Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

    Report Post
    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast
    Results 21 to 40 of 51
    1. #1
      dosama's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th December 2010
      Posts : 736
      Rep Power : 573
      Likes Received
      296
      Likes Given
      1

      Default CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Source Tanzania Daima

      BAADA ya suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi nchini kupigwa danadana, sasa Waislamu wametaka suala hilo liingizwe kwenye Katiba mpya.

      Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiliweka suala la uanzishwaji wa mahakama hiyo katika ilani yake ya uchaguzi mwaka 2005/2010 na kuahidi kushughulikia.

      Hata hivyo, suala hilo halikushughulikiwa na katika ilani yake ya mwaka 2010 hakikuliweka suala hilo.

      Mwaka jana akizungumza katika Baraza la Iddi mjini Dodoma, Rais Kikwete alinukiwa akisema serikali haitaanzisha mahakama hiyo na badala yake Waislamu wenyewe ndio waianzishe.

      Hoja hiyo ilipingwa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na kutoa kauli kuwa watatumia maandamano ya usiku na mchana, kushinikiza kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

      Akizungumza katika mahafali ya nne ya wahitimu wa Kiislamu katika Chuo cha Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya jumuiya na taasisi za Kiislamu nchini kukaa na kukubaliana jambo hilo liingizwe katika katiba ili liweze kufanikiwa.

      Kutokana na hali hiyo, aliwahamasisha Waislamu nchini kujitokeza kwa wingi katika Tume ya Katiba inayoongozwa na Jaji mstaafu, Joseph Warioba na kutoa maoni yao kuhusu jambo hilo, ili hatimaye liweze kuingizwa katika Katiba mpya.

      “Nchi yetu imo katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba mpya. Katiba ni dira na ngome inayolinda haki na kuweka misingi ya maendeleo kwa wananchi. Tukio hili ni kubwa, ambapo kila jamii hupigania haki zake za msingi kuzingatiwa.

      “Katiba iliyopo ambayo Waislamu hawakushiriki, imechangia kwa kiasi kikubwa kuwaathiri kiimani, kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa maana hiyo mchakato huu ni fursa muhimu kwa Waislamu kuhakikisha haki zao za msingi zinaingizwa ndani ya Katiba mpya,” alisema.

      Alisema katika jambo hilo wanataka katiba isajili mahakama hiyo, mashauri ya ndoa, talaka, watoto, vifo, mirathi, wosia, wakfu na biashara yasikilizwe na kadhi na bila kutafutwa ridhaa ya mtu au warithi pamoja na mahakama hiyo kuwapa msaada wa nguvu za dola.

      Alisema kwa kuwa suala hilo limechukua muda mrefu ni vema sasa utekelezwaji wake uwekwe kwa mujibu wa katiba.

      “Wakati umefika kwa Waislamu kupigania na kwenda kutoa maoni katika tume ya katiba, ili tuweze kupata Mahakama ya Kadhi. Waislamu wamekuwa wakipuuzwa katika masuala mbalimbali kutokana na kutowekwa katika katiba lakini sasa umefika wakati wa kupeleka maoni na si kuendelea kulalamika,” alisema.

      Aidha, Sheikh Ponda alisema jumuiya hiyo ambayo ni jukwaa la Waislamu la kuratibu mchakato wa Katiba nchini, masuala mengine ambayo Waislamu wanayapigania yaonekane kwenye katiba mpya, ni kuingizwa katika katiba mpya siku ya Ijumaa kutambulikuwa kuwa ni siku ya ibada ambayo itawasaidia Waislamu kupata fursa ya kwenda kuabudu kwa uhuru zaidi.

      “Pia tunataka katiba itambue uwepo wa Mwenyezi Mungu, itoe uhuru wa kuabudu, kwani katiba iliyopo haijatoa uhuru huo na ndiyo maana Waislamu wanazuiliwa ibada pamoja na kuvaa hijabu vyuoni, majeshini na asasi za serikali.

      Alisema kuwa pia wanataka katiba itoe usawa katika elimu kwa maana ya katiba kutamka uwakilishi sawa kwa Wakristo na Waislamu katika Baraza la Mitihani la Taifa.

      “Kabla na baada ya uhuru chombo hiki kimeendelea kutawaliwa na Wakristo na kusababisha upendeleo mkubwa katika uteuzi na usahihishaji wa mitihani, kuwe na uteuzi wa maofisa elimu wakuu wa shule,” alisema.

      Aidha, alisema wanataka sheria ya ugaidi ifutwe, kuwapo kwa uwakilishi wa dini bungeni, pamoja na baraza la madiwani na mawaziri kuwa na uwakilishi wa dini.

      “Pia tunataka katiba iruhusu vyama vya siasa vya kidini, Waislamu na Wakristo wapokezane urais, serikali ya Tanganyika irejeshwe, kuwapo kwa muungano wa serikali tatu, urais wa muungano uwe wa awamu pamoja na kuwapo kwa serikali ya majimbo,” alisema.

      Sheikh Ponda kuwa masuala mengine wanayotaka kuwamo katika Katiba mpya ni mgombea binafsi, matokeo ya urais kupingwa mahakamani, rais kutounda tume ya uchaguzi, adhabu ya kifo iwekwe ndani ya katiba, misamaha ya kodi na mikataba ya kanisa na serikali ifutwe na kikosi cha kupambana na rushwa kuundwa upya na kuingizwa kwenye katiba.

      Concern;

      Jamani sijafafanuliwa vzr juu ya haya.

      Sheria ya ugaisi ifutwe kuna nini nyuma yake?
      Haki ya kusoma hivi hawa watu mmekatazwa na nani kusoma? Mponda elimu yako ni darasa la ngapi na kwa nini?
      Utawala wa kupikezana kwa manufaa ya nani?
      Uhuru wa kuabudu nani kawanyima?
      Sheria ya biashara kwa ...... sijaelewa kivp
      Last edited by dosama; 27th May 2012 at 07:37.

    2. Miaka 50

    3. #21
      Ronn M's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Location : Moshi~Arusha
      Posts : 1,283
      Rep Power : 611
      Likes Received
      660
      Likes Given
      403

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Duh, vyama vya siasa vya kidini! Uraisi wapokezane waislamu na wakristo! Sheria ya ugaidi ifutwe! . . .dah, kweli mwenye akili na mjinga hujulikana kwa maneno yao

    4. #22
      Sideeq's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Posts : 1,588
      Rep Power : 797
      Likes Received
      203
      Likes Given
      0

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Quote By Shardcole
      Dah! Haya mapendekezo ya huyu shehk ponda kama yana uchochezi fulani hivi? Polis wa intelejensia hebu fanyeni kazi yenu kama mlivyofanya kwa Nassary,
      ha ha ha ha
      Daima huwa ninafikiri kuwa Tanzania inaheshimu uhuru wa mtu kutoa mawazo yake!......unawatisha wengine kutoa mawazo yao sasa.
      Simjui Sheikh Ponda na mawazo yake ameyatoa kama Sheikh Ponda! zijadiliwe hoja zake kwa hoja badala ya kukashifu "Waislamu waende shule", wanaozesha watoto wadogo kwa ajili ya pilau n.k

    5. #23
      melxkb's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th September 2010
      Posts : 202
      Rep Power : 481
      Likes Received
      55
      Likes Given
      165

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Quote By Nnauye Jr
      Dosama,
      SASA HAPA THREAD YAKO NA STORI MBONA HAVINA UHUSIANO???!!! IKO WAPI SEHEMU YA STORI INAYOONYESHA CCM KURUHUSU MAHAKAMA YA KADHI KWENYE KATIBA??!!!!!!!!UNAPOTUMWA, AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO KABLA YA KUPELEKA ULICHOTUMWA!
      Nakubaliana na mtoa Mada kwa maana kwamba thread yake inalenga kukumbushia kile kilichokuwa kimewekwa kwenye ilani yenu ya CCM 2005/2010 kuhusu uanzishwaji wa mahakama ya kadhi jambo ambalo halina tofauti sana na maoni ya shiekh Issa Ponda = CCM ilani 2005/2010. As simple as that, kama ulikuwa umeshasahau Mr. Nape Nnauye Jr2.

    6. #24
      Eng. Y. Bihagaze's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 8th September 2011
      Location : Czech(but now in DAR)
      Posts : 766
      Rep Power : 5116
      Likes Received
      579
      Likes Given
      111

      Default

      Quote By dosama
      Source Tanzania Daima


      Alisema katika jambo hilo wanataka katiba isajili mahakama hiyo, mashauri ya ndoa, talaka, watoto, vifo, mirathi, wosia, wakfu na biashara yasikilizwe na kadhi na bila kutafutwa ridhaa ya mtu au warithi pamoja na mahakama hiyo kuwapa msaada wa nguvu za dola.

      Wazo langu si vema sana kushinikiza kile kiwekwe kwenye katiba kile kisiwekwe..

      Kwa upande mkubwa jamii kubwa hatujaelewa viongozi wetu wanamaanisha nini kiwekwe kwenye Katiba kuhusu ndoa, talaka, mirathi, wosia na mengineyo. Jamani tuwe Na Moyo Wa kheri wa binaadam, tuambiwe Kwa uwazi ni nini kibadilike Na kibadilikeje? Cha sasa kina kasoro gani Na kitachobadilika kitabadilikaje tuelewe Na jamii yote Kwa ujumla inaweza kuunga mkono bila shaka. Lakini tukiendelea kusema mwanamke Hana HAKI ya Urithi, mwanamke anany'ang'anywa kila kitu mumewe akifa , mwanaume anaongeza wanawake wa kuoa hata Kama uchumi hauruhusu, Kama mambo yataendelea Kua hivi Basi Shekhat wote tutasema Na Katiba itambue mwanamke kumtaliki mwanaume, mwanamke kuandika wosia Na mengineyo..
      Mie kila siku nasema tukae tujadiliane mnasema nyie Hamna HAKI ni wa kutawaliwa tu, jamani DUNIA ya utandawazi hii tunaelekea wapi tusipobadili mitazamo..
      DUNIA tuliyonayo watu wamechakachua mapenzi halisi ya Dini, wamedidimiza tamaa zao Na mambo Yao Na kutubebesha kwamba ndivyo DINI Inavyotaka . . Jamani hii itakubalika wapi?.. Mbona Mtume ameandika mambo mengi Kwa Ufasaha kwanini wanadamu viongozi wetu mnabadilika, Ogopeni Jehanam ya Moto..wekeni waziwazi nini kibadilike Na kibadilikeje sio kutaka kutukandamizia mbali wengine.. Niko tayari kufungua mjadala wa wazi Kwa yeyote anayetaka kutuelewesha .. Inshallah
      alibaba likes this.

    7. #25
      Mnyonge Namba1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2012
      Posts : 402
      Rep Power : 449
      Likes Received
      78
      Likes Given
      0

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Haya ni matokeo ya kuwa na viongozi wa dini wasio na elimu dunia ya kutosha
      alibaba likes this.

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      Mkira's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th May 2006
      Posts : 417
      Rep Power : 1140
      Likes Received
      36
      Likes Given
      7

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Quote By Nnauye Jr
      Dosama,
      SASA HAPA THREAD YAKO NA STORI MBONA HAVINA UHUSIANO???!!! IKO WAPI SEHEMU YA STORI INAYOONYESHA CCM KURUHUSU MAHAKAMA YA KADHI KWENYE KATIBA??!!!!!!!!UNAPOTUMWA, AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO KABLA YA KUPELEKA ULICHOTUMWA!

      Nape ninakuja 2015 kila nikifikira nafsi yangu inanituma nije lakini ninajua ni kzi kubwa tena ngumu lakini dawa katika speech ayngu nitakayotoa wakati huo wa kuchukua form itataka moyo maana itasema viongozi wa juu na kuwataka wake kimya ili tujaribu kuiomboa CCM, lakini hao watoto wao wanojiingiza humo kwa sasa wanapaswa kufirikia mara dufu kuwa tunakuja kusafisha chama kwa hiyo wasidhani CCM ni kimbilio lao kuja kuficha au kuendeleza dhambi ya KUWAFANYA WATANZANIA KUENDELEA KUWA MASIKINI!

      jana nilikuwa ninasikikiliza siasa za ghana kwa kuwa ninmkubali sana huyu mwana dada nisikia kumbe CPP ya kwame nkruma nusra ifutike katika ramai ya ghana! wana mbunge mmoja tu na sasa MWANE LAKINI ANAJITAHIDI KUKIOMBOA JAPO KIPTATE WABUNGE WENGI 2012!

      NAPE HUKO NYUMA NILIKUWA ninakukubali lakini jinsi unayojibu CHADEMA ninakushangaa wewe unapaswa kutaka chadema iwepo ila CCM IAFNYIE KAZI MABADILIKO INAWEZEKANA JAPO WALIOPO MADARAKANI KWA SASA WAMEKISASABISHIA CHAMA KUCHUKIWA KIASI HIKI!

      badala ya kujirekebisha nyie mansema mtahahkisha chadema inakufa ndai ya mwaka mmoja ili IWEJE CCM IENDELEE KUVURUNDA HALI YA WATANZANIA NA KUGAWA MADINI YETU KAMA NJUGU HUKU WANBUNGE WENGI WA CCM WAKIKENUA MENO!?

      NInakuja 2015 kama miujiza na tutavuka tu mkinikataa !!!?

    10. #27
      Mkira's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th May 2006
      Posts : 417
      Rep Power : 1140
      Likes Received
      36
      Likes Given
      7

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Quote By Nnauye Jr
      Dosama,
      SASA HAPA THREAD YAKO NA STORI MBONA HAVINA UHUSIANO???!!! IKO WAPI SEHEMU YA STORI INAYOONYESHA CCM KURUHUSU MAHAKAMA YA KADHI KWENYE KATIBA??!!!!!!!!UNAPOTUMWA, AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO KABLA YA KUPELEKA ULICHOTUMWA!


      Hon. Samia Nkrumah speech: CPP MARKS POSITIVE ACTION DAY - YouTube


      ccm inatakiwa courage ya kukataa dhambi bila kuogopa jk hawezi kukupiga wala kukufukuza kwa sasa ya nini umtumikie! be strong usipende kulipiza visasi chapa kazi niliwahi kukaa na wewe somewhere courtyard ila sikupenda majigambo! ila wewe ni mzalendo lakini baada ya kushika nafasi hiyo unaelekea kuogopa aliekupatia! tumia nafasi uliyo nayo mpunguze madaraka ya chairman katika katiba ya CCM ile wanachama wawe na uhuru wa kuongea na kuomuona chairman kama mungu mtu!

    11. #28
      Hofstede's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2007
      Posts : 3,604
      Rep Power : 21341
      Likes Received
      981
      Likes Given
      988

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Quote By Nnauye Jr
      Dosama,
      SASA HAPA THREAD YAKO NA STORI MBONA HAVINA UHUSIANO???!!! IKO WAPI SEHEMU YA STORI INAYOONYESHA CCM KURUHUSU MAHAKAMA YA KADHI KWENYE KATIBA??!!!!!!!!UNAPOTUMWA, AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO KABLA YA KUPELEKA ULICHOTUMWA!
      Pamoja Mkuu Nape, hawa watu sidhani kama wanatumwa ila nafikiri wana agenda ya kuvuruga mchakato wa katiba kwa kuanza kutoa matamko ya nini kiingie kwenye katiba mpya wakati ni suala la mjadala tume ikianza kuwauliza wananchiwote pamoja na wao kama chama watakuwa na haki ya kutoa mapendekezo yao but not guaranteed kuwa part of the new constitution. Mbaya zaidi wanatsingizia CCM kama upenyo kwa kuwa ndiyo iliyoanzisha hizi sarakasi.

      Kila kikundi kikija na madai yake wakati huu basi tutasgindwa na mchakato kuwa failure. Watu wakae na agenda zao au waziweke wazi bila ya kuanza kuonesha ni nani mwenye authority ya nini kiingie wapi na nini kisiingie. Huu utakuwa usanii na ufujaji wa pesa za walipa kodi kwani tukiruhusu haya mchakato mzima utakuwa 'Failed Ab initio'

    12. #29
      Mafaobongo's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 6th June 2011
      Posts : 3
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Kwani Waislamu wakianzisha mahakama zao na kuziendesha wenyewe wanapungukiwa nini, mbona wakristu wana mahakama zao na wanaziendesha wenyewe na hawapigi kelele. Je na wao waanze kudai iwekwe kwenye katiba? na wapagani nao? Tutakuwa na mahakama ngapi? Sasa sheria ya ugaidi ikifutwa halafu itawasaidia nini waislamu. Badala ya kulaani ugaidi ambao unatia doa dini yao kwa wale wanaoua watu, hata na waislamu wenzao kwa kutumia kigezo cha dini: MI NAONA WANGELAANI UGAIDI NA KULAANI WALE WANAOTUMIA DINI NZURI YA UISLAMU KWA KUTIMIZA UGAIDI. kufuta sheria ya ugaidi ni kuukumbatia ugaidi!

    13. #30
      GeniusBrain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Location : CHADEMA Makao Makuu
      Posts : 3,806
      Rep Power : 1143
      Likes Received
      187
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Bangoo
      Kenya wameifutilia mbali hiyo kadhi, ktk katiba yao mpya hakuna hiyo kitu!.
      Nani amekuambia? Kumbe hata kusoma hujui aisee, ni aibu. Mtafute mtu akusomee katiba ya kenya

    14. #31
      GeniusBrain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Location : CHADEMA Makao Makuu
      Posts : 3,806
      Rep Power : 1143
      Likes Received
      187
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Mafaobongo
      Kwani Waislamu wakianzisha mahakama zao na kuziendesha wenyewe wanapungukiwa nini, mbona wakristu wana mahakama zao na wanaziendesha wenyewe na hawapigi kelele. Je na wao waanze kudai iwekwe kwenye katiba? na wapagani nao? Tutakuwa na mahakama ngapi? Sasa sheria ya ugaidi ikifutwa hala
      fu itawasaidia nini waislamu. Badala ya kulaani ugaidi ambao unatia doa dini yao kwa wale wanaoua watu, hata na waislamu wenzao kwa kutumia kigezo cha dini: MI NAONA WANGELAANI UGAIDI NA KULAANI WALE WANAOTUMIA DINI NZURI YA UISLAMU KWA KUTIMIZA UGAIDI. kufuta sheria ya ugaidi ni kuukumbatia ugaidi!
      mbona cdm hawalaani ukatoliki kwa kuukumbatia ukatoliki?

    15. #32
      MtamaMchungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2011
      Posts : 1,539
      Rep Power : 806
      Likes Received
      710
      Likes Given
      64

      Default

      Quote By GeniusBrain
      Nani amekuambia? Kumbe hata kusoma hujui aisee, ni aibu. Mtafute mtu akusomee katiba ya kenya
      Kwenye katiba iliyopita, mahakama iliamua kuwa mahakama za kadhi ni za kibaguzi, "discriminatory",

      Kenya to appeal
      against Islamic
      Kadhi court decision


      Hii mpya inaruhusu but it will be a matter of time before it gets the same ruling once again.

    16. #33
      Mnyalu UK's Avatar
      Member Array
      Join Date : 22nd May 2012
      Posts : 12
      Rep Power : 354
      Likes Received
      0
      Likes Given
      7

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Haswaa, mtu mwenye akili huwezi fanya hivyo

    17. #34
      Olaigwanani lang's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th April 2012
      Posts : 330
      Rep Power : 816
      Likes Received
      52
      Likes Given
      373

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Quote By nnauye jr
      dosama,
      sasa hapa thread yako na stori mbona havina uhusiano???!!! Iko wapi sehemu ya stori inayoonyesha ccm kuruhusu mahakama ya kadhi kwenye katiba??!!!!!!!!unapotumwa, akili za kuambiwa changanya na zako kabla ya kupeleka ulichotumwa!
      hapo nimekusifu kaka..watu ni kuelezwa ukweli tuu.......!

    18. #35
      Kapwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2009
      Posts : 606
      Rep Power : 604
      Likes Received
      78
      Likes Given
      47

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Quote By Nnauye Jr
      Dosama,
      SASA HAPA THREAD YAKO NA STORI MBONA HAVINA UHUSIANO???!!! IKO WAPI SEHEMU YA STORI INAYOONYESHA CCM KURUHUSU MAHAKAMA YA KADHI KWENYE KATIBA??!!!!!!!!UNAPOTUMWA, AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO KABLA YA KUPELEKA ULICHOTUMWA!
      sema baba

      mix with yours

    19. #36
      Aswel's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 93
      Rep Power : 373
      Likes Received
      24
      Likes Given
      9

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Jamani hili suala la mahakama ya kadhi litaigawa nchi bora libaki kama lilivyo, ikiingizwa mahakama ya kadhi kwa ss waislam je na wakristu wakitoka na mahakama yao itakuwaje? nchi itagawanyika kiudini tuangalie nchi ya nigeria ilivyo gawanyika na sisi ndiko tunakotaka kwenda.

    20. #37
      kalokolaVIII's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th June 2011
      Posts : 295
      Rep Power : 467
      Likes Received
      144
      Likes Given
      419

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Heshima kwenu wanaJF!
      Nape rightly said the piece of information brought on our attention by DOSAMA doesn't indicate at least in this circumstance that CCM has given a nulla osta for what is called KADHI COURT but at the same time asquintly and myopically he omits the fact that "the introduction of KADHI COURTS" is part of CCM electoral manifesto and according to CCM's rules and obligations every member of that decaying party is obliged to stand for the fulfillment of that manifesto - Nape this is abc of politics and you should know that in consideration of the position you have right now in CCM. Sasa wewe ambaye ni katibu mwenezi waCCM hauyajui haya mimi ninazidi kujiuliza NI VIGEZO GANI VILITUMIKA KUKUPATIA HIYO NAFASI???? Inawezekana ikawa kigezo kikuu kilikuwa ni UMASHUHURI WAKO KATIKA MIPASHO!!!!

      In merits, the issue of KADHI COURTS does not deserve any discussion because it's a non-issue, IT'S IMPOSSIBLE IN A SECULAR STATE as I presume Tanzania is, to subject people to different STATE LAWS having as a discriminatory factor their respective RELIGION,TRIBE,SEX,GEOGRAPHICA L LOCATION or dulcis in fundo SEXUAL ORIENTATION. It's completely lame!!!
      Sasa tumefika hapa tulipofika katika hili suala, kutokana na policy ambiguity ya CCM - CCM iliwapa matumaini ya UWONGO waumini wa dini ya Kiislamu(most of them do not even care about Kadhi and related stuff!!!) kuwa tupeni kura nasi kama shukrani tutawapatia kupitia mgongo wa serikali hiyo TAASISI YA KADHI - they lied purposely!!!!

      Hata MAHAKAMA ZA MWANZO nazo zinakingana na KATIBA maana zinaendeshwa kwa KUFUATA MILA NA DESTURI na ndio maana ADVOCATE haweki mguu MAHAKAMA YA MWANZO( najua jukwaani kuna watu waliosomea sheria wanaweza kutupatia ufafanuzi zaidi)

      In a serious nation the bleach of law is BLEACH regardless of your geographical location by the time you "conduct" that offensive/omissive act. Sasa kwa kuwa desturi na mila zinatofautiana kutoka sehemu moja kwenda nyingine basi hata hizi hazipaswi kuwepo - they are nothing but colonial remnants and this is the right time to get rid of them.
      Last edited by kalokolaVIII; 27th May 2012 at 20:16.

    21. #38
      dosama's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th December 2010
      Posts : 736
      Rep Power : 573
      Likes Received
      296
      Likes Given
      1

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Hovi CDM au CUF wanguwa zanzibar ndo wanahamasisha CCM mngefanyaje?

    22. #39
      dosama's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th December 2010
      Posts : 736
      Rep Power : 573
      Likes Received
      296
      Likes Given
      1

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Hivi CDM au CUF wanguwa zanzibar ndo wanahamasisha CCM mngefanyaje? Inavyojulikana ccm mko nyuma ya haya yote yanayotokea

    23. FJM
      #40
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,168
      Rep Power : 2566
      Likes Received
      5318
      Likes Given
      4585

      Default Re: CCM: Mahakama ya Kadhi Ruksa kwenye katiba mpya

      Hivi katiba ya sasa haitoi uhuru wa mtu kuabudu?

    Page 2 of 3 FirstFirst 123 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...