JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Majina ya wauza Madawa ya Kulevya: Kikwete anayo!

  Report Post
  Page 4 of 21 FirstFirst ... 23456 14 ... LastLast
  Results 61 to 80 of 407
  1. #1
   Mlalahoi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st August 2006
   Location : London, UK
   Posts : 2,069
   Rep Power : 1605
   Likes Received
   327
   Likes Given
   176

   Default Majina ya wauza Madawa ya Kulevya: Kikwete anayo!

   Vigogo dawa za kulevya watajwa

   Written by Mwananchi
   Monday, 18 September 2006

   *Majina yao yapelekwa kwa Rais Kikwete
   *Ni orodha ndefu ya majina ya watu 58
   *Wamo wafanyabishara, wanasiasa, viongozi wa dini
   *Mbinu wanazotumia nazo zaanikwa hadharani

   WITO wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka wananchi wajitokeze kutaja majina ya wahalifu nchini, umepata mwitikio mpya, safari hii watu kadhaa wakijitokeza kutaja majina ya vigogo wanaoongoza kwa biashara ya dawa za kulevya nchini.

   Majina hayo yako katika barua iliyoandikwa na wananchi 15 kwenda kwa Rais Kikwete, ambamo wanadai kwamba walikuwa wakitumiwa na vigogo hao kufanya biashara
   hiyo, lakini sasa wameamua kuachana nayo. Barua hiyo iliandikwa Septemba 8, mwaka huu na wahusika wanadai wamekwisha kuiwasilisha Ikulu.

   Kwa mujibu wa barua hiyo, majina 58 yameorodheshwa yakiwa katika makundi matatu makubwa, la kwanza likiwa ni waagizaji wakubwa wa dawa hizo; la pili ni
   wafadhili ambao majina yao hutumika kusafirisha dawa hizo; na la tatu ni wauzaji walioko Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.

   Katika orodha ya waandishi wa barua hiyo wanaodai kusukumwa na uzalendo na uchungu kwa nchi yao, yamo majina ya wafanyabiashara maarufu nchini na wanasiasa,
   wakuu wa taasisi nyeti, baadhi ya viongozi wa dini na maafisa wa juu serikalini.

   Kundi la kwanza lina majina 12, miongoni mwao ni wafanyabiashara maarufu katika miji ya Dar es Salaam, Morogoro, Zanzibar, Arusha na Bagamoyo na baadhi ya
   viongozi wa dini wa madhehebu fulani.

   Kundi hili linadaiwa kuwa linaingiza dawa za kulevya kwa njia mbalimbali zikiwamo, kutumia mipira ya kondomu, majokofu, vifaa vya hospitali, meli na
   marobota ya mitumba.

   Katika kundi la pili kuna watu 19, miongoni mwao wamo wanasiasa wakubwa nchini wakiongoza kundi hili, kutoka taasisi ya fedha nchini na wafanyabiashara maarufu wa
   Dar es Salaam na Zanzibar.

   Kundi la tatu lina majina 27, ambao si ya watu wenye majina makubwa, lakini ndio wanaotumika kusambaza mitaani kwa watumiaji wa dawa za kulevya.


   Mbali ya kushiriki katika kusambaza dawa za kulevya, kundi hili pia lina baadhi ya majina ya watu waliotajwa kushiriki katika kuingiza silaha nzito
   zinazotumika kwa ajili ya ujambazi kutoka nchi jirani.

   Ufukwe wa Pwani ya Bahari ya Hindi eneo la Muhoro wilayani Rufiji inaelezwa kuwa linatumika kuingizia silaha hizo kutoka nchi jirani pamoja na dawa za
   kulevya chini ya ufadhili wa mmoja wa wanasiasa nchini.

   Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere unatajwa kuwa unatumiwa na watu hawa kuingiza dawa hizo nchini kutokea nchi za nje, huku baadhi ya maafisa wa polisi
   watatu wakitajwa kuwa ndio wanaotoa ulinzi kwa watu wanaopitisha dawa hizo.

   Nyumba ya afisa wa juu mstaafu katika idara nyeti iliyopo jijini Dar es Salaam inatajwa kuwa inatumika katika kuhifadhi vijana wanaoingiza dawa za kulevya
   nchini, huku nyumba ya mfanyabiashara mmoja iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ikitajwa kuwa ndiyo inayotumika kama kituo cha kutolea pipi tumboni kwa vijana wanaotumika kuingiza dawa hizo kutoka nje ya nchi.

   Vile vile, katika kundi hili mwanamke mmoja anayefanya kazi katika taasisi moja ya fedha anatajwa kuwa anashiriki katika kuhujumu uchumi wa nchi kwa
   kusafirisha kwenda nje fedha nyingi za kigeni akitumiwa na mfanyabiashara mmoja maarufu wa dawa za kulevya nchini.

   Mipaka ya Tunduma mkoani Mbeya, Horohoro mkoani Kilimanjaro na Namanga mkoani Arusha, nayo imetajwa kuwa inatumika kupitisha dawa za kulevya kwa kutumia
   mabasi na magari mengine. Kuna kampuni mbili za mabasi nchini zinazotajwa kuongoza kutumika katika usafirishaji.

   Barua hiyo ya kurasa 10, pia inamtaja mwanamke mmoja ambaye anatumika kupitisha dawa za kulevya uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kuwa ni sugu; aliwahi
   kuhukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya, lakini hivi sasa yupo mitaani kifungo chake akitumikia mtu mwingine.

   Alipoulizwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philip Marmo, alisema hajapata barua hiyo na kwamba atalizungumzia
   baada ya kuipata.

   Naye Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, alisema hana taarifa za kuwako kwa barua hiyo. Hata hivyo, alisema kuna tume ya dawa za kulevya iliyopo
   chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo inayoshughulikia zaidi suala hilo.

   Alisema Jeshi la Polisi linafanya kazi za kukamata watu wanaojihusisha na dawa hizo na kwamba mikakati mingine ya kupambana na watumiaji inafanywa na tume
   hiyo.

   Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Polisi liongezewe uwezo wa kupambana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha vituo vya kazi askari
   waliokaa kituo kimoja kwa muda mrefu.

   Pia alilitaka Jeshi hilo lijisafishwe lenyewe kutokana na madai kwamba polisi wanahusika na baadhi ya matukio ya uhalifu nchini.


   Rais alitoa wito kwa wananchi wenye taarifa zozote za uhalifu, na wanaojua waliko majambazi wazipeleke taarifa hizo kwake kama wanaogopa kuzipeleka polisi.


   Katika kuitikia wito huo, wananchi kadhaa waliandika barua iliyooroshesha majina ya polisi 20, wakiwamo baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa na kuikabidhi kwa Waziri wa Usalama wa Rais, Bakari Mwapachu.

   Tangu wakati huo, mabadiliko makubwa yameshuhudiwa yakifanywa kwenye jeshi hilo, hata hivyo hii ni mara ya kwanza kwa watu kujitolea kuandika barua yenye
   majina na maelezo ya kina kama hii kuhusu biashara ya kulevya na kuipeleka kwa Rais.


  2. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,981
   Rep Power : 1755
   Likes Received
   32
   Likes Given
   0

   Default

   sidhani kama nitakuwa nimekosea nikisema f**k the government kwa upuuzi wote huo !!

  3. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,981
   Rep Power : 1755
   Likes Received
   32
   Likes Given
   0

   Default

   mimi leo nimeamka na vision, na nadhani bado nitaendelea kuifanyia kazi maana ilikuwa ni part ndogo kuhusu kifo cha amina, vision yenyewe ilikuwa hivi :
   Katika kikao cha hao wazee wa dawa za kulevya, walikaa kama kikao, na kwa kuwa kwa njia moja ama nyingine MEDI alikuwa amekiuka mambo yao ya siri, na mke wake ( amina ) alichochea vita dhidi yao na kutishia usalama wa hao mijemba. kwa kuwa MEDI alikiuka, ilibidi mmoja wao aondoke ( kati ya amina na medi ) na kwa kuwa medi alikuwa katika hayo mazungumzo, ilibidi acollaborate nao, ndio mikakati ikapangwa. NINA STRONG FEELING KWAMBA HIKI KIFO CHAKE KIMETOKANA NA MAMBO MAWILI, MOJA NA LA KIPAUMBELE SANA NI MADAWA YA KULEVYA KITU AMBACHO MEDI ILIBIDI AONDOKE YEYE LAKINI AKAMTENGENEZA MKEWE, BILA YA KUJALI WATOTO WAKE NA FAMILIA YAKE. na ya pili ndio hiyo hiyo sema tu nchimbi nae amekuwa katika consideration kubwa ya kumuondoa amina.

  4. Mwawado's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2006
   Location : Tulsa, Oklahoma/MFA-TZ
   Posts : 1,286
   Rep Power : 1035
   Likes Received
   162
   Likes Given
   339

   Default

   Kama ulivyosema Mheshimiwa Kada Mpinzani,

   Ni kweli sababu kubwa ilimuondoa Dada yetu Amina ni hii vita ya Madawa ya kulevya.Hakuna asiyejua kuwa MEDI nae alikuwa mmoja wa wafanya Biashara hiyo haramu (Nenda kaulize Sinza),sasa Amina aliposema kuwa anawajua wauza Unga kila mtu alishangaa,inaweza kuwa yalikuwa Majadiliano na huyo Medi,ili kumpa Umaarufu Amina!,au kutoa njia nyeupe kwa Medi ya kufanya Biashara hiyo bila Uoga kwa sababu Tu,Mkewe ametamka hadharani, na kwa maana hiyo kila Mdanganyika ataamini kuwa MEDI ameacha Biashara!

   Mimi binafsi nailaumu Srikali kwa sababu JK anayo majina ya Wauza unga wote!Hawa watu wanajuana kwani Biashara hii ni siri lakini ina Chain yake kubwa,wote wanajua kama wajuanavyo malaya au wavuta Bangi!.JK ameogopa kwa sababu Biashara hii ni kubwa kuliko tunavyodhania,ipo kutoka Ikulu mpaka kule TANDIKA.Wale wasiotaka Unafiki watakubaliana nami kuwa kuna Viongozi wakuu wa nchi walishawahi kujihusisha na biashara hii,kama sio wao binafsi basi ni mmoja ktk familia yao.Mkumbukeni Marehemu Diria na kasheshe la Uwanja wa ndege,Nenda kauliza ktk vijiwe vya Hamburg au Bonn kila mtu anamkumbuka Diplomat yule.

   Kuna wakati nilitumwa Russia kikazi na huko Moscow kulikuwa na kesi ya kijana wa kitanzania aliyeshikwa na madawa ya kulevya,adhabu ya kosa hilo huko ni kifo!,kwa kupitia Ubalozi Kijana huyo alitafutiwa dhamana na kupewa Passport ya hadhi ya kibalozi ya Angola na kukimbilia Switzerland (Ni mtoto wa kigogo).Waliomsaidia kufanya hivyo hivi sasa wana Madaraka makubwa Serikalini,wapo Ikulu na wengine Jeshini,sasa hamuwezi kuniambia kuwa JK anatoa majina ya wauza Unga hadharani NO!Hili nakataa! anafahamu madhara ya Huo unga kwani hata kwenye Familia yake anao waathirika,lakini hawezi kuthubutu kuwataja Hadharani kwani ni Miongoni mwao.

   Tuendelee tu kuwa wazi kila kitu kitajulikana hapa!Amina Wamemuua!Hakuna lolote linaloweza kufichwa kufutia kifo chake,ni kweli kwamba kama binadamu alikuwa na udhaifu,sasa wametumia udhaifu huo kumtafutia Ugomvi na mumewe na baadaye kumuondoa,ni ngumu kwa mtu mwenye Akili Timamu kuamini kwamba Amina amekufa kwa Matakwa ya M/Mungu,Ndio maana nami nakubaliana na Uchunguzi huru wa Kifo hiki!

  5. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,981
   Rep Power : 1755
   Likes Received
   32
   Likes Given
   0

   Default

   sasa mshaanza kuogopa kuchangia kuhusu hawa jamaa wauza unga au ? au wapo wengine humu humu JF ? tuambiane, tusije tukaja kufuatwa na sisi !

  6. Ogah's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2006
   Posts : 6,565
   Rep Power : 22247
   Likes Received
   1386
   Likes Given
   6173

   Default

   Duhh Mzee Mwawado,

   Hali inatisha, watu wapo Ikulu mpaka Jeshini!!!!!!!, kwa hiyo shughuli pevu hii


  7. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,981
   Rep Power : 1755
   Likes Received
   32
   Likes Given
   0

   Default

   duh ! kama hadi jeshini basi mie simo, kwani hatuwezi kuuvunja kwa kutumia ideology jamani ???????????????

  8. Mwawado's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2006
   Location : Tulsa, Oklahoma/MFA-TZ
   Posts : 1,286
   Rep Power : 1035
   Likes Received
   162
   Likes Given
   339

   Default

   Ndugu zanguni Tuwe wakweli sasa,na Tuache Uoga usiokuwa na maana,kama mtu ana datas hapa ndio mahali pake,imefika wakati sasa Uchi uitwe kwa jina lake na tuache majina ya kupamba kama Uuume au Uke!.Sipendi kuandika lugha mbaya hiyo, lakini naona wakati mwingine Lugha kali ndio inaeleweka kuliko huu Upole wa Unafiki!.

   Hivi inakuwaje JK anakaa kimya na majina alopewa toka Desemba/06.Kwa madai yake anasema akina Hosea watashughulikia,Hivi huyu Hosea ana shughuli ngapi?Kuna masuala ya Uizi-pevu unaohitaji Elimu kubwa kubaini uizi umefanywaje,huko BOT,TRA na Mawizarani hayo nakubali tumuachie Hosea,lakini hata suala hili ambalo majina tayari mnayo!Sijui tunajenga jamii ya namna gani.

   Ogah,
   Nikirudi kwenye Issue ya Moscow,Ni kweli kwamba Embassy yetu ilimtorosha kijana anayeitwa Eddy Kapera(sina uhakika kama ni jina lake halisi),Kijana huyu alikuwa na Uhusiano wa karibu na Chabaka Kilumanga(He was 1st secretary then) na wakati Mwingine alikuwa anaishi kwa General Idd Gahhu (He was Military Attachee),Sio siri kwa wale walikokuwa Lumumba University Moscow mwaka 1996/97 watakumbuka tukio hilo.

  9. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,981
   Rep Power : 1755
   Likes Received
   32
   Likes Given
   0

   Default

   hivyo baada ya invizibo kutoa hayo, mchelze unaweza kumwagwa !

  10. Icadon's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st March 2007
   Location : I'm Everywhere!
   Posts : 4,085
   Rep Power : 1982
   Likes Received
   76
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By Mwawado View Post
   Kama ulivyosema Mheshimiwa Kada Mpinzani,

   Ni kweli sababu kubwa ilimuondoa Dada yetu Amina ni hii vita ya Madawa ya kulevya.Hakuna asiyejua kuwa MEDI nae alikuwa mmoja wa wafanya Biashara hiyo haramu (Nenda kaulize Sinza),sasa Amina aliposema kuwa anawajua wauza Unga kila mtu alishangaa,inaweza kuwa yalikuwa Majadiliano na huyo Medi,ili kumpa Umaarufu Amina!,au kutoa njia nyeupe kwa Medi ya kufanya Biashara hiyo bila Uoga kwa sababu Tu,Mkewe ametamka hadharani, na kwa maana hiyo kila Mdanganyika ataamini kuwa MEDI ameacha Biashara!

   Mimi binafsi nailaumu Srikali kwa sababu JK anayo majina ya Wauza unga wote!Hawa watu wanajuana kwani Biashara hii ni siri lakini ina Chain yake kubwa,wote wanajua kama wajuanavyo malaya au wavuta Bangi!.JK ameogopa kwa sababu Biashara hii ni kubwa kuliko tunavyodhania,ipo kutoka Ikulu mpaka kule TANDIKA.Wale wasiotaka Unafiki watakubaliana nami kuwa kuna Viongozi wakuu wa nchi walishawahi kujihusisha na biashara hii,kama sio wao binafsi basi ni mmoja ktk familia yao.Mkumbukeni Marehemu Diria na kasheshe la Uwanja wa ndege,Nenda kauliza ktk vijiwe vya Hamburg au Bonn kila mtu anamkumbuka Diplomat yule.

   Kuna wakati nilitumwa Russia kikazi na huko Moscow kulikuwa na kesi ya kijana wa kitanzania aliyeshikwa na madawa ya kulevya,adhabu ya kosa hilo huko ni kifo!,kwa kupitia Ubalozi Kijana huyo alitafutiwa dhamana na kupewa Passport ya hadhi ya kibalozi ya Angola na kukimbilia Switzerland (Ni mtoto wa kigogo).Waliomsaidia kufanya hivyo hivi sasa wana Madaraka makubwa Serikalini,wapo Ikulu na wengine Jeshini,sasa hamuwezi kuniambia kuwa JK anatoa majina ya wauza Unga hadharani NO!Hili nakataa! anafahamu madhara ya Huo unga kwani hata kwenye Familia yake anao waathirika,lakini hawezi kuthubutu kuwataja Hadharani kwani ni Miongoni mwao.

   Tuendelee tu kuwa wazi kila kitu kitajulikana hapa!Amina Wamemuua!Hakuna lolote linaloweza kufichwa kufutia kifo chake,ni kweli kwamba kama binadamu alikuwa na udhaifu,sasa wametumia udhaifu huo kumtafutia Ugomvi na mumewe na baadaye kumuondoa,ni ngumu kwa mtu mwenye Akili Timamu kuamini kwamba Amina amekufa kwa Matakwa ya M/Mungu,Ndio maana nami nakubaliana na Uchunguzi huru wa Kifo hiki!
   Cha muhimu kwenye hili swala ni raia wote tushirikiane na kuwataja wale wote wanaojishughulisha na hii biashara, inanikumbusha story nilisoma last week ya waganda na kutaja majina ya drug barons huko kwao na jinsi wanavyoperate kwa kutumia Diplomatic Passport, nadhani kuna wasafirishaji wawili wameshikwa Heathrow mmoja kama two weeks ago wote wakiwa na Diplomatic passports na mmoja wao alikuwa secretery kwenye wizara yao ya mambo ya nje.
   Hating gets you no where, have a safe trip!

  11. DAR si LAMU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st March 2007
   Posts : 3,080
   Rep Power : 5871
   Likes Received
   216
   Likes Given
   27

   Default unafikiri utani? eeh!

   Quote By Ogah View Post
   Duhh Mzee Mwawado,

   Hali inatisha, watu wapo Ikulu mpaka Jeshini!!!!!!!, kwa hiyo shughuli pevu hii
   ....niliposema ni tall order ulifikiri ni kiswahili kirefu cha pwani? eeh?

   ....ni kazi kweli kweli!
   Dar na Lamu yote miji ya pwani, lakini haifanani!

  12. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,981
   Rep Power : 1755
   Likes Received
   32
   Likes Given
   0

   Default

   jamani mnajua hii kitu ya mtandao wa sembe sio kitu kidogo, yaani jamaa wanafanya watu wasiishi kwa amani, sasa nauliza hakuna njia yoyote ya kusolve huu upuuzi. je UN inaweza kuingilia kati na kuuvunja, LHNCR ( sijui ndio hiyo ) wanaweza kuingilia ? au nani haswa wanaweza kuja na kuuvunja huu mtandao ? naombeni tuweze kusaidia taifa ili wataifa waishi kwa amani, na haki !!

  13. Brutus
   #72
   Brutus's Avatar
   Guest

   Default

   Quote By KadaMpinzani View Post
   jamani mnajua hii kitu ya mtandao wa sembe sio kitu kidogo, yaani jamaa wanafanya watu wasiishi kwa amani, sasa nauliza hakuna njia yoyote ya kusolve huu upuuzi. je UN inaweza kuingilia kati na kuuvunja, LHNCR ( sijui ndio hiyo ) wanaweza kuingilia ? au nani haswa wanaweza kuja na kuuvunja huu mtandao ? naombeni tuweze kusaidia taifa ili wataifa waishi kwa amani, na haki !!
   UN ina idara yao ya Drugs na Crime Prevention iko Vienna.
   Ila so far.. America's DEA wamecheua.. sana sana utakuta kuna Rogue Agents kibao!!
   Game la unga sio dogo kama tunavyofikiria!
   mkandara amedokeza kwamba bei ya unga bongo ni sawa na miji kadhaa Ulaya... if you know arithmetics then 1+1=2,11 or binary number!?

  14. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,981
   Rep Power : 1755
   Likes Received
   32
   Likes Given
   0

   Default

   ok, kwani hamna njia ya kutransfer hii bizness toka tanzania hadi kenya jamani ? najua sio uungwana, but damn tumechoka nao, acha kenya nao wafaidi joto la jiwe na wakichoka nao wataihamisha kweingine, sijui rwanda sijui wapi wenyewe, their place of choice, lakini tunataka hii kitu iondoke tanzania !

  15. KadaMpinzani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st January 2007
   Location : Chadema Restaurant
   Posts : 4,981
   Rep Power : 1755
   Likes Received
   32
   Likes Given
   0

   Default

   wapitishe sembe yao mombasa, na kwenye bandari nyingine walizo nazo !

  16. Mkandara's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd March 2006
   Location : T dot
   Posts : 16,573
   Rep Power : 124739545
   Likes Received
   8260
   Likes Given
   8156

   Default

   KadaMpinzani,
   Biashara hii inatokana na uwezo wa ku laundry money!... Tanzania mchezo ndio kwanza unaiva yaani watu wanaingia na tones of money na kuondoka nazo bila kuulizwa. Benki zetu zinabadilisha fedha kama vile ni mchezo wa kawaida kwa hiyo Mafia wote wa Europe wamekita Bongo wakinunua Unga na kuusambaza duniani. Pamoja na kwamba bei yetu ni kubwa, sasa hivi Unga utatumika kuzalisha crack na aina nyinginezo ambazo zinauzwa sana kwa vijana wadogo ktk ma club ulaya na North America, Japan na kadhalika.
   This is big business kwa hiyo kuivunja hii biashara budi kuanza na kuvunja money laundry nchini, sheria kali ktk benki zetu na kuondoa kabisa uwezo wa mtu kuingia na kutoka nchini na kiasi chochote cha fedha za kigeni bila kibali maalum toka benki ya ndani ama nje. Pia Bank to Bank transfer ziwe zinachunguzwa zaidi na kibali hakitoki kwa mtu mmoja tu.
   Kisha kuvunja Mafia mob yenyewe ambayo inahitaji nguvu ya dola!.... problem kubwa ni kwamba kweli watu wanawafahamu watu wengi wanaohusika lakini hawa wote si small fish ktk biashara hii unless marehemu alikuwa na picha kubwa kama ile ya BoT scandal.
   Na sidhani kama JK ama kuna waziri nzini anaweza kusimama tena maanake kwa Mafia Mob swala lilompata kipenzi mbunge wetu hiyo ni - WARNING!.
   Exploration of reality

  17. DAR si LAMU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st March 2007
   Posts : 3,080
   Rep Power : 5871
   Likes Received
   216
   Likes Given
   27

   Default kenya tena.....

   Quote By KadaMpinzani View Post
   ok, kwani hamna njia ya kutransfer hii bizness toka tanzania hadi kenya jamani ? najua sio uungwana, but damn tumechoka nao, acha kenya nao wafaidi joto la jiwe na wakichoka nao wataihamisha kweingine, sijui rwanda sijui wapi wenyewe, their place of choice, lakini tunataka hii kitu iondoke tanzania !

   .....umesikia wao hawana?

   .....sanasana wao wata-transfer huku....hiyo nayo si ni biz tu kama nyingine?

   .....ukitaka kui-transfer,labda,mateja wote tu wa-round up halafu tuna-declare wao si watanzania halali bali wakenya,n.k,tunawasukumia kenya,rwanda,uganda na hata burundi. rahisi zaidi dr congo!

   .....biashara iwafuate huko!hapa tubaki na mabima,benzo,laksas....na majumba mahekalu!
   Dar na Lamu yote miji ya pwani, lakini haifanani!

  18. Mtu wa Pwani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 26th December 2006
   Posts : 4,747
   Rep Power : 1722
   Likes Received
   380
   Likes Given
   769

   Default

   watazalishwa mateja wengine, tatizo ni mateja? wanaouza?
   Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

  19. DAR si LAMU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st March 2007
   Posts : 3,080
   Rep Power : 5871
   Likes Received
   216
   Likes Given
   27

   Default kama umalaya tu....

   Quote By mtumwitu View Post
   watazalishwa mateja wengine, tatizo ni mateja? wanaouza?
   ....tatizo ni wanunuzi na si machangudoa.
   Dar na Lamu yote miji ya pwani, lakini haifanani!

  20. BigMan's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th February 2007
   Posts : 1,135
   Rep Power : 986
   Likes Received
   128
   Likes Given
   26

   Default

   eeh kwanini uwoga usiwepo ebu fikiria calculations sawa na zile za jamaa wa osama waliolipua balozi la marekani dar na nairobi kwa muda ama saa zinazofanana kama tofauti ni sekunde ama dakika rudi kwa amina siku aliyokufa ni siku ya madawa ya kulevya duniani sasa hiyo si body language ambayo pia inaonyesha jamaa wapo makini kupita kiasi ?

  21. Mkandara's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 3rd March 2006
   Location : T dot
   Posts : 16,573
   Rep Power : 124739545
   Likes Received
   8260
   Likes Given
   8156

   Default

   Amina siku aliyokufa ni siku ya madawa ya kulevya duniani
   What a coincidance!
   Exploration of reality


  Page 4 of 21 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Walikamatwa na madawa ya kulevya
   By massai in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 4
   Last Post: 22nd August 2011, 20:07
  2. Wauza Dawa Kulevya Wanyongwe
   By X-PASTER in forum Habari na Hoja mchanganyiko
   Replies: 6
   Last Post: 22nd August 2011, 16:18
  3. UN yahusishwa na madawa ya kulevya...
   By ngoshwe in forum International Forum
   Replies: 2
   Last Post: 10th June 2010, 18:09

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...