Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

    Report Post
    Page 1 of 4 123 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 74
    1. #1
      zimmerman's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th February 2011
      Posts : 347
      Rep Power : 567
      Likes Received
      260
      Likes Given
      66

      Default Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Jana usiku nimemsikiliza kwa makini mheshimiwa Tundu Lissu kwenye kipindi cha Kipima Joto cha ITV kuhusu mada iliyosema, Je kundi la Uamsho lipo juu ya sheria? Argument ya Lissu ilikuwa kwamba fujo zote za Uamsho kuchoma moto makanisa kule Zanzibar, zisitazamwe kidini bali ziaminike zaidi kuwa ni frustrations za kisiasa hasa hasa kuhusu Muungano kwamba serikali imewaminya watu kuzungumzia uwepo au kutokuwepo kwa Muungano, bali imewapa option ya kutoa maoni ya kuuboresha.

      Akakoleza chumvi zaidi bwana Lissu pale alipotoa mifano ya Kanisa la kwanza East Africa kujengwa Zanzibar, na kwamba kule Egypt Ukristo umekuwepo more than 2, 000 years (Coptic Church), na uko kote (Zanzibar na Egypt) Waislamu walio wengi wameishi pamoja kwa amani na Wakristo walio wachache. Kwa hiyo udini wa Waislamu kuwachukia Wakristo kutokana na imani yao hauwezi kuwa hoja halisi iliyosababisha mali za Wakristo kuharibiwa hivi karibuni na Waislamu huko Egypt na Zanzibar bali siasa ndo mshtakiwa wa kwanza.

      Kwa haraka haraka unaweza ukaaminishwa na hoja hii ya Lissu pamoja na ushawishi wake wa hoja hiyo. Pamoja na kwamba mimi binafsi namkubali Lissu lakini hapa kaonyesha udhaifu mkubwa. Ni kama vile bwana Lissu kapitiwa hivi na mambo yanayoendelea ulimwenguni kuhusiana na vikundi vya aina ya Uamsho kwenye nchi zingine. Kuanzia kwa baba lao Al Qaeda, Al Shabab ya Somalia, Boko Haramu ya Nigeria, Taleban ya Pakistan na Afghanstan, na kadhalika.

      Kwa maoni yangu Uamsho ni kikundi tu cha kigaidi kama vikundi vinginevyo vyote nilivyotaja hapo juu, tofauti yake ni kwamba kipo katika hatua za kwanza za kuelekea ugaidi original. Vikundi vyote vya kigaidi hasa vile vinavyotumia uislam huwa vina jambo moja linaloviunganisha. Vyote ni fundamentalist kwenye theolojia yake na vinasukumwa na nia (kwao ni nia njema) ya kutaka kutakasa dini yao kutokana na hatari wanayohihisi kwamba nguvu za kisecular na kikiristo zinaikaba na wanataka kurudisha enzi zile za Uislam safi (sharia itawale serikali, “uchafu” wote kama bar, guest houses, na kadhalika usafishwe ili kurudisha imani halisi na iliyo safi).

      Al Qaeda kiliundwa baada ya Wamarekani kuweka bases zake za kijeshi Saudi Arabia ili kuipiga Iraq miaka ya 90, maana Osama bin Laden aliona ni aibu kwa nchi yake yenye makazi mawili matakatifu ya Allah (Mecca na Medina) kuweka bases za kijeshi, ishara ya kutawaliwa na Kafir mkuu, Marekani.Na kumbuka katika Uislamu siasa na dini haviwezi kutenganishwa, Lissu yampasa ajielimishe vizuri na theology ya Kiislamu.

      Boko Haramu, tafsiri yake ni Western Education is Haram, yaani elimu ya Magharibi ni haramu, unaweza kupata hisia kwamba dini inawasukuma kusafisha kila kitu kilicho na ideals za kimagharibi ukiwemo Ukristo na ndio maana Makanisa hayatakiwi kuwepo kule kaskazini mwa Nigeria.

      Uamsho ya Zanzibar ina vichembe hivyo hivyo vya kuhisi Zanzibar inaanza kukengeuka kutoka kwenye Uislam sahihi. Muungano unachukuliwa kama culprit wa kwanza aliyesababisha Zanzibar kujaa baa, vijiwe vya kiti moto, Makanisa ya Kikristo kila shehia ya Zanzibar, watoto wa kike wa kizanzibari kuanza kuvaa kama wabara, na megineyo mengi.

      Wale wote wanaotumia hoja ya kanisa la kwanza EA kujengwa Zanzibar, wanasahau kwamba enzi zile kanisa lilelilionekana kama siyo threat kwa utamaduni wa kiislamu, after all waliosali mule ni wazungu wawili watatu pamoja na weusi wachache. Kanisa lenyewe moja. Zanzibar ya sasa imebadilika sana siku za hivi karibuni. Makanisa yameongezeka sana na hili linawatisha Wazanzibari. Maredio mengi ya FM yameanzishwa na muziki wa bongo fleva unapigwa sana ikiwemo chombeza chombeza sex stories kwenye hizo redio.

      Hili linawakera sana mafundamentalists na wanaona pa kuanzia ni Muungano kuuvunja ili wapate control kamili ya kuendesha serikali kwa kanuni zisizofungamana kwa namna yoyote na katiba ya kisecular ya serikali ya Tanganyika.

      Lissu anaweza akawa na nia nzuri ya kutofungamanisha mainstream Islam na vurugu zinazojithibisha kidini. Lakini ukweli upo pale pale kwamba Uamsho na vikundi vinginevyo vilivyopo huko Zanzibar vipo motivated zaidi na dini. Tafsiri yao ya fundamentalist Islam ya kutotenganisha dini na serikali inaweza isiwe muafaka kwa wakati huu lakini hilo ndilo linalowasukuma. Kwao Uislam Zanzibar umeingiliwa na yapaswa kuusafisha.

      Kuvunja Muungano ni hatua ya kwanza, na kama wakifanikiwa hatua zingine zitafata.
      Last edited by zimmerman; 5th June 2012 at 10:18.
      Meshili, MpendaTz, rifwima and 6 others like this.


    2. #2
      kipuyo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th July 2009
      Posts : 238
      Rep Power : 550
      Likes Received
      74
      Likes Given
      74

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Mimi naona kama Tundu Lissu alikusudia kusema alioyasema ili kuepuka upotoshaji ambao ungetokea baada ya hapo.

      CCM na watu wao wangeshadadia kuwa CHADEMA imeendeleza vita dhidi ya uislamu maana asingeweza kuutaja uamsho bila kuingiza uislamu.

      Hivyo mimi nampongeza kwa kukwepa mitego ya maadui.

    3. #3
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,540
      Rep Power : 37792
      Likes Received
      5004
      Likes Given
      2348

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      ​@zimmermanNinachoamini ni kwamba Tundu yupo sahihi, na wanaochoma makanisa kule zanzibar siyo Kikundi cha Uamsho, bali vijana wa Dr. Shein ili wazanzibari na jamii iseme hawa jamaa wanachoma makanisa.

      Hata mimi mwanzoni nilidhani kwamba waliochoma makanisa ni Uamsho, kumbe siyo!
      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    4. #4
      Mark Francis's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th November 2010
      Location : Ubungo, DSM
      Posts : 453
      Rep Power : 588
      Likes Received
      239
      Likes Given
      46

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Umeandika kama hujapita shule, manake ungekua umepita ungefundishwa namna ya kuandika insha (essay) inayoeleweka na sio hiyo inayochosha...!!
      "Better to be hurt by the truth than comforted with a lie"

    5. #5
      Kiganyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th April 2012
      Posts : 1,162
      Rep Power : 987
      Likes Received
      709
      Likes Given
      400

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Hivi Ugaidi maana yake nini??

      Who coined the word 'ugaidi'??

      Hivi kweli muungano wetu ni 'SACRED' au ni dogmatism za wanasiasa wanaofaidika kisiasa na ki maslahi na Muungano huu??

      Kwa nini suala hili lilipelekwa kwa hati ya dharula bungeni tena jumapili na j3 ikatangazwa Muungano??

      Kwa nini Serikali iwaamulie wananchi suala la kujadili na namna gani ya kujadili, hivi sisi wanadamu ni mahayawani na hatuna haki ya kukubali au kukataa??

      Kwa nini Mwanasheria kutoka kituo cha Sheria na haki za binadamu alikuwa na kigugumizi sana ili hali akikili kuwa hata katika zile aina mbili za miunngano tunazojifunza darasani yani fed na uni muungano huu haupo hata kati ya hizo mbili??

      Hoja tuangalie sababu ya kwa nini Nyerere na Karume waliridhia kama bado ziko valid hadi sasa ni mufilisi kwani hakuna anayefahamu ni sababu zipi zilipelekea muungano kuwepo!

      Nadhani kwa kuwa sisi ni wanafiki sana basi tuendelee na unafiki wetu na tujadili kuuboresha Muungano!


    6. #6
      Mlitika's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2012
      Posts : 414
      Rep Power : 522
      Likes Received
      224
      Likes Given
      326

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Unge-edit kidogo basi tupio lako, maana inachosha kufuatilia matiki yako

    7. #7
      Wakumulika's Avatar
      Member Array
      Join Date : 31st January 2012
      Posts : 15
      Rep Power : 376
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Katika kutendea haki mambo hakikisha haumung'unyi maneno,
      kwahili Lissu amechemka kwa mtanzamo wa karibu lakini kwa yule anayetazama mambo zaidi ya pale na jinsi anavyo yaona lissu yuko sahihi kabisaaaaa, katika hili watu watatafuta mchawi hata kwa nguvu ilimradi dhamira yao ya kisiasa itimie.

      Mambo ya UAMSHO yatamalizwa na CCM na UAMSHO, kushindwa kwao kufikia muafaka na UAMSHO na ajenda zao za siri hicho ndio kifo cha CCM na Muungano wake

    8. #8
      kelvito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th May 2012
      Posts : 388
      Rep Power : 526
      Likes Received
      97
      Likes Given
      74

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      unaonekana unapoint ila mwalimu mpaka aipate hiyo point yako duuu!
      kama ni mimi nasahihisha mpaka hapo una negative 10!
      Freedom consists not in doing what we like, but in having the right to do what we ought. by John Paul II

    9. #9
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,703
      Rep Power : 1281
      Likes Received
      1321
      Likes Given
      1711

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Quote By kipuyo View Post
      Mimi naona kama Tundu Lissu alikusudia kusema alioyasema ili kuepuka upotoshaji ambao ungetokea baada ya hapo.CCM na watu wao wangeshadadia kuwa CDM imeendeleza vita dhidi ya uislamu maana asingeweza kuutaja uamsho bila kuingiza uislamu .Hivyo mimi nampongeza kwa kukwepa mitego ya maadui.
      Kama amekwepa mitego ya maadui huku anajua kwamba hali halisi ni kama hiyo aliyoisema zimmerman basi anakuwa amekosea sana, japo hoja zote mbili zinamashiko kwa kweli.

      Isipokuwa kwenye swala la mauaji tu, lakini naunga mkono jitihada za waislamu kuhakikisha kwamba misingi ya imani yao haichafuliwi, nikichukulia kwamba maelezo ya bwana zimmerman ni sahihi basi dunia inalazimika kujipanga namna ya kuishi na jamii ya kiislamu bila mikwaruzano kwa kuheshimu mira na desturi zao kwa kadri zinavyoelekezwa kwenye mafundisho yao.

      Lakini pia, kutokea kwenye msimamo wa mheshimiwa lisu, watanzania ni lazima tujiulize ni kitu gani kinasababisha watu wanashindwa kufanya ideological politics, hapa ndio mashitaka yote yanapojikuta yakielekezwa kwa chama cha mapinduzi kwa sababu ya mkakati wake wa kuendesha siasa kandamizi.

      CCM ni lazima ikubali hathali za democrasia kwenye mustakabali wake, democrasia nchini mwetu imekuwa mpaka kufikia hatua ya kukibwaga chama hiki, CCM ni lazima ikubali kuachia nchi kwa amani na utulivu, kilichotokea zanzibar kinaweza kabisa kabisa kutokea hata bagamoyo, hata sasa.

    10. #10
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,703
      Rep Power : 1281
      Likes Received
      1321
      Likes Given
      1711

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Quote By MARQ View Post
      Umeandika kama hujapita shule, manake ungekua umepita ungefundishwa namna ya kuandika insha (essay) inayoeleweka na sio hiyo inayochosha...!!
      Content yake unaionaje, acha kutafuta sababu za uvivu wa kusoma.

    11. #11
      Angel Msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Posts : 6,358
      Rep Power : 1848
      Likes Received
      1412
      Likes Given
      0

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      %kubwa ya wazanzibar wazawa ni waislam, na wakristo wengi walioko zanzibar ni wahamiaji toka bara, kuwachomea makanisa, baa, nyumba ni ishara ya kuwafukuza warudi kwao bara, na yote hii inatokana na wazanzibari kutokuuhitaji muungano.

    12. #12
      Ruhazwe JR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2011
      Posts : 3,177
      Rep Power : 2893
      Likes Received
      777
      Likes Given
      723

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Mkubwa!...tafadhari sana tena sana, nakuhakikishia Waziri wangu wa sheria na katiba ni Lissu, hakuna mahala popote ambapo amekosea,tatizo lipo kwako kwa hukuelewa nini mantiki ya waziri wangu,na uwalewa wako ni mdogo juu ya kinachoendelea zanzibar.

      Iko hivi watu waliochoma makanisa ni pandikizi ili kuua hoja ya muungano walio kuwa nayo watu wa uamsho. Ndio maana wazir wangu wa sheria akasema hoja ya udini/kuchoma makanisa ni hoja ya kujishikiza hoja ni muungano...chezea Lisu wewe
      Last edited by Ruhazwe JR; 2nd June 2012 at 12:41.

    13. #13
      bumes's Avatar
      Member Array
      Join Date : 26th May 2012
      Posts : 58
      Rep Power : 367
      Likes Received
      12
      Likes Given
      1

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Kweli namimi nilimshagaa Mh TUDU LISU he was not objectve nilidegemea atasema.

      Kilavurugu sehemu yote watu wanatumia kwakufanya matakwa yao kama ZANZIBAR, WAIZI WAKATUMIA VURUNGU KUIMBA, WABAGUZI WADINI WAKAENDA KUCHOMA MAKANISA.

      Kama ni frustrations tu kwanini hawakuenda kuvuja ma misikiti, bar, mahotel humo machafu megi yanafanyika.


      Nimulize kitukimoja.


      THE DAY ZANZIBAR WILL WILL HAVE AUTONOMY, SINCE YOU SEEM TO KNOW A LOT OF THINGS HOW CAN YOU ANALYSE THE STEREOTYPE SECURITY SITUATION OF TANZANIA MAINLAND ?

    14. #14
      yaya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th June 2011
      Posts : 690
      Rep Power : 542
      Likes Received
      216
      Likes Given
      67

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Quote By Sangarara View Post
      Kama amekwepa mitego ya maadui huku anajua kwamba hali halisi ni kama hiyo aliyoisema zimmerman basi anakuwa amekosea sana, japo hoja zote mbili zinamashiko kwa kweli.

      Isipokuwa kwenye swala la mauaji tu, lakini naunga mkono jitihada za waislamu kuhakikisha kwamba misingi ya imani yao haichafuliwi, nikichukulia kwamba maelezo ya bwana zimmerman ni sahihi basi dunia inalazimika kujipanga namna ya kuishi na jamii ya kiislamu bila mikwaruzano kwa kuheshimu mira na desturi zao kwa kadri zinavyoelekezwa kwenye mafundisho yao.
      .
      Mkuu, mimi ninaamini kwamba katika nchi mabazo serikali zake hazina dini, wananchi wake wote ni sawa na wana haki sawa za kijamii.

      Kwa misingi hiyo haitakiwi dini fulani ijione kwamba yenyewe ina haki zaidi ya nyingine hadi kulazimika wengine kuishi kwa kuwapendezesha wao na sheria zao.

      Kinachotakiwa kufuatwa ni sheria za nchi ambazo huwa zimeridhiwa na wanachi au kupitia wawakilishi wao bila kuipendelea dini yoyote.

      Kama alivyowahi kusema Mzee Ruksa wakati fulani kwamba kama kuna mtu anataka kula chura mwache ale ili mradi hakulazimishi nawe umle.

    15. #15
      Mark Francis's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th November 2010
      Location : Ubungo, DSM
      Posts : 453
      Rep Power : 588
      Likes Received
      239
      Likes Given
      46

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Quote By Sangarara View Post
      Content yake unaionaje, acha kutafuta sababu za uvivu wa kusoma.
      Sio kila mtu ana muda wa kupoteza, wengi tupo busy kulijenga taifa letu. Tunatumia muda mfupi kujua nini kinachoendelea katika nchi yetu na kuchangia mawazo yetu. Hata kama content ni nzuri, lakini kama uandishi ni ubaya ujumbe unaweza usifike kama ulivotarajiwa. Pia wengine wana matatizo ya macho ambayo hayawezi kuhimili kusoma sentensi mfululizo zisizokua na paragraph. Kama wewe ndo mwalimu wake, JIPANGE.
      Sangarara likes this.
      "Better to be hurt by the truth than comforted with a lie"

    16. #16
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,703
      Rep Power : 1281
      Likes Received
      1321
      Likes Given
      1711

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Quote By MARQ View Post
      Sio kila mtu ana muda wa kupoteza, wengi tupo busy kulijenga taifa letu. Tunatumia muda mfupi kujua nini kinachoendelea katika nchi yetu na kuchangia mawazo yetu. Hata kama content ni nzuri, lakini kama uandishi ni ubaya ujumbe unaweza usifike kama ulivotarajiwa. Pia wengine wana matatizo ya macho ambayo hayawezi kuhimili kusoma sentensi mfululizo zisizokua na paragraph. Kama wewe ndo mwalimu wake, JIPANGE.
      Basi bwana, nadhani amekuelewa.
      Mark Francis likes this.

    17. #17
      Comi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2011
      Posts : 1,031
      Rep Power : 596
      Likes Received
      164
      Likes Given
      2

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Lissu alienda kama mwanachama na kiongozi wa cdm lakini yeye akaongelea kama raia na hapo hapo aliongelea kama kiongozi wa chama makini. Lazima uwe na akili za ziada ndio uelewe
      "YOU IMAGINE WHAT YOU DESIRE,YOU WILL WHAT YOU IMAGINE AND AT LAST YOU CREATE WHAT YOU WILL"
      GEORGE B. SHAW

    18. #18
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,703
      Rep Power : 1281
      Likes Received
      1321
      Likes Given
      1711

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Quote By yaya View Post
      Mkuu, mimi ninaamini kwamba katika nchi mabazo serikali zake hazina dini, wananchi wake wote ni sawa na wana haki sawa za kijamii.
      Kwa misingi hiyo haitakiwi dini fulani ijione kwamba yenyewe ina haki zaidi ya nyingine hadi kulazimika wengine kuishi kwa kuwapendezesha wao na sheria zao.
      Kinachotakiwa kufuatwa ni sheria za nchi ambazo huwa zimeridhiwa na wanachi au kupitia wawakilishi wao bila kuipendelea dini yoyote.
      Kama alivyowahi kusema Mzee Ruksa wakati fulani kwamba kama kuna mtu anataka kula chura mwache ale ili mradi hakulazimishi nawe umle.
      Mkuu ni lazima tuishi maisha ya kuvumiliana na kujaliana kama tunadhamira ya kweli ya kuishi kwa amani na utulivu kwenye jamii zetu, wakirsto wanaelekezwa kwamba kama kula kwao nyama kuna mkwaza mtu mwingine basi na waache kuila hiyo nyama, wanaekekezwa kuwapenda jirani zao kama wanavyojipenda wao, na wanashauriwa kutokuwaudhi watu wengine, hii ni katika kuhakikisha kwamba jamii za kikirsto zinaishi kokote pale duniani bila kukorofishana na jamii zenye imani tofauti.

      Nikiwa mdogo nyumbani, ilikuwa ni marufuku kula kuku ambaye hajachinjwa na muislamu, kwa sababu waislamu huchukulia kuku ambaye hajachinjwa na muislamu ni nyamafu na hastahiri kuliwa, sasa kama kweli mmeamua kuishi kidugu kumuachia muislamu achinje kuku kuna matatizo gani.

      Nasisitiza kwamba dunia inawajibika kujifunza namna ya kuishi na waislamu na kuziheshimu taratibu hizo, hakuna haja ya ushindani kwenye hili, athari za kutofanya hivi zinaeleweka vizuri sana, hata wewe yaya unazitambua acha ubabe na ubinafsi.

    19. #19
      Ruhazwe JR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2011
      Posts : 3,177
      Rep Power : 2893
      Likes Received
      777
      Likes Given
      723

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      wakuu!..,.Sangara na yaya mbona mi naona kama mnabishana mawazo sawa? Au!....emu nipeni ufafanuzi mi sijawaelewa

    20. #20
      Shardcole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th January 2012
      Posts : 4,826
      Rep Power : 1375
      Likes Received
      1096
      Likes Given
      4

      Default Re: Tundu Lissu, kwa hili, kachemka

      Ukweli ni kwamba Lissu jana kachemsha yani hajui kama uhamsho ni magaidi?

      Haya mambo mi yananitia wasiwasi kabisa kwa maana ya jinsi ninavyomjua lissu alivyomsema ukweli pasipo kuogopa ila jana kaogopa screen! Nakumbuka kwenye hoja ya muungano bungeni lissu alichambua ukweli wote tena pasipo kuogopa lakini jana kaogopa kutetea wabara na wakristo waloonewa kule zenji na mpaka sasa wamefika wanasiasa 3 walojikanyaga kuhus hili akiwemo mtatiro na zitto'

      NDIO MAANA MIMI HUWA NAMKUBALI SANA LEMA MAANA YEYE HUWA HAFICHI KITU NA KWENYE UKWELI HUSEMA PASIPO KUOGOPA.

    Page 1 of 4 123 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...