kwa kipindi nilichomfahamu dr slaa kama mbunge na baadae mgombea uraisi nikiri kuwa mwonekano wake umebadilika sana.dr.slaa amepungua sana yaani amekonda mno isipokuwa ubongo wake ndio haujakonda kwani bado akisimama jukwaani anatema cheche kama kawaida.
Mambo mengi yanaweza kuwa yamechangia mfano umri lakini nionavyo mimi cdm wanamtumia sana huyu mzee wa watu kwa kiwango ambacho nahisi hakizingatii wala kutambua hitaji la mzee huyu kupumzika na kujenga afya yake.dr slaa yupo kila mahali kwa kila kitu.iwe mkutano iwe oparesheni iwe kupokea wanachama na hata mikutano ya waandishi wa habari.anazunguka mikoani kwenye mikutano isiyokwisha.anashiriki mikutano ya ndani na kufungua matawi.ndiyo nakubali huyo ni katibu mkuu lakini kiukweli nahisi dr slaa anachoshwa na kuzeeshwa zaidi na shughuli hizo.
cdm wanapaswa kuinua na kuwafunda makada vijana waende huko mkioani kukomaa na ccm ana wapambe wao na sio kumwacha dr.slaa akihangaika kama hakuna vijana.ni muda wa heche na viongozi wenzie wa bavicha kuacha malumbano ya kwenye magazeti na kujikita katika ujenzi wa chama mikoani.kazi hizo wapewe kina lema ,lissu mbowe zitto nassari na wengine ambao bado ni vijana wadogo.
kama kweli cdm mnamuhuitaji slaa katika mipango yenu ya baadaye,huu ni muda wa kutafakari namna ya kuutumia uwezo na kipaji alichopewa na mungu .
Nawasilisha.

Reply With Quote



Follow Us Here