Mzee Mwanakijiji, hao makamanda dhidi ya ufisadi wamegawanyika makundi mawili, miongoni mwao wamo wanapinga ufisadi kwa sababu wanauchungu wa dhati na umasikini wa Watanzania ambao ufisadi umechangia kuongezeka kwa umasikini na unaendelea kuitafuna nchi na utaendelea kwa miaka kadhaa ijayo.
Kundi la pili ni la wapinga ufisadi wanaopigania nafsi zao, wanahasira kwa sababu nao wanataka share yao kwenye huo mkate na nafasi zikiwakalia vazuri, nao watafisidi vile vile hivyo nawaweka kundi moja na mafisadi tuu.Kwa mtazamo huo kuna makamanda wenye uchungu na makamanda mafisadi.
Swali ni jee ndani ya CCM, wanapigania nini?. Jibu langu la jumla ni kuwa wanapigania nafsi zao just for survival na wakishapata uhakika wa survival baada ya 2010, mtawashuhudia nao wakifisidi ushahidi ni 'time will tell'.
Kitu kibaya zaidi kuhusu baadhi ya hawa makanda ambacho mtakishuhudia ni kwa baadhi yao kuwapigia magoti mafisadi ili kuwanusuru na panga la CCM kupitishwa kugombea 2010 na wakishapitishwa, wataungana na kuwa kitu kimoja kwa ajili ya kuweka mikakati ya 2015.
Baadhi watakao piga magoti ni wale ambao nguvu ya mafisadi kuhakikisha hawateuliwi na CCM kugombea itatumika, na wakisha toswa na CCM, watatamani kukimbilia upinzani sio ili kuendeleza mapambano, bali kujaribu kuokoa mkate wao wa kila siku na nawahakikishieni, kama mafisadi watamwaga fedha kuhakikisha makamanda hawapiti, na wakihamia upinzani, ndio kwanza sasa chama kitamwaga mapesa zaidi kuhakikisha hakishindwi.
Baadhi ya makamanda watapigwa chini na hapo ndipo itakuwa mwisho wa habari yao, kitakachofuatia ni kwenda kuwalamba miguu mafisadi kwa kurejea CCM wakiwa wametahayari kama alivyofanya yule kinara wa kundi la G-55.
Hizi harakati za kujipambanua kwa pamoja na kuzungukiana majimbo ya wapiganaji zamu kwa zamu huku wakitoa michango ya shilingi 500,000 walizopewa na mshitiri, wakisindikizwa na ka 'kipindi maalum' ndani ya taarifa za habari (no 10min news clip) ya kwenye TV ya mshitiri, hizi ni nyimbo tuu za shangwe na mapambio ya kujinusuru na panga la uteuzi wa CCM mwaka 2010, baada ya hapo kutakuwa hawana hili wala lile.
Sibezi juhudi za makamanda, bali mbinu zilizotumika kuwapambanua bungeni tukianzia kwenye ripoti ya Richmond iliyotumika kumchapa bakora EL kwa kumuhukuma bila kupewa fursa ya kusikilizwa, hivyo ukamanda wao unapimwa ni kwa kiasi gani wanaweza kuzungumza kwa jazba na mapokezi makubwa makubwa kuashiria wananchi wanawakubali.
Wapiganaji wa kweli ni wale ambao wako tayari to take risk kwa kusimama mbali na uvundo kuwathibitishia watanzania kuwa huku tuliko chama kimetekwa na mafisadi, hivyo baada tuu ya kuvunjwa Bunge mwakani, wataonyesha waliposimama na wananchi watawachagua kwenye chama chochote watakacho simama nacho na hawa ndio watakuwa wapiganaji wa kweli kweli.
Wale makamanda wanaopigania nafsi zao, mtawatambua kwa kutokubali kurski nafasi zao ndani ya CCM ambako mafisadi wana upper hand. Hawa watasubiri mpaka watakapo temwa na CCM ndipo waje upande wa pili kujaribu kamari ya upinzani, hawa ndio watakao kwenda na maji kwa sababu upinzani Tanzania ni kwenye baadhi tuu ya maeneo, kuna maeneo mengi CCM inachaguliwa sio kwa sababu imekubalika sana, bali kwa sababu ya mazoea tuu na kukosekana kwa elimu ya uraia.
Kuna sehemu hata akisimamishwa mgombea kiazi vipi, atapita tuu.Kwa vile CCM ina wenyewe, na baadhi ya wenyewe hao ndio hao hao mafisadi na wengine wao ndio hao makamanda, hapa ni mwendo wa mwenye kisu kikali ndie anayekula nyama, na ili ukubaliwe kula nyama ni lazima uchague upande, either with us, or against us, maadamu wenye guvu ni mafisadi, mwenye nguvu mpishe, hao makamanda watajikuta kuliko kuriski loosing, wakijua hawawezi kuwashinda, watatumia formular ya 'if you can't beat them, join them' watajiunga nao na wote wakuwa kwenye tenga moja la samaki, na wote watakuwa ndio hao hao.
Follow Us Here