Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Nape si mwanachama wa CCM

    Report Post
    Page 4 of 8 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 148
    1. #1
      Eng. Y. Bihagaze's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 8th September 2011
      Location : Czech(but now in DAR)
      Posts : 769
      Rep Power : 5117
      Likes Received
      584
      Likes Given
      111

      Default Nape si mwanachama wa CCM

      Attachment 54878 . . ? Attachment 54879!!!

      Kutokana na wimbi la wananchi kuchukizwa na mfumo wa CCM na serikali yake na kiasi cha wanachama wengi kukihama chama hiki kikongwe, vile vile kutokana na ukweli kwamba chama hiki kikongwe kimepoteza mwelekeo kwa kasi na kustawisha majungu, udini, fitina na umaskini miongoni mwa jamii ya watanzania, Ububu au ukiziwi wa viongozi wake kwenye kero wazi zinazowasumbua wananchi kama migomo ya madaktari na chochezi za ubaguzi, baadhi wa wanachama wa CCM wameguswa na matukio ya upepo yanayokiandama chama chao hiki.


      Fukuto la minong’ono kwamba kuna watumishi wengi wa serikali wakiwemo wanajeshi wana vyeti feki, limesokota hisia kwa kundi la wanachama wa CCM nao kuingiwa na mawazo kwamba isitoshe ndani ya CCM kuna vidudu-mtu ambao si wana CCM, lakini wako ndani ya Chama ili Kukidhoofisha na kukiua isitoshe baadae waunde vyama vyao kama ilivyokuwa kwa baadhi ya Vyama kongwe barani humu.


      Vuguvugu la kishawishi hiki kiliwasukuma wanachama hawa kwa siri kuunda kikosi kazi ili kuchunguza uhalali wa uanachama kwa baaadhi ya Viongozi wa chama chao ambao waliwalenga kama wavunjaji wakuu wa Chama. Baada ya wiki chache za uchunguzi wao wameorodhesha na kugundua kwamba baadhi ya viongozi wao kimsingi si wanachama wa Chama hiki. Wana-ccm hawa wakachomoa karatasi moja ya mtuhumiwa ambayo waliipenyeza kwenye meza yangu na mimi bila kumung’unya maneno LAZIMA niweke wazi suala lao kwa manufaa ya Umma. Kwa ridhio langu mwenyewe, na kama nazusha basi ntakua nimekiuka JF rules na nastahili kupigwa BAN!!, lakini nachokitoa ni uchunguzi uliojitosheleza ..


      Nasema Nape, Moses Nnauye, si MWANACHAMA HALALI wa CCM, nikiwasilisha hoja ! Viongozi wote wa CCM mjue, kamati Kuu Ijue, Sekretariat ya Chama nayo ijue HILI..


      1. Nape hana KADI ya CCM. Ingawa katiba haitaji moja kwa moja kwamba mwanachama wake itampatia kadi maalum yenye namba, ni utaratibu uliozoeleka wa kila mwanachama kuwa na kadi ya Chama Chake, Nape hana kadi Yoyote labda ya CCJ, mfukoni kwake kwa sasa. Kama atakuwa nayo basi aikate LEO baada ya kuona bandiko hili..labda. Kadi inuzwa kwa Tsh 500. Nape hana. Hana na anajua kwamba anatakiwa kuwa nayo muda wote. Na kama anayo naahidi kupigwa BAN!! Hapa JF na najiunga na CCM LEO, aniambie tu namba na tawi alilokata kadi hiyo.. HANA HANA HANA.. NASISITIZA SI MWANA CCM.

      2. katika sehemu ya pili, fungu la kwanza Ibara ya Tisa ya katiba ya CCM, inasema mwanachama anayeomba uanachama wa CCM, atajaza fomu maalum ya uanachama na kuipeleka kwa katibu wa tawi analoishi. Nape hana tawi, hakuna kumbukumbu Popote kwamba mweshimiwa Huyu aliwahi kujaza Form za mwanachama, wala tawi husika. Anaeleaelea tu . kama analo ataje tawi husika tuone form husika na lazima tuwajibike kama tumemnangia makosa.


      2. Katiba ya CCM, kwenye Ibara ya 10, Fungu hilo hilo inasema kamati ya Siasa ya halmashauri kuu ya CCM itakaa na kutoa maamuzi ya mwisho juu ya maombi ya mwanachama husika . hakuna Miniti zozote na Popote ambapo Halmashauri kuu ya CCM ilikaa na kumpitisha Nape na wengineo kwenye orodha ya Kikosi kazi hicho kwamba ni wanachama wa CCM. Kama kipo aseme tuwajibike..

      3.
      Na Ibara ya 11 ya Fungu hilo inaainisha kwamba

      Mtu akiwa mwanachama itabidi atekeleze yafuatayo.

      a).
      Atatoa kiingilio cha uanachama ( Nape hajawahi kulipa kliingilio popote hapa Duniani cha uanachama wa CCM, kama amelipia hata kama ni kuzimu atuonyeshe risiti husika)

      b). Atalipa ada ya Kila mwezi au akipenda atalipa kwa mwaka mzima (nape hajawahi kulipa ada hii jamani. Uhai wa Chama unategemea ada kutoka kwa wanachama wake, mwanachama Huyu hajawahi kulipa ada Yoyote, ni usanii sanii tu, kama anayo atuonyeshe risiti zote, au aseme amelipia kwenye tawi gani kikosi kazi kitafuatilia leo leo yeye ni kiongozi, hakuna usiri kwenye mambo haya, ni ya wazi kabisa, sijamtaka atuonyeshe account yake ina kiasi gani?, ni uhalali wa uanachama wake tu, na hili ni jambo la wazi kabisa)

      Pamoja na mapungufu mengine mengi yaliyojitokeza, kikosi kazi hicho kimebaini kwamba baadhi ya viongozi wake wakuu si wanachama wa Chama hicho. Imagine Mtu mpaka anapewa kuwa Katibu Mwenezi wa Chama, hana sifa za Uanachama, unategemea atakuwa kwa maslahi ya Chama kweli au pana agenda ya siri hapo, alihoji mjumbe mmoja.


      Ni Vema wanachama wa CCM wakawa macho na baadhi ya Viongozi wao, kauli aliyoitoa mweshimiwa huyu juzi kwamba CCM haifi hata akibaki peke yake, anamaanisha kila mtu sasa aondoke CCM ili abaki peke yake. Wazee wa mji waliokuwa kwenye kikao, wakimwelezea kwanini vijana walisusia mkutano wake , na kero ambazo zinakiandama chama, mweshimiwa huyu hakujali kujibu hoja husika badala yake alizidi kutoa matamshi tata ya kubariki watu kuondoka CCM abaki peke yake, akishabaki peke yake then, akibadili jina au..


      Hutakiwi kujibu hoja Ngumu kwa majibu laini, jipange, kanunue kadi, uwe na tawi, Lipa ada Zote, jenga chama chako, Kiongozi lazima uwe mfano, ukiona inakukera achana na Uongozi nenda kaendeleze NGO aliyoiacha Mzee.
      Last edited by Eng. Y. Bihagaze; 29th May 2012 at 13:57.
      Pathologically.."women must bear all loves" ..Atheisms .

    2. RukaaJuu Final

    3. #61
      MpigaKelele's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 6th November 2010
      Posts : 2,207
      Rep Power : 960
      Likes Received
      490
      Likes Given
      1456

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      Inawezekana akawa hana kadi ya CCM huyu Kijana, hilo hapo juu sio jibu.

      Nape: Bora ungekaa kimya kuliko kujibu ulivyojibu.

      Unajua Nape, umeniangusha sana, niliwahi kukupigia upatu kuwa utakuja kuinusuru CCM hasa uliposhupalia issue ya Jengo la Umoja wa Vijana na Uvuaji gamba. Sasa naanza kuamini kuwa nilikosea sana kwa upatu huo.

      Nape, Jamii Forums ni mahali watanzania wengi na raia wa nchi nyingine, siku hizi, wanokufahamu wanatembelea mara kwa mara, hivyo unapotoa majibu kama haya kwa swali zito kama hili unazidi kupunguza credibility ya wale waliokupa nafasi hiyo ktk chama pamoja na wewe binafsi.

      Nape kuwa makini na majibu yako.

      Ni ushauri wa MpigaKelele
      Yo Yo likes this.
      Curiosity.........
      A well tight cornered rat can bite a Cat...

    4. #62
      ALEX PETER's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th January 2012
      Posts : 100
      Rep Power : 391
      Likes Received
      21
      Likes Given
      60

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      Quote By Nnauye Jr
      Hahahaaaaaah!!!!! Chandimu nimewashika pabaya sanaaaa. Nilikuwa sijacheka siku nzima, sasa mpaka mbavu zinaumaaa......aaaaaah!hakika huku ni kutapatapa kwa hali ya juu sana......


      mbona hujibu hoja na shutuma juu yako

    5. #63
      Challenger's Avatar
      Member Array
      Join Date : 5th September 2007
      Location : Mafinga
      Posts : 53
      Rep Power : 609
      Likes Received
      18
      Likes Given
      8

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      Jamani mimi ninachojua kuwa Nape pale CCM anapita tu nyumbani kwake ni Chadema, angalia vazi analotinga (ni gwanda pure) huwa anapotezea kwa kuvaa gwanda la rangi ya kijani. Nape Muda ukifika rudi nyumbani Chadema

    6. #64
      hashycool's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2010
      Location : network search....
      Posts : 4,957
      Rep Power : 1457
      Likes Received
      559
      Likes Given
      141

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      Quote By Nnauye Jr
      Hahahaaaaaah!!!!! Chandimu nimewashika pabaya sanaaaa. Nilikuwa sijacheka siku nzima, sasa mpaka mbavu zinaumaaa......aaaaaah!hakika huku ni kutapatapa kwa hali ya juu sana......
      he! huyu vipi?
      OKW BOBAN SUNZU likes this.
      hivi vrusi vya H.I.V na wewe nani mchokozi?

    7. #65
      Tuyuku's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Posts : 658
      Rep Power : 560
      Likes Received
      139
      Likes Given
      16

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      makubwa!

    8. Miaka 50

    9. #66
      masopakyindi's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 5th July 2011
      Posts : 3,748
      Rep Power : 4197
      Likes Received
      1009
      Likes Given
      416

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      Kweli Nape hana kadi ya CCM , kama Mbowe vile vile asivyokuwa na kadi ya CDM.
      "If you don't know where you are going, any road will get you there-nowhere”

    10. #67
      Mdundulizaji's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th March 2012
      Posts : 98
      Rep Power : 456
      Likes Received
      13
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By mtotowamjini
      mtoa mada sijui ana stress gani leo...sa hapo juu umesema kua ni jambo la kawaida kuwa mwanachama wa ccm na usiwe na kadi ya ccm. Hapo hapo tena unasema Nape sio mwanachama wa ccm kwa sababu hana kadi ya ccm. Daahh wabongo bana
      naona magamba mnahaha pa kutokea; usilazimishe nukuu hewa!

    11. #68
      Shardcole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th January 2012
      Posts : 4,393
      Rep Power : 1284
      Likes Received
      1032
      Likes Given
      4

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      Jamani huyu nape hana kadi ya CCM bali anayo kadi ya UHAMSHO ya wale wazenji so kama mwenyewe ataniruhusu basi ni-apload, maana hata ccm ni tawi la uhamsho sema tu uhamsho wao wanachoma makanisa na ccm wao wanachoma kodi zetu kwa matumbo yao.

    12. #69
      Shardcole's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th January 2012
      Posts : 4,393
      Rep Power : 1284
      Likes Received
      1032
      Likes Given
      4

      Default

      Quote By Nnauye Jr
      Hahahaaaaaah!!!!! Chandimu nimewashika pabaya sanaaaa. Nilikuwa sijacheka siku nzima, sasa mpaka mbavu zinaumaaa......aaaaaah!hakika huku ni kutapatapa kwa hali ya juu sana......
      kaka kuchekacheka ni ishara ya ya ukameruni.

    13. #70
      tindikalikali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2011
      Posts : 3,081
      Rep Power : 1214
      Likes Received
      392
      Likes Given
      89

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      mpaka muda huu hujajibu chochote?

    14. #71
      Manumbu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2009
      Location : Close to U
      Posts : 1,127
      Rep Power : 724
      Likes Received
      259
      Likes Given
      760

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      Quote By Nnauye Jr
      Hahahaaaaaah!!!!! Chandimu nimewashika pabaya sanaaaa. Nilikuwa sijacheka siku nzima, sasa mpaka mbavu zinaumaaa......aaaaaah!hakika huku ni kutapatapa kwa hali ya juu sana......
      Brother can't u see hii kitu is very likely to go out of control? Bora ujibu swali au ukae kimyaa as if hujaiona hii forum. majibu mepesi au ya kejeli itaiongezea nguvu hii hoja na ku-back fire.
      "Falling Down does not mean being Buried" - Manumbu on 1st June 2011

    15. #72
      ZeMarcopolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2008
      Posts : 7,201
      Rep Power : 5040
      Likes Received
      2438
      Likes Given
      2227

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      Kinachonishangaza ni kwamba thread ambazo ziko "empty" ndizo zinachangiwa zaidi. Tumekuwa jamii inayopenda mijadala "empty", halafu tunategemea kuna siku maendeleo yataanguka kama manemane!
      Tata likes this.
      "To greed, all nature is insufficient"

    16. #73
      Ringo Edmund's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th May 2010
      Location : MDAWI
      Posts : 3,671
      Rep Power : 1361
      Likes Received
      885
      Likes Given
      586

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      ukistaajabu ya musa utayaona ya ccm.
      hilo ni jibu la katibu mwenezi wa chama kikongwe(dudu kubwa kama usemi wa wasira)
      jaribu kufikiri level ya tawi huyo mwenyekiti wa tawi atakuwaje?
      mnakumbuka kule igunga kuna kiongozi wa ccm alichoma banda la kuku akasema ni chadema?we mtu anataka kukuuwa anashindwa kuelewa tofauti ya banda la kuku na mahali mtu analala?


      sina mbavu kweli kawashika pabaya.
      ​kusema ni fedha na kusikilizwa ni zahabu.

    17. #74
      KOMBAJR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th November 2011
      Posts : 3,873
      Rep Power : 5953
      Likes Received
      803
      Likes Given
      229

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      Quote By Nnauye Jr
      Hahahaaaaaah!!!!! Chandimu nimewashika pabaya sanaaaa. Nilikuwa sijacheka siku nzima, sasa mpaka mbavu zinaumaaa......aaaaaah!hakika huku ni kutapatapa kwa hali ya juu sana......
      Jibu Hoja na siyo porojo ndiyo majibu yenu haya kumbe hata kurugenzi nao wameiga kwako.

      Hakuna Haja ya kuleta mipasho hapa kudhirisha uongo au ukweli tupia kadi yako hapo scan copy siyo porojo
      Face Reality As it Is, Not As it Was or As You Wish It To Be.

    18. #75
      SHIMBONONI's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th September 2011
      Posts : 91
      Rep Power : 406
      Likes Received
      24
      Likes Given
      35

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      Mkuu Nape, Tafadhali jibu hoja hii kuondoa Ukungu wa taarifa iliyotolewa dhidi yako.

    19. #76
      petrol's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 140
      Rep Power : 439
      Likes Received
      45
      Likes Given
      0

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      JF acheni kupoteza muda wa watu na porojo. Itakuwaje apite chujio la uteuzi za mamlaka kuu katika chama - mwenyekiti, cc na mpaka nec ya ccm? tuache kudanganyana.

    20. #77
      ghwanga's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th November 2011
      Posts : 163
      Rep Power : 413
      Likes Received
      11
      Likes Given
      26

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      jAPO NILISTUKIA ILA STILL KUNA kuna kitu cha msingi ambacho either kwa kutojua au kujua ameamua kutujuza;kwamba huaminiki ndani ya chama.Vinginevyo usingeweza kupata wazo lakuja na huu uzi au unacheka kinafiki kwa kuwa huwezi kujibu hoja.hivyoo kwa sababu wewe ni mwimbaji na mpiga gitaa mzuri,nakuomba uiongoze chichiem kuimba wimbo wa kishujaa,ushujaa wa wizi,haya anzisha,Ilale pema chichiem,ilale pema chichiem,itakua huzuznisha kujivua gamba*2,safari yake imefika ya kwenda moton*2>OOOOOOOOOOOOhh,what such a sweeety song!

    21. #78
      Eng. Y. Bihagaze's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 8th September 2011
      Location : Czech(but now in DAR)
      Posts : 769
      Rep Power : 5117
      Likes Received
      584
      Likes Given
      111

      Default

      Quote By petrol
      JF acheni kupoteza muda wa watu na porojo. Itakuwaje apite chujio la uteuzi za mamlaka kuu katika chama - mwenyekiti, cc na mpaka nec ya ccm? tuache kudanganyana.

      Petrol taratibu, nishati hiyo ambayo ni username yako ndiyo inayoleta kasheshe huko Zenji, Sio Mimi ni Katiba ya CCM , ndivyo inavyosema kwenye fungu la pili, uanachama .. Soma Kwa makini, katiba hawajatungiwa Mbwa Bali binadam wanachama husika,Na Lazima Kiongozi Yeyote ahakikishe shahada ya ufuasi Wa Chama Kwa kuzishika taratibu zote husika za Chama..
      Kama katiba wametungiwa mbwa Basi hatuna nchi Wala Kitu kinachoitwa Tanzania..
      Mimi nasema Nape Kama anataka kuendelea kuwa mwana-CCM , Basi kesho aanze kutimiza taratibu zote za uanachama .. Ni Hilo tu Wala hatutaki matatizo Na Mtu YEYOTE!! Kisim Ngriii!! Ngriiii!!
      Maganga Mkweli likes this.

    22. #79
      petrol's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 140
      Rep Power : 439
      Likes Received
      45
      Likes Given
      0

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      Salma 2015, labda hukunipata. Nilichohoji ni kwamba itawezekanaje apitishwe na waheshimiwa wakuu na vikao vizito katika ccm wakati siyo mwanachama. Unataka kujenga hoja ya ziada kuwa watu wanateuliwa bila kuhakiki hata kitu cha lazima kama uanachama wa mteuliwa. Na waliompendekeza walianza na sifa gani kama siyo mwanachama, hata kama 'mfu'. Kama unayoeleza ni kweli, na nape mwenyewe kanyamaza, basi tanzania tuna tatizo kubwa zaidi ya kustaajabu ya musa.

    23. #80
      nketi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th February 2012
      Posts : 291
      Rep Power : 425
      Likes Received
      52
      Likes Given
      7

      Default Re: Nape si mwanachama wa CCM

      NAPE NNAUYE KIJANA MNAFIKI SANA Hapo

    Page 4 of 8 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...