Shambulio la wabunge: Mbowe unda task force ya kumuona rais
Tukio lililotokea mwanza inabidi liitwe kwa staiki yake ni tukio la kigaidi na cdm inabidi ilichukulie very serious
bila hivyo mara ya pili ataondoka mtu kabisa. ili kumfanya mkuu wa polisi afanye kazi kama inavyotakiwa inabidi
mbowe aombe kikao na Rais kikwete na kwenye kikao hicho saidi mwema lazima awepo ili atoe maelezo ya kushiba kuhusu vijana wake kuhusika ktk shambulio hili na inawezekana uongozi wa mkoa wa mwanza nao huenda unausika kwahiyo ili
kuakikisha hatua madhubuti zinachukuliwa basi lazima chadema wam involve jk kwa sababu yeye ndiye aliyewapa kazi na ndio mwenye uwezo wa kuwatimua. swala la usalama wa wabunge wake chadema inabdi ilichukulie very serious na hii ni njia mojawapo ya kuakikisha wahusika
wanaadhibiwa kikamilifu.
re: Shambulio la wabunge: Mbowe unda task force ya kumuona rais
kila kitu kuonana na rais? No. Cdm iende mwanza ikawashitaki hao wahalifu kwa wananchi. Wakati kesi ikiendelea mahakamani cdm ifanye mikutano ya hadhara mwanza kulaani vikali mashambulio hayo.
Halafu kumbe kiwia ni mwanaume? Hasikiki sana kama wenzake kina machemli na wenje
Re: Shambulio la wabunge: Mbowe unda task force ya kumuona rais
Mimi nadahani hili suala liko wazi kabisa,kipindi CCM inaadhimisha miaka 35 ya kuzaliwa kwake tulionyeshwa kwenye TV sungusungu wa CCM wenye silaha za jadi pale uwanja wa CCM Kirumba so naona hao vijana walikua sasa wanazijaribu kuona kama zina makali yanayotakiwa though am telling you hii ni hatari sana ikiachwa bila kupatiwa ufafanuzi wa kina. Hata nchi zingine mambo yalianza kidogo kidogo maana kesho inaweza ikawa ni zamu yao tena kwa kiwango cha hali ya juu.
First they came for the Jews and I did not speak
out because I was not a Jew.
Then they came for the Communists and I did
not speak out because I was not a Communist.
Then they came for the trade
unionists and I did not speak out because I was not a trade
unionist.
Then they came for me and there was no one left to speak out
for me.
By Pastor Niemoller
There is a saying in aviation "You haven't crashed until you've crashed. Until then, keep flying the plane".
Re: Shambulio la wabunge: Mbowe unda task force ya kumuona rais
Nashauri kwa sababu jeshi la policcm limekuwa likifanya kazi zake kwa misingi ya kibaguzi na uonevu, mara nyingi wameshindwa kudhibiti uhalifu, hawa waliopewa pikipiki siku hizi wamekuwa ni adui namba moja wa waendesha bodaboda lengo la wao kupewa pikipiki limekuwa siyo kwa ajili ya kulinda usalama tena bali ni kwa ajili ya ujasiliamali. Trafic ndo usiseme badala ya kukaa barabarani kuhakikisha madereva hawafanyi makosa wao wanajificha na kuvizia madereva wafanye makosa na kuwatishia notifications za shilingi 20,000/- ili madereva wajilengeshe wao wenyewe kutoa kiasi chini ya hicho ambacho hatimaye huishia mifukoni mwao. Hawa wanaoitwa wapelelezi ndo usiseme wao wanachukua pesa kwa mtuhumiwa ili wampendelee katika uchunguzi na kwa anayeshitaki naye usizani hatakwanguliwa, yapo mengi ambayo jeshi la policcm wamekuwa wakiyafanya kiasi mapendekezo yangu kama 2015 tutapata ukombozi wa kweli hili jeshi ni la KULIVUNJA na kuundwa upya.
Re: Shambulio la wabunge: Mbowe unda task force ya kumuona rais
Kumuona Kikwete juu ya shambulio la wabunge wa CHADEMA Mwanza ni kujiua kisiasa.Kwenda mahakamani pia ni kujiua kisiasa.Njia ni moja tu,CHADEMA TAIFA IENDE KUSHITAKI KWA UMMA WA MWANZA KISHA WANAMWANZA WASEME WENYEWE AINA YA HATUA ZA KUCHUKUA DHIDI YA ccm na Polisi
Follow Us Here