Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

    Report Post
    Page 12 of 14 FirstFirst ... 21011121314 LastLast
    Results 221 to 240 of 262
    1. EMT
      #1
      EMT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2010
      Location : Mahuta
      Posts : 8,890
      Rep Power : 61724
      Likes Received
      7167
      Likes Given
      6430

      Default Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Katika Baraza jipya la mawaziri kuna wabunge wapya ambao waliteuliwa na Rais jana na leo kuwa mawaziri. Mawaziri hao ni Prof. Sospeter Muhongo ambaye aliteuliwa na Rais kuwa mbunge jana na leo ametuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Mwingine ni Bi. Saada Mkuya Salum aliyeteuliwa na Rais kuwa mbunge masaa machache kabla ya kuteuliwa tena kuwa Naibu Waziri wa Fedha (huyu tayari ameshabatizwa "Waziri Voda fasta").

      Kwa mujibu wa taarifa toka Ikulu uteuzi wao kama wabunge unaanza mara moja. Kikao cha bunge kinatarajiwa kuanza tena Juni mwaka huu ambapo tutategemea wabunge wateule kuapishwa. Hata hivyo, mawaziri wote wapya wanatarajiwa kuapishwa tarehe 7 Mei mwaka huu. Hii inamaanisha kuwa Prof. Sospeter Muhongo na Bi. Saada Mkuya Salum wataapishwa kuwa Waziri na Naibu Waziri kabla ya kuapishwa kuwa wabunge.

      Je, inawezekana Waziri au Naibu waziri kuapishwa kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge?

      ============================== ===================

      Majibu ya Naibu Spika, Job Ndugai:

      Hata hivyo taarifa ya Ikulu haikusema wabunge hao wateule wataapishwa lini na wapi, lakini Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alipoulizwa jana alisema alisema kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, mtu yeyote anayeteuliwa kuwa mbunge, ataapishwa katika mkutano wa Bunge unaofuata baada ya uteuzi wake, bila kujali ni mbunge wa kuteuliwa au wa jimbo.

      Ndugai alisema kwa msingi huo, wabunge hao wateule wataapishwa wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge la Bajeti unaotarajiwa kuanza mjini Dodoma, Juni 12.

      Alipoulizwa itakuwaje ikitokea wateule hao wa Rais wakateuliwa pia kuwa mawaziri na kuendelea na kazi kabla ya kuapishwa kuwa wabunge, Naibu Spika alisema kwa hali ya kawaida, hilo haliwezekani.

      “Kwa mujibu wa Katiba, mawaziri watateuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, na anakuwa mbunge mteule hadi pale anapoapishwa, na ndiyo maana baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu, kazi ya kwanza ya Bunge ni kuchagua Spika na Naibu Spika, ambao baadaye watafanya kazi ya kuwaapisha wabunge, na ndipo atateuliwa Waziri Mkuu na kisha mawaziri,” alifafanua Naibu Spika

      Source: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=29712

      ============================== ==========================

      TAARIFA YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KWA VYOMBO VYA HABARI

      Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 4 Mei, 2012 alitangaza mabadiliko katika safu ya Baraza la Mawaziri. Katika uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Mheshimiwa Rais aliwateua Mawaziri wapya kutoka miongoni mwa Wabunge aliokuwa amewateua na kuwatangaza. Baada ya uteuzi huo, kumetolewa maoni kwamba hatua ya Mheshimiwa Rais kuwateua Wabunge Wapya ambao hawajaapishwa Bungeni kuwa Mawaziri ni kitendo cha uvunjaji wa Katiba.

      Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayachukulia maoni haya kama ni jambo lenye maslahi ya jamii na linalohitaji kufafanuliwa; kwa upande mmoja lakini pia, kutolewa kwa elimu ya Umma; kuhusu Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge.

      Msingi wa Katiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4) kwamba:

      “Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge”

      Pili, ni mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e) yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa Wanawake. Wabunge aliowateuwa Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii.

      Tatu, baada ya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbunge anakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada ya kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa viti maalum au anapochaguliwa na Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake ya uteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e). Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitaji kuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge. Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli za Bunge.

      Katiba ya nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo awe ameapishwa Bungeni kwanza. Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia ni kwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.

      Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria. Aidha, katika kutekeleza madaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele ya Rais hata kama hajaapishwa Bungeni. Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokea uteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa. Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwa katika kikao cha Bunge kijacho.

      Bila shaka ufafanuzi huu utaleta uelewa katika jambo hili na kuepusha mikangayiko isiyokuwa ya lazima.

      Imetolewa na Jaji Frederick M. Werema (Mb)
      MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

      06 Mei, 2012
      Last edited by EMT; 7th May 2012 at 13:22.
      “Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.

    2. Miaka 50

    3. #221
      Mtanzania's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2006
      Location : UK
      Posts : 5,276
      Rep Power : 5566
      Likes Received
      288
      Likes Given
      77

      Default

      Quote By Pasco
      Kwa tafsiri yangu, huu ni uvunjaji tuu wa katiba!. Niliuliza swali, JK alipoyasamehe yale majizi ya EPA alitumia kifungu gani?. Hivi rais anayo mamlaka kuizuia sheria isichukue mkondo wake?!.

      Katiba inasema rais kwa mashauriano na waziri mkuu atateua mawaziri miongoni mwa wabunge. Mbunge mteule anakuwa mbunge pale tuu baada ya kuapishwa!. Unless hata mbunge mteule ni mbunge kamili hata kabla ya kuapishwa!. What is significance ya kiapo?.

      Uteuzi wa wabunge hao wapya umefanyika kwa mujibu wa katiba ila hao ni wabunge wateule tuu!. Kuwateua wabunge wateule kuwa mawaziri pia ni kwa mujibu wa katiba. Kwa tafsiri yangu, rais hawezi kuwaapisha wateule hao kuwa mawaziri kabla hawajaapishwa kuwa wabunge!. Ubunge ni pre-condition ya uwaziri unless we just put the cart before the horse!.

      Huo nao ni uvunjaji wa katiba!. Kwa jinsi tulivyojaza wanasheria vilaza, hakuna wa kumshauri rais kuwa mbunge mteule si mbunge mpaka ale kiapo!.

      Kama alivyoisamehe ile mijizi ya EPA, hakuna aliemwambia rais kuwa hana mamlaka hayo ya kuizuia sheria kuchukua mkondo wake!. Japo alichukua uamuzi huo kwa kutolikata tawi alilolikalia, kama aliwapenda sana angeacha sheria ichukue mkondo wake halafu kwa mamlaka yake akawasamehe!.

      Mamlaka ya rais ni kusamehe wafungwa sio kuisamehe mijizi kabla haijafikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Ule ulikuwa uvunjaji wa katiba na akiwaapisha wabunge wateule kuwa mawaziri kabla hawajawa wabunge nao ni uvunjaji wa katiba!.

      Pasco.
      Mkuu Pasco,
      Hapo umechemsha au sheria uliyosomea imeanza kuzidiwa na uandishi wa Habari?

      Mbunge ni mbunge tu hata kabla ya kuapishwa na spika na ndio maana hata kifungu 68 wametumia Wabunge wakati wanakuwa hawajaapishwa.

      Ili kushiriki shughuli za bunge Kama mbunge ndio lazima uape kwa spika. Lakini kushiriki shughuli za bunge mbona kuna watu wengi tu wanashiriki ambao sio Wabunge na hawaapishwi? Kwa mfano watendaji mbalimbali ambao wabaitwa bungeni kama vile BOT au Tabesco nk.

      Kwasasa Hawa mawaziri watafanya kazi Kama executives na wanaweza hata wakakutana na kamati za bunge kwa mfano wakati wanapanga budget ila hawawezi kuingia bungeni kuchangia mijadala au kujibu hoja za Wabunge bila kuapa kwanza.
      Pasco and MTAZAMO like this.

    4. #222
      Gibbs's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 49
      Rep Power : 369
      Likes Received
      16
      Likes Given
      9

      Default

      Quote By Kimbunga
      Mkuu Mzee Mwanakijiji na Pasco ilibidi jana nipitie Katiba kwa Makini na kugundua yafuatayao:

      1. Wote tunakubaliana kwamba Waziri ama Naibu Waziri lazima awe Mbunge. Ibara ya 55 (4) inasema "Mawaziri na Manaibu Waziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge"
      2. Kwamba kwa mujibu wa Ibara ya 68 Mbunge anatakiwa kuapa kiapo cha utii
      3. Sasa inakuja Ibara ya 69 (1) yenyewe inasema hivi: "Kila Mbunge atatakiwa, kabla ya kumalizika siku thelathini tangu aapishwe Kushika Madaraka yake kama Mbunge kuwasilisha kwa Spika nakala mbili za tamko rasmi kwamba hajapoteza sifa za uchaguzi kwa mujibu wa masharti ya aya ya (d) ya ibara ndogo ya (2) ya Ibara ya 67." Hiyo bold ni msisitizo wangu.

      Kwa maana hiyo hiyo ibara ya 69 (1) ni kwamba madaraka ya ubunge yanashikwa baada ya kuapishwa, ukiwa hujaapishwa unakuwa huna madaraka ya ubunge!

      Kuna kamchanganyiko hapa.
      Watu tunasahau kitu kinachompa nguvu ktk JMT ni katiba pekee.

      Hadi katiba ikutambue ndio unapata nguvu, isipokutambua basi.

      Ili katiba ikutambue kuwa wewe ni mbunge ni lazima ule kiapo.

      Ili katiba ikutambue kuwa wewe ni waziri lazima uwe mbunge.

      Ili katiba ikutambue lazima uwe na sifa, je wanazo sifaa hizo

      J3 wakila kiapo cha uwaziri kabla ya Ubunge katiba haitowatambua.

      Raisi hayupo juu ya katiba kwani anatakiwa kutekeleza yaliyo katika katiba.

      Akivunja atakuwa amevunja kiapo and that is the serious offence kwa Watanzania.

      Natumai asianze kucheka tu na kulidharau hili. Inabidi aiheshimu ofisi aliyopewa
      Pasco likes this.

    5. #223
      Ronn M's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Location : Moshi~Arusha
      Posts : 1,283
      Rep Power : 611
      Likes Received
      660
      Likes Given
      403

      Default

      Quote By Kiranga
      Endelea kusoma utaona Rais mteule anaweza kuwa rais kamili hata kama hajaapishwa (kwa hali yoyote), kabla ya siku saba. Kitabu chetu hiki kwa kila sheria kinachoitoa, kinatoa sheria nyingine ya kuivunja.

      42.-(1) Rais mteule atashika madaraka ya Rais mapema iwezekanavyo baada ya kutangazwa kwamba amechaguliwa
      kuwa Rais, lakini kwa hali yoyote itabidi ashike madaraka kabla ya kupita siku saba.

      Halafu hapohapo unaambiwa

      (5) Kila Rais mteule na kila mtu atakayeshikilia kiti cha Rais,kabla ya kushika madaraka ya Rais, ataapa mbele ya Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, kiapo cha uaminifu na kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake
      kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge.

      Kwa hali yoyote ina maana rais mteule anaweza kushika madaraka ya urais bila kuapishwa? If so mbona (5) inasema kabla ya mtu kushika madaraka ya urais ataapa mbele ya Jaji?

      Hivi waandishi wa katiba walielewa maana ya "kwa hali yoyote"? Au ndiyo kutafsiri viingereza vya watu?
      Hakuna tatizo kwenye uandishi. Kama nilivyosema mwanzo, kuna provisions ambazo ni more procedural and they dont affect substance. Inawezakutokea circumstances ambazo zimepita 7days na hajala kiapo. Atakuwa raisi kamili. Mfano akaumwa siku ya pili na kukimbizwa nje ya nchi for lets say 30days! Do u think akirudi atakuwa ameupoteza uraisi coz hakuapa?

    6. #224
      Mwanaweja's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th February 2011
      Posts : 3,454
      Rep Power : 1110
      Likes Received
      457
      Likes Given
      929

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      sheria zetu zinahitaji marekebisha mengi sana maana zinakizana sana kwa kifupi zinamapungufu mengi sana ndio maana yanatokea haya

    7. #225
      Ndachuwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th March 2006
      Location : ARUSHA
      Posts : 2,656
      Rep Power : 1211
      Likes Received
      542
      Likes Given
      416

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Ibara ya 55.4. inasema "Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge."

      Na ibara ya 56 inasema "56. Waziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka
      awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia
      kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake
      kitakachowekwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge."

      Je, mbunge akitangazwa na tume ya taifa ya uchaguzi kuwa mbunge na kabla hajaapishwa Bungeni anaweza kuteuliwa kuwa waziri? Je, kuwa waziri si ni sehemu ya mojawapo ya shughuli za Mbunge?
      Kuwa Waziri ni sehemu ya kazi za Kibunge. Rejea kesi ya uchaguzi ya Basil Mramba mwaka 1988 wakati huo akiwa waziri wa Viwanda na Biashara. Basili Mramba alishindwa kwenye kesi ya uchaguzi na alipoteza uwaziri pale pale mahakamani i.e. aliingia mahakamani kusikiliza hukumu ya kesi yake gari likiwa na bendera aliondoka gari bendera ikiwa imeshushwa. Tusiyumbishana Mh. Raisi amevunja katiba ya Jamhuri ya Tanzania, tusubiri Wasomi wa CDM pale ANC leo watasema nini

      "Effective leadership is not about making speeches or being liked; leadership is defined by results not attributes" Peter Drucker

    8. FemaTV & Radio

    9. #226
      jogi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2010
      Posts : 3,985
      Rep Power : 1213
      Likes Received
      972
      Likes Given
      247

      Default

      Quote By Kiranga
      Wale wanaomchagua Spika wana madaraka ya wabunge au hawana?
      wametambuliwa ubunge wao by only one sircumstance, hakuna wa kuwaapisha, lakini panapokuwepo wa kumuapisha mbunge mteule, no way you can fool me, hawi mbunge mpaka aapishwe na ajaze forms za kutokupoteza sifa za kuwa mbunge.
      Mzee Mwanakijiji likes this.

    10. #227
      Ronn M's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Location : Moshi~Arusha
      Posts : 1,283
      Rep Power : 611
      Likes Received
      660
      Likes Given
      403

      Default

      Quote By Ndachuwa
      Kuwa Waziri ni sehemu ya kazi za Kibunge. Rejea kesi ya uchaguzi ya Basil Mramba mwaka 1988 wakati huo akiwa waziri wa Viwanda na Biashara. Basili Mramba alishindwa kwenye kesi ya uchaguzi na alipoteza uwaziri pale pale mahakamani i.e. aliingia mahakamani kusikiliza hukumu ya kesi yake gari likiwa na bendera aliondoka gari bendera ikiwa imeshushwa. Tusiyumbishana Mh. Raisi amevunja katiba ya Jamhuri ya Tanzania, tusubiri Wasomi wa CDM pale ANC leo watasema nini

      With respect hapo nadhani sio sawa! Alipoteza uwaziri coz alipoteza ubunge, a necessary requirement to be a minister. I do see how being a minister is one of parliamentary responsibilities

    11. #228
      satellite's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th November 2010
      Location : HOMELAND SECURITY
      Posts : 546
      Rep Power : 540
      Likes Received
      94
      Likes Given
      60

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Quote By Feedback
      EMT

      Mimi bado nakazia mbunge anaweza kuapishwa sehemu yeyote, labda niambiwe neno 'katika bunge' ni ndani ya ukumbi wa bunge na si ofisini.
      Labda niulize hivi mbunge akiwa kwenye maeneo ya bunge na si ukumbini atahesabika amehudhuria bunge?
      Jibu very simple huwezi kuwa maeneo ya shule/college then useme umehudhuri lecture wakati hukuwepo lecturer room automatically unakua haupo

    12. EMT
      #229
      EMT's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2010
      Location : Mahuta
      Posts : 8,890
      Rep Power : 61724
      Likes Received
      7167
      Likes Given
      6430

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Version ya Kiingereza ya Katiba inaongelea a Member of Parliament na National Assembly. Kuna tofauti kati ya Parliament na National Assembly? Kwa mfano, Ibara ya 68 inasema "Every Member of Parliament shall be required to take and subscribe before the National Assembly the oath of allegiance before commencing to take part in the business of the National Assembly."

      Kwa hiyo, madhumuni ya kiapo ni kumwezesha tuu a Member of Parliament kushiriki kwenye shughuli za National Assembly? Kwa maana nyingine, Mbunge anaweza kuwa a Member of Parliament hata kama hajaapishwa? Kwa maana hiyo basi a Member of Parliament anaweza pia kuteuliwa kuwa na waziri hata kabla hajaapishwa? Ibara ya 55(4) inasema "All Ministers and Deputy Ministers shall be appointed from among Members of Parliament."
      Pasco likes this.
      “Wanaotaka kuhashua wanatoa rushwa. Wanaotaka kuhashukwa nao wanataka rushwa. Hahashukwi mtu bila rushwa, na mtu hahashui bila rushwa na hapo ndipo tatizo lilipo.” - Mie mwenyewe.

    13. #230
      Kobello's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th February 2011
      Posts : 2,946
      Rep Power : 1659
      Likes Received
      1107
      Likes Given
      191

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Quote By Ndachuwa
      Kuwa Waziri ni sehemu ya kazi za Kibunge. Rejea kesi ya uchaguzi ya Basil Mramba mwaka 1988 wakati huo akiwa waziri wa Viwanda na Biashara. Basili Mramba alishindwa kwenye kesi ya uchaguzi na alipoteza uwaziri pale pale mahakamani i.e. aliingia mahakamani kusikiliza hukumu ya kesi yake gari likiwa na bendera aliondoka gari bendera ikiwa imeshushwa. Tusiyumbishana Mh. Raisi amevunja katiba ya Jamhuri ya Tanzania, tusubiri Wasomi wa CDM pale ANC leo watasema nini

      CDM viongozi wao ni wapotoshaji wakubwa wa sheria. Kinachosikitisha zaidi, CCM sometimes they fall for it!
      Kitakuwa kichekesho kama watazungumzia hili.
      Keeping quiet is a war crime.

    14. #231
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,499
      Rep Power : 46709
      Likes Received
      16347
      Likes Given
      8418

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Quote By Kiranga
      Wale wanaomchagua Spika wana madaraka ya wabunge au hawana?
      hawana madaraka ya wabunge kabla ya kuapishwa; wanaruhusiwa jambo moja kufanya kabla ya kushika madaraka hayo; kupiga kura ya kuchagua spika.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    15. #232
      JamboJema's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 14th June 2011
      Location : Mwanza
      Posts : 742
      Rep Power : 550
      Likes Received
      75
      Likes Given
      216

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Mkanganyiko wote huu bado rais wetu anayo furaha tu kuendelea na jambo hili kama anavyolipeleka! Ikitokea 'Mtikila' fulani akatokea na kulihoji hili mahakamani na mahakama ikasema kilichofanyika sicho, watu wataficha wapi nyuso? Na yale watakayokuwa 'wameyatenda' hawa 'mawaziri' kwa capacity yao ya uwaziri yatakuwa batili?
      Nchi hii kweli wakati mwingine inabidi usiwe ukifikiri ili uishi kwa raha. Katiba ingeongoza kuwa kwenye mkanganyiko kama huu 'mahakama' -kama mtafsiri wa sheria, ihusike kutoa tafsiri kabla ya hatua kuanza kuchukuliwa.
      Just THINKING ALOUD!
      Uchakavu wa Mahakama si nafuu ya hukumu!

    16. #233
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,477
      Rep Power : 6168
      Likes Received
      3045
      Likes Given
      1017

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Mkuu MpigaKelele hizo ni changamoto za kikatiba. Tunajaribu kuzichambua. Wametumia Ibara ya 68 lakini Ibara ya 69 inatuingiza kwenye utata. Mwanzoni niliamini kuwa iko sawa kwa kurejea ibara ya 68 lakini baadaye nikajishughulisha na kuigundua hiyo ibara ya 69 nikapata changamoto hiyo. Tunajitahidi kuonyesha changamoto hizi ili tupate tafasri ya kisheria.

      Mkuu pia nimegundua kwamba kiswahili chetu nacho kina tabu kidogo. Kama alivyosema EMT kwa mfano neno parliament (spika na wabunge) na National Assembly (bunge na Rais) sisi yote kwa kiswahili tunasema ni bunge hatuyatenganishi.
      CCM na CDM vyote ni vyama vya siasa vinavyoongozwa na wanasiasa; tofauti yao kubwa ni moja kwamba kimoja kina dola kingine kinataka kushika dola.

    17. #234
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,130
      Rep Power : 41571
      Likes Received
      6037
      Likes Given
      1054

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      hawana madaraka ya wabunge kabla ya kuapishwa; wanaruhusiwa jambo moja kufanya kabla ya kushika madaraka hayo; kupiga kura ya kuchagua spika.
      Kwa hiyo wanamchagua Spika kwa madaraka gani?
      Banda lishavunjika, jogoo kaondoka. Vifaranga hangaika, kumtoa nyoka.


    18. #235
      Njaare's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2010
      Posts : 568
      Rep Power : 660
      Likes Received
      92
      Likes Given
      167

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Quote By Kimbunga
      Mkuu EMT wenzio tangia juzi tumelifanyia kazi hilo suala na tukapata jawabu. Anaweza akashika uwaziri bila kuapishwa ila.hawezi kushiriki shughuli za bunge kabla ya kuapishwa. hiyo wataapishwa june kabla ya kuanza sughuli za bunge
      Mkuu mimi naona bado hii ibara haitoshelezi. Hawa ni wabunge wateule. Katiba inamtaka rais ateue miongoni mwa wabunge. Kisheria kuna tofauti kati ya mbunge na mbunge mteule. Kumbuka juzi swali la mbunge mteule Pareso liliondolewa. Kabla ya Bunge kuna vikao vya kamati na waziri atatakiwa kuhudhuria na kujibu au kutolea maelezo baadhi ya mambo. Au tunaomba maana ya shughuli za kibunge.

    19. #236
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,499
      Rep Power : 46709
      Likes Received
      16347
      Likes Given
      8418

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Quote By Kiranga
      Kwa hiyo wanamchagua Spika kwa madaraka gani?
      kuwa wabunge wateule na hicho ndicho pekee wanachoweza kufanya. Katiba inawaruhusu kufanya jambo moja tu kabla ya kuapishwa - kumchagua Spika kwanza.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    20. #237
      Njaare's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2010
      Posts : 568
      Rep Power : 660
      Likes Received
      92
      Likes Given
      167

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Quote By Mtanzania
      Mkuu Pasco,
      Hapo umechemsha au sheria uliyosomea imeanza kuzidiwa na uandishi wa Habari?

      Mbunge ni mbunge tu hata kabla ya kuapishwa na spika na ndio maana hata kifungu 68 wametumia Wabunge wakati wanakuwa hawajaapishwa.

      Ili kushiriki shughuli za bunge Kama mbunge ndio lazima uape kwa spika. Lakini kushiriki shughuli za bunge mbona kuna watu wengi tu wanashiriki ambao sio Wabunge na hawaapishwi? Kwa mfano watendaji mbalimbali ambao wabaitwa bungeni kama vile BOT au Tabesco nk.

      Kwasasa Hawa mawaziri watafanya kazi Kama executives na wanaweza hata wakakutana na kamati za bunge kwa mfano wakati wanapanga budget ila hawawezi kuingia bungeni kuchangia mijadala au kujibu hoja za Wabunge bila kuapa kwanza.
      Mh! Haikosi wewe ndo mshauri wa JK

    21. #238
      Anheuser's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2011
      Posts : 1,295
      Rep Power : 672
      Likes Received
      335
      Likes Given
      135

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Quote By Kiranga
      Ibara ya 68 haimuiti mtu aliyechaguliwa/teuliwa kuwa mbunge "mbunge mteule" inamwita "mbunge".
      Ibara hiyo isingeweza kusema "mbunge mteule" kwa vile si wabunge wote huteuliwa.


      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Jibu langu mimi ni hapana! Unless kama kuna precedence ambayo watu wanaweza kutukumbusha
      Kama jambo ni kosa "unless lina precedence" basi siku ilipotokea hiyo "precedence" kabla yake kulikuwa hakuna "precedence" kwa hivyo lilikuwa kosa na kurudia kosa lenye "precedence" hakubariki kosa kuwa si kosa kwa sababu ni kosa kubwa zaidi kurudia kosa.

    22. FJM
      #239
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,170
      Rep Power : 2568
      Likes Received
      5318
      Likes Given
      4585

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Quote By Mtanzania
      Mkuu Pasco,
      Hapo umechemsha au sheria uliyosomea imeanza kuzidiwa na uandishi wa Habari?

      Mbunge ni mbunge tu hata kabla ya kuapishwa na spika na ndio maana hata kifungu 68 wametumia Wabunge wakati wanakuwa hawajaapishwa.

      Ili kushiriki shughuli za bunge Kama mbunge ndio lazima uape kwa spika. Lakini kushiriki shughuli za bunge mbona kuna watu wengi tu wanashiriki ambao sio Wabunge na hawaapishwi? Kwa mfano watendaji mbalimbali ambao wabaitwa bungeni kama vile BOT au Tabesco nk.

      Kwasasa Hawa mawaziri watafanya kazi Kama executives na wanaweza hata wakakutana na kamati za bunge kwa mfano wakati wanapanga budget ila hawawezi kuingia bungeni kuchangia mijadala au kujibu hoja za Wabunge bila kuapa kwanza.
      Mtanzania, naona unatafsiri vibaya maana ya maneno 'kushiriki shughuli za bunge'. Wabunge are 'legislatures, wanatunga sheria na ndio sababu miswaada yote lazime ipite bungeni.

      Sijawahi kusikia governor wa bank kuu, au mkurugenzi mkuu wa Tanesco akishiriki kupitisha muswada bungeni? Wanaweza kuwa kwenye jengo au hata kukaa kwenye sehemu ya wageni lakini hawawezi kushiriki kupitisha miswada! Na kama kuna jambo wabunge wanataka kupata ufafanuzi au semina toka kwa governor au mtu wa Tanesco, basi watafanya hivyo NJE YA UKUMBI unaotumiwa kujadili mambo ya kibunge. Mtu yoyote ambaye si mbunge hawezi kuhudhuria bunge hadi pale kipengele husika kitakapotenguliwa. Tofautisha 'lobby area' na bunge' .

      Sasa tukirudi kwenye ubunge wenyewe, kuna mbunge mteule na baada ya kuapa anakuwa mbunge kamili. Mbunge mteule hawezi kushiriki shughuli zozote za kibunge kabla y kula kiapo. Na ndio maana kwa mfano Mh Cecilia Pareso alipowasilisha maswali yake bungeni (mwezi mmoja baada ya kuteuliwa kuwa mbunge) swali lake liliondelewa kwa sababu wakati anawasilisha bado alikuwa mbunge mteule (alikuwa hajala kiapo).

      How about Mawaziri
      Kwa katiba ya sasa mawaziri na naibu mawaziri lazima watokane na wabunge. Kumbuka mawiziri na manaibu (kwa katiba ya sasa) nao wanashiriki shughuli za bunge kama legislatures na pia kama executive. Sasa kama bado ni mbunge mteule utashiriki vipi shughuli za bunge? Utajibu swali la kama nani? utapeleka muswada kama nani? (ref mfano wa Mh Cecilia Pareso aliyokataliwa kuuliza swali kwa sababu alikuwa bado hujala kiapo).

      Kama tutatumia katiba kikamilifu basi mawaziri hawa watatu hawawezi kupeleka muswada, kujibu maswali bungeni mwezi ujao hadi pale watakapokula kiapo.

      Kwa kifupi ninachoona hapa ni kwamba nchi imekuwa inaendeshwa kwa mazoea, sheria/katiba ya nchi imekuwa compromised so many times. Pengine huko nyuma watu walikuwa hawaulizi na hivyo wakubwa wakajiozesha 'kuzuka'.
      Na ninashangaa sana Mwanasheria Mkuu anafanya nini? Kuna mlolongo wa madudu mengo kisheria utadhani hatuna mwanasheria huko serikalini! Ni aibu tunajadiili mambo so basic kwenye katiba wakati kuna office ya mwanasheria mkuu. Aibu.

    23. #240
      Joss's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2009
      Posts : 715
      Rep Power : 651
      Likes Received
      126
      Likes Given
      121

      Default Re: Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

      Katika katiba mpya inabidi tubadili utaratibu, waziri asiwe mbunge, hii itaondoa mgongano wa kiutendaji na kimamlaka kati ya bunge na serikali.

    Page 12 of 14 FirstFirst ... 21011121314 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...