Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea
Leo inangojewa kwa hamu kwa CCM na CDM kwani mpaka sasa ktk kesi za kupinga ubunge CCM ineshinda mechi za Arusha (Lema) pekee na wamepigwa chini Sumbawanga, Bihalamuro na Singida na leo inaelekea CDM kuendeleza ushindi. Wakati huohuo Ubungo na Igunga zangojewa. Ifahamike wizara ya sheria imezitaka mahakama kumaliza kesi zote tarehe 4/5/2012
Naelekea mahakamani kwa Updates zote. Kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili haijalishi
FINALLY: Makongoro Mahanga kashinda kesi!
By SEBM
Wanabodi,
Hukumu hii inatarajiwa kuanza kusomwa muda wa saa 4 kamili asubuhi ya leo.Pamoja na madai mbalimbali yaliyowasilishwa na mdai akiwakilishwa na wakili Peter P. Kibatala wa Trustmark Attoneys, hapa chini nibaadhi ya hoja za upande wa mlalamikaji:
1. Msimamizi Wa Uchaguzi alitangaza matokeo pasipo kujumuisha vituo 120 vya Kiwalani, 129 Vingunguti, 4 buguruni, 2, Tabata na 4 Kipawa
2. Vituo tajwa hapo juu, havikufanya mahesabu na majumuisho ya uhesabu wa kura (Fomu 21B)
3. Fomu ya kurekodi matokeo (21B) hazikusambazwa katika baadhi ya vituo na hivyo kuwafanya wahusika kuweka matokeo kwa kutumia karatasi za kawaida(plain papers) ambazo ni rahisi kufanyiwa forgery na ubaya wowote.
4. Afisa Mtendaji Kata ya Tabata - Imelda Kafanabo – alikamatwa na fomu batili zenye matokeo yasiyo halali (ushahidi wa video uliambatanishwa)
5. Mwananchi mwingine alikamatwa Anatoglu akiwa na fomu na mihuri isivyo halali ikiwa imempa(video iliambatanishwa ikimwonyesha mtuhumiwa akikamatwa)
6. Maboksi ya kuhesabia kura kutoka Kata ya Buguruni yenye namba 15134, 151305, 151083, 15144, 15109, 15129, 151302 yalikuwatwa yakiwa wazi, hayana lakiri.
7. Mdai akiwa na wagombea wenzake wa Civic United Front (CUF) na Sauti ya Umma (SAU) walitoa malalamiko ya mdomo kuhusu kukosekana kwa kura kutoka kata za Vingunguti, Buguruni na Kiwalani. Pamoja na mapungufu hayo, Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza matokeo kwa kusema kwamba “ameamriwa kutangaza matokeo mpaka kufikia saa 8 mchana siku ya tarehe 03/11/2010” na aliwakataliwa wadai fursa ya kuweka madai yao kwa maandishi.
8. Mahesabu ya kura kutoka katika vituo yalionyesha Mpendazoe kupata kura 56,962 na Mahanga 44,904.
Mdai ameomba yafuatayo: (1) Matokeo yaliyotangazwa na kumpa Ushindi Milton Makongoro Mahanga yatambulikane kuwa ni batili(null and void)
(2) Mahakama itangaze uchaguzi wazi, huru na wa haki kwa jimbo la Segerea ufanyike
(3) Au vinginevyo, bila kuathiri mambo yoyote, Mahakama imtangaze Fred Mpendazoe kama mbunge halali wa jimbo la Segerea
(4) Haki yeyote ambayo mahakama itaona inafaa kumpa Mdai
(5) Gharama za Kesi
UPDATES:
By carmel
Chadema nao wamepiga kambi hapa mahakamani na magwanda yao kama kawa...
By Nyauba
Mahakamani ulinzi umeimarishwa sana. Nipo eneo la tukio nje na kwa kweli hakuna speaker kusikia kinachoendelea. Ila raia wamejitokeza kwa wingi na skafu za cdm zipo..
1. Bado kesi haijaanza
2. Hakuna speakers zilizowekwa nje kitu kinachopelekea kujua kinachoendelea ndani, walio ndani simu zimezimwa!
By emmanuel1976
Jaji Profesa Ibrahim Juma ameshaanza kusoma hukumu kama ilivyotarajiwa na watu wengi wamezuiwa nje ya ukumbi wa mahakama
re: Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea
By Bondpost
Take it easy ndugu, judge Prof. Ibrahim Juma ni kichwa sana, namfahamu toka akiwa UDSM pale akiwa lecturers mpaka kuwa Dean wa faculty of law, ni mtu safi na mpenda maadili na hana kashfa za kitoto. Ninaimani na lolote atakaloona linafaa katika hukumu hiyo. Leo kila upande utegemee lolote na kukubali kitakachesemwa na mahakama, either cdm au ccm la muhimu ni kuwa tayari kukubali.
NAKUBALIANA NAWE, HUYU NI KTK MAJAJI BORA AMBAO NDG. RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEPATIA BEYOND DOUBTS KUWA WELEDI NDIO UMEMFIKISHA HAPO.....NI VILE TU PROF NI Jr. KTK JUDICIARY SYSTEM YETU LAKINI NAAMINI HUYU NI JAJI KIONGOZI TARAJIWA NA PIA HUYU NDIE MRITHI SAHIHI WA OTHMAN CHANDE NA MWINGINE NI COMRADE BOB MAKARAMBA , NAMKUBALI SANA HUYU MTU......KWA WELEDI NA KUHESHIMU MIZANIA YA KISHERIA.
WITO WANGU KTK KESI HII HAKUNA MSHINDI BALI HAKI IATASHINDA NA NAWAMBIA MLALAMIKAJI/MLALAMIKIWA ASITOKEE MTU KUIPINGA HAKI ITAMUADHIRI KULE COURT OF APPEAL.
"SAFARI YA MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI BADO NI NDEFU NA YENYE VIKWAZO LUKUKI"-1995-2005 RAIS B.W. MKAPA
re: Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea
By Mkwanda
Duh!sikutegemea kua dar leo ingegeuka na kua biharamlo.mtu kaanzisha thread saa 12 alfajiri halaf kapiga kimya.
Hili jambo siyo fair kabisa. Kama unataka kuanzisha uzi halafu unalala mpaka sasa mbili unategemea uende mahakamani ukalete update ni lazima ukute nafasi hakuna.'
Kwa kweli nashangaa hata akina Mutuzi sijui le baharia hamna kitu.
Hakika biashara kichaa zipo nyingi sana, lakini biashara kichaa kubwa kuliko zote ni kupenda usipopendwa, haijalishi hata kama ni mkeo!!!!!
re: Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea
By Ciril
Hii tabia ya kuzuia raia kusikiliza kesi polisi wameitoa wapi?
Kama wamezuiwa basi tumekwisha....maana hata ya lema walizuiwa akagombana nao baadae wakaruhusiwa lakini wakawekwa mitaka kami mia kutoka chumba ambako kesi ilikuwa inasomewa....
Nobody can give you freedom. Nobody can give you equality or justice or anything. If you're a man, you take it.... Malcolm X Nasubiri 'breaking news... '
Hata mimi nashangaa. Yule jamaa aliyekuwa kule mahakamni singida kumbe alifanya kazi nzuri sana pamoja na wenzake. Manake alikuwa akileta jinsi hoja zilivyokuwa zikipanguliwa lkn leo naona watu wanaanza mambo mengine. Afadhali ningebaki pale nje ya mahakama nikawa napata tetesi.
re: Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea
By PrN-kazi
tukiachana na maswala ya uswahiba na tuhuma za uchakachuaji: Mahanga kiutendaji yeye kama Naibu Waziri wa Kazi yuko vizuri na hakika anapiga mzigo; kwahiyo kuendelea kuwemo kwenye orodha ya Baraza la Mawaziri si jambo la kushangaza.
Tulipata updates za hukumu za mikoani lakini hapa Dar hatupati kitu. Ni uoga au?
Tatizo la watu wengi wa Dsm nguvu Yao ipo kwenye midomo tu lakini utendaji ni ziro,sio wajasiri kabisa.Arusha katika kesi ya Lema waliwazuia wananchi kuingia mahakamani lakini walishindwa na palizuka ugomvi mkali watu/raia walikuwa wakiusukuma ukuta udondoke watu waingie ndani,polisi kuona hivyo wakalegea na kufungua geti wenyewe sababu mziki wetu huku Arusha wananujua.Polisi walishafanya hivi mara kibao katika muendelezo wa kesi ya Lema lakini raia walikuwa majasiri sana.
re: Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea
vipi bado tu?
“Ndg wananchi ubunge siyo utendaji, ni uwakilishi tu ndio maana unaweza kukaa bungeni muda wote wewe ni kusinzia tu,”. S.Wassira,7/10/2010 ktk kampeni,Bunda.
re: Makongoro Mahanga ashinda kesi ya uchaguzi jimbo la Segerea
By tuko
bora hata ile ya biharamulo... Kumbe mijitu ya dar fakrandi kabisa, ujanja mdomoni tu...
mkuu hapa ndipo dsm, ndio ikulu, ndio hq ya mahakama tanzania, ndio makao makuuu ya polisi,uwt,magereza,mgambo kwa hiyo unategemea waache heshima ya mahakama ichezewe na twit family,fbfamily na jamiiforum? Hapana, hapana, hapana......siasa majukwaani si mahakamani, acha tusubiri yatajulikana punde
"SAFARI YA MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI BADO NI NDEFU NA YENYE VIKWAZO LUKUKI"-1995-2005 RAIS B.W. MKAPA
Follow Us Here