Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

    Report Post
    Page 4 of 5 FirstFirst ... 2345 LastLast
    Results 61 to 80 of 87
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22277

      Default Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Kutokana na hali ya kusubiria baadhi ya wajukuu zake marehemu waishio Ulaya, mazishi ya aliyekuwa Rais wa Chama cha TAA (kabla ya kumkabidhi kiti hicho kwa Mwl. Nyerere) Dr. Vedastus Kyaruzi hayatafanyika leo (Alhamis, 24/05/2012) bali yatafanyika siku ya Jumamosi 26/05/2012 huko Kyaka kijijini Nyabihanga katika wilaya ya Missenyi
      Wanabodi,

      Nimepokea taarifa za kifo cha mmoja wa waanzilishi wa chama cha TAA na baadae TANU, Dr. Vedastus Kyaruzi kilichotokea juzi hapa jijini Dar es Salaam na mwili wake kusafirishwa leo kuelekea Bukoba kwa mazishi yatakayofanyika J.5.

      Habari hizi ni kwa mujibu wa Bw. Prosper Vedasto wa Channel Ten.

      Kwa wafuatiliaji wa historia ya siasa za Tanzania, Mzee Kyaruzi ametajwa sana katika makala za Maalim Mohamed Said kuwa yuu miongoni mwa mashujaa wa nchi hii waliosahaulika au tulio sahaulishwa na inawezekana ndio maana hata msiba wake uko low profile!.

      Nadhani nisingekutana na Bw. Prosper, msiba huu muhimu ungeweza kutupita juu kwa juu!.

      Quote By Familia
      Tunaomba tusahihishe taarifa kutoka kwa Bw. Prosper;

      Dr.Vedastus Kyaruzi amefariki jana usiku wa saa 1:20 usiku na umauti umemkuta akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa huko Bukoba mjini.

      Mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi ya tarehe 24 Mei,2012.
      Kwa msiomfahamu Dr. Kyaruzi, hapa anaelezewa vizuri na mwana JF mwenzetu, mpigania uhuru mwenzake!.

      Quote By Mpigania Uhuru
      Wanasiasa katika jamii yetu wamekuwa wakiwachukulia madaktari kama watu ambao muda mwingi wako na wagonjwa na wajui mambo ya kijamii yanayoendelea, imefika wakati hata sitahiki zao ambazo ziko wazi katika "goverment standing order' wananyimwa bila sababu ya msingi. Mfano intern drs waliodai mshahara wao wa mwezi ambayo ni haki yao, baadae walipewa na kufukuzwa muhimbili!

      Ukweli ni kwamba drs wamehusika sana katika ukombozi wa kisiasa wa tanganyika na dunia kwa ujumla.

      Naomba nitoe mifano miwili.

      Kwanza ni Dr. Vedasto Kyaruzi ambaye alikuwa president wa TAA mwaka 1950 na katibu wake akiwa Abdulwahid Sykes. Kabla ya kuingia kwa huyu daktari TAA ilikuwa ni chama cha kijamii ambacho hakikuwa na mwelekeo wa kudai uhuru.

      Dr. huyu ndiye aliyeleta mapinduzi makubwa akiwa kama president wa TAA wakati Nyerere anakuja kujiunga na harakati za kudai uhuru msingi mkubwa ulishaandaliwa na huyu Dr. kyaruzi, kwa bahati mbaya watanganyika wengi hawajui/hawajaelezwa mchango wake i.e forgatten people.

      Mfano wa pili ni Dr. Che Guevara huyu alikuwa ni daktari na mwanamapinduzi wa ukweli ambaye amepigana vita vya msituni na kufanikisha uhuru wa CUBA, ukombozi wa DRC etc.

      Sasa hivi kuna harakati nyingi za ukombozi wa jamii yetu zikioongozwa na CHADEMA.

      Madaktari nao sasa wameamua kujiunga katika vita hii. Mfano mzuri ni Mh. Zitto leo alivyojitokeza bungeni kajitokeza kuwatetea ingawa inaonekana anaweza kupata upionzani mkali kutoka vyama vingine.

      Kwa vile fikra za madaktari hawa zinaendana na fikra za CHADEMA ni ukweli usiopingika kwamba madaktari watapambana bega kwa bega kama alivyofanya dr. Che Guevara na Fidel Castro.

      Drs are people of their words, when they say it they mean it. When they are ready to die for something, they know know what death is, because they have been seeing dead people everyday!

      Hii ndio tabia ya Drs (people of their words) ambayo pinda alikuwa haijui, alifikiri akipiga mkwala, kesho watakuwa wanakanyagana kuwahi ofisini.
      Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa,
      Jina Lake Lihimidiwe!.

      RIP Dr. Kyaruzi!.

      Pasco.

      TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Fabian Massawe kuomboleza kifo cha Mzee Dkt.Vedastus Nshunju Kyaruzi ambaye aliaga dunia mwishoni mwa wiki kwenye Hospitali ya Mkoa wa Kagera mjini Bukoba baada ya ugonjwa wa muda mfupi.

      Katika uhai wake, Dkt. Kyaruzi ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 92 alipata kuwa Katibu Mkuu wa Vyama vya Tanganyika African Association (TAA) na Tangayika African National Union (TANU), Mwakilishi wa Kudumu wa Tanganyika katika Umoja wa Mataifa (UN), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ulinzi na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto (UNICEF), Kanda ya Afrika, Kusini mwa Jwangwa la Sahara, akiwa na Makao yake Mjini Lagos, Nigeria.

      Katika salamu zake za rambirambi, Rais Kikwete amesema kuwa amehuzunishwa na kufadhaishwa na habari za kifo cha Balozi Kyaruzi ambaye alilitumikia Taifa la Tanzania na nchi nyingine kwa miaka mingi na kwa uaminifu,uadilifu na ufanisi mkubwa katika nafasi mbali mbali ambazo alipata kuzishikilia katika maisha yake.

      “Nimepokea habari za kifo cha Mzee Kyaruzi kwa huzuni kubwa kwa sababu ya mchango mkubwa ambao aliutoa katika maisha yake kwenye utumishi wa taifa letu kuanzia kwenye nafasi za uongozi wa kijamii na kisiasa katika vyama vya TAA na TANU hadi kwenye utumishi wa Serikali huru ya Tanganyika na kwenye Umoja wa Mataifa,” amesema Rais Kikwete katika salamu zake.

      Ameongeza Rais Kikwete: “Nakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Kagera salamu za rambirambi za dhati za moyo wangu kufuatia kifo cha Mzee Kyaruzi. Nakuomba pia kupitia kwako unifikishie salamu zangu kwa wana-familia wote wa familia ya Marehemu Kyaruzi. Wajulishe kuwa niko nao katika wakati huu mgumu wa maombolezo. Naungana nao katika kuomboleza msiba huu mkubwa. Nawaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu, Naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, ailaze peponi pema roho ya Marehemu Vedasto Nshunju Kyaruzi. Amen.”

      Imetolewa na:
      Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
      Ikulu.
      Dar es Salaam.

      24 Mei, 2012

    2. RukaaJuu Final

    3. #61
      linux1's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 4
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      je waasisi wengine wa chama na wapigania uhuru wanaenziwa vipi.Au mpaka mauti ziwakute ndiyo serikali inajiweka kimbelembele.

    4. #62
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,543
      Rep Power : 1758
      Likes Received
      2398
      Likes Given
      166

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Son of Alaska
      Mohamed Said wewe kama binadamu lazima utakuwa na mapungufu yako-lakini makala zako zimetufungua macho sana.
      SOA\\Upungufu ndiyo sifa ya binadamu.Alekamilika ni Allah SW peke yake.

      M
      Son of Alaska and Mzee Kijana like this.

    5. #63
      Mag3's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 31st May 2008
      Posts : 3,541
      Rep Power : 1805
      Likes Received
      2464
      Likes Given
      2505

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Kwa faida ya Wasomaji na wanajamvi wenzangu naomba tu kuweka mambo manne sawa wakati tunamuenzi Dr. Vedasto Kyaruzi (RIP).

      1. AA ilianzishwa mwaka 1929 mwasisi wake na Raisi akiwa Cecil Matola.
      2. AA ilidumu hadi mwaka 1948 ikazaliwa TAA mwasisi wake na Raisi akiwa Dr. Vedasto Kyaruzi.
      3. TAA ilidumu hadi mwaka 1954 ikazaliwa TANU, mwasisi wake na Raisi akiwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
      4. TANU ilidumu hadi mwaka 1977 ikazaliwa CCM.

      Nawatakia majadiliano mema.
      The true sign of intelligence is not knowledge but imagination.
      Education is what remains after one has forgotten what one has learned in School
      -Albert Einstein.

    6. #64
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,435
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4795
      Likes Given
      2861

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Kwanza kabisa nimshukuru Mkandara kwa 'link' katika moja ya post zake ambayo inatupa ufahamu mwingine wa historia kwa kiasi chake.

      Pili, tukubaliane kuwa msiba wa Dr Kyaruzi haukupewa uzito unaostahili. Nilidhani baada ya Rais Kikwete kuwatambua waasisi na wale waliotuwezesha kufika miaka 50 pengine ungekuwa mwanzo mpya wa kuwaenzi wazee wetu. Mtu kama marehemu ambaye amekitumikia chama na serikali hakutendewa ilivyopaswa wakati tunampeleka mapunzikoni.
      Ni wazi kuwa Dr alishiriki sana katika siasa za ndani na nje na mchango wake 'hatuwezi kuuwekea thamani'

      Kwa hali yoyote huyu ni mzalendo bila kujali itikadi zake au ukabila. Mohamed Said ameandika kuwa alipohamishiwa Morogoro alikuwa anafanya ziara kila mwisho wa wiki kukijenga chama. Hakusubiri posho au allowance na alitoa nauli yake. Dr Kyaruzi hakufanya hivyo kuwakomboa Wahaya, alifanya hayo kuwakomboa Watanganyika.

      Dr alishirikiana na watu wa aina zote wakiwa na lengo moja la kukiacha kizazi hiki kikiwa huru. Nina uhakika katika mambo yaliyompa faraja ndani ya dhiki za dunia hii ni kuona watoto na wajuu zake wakisafiri kutoka Bukoba na kwenda popote bila kibali au kufuatiliwa na mkoloni.

      Hizi ndizo thamani walizotuachia akina Dr Kyaruzi, Sykes, Plantan, Chaurembo, Lugazia, Tsere, Nyerere, Kawawa, Bibi titi, Rupia, Kirlo n.k.

      Kama kuna makosa tunayoyafanya wakati huu wa msiba ni kutaka kuwaweka wazee hawa katika makundi. Lile kundi la muhimu na kundi saidizi. Ni utovu mkubwa wa heshima tutakapozichukua jitihada za hawa wazee na kuzigawa kwa makundi na viwango kulingana na matakwa ya nafsi zetu.

      Mchango wa Abd Sykes kama kiongozi ni wa nyakati zake kama walivyokuwa waliomtangulia na waliofuata.
      Inapotokea mfadhili wa chama kama Rupia kutajwa tu kwa ufadhili wake na si mchango katika chama inatia maudhi.
      Sijui kama John Rupia alichangia kwasababu alikuwa anawakilisha kundi fulani katika jamii. Na kama ni si hivyo kwanini basi atokee mtu aseme shughuli za mapambano zimeongozwa na watu fulani zaidi ya wengine?

      Tuwaenzi wazee wetu hata waliobadilisha pancha za magari wakati wa kudai uhuru. Tukumbuke kuwa hawakufanya hivyo kuwakilisha makundi bali uzalendo wa nchi yao. Uzalendo ndio utuunganishe na wala usitugawe kama inavyoanza kujitokeza.

      Ahsanteni wazee wetu mliotuacha huru, Pumzika kwa amani Dr Kyaruzi kama tunavyowaombea wale waliokutangulia
      Ogah likes this.

    7. #65
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,543
      Rep Power : 1758
      Likes Received
      2398
      Likes Given
      166

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Mag3
      Kwa faida ya Wasomaji na wanajamvi wenzangu naomba tu kuweka mambo manne sawa wakati tunamuenzi Dr. Vedasto Kyaruzi (RIP).

      1. AA ilianzishwa mwaka 1929 mwasisi wake na Raisi akiwa Cecil Matola.
      2. AA ilidumu hadi mwaka 1948 ikazaliwa TAA mwasisi wake na Raisi akiwa Dr. Vedasto Kyaruzi.
      3. TAA ilidumu hadi mwaka 1954 ikazaliwa TANU, mwasisi wake na Raisi akiwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
      4. TANU ilidumu hadi mwaka 1977 ikazaliwa CCM.

      Nawatakia majadiliano mema.
      Mag3,

      Naomba nitoe maelezo kidogo.

      Cecila Matola hakuasisi African Association ingawa alikujakuwa kiongozi wake. Fikra ya kuanzishwa kwa AA ilitolewa kwa Kleist Sykes na Dk. Aggrey alipotembelea Tanganyika mwaka 1924. Habari kamili ya AA zinapatikana katika kitabu alichohariri John Iliffe "Modern Tanzanians" katika "The Townsman: Kleist Sykes" kama alivyoandika mjukuu wa Kleist, Daisy Aisha Sykes.

      TAA haikuzaliwa mwaka 1948 bali AA ilibadili jina tu mwaka huo wa 1948 baada ya kutengana na Zanzibar.

      TANU haiukuasisiwa na Nyerere bali na Abdulwahid Sykes. Habari za TANU zinaweza kupatikana katika kitabu "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924 1968... "

      CCM ndiyo iliyoasisiwa na Nyerere.

    8. Miaka 50

    9. #66
      Mzee Kijana's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 25th November 2011
      Posts : 126
      Rep Power : 403
      Likes Received
      30
      Likes Given
      40

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Mkandara
      Jamani isitokee ktk kifo cha huyu babu wetu, kamanda wetu mkaanza unafiki na majungu. Dr.Kyaruzi na Nyerere wote walikutana Tabora secondary, ikiitwa Milambo secondary. Na wote walikwenda Makelele Uganda. Nawaomba sana msome maelezo yake mwenyewe marehemu Dr. Kyaruzi ukurasa wa 394 pia ni vizuri sana mkisoma habari hii toka nyuma na kuendelea mpate kujua mengi ya historia ya nchi yetu na watu waliohusika ambao hadi leo hawafahamiki na kwa sababu mbali mbali. Kifupi dr. mwenyewe anasema Nyerere alikuwa na tabia ya kuamini watu wasioaminika na kweli kabisa haya ndio mapungufu makubwa ya Nyerere ambayo yame tugharimu sana.

      RIP Dr. Kyaruzi - Mpambanaji.
      Mkuu hapo kwenye red hebu fafanua vizuri maana tunashindwa kukuelewa. Tabora secondary (Tabora school) na Milambo ni shule mbili tofauti. Sisi tuliosoma huko tunajua vizuri. Milambo haikuwa ikiitwa Tabora secondary bali Saint Mary enzi za ukoloni. Nyerere alisoma Tabora School baadaye Makerere na Edinburg halafu akaja kufundisha Saint Mary, Milambo na huo ndio ukweli. Sijui Dr. Kyaruzi na Nyerere walikutana wapi ktk shule hizo mbili.

      Hoja ya kusahaulika Dr. Kyaruzi si ngeni kwa watu tunaomjua Nyerere na historia ya nchi hii. Kwa ujumla Nyerere kwa makusudi mazima aliamua kuiandika upya historia ya nchi hii kwa kujitukuza binafsi na kuwapoteza mashujaa wengine. Hii ni roho mbaya ambayo kamwe haitasameheka. Mohamed Said ameyaandika haya kwa kina kabisa. Hali ni mbaya kiasi hata wasomi wetu wengi hawawajui vinara hasa waliopigania uhuru wa nchi hii zaidi ya Nyerere. Kwa mfano, kuna mtu anaitwa Martin Kayamba huyu mwaka 1922 ambao ni mwaka aliozaliwa Nyerere alianzisha Tanganyika Territory African Civil Servants Association kupigania haki za wafanyakazi. Wangapi ktk sisi tunaomjua huyu?
      Bukyanagandi likes this.

    10. #67
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,543
      Rep Power : 1758
      Likes Received
      2398
      Likes Given
      166

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      DK. VEDASTO KYARUZI DAKTARI MWANAHARAKATI WA TAA
      Na Mohamed Said
      Utangulizi
      Katika moja ya misiba mikubwa iliyoikumba Tanzania ni kukosekana kwa historia inayoweza kuaminika kuhusu mashujaa wake waliopigania uhuru kutoka kwa Waingereza. Gazeti la Raia Mwema (Mei 23 - Mei 29, 2012) limefahamisha umma kuhusu kifo cha Dk. Vedasto Kyaruzi na kwa muhtasari wakaweka sifa zake. Kwa bahati mbaya sana sifa walizoweka hazikuwa za kweli kwa kiasi fulani. Mfano ni pale makala iliposema Dk. Kyaruzi ndiye aliyemwachia uongozi Nyerere katika TAA na kuwa alikuwa rais wa kwanza wa TAA. Ukweli ni kuwa Nyerere na Dk. Kyaruzi hawakupata kukutana katika uongozi wa TAA kwa hiyo isingewezekana kwa Dk. Kyaruzi kumwachia Nyerere uongozi. Wakati Nyerere anaingia TAA Makao Makuu, Dar es Salaam mwaka 1952 Kyaruzi alikuwa keshaondoshwa Dar es Salaam na wakoloni kapelekwa Nzega na chama kilikuwa chini ya uongozi wa Abdulwahid Sykes akiwa katibu na kaimu rais. Abdulwahid ndiye aliyeikabidhi TAA kwa Nyerere mwaka 1953. Jingine ni kuwa Kyaruzi wala hakuwa rais wa kwanza wa TAA kwani chama kilianzishwa Dar es Salaam mwaka 1929 kikijulikina kama African Association na wakati huo Dk Kyaruzi alikuwa bado mtoto mdogo. Mwaka wa 1948 ndipo kilipokuja badilishwa jina na kuitwa Tanganyika African Association (TAA) Kwa nia njema kabisa naweka hapa maisha ya siasa ya Dk. Kyaruzi kama nilivyoyaandika katika moja ya sura za kitabu changu “Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924 - 1968...” Katika makala haya nimefanya mabadiliko hapa na pale ili kumwezesha msomaji kufuatilia siasa za TAA kama zilivyokuwa wakati wa uongozi wa Dk. Kyaruzi mwaka wa 1950.
      Juhudi za Kubadili Uongozi Mkongwe wa TAA Uliochoka, 1949 - 1950
      Kwa miongo miwili kuanzia mwaka wa 1929 Chama cha African Association kilikuwa mikononi mwa viongozi watu wazima sana mfano wa Mzee bin Sudi na Mwalimu Thomas Sauti Plantan ambae alikuwa rais wa chama hicho mwaka wa 1949. Mzee bin Sudi na Kleist Sykes walipata vilevile kuwa rais na katibu wa African Association na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika kwa wakati mmoja katika miaka ya 1930. Vyama hivi viwili vilikuwa vikifanya harakati zake kwa karibu na ushirikiano mkubwa kwa kuwa viongozi wake walikuwa viongozi wa ngazi ya juu katika vyama hivyo viwili. Siasa za kikoloni zilikuwa zikibadilika na kwa hivyo zilihitaji damu change kama za akina Dk. Kyaruzi zenye mawazo na mbinu mpya ili kuongoza harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Serikali ya kikoloni ilikuwa kila uchao inabadili mitindo, hila na mbinu za ukandamizaji ili kuendeleza utawala wake. Ukitazama mwelekeo wa siasa na mazingira ya wakati ule, uongozi wa wazee katika African Association, kwa hali yao na kutokana na mambo yalivyokuwa yakiwakabili, walikuwa hawana uwezo wa kukabiliana na changamoto ya ukoloni. Lakini pamoja na yote hayo, wazee hawakutaka kuachia madaraka. Jambo hili lilizusha mvutano baina ya wazee na wanasiasa vijana. Vijana hawa walikuwa akina Abdulwahid na Ally Sykes (ambao baba yao, Kleist Sykes ndiye aliyeasisi African Association), Tewa Said Tewa, Stephen Mhando, Waziri Dossa Aziz, James Mkande, na wale madaktari watano - Vedasto Kyaruzi, Joseph Mutahangarwa, Luciano Tsere, Michael Lugazia na wengineo. Haya yalikuwa ni mapambano baina ya kizazi kipya na kile cha kale. Vita Kuu ya Pili ilikuwa imemalizika na ukoloni katika Tanganyika sasa ukawa unakabiliwa na changamoto mpya kutoka kwa vijana wasomi toka Chuo cha Makerere na askari wa Tanganyika waliopigana Burma katika Vita ya Pili Vya Dunia chini ya King’s African Rifles (KAR).
      Katika mvutano huu wa madaraka kwa upande wa vijana waliokuwa wakiinukia alikuwepo kijana wa Kidigo kutoka Tanga aliyehitimu Makerere, Hamza Kibwana Mwapachu. Mwapachu alikuwa ameajiriwa na Idara ya Maendeleo ya Jamii kama 'Assistant Welfare' Officer (Msaidizi wa Ustawi wa Jamii), Ilala Welfare Centre mjini Dar es Salaam. Historia ya Mwapachu katika siasa ilianza Makerere College, Uganda ambako alijihusisha na mambo ya siasa wakati alipokuwa mwanafunzi. Mwaka wa 1947 Mwapachu akiwa Tabora alichaguliwa kuwa katibu wa African Association, Julius Nyerere akiwa naibu wake. Mwapachu na Abdulwahid walikuwa na usuhuba mkubwa. Mwaka wa 1950 Mwapachu alikuwa na umri wa miaka 32 na Abdulwahid alikuwa na umri wa miaka 26, mdogo kwa Mwapachu kwa miaka sita. Vijana hawa wawili walikuja kugeuza mwelekeo wa TAA na wakaingiza ndani ya chama hicho aina mpya ya uongozi na ushawishi uliokuwa haujapata kuonekana katika historia ya Tanganyika. Lakini wote wawili walifariki dunia katika ujana wakiwa na umri wa miaka 44 tu. Na wote wawili wakaja kusahauliwa na historia. Hakuna kati yao ambaye hii leo jina lake linahusishwa na historia ya Tanganyika ingawa wao ndiyo waliomvuta Nyerere katika TAAna siasa za Dar es Salaam ya miaka ya mwanzo ya 1950. Kupitia vijana hawa wawili ndipo historia ya Dk. Kyaruzi ilipoanza. Uongozi wake ulikuwa mfupi katika TAA lakini uongozi huo ulifanya makubwa na kubadilisha sura ya harakati. Katika siku zake za mwisho Dk. Alipata kumwambia mmoja wa watoto wa Hamza Mwapachu kuwa, “Kama si mipango waliyoweka baba yako na Abdulwahid mwaka 1950 tusingelipata uhuru mwaka 1961.” Ofisi ya Mwapachu pale Ilala ilikuwa kituo cha mijadala ya siasa nyakati za mchana. Jioni vikao hivyo vya majadiliano vilihamia Tanga Young Comrades Club. Hiki ilikuwa kilabu maarufu ya vijana wa mji kukutana. Kilabu hii ilikuwa New Street (sasa Mtaa wa Lumumba) karibu na ofisi ya TAA. Mijadala ya siasa nyumbani kwa Abdulwahid au katika ofisi ya Mwapachu Ilala au Tanga Club kidogo kidogo ikawa inaingia katika nadharia ya vipi vijana wangeweza kuuondoa madarakani uongozi wa Mwalimu Thomas Sauti Plantan ndiye aliyekuwa rais wa katibu wake Clemet Mohammed Mtamila. Si kwamba Tanganyika wakati ule ilikuwa na uhaba wa maswala ambayo yangeweza kuamsha mijadala ya siasa. Kulikuwa na mambo kadhaa ambayo kama yangetumiwa kwa ustadi na uongozi wa TAA, shida hizo zingeweza kuleta kwa watu hisia za manung’uniko na chuki dhidi ya serikali ya kikoloni. Vitu ambavyo TAA ingeweza kuvitumia kuwafitini Waingereza dhidi ya wananchi. Unahitaji tu kuzipitia tahariri za Ramadhani Mashado Plantan katika gazeti lake alilokuwa akihariri mwenyewe lililojulikana kama “Zuhra” ili kuweza kufahamu siasa ilivyokuwa ikitokota chini kwa chini Tanganyika katika miaka ya 1950. Rais wa TAA Mwalimu Thomas Plantan na damu yake ya Kizulu ya kupenda vita, baada ya kuwa yupo kwenye nchi yenye amani, aliielekeza bunduki yake porini kuwinda wanyama. Hakuwa na muda kama rais wa TAA kushughulika na masuala ya TAA. Uhodari wake katika kuwinda bado hadi miaka ya 1970 iliweza kushuhudiwa nyumbani kwake Mtaa wa Masasi, Mission Quarters. Kuta za nyumbani kwake zilikuwa zimepambwa na mafuvu ya vichwa vya wanyama aliowaua huko porini Mwalimu Thomas Plantan hakuwa na muda wa kuitisha mikutano au kushughulikia mambo ya TAA kwa sababu alitumia wakati wake mwingi porini. Makao Makuu ya TAA mjini Dar es Salaam yalikuwa kama vile yamegubikwa na usingizi mzito. Barua kutoka matawini hazikuwa zikijibiwa. Baya zaidi, hakukuwepo na mawasiliano yoyote na Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, mjini New York ambalo ndilo lilikuwa likiitawala Tanganyika kama nchi ya udhamini. Juu ya haya ndani ya TAA na uongozi wake kulikuwa na hali na sura nyingi za ukinzani. Schneider Abdillah Plantan mmoja wa viongozi wa TAA alikuwa siku nyingi amekwishaonyesha chuki yake dhidi ya Waingereza na kwa ajili hiyo akawekwa kizuizini wakati wa Vita Vya Pili kwa kuonyesha msimamo wa kumuunga mkono Hitler dhidi ya Waingereza. Yeye mwenyewe mwaka 1914 alipigana Vita vya Kwanza vya Dunia dhidi ya Waingereza akiwa askari katika jeshi la Wajerumani akiwa na ndugu yake Kleist Sykes (wakati ule akijulikana kama Kleist Plantan), Mashado Plantan alikuwa na gazeti lake “Zuhra” ambalo lilikuwa ndiyo sauti ya African Association. Lakini watu hawa walikuwa wazee na wamechoka. Hawakuwa na jipya katika siasa mbali na kuuchukia utawala wa kikoloni. Walipochoshwa na uongozi huu wa wazee na walipoona hakuna lolote la maana liliokuwa siku moja wakati wa alasiri, Abdulwahid na Mwapachu bila ya kumshauri mtu yeyote wakitokea Tanga Club, New Street, walivamia ofisi ya TAA na kufanya mapinduzi kwa kumtoa msobe msobe Clement Mtamila ofisini kwake. Abdulwahid alikuwa bingwa wa ngumi wa Tanganyika na Kenya katika kikosi chake wakati wa vita. Hakupata tabu sana kumtoa nje ya ofisi Mtamila. Baada ya vurugu hii ambayo ilikuwa gumzo la mji kwa wakati ule wazee walisalimu amri na wakaamua kuitisha uchaguzi. Maofisa Wazungu kutoka serikalini walihudhuria mkutano huu kama mbinu ya kuwatisha vijana waliokuwa wakishinikiza mageuzi katika TAA. Bila woga Schneider Plantan aliwakabili na kuwaeleza kuwa uchaguzi utafanyika watake wasitake. Shneider alipigwa risasi mguuni vitani kwa hiyo alikuwa akichechemea. (Katika moja ya sifa zake ni kuwa alikuwa mtu shujaa sana. Hamuogopi yeyote. Shneider ndiyo mtu pekee katika historia aliyesimama uso kwa uso na Nyerere na Shneider akamtukana Nyerere nyumbani kwake Msasani huku akimtazama usoni). Mwezi Machi mwaka 1950, katika Ukumbi wa Arnatouglo, kijana wa Kihaya, Dk. Vedasto Kyaruzi alichaguliwa kuwa rais wa TAA na Abdulwahid Sykes katibu wake. Dk. Kyaruzi alipochukua uongozi, TAA ilikuwa na shilingi 87.00 Barclays Bank, Dar es Salaam. Huu ndiyo ulikuwa mwisho wa wazee, kuongoza TAA. Vilevile ndiyo ukawa mwanzo wa uzalendo na utaifa Tanganyika. Abdillah Schneider Plantan na mdogo wake Ramadhani Mashado Plantan walimuuunga mkono Dk. Kyaruzi katika kuipa TAA uhai mpya ingawa aliyetolewa madarakani alikuwa kaka yao mkubwa Mwalimu Thomas Sauti Plantan. Hivi ndivyo Dk. Kyaruzi alivyoingia katika uongozi wa TAA.
      Dk. Kyaruzi Katika Kamati Ndogo ya Siasa Ndani ya TAA, 1950 - 1951
      Hakuna nyaraka zozote zinazoonyesha kama African Association ilikuwa imetayarisha mpango wa kushughulikia hali ya siasa. Kuelewa mwelekeo wa siasa wakati ule inabidi mtu atazame mwenendo wa viongozi wa TAA na jinsi walivyokuwa wakiyashughulikia mambo tofauti yaliyokuwa yakiwadhili wananchi. Jambo la kwanza walilofanya Dk. Kyaruzi na Abdulwahid Sykes mara tu baada ya kuingia madarakani ni kuunda TAA Political Subcommittee (Kamati Ndogo ya Siasa ya TAA) iliyomjumuisha Sheikh Hassan bin Amir kama mufti wa Tanganyika na Zanzibar; Dk. Kyaruzi, Mwapachu, Said Chaurembo aliyekuwa liwali wa mahakama ya Kariakoo; John Rupia na Stephen Mhando. Kazi ya kamati hii ilikuwa ni kushughulika na masuala yote ya siasa katika Tanganyika. Kuundwa kwake ndiyo hasa ulikuwa mwanzo wa siasa za dhahiri katika Tanganyika na mwanzo wa harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Kwa kipindi cha miaka ishirini na moja African Association ilifanya kazi chini ya katiba isiyokuwa ya siasa. Kwa mara ya kwanza mwaka 1950, TAA chini ya uongozi mpya, ilijipa hadhi ya chama cha siasa, siyo kwa kubadilisha katiba yake bali kwa kuunda kamati ya siasa ndani ya chama. Kamati hii ilikuwa na watu wenye kuwakilisha maslahi na uwezo tofauti, wakiwa halikadhalika wanatokana na uzoefu na hali tofauti. Sheikh Hassan bin Amir Muunguja alikuwa ndiye mufti wa Tanganyika na aliwakilisha Waislam ambao hasa ndiyo waliokuwa wakiongoza mapambano dhidi ya serikali. Said Chaurembo aliwakilisha Wazaramo wa Dar es Salaam na vitongoji vyake. John Rupia kutoka Mission Quarter alikuwa mfanya biashara tajiri na mfadhili wa chama. Stephen Mhando Mbondei kutoka Muheza alijulikana kwa misimamo mikali aliwawakilisha wasomi wa Makerere, Dk. Kyaruzi akiwa mmojawapo. Uongozi huu ndiyo ulioweka msingi wa kuundwa kwa TANU chama kilichokuja kung’oa ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika. Baada ya kuunda kamati hii uongozi wa TAA ulianza kuyaandikia matawi ya TAA ili kuyahuisha. Jambo kubwa lililokabili TAA na ile kamati ya siasa ilikuwa ni hadhi ya Tanganyika kama nchi ya udhamini chini ya Umoja wa Mataifa. Uongozi wa TAA ulimuingiza katika kamati ya siasa Earle Seaton, mwanasheria kutoka Bermuda aliyekuwa akikaa Moshi ili aishauri kamati kuhusu mambo ya sheria ya katiba. Seaton alitakiwa kuishauri jinsi ya kuliendea shauri la kutaka Uingereza itoe uhuru ili Tanganyika ijitawale yenyewe kwa kuwa nchi hiyo haikuwa koloni, bali nchi chini ya udhanini wa Umoja wa Mataifa. Mwaka wa 1948 Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa tayari lilikuwa limetuma ujumbe wake wa kwanza kuzuru Tanganyika. Lakini hakuna jambo lolote la manufaa lilipatikana kutoka kwa ujumbe huo. Makao Makuu ya TAA mjini Dar es Salaam chini ya Dk. Kyaruzi na Abdulwahid ikiungwa mkono na kamati ya siasa sasa ilikuwa ikiamka kutoka kwenye usingizi mzito. Kilichotakiwa ilikuwa ni kupata maswala yakutoa changamoto kwa akili za wale wasomi vijana. Uongozi wa chama cha TAA haukuwa na haja ya kuangaza mbali. Changamoto ilikuja kwa sura ya Constitutional Development Committee (Kamati ya Mapendekezo ya Katiba) iliyoundwa na Gavana Edward Twining na mgogoro wa ardhi ya Wameru. Uingereza ilikuwa ikitawala Tanganyika chini ya kifungu 76 na 77 cha Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Kama mamlaka tawala Uingereza ilitarajiwa kuanzisha na kuendeleza maendeleo ya siasa, uchumi na ya kijamii ya Tanganyika hadi kufikia wakati ambao watu wake wangekuwa tayari kujitawala. Lakini Waingereza walifanya khiyana na hawakutimiza ahadi hiyo. Walijihusisha na kulinda maslahi yao wenyewe ya kikoloni na yale ya watu weupe wachache na wakaendelea kuwapuuza Waafrika waliokuwa wengi na wenye nchi. Labda kwa kuanua ngoma juani, Gavana Twining alikaribisha mapendekezo kutoka kwa watu mashuhuri, vyama vya ustawi wa jamii na Native Authorities, kutaka mapendekezo ya jinsi Tanganyika itakavyotawaliwa. Kamati ya siasa ya TAA ilipeleka mapendekezo yake ambayo yalitiwa sahihi na wajumbe wote wa kamati ya siasa. Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, John Rupia, Stephen Mhando na Said Chaurembo. Katika taarifa yake ya TAA ya mwaka ya 1950 Abdulwahid aliandika: “Kwa ajili ya maslahi ya Waafrika na kulinda maslahi ya chama hiki na yale ya jumuiya ya Waafrika kwa ujumla, chama kimeweka wakili atakayeshauri juu ya mambo ya sheria. Wakili huyo ni Bwana E. E. Seaton wa Moshi. Mara kwa mara amekiandikia chama hiki juu ya masuala mbali mbali ya siasa, na kwa kiasi kikubwa ushauri wake umesaidia wakati chama hiki kilipokuwa kikitayarisha mapendekezo juu ya katiba.”
      Uongozi wa Dk. Kyaruzi na Abdulwahid ulitambua kuwa matatizo mengi kuhusu haki za Waafrika yalikuwa masuala ya kisheria ambayo yalihitaji ushauri wa wanasheria. Kwa mara ya kwanza kwa msaada wa Seaton, TAA kilitoa hoja zake zilozotiwa nguvu na ukweli hoja na kwa tarakimu zilizoonyesha udhalimu ndani ya mfumo wa kikoloni ambao ulikuwa kinyume na Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Memorandum ya TAA kwa Constitutional Development Committee ambayo Pratt amesema iliandikwa kwa utaalamu wa hali ya juu na uongozi wa makao makuu ya Tanganyika African Association ilipendekeza kuwa ndani ya baraza la kutunga sheria Waafrika watashika nusu ya viti kwa miaka kumi na mbili na baada ya hapo ipigwe kura kuwachagua wajumbe. Kufuatia mwamko huu wa chama, serikali ilishtuka na ikaanza kuingia hofu, ikaamua kumpa uhamisho Dk. Kyaruzi, rais wa TAA, kutoka Dar es Salaam kwenda Hospitali ya Gereza la Kingolwira karibu na Morogoro. Serikali ya kikoloni iliamini kwa kufanya hivyo itaweza kupunguza kasi ya TAA katika uwanja wa siasa. Serikali ilidhani kwa kumtoa Dk. Kyaruzi Dar es Salaam, jambo hilo lingedhoofisha uongozi wa TAA pale makao makuu. Lakini Dk. Kyaruzi hakukwazwa na huo uhamisho. Kila mwisho wa juma alisafiri Dar es Salaam kushauriana na Abdulwahid. Serikali ilipotambua kuwa uhamisho huo haukuathiri chochote katika mchango wa Dk. Kyaruzi kwenye uongozi wa TAA, alihamishwa tena kutoka Kingolwira hadi Nzega mbali kabisa na Dar es Salaam. Hapo ikawa Dk. Kyaruzi amepatikana. Dk. Kyaruzi alikuwa sasa yuko kwenye “kifungo kisicho rasmi cha kisiasa” alichogubikwa na Waingereza asijihusishe tena na siasa za kudai uhuru. Dk. Kyaruzi hakurejea tena katika siasa za uzalendo pale Makao Makuu New Street. Waingereza wakafuatia mwaka 1951 na 1953 kwa kutoa sekula za kukataza watumishi wa serikali kujihusisha na siasa wakiwakusudia watu kama Dk. Kyaruzi.
      Gavana Twining iliyapuuza mapendekezo ya kamati ya TAA. Serikali iliendelea na mipango yake ya muda mrefu ya kuwaimarisha Wazungu na Waasia waliokuwa wachache na kuwasukuma kando Waafrika kinyume kabisa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu nchi zilizokuwa chini ya udhamini. Waafrika wengi wenye elimu walionelea kuwa mapendekezo ya TAA ndiyo yangekuwa msingi wa katiba ya baadaye ya Tanganyika kama jamii ya watu wa rangi zote. Lakini moyo wa mapendekezo yale ya TAA haukufa. Mapendekezo yale yaliletwa tena katika mkutano wa kuanzishwa kwa TANU tarehe 7 Julai, 1954. Mapendekezo hayo ndiyo baadaye yalitiwa katika hotuba ya Julius Nyerere aliyoisoma mbele ya Baraza la Udhamini la Umoja wa Mataifa, New York, mwezi wa Machi, 1955. Nyaraka hii imepotea. Haipo katika Maktaba ya CCM, Dodoma wala katika jalada lake na katika “microfilm” ilipohifadhiwa Tanzania National Archive (Nyaraka za Taifa).
      Hitimisho
      Katika miaka hii ya karibuni nimesoma makala kadhaa ambazo Dk. Kyaruzi akifanyiwa mahojiano na waandishi wa magazeti tofauti na katika kila makala Dk. Kyaruzi hakuacha kuweka msisitizo kuwa yeye ndiye aliyemuachia TAA Nyerere. Hiki ni kitu ambacho mimi kama mtafiti na mwandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika kilikuwa kikinitaabisha sana. Kilichokuwa kikinipa shida ni kuwa nilikuwa nikifahamu kuwa Dk. Kyaruzi aliingia katika uongozi wa TAA mwaka 1950 pamoja na Abdulwahid Sykes. Nilikuwa najua kuwa waliomsaidia kuingia katika uongozi walikuwa watu wa mjini akina Plantan na Sykes. Vipi watu hawa hakuwa anawakumbuka? Wakati Nyerere anachukua uongozi wa TAA mwaka 1953 Kyaruzi hakuwa Dar es Salaam. Hiki ni kitu kikinishughulisha sana. Jambo hili likishighulisha sana fikra zangu kwa kujiuliza mbona Kyaruzi anamruka Abdulwahid Sykes katika historia yao ya uongozi wa TAA mwaka wa 1950 na kumwingiza Nyerere ilhali Nyerere wakati ule hakuwa anafahamika na yeyote katika duru za siasa za Tanganyika? Nikawa nashangaa nikijiuliza kwani Dk. Kyaruzi hajui kuwa Nyerere aliingia katika uongozi wa TAA mwaka 1953? Nilikuwa nikijifariji kwa kusema kuwa haya ndiyo matatizo ya historia ya uhuru wa Tanganyika. Lakini jambo linalonisikitisha sana ni kujua kuwa katika miaka ya 1970 Dk. Kyaruzi alipeleka mswada wa maisha yake kwa mchapaji mmoja wa vitabu ili mswada wake uhaririwe na kuchapwa kitabu. Mchapaji yule ambae lilikuwa shirika la umma lilikataa kuchapa kitabu kile. Sijui kwa nini walikataa kuchapa kitabu kile ambacho kwa hali yeyote ile ingelikuwa hazina kubwa kwa vizazi vijavyo nah ii leo wakati wa umauti wake tungelimjua bila wasiwasi Dk. Kyaruzi na mchango wake katika uhuru wa Tanganyika na jinsi kama alivyosema mwenyewe vipi alimwachia TAA Nyerere.
      25 May 2012
      Ogah, Bukyanagandi and The Boss like this.

    11. #68
      Bukyanagandi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Location : DSM
      Posts : 1,956
      Rep Power : 923
      Likes Received
      718
      Likes Given
      1475

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Songoro
      Haya ndo mapungufu ya Mwl Nyerere,Aliwapoteza kwenye Historia akina Kyaruzi ili abaki pekee kwenye Historia na kuna vijitu vinaamini uhuru wa nchi hii ni matokeo ya harakati za miaka 6 i.e 1954 (kuzaliwa TANU) mpaka uhuru wa 1961, Hawajui kuwa Tanu imekuja kukamilisha kazi za wakongwe kama DR.Kyaruzi, Kwa mfano ukiwauliza vijana wasomi wa kisasa wakutajie wapigania Uhuru 10 wa nchi hii,itawachukua muda sana na kama wakijitahidi watakutajia waliokuwa mawazir wa kwanza wa Serikali wakati hao wapigania uhuru walitupwa kulleeeeeeee!!!!!! Watoto wetu hawajui kuwa Professa Babu ni Nguli wa Siasa ya Ujamaa Duniani mpaka leo wajamaaa Dunia nzima wanaadhimisha SIKU ya kifo chake kwa Mijadala yenye Afya.Buriani Dr.Kyaruzi historia ya VITABUNI umeachwa lakin kamwe vifuani mwa wapenda ukweli utadumu!
      Mkuu mimi jambo hili huwa lina nikasilisha kweli kweli, niliwahi kuzungumzia humu mambo hayo na nilimtaja Dr.Kyaruzi among others; inaonekana kulikuwa na ajenda ya SIRI ya kufuta kabisa majina ya watu walio kuwa na ujasiri wa kuanzisha harakati za kumpinga mkoloni ki kweli kweli na victims wengi ni wale walio kuwa wasomi na wale walio kuwa wanadhubutu kuhoji mambo yaliyo kuwa yankwenda ndio sivyo, wanajengewa uadui wa kudumu hata wakiaga dunia viongozi husika awaendi kwenye mazishi yao; wanakosa utu wa kujifunza kusahame - binadamu anakuwa na a lifetime sworn enemy real or imaginary, watu waliokuwa na uwezo kielimu na kuona mbali wanaikimbia nchi kwa kuogopa binadamu mwenzao, wanaondoka na kwenda kunufahisha nchi nyingine!

      Namshukuru sana Mh. Raisi J.Kikwete, ingawa alikuwa aonyeshi moja kwa moja kwamba naye kama binadamu swala hili lilikuwa linamu-haunt kama sisi wengine walala hoi, Raisi alitumia ujasiri wa hali ya juu kwa kuwatunukia nishani marehemu na walio hai ambao walihusika na ukombozi wa Mwafrica tangu enzi za TAA kitu ambacho kilikuwa kama ni haramu vile kutajwa kwenye Serikali ya hawamu ya kwanza! Namshukuru sana Raisi Kikwete kwa hilo, wakati mwingine nilikuwa nafikili nchi yetu ilikuwa inakumbwa na majanga yasiyo na kichwa wala miguu kwa sababu za rahana za marehemu hawa ambao Serikali yetu ilikuwa imewasahau KABISA na kuwafuta kwenye historia.

      Serikali ya hawamu ya kwanza ilikuwa imepania kupindisha pindisha historia ya nchi yetu sijuhi kwa manufaa ya kina nani? Tangu niko shuleni historia ilikuwa inaonekana kana kwamba kupigania uhuru kulianzia mwaka 1954, mambo ya TAA yalikuwa yanatajwa kujuu juu tu, wanataja majina ya magavana wa Kingereza kuanzia 1920s -1961 lakini inapokuja kwenye swala la TAA wameandika neno TAA lakini awataji nani alianzisha nani kafanya nini-wako kimya KABISA!

      Dr. Kyaruzi nilikuja kujulishwa na baba yangu mzazi pale katika hospitali yake mjini Bukoba wakati huo alikuwa amefiwa na mtoto wake ambaye alikuwa pilot huko Ulaya kama nakumbuka vizuri; mimi nilifikili ni Daktari tu wa binadamu and had nothing to do na mambo ya uwanaharakati au kama aliwahi kuwa kiongozi wa kwanza wa TAA - what a humble man, alikuwa hana makuu hata kidogo na alikuwa ni mtu wa matani sana. Sikumbuki kama naye alipewa nishani yoyote kama kumbukumbu!

      R.I.P Dr. Vedastus Kyalakishaija Kyaruzi utakumbukwa milele - AMEN.

    12. #69
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member "template/JamiV1/default/buttons/viewpost-right.png" alt="View Post" />style="display:none;visibility:hidden;" data-cfsrc="images/icons/icon1.png" alt="Default" />
      Quote By Mohamed Said View Post
      Mag3,

      Naomba nitoe maelezo kidogo.

      Cecila Matola hakuasisi African Association ingawa alikujakuwa kiongozi wake. Fikra ya kuanzishwa kwa AA ilitolewa kwa Kleist Sykes na Dk. Aggrey alipotembelea Tanganyika mwaka 1924. Habari kamili ya AA zinapatikana katika kitabu alichohariri John Iliffe "Modern Tanzanians" katika "The Townsman: Kleist Sykes" kama alivyoandika mjukuu wa Kleist, Daisy Aisha Sykes.

      TAA haikuzaliwa mwaka 1948 bali AA ilibadili jina tu mwaka huo wa 1948 baada ya kutengana na Zanzibar.

      TANU haiukuasisiwa na Nyerere bali na Abdulwahid Sykes. Habari za TANU zinaweza kupatikana katika kitabu "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924 1968... "

      CCM ndiyo iliyoasisiwa na Nyerere.
      Maalim Mohamed Said, correct me if I'm wrong.

      1. Muasisi ni nani?.
      Nijuavyo mimi, Muasisi ni aliyetoa wazo au kiongozi wake wa kwanza?. Kwa vile kiongozi wa kwanza wa AA ni Cecil Matola, then yeye ndie muasisi aliyeasisi hata kama wazo lilitolewa na Kleis Sykes!.
      2. Kuzaliwa kwa Chama ni kupi?. Nijuavyo mimi kuzaliwa kwa chama ni siku kile chama kinapoanza kuoparate kwenye jina jipya regardless kilikuwa nini kabla!. Kwa mukhtadha huo, TAA ilizaliwa mwaka 1948 na muasisi wake ni Dr. Vedastus Kyaruzi hata kama wazo lilitolewa na Kleist Sykes na siku hiyo ndiyo TAA ilizaliwa hata kama ni AA ilijibadili jina na kuitwa TAA!.

      Vivyo hivyo mwaka 1954 ndio Tanu ilizaliwa na muasisi wake ni Mwalimu JK Nyerere hata kama siku hiyo ndio TAA ilijigeuza TANU na Muasisi ni Mwalimu hata kama aliyetoa wazo ni Abdulwahid Sykes!.

      Ni kwa kutumia mukhtadha huo huo kuwa CCM ilizaliwa Feb. 5, 1977 na muasisi wake ni Mwalimu hata kama wazo lilitolewa na Sheikh Thabit Kombo na asili yake ni muungano wa TANU na ASP!.

      Naheshimu sana mchango wako ila naomba usilazimishe majina ya kina Sykes ndio waanzilishi wa AA na TAA simply kwa sababu wao ndio walitoa wazo!.

      Pasco.

    13. #70
      Bukyanagandi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Location : DSM
      Posts : 1,956
      Rep Power : 923
      Likes Received
      718
      Likes Given
      1475

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Mohamed Said
      DK. VEDASTO KYARUZI DAKTARI MWANAHARAKATI WA TAA
      Na Mohamed Said
      Utangulizi
      Katika moja ya misiba mikubwa iliyoikumba Tanzania ni kukosekana kwa historia inayoweza kuaminika kuhusu mashujaa wake waliopigania uhuru kutoka kwa Waingereza. Gazeti la Raia Mwema (Mei 23 - Mei 29, 2012) limefahamisha umma kuhusu kifo cha Dk. Vedasto Kyaruzi na kwa muhtasari wakaweka sifa zake. Kwa bahati mbaya sana sifa walizoweka hazikuwa za kweli kwa kiasi fulani. Mfano ni pale makala iliposema Dk. Kyaruzi ndiye aliyemwachia uongozi Nyerere katika TAA na kuwa alikuwa rais wa kwanza wa TAA. Ukweli ni kuwa Nyerere na Dk. Kyaruzi hawakupata kukutana katika uongozi wa TAA kwa hiyo isingewezekana kwa Dk. Kyaruzi kumwachia Nyerere uongozi. Wakati Nyerere anaingia TAA Makao Makuu, Dar es Salaam mwaka 1952 Kyaruzi alikuwa keshaondoshwa Dar es Salaam na wakoloni kapelekwa Nzega na chama kilikuwa chini ya uongozi wa Abdulwahid Sykes akiwa katibu na kaimu rais. Abdulwahid ndiye aliyeikabidhi TAA kwa Nyerere mwaka 1953. Jingine ni kuwa Kyaruzi wala hakuwa rais wa kwanza wa TAA kwani chama kilianzishwa Dar es Salaam mwaka 1929 kikijulikina kama African Association na wakati huo Dk Kyaruzi alikuwa bado mtoto mdogo. Mwaka wa 1948 ndipo kilipokuja badilishwa jina na kuitwa Tanganyika African Association (TAA) Kwa nia njema kabisa naweka hapa maisha ya siasa ya Dk. Kyaruzi kama nilivyoyaandika katika moja ya sura za kitabu changu “Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924 - 1968...” Katika makala haya nimefanya mabadiliko hapa na pale ili kumwezesha msomaji kufuatilia siasa za TAA kama zilivyokuwa wakati wa uongozi wa Dk. Kyaruzi mwaka wa 1950.
      25 May 2012
      Tunashukuru sana ndugu yetu Mr. Saidi - unatoa mchango mzuri sana kwenye mambo ambayo yalikuwa yamefutwa kabisa katika historia ya TAIFA letu, tunakuombea afya njema.

    14. #71
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22277

      Default

      Quote By Mag3
      Kwa faida ya Wasomaji na wanajamvi wenzangu naomba tu kuweka mambo manne sawa wakati tunamuenzi Dr. Vedasto Kyaruzi (RIP).

      1. AA ilianzishwa mwaka 1929 mwasisi wake na Raisi akiwa Cecil Matola.
      2. AA ilidumu hadi mwaka 1948 ikazaliwa TAA mwasisi wake na Raisi akiwa Dr. Vedasto Kyaruzi.
      3. TAA ilidumu hadi mwaka 1954 ikazaliwa TANU, mwasisi wake na Raisi akiwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
      4. TANU ilidumu hadi mwaka 1977 ikazaliwa CCM.

      Nawatakia majadiliano mema.
      Mag3, asante kwa hii'.

    15. #72
      Bukyanagandi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Location : DSM
      Posts : 1,956
      Rep Power : 923
      Likes Received
      718
      Likes Given
      1475

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Pasco
      Maalim Mohamed Said, correct me if I'm wrong.

      1. Muasisi ni nani?.
      Nijuavyo mimi, Muasisi ni aliyetoa wazo au kiongozi wake wa kwanza?. Kwa vile kiongozi wa kwanza wa AA ni Cecil Matola, then yeye ndie muasisi aliyeasisi hata kama wazo lilitolewa na Kleis Sykes!.
      2. Kuzaliwa kwa Chama ni kupi?. Nijuavyo mimi kuzaliwa kwa chama ni siku kile chama kinapoanza kuoparate kwenye jina jipya regardless kilikuwa nini kabla!. Kwa mukhtadha huo, TAA ilizaliwa mwaka 1948 na muasisi wake ni Dr. Vedastus Kyaruzi hata kama wazo lilitolewa na Kleist Sykes na siku hiyo ndiyo TAA ilizaliwa hata kama ni AA ilijibadili jina na kuitwa TAA!.

      Vivyo hivyo mwaka 1954 ndio Tanu ilizaliwa na muasisi wake ni Mwalimu JK Nyerere hata kama siku hiyo ndio TAA ilijigeuza TANU na Muasisi ni Mwalimu hata kama aliyetoa wazo ni Abdulwahid Sykes!.

      Ni kwa kutumia mukhtadha huo huo kuwa CCM ilizaliwa Feb. 5, 1977 na muasisi wake ni Mwalimu hata kama wazo lilitolewa na Sheikh Thabit Kombo na asili yake ni muungano wa TANU na ASP!.

      Naheshimu sana mchango wako ila naomba usilazimishe majina ya kina Sykes ndio waanzilishi wa AA na TAA simply kwa sababu wao ndio walitoa wazo!.

      Pasco.
      Hata bila kusoma hadi mwisho hoja yako, nilishajua tatizo liko kumtaja/kutaja familia ya Sykes mara kwa mara - mimi nafikili watu wanaosoma makala hizi wana uwezo mkubwa wa kuchambanua mambo na kujua ni yupi alikuwa ni muasisi wa kipi regardless ya time frame.

    16. #73
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,543
      Rep Power : 1758
      Likes Received
      2398
      Likes Given
      166

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Bukyanagandi

      Hapana haja ya kurejea katika ubishi huu.
      Kila mtu anaweza kuamua kipi aamini.

      Ila mie hupenda kuandika kile ambacho hakikuwa kinajulikana na wengi.

      Nadhani yeyote aliyesoma taazia yangu ya Dk. Kyaruzi bila shaka kapata faida kujua hali ya mambo yalivyokuwa mwaka 1950.

    17. #74
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,543
      Rep Power : 1758
      Likes Received
      2398
      Likes Given
      166

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Bukyanagandi
      Tunashukuru sana ndugu yetu Mr. Saidi - unatoa mchango mzuri sana kwenye mambo ambayo yalikuwa yamefutwa kabisa katika historia ya TAIFA letu, tunakuombea afya njema.
      Ndugu yangu tatizo la historia ya uhuru wa Tanganyika ni kubwa sana.

      Si sisi tu tunaoliona bali hata wasomi nje ya mipaka yetu weshajua kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika inahitaji utafiti mpya ili ikamilike kwa kiasi fulani.

      Mwaka jana nilialikwa University of Ohio na Northwestern University, Evanston Chicago, Marekani kisha nikaalikwa Zentrum Moderner Orient, Berlin Ujerumani ambako nilitoa mihadhara kuhusu historia ya Tanganyika na mambo mengine.

      Naamini juhudi hizi mpya ndani na nje ya nchi yetu zitazaa matunda na huko mbele Insha Allah hali itabadilika.

      Angalau serikali imemtambua Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally kama wapigania uhuru wa Tanganyika na wamewapa medali katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

      Swali linakuja lini watamtambua Kleist Sykes baba na mwalimu wa hawa wanae katika siasa na kumpa medali ikiwa si kwa kuasisi African Association basi kwa kujenga jumba ambalo TANU ilikujazaliwa...

      Abdu kapewa medali "post-humus."

      Angalau wametoa ingawa wamechelewa kwa nusu karne.
      Hili si dogo na wala hatuna haja ya kujua kwa nini wamechelewa na kwa nini wameamua kutoa hivi sasa.

      Ingawa kusubiri kwa miaka 50 ni kukubwa sana.

      Kuna sahib wangu mmoja anasema wametoa kwa sababu Mohamed Said kawasomesha historia ya kweli...

      Kwa nini Dk. Kyaruzi hakupewa medali au Dk Luciano Tsere, Dk. Michael Lugazia, Dk. Joseph Mutahangalwa, Dk. Wilbard Mwanjisi...

      Lakini naamini iko siku watatoa na si muda mrefu unaokuja Insha Allah.

      Hawa wote walikuwa madaktari na nimetaja mchango wao katika kitabu changu katika kuamsha wananchi baada ya Vita Kuu ya Pili hadi kufikia 1954 TANU ilipoasisiwa.

      Vipi hawa hadi leo hawatajiki...

      Kwanini Hamza Kibwana Mwapachu hakupewa medali pamoja na marehemu Abdulwahid wakati harakati zao zilikuwa zimefungamana ndani ya TAA...

      Hivi ndivyo vitu vingetushughulisha kwa sasa na kuwazindua viongozi wetu wavishughulikie...

      Kunga'ngania nani muasisi wa nini bila kujua taarifa zao kamili hakuboreshi historia ya nchi yetu.
      The Boss likes this.

    18. #75
      chama's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 6th August 2010
      Posts : 4,934
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1177
      Likes Given
      915

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Bwana Mohamed Said
      Utafiti wako una mashaka mengi pamoja na hizo propaganda zako hutaweza kamwe kuibadili historia ya Taifa hili; wewe ukiwa kama mtafiti kama unavyojinadi inakuwaje huwahoji wahusika wakiwa hai? mfano ni huu "Katika miaka hii ya karibuni nimesoma makala kadhaa ambazo Dk. Kyaruzi akifanyiwa mahojiano na waandishi wa magazeti tofauti na katika kila makala Dk. Kyaruzi hakuacha kuweka msisitizo kuwa yeye ndiye aliyemuachia TAA Nyerere" Dr. Kyaruzi amefariki majuzi tu nadhani ulikuwa na nafasi nzuri sana ya kumuhoji akiwa hai; watafiti wa kweli hawasubiri watu wafe ili wahoji kauli zao; binafsi nakuona ni mpotoshaji mwenye agenda binafsi.

      Chama
      Gongo la Mboto DSM
      Ogah likes this.

    19. #76
      Bukyanagandi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2009
      Location : DSM
      Posts : 1,956
      Rep Power : 923
      Likes Received
      718
      Likes Given
      1475

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Mohamed Said
      Ndugu yangu tatizo la historia ya uhuru wa Tanganyika ni kubwa sana.

      Si sisi tu tunaoliona bali hata wasomi nje ya mipaka yetu weshajua kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika inahitaji utafiti mpya ili ikamilike kwa kiasi fulani.

      Mwaka jana nilialikwa University of Ohio na Northwestern University, Evanston Chicago, Marekani kisha nikaalikwa Zentrum Moderner Orient, Berlin Ujerumani ambako nilitoa mihadhara kuhusu historia ya Tanganyika na mambo mengine.

      Naamini juhudi hizi mpya ndani na nje ya nchi yetu zitazaa matunda na huko mbele Insha Allah hali itabadilika.

      Angalau serikali imemtambua Abdulwahid Sykes na mdogo wake Ally kama wapigania uhuru wa Tanganyika na wamewapa medali katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

      Swali linakuja lini watamtambua Kleist Sykes baba na mwalimu wa hawa wanae katika siasa na kumpa medali ikiwa si kwa kuasisi African Association basi kwa kujenga jumba ambalo TANU ilikujazaliwa...
      Mkuu, nashukuru sana kwa jitihada zako zisizo na kifani - ume-devote muda wako mwingi sana ukifatilia/kufanya utafiti kuhusu historia ya kweli ya TAIFA letu, Mungu akubariki. Kuhusu madaktari wanaharakati ambao ndio walikuwa first Makererian - hata mimi nashangaa walivyo sahauliwa kwa kutunukiwa nishani after their PASSING. Mimi naona tumshukuru sana Raisi wetu mpendwa Jakaya Kikwete kwa kupata ujasiri wa kutoa hizo nishani aganist all odds, nilikuwa najiuliza sana imekuwaje mpaka JK anafikia hatua ya kufanya kitendo hiki cha kijasiri - baada ya kujikuna kichwa kwa muda mrefu nikakumbuka kwamba baba yake JK Mzee Alfan bila shaka alikuwa anawajua kwa majina watu walio shiriki katika harakati hizi kikamilifu na siyo mapandikizi ambao hawakufanya lolote zaidi ya kufitinisha wenzao; sina shaka mapandikizi hawa ndio walihusika katika kuharibu/distort historia ya Taifa letu mpaka wakafikia hatua ya kuharibu microfilms, copy ya speech ya Kambarage aliyo itoa Umoja wa mataifa! walikuwa hawataki tujue nani alimuandikia speech hiyo, kufuta sura za baadhi ya wanaharakati kwenye picha za pamoja zilizo pigwa TABORA; yaani wakaiga mambo ya Stalin aliyo kuwa anayafanya URUSI wakati wa enzi zake, walikopi mbinu zote za Stalin isipokua mambo ya GULAG.

      Tukirudi kwenye point, nataka kumalizia kwamba Mzee Alfan sina shaka alimweleza historia ya kweli mwanae JK, kwani mikutano na mambo mengi ya harakati yalikuwa wakati mwingine yanafanyika Bagamoyo. Nadhani kutokana na ukweli huo pia na ungwana alio zaliwa nao JK, aliona haitakua vizuri amalizie ngwe ya kipindi chake cha pili bila ya kuwakumbuka majasiri hawa.

      Kuhusu idadi ya wale walio tunukiwa nishani kuwa pungufu, mimi nafikili wajanja wanaweza kuwa wamempa list pungufu kwa makusudi! Au walikua awajuhi vizuri idadi kamili ya wanaharakati walio husika katika nyanja HIYO kutokana na wao kutofahamu historia ya kweli ya nchi yetu .

      Lakini ndugu nakuhakikishia kwamba mpe muda JK atahakikisha wahusika wote wamepata nishani kabla ya kipindi chake kumalizika. Kwa leo huo ndio mchango wangu Ndugu Said. nakutakia kila la kheli.
      Last edited by Bukyanagandi; 2nd June 2012 at 11:56.

    20. #77
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,543
      Rep Power : 1758
      Likes Received
      2398
      Likes Given
      166

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Bukyanagandi
      Mkuu, nashukuru sana kwa jitihada zako zisizo na kifani - ume-devote muda wako mwingi sana ukifatilia/kufanya utafiti kuhusu historia ya kweli ya TAIFA letu, Mungu akubariki. Kuhusu madaktari wanaharakati ambao ndio walikuwa first Makererenian - hata mimi nashangaa walivyo sahauliwa kwa kutunukiwa nishani after their PASSING. Mimi naona tumshukuru sana Raisi wetu mpendwa Jakaya Kikwete kwa kupata ujasiri wa kutoa hizo nishani aganist all odds, nilikuwa najiuliza sana imekuwaje JK akafikia hatua ya kufanya kitendo hiki cha kijasiri - baada ya kujikuna kichwa kwa muda mrefu nikakumbuka kwamba baba yake JK Mzee Alfan bila shaka alikuwa anawajua kwa majina watu walio shiriki katika harakati hizi kikamilifu na siyo mapandikizi ambao hawakufanya lolote zaidi ya kufitinisha wenzao sina shaka mapandikizi hawa ndio walihusika katika kuharibu/distort historia ya Taifa letu mpaka wakafikia hatua ya kuharibu microfilms, speech ya Kambarage aliyo hitoa Umoja wa mataifa! walikuwa hawataki tujue nani alimuandikia speech hiyo, kufuta sura za baadhi ya watu kwenye picha za pamoja zilizo pigwa TABORA; yaani wakaiga mambo ya Stalin aliyo kuwa anayafanya URUSI wakati wa enzi zake.

      Tukirudi kwenye point, nataka kumalizia kwamba Mzee Alfan sina shaka alimweleza historia ya kweli mwanae JK, kwani mikutano na mambo mengi ya harakati yalikuwa wakati mwingine yanafanyika Bagamoyo. Kwa hiyo JK alikua anajua anacho fanya, wajanja wanaweza kuwa wamempa list pungufu kwa makusudi au walikua awajuhi vizuri idadi kamili ya wanaharakati walio husika nyanja HIYO. Lakini ndugu nakuhakikishia kwamba mpe muda JK atahakikisha wahusika wote wamepata nishani kabla ya kipindi chake kumalizika.

      Kwa leo huo ndio mchango wangu Ndugu Said. nakutakia kila la kheli.
      Ndugu yangu Buk,
      Ahsante sana kwa mchango wako.

      Umenifariji.

      M

    21. #78
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,543
      Rep Power : 1758
      Likes Received
      2398
      Likes Given
      166

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By chama
      Bwana Mohamed Said
      Utafiti wako una mashaka mengi pamoja na hizo propaganda zako hutaweza kamwe kuibadili historia ya Taifa hili; wewe ukiwa kama mtafiti kama unavyojinadi inakuwaje huwahoji wahusika wakiwa hai? mfano ni huu "Katika miaka hii ya karibuni nimesoma makala kadhaa ambazo Dk. Kyaruzi akifanyiwa mahojiano na waandishi wa magazeti tofauti na katika kila makala Dk. Kyaruzi hakuacha kuweka msisitizo kuwa yeye ndiye aliyemuachia TAA Nyerere" Dr. Kyaruzi amefariki majuzi tu nadhani ulikuwa na nafasi nzuri sana ya kumuhoji akiwa hai; watafiti wa kweli hawasubiri watu wafe ili wahoji kauli zao; binafsi nakuona ni mpotoshaji mwenye agenda binafsi.

      Chama
      Gongo la Mboto DSM
      Bwana Chama,

      Ahsante kwa mchango wako.

      Tuanze na hili la agenda.

      Kwa hakika lazima nikiri kuwa kwa hakika nilikuwa na agenda na nashukuru kuwa azma ya agenda hiyo imekamilika.

      Bila ya kuwa na agenda mtu huwezi kufanya lolote.

      Jambo lolote huanza kwa kuliwaza katika fikra kisha kinafuatia kitendo.

      Hili la pili la "mashaka mengi" katika historia niliyoandika hili ni jambo la kawaida katika dunia ya usomi. Unaandika jambo watu wanasoma na wako watakaotilia mashaka kazi yako na wapo watakayoiamini.

      Sasa kuhusu mie "kuibadili" historia ya taifa hili hili nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na mfano ndiyo huu leo watu wanamsoma Dk. Kyaruzi katika sura nyingine kabisa. Na si wanamsoma Dk. Kyaruzi peke yake wanawasoma watu aliokuwa nao wakati wa kuitoa TAA mikononi mwa wazee wa enzi za Wajerumani waliokuwa madarakani.

      Wanawasoma Mwalimu Thomas Sauti Plantan, Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Mashado Plantan na gazeti lake "Zuhra" lililokuwa sauti ya Watanganyika likipambana na "Tanganyika Standard."

      Hawa ninakutajia kwa uchache tu lakini ukipenda tunaweza kuingia hata katika TAA Political Sub Committee Kyaruzi akiwa na Abdulwahid Sykes, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Said Chaurembdo, Mwalimu Steven Mhando, Hamza Kibwana Mwapachu nk.

      Mwisho ni kuhusu kuhojiwa kwa Dk. Kyaruzi.

      Mara kadhaa nimemuomba mjukuu wake na somo yake mwandishi Kyaruzi afanye mahojiano na babu yake na aandike maisha yake.

      Niliamini hapa patapatikana mengi ya faida katika kuitunza historia ya nchi yetu.

      Nadhani hili litakuwa limefanyika Insha Allah tusubiri kusoma kitabu.

      Ushauri wangu kwako.

      Usiandike vitu hivi huku umekasirika na kutupa shutuma...mimi sijinadi kuwa "mtafiti."
      Lakini wakati Dk. Harith Ghassany anaandika kitabu chake maarufu kuhusu ukweli wa mapinduzi ya Zanzibar "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru" nilikuwa msaidizi wake na katika kitabu chake kanitaja kama "Mtafiti Msaidizi" ingawa kazi yangu khasa ilikuwa kumwendesha dk na kumfungulia milango.

      Kunadi unakuwa mnadani unatafuta dau.
      Mimi kwa bahati mbaya au nzuri si dalali katika mnada.

      Kuna wanaoniita "scholar" kwa lugha yao na kila nikisimama kuzungumza huwasikia wakinijulisha kwa wasikizaji kwa neno hilo.

      Hiki ni Kizungu.
      Sijui nini maana yake kwa uhakika.
      Last edited by Mohamed Said; 2nd June 2012 at 13:43.

    22. #79
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,672
      Rep Power : 977
      Likes Received
      584
      Likes Given
      10

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Nawashukuruni wote kwa maarifa na elimu nimeipata kupitia michango yenu. Nimepata jibu ni kwanini mambo mengi mazuri yaliyo asisiwa awamu ya kwanza leo yamekufa ama yanasuasua! Mwalimu Nyerere aliwaamini watu wasioaminika! Hapa ndiyo chanzo cha uwongo,majungu na fitina ambazo leo zimeiua CCM! Ndicho chanzo cha wasomi makini,wazalendo na wachapa kazi kuikimbia siasa kwasababu za majungu,chuki,fitina na uwongo!

    23. #80
      chama's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 6th August 2010
      Posts : 4,934
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1177
      Likes Given
      915

      Default Re: Mpigania Uhuru na Mwasisi wa TAA, Dr. Vedastus Kyaruzi afariki dunia!

      Quote By Mohamed Said
      Bwana Chama,

      Ahsante kwa mchango wako.

      Tuanze na hili la agenda.

      Kwa hakika lazima nikiri kuwa kwa hakika nilikuwa na agenda na nashukuru kuwa azma ya agenda hiyo imekamilika.

      Bila ya kuwa na agenda mtu huwezi kufanya lolote.

      Jambo lolote huanza kwa kuliwaza katika fikra kisha kinafuatia kitendo.

      Hili la pili la "mashaka mengi" katika historia niliyoandika hili ni jambo la kawaida katika dunia ya usomi. Unaandika jambo watu wanasoma na wako watakaotilia mashaka kazi yako na wapo watakayoiamini.

      Sasa kuhusu mie "kuibadili" historia ya taifa hili hili nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana na mfano ndiyo huu leo watu wanamsoma Dk. Kyaruzi katika sura nyingine kabisa. Na si wanamsoma Dk. Kyaruzi peke yake wanawasoma watu aliokuwa nao wakati wa kuitoa TAA mikononi mwa wazee wa enzi za Wajerumani waliokuwa madarakani.

      Wanawasoma Mwalimu Thomas Sauti Plantan, Schneider Abdillah Plantan na Ramadhani Mashado Plantan na gazeti lake "Zuhra" lililokuwa sauti ya Watanganyika likipambana na "Tanganyika Standard."

      Hawa ninakutajia kwa uchache tu lakini ukipenda tunaweza kuingia hata katika TAA Political Sub Committee Kyaruzi akiwa na Abdulwahid Sykes, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Said Chaurembdo, Mwalimu Steven Mhando, Hamza Kibwana Mwapachu nk.

      Mwisho ni kuhusu kuhojiwa kwa Dk. Kyaruzi.

      Mara kadhaa nimemuomba mjukuu wake na somo yake mwandishi Kyaruzi afanye mahojiano na babu yake na aandike maisha yake.

      Niliamini hapa patapatikana mengi ya faida katika kuitunza historia ya nchi yetu.

      Nadhani hili litakuwa limefanyika Insha Allah tusubiri kusoma kitabu.

      Ushauri wangu kwako.

      Usiandike vitu hivi huku umekasirika na kutupa shutuma...mimi sijinadi kuwa "mtafiti."
      Lakini wakati Dk. Harith Ghassany anaandika kitabu chake maarufu kuhusu ukweli wa mapinduzi ya Zanzibar "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru" nilikuwa msaidizi wake na katika kitabu chake kanitaja kama "Mtafiti Msaidizi" ingawa kazi yangu khasa ilikuwa kumwendesha dk na kumfungulia milango.

      Kunadi unakuwa mnadani unatafuta dau.
      Mimi kwa bahati mbaya au nzuri si dalali katika mnada.

      Kuna wanaoniita "scholar" kwa lugha yao na kila nikisimama kuzungumza huwasikia wakinijulisha kwa wasikizaji kwa neno hilo.

      Hiki ni Kizungu.
      Sijui nini maana yake kwa uhakika.
      Bwana Mohamed Said
      Utafiti wako una mapungufu mengi sana katika dunia hii wapo wapotoshaji na wanaotafuta ukweli; wapo watafiti wanaodai HIV na AIDS havina uhusiano wapo wanaodai Malnutrition inasababisha AIDS; hao wote wanajiita ni watafiti sawa na wewe; nimekuuliza kwanini hukumuhoji Dr. Kyaruzi alipodai aliingoza TAA badala ya kuja na majibu mbadala umerukia mambo mengine wewe ndiye mwenye mashaka na historia ya Taifa hili nilitumai ukiwa kama unavyojinadi mtafiti ungemtafuta Dr. Kyaruzi ili akufafanulie ni lini aliiongoza TAA; historia tunayoingelea ni takribani miaka 60; unafurahisha sana kuitwa yaani kuitwa scholar umeona ni jambo kubwa sana, wapo watu wanaitana masheikh huku hata elimu ya dini hawana wakati ni dhihaka za kidunia; na hasa unapoongelea kwenye watu wenye elimu duni au wasiojua. Utafiti wako ni wa kupinga kauli za wafu; mtafiti mwenye kutaka kujua ukweli huwakabili wahusika na kupata kauli thabiti; kama ambavyo uliweza kwenda kwa Sykes na ukasoma makaburasha; na kama unavyodai familia ilikunyima baadhi ya makaratasi (rejea matoleo yako ya nyuma) huo ni uthibitisho wa wazi utafiti ulishakuwa na mapungufu; Dr. Kyaruzi(R.I.P) amefariki juzi leo umekuja kuhoji kauli zake; sasa tumwamini nani yeye aliyeshiriki kwenye siasa wakati wa TAA au wewe uliyehadithiwa? Bwana Mohamed watifiti wa aina yako wapo wengi sana ni sawa na wale wanaodai Holocaust haikutokea!

      Chama
      Gongo la Mboto DSM
      Ogah and Jasusi like this.

    Page 4 of 5 FirstFirst ... 2345 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...