CHAKUJIULIZA WANA WA ZANZIBAR JEE BAADA YA KULIVAA HILI JINDAMIZI LA MUUNGANO ZANZIBAR IMEPIGA HATUA MBELE AU HATUA NYUMA?
Kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha kuwa Zanzibar kabla ya kuungana na Tanganyika ilikuwa mstari wa mbele kimaendeleo, si tu ukilinganisha na Tanganyika ya wakati huo, bali katika mwambao mzima wa Afrika Mashariki. Ilimiliki Currency yake mwenyewe, T.V ya rangi, viwanda vya Sukari, Reli, Viwanda vya mafuta na manukato, nyumba za kisasa kwa wananchi wake, barabara na mataa warawara, maji safi, umeme wa uhakika, n.k . Baadae mambo haya yote yakakongeshwa na kuharibiwa na jini la mdimu (Muungano).
Sasa swali linakuja hii imetokea Accidentally kuwa Zanzibar kila siku zinavyokwenda kwa kuwa kwake katika Muungano huu ndio inavyozidi kuporomoka kiuchumi, kiutamaduni na pia kimaadili, au mambo haya yalipagwa na kukadiriwa na vigogo wa Muungano? Kwa mtazamo wangu binafsi hili jinamizi la Muungano linapswa kupungwa na kutoka vichwani mwetu, mimi sipendi hata kidogo kuona kizazi kinachokuja kinasikia harufu la hili baa la Muungano.
Kwa kweli kama jungu limepikwa na J.K Nyerere akisaidiwa na top Church members basi wajuwe kuwa muda umefika dude hili hatulitaki, na shari za dude hili ziwarudie hao waliolipika na walipakuwe na wale wenyewe.

Reply With Quote


Follow Us Here