Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Zitto aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na NIPASHE jijini Mbeya, alikokuwa amekwenda kuongeza nguvu katika kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kiwira wilayani Rungwe.
Alisema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho kwa sababu anaona timu ya sasa ya uongozi wa chama hicho inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza kwa miaka mingine mitano ijayo.
“Sina interest (nia) na sifikirii kama nitagombea uongozi ndani ya chama katika uchaguzi wa ndani wa Chadema mwaka huu, naona timu iliyopo inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza chama,” alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Alisema ingawa katika uchaguzi uliopita alijitosa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho, lakini safari hii nafsi yake haimtumi kufanya hivyo kwa kuwa ana imani kuwa uongozi wa sasa unastahili kuendelea kuwa madarakani kwa manufaa na maslahi ya chama na Watanzania kwa ujumla.
Chanzo: Gazeti la Nipashe
UPDATE: Kairudia kauli hii Juni 16, 2012 akiwa Iringa (M4C)
"Nimeamua kugombea Uenyekiti wa Chadema sababu nimeona Chama kimepoteza mwelekeo na kimekuwa cha kikanda zaidi na baadhi wanajinufaishi zaidi na Chama, hivyo lengo langu ni kukifanya Chama kiwe na sura ya kitaifa tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo chama ni cha wachache mwenyekiti ni dhaifu na chama kina makundi"
"Nimeamua kubatilisha uamuzi wangu wa kugombea uenyekiti wa CHADEMA sababu nimeridhika na hali ndani ya CHAMA na nina Imani na Mwenyekiti wetu aendelee kutuongoza"
Sitagombea ubunge wa Kigoma Kaskazini mwaka 2010. Najiandaa kugombea kati ya Kahama, Kinondoni.....kwani watu wa huko wamenitumia ujumbe kuwa wananiitaji na mimi nimetuma watu wangu wafanye utafiti wa kisayansi ili niamue nikagombee wapi"
"..................Sitagom bea tena Ubunge mwaka 2010 nataka nijiandae kwenda kufundisha kwani iyo ndiyo ndoto yangu ya muda mrefu"
"Nitagombea Ubunge wa Kigoma Kaskazini mwaka 2010"
".....ndiye alietoa wazo la CHADEMA kwenda kuonana na rais kuhusiana na suala la katiba mpya"......(Ufafanuzi ulitolewa kuhusiana na suala hili kuhusu kikao gani kilitoa maamuzi hayo)
The latest kauli......"Sitagombea Uongozi ndani ya CHADEMA"
Hizi ni kauli za mtu mmoja, lakini kwasabu ya mapenzi yaliyopita kiasi cha kuwezo kupofua upeo mtu katika kufikiri, mashabiki either hawazikumbuki au wamezisahau haraka sana......hapa ndipo tatizo la msingi lilipo.....
naona fitna zimeanza kwa kuwa uchaguzi hauko mbali sn! mbowe na slaa mawesema kauli ngapi zinazogongana! siasa ndivyo ilivyo. zitto alisema maneno yale kwa malengo anayoyajua mwenyewe. usipandikiza chuki dhidi ya zitto. ni mtu muhimu sn ktk chadema
Zitto maji yamemfika shingoni, hana cha kufanya tu, anajikaza kisabuni. Nna uhakika hata Mwenyekiti kisha ona madudu yaliyopo makao makuu, mchumba kuwa bosi? Dah! hatari kubwa sana.
Zitto kajionea aah, bora akae pembeni awaachie wenye uchu wa madaraka watoane roho, hajasahau yaliyomkuta.
System At Work
"nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe
Re: Zitto kabwe:sitagombea cheo chochote ndani ya chama
By Tume ya katiba
Na angethubutu kugombea tu angeundiwa TUME. Kasoma alama za nyakati. Bora awe nje ya uongozi wapange wanayoyataka.
Kwa hizi propaganda unajisumbua bure. Chadema c sisi m, ni wanasayansi katika politiki, tulia kijana subiri kuwa mpinzani tu!
wakati Cuf wanataka kuchukua nchi mwaka 2000 CCM walikuja na single ya kusema Cuf ni waislamu na kwa sasa wanadai sisi Chadema ni chama cha wakristo sasa CCM nacho ni cha watu gani? Watu wakajibu mashetaaaaaniiiiii.!---Wana Kigoma.
....Pamoja na kansa ya uongozi wa CCM watu wataendelea kukichagua,au watu wanaweza wakachoka na kusema potelea mbali wakachagua chama KINGINE....Julius. Kambarage. NYERERE"
Wametuonyesha Jeuri ya ukaburu,tuwaonyeshe jeuri ya Umkhontho we sizwe kupitia Red Brigade.Tukiwaonyesha woga wetu, itakua silaha imara zaidi kwao kutumaliza-Ben Saanane
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama chake katika Uchaguzi wa ndani wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Zitto aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na NIPASHE jijini Mbeya, alikokuwa amekwenda kuongeza nguvu katika kampeni za uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kiwira wilayani Rungwe.
Alisema kuwa hana nia ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho kwa sababu anaona timu ya sasa ya uongozi wa chama hicho inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza kwa miaka mingine mitano ijayo.
“Sina interest (nia) na sifikirii kama nitagombea uongozi ndani ya chama katika uchaguzi wa ndani wa Chadema mwaka huu, naona timu iliyopo inatosha na inafaa kuendelea kukiongoza chama,” alisema Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Alisema ingawa katika uchaguzi uliopita alijitosa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho, lakini safari hii nafsi yake haimtumi kufanya hivyo kwa kuwa ana imani kuwa uongozi wa sasa unastahili kuendelea kuwa madarakani kwa manufaa na maslahi ya chama na Watanzania kwa ujumla.
Chanzo: Gazeti la Nipashe
UPDATE: Kairudia kauli hii Juni 16, 2012 akiwa Iringa (M4C)
Kibano alichokipata wakati alipotaka kugombea uwenyekiti wa CHADEMA, ndio sababu kubwa ya kukaa pembeni safari hii.
Vile vikao vya wazee havikuwa bure, bali viliambatana na vitisho vya kuhatarisha maisha yake. Hali hii iomemfanya Zitto kukiogopa sana chama chake kuliko hata watanzania au hata CCM kAMA WENGI WANAVYOFIKIRI.
Huo ni uamuzi wa Busara, kwani hawa watu wa CHADEMA hawajali maendeleo, hata hivyo usingepata hata kama ungegombea mkwani dDHAMBI YAKO NI KUWA HUKUZALIWA KILIMANJARO/ARUSHA.
Bora aache kugombea maana uhusiano wa Zitto na Jack Zoka ni habari mbaya kwa wapambanaji. Uhusiano kati ya Zitto na Jack Zoka ambao uliwekwa wazi na vyombo mbalimbali ni taarifa mbaya kwa wanasiasa na wananchi wanaoipenda taifa lao la Tanzania. Uhusiano huu wa Zitto na Jack Zoka ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa TISS (usalama wa taifa) umeripitiwa kuwa na historia ndefu tangu wakati wa uchaguzi mkuu. Wakati Zitto anajitapa kuwa anatetea maslahi ya wananchi, mshirika wake wa chanda na pete Jack Zoka anatuhumiwa na wanasiasa na wanachi kufanya kazi ya kuwadhuru badala ya kulilinda taifa. Kama mshirika wa Zitto anadhuru wananchi ni wazi kuwa naye Zitto ana masalahi binafsi na mabaya kwa wananchi. Maana ukitaka kujua tabia ya mtu, uliza tabia ya rafiki yake. Ni jambo la kusikitisha Zitto kuwa na uhusiano na huyu mfanyakazi wa usalama wa taifa anayedhuru watu na wakati huohuo anajidai kuwa ni mpambanaji. Uhusiano wa Zitto na Jack Zoka ulishawekwa wazi kuwa walikuwa wanawasiliana kwa simu mara kwa mara wakati wa kipindi cha uchaguzi. Tuwe macho na urafiki wao na ambao si mwema hata kidogo kwa wanasiana na wananchi wenye uchungu na taifa letu.
Wana JF wenye mapenzi mema kwa CHADEMA, nadhani ni muda muafaka sasa kuanza kutoa maoni kuhusu chama chetu hasa uongozi wake maana uongozi ujao ndio utatupa serikali 2015. kwanza nimpongeze sana Mbowe kwa kweli ameonyesha ujasiri mkubwa na ameongoza chama kwa ujasiri na ukakamavu mkubwa.
Huwezi kuitaja chadema ya leo bila kumtaja Mbowe. Baada ya kazi kubwa na ili kuonyesha chadema kina watu wazuri wengi wanaoweza kuongoza, ningeshauri tu asigombee tena akae pembeni ila abaki kwenye vikao muhimu vya chama.
Nashauri Dr Slaa sasa angeandaliwa kuwa Chairman, Zitto Kabwe awe makamu Bara, atafutwe katibu mkuu msomi mzuri ambaye anaweza kuratibu shughuli za chama kisomi, Naibu katibu pia awe msomi mzuri, tuwe na graduates makatibu wa kila jimbo la uchaguzi ambapo kazi zao itakuwa kufanya uratibu wa chama, hope chadema tutakuwa tumepiga hatua zaidi towards state house. Ni maoni tu. Peoplessssssssssssss Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Wana JF wenye mapenzi mema kwa chadema, nadhani ni muda muafaka sasa kuanza kutoa maoni kuhusu chama chetu hasa uongozi wake maana uongozi ujao ndio utatupa serikali 2015. kwanza nimpongeze sana Mbowe kwa kweli ameonyesha ujasiri mkubwa na ameongoza chama kwa ujasiri na ukakamavu mkubwa. Huwezi kuitaja chadema ya leo bila kumtaja Mbowe. Baada ya kazi kubwa na ili kuonyesha chadema kina watu wazuri wengi wanaoweza kuongoza, ningeshauri tu asigombee tena akae pembeni ila abaki kwenye vikao muhimu vya chama.
Nashauri Dr Slaa sasa angeandaliwa kuwa Chairman, Zitto Kabwe awe makamu Bara, atafutwe katibu mkuu msomi mzuri ambaye anaweza kuratibu shughuli za chama kisomi, Naibu katibu pia awe msomi mzuri, tuwe na graduates makatibu wa kila jimbo la uchaguzi ambapo kazi zao itakuwa kufanya uratibu wa chama, hope chadema tutakuwa tumepiga hatua zaidi towards state house. Ni maoni tu. Peoplessssssssssssss Powerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Una matatizo mkubwa weye!
Mbowe aondoke?
Halafu chama amwachie nani?
"If you don't know where you are going, any road will get you there-nowhere”
Una matatizo mkubwa weye!
Mbowe aondoke?
Halafu chama amwachie nani?
Unataka kutuambia kuwa Mbowe pekee ndie anaweza ndani ya Chadema? Chadema ni chama kikubwa kwa sasa nadhani tutakuwa tunaonyesha njia kama tukiendelea na utaratibu wetu wa kubadilishana kijiti hata kama tuna kiongozi imara kama Mbowe. Nyerere alikuwa kiongozo shupavu ila alifika mahali akaonyesha ukomavu wa kisiasa akang'atuka
Follow Us Here