Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Sitta autamani Urais 2015

    Report Post
    Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 92
    1. #1
      Superman's Avatar
      JF Tanzanite Member Array
      Join Date : 31st March 2007
      Location : On Move
      Posts : 5,376
      Rep Power : 1810
      Likes Received
      1380
      Likes Given
      1183

      Default Sitta autamani Urais 2015

      Please note: Huu si Mkenge wa April's Fools Day. Akili zako changanya na za Mbayuwayu!

      Source 1:
      Sitta atangaza nia kuwania urais ‘akiombwa’ | FikraPevu.com

      Source 2:
      Sitta kugombea Urais 2015

      Source 3:http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=28475 (Sitta: Ninafaa Urais)

      * ATAKA KUONGOZA MIAKA MITANO AWAACHIE VIJANA


      Na Sheilla Sezzy, Mwanza

      MWANASIASA machachari ambaye pia ni Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015 na kutamba kuwa ana nafasi nzuri kutokana na sifa alizojijengea ndani ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).

      Sitta alitaja sifa hizo kuwa ni pamoja ile ya kuwa mteule wa rais, kwa awamu zote nne za uongozi taifa, tangu Tanzania ilipotaka uhuru wake, Desemba 9 mwaka 1961.

      Spika huyo mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , alisema kwa sasa anawasikiliza wananchi kama wataona anafaa na haoni ubaya wowote wa kushika nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa taifa kwa miaka mitano tu na kuwaachia vijana waendelee.

      “Mimi nawasikiliza wananchi kama wataona nafanana na rais wanayemtaka, basi nitachukua maamuzi kwa wakati huo. Sioni ubaya wowote kama wakiniachia kuongoza nchi hii hata kwa miaka mitano halafu niwaachie vijana waendelee,”alisema Sitta.

      Alisema kuwa ifikapo mwanzoni mwa mwaka 2014, kila kitu kitakuwa wazi na haweza kukataa majukumu atayopewa na wananchi wake kwani anatambua wanamuamini kwamba ana uwezo wa kuchapa kazi.

      Sitta ambaye pia ni Mbunge Urambo Mashariki na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa( NEC) ya CCM, aliyasema hayo jana muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani kufunga kampeni za udiwani za CCM, Kata ya Kirumba.

      Mwanasiasa huyo ambaye umaarufu wake umepanda kwa kasi katika miaka ya hivi karubuni kutokana na msimamo wake wa kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi ndani ya CCM, alitamba kuwa amefanya mambo mengi ndani ya Serikali ya CCM, ambayo yamesaidia kuleta mageuzi makubwa nchini.

      Alisema kadri siku zinavyokwenda rais wa Tanzania atajulikana kwa matendo yake na kubainisha kuwa mtu mbaya hawezi kubadilika kuwa mzuri kwa kipindi kifupi.

      “Sioni sababu ya mtu kuutafuta urais wakati wananchi wanaona na wanajadili kila siku ni rais wa aina gani wanayemuhitaji kutokana na mahitaji yao,”alisema

      Alisema anachofanya kipindi hiki ni kutimiza wajibu wake na wananchi ni mashahidi kila nafasi anayopewa, anatimiza wajibu wake ipasavyo na kusisitiza kuwa amefanya mengi yanayoonekana machoni pa watu na kudhihirisha kwamba ni kiongozi bora.

      Akizungumzia umri wa urais, alisema mijadala kuwa vijana hawawezi kuongoza haina msingi. Alifafanua kuwa kiongozi mzuri ni yule mwenye uwezo wa kuwaongoza wananchi na kuwaletea maendeleo.

      Alisema rais anachaguliwa na wananchi hivyo maamuzi yote ya nani anafaa kwa nafasi hiyo na umri upi, ipo mikononi mwa wananchi wenyewe.

      Katika hatua nyingine Sitta, aliwashangaa wanasiasa wanaopigana vijembe majukwaani na kueleza kwamba tabia ya kumtukana mtu mmoja mmoja, haina maana yoyote.

      Aliwashauri viongozi wa CCM kutojibu mapigo ya wapinzani na kuwataka kutumia busara kila wanapokutana na kauli chafu kwani nia ya kudumisha amani ya nchi.

      Alionya kuwa amani ya nchi ikitoweka, itakayobebeshwa lawama ni CCM na Serikali yake.

      “Kauli nyingi za majukwaani zinachochea chuki miongoni mwa wananchi, matokeo yake zinaweza kuibua machafuko na waathirika watakuwa wananchi wenyewe, tena wale wasio na uwezo wa kujiokoa,’’ alisema Sitta.

      Alisema kuwa katika miaka 50 ya utawala wa CCM, kuna mambo mengi yamefanyika na kwamba wapinzani hawana haja kubeza kwani yanaonekana kwa macho.

      Alisema kuwa katika mafanikio hayo, kuna mengi yamefanywa na Rais Jakaya Kikwete, mfano mzuri ni kampuni tano za madini kulipa kodi na wananchi kuanza kufaidika na rasilimali za nchi yao.

      Hofu ya mahasimu wake

      Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika Tamasha Vyombo vya Habari lililofanyika wiki iliyopita kwenye Ukumbi Msasanki Beach, Dar es Salaam, Sitta alieleza kuwa anashangazwa na watu wanaoweweseka wakisikia anataka kuwania urais mwaka 2015.

      "Nashangaa watu wanapata kiwewe kusikia nataka kuwania urais, kuwania urais ni haki ya kila Mtanzania na Watanzania ndiyo watakaoamua nani ni mzuri na atawafaa," alisema Sitta na kushangiliwa na waliohudhuria tamasha hilo.

      "2015 tunataka kuwa na mwelekeo mzuri, nikiwa na maana mambo ya hongo, ubadhirifu hatutaki yawe na nafasi, alisema Sitta na kuongeza:

      Alisema watu wanatumia fedha nyingi kusaka urais na hata wengine kutumia ndumba kwa kwenda Mlingotini, Bagamoyo, kwa nia ya kutaka uongozi na matokeo yake wanaposhinda lengo lao la kwanza linakuwa kurudisha fedha walizotumia.

      Source:
      Sitta kugombea Urais 2015

      MY TAKE:
      Kwa Changamoto za leo ambayo Nchi Yetu inazo, bado Mh. Samuel Sitta hana uwezo wa kuleta mageuzi ya Kimaendeleo katika Tanzania. Alipata mafasi kamili kama Kiongozi wa moja Mhimili kamili wa Kikatiba kama Spika wa Bunge kusimamia kuondoa uovu kikamilifu pamoja na Ufisadi Mwingine lakini akaamua kukumbatia uovu kuinusuru serikali yake ya CCM.

      Japo anaweza kuwa anakubalika na baadhi, Mzee Sitta hawezi kuwa udhubutu wa kutupa Tanzania tunayoiota, na hata huko Wizara ya Afrika ya Mashariki bado hatujaziona cheche zozote.
      Pasco, bucho and Pelekaroho like this.
      Kwa kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wanyonge . . . . . . “Ni heri kutoa kuliko kupokea”

    2. RukaaJuu Final

    3. #21
      Ndinani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2010
      Posts : 2,950
      Rep Power : 1532
      Likes Received
      745
      Likes Given
      237

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      Quote By nimie
      Hana akili! angekuwa mjanja angepigania kuwepo kwa mgombea binafsi, sasa anafikiri atapitia wapi? Kwa hicho chama chake hawampitishi. Akisumbua sana ataondolewa kwa zengwe lile lile la zamu ya kina mama na Asha Migiro atasimamishwa. Labda arudi CCJ.
      Ukweli ndio huo uliousema,ccm hawawezi kumpitisha kwani mkweree atamuwekea zengwe kwanza kuwa ni mzee huu ni wakati wa vijana na halafu atasema ameanza kampeni mapema!! Kama kweli anadhamilia kusimama yeye na Lowassa wasitegegeme kuwa ccm itapitisha majina yao kwahiyo inabidi wawe na falling back position.
      Superman likes this.

    4. #22
      Juma Hamis's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th March 2012
      Posts : 58
      Rep Power : 374
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      Quote By mbwagison
      Hana ubavu! Akiwa Spika wa bunge hakututendea haki hata kidogo! aliuzima mjadala wa Richmond kidikteta, je alihongwa ahadi ya kugombea Urahisi 2015? huyu mtu ni hatari sana!
      wewe ndo huna akili timamu bila sitta vita ya ufidadi ingejulikana kama leo,siyo sitta aliyezima mjadala wa ufisadi bali ni bunge la jamhuri,hivyo unataka kumanisha sitta alikuwa na nguvu kuliko bunge lenye watu zaidi ya 300,soma mambo na uyaelewe,soma nafasi ya spika bungeni na nguvu ya bunge ndo uje na mawazo yako haya ya kijima

    5. #23
      Juma Hamis's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th March 2012
      Posts : 58
      Rep Power : 374
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      Quote By Ilongailunga
      Samuel Sitta ni mtu ambaye ameitumikia serikali ya CCM zaidi ya nusu ya Umri wake wote, na yeye alikuwa mwanamtandao.Inasikitisha sana watu kuhadaiwa eti Sitta anapinga ufisadi, Sitta anatumia neno ufisadi kwa maslahi ya kisisiasa na pia kuwachafua wapinzani wake kisiasa. Si ndo huyu Sitta alipopata nafasi ya kuwa kiongozi wa serikali bungeni povu lilimtoka kuwashambulia na kuwadharilisha wapinzani,na kuitetea serikali na chama kwa kuviita "waadilifu" na wasikivu? mnaomshabia huyu gamba opportunist ni vema muangalie na mtathmini misimamo yenu ya kisisiasa.
      wewe ndo umetumwa kuukana ukweli kuhusu mzee sitta,ni kiongozi pekee mpaka sasa aliyetumikia serikali bila kashfs yoyote ,hizo unazoleta niza kuokoteleza majalalani

    6. #24
      Butola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2010
      Posts : 1,520
      Rep Power : 783
      Likes Received
      266
      Likes Given
      647

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      ...I will support him...

    7. #25
      Mpanzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th January 2011
      Posts : 418
      Rep Power : 507
      Likes Received
      93
      Likes Given
      7

      Default

      Quote By Juma Hamis
      wewe ndo huna akili timamu bila sitta vita ya ufidadi ingejulikana kama leo,siyo sitta aliyezima mjadala wa ufisadi bali ni bunge la jamhuri,hivyo unataka kumanisha sitta alikuwa na nguvu kuliko bunge lenye watu zaidi ya 300,soma mambo na uyaelewe,soma nafasi ya spika bungeni na nguvu ya bunge ndo uje na mawazo yako haya ya kijima
      Sitta sie muasisi wa vita ya ufisadi, muasisi ni Dr Slaa, Sitta hapingi ufisadi bali anapambana na Lowasa Urais 2015 period!

    8. Miaka 50

    9. #26
      Juma Hamis's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th March 2012
      Posts : 58
      Rep Power : 374
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      Quote By Ilongailunga
      Samuel Sitta ni mtu ambaye ameitumikia serikali ya CCM zaidi ya nusu ya Umri wake wote, na yeye alikuwa mwanamtandao.Inasikitisha sana watu kuhadaiwa eti Sitta anapinga ufisadi, Sitta anatumia neno ufisadi kwa maslahi ya kisisiasa na pia kuwachafua wapinzani wake kisiasa. Si ndo huyu Sitta alipopata nafasi ya kuwa kiongozi wa serikali bungeni povu lilimtoka kuwashambulia na kuwadharilisha wapinzani,na kuitetea serikali na chama kwa kuviita "waadilifu" na wasikivu? mnaomshabia huyu gamba opportunist ni vema muangalie na mtathmini misimamo yenu ya kisisiasa.
      unatumiwa vibaya na hao mafisadi,tumia akili kutadhimini mambo,vinginevyo mitizamo yako itakuozea kichwani bila kupata wa kuinunua,muulize baba yako amelifanyia nini taifa letu ukilinganisha na mzee sitta,kwanza yawezekana hajausaidia hata mtaa mnaoishi,unapata wapi wewe ujasiri wa kuukana ukweli kuhusu mh sitta.

    10. #27
      Juma Hamis's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th March 2012
      Posts : 58
      Rep Power : 374
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      Quote By Mpanzi
      Sitta sie muasisi wa vita ya ufisadi, muasisi ni Dr Slaa, Sitta hapingi ufisadi bali anapambana na Lowasa Urais 2015 period!
      bora huyu anayepambana na fisadi kubwa hapa nchini,tunamtaka mtu aliyena ujasili kama wa sitta hata kama si sitta kwa jina ila awe mtu mwenye uthubutu kama sitta na vinginevyo,hata hivyo hata kama si slaa ila tunamtaka mtu mwenye uthubutu kama slaa,unafikria kazi iko wapi,sisi kama taifa tunahitaji mtu mwadilifu na mchapa kazi.

    11. #28
      Bongolander's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Tandale
      Posts : 4,034
      Rep Power : 1417
      Likes Received
      610
      Likes Given
      44

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      Quote By Superman

      MY TAKE:
      Kwa Changamoto za leo ambayo Nchi Yetu inazo, bado Mh. Samuel Sitta hana uwezo wa kuleta mageuzi ya Kimaendeleo katika Tanzania. Alipata mafasi kamili kama Kiongozi wa moja Mhimili kamili wa Kikatiba kama Spika wa Bunge kusimamia kuondoa uovu kikamilifu pamoja na Ufisadi Mwingine lakini akaamua kukumbatia uovu kuinusuru serikali yake ya CCM.

      Japo anaweza kuwa anakubalika na baadhi, Mzee Sitta hawezi kuwa udhubutu wa kutupa Tanzania tunayoiota, na hata huko Wizara ya Afrika ya Mashariki bado hatujaziona cheche zozote
      .
      Mkuu that is your take. Lakini tunatakiwa tuangalie what will be the main issue in 2015, will CCM stand for Ufisadi like it is now? or will it have a change like one of groups within the party thinks about. Kwa sasa kilichopo hapa Tanzania ni lack of leadership, na kufluorish na kuukumbatia ufisadi hii ndio ajenda kuu ya CCM-mtandao, na itandelea hivyo wakiendelea kuwa madarakani. Hii ndio hatari kubwa tuliyonayo Tanzania kwa sasa. 2015 kwanza kabisa tunahitaji mtu ambaye atasimama kidete kuondoa haya, na kuirudisha Tanzania kwenye mstari, otherwise tutanedelea kuwa banana republic.

      Mwenye uwezo wa kuleta Tanzania tunayoitaka ni sisi wenyewe watanzania hasa vijana, si rais. Awe CCM, Chadema au CUF. Tunachotaka ni mtu anayeweza kufanya tanzania iwe ruled by rules and laws, sio by ufisadi. Tumeona kuwa watanzania wanachapa kazi, kwa hiyo kama kuna leader tunaweza kusonga mbele.

    12. #29
      Butola's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th January 2010
      Posts : 1,520
      Rep Power : 783
      Likes Received
      266
      Likes Given
      647

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      Quote By Mpanzi
      Sitta sie muasisi wa vita ya ufisadi, muasisi ni Dr Slaa, Sitta hapingi ufisadi bali anapambana na Lowasa Urais 2015 period!
      ...na wengine wanaweza wakasema Dr.Slaa anapinga ufisadi usiomhusus huku naye akifanya ufisadi ndani ya Chadema, itategemea tu una define vipi...

      ...Lakini mwisho wa siku, ni wananchi ndio watakao amua definition itakayosimama, na believe me, kama ni uchaguzi wa Samweli Sitta na Dr.Slaa, Samweli Sitta atashinda decisively...

    13. hbi
      #30
      hbi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th February 2011
      Posts : 258
      Rep Power : 471
      Likes Received
      63
      Likes Given
      65

      Default Sitta akiri kugombea uraisi mwaka 2015

      MWANASIASA machachari ambaye pia ni Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015 na kutamba kuwa ana nafasi nzuri kutokana na sifa alizojijengea ndani ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi(CCM).

      Sitta alitaja sifa hizo kuwa ni pamoja ile ya kuwa mteule wa rais, kwa awamu zote nne za uongozi taifa, tangu Tanzania ilipotaka uhuru wake, Desemba 9 mwaka 1961.

      Spika huyo mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , alisema kwa sasa anawasikiliza wananchi kama wataona anafaa na haoni ubaya wowote wa kushika nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa taifa kwa miaka mitano tu na kuwaachia vijana waendelee.


      Habari kamili hapa

    14. #31
      Gama's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th January 2010
      Posts : 4,579
      Rep Power : 1359
      Likes Received
      425
      Likes Given
      625

      Default Re: Sitta kugombea Urais 2015

      Ametangaza nia siku ya wajinga?!, hakika naye na watakaomuunga mkono watakuwa wajinga.

    15. #32
      Ilongailunga's Avatar
      Member Array
      Join Date : 18th January 2012
      Posts : 56
      Rep Power : 382
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default

      Uko sahihi mkuu, tatizo kuna baadhi ya watu wamegeuzwa kuwa mizukule ya kisiasa! Sitta kaanza kujiita "mpinga" ufisadi 2008 wakati tayari dr.slaa alishatangaza list of shame pale mwembeyanga, Sitta na kundi lake wakapora hoja hii na kuanza kuitumia dhidi ya wapinzani wake kisiasa na kuipotosha kabisa dhana ya vita dhidi ya ufisadi kama muasisi wake dr.slaa alivyoianzisha(war against corrupt system japo alitumia majina km mifano) lakini Sitta na kikundi chako wameigeuza kuwa ni war against "corrupt" individuals within his party!

    16. bht
      #33
      bht's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 9,949
      Rep Power : 2500
      Likes Received
      1434
      Likes Given
      909

      Default

      Quote By Superman
      Haaaa haaa Mkuu wangu mimi niko poa kabisa ndo kwanza nimetia timu DSM.

      Mkuu mbona mimi nakufahamu miaka sana na wala sina issue na wewe kabisa. Napenda tu unavyosimamia hoja unazoziamini.

      Kama uko Bongo, let us meet in one of the days. Naona AshaDii kule kishawafunga kamba wengi.

      Niaje habari ya Sitta kuweka hadharani nia yake ya kuwa kuishi makazi ya sasa ya Baba Mwana-Asha?
      Urongo bana SM!

      Njoo na lile deni la Ngabu basi...lol

    17. #34
      mikatabafeki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2010
      Posts : 4,840
      Rep Power : 1398
      Likes Received
      766
      Likes Given
      1463

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      sijui Taifa la vijana litafika lini????
      when love goes wrong,nothing goes right.

    18. #35
      Kima Mchanga's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 3rd October 2011
      Location : Dynamic
      Posts : 4,501
      Rep Power : 11226
      Likes Received
      608
      Likes Given
      446

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      "Mhe" 6 ni mwanasiasa kigeugeu,mnafiki na ambaye anasukumwa na tumbo lake kufikiri!
      Hafai CCM,Hafai upinzani,hafai kokote!

    19. #36
      Nyakarungu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st May 2011
      Posts : 209
      Rep Power : 3115
      Likes Received
      122
      Likes Given
      101

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      Aliwahutubia akina nani hiyo jana, maana jana alifanya mkutano kiwanja cha mwembe sangara, na chadema tulikuwa uwanja wa manoko mita kama 600 hivi toka walipokuwa wao, waliahirisha mkutano wakingojea tumalize ili nao wapate watu, na baada ya kuona tunakaribia kumaliza muda wa kisheria, wakaamua kuweka kikao chao cha chama hapohapo ndio maana hakujadili uchaguzi wa udiwani akawa anawajadili waccm na urais

    20. #37
      Songoro's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th May 2009
      Posts : 2,222
      Rep Power : 0
      Likes Received
      487
      Likes Given
      21

      Default re: Sitta autamani Urais 2015

      Sitta akitangaza nia ni sahihi wala si mapema tena anapongezwa,akitangaza Kabwe ni mapema,mbinafsi,anatumiwa n.k

    21. #38
      mgt software's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 1,750
      Rep Power : 784
      Likes Received
      141
      Likes Given
      201

      Default Re: Sitta autamani Urais 2015

      sidanganyiki leo siku ya hamnazo
      "Mtoto wa Maskini Hachagui Malezi, Tanganyika siyo Masikini Masikini ni wewe Unayehonga Haki yako Kwa Mafisadi" Bamugileki

    22. #39
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,484
      Rep Power : 6170
      Likes Received
      3058
      Likes Given
      1020

      Default Re: Sitta autamani Urais 2015

      Safi sana waendelee kujitokeza tu tumechoka na tetesi
      CCM na CDM vyote ni vyama vya siasa vinavyoongozwa na wanasiasa; tofauti yao kubwa ni moja kwamba kimoja kina dola kingine kinataka kushika dola.

    23. #40
      NALO LITAPITA's Avatar
      Member Array
      Join Date : 25th August 2011
      Posts : 94
      Rep Power : 410
      Likes Received
      22
      Likes Given
      1

      Default Re: Sitta autamani Urais 2015

      Ikiwa walitenda vile katika mti mbichi (uspika) vipi katika mti mkavu (urais)?

    Page 2 of 5 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...