Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

    Report Post
    Page 5 of 5 FirstFirst ... 345
    Results 81 to 87 of 87
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22277

      Default Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Kutokana na hali ya kusubiria baadhi ya wajukuu zake marehemu waishio Ulaya, mazishi ya aliyekuwa Rais wa Chama cha TAA (kabla ya kumkabidhi kiti hicho kwa Mwl. Nyerere) Dr. Vedastus Kyaruzi hayatafanyika leo (Alhamis, 24/05/2012) bali yatafanyika siku ya Jumamosi 26/05/2012 huko Kyaka kijijini Nyabihanga katika wilaya ya Missenyi
      Wanabodi,

      Nimepokea taarifa za kifo cha mmoja wa waanzilishi wa chama cha TAA na baadae TANU, Dr. Vedastus Kyaruzi kilichotokea juzi hapa jijini Dar es Salaam na mwili wake kusafirishwa leo kuelekea Bukoba kwa mazishi yatakayofanyika J.5.

      Habari hizi ni kwa mujibu wa Bw. Prosper Vedasto wa Channel Ten.

      Kwa wafuatiliaji wa historia ya siasa za Tanzania, Mzee Kyaruzi ametajwa sana katika makala za Maalim Mohamed Said kuwa yuu miongoni mwa mashujaa wa nchi hii waliosahaulika au tulio sahaulishwa na inawezekana ndio maana hata msiba wake uko low profile!.

      Nadhani nisingekutana na Bw. Prosper, msiba huu muhimu ungeweza kutupita juu kwa juu!.

      Quote By Familia
      Tunaomba tusahihishe taarifa kutoka kwa Bw. Prosper;

      Dr.Vedastus Kyaruzi amefariki jana usiku wa saa 1:20 usiku na umauti umemkuta akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa huko Bukoba mjini.

      Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi ya tarehe 24 Mei,2012.
      Kwa msiomfahamu Dr. Kyaruzi, hapa anaelezewa vizuri na mwana JF mwenzetu, mpigania uhuru mwenzake!.

      Quote By Mpigania Uhuru
      Wanasiasa katika jamii yetu wamekuwa wakiwachukulia madaktari kama watu ambao muda mwingi wako na wagonjwa na wajui mambo ya kijamii yanayoendelea, imefika wakati hata sitahiki zao ambazo ziko wazi katika "goverment standing order' wananyimwa bila sababu ya msingi. Mfano intern drs waliodai mshahara wao wa mwezi ambayo ni haki yao, baadae walipewa na kufukuzwa muhimbili!

      Ukweli ni kwamba drs wamehusika sana katika ukombozi wa kisiasa wa tanganyika na dunia kwa ujumla.

      Naomba nitoe mifano miwili.

      Kwanza ni Dr. Vedasto Kyaruzi ambaye alikuwa president wa TAA mwaka 1950 na katibu wake akiwa Abdulwahid Sykes. Kabla ya kuingia kwa huyu daktari TAA ilikuwa ni chama cha kijamii ambacho hakikuwa na mwelekeo wa kudai uhuru.

      Dr. huyu ndiye aliyeleta mapinduzi makubwa akiwa kama president wa TAA wakati Nyerere anakuja kujiunga na harakati za kudai uhuru msingi mkubwa ulishaandaliwa na huyu Dr. kyaruzi, kwa bahati mbaya watanganyika wengi hawajui/hawajaelezwa mchango wake i.e forgatten people.

      Mfano wa pili ni Dr. Che Guevara huyu alikuwa ni daktari na mwanamapinduzi wa ukweli ambaye amepigana vita vya msituni na kufanikisha uhuru wa CUBA, ukombozi wa DRC etc.

      Sasa hivi kuna harakati nyingi za ukombozi wa jamii yetu zikioongozwa na CHADEMA.

      Madaktari nao sasa wameamua kujiunga katika vita hii. Mfano mzuri ni Mh. Zitto leo alivyojitokeza bungeni kajitokeza kuwatetea ingawa inaonekana anaweza kupata upionzani mkali kutoka vyama vingine.

      Kwa vile fikra za madaktari hawa zinaendana na fikra za CHADEMA ni ukweli usiopingika kwamba madaktari watapambana bega kwa bega kama alivyofanya dr. Che Guevara na Fidel Castro.

      Drs are people of their words, when they say it they mean it. When they are ready to die for something, they know know what death is, because they have been seeing dead people everyday!

      Hii ndio tabia ya Drs (people of their words) ambayo pinda alikuwa haijui, alifikiri akipiga mkwala, kesho watakuwa wanakanyagana kuwahi ofisini.
      Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa,
      Jina Lake Lihimidiwe!.

      RIP Dr. Kyaruzi!.

      Pasco.

      TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Fabian Massawe kuomboleza kifo cha Mzee Dkt.Vedastus Nshunju Kyaruzi ambaye aliaga dunia mwishoni mwa wiki kwenye Hospitali ya Mkoa wa Kagera mjini Bukoba baada ya ugonjwa wa muda mfupi.

      Katika uhai wake, Dkt. Kyaruzi ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 92 alipata kuwa Katibu Mkuu wa Vyama vya Tanganyika African Association (TAA) na Tangayika African National Union (TANU), Mwakilishi wa Kudumu wa Tanganyika katika Umoja wa Mataifa (UN), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ulinzi na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto (UNICEF), Kanda ya Afrika, Kusini mwa Jwangwa la Sahara, akiwa na Makao yake Mjini Lagos, Nigeria.

      Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kikwete amesema kuwa amehuzunishwa na kufadhaishwa na habari za kifo cha Balozi Kyaruzi ambaye alilitumikia Taifa la Tanzania na nchi nyingine kwa miaka mingi na kwa uaminifu,uadilifu na ufanisi mkubwa katika nafasi mbali mbali ambazo alipata kuzishikilia katika maisha yake.

      “Nimepokea habari za kifo cha Mzee Kyaruzi kwa huzuni kubwa kwa sababu ya mchango mkubwa ambao aliutoa katika maisha yake kwenye utumishi wa taifa letu kuanzia kwenye nafasi za uongozi wa kijamii na kisiasa katika vyama vya TAA na TANU hadi kwenye utumishi wa Serikali huru ya Tanganyika na kwenye Umoja wa Mataifa,” amesema Rais Kikwete katika salamu zake.

      Ameongeza Rais Kikwete: “Nakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Kagera salamu za rambirambi za dhati za moyo wangu kufuatia kifo cha Mzee Kyaruzi. Nakuomba pia kupitia kwako unifikishie salamu zangu kwa wana-familia wote wa familia ya Marehemu Kyaruzi. Wajulishe kuwa niko nao katika wakati huu mgumu wa maombolezo. Naungana nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa. Nawaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu, Naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, ailaze peponi pema roho ya Marehemu Vedasto Nshunju Kyaruzi. Amen.”

      Imetolewa na:
      Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
      Ikulu.
      Dar es Salaam.

      24 Mei, 2012

    2. Miaka 50

    3. #81
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,544
      Rep Power : 1758
      Likes Received
      2399
      Likes Given
      166

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By chama
      Bwana Mohamed Said
      Utafiti wako una mapungufu mengi sana katika dunia hii wapo wapotoshaji na wanaotafuta ukweli; wapo watafiti wanaodai HIV na AIDS havina uhusiano wapo wanaodai Malnutrition inasababisha AIDS; hao wote wanajiita ni watafiti sawa na wewe; nimekuuliza kwanini hukumuhoji Dr. Kyaruzi alipodai aliingoza TAA badala ya kuja na majibu mbadala umerukia mambo mengine wewe ndiye mwenye mashaka na historia ya Taifa hili nilitumai ukiwa kama unavyojinadi mtafiti ungemtafuta Dr. Kyaruzi ili akufafanulie ni lini aliiongoza TAA; historia tunayoingelea ni takribani miaka 60; unafurahisha sana kuitwa yaani kuitwa scholar umeona ni jambo kubwa sana, wapo watu wanaitana masheikh huku hata elimu ya dini hawana wakati ni dhihaka za kidunia; na hasa unapoongelea kwenye watu wenye elimu duni au wasiojua. Utafiti wako ni wa kupinga kauli za wafu; mtafiti mwenye kutaka kujua ukweli huwakabili wahusika na kupata kauli thabiti; kama ambavyo uliweza kwenda kwa Sykes na ukasoma makaburasha; na kama unavyodai familia ilikunyima baadhi ya makaratasi (rejea matoleo yako ya nyuma) huo ni uthibitisho wa wazi utafiti ulishakuwa na mapungufu; Dr. Kyaruzi(R.I.P) amefariki juzi leo umekuja kuhoji kauli zake; sasa tumwamini nani yeye aliyeshiriki kwenye siasa wakati wa TAA au wewe uliyehadithiwa? Bwana Mohamed watifiti wa aina yako wapo wengi sana ni sawa na wale wanaodai Holocaust haikutokea!

      Chama
      Gongo la Mboto DSM
      Ndugu yangu Chama,

      Mbona hili la upungufu katika utafiti wangu nishalikubali?
      Kazi yoyote ya binadamu haikosi upungufu.

      Ikiwa ni hivyo hapana haja ya sisi kurejea tena na tena katika upungufu wa utafiti wangu au wa mwandishi mwingine.

      Kuhusu kumhoji Dk. Kyaruzi si yeye peke yake ambae sikumhoji wako wengi sana sikujaaliwa kukutananao lakini nimekufahamisha kuwa nilimuomba mjukuu wake ambae ni mwandishi amfanyie mahojiano na aandike maisha ya babu yake kama Aisha Daisy Sykes alivyomuhoji baba yake Abdulwahid Sykes na tukapata kazi ambayo hadi leo tunaitumia: "Kleist Sykes: The Townsman." Kutoka kalamu ya Daisy ndipo tulipokujajua African Association iliasisiwa vipi na mengineyo katika siasa za Tanganyika kati ya 1900 hadi 1950.

      Tuingie katika "Makabursha ya Sykes" ambayo nilinyimwa.

      Ukweli ni huu.

      Nimesoma majalada yote ya Sykes isipokuwa shajara (diaries) za Abdulwahid Sykes. Hizi sikupewa na nadhani ni kwa kuwa shajara ni kitu cha ndani mwa mtu na waliona majalada yale yalitosha kwa utafiti wangu.

      Bado nashikilia kuwa shajara za Abdulwahid ni muhimu sana katika kuelewa nini kilikuwa kikipitika kati ya 1950 hadi 1954 alipokuja kuasisi TANU.

      Labda kuna usilolijua ndiyo maana umekuja na neno "kuhadithiwa" hivyo sistahili kuaminiwa.
      Si lazima uishuhudie historia ili uiandike.

      Fanya utafiti katika hilo au waulize wajuzi watakufahamisha.

      Ukiachilia mbali kuhadithiwa kwanza nikufahamishe kuwa mie mwenyewe nimeishi katika kipindi hicho lau kama nilikuwa mtoto na babu yangu Salum Abdallah alikuwa katika wanachama wa mwanzo wa African Association na TANU.

      Kwa ajili hii basi familia yangu ina mpigania uhuru.

      Sasa katika hali kama hii mie si muhadithiwa bali niliishi katika kipindi kile na watu waliosukuma gurudumu la historia ya uhuru wa Tanganyika. Kuhadithiwa kwangu hakuwezi kuwa sawa na yule ambae hata Sheikh Hassan bin Ameir hakujaaliwa kumtia machoni.

      Tuje katika holocaust.

      Napenda nikueleze kuwa katika moja ya fani zangu ni historia ya Vita Kuu ya Pili na holocaust yake khasa kipande cha Auschwitz.

      Ikiwa utachukua kisa hiki cha kukataa matanuri ya janga ya Auschwitz hapa mfano huu umekuenea wewe.
      Wewe ndiye unaeshughulishwa na kukataa na kuuogopa ukweli.

      Sie mie.

      Mimi naujua ukweli wa historia ya uhuru wa Tanganyika.

      Nimeandika vitabu vitatu katika somo hilo na nimealikwa kutoa mihadhara kwingi sana ndani na nje ya Tanzania.
      Marekani, Ulaya na Afrika.

      Ama kuwa "scholar" siwezi kukasirika kuitwa hivyo na wala sijaomba niitwe hivyo.

    4. #82
      chama's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 6th August 2010
      Posts : 4,934
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1177
      Likes Given
      915

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Mohamed Said

      Bwana Mohamed
      Nilishawahi kukueleza mtafiti unapokuwa na agenda binafsi hata ufafiti unakuwa batili; lengo la utafiti ni kutafuta ukweli ili kuelemisha jamii na si kuipotosha jamii; hizo dairies za Abdul Wahid Syskes (R.I.P) inawezekana kabisa zilikuwa na ukweli ambao ungebadilisha mtiririko mzima na hitimisho la utafiti wako; ni kweli si lazima uishuhudie historia ili uaminiwe hii tunaiongelea hapa ni takribani miaka 60 wapo watu wengi ambao wanaishi leo hii na wameishuhudia historia hii; Bwana Mohamed tumesoma historia ya Europe 1600 and beyond tumeielewa itakuja hii ya Tanzania ambayo tumeshuhudia baadhi ya vipande vyake?
      Bwana Saidi babu yako alikuwa mpigania uhuru hata mimi binafsi babu yangu alikuwa mpigania uhuru; wengi tu walipigania uhuru wetu; Bwana Said ulikuwa na nafasi nzuri sana ya kuwahoji wahusika wala ulikuwa huna sababu ya kumtuma mjukuu wa Dr. Kyaruzi amuhoji babu yake hilo lilikuwa jukumu lako wewe unayetafuta ukweli. Sikuwahi kusoma tafiti zako za Holocaust hebu nipe dondoo kama ulikataa hiyo basi kweli nitaamini nilichokiamini. Endelea kuitwa scolar mimi naitwa shekhe sijakataa

      Chama
      Gongo la Mboto DSM
      Last edited by chama; 3rd June 2012 at 10:42.

    5. #83
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22277

      Default

      Quote By chama
      Bwana Mohamed
      Nilishawahi kukueleza mtafiti unapokuwa na agenda binafsi hata ufafiti unakuwa batili; lengo la utafiti ni kutafuta ukweli ili kuelemisha jamii na si kuipotosha jamii; hizo dairies za Abdul Wahid Syskes (R.I.P) inawezekana kabisa zilikuwa na ukweli ambao ungebadilisha mtiririko mzima wa utafiti; ni kweli si lazima uishuhudie historia ili uaminiwe hii tunaiongelea hapa ni takribani miaka 60 wapo watu wengi ambao wanaishi leo hii na wameishuhudia historia hii; Bwana Mohamed tumesoma historia ya Europe 1600 and beyond tumeielewa itakuja hii ya Tanzania ambayo tumeshuhudia baadhi ya vipande vyake?
      Bwana Saidi ya babu yako alikuwa mpigania uhuru hata mimi binafsi babu yangu alikuwa mpigania uhuru; wengi tu walipigania uhuru wetu; Bwana Said ulikuwa na nafasi nzuri sana ya kuwahoji wahusika wala ulikuwa huna sababu ya kumtuma mjukuu wa Dr. Kyaruzi amuhoji babu yake hilo lilikuwa jukumu lako wewe unayetafuta ukweli. Sikuwahi kusoma tafiti zako za Holocaust hebu nipe dondoo kama ulikataa hiyo basi kweli nitaamini nilichokiamini. Endelea kuitwa scolar mimi naitwa shekhe sijakataa

      Chama
      Gongo la Mboto DSM
      Mkuu Chama, kule kwenye makaka za Maalim MS, nilimpongeza kwa kutujuza tusiyo yajua lakini nikatoa anga "He is a man with a mission" His mission ndiyo ile agenda yake sote tunaijua hiyo hakuhitaji kumhoji Dr. Kyaruzi!. MS ni very slipery kwenye kukwepa maswali yenye majibu yatakayo muumbua. Nimemuliza mtu mwenye kustahili haswa kuitwa muasisi ni nani kati ya aliyetoa wazo mkinywa kahawa na kiongozi wa kwanza?. Hakujibu!. Nikamuuliza nh wakati gani chama kinaitwa kilizaliwa, alikwepa!.
      chama likes this.

    6. #84
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,544
      Rep Power : 1758
      Likes Received
      2399
      Likes Given
      166

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By chama
      Bwana Mohamed
      Nilishawahi kukueleza mtafiti unapokuwa na agenda binafsi hata ufafiti unakuwa batili; lengo la utafiti ni kutafuta ukweli ili kuelemisha jamii na si kuipotosha jamii; hizo dairies za Abdul Wahid Syskes (R.I.P) inawezekana kabisa zilikuwa na ukweli ambao ungebadilisha mtiririko mzima na hitimisho la utafiti wako; ni kweli si lazima uishuhudie historia ili uaminiwe hii tunaiongelea hapa ni takribani miaka 60 wapo watu wengi ambao wanaishi leo hii na wameishuhudia historia hii; Bwana Mohamed tumesoma historia ya Europe 1600 and beyond tumeielewa itakuja hii ya Tanzania ambayo tumeshuhudia baadhi ya vipande vyake?
      Bwana Saidi babu yako alikuwa mpigania uhuru hata mimi binafsi babu yangu alikuwa mpigania uhuru; wengi tu walipigania uhuru wetu; Bwana Said ulikuwa na nafasi nzuri sana ya kuwahoji wahusika wala ulikuwa huna sababu ya kumtuma mjukuu wa Dr. Kyaruzi amuhoji babu yake hilo lilikuwa jukumu lako wewe unayetafuta ukweli. Sikuwahi kusoma tafiti zako za Holocaust hebu nipe dondoo kama ulikataa hiyo basi kweli nitaamini nilichokiamini. Endelea kuitwa scolar mimi naitwa shekhe sijakataa

      Chama
      Gongo la Mboto DSM
      Bwana Chama,

      Naheshimu fikra zako siwezi kukulazimisha vinginevyo.

    7. #85
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,544
      Rep Power : 1758
      Likes Received
      2399
      Likes Given
      166

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Pasco
      Mkuu Chama, kule kwenye makaka za Maalim MS, nilimpongeza kwa kutujuza tusiyo yajua lakini nikatoa anga "He is a man with a mission" His mission ndiyo ile agenda yake sote tunaijua hiyo hakuhitaji kumhoji Dr. Kyaruzi!. MS ni very slipery kwenye kukwepa maswali yenye majibu yatakayo muumbua. Nimemuliza mtu mwenye kustahili haswa kuitwa muasisi ni nani kati ya aliyetoa wazo mkinywa kahawa na kiongozi wa kwanza?. Hakujibu!. Nikamuuliza nh wakati gani chama kinaitwa kilizaliwa, alikwepa!.
      Bwana Pasco,

      Ikhtilafu lazima ziwepo.
      Nami nakubali kuwa tunapingana katika mengi.

    8. RukaaJuu Final

    9. #86
      chama's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 6th August 2010
      Posts : 4,934
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1177
      Likes Given
      915

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Mohamed Said
      Bwana Chama,

      Naheshimu fikra zako siwezi kukulazimisha vinginevyo.
      Bwana Mohamed Said
      Mbona unataka kususa kwenye mjadala hapa hatulazimishani tunajaribu kuelemishana na kutafuta ukweli; kama umekiri utafiti wako una mapungufu huoni kuwa unapotosha jamii? Hebu nipe hadithi Holocaust .

      Chama
      Gongo la Mboto DSM
      Last edited by chama; 3rd June 2012 at 18:21.

    10. #87
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,544
      Rep Power : 1758
      Likes Received
      2399
      Likes Given
      166

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By chama
      Bwana Mohamed Said
      Mbona unataka kususa kwenye mjadala hapa hatulazimishani tunajaribu kuelemishana na kutafuta ukweli; kama umekiri utafiti wako una mapungufu huoni kuwa unapotosha jamii? Hebu nipe hadithi Holocaust .

      Chama
      Gongo la Mboto DSM
      Bwana Chama

      Nisuse nini ndugu yangu?
      Hapo nimekupa jibu langu na ningelitaka kususa ningekaa kimya.

      Kuhusu holocaust.

      Ingia google.
      Humo mna kila kitu.

    Page 5 of 5 FirstFirst ... 345

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...