Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Maige: CCM itakufa

    Report Post
    Page 1 of 6 123 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 105
    1. #1
      rosemarie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 4,742
      Rep Power : 1372
      Likes Received
      285
      Likes Given
      143

      Default Maige: CCM itakufa

      MBUNGE wa Jimbo la Msalala na Waziri wa zamani wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, amedai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kitakufa kutokana na tabia ya viongozi wake kuendesha chama kwa kuegemea majungu na wivu wa madaraka.Kauli hiyo aliitoa jana katika ofisi za CCM wilaya ya Kahama, mbele ya mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja na viongozi wengine wa mkoa na wilaya.Maige alidai kuwa vitendo vya majungu na uongo uliokithiri vimechukua nafasi kubwa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali, hali ambayo itasababisha chama hicho kupoteza uwezo wa kuongoza na kuanguka.Alidai kuwa viongozi wachapakazi na wazalendo kwa nchi yao, wamekuwa wakipigwa vita kali na baadhi ya watendaji serikalini, bungeni na ndani ya chama hicho kwa maslahi binafsi.Maige alisema hasikitiki kuondolewa katika nafasi ya uwaziri, bali kinachomuuna ni kutimuliwa bila hata kupewa nafasi ya kujieleza katika ngazi zote husika ndani ya serikali na chama.“Sikupewa nafasi yoyote, iwe ni katika kamati za Bunge au ndani ya chama kama zilivyo kanuni zetu. Hakuna aliyetaka kunisikiliza, na wengi waliosikia uzushi wa tuhuma zangu, waliamini na kuchukua maamuzi,” alisema.Alidai kwa kipindi chote alichokuwa waziri, alipambana na mambo mengi mazito kwa kuzingatia kuwa wizara hiyo ni nzito na yenye utajiri mkubwa, lakini ameshangaa kuona kuwa mwisho wa uzalendo wake ni kuondolewa kwa aibu.“Silalamiki kuondoka kwa vile hiyo ilikuwa ni dhamana, lakini sikufurahishwa kuondolewa kwa tuhuma ambazo kwanza sio za kweli, na pili sikupewa fursa ya kuzijibu kwa ufasaha na kwa uchambuzi makini wa kitaalamu. Hii ni hatari kwa sababu inaua chama kwa kupoteza watendaji wenye uchungu na taifa lao,” alisema mbunge huyo.Alilaani kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM kushabikia kuondolewa kwake kwenye uwaziri ambapo walidhihirisha namna ambavyo si wakomavu wa kisiasa kwa kudhani kwamba wanamkomoa pasipo kuzama kwa kina na kubaini kuwa wao ndio watakaoathirika hasa kwa kuwa posho zao na mishahara zinatokana na jimbo hilo kuendelea kuwa mikononi mwa CCM na si vinginevyo.Alidai kuwa fitina na majungu aliyofanyiwa na viongozi wenzake ndani ya chama hicho, yamewakera wana CCM wengi, kiasi kwamba wazee zaidi ya 300 wa jimbo lake wamemfuata wakitaka awaeleze msimamo wake ikiwa atahama ama ataendelea kuwa ndani ya CCM.“Wamekuja wazee hawa, wanawake kwa wanaume na vijana wengi, wakisikitika na kile kilichonitokea. Wanataka niwaambie kama nabaki CCM au naondoka, ili nao wanifuate,” alisema.Aliongeza kuwa kwa kuwa yeye ni zao la wananchi wa Msalala, ni jukumu la wananchi kumuamlia hatima yake, na yeye atakuwa mtiifu kwao.Maige alidai inasikitisha kuona kuwa kuna nguvu kubwa za upinzani nchini, hususan chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakati wao CCM wamekalia majungu na fitina zisizo na maana.Hivyo, ametahadharisha kuwa wana CCM, wasishangae jimbo hilo likichukuliwa na wapinzani katika uchaguzi mkuu ujao, na wala hatakuwa na hasara.Aliongeza kuwa CCM yenye nyenzo zote za usafiri ikiwemo magari na pikipiki, imeshindwa kuhamasisha watu wilayani kote lakini CHADEMA wasiokuwa hata na baiskeli wamepita jimbo zima wakifanya mikutano yao na kugawa bendera zao kama njugu.Maige alimshambulia Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, akidai kuwa alipeleka taarifa ya uongo na iliyojaa unafiki kwa lengo la kumng’oa kwenye uwaziri na kwamba ndio maana baada ya lengo lao kutimia walitimkia Japan kujipongeza.Alimtaka Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa Kahama, kwa kuwa ametekeleza lengo lake la kumng’oa kwenye uwaziri sasa waketi meza ya mazungumzo kuwaletea maendeleo wananchi wa Kahama kwa kuwa kabla ya kupata wadhifa huo walikuwa marafiki na walitembea pamoja kwenye majimbo yote ya Kahama na Msalala kwenye mikutano yao.Naye Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Kahama, Hamad Masoud, alisema suala la ugomvi kati ya wabunge hao litafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya chama ili liweze kufanyiwa kazi.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja aliwapa pole wana Kahama kwa kile alichodai kumpoteza mpiganaji, na zawadi kwa wananchi wa eneo hilo, hivyo kuichezea bahati hiyo ni ujinga kwa wale wasiopenda maendeleo.“Nafasi hizi hutolewa na Rais na haulizwi; ndivyo hivyo anapoamua kumpumzisha aliyemteua pia haulizwi. Inapotokea eneo kupata waziri ni fursa nzuri ya kupiga hatua katika maendeleo leo Kahama fursa hiyo haipo tena,” alisema Mgeja.

      Tanzania Daima
      Last edited by rosemarie; 29th May 2012 at 09:02.
      Rutashubanyuma likes this.
      ccm inakufa,asante mungu umesikia kilio chetu!!!!!!!

    2. #2
      Wizzo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th November 2010
      Location : Arusha
      Posts : 440
      Rep Power : 522
      Likes Received
      82
      Likes Given
      34

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      pole maige, hamia kwenye basi kubwa cdm usibanane kwenye hako kabito ambacho kila m2 anataka kua dereva au akae siti ya mbele

    3. #3
      CHUAKACHARA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd June 2011
      Posts : 3,065
      Rep Power : 7655
      Likes Received
      998
      Likes Given
      762

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Quote By episodes View Post

      Maige asilete talalila, aueleze umma wa watanzania, dola 700,000 amezipata wapi< Mbona kabla ya kuwa waziri alikuwa hajazipata? asiwafanye wote wajinga
      Unstoppable likes this.

    4. #4
      WATANABE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 783
      Rep Power : 575
      Likes Received
      272
      Likes Given
      83

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Quote By episodes View Post
      MBUNGE wa Jimbo la Msalala na Waziri wa zamani wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, amedai kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kitakufa kutokana na tabia ya viongozi wake kuendesha chama kwa kuegemea majungu na wivu wa madaraka.Kauli hiyo aliitoa jana katika ofisi za CCM wilaya ya Kahama, mbele ya mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja na viongozi wengine wa mkoa na wilaya.Maige alidai kuwa vitendo vya majungu na uongo uliokithiri vimechukua nafasi kubwa kwa baadhi ya viongozi wa ngazi mbalimbali, hali ambayo itasababisha chama hicho kupoteza uwezo wa kuongoza na kuanguka.Alidai kuwa viongozi wachapakazi na wazalendo kwa nchi yao, wamekuwa wakipigwa vita kali na baadhi ya watendaji serikalini, bungeni na ndani ya chama hicho kwa maslahi binafsi.Maige alisema hasikitiki kuondolewa katika nafasi ya uwaziri, bali kinachomuuna ni kutimuliwa bila hata kupewa nafasi ya kujieleza katika ngazi zote husika ndani ya serikali na chama.“Sikupewa nafasi yoyote, iwe ni katika kamati za Bunge au ndani ya chama kama zilivyo kanuni zetu. Hakuna aliyetaka kunisikiliza, na wengi waliosikia uzushi wa tuhuma zangu, waliamini na kuchukua maamuzi,” alisema.Alidai kwa kipindi chote alichokuwa waziri, alipambana na mambo mengi mazito kwa kuzingatia kuwa wizara hiyo ni nzito na yenye utajiri mkubwa, lakini ameshangaa kuona kuwa mwisho wa uzalendo wake ni kuondolewa kwa aibu.“Silalamiki kuondoka kwa vile hiyo ilikuwa ni dhamana, lakini sikufurahishwa kuondolewa kwa tuhuma ambazo kwanza sio za kweli, na pili sikupewa fursa ya kuzijibu kwa ufasaha na kwa uchambuzi makini wa kitaalamu. Hii ni hatari kwa sababu inaua chama kwa kupoteza watendaji wenye uchungu na taifa lao,” alisema mbunge huyo.
      Alilaani kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM kushabikia kuondolewa kwake kwenye uwaziri ambapo walidhihirisha namna ambavyo si wakomavu wa kisiasa kwa kudhani kwamba wanamkomoa pasipo kuzama kwa kina na kubaini kuwa wao ndio watakaoathirika hasa kwa kuwa posho zao na mishahara zinatokana na jimbo hilo kuendelea kuwa mikononi mwa CCM na si vinginevyo.
      Alidai kuwa fitina na majungu aliyofanyiwa na viongozi wenzake ndani ya chama hicho, yamewakera wana CCM wengi, kiasi kwamba wazee zaidi ya 300 wa jimbo lake wamemfuata wakitaka awaeleze msimamo wake ikiwa atahama ama ataendelea kuwa ndani ya CCM.“Wamekuja wazee hawa, wanawake kwa wanaume na vijana wengi, wakisikitika na kile kilichonitokea. Wanataka niwaambie kama nabaki CCM au naondoka, ili nao wanifuate,” alisema.Aliongeza kuwa kwa kuwa yeye ni zao la wananchi wa Msalala, ni jukumu la wananchi kumuamlia hatima yake, na yeye atakuwa mtiifu kwao.Maige alidai inasikitisha kuona kuwa kuna nguvu kubwa za upinzani nchini, hususan chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakati wao CCM wamekalia majungu na fitina zisizo na maana.Hivyo, ametahadharisha kuwa wana CCM, wasishangae jimbo hilo likichukuliwa na wapinzani katika uchaguzi mkuu ujao, na wala hatakuwa na hasara.Aliongeza kuwa CCM yenye nyenzo zote za usafiri ikiwemo magari na pikipiki, imeshindwa kuhamasisha watu wilayani kote lakini CHADEMA wasiokuwa hata na baiskeli wamepita jimbo zima wakifanya mikutano yao na kugawa bendera zao kama njugu.Maige alimshambulia Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, akidai kuwa alipeleka taarifa ya uongo na iliyojaa unafiki kwa lengo la kumng’oa kwenye uwaziri na kwamba ndio maana baada ya lengo lao kutimia walitimkia Japan kujipongeza.Alimtaka Lembeli ambaye pia ni Mbunge wa Kahama, kwa kuwa ametekeleza lengo lake la kumng’oa kwenye uwaziri sasa waketi meza ya mazungumzo kuwaletea maendeleo wananchi wa Kahama kwa kuwa kabla ya kupata wadhifa huo walikuwa marafiki na walitembea pamoja kwenye majimbo yote ya Kahama na Msalala kwenye mikutano yao.Naye Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Kahama, Hamad Masoud, alisema suala la ugomvi kati ya wabunge hao litafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya chama ili liweze kufanyiwa kazi.Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja aliwapa pole wana Kahama kwa kile alichodai kumpoteza mpiganaji, na zawadi kwa wananchi wa eneo hilo, hivyo kuichezea bahati hiyo ni ujinga kwa wale wasiopenda maendeleo.“Nafasi hizi hutolewa na Rais na haulizwi; ndivyo hivyo anapoamua kumpumzisha aliyemteua pia haulizwi. Inapotokea eneo kupata waziri ni fursa nzuri ya kupiga hatua katika maendeleo leo Kahama fursa hiyo haipo tena,” alisema Mgeja.

      Tanzania Daima
      Jimbo kuwa mikononi mwa CCm na na viongozi na watendaji wa CCm kupata posho vina uhusiano gani au ndio yale yale ya Homa Shopping Centre nkatika madini yetu?

    5. #5
      Mkirua's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2010
      Posts : 3,557
      Rep Power : 1066
      Likes Received
      1288
      Likes Given
      622

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Huyu jamaa naye anatia aibu sasa... wangapi wameondolewa uwaziri kwani alikuwa na ubia na hiyo nafasi?? Mbona ananung'unika as if ilikuwa ajira?
      kibebii and Maundumula like this.
      The world suffers a lot. Not because of the violence of bad people, but because of the silence of good people!

    6. #6
      Lu-ma-ga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2010
      Posts : 1,934
      Rep Power : 834
      Likes Received
      546
      Likes Given
      8

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Maige mwizi mkubwa wewe leo ndiyo umegundua uozo wa ccm acha uzezeta wewe msukuma.Mbona tunasikia kule bulyankuru gold mine ulikuwa kwenye payroll, umewasaliti wana msalala na kukubali pension ya Bearrick.

    7. #7
      makoye2009's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2009
      Posts : 1,454
      Rep Power : 807
      Likes Received
      396
      Likes Given
      298

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Maige anaonekana kuumizwa sana na kunyang'anywa Uwaziri.

      Mimi nampa ushauri wa bure. Kwamba kama ana uhakika kuwa YUKO CLEAN ila tu wenzake ndani ya Chama chao cha Magamba-CCM wamemfanyia fitna,hujuma na majungu basi RUKSA KUHAMIA CHADEMA. Namwomba aingie kwenye mdundo wa CHADEMA wa VUA GAMBA,VAA GWANDA.

      CHADEMA tutakuwa tumejihakikishia jimbo la Msalala kulichukua mwaka 2015. Lakini tutamkaribisha kwa tahadhari kubwa. Kama akileta porojo za Vuvuzela Shibuda tutamtimua. CHADEMA siyo kichaka cha MAFISADI.

      Naamini hata uongozi wa juu wa CHADEMA hautasita kumkaribisha.

      TULIHO BABA NG'WANA MAIGE!

    8. #8
      MAMENGAZI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 718
      Rep Power : 572
      Likes Received
      105
      Likes Given
      89

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      kweli sheikh yahya R.I.P aliacha urithi mkubwa, watabiri wamekua wengi, tunaomba utabiri wako uwe kweli mheshimiwa mbunge, kife na kusiwepo wa kukifufua
      kibebii likes this.

    9. #9
      fikirikwanza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th January 2012
      Posts : 716
      Rep Power : 517
      Likes Received
      156
      Likes Given
      18

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Asahihishe kauli yake, CCM imeshakufa!!! kinachosubiriwa ni mazishi, ndugu wa karibu na mbali kama CUF, TLP na NCCR wamekwisha fika eneo la msiba, wanasaidiana kuandaa mazishi huko Znz, na Bungeni Tz.

    10. #10
      makoye2009's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2009
      Posts : 1,454
      Rep Power : 807
      Likes Received
      396
      Likes Given
      298

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Quote By CHUAKACHARA View Post
      Maige asilete talalila, aueleze umma wa watanzania, dola 700,000 amezipata wapi< Mbona kabla ya kuwa waziri alikuwa hajazipata? asiwafanye wote wajinga
      Maige amesema kwamba fedha aliyotumia kununulia hilo jumba ni pesa YA MKOPO KUTOKA BENKI WALIYOKOPESHWA KWA DHAMANA YA SERIKALI. Hiyo ni kwa WABUNGE wote .Yeye pesa yake kanunulia nyumba na Wabunge wengine wamefungua BIASHARA ambazo hawalipii hata kodi. Gharama ya nyumba anadai haifiki hizo dola kati ya 400,000-700,000 na amewaambia TAKUKURU waende kwa wakala wa uuzaji nyumba watapata bei halisi ya nyumba hiyo!

      Tunajua TAKUKURU wako kazini baada ya muda mfupi tutapata majibu nani anasema ukweli.

    11. #11
      NATA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th May 2007
      Posts : 4,259
      Rep Power : 8420
      Likes Received
      1135
      Likes Given
      390

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Atakufa yeye CCM ataaiacha, ife kwanini?

      Kwasababau yeye ameumbuliwa?
      who is Maige ndani ya CCM?
      Maundumula likes this.

    12. #12
      TaiJike's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2011
      Posts : 1,156
      Rep Power : 611
      Likes Received
      387
      Likes Given
      348

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Huu ndio undumila kuwili, kama kweli ye alistahili kwanini hakuibua haya manug'uniko yake ambayo kila kukicha sasa anazua toka amepigwa tiper.
      * Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi? * - Julius Kambarage Nyerere

    13. #13
      Ndachuwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2006
      Location : ARUSHA
      Posts : 2,685
      Rep Power : 1222
      Likes Received
      551
      Likes Given
      425

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Quote By Mkirua View Post
      Huyu jamaa naye anatia aibu sasa... wangapi wameondolewa uwaziri kwani alikuwa na ubia na hiyo nafasi?? Mbona ananung'unika as if ilikuwa ajira?
      Waliondolewa ni wengi lalini kumbuka kina Mkulo na Omari Nundu wale ni wastaafu wakati Maige ana zaidi ya miaka 20 afike umri wa kustaafu
      "Effective leadership is not about making speeches or being liked; leadership is defined by results not attributes" Peter Drucker

    14. #14
      majebere's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 2,348
      Rep Power : 0
      Likes Received
      338
      Likes Given
      120

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      mchukueni CDM huyu. CCM wamesha mstukia.

    15. #15
      CAMARADERIE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd March 2011
      Location : 1 Luthuli Street
      Posts : 4,163
      Rep Power : 2724
      Likes Received
      1590
      Likes Given
      1145

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      CCM itakufa kwa kuwa amepokwa uwaziri au kwa sababu gani?
      A compliment is something like a kiss through a veil

    16. #16
      Gagnija's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th April 2006
      Posts : 2,097
      Rep Power : 1092
      Likes Received
      697
      Likes Given
      480

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      CDM isipokuwa makini muda si mrefu itajikuta imevamiwa na majambazi wengi wa CCM kama ngao ya kujikinga na ouvu wao. That's what they did in Kenya after the ouster of KANU.
      If you are neutral in situations of injustice, you have chosen the side of the oppressor. Tutu

    17. #17
      Joseph's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2007
      Location : Zanzibar
      Posts : 2,812
      Rep Power : 1236
      Likes Received
      739
      Likes Given
      476

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Mnafiki mkubwa Maige,unabwabwaja kama mwanamke wa uswahilini,kama unaona chama chako hakikufai basi ondoka si unakaa kulalama bila kuchukua hatua.
      You can never have someone praise you,nor will anyone condemn you,never in the past,not at present and never will be in the future.

    18. #18
      Basluma Original's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th May 2012
      Posts : 33
      Rep Power : 362
      Likes Received
      8
      Likes Given
      0

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Anasema Ccm itakufa, anataka ife mara ngapi? Hajui kuwa CCM ni chama ambacho kinaongoza huku kikiwa marehemu?, washukuru sana wananchi wengi wa Tanzania kuwa mbumbumbu tofauti na hivyo sasa wangekuwa wanaongelea pumba zao kaburini.
      .
      "LONELINESS IS THE MOST TERRIBLE POVERTY".
      makoye2009 likes this.

    19. #19
      Gagnija's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th April 2006
      Posts : 2,097
      Rep Power : 1092
      Likes Received
      697
      Likes Given
      480

      Default Re: Maige: CCM itakufa

      Quote By majebere View Post
      mchukueni CDM huyu. CCM wamesha mstukia.
      Na CDM walivyo na papara, sitashangaa kweli wakilichukua hili garasa.
      If you are neutral in situations of injustice, you have chosen the side of the oppressor. Tutu

    20. #20
      Nyakageni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st February 2011
      Posts : 5,576
      Rep Power : 1611
      Likes Received
      816
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By NATA View Post
      Atakufa yeye CCM ataaiacha, ife kwanini?

      Kwasababau yeye ameumbuliwa?
      who is Maige ndani ya CCM?
      waziri 'mstaafu' aliyekimbia na masanduku ya kura za urais. Hakuna ajuaye JK alipata kura ngapi wala dr. Slaa wala Tume

    Page 1 of 6 123 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...