| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
|
#1 | |||||||||||
|
||||||||||||
|
Views: 2175
|
||||||||||||
|
#2
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Wana inferiority complex so wanakomaa na issue moja ili iwatoe.wamesahau yaliyowapeleka bungeni ...
|
|
#3
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Tatizo lao, ndugu KGM, ni kwamba Wabunge wa Kigoma hawana ushirikiano katika masuala yanayohusu maendeleo ya kwao Kigoma. Kama ulivyosema Serukamba ni mtetezi mkuu wa Mafisadi na alishiriki kwa nguvu zote kumsimamisha Zito bungeni wakati ule wa suala la Buzwagi. Ndugu yetu Msambya ni mwanasiasa aliyefilisika kimawazo na ndiyo maana uwakilishi wake ni wa udini utadhani wana-Kigoma walimtuma Bungeni kushughulika na maswala ya dini. Katika hali kama hiyo si rahisi Wabunge kama hao kusaidia kuleta maendeleo katika majimbo yao. Zito ni mtetezi wa Watanzania wote kwani ni yeye pamoja na baadhi ya Wabunge kama Dr. Slaa, Mwakyembe, Anna Kilango, n.k. walioibua maovu ya Richmond (Rich-Monduli), EPA, n.k. ambayo madhara yake ni kwa Tanzania yote hata Kigoma. Mimi nafikiri wa kuulizwa zaidi ni akina Serukamba na Msambya kama wananchi wa Kigoma waliwatuma kwenda Bungeni kutetea mafisadi na udini badala ya matatizo sugu ya Kigoma kama usafiri, umeme, maji, n.k. Ushauri wangu kwa wana-Kigoma, hakikisheni Serukamba na Msambya hawarudi Bungeni.
|
|
#4
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Kigoma ilaumuni CCM na si zaidi ya hapo mmejitakia mashida haya wenyewe .Zitto anasimamia Taifa angalau na wengine je ?
|
|
#5
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Sijamsikia hata akinyenyua mdomo wake mh ZITO. Hajui kama sisi ndio tumempeleka bungeni. watu wameitwa tu kuchukua cheque benk hawajui hata zina shilingi, mh Zito kimya kabisa na niwapiga kura wake kabisaaa. LAKINI MAMBO MENGINE ANAONGEA MNO TENA KWA POINT KABISA. HEBU ANGALIA SWALA LA DOWNS, ANASEMA NCHI ITAKUWA GIZANI, HIVI SISI KIGOMA TUNA UMEME? HALIONI HILO, HILO SIYO GIZA?. HAYA NDIO MATATIZO YA KUCHAGUA WENYEJI WA DSM, ANGEKUWA HAPA KIGOMA GIZA TOTORO TUNALO KILA SIKU HAPA. LENGO SI KUMCHAFUA LAKINI KUNA HAJA YA KUTUTETEA NA SISI WAPIGA KULA WAKE HIVI KWA JINSI ZITO ALIVYO MSEMAJI MZURI ANASHINDWA HATA KULISEMEA KWA NGUVU SWALA LA USAFIRI WA RELI KWELI? USAFIRI KIGOMA UKIENDA DIRISHANI HUPATI TIKETI. KILA SIKU WANAKWAMBIA ZIMEISHA ILI WAZIRUSHE. DAR-KIGOMA DARAJA LA TATU BILA LAKI MOJA HUPATI. HIZO ZOTE NI KERO KWA WANAKIGOMA WANAHANGAIKA KWELI. SASA TUNAHITAJI WATU WATUSEMEE NA WAYAKEMEE HAYA. LABDA KWA KUWA WAKO JIJINI DAR BASI NDIO HIVYO TENA KIMYA TU. Last edited by KGM; 28th February 2009 at 05:18 PM.. |
|
#6
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Sitasahau, ilikuwa ni mwaka 2005, hapo nilipopata fursa kufika kigoma, hakika nilibaki nimeduaa kama Tahira, nilimuuliza mwenyeji wangu tumefika? akanijibu tumefika, hakika tukashukatoka ndani ya lile gari Moshi na kuelekea Mjini, nikawa najiuliza mjini ndiyo wapi? Hakika siku ya kwanza ikapita ya pili ikapita hata nisijui ni wapi panaitwa mjini Kigoma, niliendelea kutazama vile vilima vilivyozunguka pale station, nikaendelea kusawili yale mazingira hali nzuri inayofaa kilimo, cha kushangaza watu wote wanacheza Bao na kahawa nyingi sana.............!!!, KGM; nataka nikueleze haya, ninyi ni wengi wa maneno na hamfanyi kazi, Tazama kama umefika pale kwenu mjini hakuna jengo jipya hata moja, majengo unayaona pale Kilimahewa na kule Jeshini, unajua kwa nini ? KGM; wabunge wenu wameshawasoma kuwa kutwa nzima nyie mnang'ang'ania habari za dini sasa ni kwanini msitetewe kwenye maswala ya dini tu? KGM; mshukuru Mola hata kwa kumpata huyu Kijana mbunge (zito) nadhani baada ya kutetea Taifa zima sasa ataelekeza nguvu zake hapo kigoma , naomba usitie shaka siku si nyingi neema itafunguka. |
|
#7
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Nadhani si sahihi kuwajumuisha wabunge wa Mkoa wa Kigoma katika kundi moja kimtazamo kwani huwezi kumfananisha Zitto na Serukamba na hata Kaborou kabla yake, that will be criminal. Zitto anaangalia matatizo ya kimaendeleo kitaifa wakati Serukamba na hata Kaborou kabla yake ni wabunge wa maslahi yao binafsi na ndio maana Serukamba yuko mstari wa mbele kuwatetea mafisadi bungeni kwani huko ndiko anakopata mshiko wake na ndio maana siku Lowassa alipolazimishwa kuachia ngazi juu ya kashfa ya Richmond inasemekana Serukamba alibubujikwa na machozi kwa kuondokewa na mfadhili mkuu!! Kaborou yeye aliwaambia CCM bei yake, wakamnunua na wakamhonga ubunge wa Afrika Mashariki ndio ikawa mwisho wake na watu wa Kigoma!! WanaKigoma Mtakuwa mnajidhalilisha sana tena sana kama mtamrudisha Serukamba bungeni 2010, mnao watu waadilifu wengi watakaoweza kuwarepersent effectively wakujaza nafasi hiyo .
|
|
#8
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
wacheza bao ni waswahili wa pale ujiji, wengine tunachapa kazi mtindo mmoja ndugu yangu. Lakini ki ukweli kabisa anyoyatetea zito si mabaya lakini anatakiwa awatetee na waliompeleka pale bungeni. |
|
#9
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mara ya mwisho kuwa pale kigoma ni lini wewe KGM;? maana nafikiria hata sipati jibu, uliondoka lini kule KG? NAJUA UKO TOWN MKUU.. |
|
#10
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Hakuna nyumba hata moja iliyofanyiwa uthamini, wameitwa dirishani tu. Sasa wewe kama mbunge utakaa kimya kweli, na kijijini kwake mhe zito (mwandiga) kiganza----. Kwa kifupi ni jimboni kwake kabisa.
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 06:36 PM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||