Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape

    Report Post
    Page 6 of 8 FirstFirst ... 45678 LastLast
    Results 101 to 120 of 145
    1. #1
      OMEGA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2011
      Posts : 392
      Rep Power : 476
      Likes Received
      111
      Likes Given
      51

      Default Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape

      Wakuu nimeinasa sehemu nikaona niiweke hapa jamvini

      TAMKO LA VIJANA WA BUKOBA MJINI WAISHIO DAR ES SALAAM

      Ujio wa Nape: Kagera Tumedharauliwa na Uzalendo Umedhihakiwa

      Tumejaribu kutafakari kwa kina juu ya nini hasa kilimsukuma Nape kufika Kagera na kushiriki mazishi ya muasisi wa TAA, mzalendo na mpigania uhuru aliyetelekezwa na Taifa lake, Dr. Vedasto Kyaruzi na bado ki-ukweli hatujapata majibu.

      Tunapata shida kujua dhima ya safari ya Nape kwa kuwa shughuli mahsusi alizozifanya akiwa Kagera zina kinzana kimaadili na kitamaduni na maombolezo ya misiba ya Kiafrika na hasa misiba ya Kihaya. Mjumbe aliyetumwa mahsusi toka mbali kupeleka pole kwenye msiba hategemewi atumie muda wake mwingi majukwaani kufanya siasa, tena katika mazingira ya ugenini lakini kwenye maeneo yale yale msiba unapoendelea. Kwa mpita njia ambaye amefahamishwa tukio na akahiari kufika msibani, akiendelea na shughuli zake haitakuwa ajabu na hakuna mtu mwenye akili timamu atamshangaa hata kidogo.

      Nape aliingia Bukoba tarehe 25/05/2012. Na ni uungwana kukiri kuwa alifika Kashai-Matopeni msibani kutoa salamu za pole. Lakini baada ya hapo alielekea Missenyi ambako tunaarifiwa alikuwa na mikutano ya hadhara. Watanzania mtakumbuka vema kuwa katika mikutano hiyo ndiko Nape alitoa kauli ya kutokuwa tayari kukabidhi nchi kwa wahuni! Labda ili Watanzania muweze kupima vema uelewa na akili za Nape, tuwafahamishe kuwa Missenyi ndiko iliko Kyaka na ambako maziko ya Dr. Kyaruzi yamefanyika. Tunashindwa kuelewa, hiyo mikutano ilikuwa safisha njia ya mazishi au inahusiana vipi na mtu aliyepeleka ujumbe wa maombolezo?

      Linalochanganya zaidi ni hili la Jumamosi tarehe 26/05/2012. Hii ndiyo siku ambayo Dr. Kyaruzi alipumzishwa rasmi kaburini alale kwa amani. Lakini kwa Nape akiwa Kyaka hii ilikuwa siku maalumu ya kufungua matawi na kutangaza operation yake mpya ya kisiasa iitwayo “Vua Gamba, vua Gwanda, Vaa Uzalendo”. Katika hili, ukiachilia ukinzani wa matukio kimaadili na kitamaduni, tunapata mishangao mingine; hivi Nape alikwenda Kyaka kuzika au kuzindua operation ya kisiasa? Na Je, huyu kijana anahubiri uzalendo upi? Uzalendo usiokuwa na utamaduni, Uzalendo wa kuwatelekeza na kushindwa kuwaenzi watu waliopigania uhuru wa nchi hii? Kama huo ndiyo uzalendo anaohubiri Nape, basi hauhitaji operation wala kampeni maana tayari tunao magwiji. Na hapo kwa tafsiri hii, ujio na matukio ya Nape kwenye maeneo ya msiba huu vinanapata maana halisi.

      Katika Taarifa ya Uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Chama Tawala kimearifiwa kuwa moja ya kosa lililofanyika ni kumteua mgombea ambaye mila hazikuwa zinampa fursa na tafsiri njema kufanya shughuli kama ya siasa katika muda mfupi baada ya msiba wa Baba yake. Ikiwa kosa hili la Kitamaduni limechangia Chama kupoteza Jimbo, basi pia chama kiwe tayari kwa makosa ya Nape kupoteza zaidi ya Kijiji cha Burifani na Kata nzima ya Kyaka. Na hatutoshangaa iwapo Nape au Taasisi iliyomtuma ikishindwa kuomba radhi!

      Mbali na vioja vya Nape hapo juu, kwa wasifu wa marehemu Dr. Kyaruzi, kila mmoja atakubaliana nasi kuwa Taasisi yoyote (iwe dola au chama) kuwakilishwa na mtu wa ngazi ya Nape ni dharau ya hali ya juu na ichukuliwe ni dhihaka si kwa jamii iliyostaharabika tu, bali hata kwa watu walipendao Taifa lao na kuuenzi Uzalendo. Inakuwa vigumu kuamini kuwa pamoja na ugumu wa ratiba, Rais alikosa muwakilishi makini wa hadhi inayobeba uzito sawia na mchango wa Dr. Kyaruzi katika Taifa hili. Tukio hili linaleta hisia za ubaguzi wa Taasisi za dola na chama katika kutoa uzito kwenye majanga, matatizo na misiba ya watu wa Taifa hili.

      Ni majuzi tu Taifa lilipotelewa na Mcheza Sinema nguli ambaye hapo awali hakuwahi kupata heshima yoyote ya Kitaifa. Lakini tuliona jinsi viongozi wa Serikali na Chama walivyohamia msibani na Serikali kujipa jukumu la kuubeba msiba na shughuli za mazishi. Haikupita muda, Rais akiwa ziarani Marekani, Rais wa Malawi alifariki duniani. Pamoja na uchovu wa safari tulimwona Rais akiingia nchini na kutoka kuwahi mazishi ya Rais wa nchi jirani. Kulingana uzito na umuhimu uliowekwa na Rais katika msiba huu, hakusubiri hata atatue matatizo makubwa yaliyokuwa yanaikabili serikali yake kiasi cha kutishiwa kuanguka. Lakini pia ni kawaida kusoma taarifa za Rais anazoandika katika mitandao ya kijamii (MyKj) kila anapoelekea kwenye misiba ya watu wa kawaida walioko katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam. Hili linatuongezea huzuni na kutuongoza kuamini kuwa misiba ya watu wa maeneo nje na Dar es Salaam haigusi hisia za Rais hata kama ni ya Watu waliotoa mchango mkubwa kwa Taifa hili.

      Haya yaliyotokea kwa Dr. Kyaruzi alimanusura yatokee pia kwenye msiba wa MKUU wa Majeshi Mstaafu Jenerali Ernest Mwita Kyaro. Marehemu Mwita alifariki siku chache baada ya mazishi ya Kanumba na msiba wake ulikosa sura ya Kitaifa. Isingekuwa kelele za wana-Mitandao ya Kijamii (MyKj) na wahandishi wa habari, hata Bunge lisingesimama kwa dakika moja kutoa salamu. Tabia hii ya kutelekeza wazalendo wa Taifa hili inaonekana kumea kwa kasi. Na uthaminisho wa serikali kwa watu wa Dar es Salaam unaonekana kuwa juu kuliko wa wale walioko nje ya Dar es Salaam.

      Kwa Tamko hili tunamtaka Nape Nnauye, Katibu Mwenezi wa CCM kama kweli alikuja kuwakilisha Taasisi yoyote katika msiba wa Dr. Kyaruzi, basi aiombe radhi jamii yetu kwa dharau kubwa aliyoonyesha katika msiba huu. Na kama alikuwa mpita njia tu, basi atujuze ili Jamii na historia ya Taifa imwandike rasmi Dr. Kyaruzi kama muasisi wa TAA na mzalendo aliyepigania uhuru wa Taifa lake ambaye hakuenziwa wakati wa uhai wake na hata mazishi yake hayakuhudhuriwa na mwakilishi wa Kitaifa.

      Na mwisho tunamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, yeye kama Taasisi awe Rais wa Watanzania wote; wa Dar es Salaam na Mikoani.

      Asiye na Utamaduni ni Mtumwa. Tanzania ni Moja

      Imetolewa na:
      Erick Mwemezi Kimasha
      Mhamasishaji Jamii Mkuu
      Vijana wa Bukoba Mjini Waishio Dar es Salaam

      Barua Pepe:
      [email protected]
      Simu: 0713-177-372

      Tarehe: 27/05/2012

      MAJIBU YA NAPE
      Quote By Nnauye Jr
      Nimesikitishwa sana sana NA UPOTOSHAJI MKUBWA UNAENDELEA KATIKA SAFARI YANGU YA KWENDA KAGERA! KILICHONIUMA ZAIDI NI JINSI WATU WANAVYOTAKA KUTUMIA MSIBA KAMA NGAO YAO YA KUPOTOSHA UKWELI WA SWALA ZIMA LA SAFARI YANGU KAGERA. KWA WASIOJUA AU WALIOAMUA KUPOTOSHA UKWELI KWA MAKUSUDI, DR. KYARUZI ALIKUWA RAFIKI MKUBWA WA MAREHEMU BABA YANGU MZAZI BRIG. GEN MOSES NNAUYE, HIVYO MAREHEMU KYARUZI NI SAWA NA BABA YANGU. NINA LAANI JUHUDI ZA KUTAKA KUTUMIA ZIARA YANGU KAGERA NA MSIBA WA MZEE WANGU KYARUZI KISIASA.

      NAOMBA IJULIKANE KUWA KAGERA SIKWENDA RASMI KWA AJILI YA KUHANI MSIBA, ISIPOKUWA NILIKWENDA KWA SHUGHULI ZANGU ZA KICHAMA NA KWAKWELI NILIJUA MAZISHI YAMESHAFANYIKA YA DR. KYARUZI NIKIWA DAR NIKAMWOMBA KATIBU WA MKOA KUWA NIKIWA MISENYI NIENDE NYUMBANI KUWASALIMIA WAFIWA, AKANIAMBIA HAWAJAZIKA, NA ILIKUWA WAZIKE KESHO YAKE YA SIKU NILIYOENDA KAGERA, NIKAMWAMBIA BASI NITAPITA MSIBANI KUTOA POLE. NA NDIVYO NILIVYOFANYA , NILIPOFIKA TU NIKAENDA KUTOA POLE NDIO NIKAENDELEA NA SHUGHULI ZILIZONIPELEKA KAGERA.KAGERA SIKWENDA KUHANI MSIBA NILIKWENDA KWA SHUGHULI YA VIJANA, SI BUSARA HATA KIDOGO KULAUMU BILA KUULIZA HASA KWA MHUSIKA. NINASIKITISHWA NA UAMUZI WA MWANDISHI KUJIPA USEMAJI WA VIJANA KAGERA NA KUSHINDWA HATA KUWAULIZA WAHUSIKA MAANA WAPO KAGERA NAPE ALIFUATA NINI KAGERA.

      LAKINI KUDHIHIRISHA NIA MBAYA YA MWANDISHI, MWANDISHI KAAMUA KUDANGANYA UMMA KUWA NILIKUWEPO KAGERA SIKU YA MAZISHI YA DR. KYARUZI, AMA KAAMUA KUKOLEZA KUSUDI LAKE BAYA AU HAJUI ALICHOKISEMA, UKWELI NI KWAMBA TAREHE 25/05/2012 NILIKWENDA KAGERA NA KURUDI DSM SIKU HIYOHIYO SASA HUYO NAPE WA TAREHE 26 NI YUPI? NI VIZURI KUPIMA TUHUMA KABLA YA KUZITOA.

      NINA MSAMEHE BURE MWANDISHI NA ALIOSHIRIKIANA NAO.
      TAMUCHUNGU likes this.

    2. Miaka 50

    3. #101
      Ulukolokwitanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th September 2010
      Location : ndzengelendete
      Posts : 2,589
      Rep Power : 1069
      Likes Received
      1429
      Likes Given
      259

      Default Re: NAPE afafanua ziara yake ya Bukoba na mazishi ya Dr. Kyaruzi.

      Wala sishangai kwa nini hukujua kama mazishi yameishafanyika au bado. Mara nyingi nyie watoto wa NJE YA NDOA ni vigumu kuwa na ukaribu na marafiki wa baba zenu.

    4. #102
      Kalumbesa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2010
      Location : Shamba
      Posts : 867
      Rep Power : 604
      Likes Received
      267
      Likes Given
      120

      Default Re: Tamko la vijana kutoka Kagera juu ya Nape

      Quote By Maundumula
      Shughuli za Chama ilibidi ziendelee regardless, mambo ya kuua ndege wawili...kwa hili namtetea Nape
      Nape amesema alikuwa anamheshimu kama marehemu baba yake mzee Nnauye,kwa hiyo wewe unamtetea ni sawa asihudhurie mazishi ya mtu anayemweshimu kama mzazi wake kisha aende kufanya shughuli za chama na kucheza gofu?huu ndio uzalendo anao utangaza sio?
      The ballot is stronger than the bullet - Abraham Lincoln

    5. #103
      regam's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th January 2011
      Posts : 223
      Rep Power : 473
      Likes Received
      36
      Likes Given
      3

      Default Re: Tamko la vijana juu ya Nape

      Nawewe nape unajichanganya. Kilichozungumzwa na mwandishi ni kwamba wewe hukuonyesha ushiriki mkamilifu.
      umeanza kwa kusema marehemu ni sawa na baba yako sasa iweje uendelee na shughuli za kichama ilihali ulitaarifiwa kwamba bado hawajazika?
      endelea na hiyo tabia ili utuudhi wengi.

    6. #104
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1742
      Likes Received
      1518
      Likes Given
      2835

      Default Re: Tamko la vijana kutoka Kagera juu ya Nape

      watanzania bana mbona mnapenda sana kukuza vitu vidogo, ku-complicatate maisha namna hii!!!

      hili tamko ni la kipuuzi na linaonyesha ego ya wahaya....kama Nape ni mhaya sasa wamlaumu, na bado kama muhaya hizo mila na desturi it has nothing to do with msiba na shughuli za chama

      ebu tuelezeni je

      baa zimefungwa huko kwenu?
      mmewazuia watu wasilale na wake zao huko?
      wangapi wamhudhuria mazishi?

      acheni matamko matamko haya yanaonesha ujinga wetu kwenye mambo ya msingi

      kila siku watu wanakufa, kila kitu kisimame basi
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    7. #105
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1742
      Likes Received
      1518
      Likes Given
      2835

      Default

      Ujinga tu huu na wastage of time!!

      Hebu tuelezeni je,

    8. RukaaJuu Final

    9. #106
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1742
      Likes Received
      1518
      Likes Given
      2835

      Default Re: NAPE afafanua ziara yake ya Bukoba na mazishi ya Dr. Kyaruzi.

      Quote By Ulukolokwitanga
      Wala sishangai kwa nini hukujua kama mazishi yameishafanyika au bado. Mara nyingi nyie watoto wa NJE YA NDOA ni vigumu kuwa na ukaribu na marafiki wa baba zenu.
      Ulukolokwitanga una hakika baba yako unayemjua ndiye baba yako mzazi??

      ebu acha ujinga , acha personal attack sio kila mtu atafurahia comment yako!! think big kuna watoto wa nje ya ndoa wengi humu will they be happy to read your comment?

      pumbavu!!
      Shakazulu likes this.
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    10. #107
      jigoku's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2011
      Posts : 1,445
      Rep Power : 1003
      Likes Received
      365
      Likes Given
      537

      Default Re: Tamko la vijana kutoka Kagera juu ya Nape

      Nape usiwe mbishi mdogo wangu, frankly speaking unapotea sana,unajichanganya kila siku, unakurupuka kila unapotokeza,na hata hao ccm-magamba wanakutumia tu lakini hawaishi kukujadili jinsi unavyowaharibia au unavyoiua CCM yao, ungekuwa unatumia akili yako vizuri ungelijua nini cha kufanya, leo ni magamba wenzio ndio wanaokufagilia lakini ni aibu jinsi unavyojitokeza kushindana na umma unaotaka mabadiliko.

      Mbaya zaidi umekuwa mbishi kupita kiasi,hivi kwa hili la msiba wa Dr Kyaruzi huoni kama wewe binafsi umeeonekana huna maadili? Mzee Nnauye ambae alikuwa mwalimu wa baba yangu pale Kivukoni alikuacha ukiwa huna maadili. Hivi kwa nafasi yako katika chama hujui kuwa nafasi yako ni ya kitaifa, hukuja kama kupita kusalimia kwenye msiba mkubwa kama huo na kisha ukaendelea na kazi yako ya chama mfu hukutenda sawa na utamaduni wa kiafrika? Sisi kwetu usukumani ukifanya hivyo ujue adhabu yako ni kutengwa na jamii na ili uungane na jamii tena lazima ulipe faini, na uwaalike wazee na wanazengo kisha uombe msamaha wazi wazi. Sasa leo ulivyokuwa huwezi kutafakari mambo uliona ni sawa upite usalimie kisha uendelee kutangaza msiba wa CCM.

      Huyu aliyeleta uzi huu ni mwema sana, sio mnafiki anataka ujirekebishe, na uwe unapima mabo kabla ya kufanya, ila kwa kutokujua kwako umenuna.

      Kwetu sisi tunaona endelea hivyo hivyo ili kazi ya kuwapiga chini iwe nyepesi, maana Mungu anatusaidia kwa njia kama hii ya kina nape kupoteza mila, desturi na tamaduni za kiafrika hasa Tanzania.

    11. #108
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1742
      Likes Received
      1518
      Likes Given
      2835

      Default Re: NAPE afafanua ziara yake ya Bukoba na mazishi ya Dr. Kyaruzi.

      Quote By Kiranga
      Nape is semi-literate for starters, barely able to maintain the basic rules of writing.

      Huyu ndiye kada mkubwa kabisa wa chama anayeandaliwa kuchukua madaraka makubwa zaidi baadaye.

      SMH!
      hamna bana una complicate mno!! boring to read your comment and the way u have presented it!! what is he has written under pressure of counter attacking this??

      after all nani hajui ulichoandika!!!

      faultfinder!!
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    12. #109
      Kaitampunu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2011
      Location : Kwenye Corner
      Posts : 663
      Rep Power : 511
      Likes Received
      138
      Likes Given
      198

      Default Re: Tamko la vijana juu ya Nape

      Quote By Nnauye Jr
      Nimesikitishwa sana sana NA UPOTOSHAJI MKUBWA UNAENDELEA KATIKA SAFARI YANGU YA KWENDA KAGERA! KILICHONIUMA ZAIDI NI JINSI WATU WANAVYOTAKA KUTUMIA MSIBA KAMA NGAO YAO YA KUPOTOSHA UKWELI WA SWALA ZIMA LA SAFARI YANGU KAGERA. KWA WASIOJUA AU WALIOAMUA KUPOTOSHA UKWELI KWA MAKUSUDI, DR. KYARUZI ALIKUWA RAFIKI MKUBWA WA MAREHEMU BABA YANGU MZAZI BRIG. GEN MOSES NNAUYE, HIVYO MAREHEMU KYARUZI NI SAWA NA BABA YANGU. NINA LAANI JUHUDI ZA KUTAKA KUTUMIA ZIARA YANGU KAGERA NA MSIBA WA MZEE WANGU KYARUZI KISIASA.

      NAOMBA IJULIKANE KUWA KAGERA SIKWENDA RASMI KWA AJILI YA KUHANI MSIBA
      , ISIPOKUWA NILIKWENDA KWA SHUGHULI ZANGU ZA KICHAMA NA KWAKWELI NILIJUA MAZISHI YAMESHAFANYIKA YA DR. KYARUZI NIKIWA DAR NIKAMWOMBA KATIBU WA MKOA KUWA NIKIWA MISENYI NIENDE NYUMBANI KUWASALIMIA WAFIWA, AKANIAMBIA HAWAJAZIKA, NA ILIKUWA WAZIKE KESHO YAKE YA SIKU NILIYOENDA KAGERA, NIKAMWAMBIA BASI NITAPITA MSIBANI KUTOA POLE. NA NDIVYO NILIVYOFANYA , NILIPOFIKA TU NIKAENDA KUTOA POLE NDIO NIKAENDELEA NA SHUGHULI ZILIZONIPELEKA KAGERA.KAGERA SIKWENDA KUHANI MSIBA NILIKWENDA KWA SHUGHULI YA VIJANA, SI BUSARA HATA KIDOGO KULAUMU BILA KUULIZA HASA KWA MHUSIKA. NINASIKITISHWA NA UAMUZI WA MWANDISHI KUJIPA USEMAJI WA VIJANA KAGERA NA KUSHINDWA HATA KUWAULIZA WAHUSIKA MAANA WAPO KAGERA NAPE ALIFUATA NINI KAGERA.

      LAKINI KUDHIHIRISHA NIA MBAYA YA MWANDISHI, MWANDISHI KAAMUA KUDANGANYA UMMA KUWA NILIKUWEPO KAGERA SIKU YA MAZISHI YA DR. KYARUZI, AMA KAAMUA KUKOLEZA KUSUDI LAKE BAYA AU HAJUI ALICHOKISEMA, UKWELI NI KWAMBA TAREHE 25/05/2012 NILIKWENDA KAGERA NA KURUDI DSM SIKU HIYOHIYO SASA HUYO NAPE WA TAREHE 26 NI YUPI? NI VIZURI KUPIMA TUHUMA KABLA YA KUZITOA.

      NINA MSAMEHE BURE MWANDISHI NA ALIOSHIRIKIANA NAO.

      Nape, Maelezo yako yote unajitukanisha na unatuchanganya ni bora ungekaa kimya.Msibani picha zako ziko humu na ulivaa kisiasa zaidi. Kama kweli marehemu alikuwa rafiki wa marehemu babako basi ungekuwa karibu na familia ukajua ratiba kamili. Naogopa kusema ulikurupuka na huenda watu wanaweza waseme kwamba uli gate crash msibani. Kwenye hili kaka umeshikwa pabaya.

    13. #110
      Hingi Jr's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Posts : 92
      Rep Power : 374
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default Re: Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape

      Hii blog kama tulivyo wahi kusema inata watu wote wanachangia wawe wana cdm ndio maana kila wakati sisi tusio kipenda cdm wanajifanya kuziondoa na hatutachoka.CCM OYEEEE

    14. #111
      Hingi Jr's Avatar
      Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Posts : 92
      Rep Power : 374
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default Re: Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape

      hongera Nape kwa Vua Gwanda Vua Gwanda Vaa Uzalendo
      Waberoya likes this.

    15. #112
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1742
      Likes Received
      1518
      Likes Given
      2835

      Default Re: Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape

      Quote By Hingi Jr
      hongera Nape kwa Vua Gamba, Vua Gwanda Vaa Uzalendo
      ....................
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    16. #113
      Abdalla Khamis's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th June 2011
      Posts : 59
      Rep Power : 728
      Likes Received
      8
      Likes Given
      0

      Exclamation Re: Tamko la vijana juu ya Nape

      Quote By Nnauye Jr
      Nimesikitishwa sana sana NA UPOTOSHAJI MKUBWA UNAENDELEA KATIKA SAFARI YANGU YA KWENDA KAGERA! KILICHONIUMA ZAIDI NI JINSI WATU WANAVYOTAKA KUTUMIA MSIBA KAMA NGAO YAO YA KUPOTOSHA UKWELI WA SWALA ZIMA LA SAFARI YANGU KAGERA. KWA WASIOJUA AU WALIOAMUA KUPOTOSHA UKWELI KWA MAKUSUDI, DR. KYARUZI ALIKUWA RAFIKI MKUBWA WA MAREHEMU BABA YANGU MZAZI BRIG. GEN MOSES NNAUYE, HIVYO MAREHEMU KYARUZI NI SAWA NA BABA YANGU. NINA LAANI JUHUDI ZA KUTAKA KUTUMIA ZIARA YANGU KAGERA NA MSIBA WA MZEE WANGU KYARUZI KISIASA.
      Never give up mheshimiwa, keep on strugling and people will eventually understand you.

      Tunakuamini sana, tunaukubali sana uwajibikaji wako, umakini, uzalendo, huruma yako kwa wananchi na mengine mengi unayoyafanya kwa maslahi ya chama na taifa kwa ujumla.

      Tatizo la watu wengi wanatanguliza sana ushabiki, imani, itikadi na hivyo kuwafanya kuwa watumwa wa mawazo na hatimaye kuyapokea mawazo na kuyaamini bila kuyafanyia uchambuzi wa kina.

      Wanachama wanaoitwa wa chadema, ni sawa na watu walio katika chumba cha giza na hivyo hata wakiitwa wanashindwa kutoka kwasababu ya giza totoro lililowavamia. Kamwe hawataiona nuru mpaka watoke gizani. Pole yenu sana

    17. #114
      Matola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th October 2010
      Posts : 12,516
      Rep Power : 19751
      Likes Received
      5449
      Likes Given
      3641

      Default Re: Tamko la vijana kutoka Kagera juu ya Nape

      Quote By Waberoya
      Ujinga tu huu na wastage of time!!

      watanzania bana mbona mnapenda sana kukuza vitu vidogo, ku-complicatate maisha namna hii!!!
      Waberoya you may have some point on this, lakini ujuwe siku zote ukipanda ubuyu usitegemee kuvuna nyanya, CCM ndio waasisi wa mambo ya kijinga na matamko ya kipuuzi na kuna wakati uzitumia hata taasisi za dini kutimiza malengo yao.

      Kama utakumbuka Joshua Nassari baada ya kuzungumza jukwaani maneno yaliotokana na mhemko wa kisiasa pale Arusha, Freeman Mbowe kama Mwenyekiti alihutubia na kuclear ile statement.

      Kwa Tatifa lolote la watu makini kauli ya Mbowe ndio kauli rasmi ya chama, lakini cha kushangaza wanasiasa walioshindwa wakiongozwa na Nape wao ndio wakataka kuigeuza karata yao ya kisiasa, ndio maana mimi hawa watu huwa sina huruma nao maana ni wabaya kuliko ubaya wenyewe.

      Waberoya labda unaweza ukastuka nikikwambia kama mpaka sasa bado nna mashaka kama kweli ni Waislamu ndio wamechoma yale Makanisa, maana nina tabia ya kutoupumzisha ubongo wangu maana unafanya kazi muda wote.

      Ni kwa nini napata mashaka haya!!......nikiangalia CCM walichokifanya Igunga kuchoma moto banda la kuku na kusingizia Chadema imechoma ile nyumba ya kiongozi wa CCM ndio kinanipa imani hawa watu wakibanwa wako tayari kutumia mbinu zote, hali ya Zanzibar Serikali ya CCM maji yako shingoni, nina mashaka isijekuwa ni CCM ndio wamechoma makanisa ili wapate uhalali wa kuwadhibiti Uamsho.
      Waberoya and Ringo Edmund like this.
      Division four point 29 = Masters Mzumbe University. Nape Nnauye is my role model.

    18. #115
      patience96's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th August 2011
      Location : Kisorya
      Posts : 849
      Rep Power : 561
      Likes Received
      232
      Likes Given
      267

      Default

      Quote By MADAYA
      never give up mheshimiwa,keep on strugling and people will eventually understand you.tunakuamini sana,tunaukubali sana uajibikaji wako,umakini,uzalendo,huruma yako kwa wananchi na mengine mengi unayoyafanya kwa maslai ya chama na taifa kwa ujumla. Tatizo la watu wengi wanatanguliza sana ushabiki,imani,itikadi na hivyo kuwafanya kuwa watumwa wa mawazo na hatimaye kuyapokea mawazo na kuyaamini bila kuyafanyia uchambuzi wa kina. Wanachama wanaoitwa wa chadema,ni sawa na watu walio katika chumba cha giza na hivyo hata wakiitwa wanashindwa kutoka kwasababu ya giza totoro lililowavamia.kamwe hawataiona nuru mpaka watoke gizani.pole yenu sana
      mmh, hizo panctuation marks zako ni za wapi mkuu? Nimependa hizo commas na periods!

    19. #116
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1742
      Likes Received
      1518
      Likes Given
      2835

      Default Re: Tamko la vijana kutoka Kagera juu ya Nape

      Quote By Matola
      Waberoya you may have some point on this, lakini ujuwe siku zote ukipanda ubuyu usitegemee kuvuna nyanya, CCM ndio waasisi wa mambo ya kijinga na matamko ya kipuuzi na kuna wakati uzitumia hata taasisi za dini kutimiza malengo yao.

      Kama utakumbuka Joshua Nassari baada ya kuzungumza jukwaani maneno yaliotokana na mhemko wa kisiasa pale Arusha, Freeman Mbowe kama Mwenyekiti alihutubia na kuclear ile statement.

      Kwa Tatifa lolote la watu makini kauli ya Mbowe ndio kauli rasmi ya chama, lakini cha kushangaza wanasiasa walioshindwa wakiongozwa na Nape wao ndio wakataka kuigeuza karata yao ya kisiasa, ndio maana mimi hawa watu huwa sina huruma nao maana ni wabaya kuliko ubaya wenyewe.

      Waberoya labda unaweza ukastuka nikikwambia kama mpaka sasa bado nna mashaka kama kweli ni Waislamu ndio wamechoma yale Makanisa, maana nina tabia ya kutoupumzisha ubongo wangu maana unafanya kazi muda wote.

      Ni kwa nini napata mashaka haya!!......nikiangalia CCM walichokifanya Igunga kuchoma moto banda la kuku na kusingizia Chadema imechoma ile nyumba ya kiongozi wa CCM ndio kinanipa imani hawa watu wakibanwa wako tayari kutumia mbinu zote, hali ya Zanzibar Serikali ya CCM maji yako shingoni, nina mashaka isijekuwa ni CCM ndio wamechoma makanisa ili wapate uhalali wa kuwadhibiti Uamsho.
      Matola, umenifanya nicheke sana

      Kumbe hii issue nzima bado ni kisiasa zaidi kuliko hali halisi, na wengi waliolipokea hili wamelipokea kisiasa!!

      Kweli CCM ni waanzilishi wa kila kitu lakini isifike muda tuka-copy ujinga wao!!! kwa mfano mtoa tamko huyu si ni CCM?? kwani angempigia simu Nape na kutaka ufafanuzi ingeharibu nini? kutoka huku ki-matamko tamko kuna tu expose sana tabia zetu watanzania

      nimecheka kuhusu zanzibar, anyway sina comment sana, maana mimi ni mhanga wa hiyo mioto!!! let me keep silent for now.

      ukicheka na nyani utavuna mabua!! CCM wanachekana kuwalea sana watu fulani nchi hii, ambao siku zote huwa hawaleleki sana.

      spiritually hawajachoma moto ndio wamewasha moto wa injili ya Yesu Kristo!!
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    20. FJM
      #117
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,178
      Rep Power : 2569
      Likes Received
      5331
      Likes Given
      4587

      Default Re: Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape

      Nape alitakiwa avute pumzi na kuelewa nini hasa kimeandikwa kwenye huo waraka kabla ya kujibu.

      Kwa bahati nzuri au mbaya watanzania wanajua "style and level" ya ushiriki wa ccm na serikali yake kwenye misiba wanayoithamini-tumeona Kanumba. Sasa Nape alitakiwa aokoe jahazi walau nusu jahazi lakini kwa bahati mbaya anasema hakwenda huko specificaally kuhudhuria mazishi and worse he didn't even know kama marehemu Mzee Kyaruzi amezikwa au la!

      Ningekuwa mjumbe wa NEC ningepiga kelele ili uitishwe mkutano wa dharura wa NEC na kubadilisha the entire secretariat. Wote kabisa ni kuwaondoa kwa sababu they are behind this disastrous situation. Mukama atawezaje kuwaangalia usoni wazee wa ccm baada ya hii blunder? Au rais ataendelea na mtindo wake wa kuongea na wazee akiwa na jambo muhimu huku akitoa kipaumbele kwa wacheza sinema?

      Pia ningeomba kufahamishwa, kwenye huu msiba wa Mzee Kyaruzi mbunge wa Missenyi - Assumpta Mushama alishiriki kwa kiwango gani?

      Na mwisho, vijana wote waliombatana na Nape wakati watu wanalia (wenyewe) makaburini waone busara ya kuomba radhi mara moja. Ni jambo la ajabu kwa kijana wa kitanzania kuacha msiba nyumbani na kuambatana na mgeni toka mbali kwenda kucheza gofu! Hii ni laana. Ombeni radhi halafu mengine baadae.

    21. #118
      Raia Fulani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2009
      Posts : 9,258
      Rep Power : 2624
      Likes Received
      1294
      Likes Given
      834

      Default Re: Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape

      kwa hiyo kwa kauli ya nape ni kuwa ccm serikali haijatuma mwakilishi kwenye msiba wa dr kyaruzi. Kwa maana hiyo ni kuwa amekwepa kuomba samahani. Kadhalika katika majibu yake ni kuwa dk kyaruzi hajapata heshima ya kitaifa
      Beware of a sucker punch

    22. #119
      mgeni wenu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd January 2012
      Posts : 1,157
      Rep Power : 891
      Likes Received
      578
      Likes Given
      0

      Default Re: Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape

      Eti una undugu na Mwandosya?

    23. #120
      Msambaa mkweli's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 31st December 2011
      Posts : 152
      Rep Power : 403
      Likes Received
      26
      Likes Given
      1

      Default

      Quote By sir.JAPHET
      duuu, kweli nchi IMEPOTEZA DIRA
      Naunga mkono.

    Page 6 of 8 FirstFirst ... 45678 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...