Naanza kushitukia kwamba kuna mambo yamekuwa yakijadiliwa muda mrefu na wakati mwingine hata hayana tija, wakati mwingine yaki-engage mahakama, serikali na bunge!
Je hii haiwezeki kuwa ni mojawapo za athari ya kusomesha wataalamu wa sayansi(arts) jamii wengi!
Je suala la TANESCO kuonekana la kisiasa ndio dalili za mfumo huo wa elimu kuwa na waatalaamu wa arts zaidi kuliko wahandisi?
Ninachalea kusema haya kwa kuwa hoja ya TANESCO inaonekana kutosikilizwa kabisa. concern yao ya kuwepo umeme usiotosha mahitaji na kwamba serikali imekuwa ikijivutavuta kuwekeza haionekani kuonekana machoni mwa wanasiasa... nini tatizo?
Kasheshe,
Mkuu ktk hili nadhani unajaribu ku spin the issue kwa sababu tunachozungumza hapa ni hili swala la mitambo ya Dowans..
Kuna issue mbili hapa ambazo unajaribu kuziunganisha Short na Long term strategies..
Kwanza hakuna mwananchi anayepinga umuhimu wa Umeme na kwa nini serikali yetu imeshindwa kutekeleza long term plan ya kuzalisha umeme..Hilo halina ubishi wala mjadala iwe kwa wanasiasa, wasomi au wananchi kabuntas kama sisi.. mahitaji ya UMEME hayana elimu ya art wala Uhandisi isipokuwa ni chombo gani kinahitajika..tatizo ipo ktk utekelezaji wa short term plan ambayo tayari imekwisha fanyiwa kazi na hao hao wasomi wahandisi unaowazungumza.. wametumia art kutuzuga wananchi wote. sasa sijui walisomea art au Uhandisi.
Mkuu wangu kinachogomba hapa labda nikiweke sawa.. ni Hivi kama sisi tumekwenda kwa daktari na ametuandikia dawa ya maleria iwe Chloroquine, hakuna anayepinga maamuzi hayo, isipokuwa tunachopinga ni maamuzi ya mtu alioyekwenda dukani kununua dawa hiyo..Kwanza kanunua dawa toka kwa mlanguzi feki - made in India kwa gharama ambayo ni kubwa..Kinachogomba zaidi ni madai yake yanayolenga zaidi sababu za maradhi yetu na somo zito kuhusiana na Maleria wakati sisi tunachouliza ni kidogo sana why.. kinahusu hiyo dawa sio maradhi yetu..hatupati jibu!
Nachoomba hawa wahandisi unaotaka kuwasifia watueleze kwa undani kuhusu hii mitambo ya Dowans na sio kiza kinachotuandama, hilo tunafahamu toka mwanzo na ndio maana serikali iliwapa go ahead Tanesco kununua mitambo ya dharura badala yake wao wakatufungashia mitambo ya mashinga!..
Sasa nani artist hapa ikiwa huyo msomi mwenyewe anatumia art kufanya maamuzi yanayohitaji elimu yake..Kulikuwa hakuna wakati una viongozi wsomi na wahandisi kama unavyotaka kuliko wakati wa Mkapa lakini ndio wakati Umeme,Maji na vitu vyote vimetupwa nje ya elimu zao..walichofikiria ni UTAJIRI!.. na ktk swala la mitambo ya Dowans kinaendelea hapa ni imani hiyo ya UTAJIRI..imani ambayo wananchi tumechoka nayo! kwa nini hawa wasomi hawaelewi hilo?
So artist can be anyone, msomi, mwanasiasa na hata raia asokuwa na elimu..Ni kipaji kinachotegemea wajinga wangapi wanaingia!
Re: Nini chanzo cha mijadala mingi isiyoisha? Je ni mfumo wetu wa Elimu?
Watanzania tunafundishwa kuwa wanasiasa. Profession pekee inayoheshimika na inayolipa ni siasa. Ndio maana hata maprofesa wanaacha kaza zao, madaktari, wanajeshi na hata majambazi wanatafuta kuingia kwenye siasa. MIjadala ikiisha ina maana kutakuwa hakuna siasa.
Heshima mbele, yaani nilichoeleza ndio exactly unachofanya... post yako imejaa siasa sana, najua wewe umesoma arts... hivyo ni fani yako!
Maswali yote ya msingi uliyonayo ukipeleka TANESCO wanakupa majibu yote bila hata kukupa tarehe...
Kuacha nchi kuongozwa zaidi na siasa... itatumaliza.
Nchi kuongozwa na siasa sisahihi, lakini ukweli ni kwamba CEO's combines both political interest and technical fact to make decisions. Worse enough to public enterprises political interest is given high weight than technical ones. In this case, a serious political opinion in favour of technical fact is sought for better social outcome, and this is the premise where this argument stands in.
Re: Nini chanzo cha mijadala mingi isiyoisha? Je ni mfumo wetu wa Elimu?
Hii Kashshe kweli kweli! Usitetereke umekutana na wanasiasa wa humu ndani-wajibu kwa siasa za humu ndani,.
Kwa kweli uelevu wangu hakuna mijadala inayoisha-nafikiri pale kunapokuwa na makubaliano kidogo basi, wadau(wanasiasa) huwa wanaita huwo mjadala hauendelei- vile vile na wale ambao huwa hawakubaliani- huwa wanachoka kutokubaliana na hivyo kuita mjadala umekwisha ama haupo!
Vyanzo vya mijadala? ni hii hapa kama wewe ulivyoanzisha unatafuta nini?
Una elimu gani ya kuanzisha huu mjadala? Siasa kama sayansi?
Hivi wadau ARTS ni sayansi?
Uelevu wangu arts ni ubobeaji wa kiaina, na sayansi uchunguzi wa kimahesabuhesabu au?
Anza kwa kumwuliza BFF wako anayesema kila siku hapa kuwa Tanzania hakuna waandishi wa habari halafu anaanza kumpondea "mwandishi" mwingine wa habari mwenye redio ya mtandaoni...
Wakimuelewa Andy Rooney basi kutakuwa hakuna tena tatizo...
Re: Nini chanzo cha mijadala mingi isiyoisha? Je ni mfumo wetu wa Elimu?
Kasheshe,
..mada yako imenifanya nikumbuke habari iliyopata kuandikwa kuhusu ziara ya Robert Mc Namara chuo kikuu cha DSM.
..viongozi walimtembeza maeneo mbalimbali ya chuo, lakini walipofika faculty of Law wakamwambia McNamara kwamba Law ndiyo kitivo kianzilishi na fahari ya UDSM.
..baada ya maelezo hayo, Robert McNamara alitoa kauli kwamba, ikiwa kilimo ndiyo uti wa mgongo uchumi wa Tanzania, ingetegemea kitivo cha kilimo kiwe cha kwanza taifa lilipoamua tulipoamua kuanzisha chuo kikuu.
..nadhani taifa letu limejenga mazingira ya kuwakweza wanasiasa kuliko taaluma yoyote ile. inashangaza kwamba wanasiasa wanalipwa mafao mazuri kuliko wataalamu waliobobea ktk fani zao.
Watanzania tunafundishwa kuwa wanasiasa. Profession pekee inayoheshimika na inayolipa ni siasa. Ndio maana hata maprofesa wanaacha kaza zao, madaktari, wanajeshi na hata majambazi wanatafuta kuingia kwenye siasa. MIjadala ikiisha ina maana kutakuwa hakuna siasa.
Kwa nini wataalamu wetu hukimbilia kujifanya "victims" na kutafuta visingizio vya kulaumu wanasiasa?
I am sick and tired of this fingerpointing.
Kama wataalamu walishafanya utafiti wao katika hili tangu mwaka 47, kwa nini kama wanasiasa walionekana kulegalega hawakuuambia umma wa Watanzania ukweli?
Kwa nini iwe sisi wakimbizi humu JF ndio tuwe na uzalendo wa kuongea na kubainisha matatizo bila woga, na wataalamu wetu wawe kunguru mwoga?
Kingine ni hicho cha kusema ni kwenye siasa pekee ndipo kuna uponeo.
Tabaka la wasomi wetu ni sawa na wanasiasa wetu wanavyopenda misaada na kuziba viraka. Msimsingize Nyerere na University College kuwa ndio shina lwa Sayansi kuyumba.
Tuna wataalamu kibao katika kila nyanja ya sayansi, anza kilimo, hali yahewa, mifugo, afya, lishe, kemia, fizikia, uhandisi, umeme, kompyuta, mawasiliano na mengine kem kem, lakini badala ya wataalamu hawa kujitutumua na kuwa wabunifu wa kufanya kazi bila kuambiwa na wanasiasa, wanasubiri kila siku wanasiasa waongee au wapewe amri.
Why play victim and inferiority complex mentality?
Same is those in ni Science, fields, Lawyers, Accounts, Economists etc. Every Msomi in Tanzania enjoys to play a victim and later point a finger to a Politician kuwa eti Politician ni tatizo.
No tatizo la kwanza ni wewe mtaalamu ambaye unashindwa kufanya kazi yako kwa umakini na ufanisi!
__________________
Amani Iwe Nanyi,
Camerlengo
Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka
"Any existence deprived of freedom is a kind of death." Gen. Michel Aoun
'Who comes to give greeting to the Inkosi-kaas? Who would taste her kiss, whereof the fruit is death? I, the Woodpecker, I, the Slaughterer, I the Swiftfooted! I, Umslopogaas!"
..lawama zako ni rahisi sana kuzitoa ukizingatia kwamba uko kwenye mtandao huku ukitumia jina la bandia.
Well iwe lawama au kubaini ufisadi, kama hao wataalamu wote wnajua ni kazi kulipua ngoma, kwa nini wasije basi huku JF au wakatafuta watu watuletee khabri tuzilipue kama lile sakata la ATCL au Benki ya Posta?
__________________
Amani Iwe Nanyi,
Camerlengo
Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka
"Any existence deprived of freedom is a kind of death." Gen. Michel Aoun
'Who comes to give greeting to the Inkosi-kaas? Who would taste her kiss, whereof the fruit is death? I, the Woodpecker, I, the Slaughterer, I the Swiftfooted! I, Umslopogaas!"