Re: Taarifa ya Mwaka:Miaka 3 Baadaye... Asanteni!

By
Mzee Mwanakijiji
Leo Machi 1, 2009 ni miaka mitatu tangu tuanze kuandika kama wanaharakati na kuanza matangazo yetu yenye kujenga hoja mbalimbali. Ni miaka mitatu ambayo imetimia ndani yetu moto wa mwamko mpya ukizidi kuwaka na kuchochewa kila siku kama tanuru ya kufua chuma!
Katika kuangalia mwaka uliopita na kutazama mwaka huu mpya tumeandaa ripoti yetu hii ya shughuli zetu kama tulivyofanya mwaka jana. Kwa mara ya kwanza tumeenda mbele zaidi kwa kuweka mambo mengi wazi ambayo tunaamini kwa wale mashabiki, wanachama na wanaotuunga mkono kuweza kufahamu.
Tunatumaini taarifa hii ni kile kidogo tunachofanya katika kuwajibika mbele zenu.
Kwa unyenyekevu mkubwa naomba kuwasilisha.
Hii nayo iwe ushuhuda!
M.M. Mwanakijiji
Mzee Mwanakijiji,
Laiti wote tungekuwa tuko wazi namna hii na hata kuonyesha nia, madhumuni na mpaka gharama na michango kaa ulivyoonyesha, tungefika mbali sana!
Amani Iwe Nanyi,
Camerlengo
Plu Camerlenghi- Revolutionary Right Reverend Kishoka
"Any existence deprived of freedom is a kind of death." Gen. Michel Aoun
'Who comes to give greeting to the Inkosi-kaas? Who would taste her kiss, whereof the fruit is death? I, the Woodpecker, I, the Slaughterer, I the Swiftfooted! I, Umslopogaas!"
Follow Us Here