Posted by EMT | May 14, 2012 (Baadae comments zikapotea wakati wa marekebisho ya server)
Kulikuwa na thread hapa leo kuhusu kukamatwa kwa mbunge wa Chadema huko Marekani lakini imeondolewa baada ya Chadema kutoa tamko rasmi la kukanusha kuwa huyo mbunge hajakamatwa. Hata hivyo, kulikuwa na suala la msingi la kujadiliwa kwenye ile thread. Suala hili linahusu tuhuma za mbunge wa Tanzania kuishi nje ya nchi. Kwenye tamko la Chadema hawakugusia kabisa hili suala. Tuhuma za mbunge wa Chadema kuishi nje ya nchi zimekuwepo kwa muda sasa lakini Chadema hawajawahi kutolea tamko.
Nimecheki Facebook profile ya huyo mbunge inasema anafanya kazi katika Bunge la Tanzania. Pia profile inasema anaishi Dar Es Salaam. Philosophy yake: she believes in God. Views zake za kisiasa ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Favourate quotes yake: I'm not the victim of my mistakes, I take them and grow from them.
Kama kweli anaishi Marekeni halafu anadanganya anaishi Dar Es Salaam huu si utakuwa ni uongo namba moja? Taratibu zinasemaje kuhusu mbunge kudanganya makazi yake? Kama ni Mbunge na kweli anaishi Marekani, taratibu zinasemaje kwa mbunge kuwa na makazi yake nje ya nchi? Kama ni mbunge wa CHADEMA na anaishi Marekani, chama chake kinasemaje kuhusu kuishi kwake nje nchi? Hivi karibuni Mh Mbowe na Mh Wenje walikuwa Marekani, je walikutana na huyu mbunge wa chama chake? Chadema inaweza kueleza walipa kodi ni kwa nini mbunge wao anaishi Marekani?
Mei 27, 2012, Zitto, John Mnyika, Mh. Joseph Mbilinyi, Mh Ezekiel Wenje, na Mh, Peter Msigwa watafanya mkutano Maryland, Marekani. Kwenye mkutano huo pia atakuwepo Mh Leticia Nyerere. Je, kama hizi tuhuma ni za kweli, hawa washimiwa wa Chadema wanaoenda Marekani kwenye huo mkutano wanasemaje kuhusiana na makazi ya mbunge mwenzao kuwa Marekani na tuhuma nyingine za kuwa na kesi zinazomkabili mahakani huko Marekani?
Huyu mheshimiwa mbunge ameshakuwa na kesi 7 Marekani, tano zimeshafungwa na mbili bado ni active. kwenye kesi zote yeye alikuwa ni defendant. Mnaweza kuangalia wenyewe hapa: Maryland Judiciary Case Search (Maryland Judiciary Case Search). Ingekuwa bora kama Chadema badala tuu ya kukanusha kuwa mbunge wao amekamatwa pia watoe tamko juu ya tuhuma za mbunge wako kuishi marekani.

Reply With Quote



Follow Us Here