JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

  Report Post
  Results 1 to 14 of 14
  1. Mzee Mwanakijiji's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2006
   Location : Kijijini
   Posts : 32,118
   Rep Power : 87995664
   Likes Received
   24672
   Likes Given
   13382

   Default Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Ninaendelea na ule ukosoaji wangu wa mchakato wa kufikia katiba mpya; mengi ambayo ninayaandika hapa nilishayaandika nilipokosoa kwa mara ya kwanza mswada wa mchakato huu pale ulipowasilishwa kwa mara ya kwanza. Kwa vile mchakato ndio hivyo unaendelea napenda kuendelea kuonesha kuwa sababu zangu binafsi za kutounga mkono mchakato huu ulivyo sasa bado zipo.

   TATIZO LA IBARA YA 34
   Ibara ya 34 ya sheria ya kusimamia mchakato huu (haijafanyiwa marekebisho kushughulikia tatizo hili) inasema "Mtu ambaye jina lake limeingizwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililoanzishwa chini ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 1984, atakuwa na haki ya kupiga kura isipokuwa kama mtu huyo atakuwa amezuiwa kupiga kura na sheria nyingine yoyote"

   Kimsingi, hakutakuwa na uandikishaji mpya wa wapiga kura kwa ajili ya kura ya maoni. Hili NI TATIZO. Kama kuna watu hawataki kushiriki katika kura za vyama vya siasa vya wagombea lakini wanataka kushiriki kwenye kura ya maoni wanazuiwa kufanya hivyo. Sasa, katika hali ya kawaida tunaweza kusema kuwa kama wanataka kupiga kura basi wajiandikishe kupiga kura lakini kama tulivyoona hivi karibuni kwamba kule Arumeru mwaka mmoja baadaye wametumia daftari la mwaka 2010!

   BILA ya kuweka kwenye sheria lazima (lugha ya "shall") kutaka tume za uchaguzi kufanya maboresho ya daftari la wapiga kura angalau si chini ya miezi mitatu kabla ya kura maoni kuna watu wengi wanaweza kuwekwa nje ya kupigia kura ya maoni na hivyo kuwanyima haki yao ya kutumia ile ambayo nimeita kwenye ile mada nyingine "their sovereignty" kuamua katiba yao. NI LAZIMA kuwepo uandikishaji wa wapiga kuwa kwa ajili ya kura ya maoni; SI SAHIHI hata kidogo kutumia daftari la kawaida la wapiga kura au kutoweka kwenye katiba haja kwa tume za uchaguzi kufanya updating ya daftari hilo

   TATIZO LA IBARA YA 36
   Mojawapo ya sababu hizo ni hii inayohusiana na Uhalali wa kura ya maoni. Ibara ya 36 nina uhakika haikufanyiwa marekebisho kushughulikia tatizo nitakalolieleza hapa inazungumzia matokeo ya kura ya maoni. Kwamba, kura ya maoni itaitishwa na itakuwa ni ya siri na kuwa uhalali wake utakuwa kukubaliwa kwa katiba na wapiga kura asilimia 50 kutoka bara na asilimia 50 kutoka visiwani. Inasema hivi ibara hiyo kuhusu hili "Matokeo ya kura ya maoni yataamuliwa kwa msingi wa kuungwa mkono kwa asilimia inayozidi hamsini yajumla ya kura zote zilizopigwa kutoka Tanzania Bara na asilimia inayozidi hamsini ya jumla ya kura zote zilizopigwa kutoka Tanzania Zanzibar."

   Sasa kwa juu mtu anaweza asione tatizo lakini hili nimedokeza kwenye mada nyingine sitarudia hapa. Tatizo langu kubwa ni kwamba ibara nzima ya 36 haifungi kiasi hicho cha kura na idadi ya watu watakaojitokeza kupiga kura. KIMSINGI asilimia 50 ya watakojitokeza kupiga kura itaamua katiba mpya. Hii ina maana gani?

   a. HAIJALISHI ni kiasi gani cha watu kitajitokeza kupiga kura. Kwa mfano, katika chaguzi zetu zote kuu kabla ya 2010 idadi ya wapiga kura (voters turnout) haikuwa chini ya asilimia 70 ya waliojiandikisha kupiga kura isipokuwa mwaka 2010 ambapo kwa mara ya kwanza voters turn out ilikuwa chini ya asilimia 50! Hii ina maana ya kwamba, idadi ya wananchi wachache inaweza kuamua katiba mpya!

   b. Kutokana na hilo la "a" hapo juu ni wazi kuwa kama daftari la wapiga kura litakuwa na watu milioni 25 tukasema kuwa ni asilimia 50 tu watajitokeza kupiga kura basi watu milioni 12.5 watapiga kura. Lakini tukisema kuwa katika hawa asilimia 50 tu inahitajika kuhalalisha katiba mpya ina maana watu milioni 6.25 ndio wataamua katiba mpya.

   c. Tukikubali kinadharia tu kuwa hilo la "b" ni kweli kwenye taifa la watu karibu milioni 46 (makisio ya chini ya wakati wa kura ya maoni) basi kiasi cha watu watakopiga kura kutupatia katiba mpya itakuwa ni kama asilimia 13.5 tu ya Watanzania?

   HII INA MAANA GANI?

   1. Ni lazima wananchi wengi zaidi wapewe nafasi ya kujiandikisha kupiga kura kutoa maoni yao
   2. Uhalali wa kura ya maoni ufungwe na kiasi cha watu watakaojitokeza kupiga kura - yaani ili kura ya maoni iwe na uhalali basi siyo chini ya asilimia 70 (tunaweza kuweka juu kidogo) ya wapiga kura lazima wajitokeze kupiga kura.
   3. Katika wale watakaojitokeza kupiga kura siyo chini ya asilimia 70 wakikubali basi iwe KATIBA MPYA.

   Mambo hayo matatu yakikubaliwa japo kwa kiasi cha karibu na hicho, Katiba Mpya - hata kama wakiacha mchakato mwingine kuwa kama ulivyo - itatokana kwa kiasi kikubwa na watu wengi zaidi kuliko mchakato ulivyo sasa unavyopendekeza na kutengeneza. Kwani, kwa mchakato wa sasa haiitajiki watu wengi kushiriki wala kupiga kura na hivyo hailazimishi majadiliano na makubaliano mbalimbali ni kana kwamba mkakati mzima ni kutoruhusu mijadala mikali yenye kutishia kupatikana kwa katiba yenyewe!
   Last edited by Mzee Mwanakijiji; 16th April 2012 at 06:43.
   [email protected]
   The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

  2. MNYISANZU's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 21st October 2011
   Posts : 7,053
   Rep Power : 17398077
   Likes Received
   1038
   Likes Given
   83

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Kwa jinsi sheria ilivyo "wananchi tumepigwa bao na CCM mapema"

  3. MtamaMchungu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th April 2011
   Posts : 3,107
   Rep Power : 1252
   Likes Received
   1323
   Likes Given
   176

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Mwanakijiji umenifungua macho sikuliona hili jambo. Binafsi nilipoteza kitambulisho cha mpiga kura, kama hakutakuwa na uandikishaji mpya, sitapiga kura.

   Siku zinavyozidi kwenda naanza kuona dalili za hii katiba kuishi muda mfupi. As I said on your other post, kilichobaki ni damage limitation. Tuhakikishe tunapata at least a framework itakayowezesha kupata viongozi waliochaguliwa na watu na sio waliojichagua wenyewe ili tuje tutengeneze katiba ya watu.

  4. Lyimo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 7th March 2006
   Posts : 3,798
   Rep Power : 26586
   Likes Received
   1979
   Likes Given
   825

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Kama kweli serikali hii imeamua kwa dhati kwamba tupate katiba mpya yenye ridhaa ya wananchi wake, basi italifanyia kazi swala hili la msingi pamoja na mengine. Ila ninawasiwasi mkubwa kwenye kutekeleza hili,Kama ilishindikana kurekebisha daftari la jimbo la Arumeru katika uchaguzi mdogo kwa sababu za ajabuajabu, sembuse nchi nzima itawezekana? Nikweli tunahitaji katiba mpya, ila mazingira ya upatikanaji wake hatujayafanyia kazi.
   "Wisdom is not a product of schooling, but of the lifelong attempt to acquire it"

  5. Mzee Mwanakijiji's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2006
   Location : Kijijini
   Posts : 32,118
   Rep Power : 87995664
   Likes Received
   24672
   Likes Given
   13382

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Binafsi ningekubali kidogo uhalali wa mchakato huu endapo sheria ingefanyiwa marekebisho kutoa uwezekano wa watu wengi zaidi kuhusisha ama katika mjadala au katika kupiga kura. Kwa sasa hivi, inaonekana watu wengi watahusishwa kwenye mjadala lakini kwenye kura ya maoni - hasa ikitokea voters suppression - basi watu wachache wanaweza kujitokeza kupiga kura!!
   [email protected]
   The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

  6. Kimbunga's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 4th October 2007
   Location : Jimboni kusaka ridhaa
   Posts : 10,998
   Rep Power : 7214
   Likes Received
   5186
   Likes Given
   1702

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Quote By Mzee Mwanakijiji View Post

   Mkuu MMM suala la kuwaaandikisha watu wengi ni muhimu zaidi. Pia baada ya kuboresha daftari kuwe na elimu tosha ya uraia na umuhimu wa kupiga kura ya maoni ili watu wengi wajitokeze siku ya kura ya maoni. Tume ya Katiba mpya na Tume ya Uchaguzi zijitahidi kutoa elimu ya uraia na umuhimu wa kura ya maoni. Pia vyama vya siasa vipewe nafasi ya kupiga kampeni kama ilivyokuwa kwenye Mchakato wa Kura ya Maoni huko Kenya.

   Ikitolewa elimu ya kutosha tutapata wapiga kura wengi na ule wasiwasi wa watu 6.25 milioni unaweza kupunguzwa.

   Suala la 70% naona kama hiyo % iko juu. Naona sehemu nyingi maamuzi hufanywa kwa kuzingatia 50% yaani anayepata 50%+ anakuwa ameshinda.

  7. Mzee Mwanakijiji's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2006
   Location : Kijijini
   Posts : 32,118
   Rep Power : 87995664
   Likes Received
   24672
   Likes Given
   13382

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Quote By Kimbunga View Post

   yeah inawezekana lakini hatari yake ni kuwa miaka inayokuja kuna watu watalalamika kuwa wananchi wengi hawakushirikishwa. Kumbuka kuwa katiba ya sasa inalalamikiwa sababu mojawapo ni kuwa watu hawakushirikishwa. Sasa endapo itatokea kuwa watu waliopigia kura ni milioni 2 au 3 kuna kizazi kitakuja na kusema katiba hiyo haikutoka kwa wananchi kweli!! Halafu watu kama Kenya wao walifunganisha kura ya katiba mpya na idadi ya majimbo - sheria yao ilisema pamoja na kutumia asilimia hamsini kukubali kuwa pia "at least twenty-five percent of the votes cast in at least five of the eight provinces".

   Sisi tumeiweka huru sana; fikiria kwa mfano (na ninaliona hili sasa) wapiga kura wengi (ya wale asilimia 50) wanatoka mijini zaidi je watu wakijijini watasema wamewakilishwa? au fikiria kama wapiga kura wengi wa ile asilimia 50 watatoka kwenye mikoa mitano tu (Dar, Mwanza, Tanga, Arusha na Mbeya) je ni sawa kwa mikoa mingine?
   [email protected]
   The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

  8. Kasimba G's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th January 2011
   Location : Dar es Salaam
   Posts : 2,020
   Rep Power : 95447
   Likes Received
   654
   Likes Given
   918

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Mimi kuna kitu nina wasiwasi nacho na sijawahi kuki-expose, niliishafanya random research huko mikoani sehemu furani, nikakuta wanakijiji wengi tuu say asilimia more than 80 walipiga kura eneo husika lakini kwenye daftari wanaindicate kuwa asilimia 35 wamepiga kura, Kuna hiden agenda hapo! Daftari la kupiga kura silo lenyewe, limeboreshwa kupita kiasi sasa imagine asilimia nearly 20 hawakupiga kura tume inasema asilimia 65 hawakupiga kura! Wengine wametoka wapi?

   Naona zoezi namba moja lisiwe kuongeza wapiga kura, liwe kuandikisha upya ili, liwaondoe wapigakura hewa ambao according to my random research ni kama atmost 40% hivi

  9. Mzee Mwanakijiji's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2006
   Location : Kijijini
   Posts : 32,118
   Rep Power : 87995664
   Likes Received
   24672
   Likes Given
   13382

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Kasimba kwani uchaguzi mkuu wa 2010 walisema wangapi wamejiandika kupiga kura? na wangapi walipiga? halafu wakafurahia ushindi wa "asilimia 61.2" ya wapiga kura which in reality was about 30 ya waliojiandikisha kupiga kura?
   [email protected]
   The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

  10. Kasimba G's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th January 2011
   Location : Dar es Salaam
   Posts : 2,020
   Rep Power : 95447
   Likes Received
   654
   Likes Given
   918

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   ni below 50%, lakini siyo kweli, ila nadhani kuna wapigakura wa akiba ambao ni wengi saana tuu, yeah, kuna baadhi ya maeneo turnup haikuwa nzuri lakini it is not to that extent, tatizo ni hao wa akiba akina noname bin noname!

  11. jouneGwalu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th April 2011
   Location : Studio
   Posts : 2,638
   Rep Power : 5669065
   Likes Received
   1606
   Likes Given
   2369

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Hilo unalolisema ni linafahamika sana na hzo njia mbadala unazoshauri pia zinafahamika sana!
   Ninachotaka kusema ni kuwa, hali imewekwa hvyo kwa malengo maalumu.
   Poti hapa hamna muandika katika mpya, we umewahi kuona wapi watu kwenye hatua za mwanzo tu za kujenga kitu kipya wanazungumzia marekebisho? Ndivyo ilivyo ukihoji masuala ya muenendo kwanzia sheria ya mchakato, uteuzi wa tume na wajumbe wake utaambiwa ooh hatuwezi kuwa wakamilifu ndio maana kuna nafasi ya kufanya marekebisho baadae!
   Hamna katiba mpya hapa, nasubiri niuone huo waraka ulioandaliwa kwenda kwa wakuu wa mikoa na wilaya hapo ntakukumbusha tena kuwa Hamna Katiba Mpya hapa.
   Toka 1985 hadi sasa pale Ikulu hajawahi kukaa KIONGOZI tumeweka majizi, wahuni na wasanii wameasisi jamii ya kipuuzi , majuha na mazuzu......
   Jamii ya namna hii haiwezi kuandika Katiba Mpya.

  12. zumbemkuu's Avatar
   JF Bronze Member Array
   Join Date : 11th September 2010
   Location : street dweller
   Posts : 8,636
   Rep Power : 355221033
   Likes Received
   4046
   Likes Given
   13808

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   hivi hakuna uwezekano kwenye hiyo katiba kukawepo sheria kuwa kila aliyejiandikisha kupiga kura lazima apige kura hata kama ni mgonjwa?
   ''Overcome the devils with a thing called love'' bob marley

  13. Kimbunga's Avatar
   JF Platinum Member Array
   Join Date : 4th October 2007
   Location : Jimboni kusaka ridhaa
   Posts : 10,998
   Rep Power : 7214
   Likes Received
   5186
   Likes Given
   1702

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Quote By Mzee Mwanakijiji View Post
   yeah inawezekana lakini hatari yake ni kuwa miaka inayokuja kuna watu watalalamika kuwa wananchi wengi hawakushirikishwa. Kumbuka kuwa katiba ya sasa inalalamikiwa sababu mojawapo ni kuwa watu hawakushirikishwa. Sasa endapo itatokea kuwa watu waliopigia kura ni milioni 2 au 3 kuna kizazi kitakuja na kusema katiba hiyo haikutoka kwa wananchi kweli!! Halafu watu kama Kenya wao walifunganisha kura ya katiba mpya na idadi ya majimbo - sheria yao ilisema pamoja na kutumia asilimia hamsini kukubali kuwa pia "at least twenty-five percent of the votes cast in at least five of the eight provinces".

   Sisi tumeiweka huru sana; fikiria kwa mfano (na ninaliona hili sasa) wapiga kura wengi (ya wale asilimia 50) wanatoka mijini zaidi je watu wakijijini watasema wamewakilishwa? au fikiria kama wapiga kura wengi wa ile asilimia 50 watatoka kwenye mikoa mitano tu (Dar, Mwanza, Tanga, Arusha na Mbeya) je ni sawa kwa mikoa mingine?
   Mkuu hapo kwenye blue nadhani ndipo penye shida. Hiyo 50%+ inaweza kuwepo lakini pia tuifunganishe kwenye maeneo ama kwa aina yoyote ile ili tupate uwakilishi wa kila eneo. Kwa kweli huenda 50% ikaja toka mijini na vijijini wakawa hawana uwakilishi wa kujivunia japo tunaambiwa more than 70% wa Watanzania wanaishi vijijini. Naona sisi tumeangalia Bara na Zanzibar tu kwamba 50%+ bara na 50%+ Zanzibar!

  14. Mzee Mwanakijiji's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th March 2006
   Location : Kijijini
   Posts : 32,118
   Rep Power : 87995664
   Likes Received
   24672
   Likes Given
   13382

   Default Re: Kutofunganisha Kura ya Maoni na Idadi ya watakaopiga kura ni TATIZO KUBWA lenye MKAKATI

   Na hili ni rahisi kuliona hasa kwa kuangalia mgawanyo wa kura za uchaguzi uliopita (distribution of votes) ukichora kwenye graph unaweza kuona kabisa ni maeneo gani CCM ilishinda na wapi upinzani ulishinda..
   [email protected]
   The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...