asingesingizia kuwa amepata hela (sehemu ya dola laki 7 tu!) kutokana na biashara ya usafirishaji aliyofungua yeye na mkewe. Mkewe mwenyewe jamani, hata si wa kusingizia...Maige mwogope Mungu unayetaka akupiganie
      Sent from my Nokia rinGo using JamiiForums

    12. #30
      BULOLE BUKOMBE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th April 2011
      Posts : 361
      Rep Power : 484
      Likes Received
      60
      Likes Given
      287

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Quote By andishile
      ni kweli kuwa mara nyingi mtenda mema hufanyiwa hiyana,lakini kwako hapana!sasa kinachokufanya upite majukwaani kuiponda ccm,upite jukwaani kuwaponda viongozi wa sekretarieti ya ccm ni nini? wakati ulipokuwa waziri hukufanya hivyo?au kama ulijua ccm haifai,kilichokufanya ukubali kuitumika kama waziri wa serikali yake ni nini?haifai baada ya wewe kutolewa uwaziri?umejishushia sana hadhi!piga ua garagaza,wee ni mbunge wa ccm,ungekaa kimya mngekosoana ktk vikao vya chama!
      Hapana kwa mujibu wa maelezo yake mimi nashawishika kuamini analosema tumsikilize mtu kama KAMRANI NI TISHIO TANGU ZAMANI NA HAKAMATIKI KITENDO CHA KUMKAMATA HUYO JAMAA KILIGUSA MASLAHI YA WATU WENGI NDANI YA SYSTEM NA ZAIDI YA YOTE HUWEZI KUJUA TATIZO MPAKA UMEPATA TATIZO

    13. #31
      Kakulwa P's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th February 2012
      Posts : 201
      Rep Power : 408
      Likes Received
      69
      Likes Given
      10

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Hakuna aliyepata Mshtuko wowote kwa kufukuzwa kwa Maige.
      Twiga auze yeye, Vitalu auze yeye, Wanyama hai auze yeye, sisi tupate Mshtuko wa nini bwana labda wale wafagiaji wake nyumbani kwake watakosa kazi. Hakuna hiyana umevuna ulichopanda siyo muadilifu hata kidogo.

    14. #32
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,647
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Maige, why now? Andika kitabu basi tujue moja na tuchukue hoja zako kama reference in the future.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    15. #33
      Bitende's Avatar
      Member Array
      Join Date : 20th August 2011
      Posts : 33
      Rep Power : 399
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Nikweli mkuu ana hote kahama inaitwa MIAMI HOTERI

    16. #34
      Mwanawalwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2012
      Posts : 336
      Rep Power : 419
      Likes Received
      92
      Likes Given
      53

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      kwani maige alizaliwa ili awe waziri mbona anambwelambwela sana ushauri wangu Maige you can make it big even without being a minister lyf goes on bana ,kulalamika won't change anything try paln b yeeeeeeeeee ecccm yeneye makoye

    17. #35
      andrewk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th April 2010
      Posts : 2,229
      Rep Power : 908
      Likes Received
      283
      Likes Given
      60

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      huyu jamaa siasa kavamia kabisa, hawezi kaa kimya tu?

    18. #36
      Safari_ni_Safari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2007
      Location : Kibaruani
      Posts : 12,014
      Rep Power : 24158
      Likes Received
      4738
      Likes Given
      2652

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      HUU UVAAJI GANI?


      Soki Ozali Mwasi Yaka, Soki Ozali Mobali Koya Te


    19. #37
      mtotowamjini's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Location : None of Your Business
      Posts : 4,533
      Rep Power : 1263
      Likes Received
      1109
      Likes Given
      28

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      mbona mawaziri wengine wamebakishwa?? kwanini yeye atolewe kama alikua hana kosa...mi bado simuamini sawa alikua anafanya kazi hatujakataa lakini naamini aliiba
      Every saint has a past, every sinner has a future' ...Oscar Wilde

      One man's good fortune is another man's misfortune


    20. #38
      Mnamzelu Miye's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 24
      Rep Power : 357
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Mhe. Ezekiel Maige: "Mara nyingi watenda mema hufanyiwa hiyana"

      Inahitajika Maige apewe ushauri nasaha na si vinginevyo, atakuwa ameatirika kisaikolojia, si bure kwa aliyekuwa mtu makini kuendeleza mijadala ambayo hata iweje, haitamrudisha katika nafasi ya Uwaziri.
      Quote By Ogah
      Kwa hiyo uliwavamia "ovyoovyo"...........wewe Maige ni hovyo kabisa............[/LEFT]
      [/SIZE][/COLOR]

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...