Hoja Nzito: Makala mbalimbali - JamiiForums |The Home of Great Thinkers

Go Back   JamiiForums |The Home of Great Thinkers > Public Forums > Jukwaa la Siasa


Jukwaa la Siasa Tanzania & World Politics General Discussion Forum. You need to be registered in order to post your comment(s)


Reply
 
LinkBack Thread Tools Rate Thread Display Modes
Old 9th December 2006, 01:30 PM   #1
Hoja Nzito: Makala mbalimbali
maggid maggid is offline 9th December 2006, 01:30 PM

CCM: The party and the power
By Maggid Mjengwa,

When I was asked to share my views on 45 years of independence, I came to think of two major events in which any one who want to go through our 45 years of Independence must take them into account.

( Makala hii ilichapwa na jarida la Rai juzi alhamisi)

Sherehe mchana , jioni matanga
Na maggid mjengwa,

KUNA kisa cha mwanamke masikini aliyesubiri kwa miaka mingi kupata mtoto. Alisubiri mno mpaka akaingiwa hofu, kuwa huenda asipate mtoto maishani mwake. Hali hiyo ilipelekea wanakijiji wenzake kuvumisha ugumba.

Awamu ya Nne inaikanaje mizigo hii ya Awamu ya Tatu?
Na Nizar K Visram

HIVI majuzi Waziri Mkuu Mheshimiwa Edward Lowassa alituambia kuwa wanaoilaumu Awamu ya Nne kwa matatizo ya umeme hawaitendei haki kwa sababu matatizo hayo yalirithiwa kutoka awamu zilizopita.

( Makala hii ilichapwa katika jarida la Rai juma la jana)



Mbona haya si mageni, na kwanini hatujifunzi kwa kasoro hizi?

( Makala hii imechapwa na Mwananchi siku ya Mapinduzi, Jan.12)

Na Nizar K Visram
Miaka 43 imepita tangu Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoanzia tarehe 12 Januari 1964 na kuendelea. Wengine huwa tunazungumzia Mapinduzi kana kwamba ni tukio la siku moja tu badala ya mchakato mzima wa mageuzi ya kimsingi katika jamii, mchakato unaoanza kabla na kuendelea baada ya tukio lenyewe.

CCM inakwenda wapi?
Na Maggid Mjengwa,

KWA binadamu, ili ujue unakokwenda ni busara ujue ulikotoka na ulipo sasa. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatimiza mika 30 tangu kuzaliwa kwake.

maggid
Senior Member
Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
Join Date: Sun Dec 2006
Posts: 84
Thanks: 0
Thanked 19 Times in 5 Posts
Views: 2078
Reply With Quote
  #2  
Old 25th February 2007, 01:16 PM
maggid maggid is offline
maggid has no status.
Senior Member
Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Sun Dec 2006
Posts: 84
Thanks: 0
Thanked 19 Times in 5 Posts
Rep Power: 24
maggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enough
Default Kichuguu

Asanteni sana kwa changamoto zako.

Nahofia kuwa unasukumwa na jazba na pengine chuki katika kuwasilisha hoja zako, na ndio sababu nashawishika kuamini kuwa umeamua tu kutopenda kile nifanyacho. Nilidhani kwa njia za kistaarabu ungenielimisha juu ya taratibu, kama zipo, zenye kuniondolea uhuru wa kuweka post zangu humu ukumbini pamoja na link ya blogu yangu.

Maana, bado siioni dhambi niifanyayo maana link ya blogu yangu ni ya blogu yangu na ina post za wengine pia ninazoziingiza huko achilia mbali picha.Kwamba simlazimishi yeyote yule kufungua blogu hiyo.

Napata taabu pia kujadiliana nawe Kichuguu maana mbali ya kuwa unaitwa Kichuguu, Senior Member na Expert sijui lolote kuhusu wewe. Isije ikawa katika harakati za kimaisha nilipata kukwaruzana nawe. Sijui kwa vile sikufahamu hata kwa jina lako halisi. Na labda hili ndilo tatizo langu, kwamba sifichi utambulisho wangu kama ufanyavyo wewe, sina hulka hiyo kama hakuna lazima ya kufanya hivyo. Laiti ningejiita "nyasi" huenda usingeniandama hivyo.

Mimi nilidhani hili jukwaa ni kama soko la fikra. Nikiwa na nyanya zangu natandika gunia na kuzipanga. Kila mtu ana uhuru wa kusimama kuziangalia/ kununua au kupita tu. Na kwamba kama sina cha kuchangia kwa yalioingizwa na wengine inatosha kusoma tu. Sasa hii lazima ya kuchangia mada inatoka wapi?

Kama mtu akikujibu " Sina maoni, hayo pia ni maoni". Yaheshimu.
/maggid
Reply With Quote
  #3  
Old 25th February 2007, 04:10 PM
maggid maggid is offline
maggid has no status.
Senior Member
Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Sun Dec 2006
Posts: 84
Thanks: 0
Thanked 19 Times in 5 Posts
Rep Power: 24
maggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enough
Default

Padri Karugendo: Kikwete Na Bongo Flava!

( Makala hii ilichapwa na RAI majuma kadhaa yaliyopita)

Na Padri Privatus Karugendo,

“Afrika nakutamani, nikikumbuka sifa zako, ingawa niko nchi mbali furaha haishi moyoni. Sina budi kukumbuka, Afrika nakutamani…

Utumwa ni kitu kibaya, tuliuuzwa kama samaki, samaki wa kwetu wanono, si kama hawa wa Amerika..”.

Hizi ni baadhi ya beti za wimbo ulioimbwa na watumwa enzi zile. Kama tujuavyo utuma ni unyama wa hali ya juu, ni nyanyasaji uliopindukia. Wakati ule wanyonge walionewa na haki zao kama binadamu zilipotea. Kwa kujituliza waliimba na wakati mwingine kucheza muziki.

Kuna mifano mingi inayoonyesha jinsi nyimbo, ngoma na muziki zilivyo kitulizo cha watu wanaoonewa. Daima inakuwa njia yao ya kujituliza, kutoa ujumbe katika jamii lakini pia kama njia ya kuhamasisha wanaoonewa kushikamana na kupigania kaki zao. Sauti ya wanyonge inapenyeza kwa ukali wa ina yake kupitia nyimbo, muziki na ngoma.

Baadhi ya waimbaji mashuhuri wa Amerika ni weusi. Vipaji vyao viliibuka katika harakati za kutetea haki zao kule Amerika. Lakini pia kwa vile walikwa wakibaguliwa katika kazi nyingine nzuri, waliishia kuwa wanamuziki, na michezo mingine kama ngumi, mpira, kukimbia n.k.

Hoja ninayotaka kuijenga hapa ni kwamba nyimbo, muziki na ngoma vimekuwa kichochocheo cha mapambabo, harakati na wakati mwingine vita, kwa watu wanaoonewam, wanaobaguliwa na wanaotawaliwa wa mabafu. Mfano mzuri ni ule wa Amerika, kwa kutumia nyimbo na muziki, walishikamana na kuunda vikundi vya kutetea haki zao. Hamasa iliyojengwa kupitia nyimbo na muziki, ilikuwa ni ya hali ya juu.

Afrika ya kusini ni mfano mwingine. Waimbaji mashuhuri kama Miriam Makeba na wengine wengi walitumia nyimbo na muziki kuhamasisha mapambano ya ubaguzi wa rangi. Nyimbo zao na muziki vilitoa ujumbe ndani na nje ya nchi. Nyimbo, kule Afrika ya Kusikini, ilikuwa sehemu ya mapambano. Ile sinema ya Sarafina, iliyovuma sana, kwa kiasi kikubwa imetawaliwa na nyimbo, hata wakati wa mazishi ya mashujaa waliokufa wakipambana na makaburu, nyimbo zinakuwa sehemu ya maombolezo, kitulizo na kichocheo cha kuendeleza mapambano.

Mfano mwingine ni wa hapa nyumbani, Wanawake wa TANU, walitumia Taarabu, ngoma,ngonjera na mashairi, kuwahamasisha watanganyika kushikamana na kumfukuza mkoloni. Ujumbe uliopitishwa kwenye nyimbo, ulipenyeza kila sehemu ya nchi na hata nchi za nje. Watu walikusanyika kusikiliza taarabu na mwishowe jukwaa la taarabu, lilibadilika na kuwa jukwaa la kisiasa. Watu walikuwa wanakubali kusikiliza baada kuhamasikika kutokana na ujumbe uliokuwa ukipenyezwa kupitia nyimbo za taarabu.

Inaelekea mwanadamu ana tabia ya kutumia nyimbo kuelezea machungu aliyonayo moyoni, machungu ya jamii na wakati mwingine machungu ya taifa. Hata enzi za waisraeli, tunawasikia wakiimba: “ Kando kando ya mito ya Babeli, ndo tuliketi na kuimba, tulipoikumbuka Sayuni..” Hata kitabu chote cha Zaburi ni nyimbo walizoziimba, wakimlilia Mungu, wao kuwaletea ukombozi.

Juzi, nimemsikia Rais Kikwete, akisema kwamba anapendelea kusikiliza muziki, lakini siku hizi kila akifungulia runinga hakuti nyimbo zake za zamani, anachokikuta ni muziki wa Bongo Flava. Aliyasema haya wakati alipohojiwa na BBC. Hivyo amelazimika uisikiliza misiki ya Bongo Flava na anaipenda. Sikushangaa kusikia hivyo, maana mtu anayependa muziki, kama Rais wetu, hawezi kuacha kuipenda miziki ya Bongo Flava, au kwa lugha yetu, miziki ya kizasi kipya. Mwanzoni, unafikiria ni utani au ni vichaa Fulani. Lakini ukisikiliza kwa makini unagundua utamu na furaha ya Bongo Flava. Rais Kikwete, alisema kwamba hata yeye mwanzoni hakuelewa, lakini baadaye ameelewa na anapenda sana Bongo Flava. Ningepata nafasi ya kukaa kitako na Rais Kikwete, ningeuliza swali moja: Bongo Flava inafurahisha, ujumbe wake unapata?

Hata wakiimba “Kamongo”, “Utaliona Jiji na mitaa yake”, “Umasikini huu utaisha lini” “Mme Bwege”, “Salam zako Mjomba” nk wanakuwa na ujumbe mzito. Wakati mwingine maneno yao yanachekesha, lakini yanakuwa na ujumbe kwa jamii ya watanzania.

Mimi ninaamini kwamba ujumbe wa Bongo Flava ni mchungu. Kwa mtu anayejali maisha ya leo na kesho kwa taifa letu, ujumbe wa Bongo Flava, ni lazima utauona ni mchungu. Muziki unapendeza, wanacheza vizuri na kuonyesha ubunifu wa hali ya juu, lakini maneno yao yanachoma kwa ncha kali. Ujume wao hauna tofauti na ujumbe ulio kwenye nyimbo za watumwa, hauna tofauti na ujumbe wa nyimbo za waamerika weusi wakati wanatetea haki zao na hauna tofauti na ujumbe wa nyimbo za Afrika ya Kusini wakati wa kupambana na ubaguzi wa rangi. Bongo Flava, ina ujumbe wa wanyonge, watu wanaonyanyaswa na wasiosikilizwa. Bongo Flava inabeba sauti za watoto yatima, watoto wa mitaani, machinga, vijana wa vijiweni wasiokuwa na ajira, walalahoi nk

Hapo juu, nilisema kwamba waamerika weusi baada ya kushidwa kupata kazi kati nyaja nyingine, kwa vile walikuwa wakibaguliwa na kunyimwa elimu bora, waliishia kwenye muziki na michezo. Na hapa Tanzania, muziki umeanza kuwa kimbilio la vijana wengi. Kila kukicha vijana wapya wanaibuka na nyimbo za Bongo Flava. Hapa pia kuna ujumbe mzito. Ni lazima hii itufikirishe. Ni kweli vijana wote hawa wana vipaji vya kuimba au ni kwa vile hawana ajira na hakuna mtu wa kuwasikiliza kuhusu tatizo hilo la ukosefu wa ajira?

Nimedokeza kwamba wanyonge wakianza kupitisha ujumbe kwenye nyimbo, muziki na ngoma, wanahamasisha mapambano na wakati mwingine kuchochea vita. Hii imetokea sehemu nyingi duniani. Ndo maana ninafikiri kwamba haiwezi kuwa kinyume hapa Tanzania. Swali langu linalenga hapo. Je, Rais wetu anafurahia tu Bogo Flava, au anatafakari ujumbe mchungu unaopenyezwa kwenye nyimbo hizo? Na kama anatafakari juu ya ujumbe mchungu wa Bongo Flava, je anachukua hatua gani? Au ni kweli anaweza kukubaliana na mimi kwamba Bongo Flava, wanabeba ujumbe mchungu? Au ni matatizo yaliyo kwenye kichwa changu?

Mfano, akisikia wimbo wa Bongo Flava, unaoelezea manyanyaso ya upatikanaji wa Visa, anatafakari nini? Yeye amekuwa waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa kwa miaka kumi. Anajua jinsi watanzania wasivyotoka sana nje ya nchi ukilinganisa na nchi jirani za Uganda na Kenya. Yeye anajua vizuri umuhimu wak utoka nje, maana anatetea safari zake nje ya nchi kwamba ni lazima: “ Nikikaa tu ndani ya nchi tutaishia kugawana mihogo” Nilimsikia akitoa hoja hiyo wakati akihojiwa na BBC. Hivyo anajua umuhimu wa mtu kutoka na kwenda kutafuta. Lakini mashariti makubwa ya upatikanaji wa visa yanawafanya watanzania kufungiwa ndani ya Taifa lao. Je, ujumbe wa Bongo Flava, kuhusu tatizo la upatikanaji wa visa unamsukuma kuchunguza kero hizo zinazotolewa na vijana. Niliposikia wimbo huo kwa mara ya kwanza, nilifikiria vijana wamechanganyikiwa mpaka niliposhuhudi mimi mwenye mtu akinyimwa visa pale kwenye ubalozi wa Amerika. Niliandika makala ndefu nikielezea yale ambayo niliona si haki; mfano kufikiria kwamba kila anayeomba anataka kuhamia Amerika, na maswali wanayouliza ya kama mtu ana gari, ana mshahara mkubwa nk. Tena nilidokezea kile kitendo cha mtu kulipia visa dola 100 kabla ya kupata visa, na asipopata visa, pesa hizo zinachukuliwa. Hili limeshughulikiwa kiasi gani? Bongo Flava, wanaendelea kuimba na kusambaza ujumbe ndani n nje ya nchi. Je, Mheshimiwa Rais, ujumbe huu unaingia kwenye furaha yake na katika tafakuri zake? Ni kweli muziki unafurahisha, lakini unafurahisha zaidi unapoingia ndani ya fikira na kuamsha hisia Fulani!

Ninapoandika makala hii vijana wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam, wanaandaa maandamo kupinga uamuzi wa asilimia 40, ya mkopo kulipwa na wazazi. Ni wazi wapo wazazi wenye uwezo huo, lakini asilimia kubwa ya wanafunzi wa Tanzania, ni ya wazazi wasiokuwa na uwezo. Ni wazazi masikini. Ni wazazi wanaolima Korosho, Pamba na Kahawa, na kucheleweshwa kulipwa na wakati mwingine hawalipwi mpaka ziundwe tume! Ni wazazi wanaotegemea kilimo cha mvua, isiponyesha, hakuna mapato! Kuna wimbo wa Bongo Flava, unasema: “ Umasikini huu, utaisha lini?”. Ni kweli asilimia kubwa ya watanzania ni maskini. Lakini serikali inaonyesha picha tofauti. Ukiangalia mashangingi yanayokuwa kwenye misafara ya viongozi, ukijaribu kuhesabu mafuta yanayotumika kwenye mashangingi yaho, ukihesabu pesa zinazotumika kununua vipuri vya mashangingi hayo, ukihesabu posho za wale wote wanaokuwa kwenye misafa hiyo, ni vigumu kusema kwamba Tanzania ni nchi maskini. Utajiri mkubwa unaoonyeshwa na serikali ni mkubwa kiasi cha kshangaa ni kwanini Serikali iwatake wazazi maskini kuchangia asilimia 40 za mkopo. Nimetoa mifano michache, lakini yako mengi, mfamno kuna haja gani serikali kununua samani za mamilion kutoka Afrika ya kusini wakati vijana wa Jua Kali, wana uwezo mkubwa wa kutengeneza samani nzuri na bora? Kwanini mamilioni haya yasingetumika kutoa mikopo kwa vijana wetu wanaosoma elimu ya juu? Semina zinazoendeshwa kwenye mahoteli ya kitalii, zinachukua pesa nyingi ambazo zingesaidia kuwasomesha vijana wetu.

Bongo flava, imebeba ujumbe mzito wa Wamachinga. Ni kiasi gani serikali imewashughulikia vijana hawa baada ya kuwafukuza katikati ya jiji la Dar-es-salaam? Kuna ahadi nyingi za maneno matupu, lakini matendo hayaonekani. Vijana wanarudi katikati ya jiji na kufanya shughuli zao kwa kujificha na kuwapiga chenga maaskari wa jiji. Wa vile watu wanawahitaji, wanawafichia biashara zao na kuwalinda kwa mbinu zote

Bongo Flava, inabeba ujumbe wa watoto wa mitaani. Ni kiasi gani serikali inashughulikia tatizo hili la watoto wa mitaani, ambao kesho wataitwa familia za mitaani? Serikali ina mbinu gani za kuhakikisha vijana hawa wanapata viwanja na kujenga nyumba? Kwani serikali isipunguze matumizi yake makubwa, na badala yake ikaanzisha progamu ya kuwashughulikia watoto hawa wa mitaani.

Bongo Flava, inabeba ujumbe wa watoto yatima. Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha watoto hawa wanapata malezi bora, elimu bora na baadaye kuweza kujitegemea?

Bongo Flava, inabeba ujumbe wa ugonjwa hatari wa UKIMWI. Ni kiasi gani serikali inashughulikia swala hili la UKIMWI? Kuna ukweli kwamba pesa za kupambana na ugonjwa huu zinatafunwa na wajanja wachache. Kuna habari kwamba mashine za kupima virusi pale Muhimbili zilinunuliwa kwa utata mkubwa – watu wanatumia ugonjwa huu kujinufaisha. Serikali inasambaza dawa za kupunguza makali ya UKIMWI, bila kuwapatatia wagonjwa vyakula. Matokeo yake, wagonjwa wanauza madawa hayo, ili wapate pesa za kununulia chakula. Ni nani anafuatilia jambo hili?

Bongo Falava, inabeba ujumbe wa ufa mkubwa unaoendelea kupanuka kila siku kati ya walionacho na wasiokuwanacho. Ufa mkubwa kati ya matajiri masikini. Hii ni changamoto kubwa inayolisakama taifa leu. Serikali ina mipango gani kupunguza ufa huu, maana kadiri ufa unayoendelea kuongezeka ndivyo na mashaka ya kizazi kichacho kishi kwa amani yanaongezeka.

Bongo Flava, ni kioo cha jamii, ni sauti ya wanyonge na sauti ya asilimia kubwa ya watanzania. Kusema kweli, watu wengi wanaanza kuipenda, si kwa kusikia na kufurahi tu, bali na kutafakari pia. Imani yangu ni kwamba Mheshimiwa Rais Kikwete, ana wasaidizi wengi na washauri wa kutosha. Kama yeye alikuwa hajaanza kutafakari juu ya ujumbe mchungu wa Bongo Flava, ni bora afanye hivyo maana matokeo ya hamasa ya Bongo Fava, hayawezi kuwa tofauti na sehemu nyingine za dunia.
Reply With Quote
  #4  
Old 25th February 2007, 08:10 PM
Mkandara Mkandara is online now
Mkandara Aviator
JF Premium Member
Points: 578,599, Level: 100 Points: 578,599, Level: 100 Points: 578,599, Level: 100
Activity: 3% Activity: 3% Activity: 3%
 
Join Date: Fri Mar 2006
Location: T dot
Posts: 7,284
Thanks: 460
Thanked 725 Times in 321 Posts
Rep Power: 80
Mkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the roughMkandara is a jewel in the rough
Default

Mjengwa,

Kuna moja kubwa nimejifunza toka message yako hapo juu na hasa kipande hiki:-
Quote:
Afrika ya kusini ni mfano mwingine. Waimbaji mashuhuri kama Miriam Makeba na wengine wengi walitumia nyimbo na muziki kuhamasisha mapambano ya ubaguzi wa rangi. Nyimbo zao na muziki vilitoa ujumbe ndani na nje ya nchi. Nyimbo, kule Afrika ya Kusikini, ilikuwa sehemu ya mapambano. Ile sinema ya Sarafina, iliyovuma sana, kwa kiasi kikubwa imetawaliwa na nyimbo, hata wakati wa mazishi ya mashujaa waliokufa wakipambana na makaburu, nyimbo zinakuwa sehemu ya maombolezo, kitulizo na kichocheo cha kuendeleza mapambano.

Mfano mwingine ni wa hapa nyumbani, Wanawake wa TANU, walitumia Taarabu, ngoma,ngonjera na mashairi, kuwahamasisha watanganyika kushikamana na kumfukuza mkoloni. Ujumbe uliopitishwa kwenye nyimbo, ulipenyeza kila sehemu ya nchi na hata nchi za nje. Watu walikusanyika kusikiliza taarabu na mwishowe jukwaa la taarabu, lilibadilika na kuwa jukwaa la kisiasa. Watu walikuwa wanakubali kusikiliza baada kuhamasikika kutokana na ujumbe uliokuwa ukipenyezwa kupitia nyimbo za taarabu.

Inaelekea mwanadamu ana tabia ya kutumia nyimbo kuelezea machungu aliyonayo moyoni, machungu ya jamii na wakati mwingine machungu ya taifa. Hata enzi za waisraeli, tunawasikia wakiimba: “ Kando kando ya mito ya Babeli, ndo tuliketi na kuimba, tulipoikumbuka Sayuni..” Hata kitabu chote cha Zaburi ni nyimbo walizoziimba, wakimlilia Mungu, wao kuwaletea ukombozi.
Je, huu sio wakati muafaka kwa vyama vya upinzani kutumia nafasi hii kutangaza mabaya ya serikali yetu?. Pengine rais na wananchi wanaweza kupata mwamko zaidi kupitia muziki wetu na hasa hii Bongo fleva?..
Navishauri vyama vya upinzani kutumia nafasi kama hizi kuwa promote vijana wetu ktk mapambano haya kupitia muziki!...

Hivi wale vijana wa kundi la Wagosi wa kale wameishia wapi?
__________________
Exploration of reality
Reply With Quote
  #5  
Old 25th February 2007, 08:50 PM
Jasusi Jasusi is online now
Jasusi is a truth seeker
JF Premium Member
Points: 277,411, Level: 100 Points: 277,411, Level: 100 Points: 277,411, Level: 100
Activity: 23% Activity: 23% Activity: 23%
 
Join Date: Fri May 2006
Posts: 4,143
Thanks: 1,081
Thanked 558 Times in 289 Posts
Rep Power: 32
Jasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enoughJasusi will become famous soon enough
Default

Mkandara,'
Ni Wagosi wa Kaya. Nadhani hawa vijana wako ahead of the curve. Ukisikiliza wimbo "Kura Yako," usingeamini kuwa wabongo wangekubali kurubiniwa kwa t-shirt, kanga, na shilingi elfu mbili hadi elfu tano kuwapigia kura hawa wajanja walioko madarakani hivi sasa. Lakini you know what? Hope springs eternal. Siku moja ujumbe utafika.
Reply With Quote
  #6  
Old 27th February 2007, 07:54 PM
Mgumu Mgumu is offline
Mgumu has no status.
Senior Member
Points: 128,427, Level: 100 Points: 128,427, Level: 100 Points: 128,427, Level: 100
Activity: 0% Activity: 0% Activity: 0%
 
Join Date: Fri Nov 2006
Posts: 233
Thanks: 0
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 24
Mgumu will become famous soon enoughMgumu will become famous soon enoughMgumu will become famous soon enoughMgumu will become famous soon enoughMgumu will become famous soon enoughMgumu will become famous soon enoughMgumu will become famous soon enoughMgumu will become famous soon enough
Default Remmy Ongara allimba...

Muziki una nguvu sana 'hata kabla m/kiti kuhutubia ni muziki unaanza kuwakusanya watu'

hii ni dalili njema kwani muzikii huu unasikilizwa mpaka vijijini, muziki huu unafungua fikra ya udadisi kwa wadanganyika. Muziki huu ni safari kwa ukombozi wa wadanganyika.

Ila kuna umafia huwa unafanyika, maranyingi ukikaribia uchaguzi, zile nyimbo za wakina Prof. J , Dr Levy ..... huwa hazisiskiki kupigwa kwenye radio na vituo vya TV.

kuna wimbo wa 'Salam kwa mjomba' wa parapanda huu wimbo ni mwiba mkali lakini ni nadra sana kuusikia radioni, wimbo huu ulipotoka ulionyeshwa sana kwenye vituo vya TV lakini sasa umeanza kupotea.
__________________
Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili
Reply With Quote
  #7  
Old 11th March 2007, 05:10 PM
maggid maggid is offline
maggid has no status.
Senior Member
Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Sun Dec 2006
Posts: 84
Thanks: 0
Thanked 19 Times in 5 Posts
Rep Power: 24
maggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enough
Default

Karugendo: Wasomi Wetu Na Makala Za Rai

Ujenzi wa jamii yoyote unategemewa hufanywe na wanajamii wenyewe. Zipo njia mbalimbali za kuwashirikisha wanajamii katika ujenzi wa jamii yao kulingana na uwezo wa kipaji, elimu, taaluma nakadhalika. Katika makala haya nataka kuongelea mchango wa wanaelimu, wasomi, katika jamii inayopita kwenye barabara yenye makorongo huku nikitizama kama kila msomi anasitahiki kuitwa muelimika na ubora wa mchango unaohitajiwa na jamii kutoka kwa msomi na muelimika.

Ni dhahiri kwamba jamii inawahitaji wasomi, na si wasomi tu bali walioelimika, ili kuweza kuivusha katika milima na mabonde ya ulimwengu wa sasa kuyaelekea mafanikio katika maendeleo. Nasema hivyo kwa vile nina mashaka kama kweli kila msomi anakuwa ameelimika. Inabidi tujiulize kuelimika ni kupi, ni kusoma madarasa mengi, vidato vingi, miaka mingi katika vyuo? Tukitaka kupata jibu muafaka kwa kuwatendea haki hao wasomi wetu lazima tutafakari kwanza tukizingatia mienendo yao katika jamii. Baada ya hapo inajibainisha kuwa kuelimika ni kuwa na uwezo wa kuona, kutambua na kufafanua mambo katika usahihi wake kisha kutoa au kuchangia mawazo yenye kuleta utatuzi kila penye utata. Vinginevyo kusoma kutakuwa ni kupoteza muda bure katika madarasa.

Kama kuchukua muda mrefu sana madarasani tunaweza kukuita kuelimika tunapata nini tunapolinganisha ubora wa elimu ya mtu aliyekaa muda mrefu sana madarasani kutokana na kukariri miaka na ya yule aliyekaa muda mfupi kufuatia uwezo wake wa kuyamudu vyema masomo yake? Mathalan, mtu mmoja ilimchukua miaka 6 kupata stashahada ya juu badala ya miaka 3 ya kawaida kwa vile ilimlazimu kukariri kila mwaka. Kwa maana hiyo kama kukaa muda mrefu madarasani kingekuwa kigezo cha ubora wa elimu basi mtu yule stashahada yake ndiyo ingelikuwa bora kuliko zote kwa sababu kaisotea miaka 6 badala ya 3 ya kawaida.

Naye mtu aliyesoma na kuelimika inabidi tumtambue vipi? Kwa kuonyesha vyeti vyake, kututajia miaka aliyomaliza akiyasugua madawati darasani au kwa uwezo wake wa kutambua na kufafanua masuala mbalimbali yanayoigusa jamii yake kwa kutumia upeo wa elimu yake? Bila shaka hili la mwisho ndilo linalopaswa kutumika kama kipimo cha mtu aliyeelimika ambaye ndiye jamii inayemuhitaji. Matatizo ya jamii hayawezi yakatatuliwa na vyeti vya shahada au stashahada wala idadi ya miaka aliyomaliza mtu akivihenyekea.

Njia za kuchangia unjezi wa jamii zipo za aina mbalimbali mojawapo ikiwa ni hii ya upashanaji habari kwa kutumia magazeti. Mbali na kupata habari za matukio katika magazeti watu wanashauri, wanatahadharisha, wanakemea, wanafundisha nakadhalika. Na kwa njia hii ndipo jamii inapohitaji mchango wa wasomi wake kutoka katika hazina yao ya elimu. Huu ndio wakati mzuri wa kuwabaini wasomi walioelimika na wale waliopoteza muda wakisotea vyeti bila kuelimika. Sitegemei msomi asiyekuwa na hazina ya elimu ya kumwezesha kutoa mchango wa kile anachokijua kwa jamii kunishawishi kwa namna yoyote kuwa ameelimika. Basi kama hawezi kutoa walau awe tayari kupokea kinachotolewa na wangine ili aweze kukifanyia kazi.
Wapo wanaodhani kuwa mchango wa mawazo unatoka upande mmoja tu wa waandishi bila kuelewa kuwa hata kusoma mawazo ya wengine ni kushiriki katika michango ya mawazo. Sababu mawazo yakitiwa kwenye makaratasi tu bila kusomwa hayawezi kuchangia wala kusaidia lolote. Kwa mantiki hii mwandishi na msomaji wote wawili wanakuwa wameshiriki kimawazo katika mada inayokuwa inaongelewa

Michango mingi ya mawazo imekuwa ikitolewa kupitia kwenye magazeti kwa njia za makala na waandishi mbalimbali ambayo kwa namna moja au nyingine imekuwa ikifanyiwa kazi na sehemu zinazohusika kwa manufaa ya jamii.

Ipo mifano mingi hai inayoonyesha jinsi makala yanayoandikwa kwenye magazeti yanavyofanyiwa kazi iwe na Serikali, taasisi na hata mashirika ya Kimataifa pamoja na Balozi zilizopo hapa nchini. Hivyo yanapotokea mabadiliko yoyote yenye kupunguza au kuondoa hadha kwa jamii isifikiriwe kwamba ni matokeo ya sala na maombi ya waamini tu bali ni mchango wa mhimili wa nne wa nchi ambao ni vyombo vya habari.

Kuna vyombo vya habari vilivyotokea kujijengea heshima kutokana na umakini wake wa upashaji habari hapa nchini. Mojawapo ya vyombo vilivyojipatia heshima hii ni gazeti hili la Rai. Watu makini wanapenda kupitisha mawazo yao kwenye gazeti hili. Natumia neno makini badala ya wasomi sababu nimegundua kuwa siyo wasomi wote ni makini kama nilivyoonyesha hapo mwanzo kwamba kumbe siyo wasomi wote wanaokuwa wameelimika. Dhana hii imejengeka kichwani mwangu baada ya kuwa nakutana na watu wenye elimu ya kiwango cha Shahada ya Chuo Kikuu wanaonidhihaki kwamba kwanini nahangaika na magazeti ya Kiswahili kama Rai. Kwao, kwa vile wamesoma katika lugha ya kigeni, ili kuonyesha usomi wao ni lazima wasome magezeti yaliyoandikwa katika lugha za kigeni hasa Kiingereza. Sasa kweli hapa kuna kuelimika?

Kwa wasomi hawa cha maana ni lugha iliyotumika na wala siyo maudhui ya kilichoandikwa. Mtu anakucheka wewe unayesoma Rai akikufananisha na mtu anayesoma gazeti la udaku kisa eti kwa vile ni gazeti la Kiswahili wakati huo yeye akiwa anatamba mkononi ameshika gazeti la udaku la Kimarekani la Ebony kwa uhakika kabisa kwamba hayo ndiyo magezeti ya kisomi!

Baadhi ya waosmi wetu wanasema kwamba wanashindwa kusoma Rai kwa vile limejaa makala ndefu za siasa zinazochosha kusoma! Ndiyo, tunakubali hawa ni wasomi, lakini je, tukubali hivyo hivyo kwamba hawa wameelimika? Mtu anayeshindwa kusoma gazeti la Rai kwa kisingizio cha kwamba linachosha kwa makala zake ndefu wakati akijigamba kuwa na shahada ya Chuo Kikuu anawezaje kutushawishi kuwa ameelimika? Ni njia gani anayotaka aitumie kuielewesha jamii yake kile anachokijua bila kutumia lugha inayoeleweka kwa wanajamii walio wengi? Sababu gazeti hili ni kati ya vyombo vya habari makini ambacho watu wenye tafakuri za kina wanakipendelea kukitumia kupashana habari na pia kujadili mambo mbalimbali mazito kwa mepesi yanayoihusu na yaliyoizunguka jamii yao. Sasa msomi huyu anayeona uvivu wa kutumia chombo hiki japo kwa kushiriki kupata mawazo ya wenzake kwa kuyasoma tu unategemeaje mchango wake wa mawazo ya kiusomi katika jamii yetu hii ambayo bado inahitaji kila aina ya mawazo bunifu ili iweze kujisimamia? Mtu wa aina hii ana haki gani ya kuitwa muelimika?

Kijana mmoja mwenye shahada katika fani ya biashara siku moja akiongea kwa mikogo na kuonyesha alivyoridhika na elimu yake hiyo akawa anasema kwamba yeye hana muda wa kusoma gazeti la Rai lililojaa makala za Siasa. Yeye anasema kwamba mtu amuulize nanna ya kufanya ili kukwepa kodi za TRA. Nilipomchokonoa zaidi nikagundua kumbe hana la kuchangia katika mada mbalimbali zinazotoka katika gazeti hili. Ni kweli hana la zaidi la kuchangia katika masuala yanayohusu jamii aliyomo zaidi ya yale aliyokariri shuleni yanayohusu fani yake. Naye huyu eti ameelimika!

Katika hatua nyingine inayoonyesha jinsi athari za wasomi wasioelimika zilivyosambaa na kuanza kuviingilia hata vyombo vya hatari, mhariri mmoja wa gazeti marufu hapa nchini alinitaka nimwandikie makala kuhusu mada fulani. Nilipomuandikia na kumpelekea akaanza kunilalamikia kwamba mimi nimeisha athiriwa na mtindo wa uandishi wa Rai ambao ni wa kurefusha sana makala. Anadai kuandika mambo mengi ni kuwachosha wasomaji. Nilishindwa kuelewa ni wasomaji wa aina gani anaowalenga kwa gazeti lake. Kama walengwa ni watoto wa chekechea naweza nikaamini kwamba kuwaandikia mambo mengi kweli nikuwachosha. Lakini kama walengwa ni watu wazima hoja za kuhofia kuwachosha zinaletwa na kile nilichokuwa nikikiongelea, tatizo la kusoma bila kuelimika. Sababu pamoja na mhariri yule kuwa makini kutowachosha wasomaji wake bado sioni kama gazeti lake linakaribia hata robo ya umaarufu wa gazeti la Rai analodai linawachosha wasomaji wake.

Jamii yetu bado ni duni, kwa maana hiyo bado zinahitajika kufanywa tafiti mbalimbali za kuwaelimisha wanajamii namna ya kuukabili na kisha kuondokana na uduni huu tuliomo. Na mara nyingi tafiti huwekwa kwenye machapisho. Swali ninalojiuliza ni iwapo mtu anaona uvivu wa kusoma ukurasa mmoja wa makala kwenye gazeti anawezaje kupata nguvu za kusoma kitabu cha ripoti ya utafiti chenye kurasa 200 au 300 au hata jarida lenye kurasa 100? Na kwa namna hii ni muujiza gani utakaotumika kuwaelimisha watu wasiotaka kusoma kujiondoa katika uduni wa maisha wakati wanaotegemewa kuongoza njia, wasomi, ndio wanaokatisha tamaa ya usomaji kwamba maandishi mengi yanachosha?

Mfano, katika Serikali ya awamu ya pili, aliyekuwa Rais wakati huo Ali Hassani Mwinyi aliunda tume ya kuchunguza matatizo ya ardhi iliyojulikana kama Presidential Commission of Inquiry into Land Matters, iliyokuwa chini ya Profesa Issa Shivji. Tume hiyo ilitoa ripoti iliyokuwa katika Kiingereza na baadaye ukatengenezwa muhtasari kwa Kiswahili ulioitwa Ardhi ni Uhai. Jambo la kusikitisha ni kwamba sidhani kama kuna mwananchi wa kawaida aliyewahi kusoma ripoti hiyo na matokeo yake ni matatizo ya ardhi kuzidi kuongezeka kila kukicha. Na kwa upande wa wasomi atakayekuwa aliwahi kuisoma ripoti hiyo pengine ni yule aliyejua angeulizwa kwenye mtihani. Vinginevyo tafiri zinazofanyika nchini ni kazi bure hususan zikiwekwa kwenye machapisho. Na hili ni tatizo linalokuzwa na wasomi.

Jambo lingine linalonitatiza katika uandishi ni namna ya kuuweka uandishi katika hali ya kumshawishi mtu asiyekuwa na utamaduni wa kupenda kusoma kuyasoma yale uliyoyaandika. Nimekuwa nikikutana na changamoto mbalimbali kutoka kwa wasomaji. Wapo wanaodai kwamba makala tunazoandika kwenye Rai inabidi tuzipendezeshe zaidi, sijui kuzipendezesha kivipi. Pengine kila makala kuiwekea picha nzuri ya kuchora. Kuna wanaodai kuwa takwimu zinazotolewa kwenye makala za Rai hazijitoshelezi. Nadhani hawa ni wale wanaotaka wakisoma kitu kwenye Rai basi moja kwa moja waingie kwenye vyumba vya mitihani ili kuwakomesha watahini. Yaani mtu anataka akishasoma Rai asiwe tena na haja ya kumsikiliza mwalimu au kusoma vitabu. Na kuna wengine wanaotaka makala ziwe sahihi kama vitabu vya kiada!

Mara zote nimekuwa nijitetea kwamba makala ni mawazo ya watu wanayoyatoa kama mchango katika kuwakumbusha wanajamii wenzao kufanya tafakuri juu ya masuala mbalimbali yanayoihusu jamii yao. Na sio kwamba mawazo ya waandishi wa makala ndiyo yanayopaswa kuwa mwanzo na mwisho wa kila kitu. Mwandishi wa makala anapoamua kuchokoza mada fulani isieleweke kwamba yeye anajua kila kitu kuhusu mada hiyo, ila anachotafuta ni kupata mchango wa mawazo kwa kuwashirikisha wasomaji. Kwa maana hiyo msomaji aliye makini anapoona kwamba kuna pahala panahitaji kujaziwa katika mada inayoongelewa na mwandishi inabidi ajishughulishe kwa kukitafuta kile anachoamini ni ukweli wa kujazia hata kama ni kukifuata makitaba. Na bahati nzui siku hizi kuna makitaba zimezagaa kila pahala, ukiingia kwenye mkahawa wa mtandao (internet café) unapata makitaba nzuri sana. Unapata ukweli unaoutafuta, unachangia katika mada husika na kuinufaisha jamii. Huku ndiko tunakoweza kukuita kuelimika hata bila kusugua madawati.

Wale wanaotegemea kupata kila kitu kwenye gazeti la Rai nilikuwa nawatania kwamba nitamshauri mhariri aangalie upya bei ya gazeti lake, sababu kwa shilingi 500 tu mtu anategemea kupata maarifa ambayo vinginevyo ingebidi ayapate kwa sh. 10,000 na zaidi. Kwa hoja hiyo basi, nasita kukubaliana na wote wanaodai kuwa waandishi wa makala wa gazeti la Rai wanakuwa hawafanyi tafiti za kutosha juu ya mada wanazoamua kuziongelea. Na pia napingana na wale wanaodai kuwa takwimu zinazotolewa na baadhi ya waandishi haziwatoshelezi wasomaji. Inabidi tujenge mazoea ya kutofautisha waandishi wa makala katika magazeti na waandishi wa vitabu au wahadhiri.

Namalizia kwa kusema kwamba usomi huondoa ujinga na kumuelimisha mtu. Elimu humfanya mtu kuyamudu mazingira aliyomo, kwahiyo inabidi aitumie kwa manufaa yake na kwa manufaa ya jamii aliyomo. Pungufu ya hapo itakuwa ni kuulazimisha usomi uonekane ni kitu kisicho na tija kwa jamii zaidi ya watu kupoteza miaka mashuleni wakisotea vyeti.
Reply With Quote
  #8  
Old 11th March 2007, 05:13 PM
maggid maggid is offline
maggid has no status.
Senior Member
Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Sun Dec 2006
Posts: 84
Thanks: 0
Thanked 19 Times in 5 Posts
Rep Power: 24
maggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enough
Default

Nizar: Tunahitaji Tume Huru Kashfa Ya Rada

Na Nizar K. Visram

Alipokuwa nchini Sweden Rais Jakaya Kikwete alisema kitu ambacho kiliwakuna waandishi karibu wote. Magazeti yalijaa vichwa vya habari vinavyomnukuu Rais akisema “Mwacheni Mkapa” au “Muacheni Mzee Mkapa” au “Mkapa asisakamwe kwa rada” au “Rais Kikwete amtetea Mkapa” au “Kikwete amlinda Mkapa” au “Kikwete amkinga kifua Mkapa”

Ni nadra kuona magazeti yakicharuka kiasi hicho na kukubaliana kutoa kipaumbele kwa matamshi ya Rais Kikwete na kutumia maneno karibu sawa. Siku hizi katika safari zake za mara kwa mara nje ya nchi huwa anasema mengi na waandishi wake wanaoambatana naye hufanya kazi ya ziada kutuma habari huku nyumbani. Baadhi ya waandishi hawa ni wa magazeti ya binafsi; sielewi ni nani anayegharamia safari zao, Ikulu au magazeti yenyewe.

Hata hivyo habari hizo zinapotumwa huku nyumbani vyumba vya habari huwa waangalifu sana ingawa mara nyingi inachusha kuona maneno yale yale yakirudiwa. Wengine hutumia utaalamu wao na kuelezea zaidi ya yale yaliyoandikwa na waandishi wa Ikulu, na wengine hurudia yale yale yaliyotumwa na Ikulu bila ya uchambuzi.

Lakini mara hii Rais alipomkingia kifua Rais Mstaafu wote walikubaliana kuwa ni habari muhimu. Kwanini habari hiyo iliwakuna wengi? Ni kwa sababu imezungumzia wazo ambalo linazungumzwa na Watanzania mitaani na katika vyombo vya habari.

Ni suali la maana sana lililoulizwa na yule Mtanzania mwenzetu anayeishi Ubelgiji alipomwambia Rias Kikwete kuwa ni vizuri serikali itoe ufafanuzi kuhusu suala zima la ununuzi wa rada kutoka Uingereza, na ikiwezekana basi hata Rais Mstaafu atoe tamko na kueleza mambo yalikuwaje.

Kuna masuala mawili yanayojitokeza hapa. Moja ni kuwa serikali haiwezi kukaa kimya na kujifanya kuwa haihusiki na kashfa hii ambayo eti ni ya Uingereza peke yake. Pili kuna suala la viongozi waliostaafu kuwajibika kwa yale waliyoyatenda walipokuwa madarakani.

Ni suala la msamaha wa kisheria wanaopewa hata pale inapoeleweka kuwa walifanya kosa la makusudi ambalo si sehemu ya kazi zao. Kupokea rushwa au kupora mali ya umma si kosa linalotokana na utendaji wa kazi ya urais popote pale. Sasa huo msamaha ni kwa mambo gani?

Kuhusu huu ununuzi wa rada tumekuwa tukiimbiwa wimbo wa kwaya, eti ni aibu ya Waingereza ambao wametutapeli na kutukupua dola 12 milioni zaidi ya bei ya kawaida ya rada ambazo alilipwa dalali. Eti waliongeza bei kwa asilimia 30 na kwa hiyo waturudishie Kweli ni hayo tu au kuna zaidi tunaficha?

Na tunamficha nani? Kwa sababu haiingii akilini kuwa unaponunua kitu chochote sokoni au dukani basi utafumba macho na kutoa bei unayoambiwa hata kama ni zaidi kwa asilimia 30. Sembuse rada yenye thamani ya mabilioni ya shilingi na wewe ni serikali inayoajiri wataalamu wa kienyeji na kigeni.

Ni kweli inaingia akilini kuwa serikali yetu hii ilichomoa mabilioni na kuwapa BAE bila ya kuuliza bei halisi? Tunaambiwa zabuni ilitangazwa na wazabuni wanne waliwasilisha tenda zao. Kama ni hivyo ilikuwaje basi tulishindwa kugundua utapeli huu? Au wote wanne hao walizidisha kwa asilimia 40 na 50 na tulishindwa kutambua? Je serikali inaweza kutuamabia ni akina nani hao wazabuni na ni kiasi gani walichotaka?

Kama licha ya kuwa na wataalamu wote hao na licha ya kuitisha tenda kwa mujibu wa sheria na kanuni bado tumetapeliwa, basi tunachoweza kusema ni kuwa kuna kasoro za kimsingi miongoni mwa hao maofisa na viongozi waliotapeliwa. Kwa nini tusikubali hilo na kuwajibika? Wengine wamestaafu na wengine wangalipo madarakani. Wote hao wanapaswa kuwajibishwa. Siyo kuwatupia lawama BAE na serikali ya Uingereza tu bali nasi pia yujiulize na kujichunguza.

Kwa sababu kama tumetapeliwa katika hii rada, je hakuna uwezekano kuwa tumetapeliwa pia katika ununuzi wa ndege ya rais, katika ununuzi wa helikopta za kijeshi, katika ujenzi wa haya majengo ya kifahari ya Benki Kuu, katika utengenezaji wa vitambulisho vya uraia na kadhalika?

Serikali ambayo inatapeliwa dola milioni 12 katika rada bila shaka inaweza pia ikatapeliwa katika mengi mengineyo. Hali hii inatisha. Inahitaji tume huru ichunguze kwa kina na mapana na kutupatia ripoti kamili. Tunahitaji tume ya nguvu zaidi ya ile ya Jaji Warioba.

Wala tusitegemee kuwa eti TAKURU itafanya kazi hiyo. Kama ingekuwa na nia na utashi wa kisiasa basi jambo la kwanza ni kuona yule dalali aliyekula dola 12 milioni je ameziweka wapi? Je akaunti yale huko Uswisi inaonyesha fedha hizo zimehifadhiwa huko? Kama hazipo huko, amezifanyia nini fedha hizo? Amewekeza wapi? Amewapa akina nani? Kama ametoa sadaka basi atueleze ili tuchunguze pia na akaunti za hao waliopewa hiyo sadaka.

Katika tume huru yenye nguvu za kisheria angepaswa ajibu masuali haya rahisi. Lakini je tuna nia ya kumbana na kujua ukweli? Labda tunaachia SFO huko Uingereza. Fedha tumelipa siye, tumetapeliwa siye, kwa nini uchunguzi tuwaachie wao?

Suala zima ni la utashi wa kisiasa. Je watawala wetu kweli wana nia thabiti ya kuwafichua vigogo au tunapigwa chenga tu na hii danganya toto ya kuwaachia wale krismasi kwanza kisha ndio tuwabane?

Katika hili la rada, labda ni kwa sababu tuna wasiwasi kuwa kuna watu hapa wamekula wote na huyo dalali. Muulize raia yeyote barabarani naye atakuambia anaamini kuna rushwa imepita. Kama hayo si kweli kwanini basi tukwepe utafiti? Tuliwasikia mawaziri wakisema ununuzi huo ulikuwa safi na halali, eti fedha zilitolewa na Bunge kwa hiyo ununuzi huo umepitishwa na bunge. Yaani tangu lini Bunge lina uhuru wa kudadisi na kujua siri ya mikataba na zabuni za mabiloni? Bunge lilishiriki katika mikataba ya IPTL, Richmond, migodi na BAE?

Sasa tunaambiwa kuwa Waziri wa Fedha anaomba msaada wa wachunguzi wa kimataifa ili kufichua mabilioni yaliyoliwa kupitia Benki Kuu, hasa katika ule mpango wa kununua madeni. Kwa nini asizungumzie na rada pia?

Mimi nilifikiri kuwa pamoja na hilo tungeteua tume huru ikisimamiwa na Bunge ili kuchunguza hii kashfa ya rada pamoja na mengineyo tuliyotaja hapo juu. TAKURU tuwaache wasubiri hiyo Krismasi imalizike ndipo waaanze kuwakamata vigogo na kuwahoji. Wanasema wanatafuta ushahidi kwanza. Kwani wanapowabana makatibu kata, mahakimu na makarani wa mahakama za mwanzo na madiwani wanapataje ushahidi haraka haraka?

Ndipo tunarudia lile suala la kulindana. Kuna tatizo kubwa hapa nalo ni ile sheria inayowalinda watawala wanapostaafu. Eti tuwaachie wapumzike na kufaidi mali walizotukupua. Ni tatizo ambalo lipo si hapa Tanzania tu bali Afrika nzima na hata kwengineko. Tena huko Ulaya na Marekani kuna magwiji wa rushwa na ulaji zaidi ya hapa kwetu. Tofauti ni kwamba wao angalao huwa wanajaribu kuchukua hatua hata kama ni ndogo, sisi tunasema tuwaachie wazee wapumzike.

Kwani kule Zambia walifanya makosa walipomfikisha Rais Mstaafu Frederick Chiluba mahakamani? Yeye na wafanyabiashara wake walifunguliwa mashataka ya kusababisha dola 488,000 kuyeyuka. Kabla ya hapo alishitakiwa katika mahakama ya Zambia kuwa alisababisha kupotea kwa dola milioni 35. Baada ya muda mashtaka yakafutwa (labda kulindana) lakini yakafunguliwa tena katika mahakama ya Uingereza.

Huyu ni rais aliyechaguliwa mwaka 1991 na nakumbuka wengine hapa walifurahi sana kuwa eti angalao sasa chama cha upinzani kimeshinda uchaguzi na kuking’oa chama tawala. Tulifurahi kuona kuwa kondakta wa basi akipanda cheo na kufikia urais. Tukasema sasa Zambia imepata rais ‘mlalahoi’. Chiluba alitawala miaka kumi na matokeo yake ni nchi kuzidi kudidimia kutokana na ulaji na unyonyaji.

Zambia iliyokuwa maarufu duniani kwa uzalishaji wake wa shaba ikawa ni moja ya nchi masikini wa kutupwa. Mnamo Disemba 2002 deni lake la kimataifa lilifikia dola bilioni 5.4. Ulipaji wa riba tu ulichukua asilimia 20 ya mapato ya serikali. Raia wake zaidi ya asilimia 80 wanaishi maisha ya ufukara na umri wa wastani ni chini ya miaka 40.

Yote haya wakati Zambia ilitekeleza sera za ubinafsishaji na soko huria kama ilivyoamuliwa na Benki ya Dunia na shirika la fedha duniani (IMF) .

Hii ni hali ambapo vigogo wamekuwa wakipora nchi kwa kutumia mbinu kadha. Wengine walihongwa na kulipwa kile wanachokiita kamisheni kwa kutoa zabuni na kusaini mikataba ya kimataifa ambayo haikutimizwa baada ya fedha kuliwa. Shaba iliyouzwa nje ililipwa bei duni wakati mafuta yaliyokuwa yakiagizwa kutoka nje yaligharimu bei ya juu. Vigogo wakawa wanatia mfukoni faida kutokana na tofauti hizo za bei.

Wachunguzi walisema kuwa vigogo walipora nchi na fedha kuzificha katika mabenki ya Uingereza, Marekani, Ubelgiji, Afrika Kusini na nchi za Caribbean.

Chiluba alishitakiwa yeye na aliyekuwa mkuu wake wa usalama wa taifa, Xavier Chungu, pamoja na mawaziri wake na maofisa wake waandamizi. Walikabiliwa na mashitaka 168 ya wizi wa zaidi ya dola 40 milioni. Inasemekana fedha hizi zilichukuliwa kutoka wizara ya fedha na kuwekwa katika akaunti ya Benki ya Taifa ya Zambia (Zanaco) tawi la London. Ni akaunti iliyodhibitiwa na Chiluba.

Serikali ya huko iliunda tume ya uchunguzi ambayo ilichunguza miaka kumi ya utawla wa Chiluba wakati nchi ilipoporwa na vigogo na wafanyabiashara wa kitaifa na kimataifa. Tume ilichunguza zaidi ya kampuni 400 na watu 150. Ikakamata majengo 16. Chiluba naye alipobanwa mawakili wake wakadai kuwa analindwa na katiba. Mara moja Rais Levy Mwanawasa na Bunge walifanya mabadiliko ya katiba na Chiluba akavuliwa kinga iliyokuwa imemsitiri.

Mfano mwengine ni wa Guinea-Bissau ambako watawala wa kijeshi wamekuwa wakifanya mipango ya kumhukumu rais mstaafu Joao Bernardo Vieira kwa mashtaka ya rushwa. Vieira akakimbilia ubalozi wa Ureno na kuomba hifadhi ya kisiasa
Huko Nigeria nako vita dhidi ya rushwa imekuwa ikiongozwa na tume ya kupambana na uhalifu wa kiuchumi (EFCC). Mwenyekiti Nuhu Ribadu anasema katika muda wa miaka miwili tume yake imefanikiwa kurudisha dola bilioni tano zilizoporwa na watu 82 wamefunguliwa mashtaka. Kati yao wamo aliyekuwa mkuu wa polisi, waziri na gavana wa jimbo. Bwana Ribadu anasema tatizo analokabiliwa ni kuwa viongozi wa kitaifa na magavana wana kinga za kisheria.
Mmojawapo ni Makamu wa Rais Atiku Abubakar. Ripoti ya EFCC inamtuhumu kuwa amepora zaidi ya dola milioni 100 kutoka mfuko wa serikali. Sasa anafanya bidii agombee urais. Wakati huohuo EFCC imetoa majina ya wanasiasa 135 ambao hawawezi kugombea uchaguzi kwa sababu ya kukabiliwa na tuhuma za rushwa. Mmojawapo ni Atiku.

Halafu pia kuna mfano maarufu wa aliyekuwa rais wa Zaire (DRC) Mobutu Sese Seko pamoja na rais wa zamani wa Nigeria, Jenerali Sani Abacha. Hawa wawili wamo katika orodha ya marais kumi walio waporaji wakubwa duniani.

Wengineo ni akina Mohammed Suharto wa Indonesia ambaye inasemekana amepora dola bilioni 15 hadi 35, Ferdinand Marcos wa Philippines aliyepora kati ya dola 5 na10 billion, Slobodan Milosevic wa Serbia/Yugoslavia (dola billioni moja), Jean-Claude Duvalier wa Haiti (dola milioni 300-800), Alberto Fujimori wa Peru (dola milioni 600), Pavlo Lazarenko wa Ukraine (dola milioni 114-200), Arnoldo Alem wa Nicaragua (dola milioni 100) na Joseph Estrada wa Philippines (dola milioni 78-80).

Nchini Angola IMF imegundua kuwa kiasi cha dola bilioni moja hadi tano zinazotokana na kodi ya mafuta hupotea kila mwaka. Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu, Global Witness, mnamo mwishoni mwa miaka ya 1990 mamilioni ya dola alikuwa akipewa Rais Eduardo dos Santos na kampuni ya mafuta ya Exxon Mobil na mengineyo ili kupigana na waasi waliokuwa wakipinga utawala wake.

Na gazeti la Los Angeles Times linasema kuwa huko Equatorial Guinea makampuni ya mafuta kutoka Marekani yaliweka zaidi ya dola milioni 300 katika akaunti iliyokuwa ikidhibitiwa na rais wa nchi hiyo. Hali kama hiyo inaonekana pia huko Gabon.

Haya ni baadhi ya matatizo tunayokabiliana nayo katika Afrika. Tusijidanganye kuwa matatizo ya Nigeria na Angola na Equitorial Guinea hayapo katika nchi zingine. Mfumo ni ule ule kote katika Afrika kuanzia Nigeria hadi Afrika Kusini na Tanzania.

Ndio maana tunahitaji kupambana na hii kinga waliojiwekea watawala wanapotuambia tuwaache wapumzike. Tunahitaji watu kama mchungaji David Gitari wa Kenya ambaye alisimama kwenye altari na kusema Rais Daniel Rais Moi aondoke madarakani. Aliwaambia waumini kuwa wakati wa kupigania uhuru watawala wetu katika Afrika walituahidi kuwa wangepiga vita umasikini, ujinga na maradhi lakini vita hivyo vimeshindikana na wananchi wamezidi kuwa masikini kuliko walivyokuwa wakati wa uhuru. Akasema leo hii Kenya ni miongoni mwa nchi tano masikini sana ulimwenguni.

Labda Gitari angeongeza pia kwa kusema kuwa wakati huo huo watawala wetu ni miongoni mwa matajiri wa kupindukia duniani, wakisaidiwa na mabwana zao wa IMF, WB na makampuni ya mafuta na madini.

Na ndio maana tunasema wanastahili wawajibishwe na kutuambia waliupata wapi utajiri huo. Huko Kenya wananchi wanadai kuwa wawajibishwe kutokana na kashfa ya Goldenberg ambayo watawala wanajaribu kuificha.

Na hapa Tanzania nako ni lazima wawajibishwe kutokana na kashfa za BAE na kadhalika ambazo watawala wetu wanajaribu kuzifunika.


nizarvisram@ctvsatcom.net

Last edited by Ole; 11th March 2007 at 08:39 PM..
Reply With Quote
  #9  
Old 12th March 2007, 04:33 PM
maggid maggid is offline
maggid has no status.
Senior Member
Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Sun Dec 2006
Posts: 84
Thanks: 0
Thanked 19 Times in 5 Posts
Rep Power: 24
maggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enough
Default

CCM: Inavua Kambale Kwa Kukausha Lambo!

( Makala hii ilichapwa na RAI juma hili)

Na Maggid Mjengwa,

LAMBO ni bwawa la kufugia samaki. Mwenye bwawa ana njia mbili za kuvua samaki ; kutumia nyavu au ndoano. Lakini, kama akiona anaambulia dagaa tu, basi, huenda akaamua kutumia njia ya mkato. Njia hii si nzuri na haishauriwi. Ni njia ya kukausha lambo kwa kupasua ukingo wa lambo kuruhusu maji kupotelea ardhini. Mtu huyu atabaki akifurahia kuona kambale wakubwa wakihangaika hadi kufa kwa kukosa muhimu kinachowafanya waishi, maji. Na mtu huyu, baada ya kuwatafuna kambale akawamaliza, siku atapodai ana mipango ya kutengeneza lambo lingine afuge samaki wake, si wengi watakaomwelewa.

Wahenga walinena; tembea ujionee. Hii ina maana pia; tembea ujifunze. Maswali unayoulizwa ugenini yaweza pia yakawa ni ushauri. Hivi karibuni Rais wetu Jakaya Kikwete alikuwa ziarani ughaibuni, akiwa nchini Denmark alikutana na hoja nzito kutoka kwa Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa nchi hiyo Bi. Ulla Termas. Hoja ya mama huyu ilihusu mwenendo wa kidemokrasia katika Tanzania na hususan udhaifu wa vyama vya upinzani. Kimsingi Waziri yule alionyesha wasiwasi wake na serikali yake juu ya hali hiyo.

Hakika hoja hii si ngeni kwetu Watanzania. Tofauti na Waziri yule wa Denmark, sisi ndio tunaoona hali halisi ya kila siku na ndio wenye kuathirika moja kwa moja. Hoja hii tunayo; aidha tunakosa ujasiri wa kuiweka hadharani au tunajua majibu tutakayopewa hata tukiuliza, hivyo basi , hatuoni haja ya kuuliza.

Wakati mwingine tunafanya makosa kwa kufanya mambo kwa kuangalia maslahi ya miaka 20 au 25 mbele. Muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Miaka hiyo 20 au 25 ijayo wengi wetu huenda tusiwepo tena hapa duniani, lakini, Tanzania kama nchi itabaki, tuna kizazi tutakachokiacha. Mipango na maamuzi yetu tunayoyafanya sasa ilenge kwenye kuhakikisha maslahi ya Tanzania kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kimsingi, Waziri yule wa Denmark alihoji juu ya mwenendo wa kidemokrasia katika nchi yetu. Na kwa vile CCM ni chama tawala, na Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa chama hicho, basi, hoja ililengwa kwa muhusika mkuu.

Rais Kikwete alifafanua, kuwa kwa vyama vya upinzani kukosa ushindi kunatokana na wao kutokuwa na sera mbadala kuliko zile za CCM, na kwamba pengine havijiandai na kujinadi vizuri. Pamoja na ufafanuzi huo wa Rais, bado nahofia, kuwa swali hili bado litamwandama Rais hata siku zijazo. Maana, dunia imebadilika na serikali za nchi zimebadilika pia.

Mathalan, miaka ile ya sabini kamwe tusingeota kwa nchi kama Denmark kutoa shinikizo kwa Tanzania kupitisha kwenye Bunge la Tanzania muswaada wa sheria ya rushwa kama inavyotarajiwa kufanyika mwezi ujao kule Dodoma. Kinachotokea sasa ni kwa wapiga kura wa nchi hizi za wakubwa kuanza kuhoji misaada ya kiuchumi inayotolewa na nchi zao kwa nchi masikini kama ya kwetu. Nchi ambazo, nyingine wanadai hazina misingi imara ya demokrasia; uwepo wa ushindani wa vyama vingi ni moja ya misingi hiyo.

Kwa zaidi ya miaka 12 nimepata kuishi na kusoma katika nchi ya Sweden. Ni katika nchi ile, kwa mara ya kwanza nilisikia dhana ya ”Udikteta wa asilimia 90”. Hapa waliimaanisha nchi zenye marais au vyama vinavyopata ushindi wa kishindo wa asilimia 90 au hata 99.9.

Kwa Msweden wa kawaida ni taabu sana kwake kuamini, kuwa katika nchi yenye kufuata misingi ya demokrasia na kuruhusu chaguzi huru na za haki, Rais au chama kinaweza kupata ushindi wa asilimia 90 au 99.9. Wasweden hawa wamefundishwa shuleni, kuwa hayo huwa ni matokeo ya kupangwa katika tawala za kidikteta kwa vile kwenye chaguzi huru na za haki si rahisi kuvuka hata asilimia 80, kwani, wanadamu wana hulka ya kuwa na fikra tofauti. Hata katika familia moja ya baba, mama na watoto, bado kunaweza kukawa na tofauti za kufikiri miongoni mwa wanafamalia.

Naam. Dunia imebadilika na upepo wa kisiasa pia. Leo kuna baadhi ya nchi za Kimagharibi zinazotawaliwa na vyama vyenye itikadi za mrengo wa kulia; Sweden, Denmark na Ujerumani ni mfano wa nchi hizo. Moja ya ahadi ya vyama hivi kwa wapiga kura wao waliowaingiza madarakani ni kuhakikisha sera ya misaada ya nchi hizo zinaangaliwa upya na kwamba fedha za walipa kodi wao hazitaelekezwa kwenye nchi zenye kukiuka misingi ya kidemokrasia. Hivyo basi, baadhi ya maamuzi ya serikali hizi ni shinikizo toka kwa wapiga kura wao.

Tukirudi kwenye hoja ya Waziri yule wa Denmark; tunadhani ni kweli, kuwa ndani ya CCM kuna baadhi, ambao sio tu wanaota kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja , bali wanatekeleza kwa vitendo azma ya kutaka kuturudisha kwenye mfumo wa chama kimoja.

Na kama ilivyokuwa kwa mvuvi wa kambale kwenye lambo. Lengo laweza kuwa ni kuumaliza upinzani kwa ”kuwavua” viongozi wakuu wa vyama vya upinzani. Ikishindana, basi, mkakati ni kukausha lambo na kuwaacha wakitapatapa topeni. Malengo hapa yaweza kuwa mawili; kuudidimiza upinzani nje ya CCM na kukamilisha lengo la pili la kuudidimiza upinzani ndani ya CCM. Itafika mahala, hata wale wapinzani ndani ya CCM watajiuliza; ” Hivi nikiwa mpinzani ndani ya chama, nikifanyiwa fitna kisha nikatolewa nje ya chama, nitakwenda wapi? Bila shaka, ndani ya CCM kuna wanaojiuliza swali hili. Jibu wanalipata kisha wanabaki kunung’unika tu.

Lakini kama Chama, CCM ya sasa imebadilika. CCM ya leo ni mkusanyiko wa watu wa kila aina. Kuna waliongia kwa kutazama maslahi ya chama, lakini kuna wengi pia, walioingia na wanaoingia ndani ya chama hicho kwa kuangalia maslahi yao.

CCM ya jana ilikuwa kweli ni kimbilio la Makabwela. Lakini, CCM ya sasa inakimbiliwa na wafanyabiashara, wasomi wenye kuacha taaluma zao na wajanja wengine. Watu hawa wako tayari kutumia mamilioni ya shilingi kukimbilia uongozi ndani ya chama hicho. Wengine wanakimbilia ndani ya chama kujificha, kuficha maovu yao, kulinda na kutetea maslahi yao binafsi. Wanaamini, kuwepo kwao ndani ya Chama ni kwa Chama kuwasaidia wao na si kinyume chake.

Naam. Siasa ni hatua za majadiliano endelevu. Majadiliano yasiyokoma. Si suala la uchaguzi mkuu halafu basi, kusubiri uchaguzi ujao. Vyama vingi si uadui. Mwenye ajenda ya kutaka kuua upinzani kwa maana ya kutokubali fikra nyingine zijitokeze, basi huyo ana dhambi anayotaka kuificha. Na hafanyi hilo kwa maslahi ya wengi na ya taifa bali ya kwake mwenyewe na ya wachache katika jamii.
Reply With Quote
  #10  
Old 14th March 2007, 03:23 PM
maggid maggid is offline
maggid has no status.
Senior Member
Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100 Points: 265,620, Level: 100
Activity: 1% Activity: 1% Activity: 1%
 
Join Date: Sun Dec 2006
Posts: 84
Thanks: 0
Thanked 19 Times in 5 Posts
Rep Power: 24
maggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enoughmaggid will become famous soon enough
Default

Kikwete Na Ndoto Ya Ngurdoto!

Na Nizar K Visram

Tarehe 13 Machi 2006 viongozi wa nchi hii walikutana katika hoteli ya kitalii kule Ngurudoto kwa kile walichokiita semina elekezi. Semina hiyo ya kuelekezana ilikutanisha Rais, Makamo wa Rais, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongozi, Mawaziri na manaibu wao, makatibu wakuu na manaibu wao.

Hatukuambiwa kuhusu maofisa, wapambe, waandishi, makatibu muhtasi, makarani, madereva na kadhalika ambao walichangia katika gharama hata kama si katika mjadala

Rais Kikwete alitoa sababu kuu mbili za semina hiyo ya Ngurdoto
Kwanza alitaka viongozi wafahamiane kwa karibu. Pili, alipenda viongozi wapate fursa, “katika mazingira tulivu kama ya Ngurdoto Mountain Lodge ya kutafakari kwa kina na kubadilishana mawazo kuhusu majukumu na changamoto
zinazowakabili katika kuwatumikia Watanzania kwa ukamilifu na uadilifu”

Mimi nilifikiri kuwa Rais Kikwete alipotembelea wizara zote pamoja na idara na taasisi zake alikuwa na lengo la kufahamiana na viongozi na matatizo yao na kupata fursa ya kuongea nao wakiwa wako kazini. Pia tunaelewa kuwa mawazi wote na wabunge wote huwa wanakutana kwa miezi kadha pale bungeni na katika kamati za bunge na kufanya kazi kwa pamoja..

Licha ya yote hayo Rais aliona ilipasa wakutane katika hoteli ya kitalii kwa siku tatu ili “wafahamiane zaidi”. Wananchi walianza kujiuliza utamaduni huu umetoka wapi na mantiki yake ni nini hasa.

Je ilikuwa ni lazima wakutane huko mlimani ili waondoke na “upeo mpya, mtazamo mpya, ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya” katika utendaji wao na utekelezaji wa majukumu na wajibu wao, kama alivyosema Rias?

Je iliwalazimu kukutana kisiri pale Ngurdoto ili waelewe kuwa wajibu wao wa kwanza ni “kujua kwa uhakika wananchi wanataka nini, wana shida gani, wanakerwa na lipi baya?” Kwa nini wasikutane na wananchi kule kijijini ili kujua shida zao nini na wanataka nini?

Licha ya yote hayo kuna maneno ya maana na mazito ambayo yalisemwa na Rais pale Ngurdoto. Aliwaambia viongozi wenzake kuwa “Watanzania wanapenda kuwa na viongozi ambao wanawasikiliza, wanaojali kushughulikia mambo yao, wanaoheshimu maadili ya utumishi wa umma”

Alisema kiongozi yeyote wa Kitanzania anatakiwa awe “mchapa kazi hodari, anayesikiliza na kujali shida za wananchi, aliye mwadilifu, asiyeomba wala kupokea rushwa katika kuwatumikia wananchi, anayechukia maovu na dhuluma”

Haya ndiyo yaliyosema na Rais Kikwete kule Ngurdoto mwaka mmoja uliopita. Alikumbusha Mwongozo wa TANU ambao vigogo wengi leo wamesahau na wasingependa hata kukumbushwa. Wakamsikiliza (labda huku wakiguna) akinukuu Mwongozo wa TANU kwa kusema “sisi viongozi ni lazima tuwe tayari kufanya uchambuzi wa ukweli kuhusu hali ilivyo na kuwa tayari kukiri mapungufu. Vilevile, tuwe wepesi kufanya masahihisho, kujikosoa na kukosolewa”

Mimi nilitegemea kuwa angenukuu pia ile ibara ya 15 isemayo “Kiongozi asiwe mnyapara” ambayo ilivuma sasa miaka ile ya 1971.

Hata hivyo Rais alidiriki kuwaambia vigogo pale Ngurdoto kuwa:

“Baadhi ya watumishi wa Serikali badala ya kuwahudumia wananchi sasa wamegeuka kuwa mabwana, wana jeuri na wanatumia nafasi walizonazo kujinufaisha binafsi. Si jambo la ajabu kuona watumishi wa
umma wakitenda mambo kinyume na maadili ya taaluma zao.
Wanafanya hivyo kwa makusudi kabisa. Mara nyingi
kinachowafanya wafanye hivyo ni kutafuta maslahi binafsi”

Hayo ni maneno mazito sana. Ni maneno ya busara. Inanikumbusha ile hotuba yake alipokuwa akizindua Bunge mwishoni mwa 2005. Ni wangapi katika ile semina ya Ngurdoto waliondoka wakiwa wanaamini kwa dhati maneno haya? Ni wangapi walinuia kutekeleza? Ni jambo la kusikitisha sana iwapo semina kama hizi zitakuwa ni tukio la mara kwa mara kwa vigogo kukutana huko mahotelini na kujichana.

Tukiacha hizi nasaha za kisiasa, kuna mengine pia aliyoyasema kuhusu hali ya kiuchumi na maendeleo ya jamii. Muhimu zaidi ni hili suala zito la ajira ambalo limekuwa likiwaumiza vichwa watu wengi katika nchi hii. Hii ahadi ya ajira milioni moja ni ya maana sana na inapaswa ichunguzwe na kuchambuliwa kwa kina. Kwa maoni yangu ni ahadi moja ambayo ina lengo linaloeleweka, linalohesabika na lisiloepukika. Ni tofauti na ahadi zingine ambazo zinaelea hewani kama vile kusema hali bora kwa wote.

Kuhusu hili ahadi ya ajira milioni moja Rais aliiambia semina ya Ngurdoto kama ifuatavyo:.

“Ahadi hii inawahusu hasa mamia (labda angepaswa aseme maelfu) ya vijana wanaomaliza shule na vyuo kila mwaka na watu wazima wenye elimu na ujuzi lakini ambao wameshindwa kabisa kupata ajira yoyote. Ni vyema pia hapa tujiulize, je, tutafanyaje ili kuwapatia Watanzania hawa ajira ya kujiajiri au kuajiriwa? Je, tunao mkakati wa kutekeleza ahadi yetu? Maana nao wanasubiri kwa hamu kubwa kuona jinsi gani tutatimiza ahadi yetu kwao. Hili nalo lazima tukiri kuwa ni deni”

Kweli ni deni.Tayari wananchi wanauliza zikowapi hizo ajira. Ili kujibu suala hili ni vizuri tuangalie uchumi wa nchi yetu na kuona kama kweli una uwezo wa kuzalisha ajira milioni moja ifikapo 2010.

Uchumi wa nchi hii umekuwa ukikua kwa asilimia 4 kila mwaka. Ukuaji huu hautoshi kuweza kuboresha maisha ya wananchi. Halafu tena uchumi wenyewe unategemea kwa kiasi kikubwa misaada ya wafadhili, pamoja na mzigo wa deni la dola bilioni 7.5. Riba tu inachukua asilimia 40 ya matumizi yote ya serikali

Tukichukulia sekta ya viwanda, ni ndogo mno. Mnamo 2002-2003 sekta hii iliathirika vibaya sana kutokana na ukame na kukosekana kwa umeme. Uzalishaji viwandani ulianguka na kufikia asilimia 30 tu.

Kuanzia 2003 tukaikabidhi Tanesco kwa kampuni ya kigeni na hali ya umeme ikawa mbaya zaidi kufikia 2006. Uzalishaji ukazidi kudidimia. Net Solution tuliyoingiza Tanesco kwa kutumia FFU sasa imetutumbukia nyongo. Na bei ya umeme inazidi kuongezeka kiasi kwamba tunazidi hata nchi za SADC, siyo tu katika gharama ya umeme bali pia na bei ya maji na mafuta. Yote haya maana yake ni kuongezeka kwa gharama za uzalishaji, ambao ni mzigo kwa mwananchi wa kawaida, mzalishaji na muwekezaji.

Huu ndio uchumi tunaotegemea kuzalisha ajira milioni moja katika miaka mitano. Mwaka mmoja umepita na tunaendelea na wa pili. Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, John Chiligati aliuambia mkutano wa sekta binafsi kwamba serikali haina hata takwimu ya watu wanaoajiriwa kila mwaka na sekta binafsi. Yaani serikali ingali inaiomba sekta binafsi itoe takwimu ya ajira zake, kitu ambacho kimeshindikana.

Ila tunachoambiwa ni kwamba kwa wastani asilimia 13 ya wananchi hawana kazi katika nchi nzima. Dar es Salaam hali ni mbaya zaidi kwa vile asilimia 46.5 ya wasio na kazi huishi hapa jijini. Katika miji mingine ni asilimia 25.5. Hata vijijini asilimia 8.4 ya wakaazi hawana kazi. Na ukichukua vijana kati ya miaka 15 hadi 24 ni asilimia 28 wanaozurura huko vijijini.

Tumekuwa tukiimba wimbo wa wasio na kazi warudi vijinini wakalime, bila ya kufikiria kuwa hata huko nako kuna ukosefu mkubwa wa kazi. Wanatoka vijijini kusiko na kazi na kuja jijini ambako wanakuta hali ni mbaya zaidi. Na wale wanaojishughulisha kwa kuuza matunda na mihogo hapa jijini wanakumbana na mgambo wanaowanyang’anya bidhaa zao, kuwapiga, kuwavua ngua na kuwatia gerezani.

Wengine watajiuliza iweje ajira ikosekane vijijini ambako kuna ardhi ya kulima. Suala la kujiuliza ni mfumo wa kilimo chetu. Ni kujiuliza kwa nini uzalishaji unaanguka huko mashambani. Kwa mfano zao la pamba limeanguka kutoka tani 84,200 mnamo 1995/6 hadi tani 46,800 mwaka 2003/04. Kahawa imeanguka kutoka tani 52,000 mnamo 1995/6 hadi tani 32,500 mnamo 2003/4. Korosho umetoka tani 82,000 hadi tani 79,000 katika muda huohuo.

Si ajabu wakulima wamepoteza imani katika kilimo cha mazao ya biashara hasa kwa vile hakilipi. Baada ya kulinyonga Azimio la Arusha, tukadharau na kuua vyama vya ushirika na kuruhusu walanguzi wavamie biashara ya nafaka. Matokeo yake ni kuwa bei ikaanguka na mara nyingi mazao ya mkulima yakaharibika. Walanguzi waliingia mitini. Rais Kikwete akabaki anapiga kelele kuwa wanunuzi wa korosho wamemwangusha. Lakini hilo ndilo soko huria ambalo limechukua nafasi ya vyama vya ushirika, kwa sababu ndivyo tulivyoamrishwa na wafadhili!

Siyo tu tuna idadi kubwa ya wasio na kazi, bali idadi hiyo inaongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mujibu wa utafiti wa ajira (Labour Survey) vijana 700,000 wanaingia katika soko la kazi kila mwaka, wengi wao wakitoka mashuleni na vyuoni. Yaani katika miaka mitano wanafikia milioni tatu na nusu. Sasa hata kama serikali itatoa ajira milioni moja katika miaka hiyo mitano bado watabaki wengi wanaotafuta ajirai.

Tumekuwa tukiambiwa kuwa Rais Kikwete katika safari zake za kimataifa kazi moja anayoifanya ni kukutana na wawekezaji na kuwashawishi kuja kuwekeza na kutoa ajira. Bila ya shaka anategemea kuwa sehemu kubwa ya ajira milioni moja itatokana na wawekezaji katika sekta binafsi. Ni vizuri tutafakari uwezekano wa kutimiza ndoto hii kwa kuangalia ajira zilizopatikana mpaka sasa kutokana na uwekezaji.

Mnamo Oktoba mwaka jana mkuu wa kituo cha uwekezaji (TIC) alituambia kuwa ajira 33,000 zilikuwa zinategemewa. Akatoa tarakimu za miradi ilioanzishwa na ajira zilizopatikana. Jedwali ifuatayo kutoka TIC inaweza kutupa mwanga:

Miradi ya wawekezaji na idadi ya ajira

Muda Idadi ya miradi Thamani
(dola milioni) Idadi ya Ajira Wastani wa ajira kwa kila mradi Wastani wa uwekezaji kwa kila ajira
(dola)
1995-2005 4,317 13,600.00 725,562 168 19,000
Jan.-Juni. 2006 357 3,200.00 33,722 94 95,000


Tunachojifunza kutoka jedwali hii ni kuwa katika awamu ya tatu (1995 hadi 2005) kila mradi kwa wastani ulitoa ajira 168, wakati kila ajira ilihitaji kwa wastani uwekezaji wa dola 19,000.

Lakini tukiingia awamu ya nne (Januari hadi Juni 2006) tunaona kuwa kila mradi unazalisha wastani wa ajira 94 na kila ajira inahitaji uwekezaji wa dola 95,000.

Maana yake ni kuwa siku hizi miradi ya wawekezaji inayopitishwa na TIC inaajiri watu wachache tukifananisha na ilivyokuwa hapo zamani. Pia fedha zinazowekezwa kwa kila mradi zinaongezeka wakati ajira inapungua, au tuseme miradi ni mikubwa zaidi lakini ajira ni ndogo zidi

Sasa kwa mtaji huu, ili kutoa ajira milioni moja tutahitaji uwekezaji wa dola bilioni 95. Hii itatuchukua miaka 13 au 14 na siyo miaka mitano kama tunavyotarajia. Hatujui Rais Kikwete katika misafara yake amefanikiwa kuwashawishi wawekezaji wangapi mpaka sasa na wamewekeza kiasi gani. Itabidi tuambiwe ili tuweze kujua iwapo ndoto ya Ngurdoto itafanikiwa au itabaki ndoto tu.

Ila tunajua kuwa ndoto moja ya JK iliyofanikiwa ni ile ya kuitisha semina elekezi mara kwa mara kama alivyoahidi kule Ngurdoto mwaka mmoja uliopita. Hivi majuzi tu wakuu wa wilaya 113 na wakuu wa mikoa 21 walikuwa na semina nyingine ya siku tano katika hoteli ya kitalii hapa Kunduchi. Lengo ni kuwafunza uongozi na maadili. Kabla ya hapo ilifanyika semina nyingine mwishoni mwa mwaka jana kule kule Ngurdoto.

Ndipo mhariri wa gazeti moja alipotamka:

“Semina hizi zinaelekea kuwa nyingi. Viongozi wamekabidhiwa ilani ya chama pamoja na makabrasha ya Mkukuta, Mkurabita na Dira ya mendeleo. Wananchi wanachosubiri kuona ni nani kati yao anatumia silaha hizo vizuri na nani anayetumia vibaya”

“Mkuu ambaye hadi leo wanafunzi katika eneo lake wanakaa sakafuni, ambaye eneo lake ni mapitio ya mihadarati, anayeshindwa kuhamasisha kilimo, huyu atabaki tu akisubiri semina elekezi katika siku zake zote za uongozi. Fedha zinazotumiwa katika semina hizi zingeweza kusaidia katika ununuzi wa madawati”

Na kwa vile gharama za hizi semina ni siri ya wakuu, labda ni vizuri kujua tu kuwa ile hoteli ya Ngurdoto chumba kimoja kinagharimu kuanzia dola 150 kwa siku hadi 2000 kwa chumba cha kirais. Na hii hoteli ya Kunduchi chumba cha kawaida ni dola 119 hadi kufikia 397 kwa siku.

Mshahara wa kima cha chini kwa Mtanzania ni sawa na dola 45 kwa mwezi. Lakini kwa asilimia 45 wasio na ajira hapa jijini hata hizo hawazipati.

nizarvisram@ctvsatcom.net
Reply With Quote
Reply

Bookmarks

Tags
hoja, makala, mbalimbali, nzito


Currently Active Users Viewing This Thread: 1 (0 members and 1 guests)
 
Thread Tools
Display Modes Rate This Thread
Rate This Thread:

Posting Rules
You may not post new threads
You may not post replies
You may not post attachments
You may not edit your posts

BB code is On
Smilies are On
[IMG] code is On
HTML code is Off
Trackbacks are Off
Pingbacks are Off
Refbacks are On


Similar Threads
Thread Thread Starter Forum Replies Last Post
JamboForums.com:- Forum Rules Spiderman Jukwaa la Siasa 197 11th September 2007 01:57 AM
UCHAGUZI MDOGO TUNDURU...Je, wapinzani wameamka? Mr. Clean Habari na Hoja mchanganyiko 146 24th March 2007 11:42 PM
Nchi haiendeshwi kwa misheni town Spiderman Habari na Hoja mchanganyiko 2 10th December 2006 10:36 AM

Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako!


All times are GMT +3. The time now is 12:17 AM.

Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com