TiGo Says
    Show/Hide This

    Topic: Majina ya wauza Madawa ya Kulevya: JK anayo

    Report Post
    Page 4 of 12 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
    Results 91 to 120 of 335
    1. #1
      Mlalahoi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st August 2006
      Location : London, UK
      Posts : 1,771
      Rep Power : 1362
      Likes Received
      122
      Likes Given
      101

      Default Majina ya wauza Madawa ya Kulevya: JK anayo

      Vigogo dawa za kulevya watajwa

      Written by Mwananchi
      Monday, 18 September 2006

      *Majina yao yapelekwa kwa Rais Kikwete
      *Ni orodha ndefu ya majina ya watu 58
      *Wamo wafanyabishara, wanasiasa, viongozi wa dini
      *Mbinu wanazotumia nazo zaanikwa hadharani

      WITO wa Rais Jakaya Kikwete wa kutaka wananchi wajitokeze kutaja majina ya wahalifu nchini, umepata mwitikio mpya, safari hii watu kadhaa wakijitokeza kutaja majina ya vigogo wanaoongoza kwa biashara ya dawa za kulevya nchini.

      Majina hayo yako katika barua iliyoandikwa na wananchi 15 kwenda kwa Rais Kikwete, ambamo wanadai kwamba walikuwa wakitumiwa na vigogo hao kufanya biashara
      hiyo, lakini sasa wameamua kuachana nayo. Barua hiyo iliandikwa Septemba 8, mwaka huu na wahusika wanadai wamekwisha kuiwasilisha Ikulu.

      Kwa mujibu wa barua hiyo, majina 58 yameorodheshwa yakiwa katika makundi matatu makubwa, la kwanza likiwa ni waagizaji wakubwa wa dawa hizo; la pili ni
      wafadhili ambao majina yao hutumika kusafirisha dawa hizo; na la tatu ni wauzaji walioko Dar es Salaam, Tanga, Mwanza, Mbeya na Zanzibar.

      Katika orodha ya waandishi wa barua hiyo wanaodai kusukumwa na uzalendo na uchungu kwa nchi yao, yamo majina ya wafanyabiashara maarufu nchini na wanasiasa,
      wakuu wa taasisi nyeti, baadhi ya viongozi wa dini na maafisa wa juu serikalini.

      Kundi la kwanza lina majina 12, miongoni mwao ni wafanyabiashara maarufu katika miji ya Dar es Salaam, Morogoro, Zanzibar, Arusha na Bagamoyo na baadhi ya
      viongozi wa dini wa madhehebu fulani.

      Kundi hili linadaiwa kuwa linaingiza dawa za kulevya kwa njia mbalimbali zikiwamo, kutumia mipira ya kondomu, majokofu, vifaa vya hospitali, meli na
      marobota ya mitumba.

      Katika kundi la pili kuna watu 19, miongoni mwao wamo wanasiasa wakubwa nchini wakiongoza kundi hili, kutoka taasisi ya fedha nchini na wafanyabiashara maarufu wa
      Dar es Salaam na Zanzibar.

      Kundi la tatu lina majina 27, ambao si ya watu wenye majina makubwa, lakini ndio wanaotumika kusambaza mitaani kwa watumiaji wa dawa za kulevya.


      Mbali ya kushiriki katika kusambaza dawa za kulevya, kundi hili pia lina baadhi ya majina ya watu waliotajwa kushiriki katika kuingiza silaha nzito
      zinazotumika kwa ajili ya ujambazi kutoka nchi jirani.

      Ufukwe wa Pwani ya Bahari ya Hindi eneo la Muhoro wilayani Rufiji inaelezwa kuwa linatumika kuingizia silaha hizo kutoka nchi jirani pamoja na dawa za
      kulevya chini ya ufadhili wa mmoja wa wanasiasa nchini.

      Uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere unatajwa kuwa unatumiwa na watu hawa kuingiza dawa hizo nchini kutokea nchi za nje, huku baadhi ya maafisa wa polisi
      watatu wakitajwa kuwa ndio wanaotoa ulinzi kwa watu wanaopitisha dawa hizo.

      Nyumba ya afisa wa juu mstaafu katika idara nyeti iliyopo jijini Dar es Salaam inatajwa kuwa inatumika katika kuhifadhi vijana wanaoingiza dawa za kulevya
      nchini, huku nyumba ya mfanyabiashara mmoja iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam ikitajwa kuwa ndiyo inayotumika kama kituo cha kutolea pipi tumboni kwa vijana wanaotumika kuingiza dawa hizo kutoka nje ya nchi.

      Vile vile, katika kundi hili mwanamke mmoja anayefanya kazi katika taasisi moja ya fedha anatajwa kuwa anashiriki katika kuhujumu uchumi wa nchi kwa
      kusafirisha kwenda nje fedha nyingi za kigeni akitumiwa na mfanyabiashara mmoja maarufu wa dawa za kulevya nchini.

      Mipaka ya Tunduma mkoani Mbeya, Horohoro mkoani Kilimanjaro na Namanga mkoani Arusha, nayo imetajwa kuwa inatumika kupitisha dawa za kulevya kwa kutumia
      mabasi na magari mengine. Kuna kampuni mbili za mabasi nchini zinazotajwa kuongoza kutumika katika usafirishaji.

      Barua hiyo ya kurasa 10, pia inamtaja mwanamke mmoja ambaye anatumika kupitisha dawa za kulevya uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere kuwa ni sugu; aliwahi
      kuhukumiwa kifungo cha miaka 35 jela kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya, lakini hivi sasa yupo mitaani kifungo chake akitumikia mtu mwingine.

      Alipoulizwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo, Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Utawala Bora), Philip Marmo, alisema hajapata barua hiyo na kwamba atalizungumzia
      baada ya kuipata.

      Naye Waziri wa Usalama wa Raia, Bakari Mwapachu, alisema hana taarifa za kuwako kwa barua hiyo. Hata hivyo, alisema kuna tume ya dawa za kulevya iliyopo
      chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ndiyo inayoshughulikia zaidi suala hilo.

      Alisema Jeshi la Polisi linafanya kazi za kukamata watu wanaojihusisha na dawa hizo na kwamba mikakati mingine ya kupambana na watumiaji inafanywa na tume
      hiyo.

      Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Polisi liongezewe uwezo wa kupambana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na kuwahamisha vituo vya kazi askari
      waliokaa kituo kimoja kwa muda mrefu.

      Pia alilitaka Jeshi hilo lijisafishwe lenyewe kutokana na madai kwamba polisi wanahusika na baadhi ya matukio ya uhalifu nchini.


      Rais alitoa wito kwa wananchi wenye taarifa zozote za uhalifu, na wanaojua waliko majambazi wazipeleke taarifa hizo kwake kama wanaogopa kuzipeleka polisi.


      Katika kuitikia wito huo, wananchi kadhaa waliandika barua iliyooroshesha majina ya polisi 20, wakiwamo baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa na kuikabidhi kwa Waziri wa Usalama wa Rais, Bakari Mwapachu.

      Tangu wakati huo, mabadiliko makubwa yameshuhudiwa yakifanywa kwenye jeshi hilo, hata hivyo hii ni mara ya kwanza kwa watu kujitolea kuandika barua yenye
      majina na maelezo ya kina kama hii kuhusu biashara ya kulevya na kuipeleka kwa Rais.


    2. #91
      Gembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2007
      Location : kamnyonge
      Posts : 2,574
      Rep Power : 1461
      Likes Received
      29
      Likes Given
      35

      Default

      jina la kwanza Rostam,naomba kuwasilisha

    3. #92
      Kite Munganga's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 19th November 2006
      Posts : 699
      Rep Power : 727
      Likes Received
      36
      Likes Given
      61

      Cool

      Quote By mkomboziufisadi View Post
      jina la kwanza Rostam,naomba kuwasilisha
      Yaelekea humjui Rostam,huyo bwana ni Mfanya biashara mahiri na safi pia hakuanza jana kushika pesa "clean money",jaribu pia kujua anatoka wapi kwa undani na ujue ndugu zake walio nje na kampuni zao ziliianza lini,kuhusu mengineyo leteni habari

    4. #93
      Gembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2007
      Location : kamnyonge
      Posts : 2,574
      Rep Power : 1461
      Likes Received
      29
      Likes Given
      35

      Default

      nyie ndio mnaolipwa na huyu mkoloni?

    5. #94
      Gembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2007
      Location : kamnyonge
      Posts : 2,574
      Rep Power : 1461
      Likes Received
      29
      Likes Given
      35

      Default

      subiri leo dr. slaa aweke mambo hadharani.alafu utaongea baadaye..kajiunge na gazeti la Rai

    6. #95
      Bongolander's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Tandale
      Posts : 3,576
      Rep Power : 1273
      Likes Received
      234
      Likes Given
      6

      Default

      Quote By kite munganga View Post
      Yaelekea humjui Rostam,huyo bwana ni Mfanya biashara mahiri na safi pia hakuanza jana kushika pesa "clean money",jaribu pia kujua anatoka wapi kwa undani na ujue ndugu zake walio nje na kampuni zao ziliianza lini,kuhusu mengineyo leteni habari
      Kwa sababu wewe unajua ingekuwa vizuri utueleze ametokea wapi, sisi tulidhani ni mtanzania mwenzetu ingawa he is nicknamed mkoloni. Itakuwa ni vizuri kama ukisema how clean his money is. Kama unaona anapigwa madongo unafair basi wewe unaweza kutoa counter attack nzuri sana ya hoja, after all JF ni sehemu ya hoja kwa hoja. Lakini ukumbuke kuwa sio wewe tu Tanzania unaemfahamu RA....uwanja ni wako lete sumu tuzisikie. Lakini usituambie kuwa ni ndugu zake wa Iran wamemtajirisha.

    7. #96
      Gembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2007
      Location : kamnyonge
      Posts : 2,574
      Rep Power : 1461
      Likes Received
      29
      Likes Given
      35

      Default

      kiye mganga,lete data kuhusu huyu RA?si unamfahamu vizuri,Kwanini kama anatupenda watanzania hatusaidii na hatulindi?anasadia kuwafadhili wasanii ambao sanaa yao tumeichoka sababu inadumaza maendeleo..
      hoja ujibiwa kwa hoja,

    8. #97
      Kite Munganga's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 19th November 2006
      Posts : 699
      Rep Power : 727
      Likes Received
      36
      Likes Given
      61

      Cool

      Quote By mkomboziufisadi View Post
      kiye mganga,lete data kuhusu huyu RA?si unamfahamu vizuri,Kwanini kama anatupenda watanzania hatusaidii na hatulindi?anasadia kuwafadhili wasanii ambao sanaa yao tumeichoka sababu inadumaza maendeleo..
      hoja ujibiwa kwa hoja,
      Msimchukie kwa kuwa anawafadhili wasanii na kumchanganya na kundi la wasanii si vizuri hasa linapokuja swala la madawa ya kulevya, ni kweli gazeti la Rai hata mie siku hizi sisomi asilani na nikiliona nachevuka moyoni

    9. #98
      Gembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th September 2007
      Location : kamnyonge
      Posts : 2,574
      Rep Power : 1461
      Likes Received
      29
      Likes Given
      35

      Arrow

      Quote By kite munganga View Post
      madawa ya kulevya,
      sijasema yuko katika group hilo,nadhania haujasoma hoja yangu vizuri

      naomba niweke tena ibara ya 22 kifungu cha pili

      "watu wote wanatakiwa na sheria kutunza mali ya mamlaka ya nchi na ya pamoja,kupiga vita aina zote za uharibufu na ubadhirifu,na kuendesha uchumi wa taifa kwa makini kama watu ambo ndio waamuzi wa hali ya baadaye ya taifa lao"

      RA ni moja spinning masters wa Mtandao,ambayo kwa njia moja ama nyingine wamehusika ubadhirifu katika sekta mbalimbali,mathalan suala la Richmond,

      kama ni mwema kwanini awadhamini Wasanii kama hana maslahi nao?

    10. #99
      Kasheshe's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 29th June 2007
      Location : Bububu
      Posts : 3,314
      Rep Power : 1231
      Likes Received
      107
      Likes Given
      96

      Default

      Umesema Wahusika Kwenye Madawa Ya Kulevya, Natamani Sana Kuwasikia Maana Hata Marehemu Amina, Hakuwahi Kuwataja Hadharani pamoja na misifa mliyompa;

      Lakini Naomba Iwe Kweli Wauza Madawa Ya Kulevya Msichanganye Mambo Tafadhali

      Nasubiri Kuona Orodha Binafsi Simjui Hata Mmoja!


      Hivi, ni mimi tu naona au kuna wengine, inaelekea Tanzania kuwa Tajiri ni dhambi hata kama upezipata fedha kwa njia za kibiashara, mtu asiniambie halali maana biashara zinazolipa siku zote sio halali.

      NB: Halali ninamaanisha hapa ni halali ya kwenye vitabu vya Mwenyezi Mungu!

    11. #100
      Msanii's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 4th July 2007
      Posts : 6,081
      Rep Power : 1849
      Likes Received
      93
      Likes Given
      18

      Default

      Kilitime bado haujaeleweka na ili ueleweke inabidi ufafanue statement yako hapo juu....
      " If you hear a voice within you say "you cannot paint", then by all means paint, and that voice will be silenced"
      msanii@jamiiforums.com

    12. #101
      KadaMpinzani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2007
      Location : Chadema Restaurant
      Posts : 5,011
      Rep Power : 1577
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      cha kushangaza mtaona hayo majina ya wauza unga wooooote ni ccm ! sasa cha kujiuliza wapinzani ( sana sana chadema ) nao hawauzi hayo madawa ? viongozi wa upinzani mbona hatusikii majina yao ? je hii ni political agenda tu ya chadema kupakazia ccm ?


    13. #102
      Chakaza's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 10th March 2007
      Location : everywhere
      Posts : 2,336
      Rep Power : 1181
      Likes Received
      317
      Likes Given
      247

      Default

      Quote By KadaMpinzani View Post
      cha kushangaza mtaona hayo majina ya wauza unga wooooote ni ccm ! sasa cha kujiuliza wapinzani ( sana sana chadema ) nao hawauzi hayo madawa ? viongozi wa upinzani mbona hatusikii majina yao ? je hii ni political agenda tu ya chadema kupakazia ccm ?
      KadaMpinzani, Acha kabisa,kama serikali hii inaweza kuwabambikia kesi wapinzani ili kuwanyamazisha, unadhani wakiuza madawa si haita pita saa 24 kabla ya kukamatwa na kutangazwa saaana kwenye vyombo vya Habari kuwa viongozi hao hawana lolote zaidi ya biashara haramu? Serikali ina wajua wauza madawa wote na wala rushwa hata JK mwenyewe amekiri hivyo hadharani. Sasa kwanini hawatajwi? Sababu kubwa ni kuwa wengi wao ni vigogo ndani ya serikali na CCM au wafadhili wao wakubwa. Ndio sababu ya kigugumizi.Nakuhakikishia kungekuwa na uchafu wa aina hiyo ndani ya viongozi wa upinzani hakika wangetumia hilo kama BOMU LA MAANGAMIZI

    14. #103
      Bongolander's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Tandale
      Posts : 3,576
      Rep Power : 1273
      Likes Received
      234
      Likes Given
      6

      Default

      Nadhani serikali imewahi kutaifisha gari la Slaa kutokana na kusafirisha dawa za kulevya. Nadhani wanaweza kuibua issue hiyo ili kummaliza.

    15. #104
      KadaMpinzani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2007
      Location : Chadema Restaurant
      Posts : 5,011
      Rep Power : 1577
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Bongolander View Post
      Nadhani serikali imewahi kutaifisha gari la Slaa kutokana na kusafirisha dawa za kulevya. Nadhani wanaweza kuibua issue hiyo ili kummaliza.
      kama ni kweli, basi wapinzani wanaweza kusema serikali inataka kuua upinzani !

    16. #105
      Kasheshe's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 29th June 2007
      Location : Bububu
      Posts : 3,314
      Rep Power : 1231
      Likes Received
      107
      Likes Given
      96

      Default

      Orodha ya wauza unga wapi?

    17. #106
      Kuntakinte's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th May 2007
      Location : Matombo, Morogoro
      Posts : 795
      Rep Power : 720
      Likes Received
      2
      Likes Given
      3

      Default Vijana 40 waachana na dawa za kulevya-JF tunalonga nini kuhusu Madawa ya kulevya.

      Vijana 40 waachana na dawa za kulevya

      2007-09-30 11:27:46
      Na Felix Andrew


      Zawadi ya vijana 40 waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam, wameacha kutumia na kuiomba serikali kuwapatia matibabu na mitaji ili waweze kuendesha maisha yao.

      Wakizungumza mwishoni mwa wiki, vijana hao walisema kuwa sasa wamechoka kutumia madawa hayo.

      ``Kwa kweli madawa haya siyo mazuri, tumeamua kuacha wenyewe bila shinikizo la mtu au kikundi chochote , lakini pia tumegundua kuwa madawa haya hayana faida yoyote ndani ya miili yetu zaidi ya kuleta chuki miongoni mwa jamii, `` alisema Bw.Toni Frederick kwa niaba ya wenzake.

      Alisema mara baada ya uamuzi huo tatizo kubwa linalowakabili kwa sasa ni namna ya kupata matibabu kwani wengi wao wameathirika kwa viwango tofauti.

      ``Tunaiomba serikali na mashirika yanayotoa huduma za afya kutupatia matibabu ili tupone kabisa na hatimaye tuweze kushiriki kazi za ujenzi wa taifa,`` alisema.

      Aliongeza kuwa mbali na matibabu vijana hao wanahitaji kupewa kazi za kufanya au mitaji itakayowasaidia kujiendeshea maisha.

      Bw. Frederick alisema kuwa wameamua kuanzisha kikundi kinachojulikana kama Kinondoni Anti Drug Network kitakachokuwa kinaewaelimisha vijana madhara ya madawa hayo.

      Aidha, alisema wanatarajia kukisajili kikundi hicho hivi karibuni na kuanza kutoa elimu hiyo katika maeneo mbali mbali wilayani humo.

      Kwa upande wao Madiwani wa Viti Maalum wa wilaya ya Kinondoni, walisema wapo tayari kuwasaidia vijana hao kimatibabu.

      Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Bi. Nuru Chaurembo, aliwaomba vijana hao kujiorodhesha majina yao na kuyawasilisha kwenye ofisi zao.

      ``Tutatongea na uongozi wa Manispaa ya Kinondoni kuangalia namna ya kuwasaidia kuwapatia matibabu, ``alisema .

      Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM tawi la Mwananyamala , Bw. Rajab Mwilima, alisema kuwa atashirikiana na viongozi wenzake kuhakikisha kuwa vijana hao wanapatiwa ajira kwenye baadhi ya makampuni.

      Aliwapongeza vijana hao kwa uamuzi wao wa kuachana na matumizi ya madawa hayo na kuwaahidi kuwasaidia mambo mbali mbali.

      SOURCE: Nipashe
      "Mwisho wa ubaya Aibu"

    18. #107
      WembeMkali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th June 2007
      Posts : 322
      Rep Power : 622
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default

      Hivi hayo majina mboni hayatajwi?..au hakuna?
      Mimi naanza na huyu bwana anaitwa Kanali Kimbau.Alikuwa mbunge(CCM-Mafia).Haya wekeni ya wengine basi.

    19. #108
      Bongolander's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Tandale
      Posts : 3,576
      Rep Power : 1273
      Likes Received
      234
      Likes Given
      6

      Default

      Wembe mkali wengine walnaofahamika kwenye public domain kwa sasa ni Idd Azan ambaye amejitahidi kukanusha, the list goes on...

    20. #109
      Shalom's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 17th June 2007
      Location : texas
      Posts : 1,333
      Rep Power : 835
      Likes Received
      54
      Likes Given
      38

      Default

      masikini kada mpinzani! ameishiwa jamani

      huyu hatakiwi kusamehewa kwa sababu analijua analolifanya

    21. #110
      mpiga picha's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 26th September 2007
      Location : Kwenye ka-studio
      Posts : 2
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      tuwapige picha eti?
      - ndoto ni za bure -

    22. #111
      Nsoba Shelutete's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 3rd August 2007
      Posts : 2
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Nawapongeza sana vijana hawa kwa uamuzi waliochukua na kugundua kwamba vitu wanavyotumia ni sumu inayoua polepole.

      Lakini Serikali ahadi zake ziko wapi za kupambana na madawa ya kulevya. Inashangaza Mkuu amekazana na kuhamasisha watu kupima ukimwi lakini amenyamaza kimya kabisa kana kwamba haoni kuhusu watu wanaokifanya kizazi cha Watanzania kuwa mazezeta kwa kuingiza/kuuza madawa bila kificho, tena jambo ambalo serikali ikiamua ni katika mwezi mmoja tu itatokomezwa. Kila kona sasa ni kuhamasisha kupima UKIMWI....

      Pamoja na ahadi za Mkuu kwamba orodha anayo ya wote wanaohusika lakini amenyamaza kimya, inatufanya tuamini kabisa usemi usemayo kwamba biashara hiyo ni ya wakubwa kwa hiyo hata Mkuu hawezi kuwagusa maana atakuwa amegusa mboni.

      Mkuu watu wanaimani naye kwamba akiamua kutokomeza uchafu huu inawezekana. Okoa kizazi hiki kisiwe cha mazezeta, ni heri hata Ukimwi mtu ukimpata mwisho wake ni kurudi kwenye udongo..lakini madawa ni kuwa na kizazi cha mazezeta!!

      Shelutete

    23. #112
      Nyangumi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th January 2007
      Posts : 582
      Rep Power : 697
      Likes Received
      3
      Likes Given
      1

      Default

      Jamani wengine hatuna Doc, lakini tuna taarifa toka kwa watu wa karibu kuwa yule mama mchungaji naye yumo.Yeye hauzi ila kazi yake ni kufadhili watu wanaokwenda leta.Rostarm hilo halina ubishi. Na Mzee K.

    24. #113
      Gigo's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 6th August 2006
      Posts : 473
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default

      Kama Kuna Mtu navuta Bangi Humu JF ajitaje!! alafu...Muwataje wanao wauzia -Haraka sana...
      Nataka Nipate Orodha niifanyie Kazi...

    25. #114
      Invisible's Avatar
      Robot Array
      Join Date : 11th February 2006
      Location : Here...!
      Posts : 8,759
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      2877
      Likes Given
      1892

      Default

      Quote By Gigo View Post
      Kama Kuna Mtu navuta Bangi Humu JF ajitaje!! alafu...Muwataje wanao wauzia -Haraka sana...
      Nataka Nipate Orodha niifanyie Kazi...
      Gigo.

      Halafu atakusaidia kuwataja wavutaji wenzie na anayewauzia
      Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!
      24/7 Email SUPPORT: support@jamiiforums.com


    26. #115
      Invisible's Avatar
      Robot Array
      Join Date : 11th February 2006
      Location : Here...!
      Posts : 8,759
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      2877
      Likes Given
      1892

      Default

      Quote By Nyangumi View Post
      Jamani wengine hatuna Doc, lakini tuna taarifa toka kwa watu wa karibu kuwa yule mama mchungaji naye yumo.Yeye hauzi ila kazi yake ni kufadhili watu wanaokwenda leta.Rostarm hilo halina ubishi. Na Mzee K.
      Si kuwa wale wanaohisiwa lazima watakuwa wanahusika kwa asilimia 100. Bado siamini kuwa wauza unga wote ni CCM. Hata upinzani wanaweza kuwepo. Muuza unga kifupi si mwanasiasa ila mfanya siasa. Anaweza kuitumia siasa kuendesha mambo yake lakini politically he is bankrupt!

      Back to the issue: Just bring the names and give some vivid evidences to accompany your argument!

      Natumaini watu wataanza bila hiyana. Kama Zitto mmojawapo sema... Invisible mmojawapo usisite kumtaja... Muhimu kuwa na reasoning inayoashiria uko sahihi.

      Karibu
      Ficha Upumbavu wako; Usiifiche Hekima yako!
      24/7 Email SUPPORT: support@jamiiforums.com


    27. #116
      Mtaalam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2007
      Posts : 1,247
      Rep Power : 797
      Likes Received
      16
      Likes Given
      0

      Default

      Nyangumi,mama mchungaji upi tena huyo jamani anayeongelewa?

    28. #117
      Gigo's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 6th August 2006
      Posts : 473
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Lightbulb

      Quote By Invisible View Post
      Gigo.

      Halafu atakusaidia kuwataja wavutaji wenzie na anayewauzia
      (((((((ok)))))))

    29. #118
      Quemu's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 27th June 2007
      Posts : 1,076
      Rep Power : 775
      Likes Received
      10
      Likes Given
      16

      Default

      Quote By Mtaalam View Post
      Nyangumi,mama mchungaji upi tena huyo jamani anayeongelewa?
      Nafikiri anamuongelea yule mama mwenye shule mmoja kubwa ya english media pale Bongo.
      We miss 100% of the shots we never take

    30. #119
      Mtaalam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2007
      Posts : 1,247
      Rep Power : 797
      Likes Received
      16
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By QuickMover View Post
      Nafikiri anamuongelea yule mama mwenye shule mmoja kubwa ya english media pale Bongo.
      duh kumbe watu wanaweza kuwa na ngozi ya kondoo kumbe ndani ni chui...mhm tupeni majina mengine basi hayo..ila angalieni wasije wakawe A.C

    31. #120
      FairPlayer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th February 2006
      Location : UK
      Posts : 3,986
      Rep Power : 1420
      Likes Received
      240
      Likes Given
      147

      Default

      Udaku daku tu, kama hamna data si mkae kimya kuliko kuleta utumbo humu! Wauza madawa wanaeleweka, wakishatajwa? AC alishawataja, akaambiwa na mumeo pia yumo!

      Nini kiliendelea vile?!
      A positive thinker!

    Page 4 of 12 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

    LinkBacks (?)


    Similar Topics

    1. Iko wapi orodha ya wauza madawa ya kulevya?
      By mmaroroi in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 0
      Last Post: 25th August 2011, 21:20
    2. Walikamatwa na madawa ya kulevya
      By massai in forum Jukwaa la Siasa
      Replies: 4
      Last Post: 22nd August 2011, 19:07
    3. Wauza Dawa Kulevya Wanyongwe
      By X-PASTER in forum Habari na Hoja mchanganyiko
      Replies: 6
      Last Post: 22nd August 2011, 15:18
    4. JK amepeleka wapi list ya vigogo wauza madawa ya kulevya????
      By Wakwetu in forum Jukwaa la Sheria (The Law Forum)
      Replies: 4
      Last Post: 14th February 2011, 22:59
    5. UN yahusishwa na madawa ya kulevya...
      By ngoshwe in forum International Forum
      Replies: 2
      Last Post: 10th June 2010, 17:09

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...