Mbowe kulifumua baraza la mawaziri kivuli; nani kuingia/kutoka?
Jana akiwa Arusha NMC, Mheshimiwa Mbowe alitoa kauli ifuatayo:-
"nakwenda kulifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri vivuli ili kuliandaa vizuri na kuwasilisha bajeti mbadala kwenye Bunge lijalo linalotarajiwa kukutana mwezi Juni".
Je ni nani ataendelea an nani atatishwa ili aendane na kasi ya mabadiliko ya JK?
Re: Mbowe kulifumua baraza la mawaziri kivuli; nani kuingia/kutoka?
Nimejaribu kusoma post zote za mkutano wa jana na bahati nzuri nilikuwepo. Sikuona aliyeleta hii habari nikashangaa maana ina umuhimu wake. Ni kweli alisema na ninaomba tujadili kwa mtazamo wa nani anafaa wizara gani na kwanini ili tupate baraza kivuli lililo bora. Nawasilisha.
Re: Mbowe kulifumua baraza la mawaziri kivuli; nani kuingia/kutoka?
By ritz
FeedbackMungi Mbowe kulifumua baraza la mawaziri kivuli.
Najua unataka kutuambia Mbowe naye atateua wabunge kivuli.
CHADEMA iko imara kuliko kipindi kingine chochote!
Mbowe atakachokifanya kwenye Baraza lake kivuli ni kuhakikisha kila waziri anaiwajibisha serikali kwa hoja, hasa katika kipindi hiki ambacho Mk.were amefanya mabadiliko ya kuwahadaa watanzania. Siku mbili kabla Jk hajabadilisha baraza lake ikulu ilitoa taarifa kwa umma kuwa baraza atakaloliteua litakuwa bora itakayokata kiu ya watanzania.
Wote tumeshuhudia alichokifanya Jk ni kuwabadilisha wezi wale wale wizara zingine.
Nyalandu, Mkuchika, Maghembe wote wezi wakubwa lakini cha ajabu Jk ameendelea kuwalinda!
"Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."
Chadema kulifumua Baraza la Mawaziri Kivuli baada ya kushindwa kazi.
Ritz acha kunywa Bangi bana. We sema ni waziri gani kivuli wa chadema aliyeshindwa?
Nakuhakikishia kuwa Mbowe atakachokifanya ni kuziba nafasi mbili ambazo zipo wazi za Regia Mtema (R.I.P.) na ya Kamanda Lema.
Mawaziri wengine watabaki na wizara zao. Labda anaweza kuwahamisha kutoka wizara moja kwenda wizara nyingine kulingana na changamoto za baraza jipya la Jk.
Mfano wizara ya Uchukuzi amepewa Mwakyembe, Nishati Prof. Muhongo sasa hawa wanatakiwa wakabiliane na mawaziri kivuli makini wa chadema.
"Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."
Follow Us Here