Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kauli ya Chagulani dhidi Manyerere (Council Mwanza) ni sahihi kwa afya ya CHADEMA?

    Report Post
    Page 9 of 9 FirstFirst ... 789
    Results 161 to 164 of 164
    1. #1
      GHOST RYDER's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th June 2011
      Posts : 961
      Rep Power : 602
      Likes Received
      422
      Likes Given
      186

      Talking Kauli ya Chagulani dhidi Manyerere (Council Mwanza) ni sahihi kwa afya ya CHADEMA?

      JF UP-CLOSE: KAULI YA CHAGULANI DHIDI MANYERERE COUNCIL MWANZA NI SAHIHI KWA AFYA YA CDM?

      Katika kikao cha Bajeti cha Halmashauri ya Jiji la Mwanza Mei 15, Diwani wa Kata ya Igoma CDM Mh. Adam Chagulani ametamka kutokuwa na imani na Meya wa Jiji hilo Mh.Jackson Manyerere kwa madai ya kuwayumbisha katika vikao hivyo.

      Akionyesha kutomuunga mkono Meya huyo, Chagulani aliiitisha kufanyika kwa zoezi la kukusanya saini za madiwani kutosheleza idadi inayokubalika kisheria kupitisha mswaada wa kupiga kura ya kutokuwa na imani na Manyerere ambaye ni kada mwenzie wa CHADEMA.

      Chagulani ambaye katika kinyang’anyiro cha kusaka Meya wa Jiji hilo alikuwa akipewa nafasi kubwa kutoka kambi ya CDM kabla ya maamuzi ya hekima yaliyotumika baada ya kuzuka kambi mbili ambazo bila shaka zingeishia kuuweka rehani umeya kwa mgombea wa CCM Stanslaus Mabula ambaye alikuwa na kiu kubwa ya dhamana hiyo, anaonekana dhahiri bado anateswa na jinamizi hilo kwa kauli ambazo sijui tafsiri yake ni nini kwa afya ya chama.

      Akizungumza kwa hisia na kuungwa mkono na madiwani wa CCM na CUF chagulani alimhoji Manyerere, ‘’ Mweyeketi kwa nini tusisign petition ya kutokuwa na imani na wewe kwa kuwa umekuwa ukituyumbisha kila mara’’ alimaliza chagulani na kushangiliwa kwa nguvu na kambi ya CCM na CUF katika baraza hilo.

      Kama haitoshi Stanslaus Mabula nae hakuwa nyuma kwa kumrushia tuhuma Meya huyo kuwa amekuwa akikiuka mara kwa mara taratibu za chama kwa kutoa nje ya vikao mijadala inayohusu halmashauri hiyo na kujadiliwa katika vikao visivyokubalika kisheria.

      UP-CLOSE DEBATE:

      1. Uko wapi umakini katika hatua hii ya Adam Chagulani Diwani wa Igoma CDM?

      2. Hakulijua hili mapema Mh. Wenje ambaye alikuwepo katika kikao na alisimama kidete kuonyesha mapungufu ya Bajeti iliyopita ya 2011/12 na kuelezea hakuna sababu ya kujadili Bajeti ya 2012/ 13 wakati iliyopita imejaa madudu?

      3. Saini 16 zimepatikana kutimiza Column ya kupiga kura ya kutokuwa na Imani na Meya Mh. Josephat Manyerere, Nini hatima ya zoezi hili na nani hasa anayeandaliwa kushika wadhifa huu?

      4. Ni kweli sasa dalili za kambi mbili ndani ya CDM zinataka kushika hatamu au ni uchu tu wa madaraka wa baadhi ya makada wa CDM?

      5. Mkakati wa kitaifa wa chama unayatazamaje haya?Karibu katika mjadala huu Mh. Mnyika, Mrema kwa Misimamo ya Chama.

      VIDEO YA TUKIO HILI NIMEIDAKA KATIKA LINK INAYOONEKANA HAPA CHINI



      ADIOS

      NEXT WEEKJF UP-CLOSE: UONGOZI UNAHITAJI VIPAJI AU TAALUMA?
      Last edited by GHOST RYDER; 18th May 2012 at 20:30.
      REAL HUSTLER

    2. RukaaJuu Final

    3. #161
      Uwezo Tunao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 6,897
      Rep Power : 2294
      Likes Received
      1154
      Likes Given
      1495

      Default Re: Tetesi...Chagulani kuhamia ccm?

      Mwacheni Chagulani aende salama kwa Baba ya wa UFISADI Tanzania.

      Lakini kubwa zaidi ni kwamba asisahau pia kuhama huo mji maana nako huenda kusikalike kwake ki-urahisa sana kulingana na jinsi ambavyo vijana CHADEMA wanavyoendelea kutafakari matendo yake ya ki-hujuma jijini Mwanza.

      Quote By nnn
      Inasemekana kuwa Adam Chagulani huenda akahamia CCM ili kuendeleze azima yake ya kuidhorotesha CHADEMA Mwanza.

    4. #162
      Sabung'ori's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th July 2011
      Posts : 824
      Rep Power : 561
      Likes Received
      233
      Likes Given
      16

      Default Re: Tetesi...Chagulani kuhamia ccm?

      ...anaenda wapi tena huyo?...si alishasema yeye ni taasisi iliyohuru!...mi siona sababu ya yeye kwenda kwenye taasisi nyingine zaidi ya kuendelea kushugulika na hiyo taasisi yake...

    5. #163
      Nyakageni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st February 2011
      Posts : 5,249
      Rep Power : 1541
      Likes Received
      769
      Likes Given
      52

      Default Re: Kauli ya Chagulani dhidi Manyerere (Council Mwanza) ni sahihi kwa afya ya CHADEMA?

      aende zake huyu dogo. Tutasafiri kupiga kura tena. Tulipiga kura kwa kuangalia chama na si wewe. Kwenda zake. Nitatoka Dar kurudi kuipigia kura CDM

    6. #164
      Borakufa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th May 2011
      Location : Tohell
      Posts : 1,164
      Rep Power : 642
      Likes Received
      260
      Likes Given
      207

      Default Re: Kauli ya Chagulani dhidi Manyerere (Council Mwanza) ni sahihi kwa afya ya CHADEMA?

      Chagulani!!! duuh! uroho wa madaraka tu huo! atakuwa ni mwenye akili ya kinyesi atakayefanya kama alivyofanya chagulani! Haiwezekani mimi na wewe timu moja halafu unawasaidia timu pinzani kutufunga ni akili mavi tu hizo

    7. Miaka 50
    Page 9 of 9 FirstFirst ... 789

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...