Tathmini ya kisayansi ya mkutano wa cdm jangwani ni kama ifuatavyo :
- Imedhihirika kweli DAR KUNA WENYEWE na si kama Arusha, kwani kwa idadi ya watu , Dar ina watu wengi kuliko Arusha , ila Arusha kwenye mikutano ya cdm watu wengi hujitokeza kuliko hata wale walioonekana jangwani pale kwenye kile ‘kijiumati’ japokuwa matangazo yalikuwa mengi. Hii yadhihirisha Dar ina wenyewe, na wengi wetu ni wakuja si wana Dar kindaki ndaki
- Mbowe adhihirisha ni mgeni na historia ya Dar. Uwanja wa Jangwani anaujua historia yake? Ni jambo la kushangaza na kustaajabisha kuuita uwanja wa jangwani ni ‘cdm square’. Wenye hadhi hiyo ni wakazi wa Dar wenye kuujua asili ya uwanja ule, mtu km Mbowe wakuja hadhi hiyo ameipata wapi? Ni jambo la ajabu na kustaajabisha
- Cdm kwa dar mambo ni magumu sana, tuliambiwa kwenye kwenye magazeti (na sijui km ni kweli) kuwa kwa arusha na yenye watu wachache kuzidi Dar watu 10,000 walirudisha kadi, ila kwa Dar na yenye watu wengi zaidi ya Arusha ni 3100 tu. Ndio narudia kusema Dar ina wenyewe sio mji wa kuvamia vamia tu
Kwa haya machache yaonyesha wazi cdm kwa Dar mna kazi ya ziada, Dar ina wenyewe sio km Arusha. Na wengi waliojitokeza kwenye ule mkutano 80% ni wakuja si wana Dar kindaki ndaki.

Reply With Quote


Follow Us Here