Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Zitto: Ndio ninautaka urais

    Report Post
    Page 1 of 43 12311 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 856
    1. #1
      Mohamedi Mtoi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th December 2010
      Location : Lushoto - Kwemakame.
      Posts : 2,048
      Rep Power : 24548
      Likes Received
      3125
      Likes Given
      354

      Default Zitto: Ndio ninautaka urais

      Mbunge mahiri na machachari kutoka chama makini Zitto Zuberi Kabwe ameweka wazi kuwa anautaka uraisi lakini akiwa atapata ridhaa kutoka kwa chama chake na wananchi kwa ujumla wao,
      NDIO NATAKA KUWA RAIS - Zitto Kabwe


      Kwanza niseme wazi kabisa kabisa kuwa Urais ninautaka.

      Ninaamini ninao uwezo wa kuwa Rais. Ninaamini nina uzalendo wa kutosha na utashi wa kuleta mabadiliko stahili wa namna nchi yetu inavyoongozwa. Ninajua kuwa nchi yetu imesahau maendeleo ya watu na kujikita katika maendeleo ya vitu. Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo (styles) badala ya mambo ya msingi (content). Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika. Ninajua nchi yetu inahitaji Uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa (transformation) badala ya mabadiliko ya juu juu (cosmetic change). Ninajua 'transformation' inahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi na hasa mabwana wakubwa wa nchi za magharibi mfano kuzuia nchi yetu kuuza malighafi tu. Ninajua rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya Umma ni kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi. Ninajua rasilimali kama Madini, Mafuta na Gesi, Ardhi n.k. ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu.


      Hivyo, nchi inahitaji Kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi. Sio kazi rahisi lakini ni kazi ambayo lazima Mtanzania mmoja aifanye. Mimi nataka kuifanya. Nina uwezo wa kuifanya.

      Hata hivyo kazi hii hata kama naitaka ni lazima wenye nchi waamue kunipa kazi hii. Ni lazima kwanza Chama changu kiseme wewe ndio mwanachama unaestahili kuifanya kazi hii. Ni lazima Watanzania wengi waseme wewe ndio mwananchi mwenzetu unayeweza kuchukua jukumu hili. Kuitaka tu haitoshi. Ni lazima wananchi wakuamini na kukupa jukumu hili.



      Sasa kama wananchi watasema huyu Zitto anapaswa kubeba jukumu hili mwaka 2015 tuache iwe. Kama watasema hapana wewe bado mpaka mwaka 2020 au hata 2025 tuache iwe hivyo. Pia Kama hawataki kabisa tuache iwe hivyo.

      Mjadala wa umri wa kugombea Urais imekuwa mjadala mkali sasa. Mjadala huu baadhi ya watu kwa sababu wanazojua wao wameamua kuita ni mjadala wa Zitto na January. Kwamba ni mjadala unaobagua Wazee. Mjadala unaopandikiza chuki na sumu za kibaguzi. Kwamba ni mjadala wa Kitabaka na kuwa Zitto na January sio tabaka stahili la vijana walio wengi. Sitamsemea January, nitajibu baadhi ya hoja za mwandishi wa makala mojawapo kama Zitto. January akitaka atamjibu naye kivyake.

      Mwandishi anasema yeye hapingi hoja ya umri, bali anapinga aina ya watu wanaoshadidia hoja hiyo. Anaipenda hoja ila hapendi watoa hoja. Hoja nzuri lakini Zitto na January wabaya. Amelisema hilo mwanzo kabisa wa makala yake. Kwa hiyo kwake yeye hoja ingeletwa na vijana wengine asingekuwa na shida wala isingekuwa hoja hatari. Kwa kuwa hoja imeletwa na Zitto na January (ingawa sisi sio waanzilishi wa hoja hii) ni hoja ya kibaguzi. Nawashangaa sana wasomi wa siku hizi. Wasomi wanaojadili watu badala ya masuala.

      Mwandishi anasema kwamba vyama vya siasa haviandai vijana kuwa viongozi. Nitamweleza.

      Chama changu kinalea na kukuza vijana kuwa viongozi. Mimi binafsi nimejiunga na chama changu nikiwa na umri wa miaka 16, mtoto. Nimekulia ndani ya chama. Nimepewa majukumu ya kawaida kabisa ya chama kama kusimika miti ya bendera, kupokea viongozi na kuandaa mikutano. Nikiwa Chuo Kikuu Mwenyekiti wa sasa wa Chadema ndugu Mbowe alikuja kuniomba sasa nishiriki kikamilifu kukijenga upya chama. Yeye alikuwa Mbunge wa Hai akitaka chama kiwe imara zaidi, akaambiwa kuna mwanachama wenu kule Mlimani. Wakati huo CHADEMA kilikuwa chama ambacho watu wanakikimbia isipokuwa watu wa Kigoma na Kilimanjaro, Shinyanga, Karatu na Ukerewe. Vijana walikuwa wanajipambanua na CCM zaidi ama CUF au TLP kuliko hiki chama cha mabwanyenye. Huu ni mwaka 2001, muongo mmoja tu uliopita. Mimi na Freeman Mbowe ndio tumefanya mabadiliko yote yanayoonekana CHADEMA. Tumeingiza watu wapya, tumeandika Katiba upya. Ilipofika mwaka 2005 tukasema Freeman Mbowe nenda kwenye Urais, tulijuwa tunashindwa lakini tulitaka kujenga chama chetu. Tukapata Wabunge. Wabunge Wakafanya kazi. Tukaingia mwaka 2010 katika uchaguzi kama chama imara tunachokwenda kuchukua dola.

      Katika mchakato huu tukaingiza vijana kwenye chama na kuwalea. John Mnyika hakuwa CHADEMA, tena alikuwa mgumu sana kuingia kwenye chama chetu. Tukampa moyo. Tukampa majukumu. Leo ni mmoja wa rasilimali watu kubwa sana katika siasa za nchi yetu. Halima Mdee hakuwa mwanasiasa kabisa. Tukampa moyo. Tukampa majukumu. Leo ni Mbunge mahiri kabisa.

      Baadhi ya watu wazima waliingia CHADEMA kufuata vijana. Vijana tulifyeka pori kwanza. Nani anasema hatulei vijana kuwa viongozi wazuri? Nani haoni hazina ya viongozi vijana hivi sasa ndani ya Bunge kutoka vyama vyote? Kuna namna bora ya kulea viongozi zaidi ya kuwapa majukumu?

      Mbowe alikuwa ananifuata pale Hall 1, tunakwenda kufanya kazi za chama usiku kucha, kusoma na kuchambua makabrasha ya kisera na mikakati. Ninarudi chuo usiku wa manane wakati wanafunzi wengine ama wapo wanajisomea au wamelala. Kazi ya kujenga taasisi inayoitwa chama cha siasa.

      Lakini kujengwa kuwa kiongozi sio kazi ya chama pekee. Ni kazi ya jamii kwa ujumla. Wakati wanafunzi wenzangu walikuwa wanaomba kufanya kazi za mafunzo kwenye taasisi kubwa Kama Benki Kuu, nikiwa mwaka wa pili Chuo Kikuu nilikwenda kufanya internship TGNP. Kujifunza Bajeti ya kijinsia na kuipa hoja za kiuchumi. Kina mama wa TGNP wakanijenga na kunipika kiuongozi.

      Chuo Kikuu sikuwa nasoma Sosholojia, lakini rafiki yangu mkubwa alikuwa Chachage. Sikuwa nasoma lugha, lakini mshauri wangu alikuwa Lwaitama. Sikuwa nasoma sheria lakini nilikuwa namwakilisha Shivji na kusoma mada zake alizopasa kuwakilisha kwenye semina kadhaa kuhusu haki za binadamu. Nimefunzwa na makundi ya watu mbalimbali na sio chama changu pekee. Jamii ndio yenye jukumu la kufunda vijana kuwa viongozi. Jamii inafanya kazi hiyo?

      Inasemwa mjadala huu ni hatari kwa namna ulivyopenyezwa. Kupenyezwa? Huu mjadala wa umri umeanza kuzungumzwa mimi nikiwa nipo Chuo Kikuu. Vijana kupitia National Youth Forum Kama Taasisi ya vijana wamekuwa wakisema jambo hili toka miaka ya katikati ya tisini. Jukwaa hili la Vijana chini ya viongozi wake kina Hebron Mwakagenda wamekuwa wakitoa Maazimio na Maazimio kwamba umri wa kugombea Urais upo juu sana toka miaka ya tisini. Taasisi ya TYVA imekuwa ikijenga hoja hii toka miaka ya 2000. Hii sio hoja mpya hata kidogo. Hoja hii haijapenyezwa. Hii ni hoja ya vijana ya miaka mingi sana. Lakini sishangai kuona inaonekana ni hoja mpya kwani watanzania uwezo wetu wa kutunza kumbukumbu ni mdogo sana. Pia tunapenda kujadili mtoa hoja na sio hoja yenyewe. Mfuatiliaji yeyote makini wa siasa za vijana wa Tanzania kupitia makongamano ya vijana anajua hii sio hoja iliyopenyezwa na Zitto au January. Kuijadili kwa kumwangalia Zitto na January ni kuchoka kufikiri.


      Hoja hii haina hatari yeyote inayosemwa na mwandishi. Hoja hii ni hoja kama hoja nyingine yeyote na inaweza kupita au kukataliwa. Hii sio hoja ya watu fulani. Ni hoja ya vijana ya siku nyingi sana. Vijana hawa wanajiona kupitia vijana wengine walio kwenye nafasi mbalimbali kisiasa au hata katika sekta binafsi. Mfano vijana wa Kigoma ninakotoka wakiniangalia wanajiona. Ndio wanaona tuko sawa. Wanaona mimi ni mwenzao. Nimekua miongoni mwao. Nimesoma nao. Nimecheza nao. Nimehangaika nao. Wanaona Ubunge nilionao ni Dhamana tu na hawanizungumzishi kama mtu kutoka tabaka fulani, bali kama mwenzao.

      Ninaishi maisha ninayoishi. Siishi Manzese kwa Mfuga Mbwa. Siishi Masaki pia. Naishi Tabata, kwenye nyumba ya kupanga. Tabata wanaishi vijana wote wale wa tabaka la chini kama asemalo mwandishi na pia tabaka la kati na labda tabaka la juu. Najua na kusikia machungu ya vijana wasio na ajira na ndio maana nahangaika kwa kutumia nafasi ya Ubunge kujaribu kuisukuma Serikali iweke sera zinazotekelezeka za kutatua tatizo la ajira kwa vijana. Ndio maana nahangaika kila siku kujenga hoja kwamba Serikali iingilie kati ukuaji wa uchumi ili pia wanyonge wafaidike. Ninasikia machungu ya vijana wasio na ajira maana ndio walionipigia kura kuwa Mbunge. Zaidi ya hayo nakutana nao sana kuzungumza namna ya kusaidiana.


      Nakutana nao mitaani kwa mijini na vijijini ninakokwenda kila wakati. Nakutana nao kwenye mitandao ya kijamii, wananiandikia na mimi ninawajibu. Nagawana nao kidogo nilichonacho ili nao waweze kijikwamua. Nawasaidia vijana wenye vipaji kukuza vipawa vyao na kupata kipato. Mwandishi anapata wapi haki ya kusema sentensi rahisi rahisi kwamba mimi sisikii machungu ya vijana wenzangu?

      Ninashinda na vijana wa aina zote, ndio kazi kubwa ya Mwakilishi anayefanya kazi yake. Nina marafiki wavuvi, mafundi seremala, waimbaji wa Bongo Flava, machinga na hata wasio na ajira. Nina marafiki wenye makampuni yao, wafanyakazi wa mashirika ya Umma, wasomi wa Vyuo Vikuu na wafanyabiashara wakubwa. Mwakilishi yeyote wa wananchi lazima asikie machungu ya jamii nzima vinginevyo hatoshi.

      Kijana mwenye umri wangu ana mambo mengi anayofanana nami. Ana mambo mengi ya kujifunza kutoka kwangu. Hapa katikati ilikuwa ni kama jambo lisilowezekana kijana wa aina yangu kutoka familia masikini kabisa kuwa Mbunge. Baada ya Zitto kuwa Mbunge na kutokana na kazi niliyofanya Bungeni katika Bunge la Tisa, vijana wengi walihamasika na kusema wanaweza. Leo tuna vijana wadogo kabisa kutoka familia za kawaida kabisa ni Wabunge na wanafanya vizuri. Kina Kafulila, kina Mkosamali, kina Silinde hawa ni watoto wa kimasikinj kabisa ambao ni wa kwanza kupata shahada kwenye familia zao. Hii ni nguvu ya 'inspiration' kutoka kwa rika linalofanana. Sugu ni mkubwa kwangu kiumri, lakini kuingia kwake siasa kumechangiwa sana na kazi zangu pamoja na wenzangu kwenye Bunge.

      Kuna vijana wengi zaidi nchini kwetu wanasema ninataka niwe kama Zitto, kama January, kama Halima Mdee. Tunazungumza nao. Tunaishi nao. Ni ndugu zetu. Ni rafiki zetu. Tunaishi nao mtaani. Tunakwenda nao kwa kinyozi mmoja. Tunakwenda muziki pamoja. Ninajua machungu ya vijana. Ninafanyia kazi machungu ya vijana. Ndio kazi yangu ya kila siku kama Mbunge, kama Mwakilishi wao.

      Mwandishi anasema mjadala unalenga kuleta ubaguzi. Sioni hoja yake. Wanaosema umri wa kugombea Urais ushushwe chini ya miaka 40 hawasemi wazee wasigombee. Wanasema tupanue wigo wa haki hii ya kugombea. Wanaozungumza ubaguzi ndio wenye kupenyeza mbegu za kibaguzi. Kwa kuwa wanawaza kibaguzibaguzi basi kila jambo huliangalia kibaguzi. Kama Katiba inasema yeyote mwenye haki ya kupiga kura ana haki ya kugombea nafasi yeyote ya uongozi, ubaguzi unatoka wapi? Hoja zote zinazotolewa na mtoa hoja kuhusu ubaguzi zinasambaza mbegu ya ubaguzi.

      Mwandishi sasa anawaambia Watanzania waanze kufikiri sasa zamu ya nani. Mimi binafsi sijawahi kusema hii ni zamu ya vijana. Ila nimesema changamoto za sasa za nchi zinahitaji mtu mwenye uwezo wa kuzikabili, ninaamini mtu huyo ni kijana. Ninaamini kuwa kila kizazi kina ajenda zake. Kizazi chetu kina kazi ya kuhakikisha uhuru wa kiuchumi wa nchi yetu. Kizazi cha kina Mwalimu kilikuwa cha ukombozi na kujenga Taifa moja. Mwandishi hamwamini Frantz Fanon?

      Hoja ya kwamba mjadala huu unataka kununua hisia za wanyonge ni hoja isiyo na [mashiko] kabisa. Mimi nimechaguliwa na wanyonge mara mbili kuwa Mbunge wao. Wanyonge wamenipa Ubunge bila kutoa rushwa. Wamenipa Ubunge kwa kuniamini. Sasa kwa nini sasa ninunue hisia zao? Hii hoja ina misingi gani? Hii ni hoja ya kubandika. Hii ni hoja ya kubumba maneno ili mwandishi aonekane kwamba anafanya uchunguzi wa kitabaka. Hakuna dhana ya tabaka katika hoja hii kama ilivyo kuwa hakuna dhana ya tabaka kwa wazee au hata wanawake. Hoja hii haizuii kwa namna yeyote ile wananchi kuhoji chanzo cha ufukara wao. Kwanza wanaosemwa kwenye hoja hii ndio wapo mstari wa mbele kuhakikisha Mali ya Nchi inatumika wa maendeleo ya wananchi. Mimi binafsi nimeanzisha mjadala wa rasilimali Madini nchini mpaka kutungwa kwa sheria mpya inayoweka misingi ya nchi kufaidika na Madini. Mimi binafsi na wenzangu tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha serikali inatekeleza sheria mpya.

      Mwandishi amesahau Buzwagi? Mwandishi amesahau hoja ya Mkonge inayotaka wanyonge wapewe mashamba ya Mkonge na wawezeshwe na Serikali kulima Katani? Mwandishi amesahau hoja ya kusimamia sekta ya nyumba ili wanyonge wasinyonywe na wenye nyumba ambayo imetolewa na mmoja wa wanaotetea hoja ya umri kushushwa? Ama mwandishi ana wanyonge wake anaowasemea? Sio hawa manamba kwenye Mkonge. Sio hawa vijana wachimbaji wadogo. Sio hawa vijana wanaoshindwa kulipa kodi ya nyumba mwaka mzima? Wanyonge wa mwandishi ni wanazuoni wanaoishi kwa fedha za walipa kodi ambao hawana shida ya kujiuliza kama watakula au watalala maana Serikali au wafadhili wa masomo yao wanawalipia malazi na chakula. Kama wanyonge wake ni hawa waliotupigia kura sisi ili kuwawakilisha Bungeni, basi mwandishi hajui asemalo.

      Hoja ya umri wa kugombea Urais, kwa kuweka pa kuanzia ama kuweka kikomo inapaswa kujadiliwa bila kuangalia majina ya wanaotetea hoja hii. Ijadiliwe kwa faida na hasara zake. Kujenga hoja kwa misingi ya kitabaka ni kuchochea ubaguzi na kunyweshea mbegu za kibaguzi. Nani ana uhakika kuwa Zitto atakuwa anaishi ifikapo mwaka 2015? Kwamba tusiandike Katiba yenye kupanua wigo wa kutoa haki ya kugombea Urais kwa sababu ya Zitto?


      Huu woga dhidi ya Zitto unatoka wapi?
      CHANZO: http://udadisi.blogspot.com

    2. Study Abroad

    3. #2
      GeniusBrain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Location : CHADEMA Makao Makuu
      Posts : 3,806
      Rep Power : 1143
      Likes Received
      187
      Likes Given
      0

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Na kwa cdm huyu ndio mtu anae faa kuwa Rais. Wengine wote wakina M & S Company wana tamaa tu za madaraka. Nawaomba wana cdm muungeni mkono Zitto na apitishwe na chama
      zomba, BinMgen and ruko dkerwa like this.

    4. #3
      TaiJike's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2011
      Posts : 1,156
      Rep Power : 606
      Likes Received
      387
      Likes Given
      347

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Asante kwa taarifa hizi mzee wa pweza, ila nimeshindwa kudownload (kasim)
      * Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi? * - Julius Kambarage Nyerere


    5. #4
      Papa D's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 615
      Rep Power : 556
      Likes Received
      88
      Likes Given
      75

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      The guy is good!! He can make some significant changes!
      RUTARE likes this.

    6. #5
      Ulukolokwitanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th September 2010
      Location : ndzengelendete
      Posts : 2,586
      Rep Power : 1069
      Likes Received
      1428
      Likes Given
      259

      Default

      Quote By GeniusBrain
      Na kwa cdm huyu ndio mtu anae faa kuwa Rais. Wengine wote wakina M & S Company wana tamaa tu za madaraka. Nawaomba wana cdm muungeni mkono Zitto na apitishwe na chama
      Kinachokusumbua wewe ni udini tu. Jaribu kuangalia habari imetoka wapi sio kukurupuka. Labda anaongelea urais 2025 Dr Slaa akishamaliza vipindi vyake, which kila mwana CDM atamuunga mkono. Lakini kwa sasa Zitto HAJAKWIVA kuwa rais na hata katiba haimruhusu
      Jasusi and KENET like this.

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      Angel Msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Posts : 6,266
      Rep Power : 1825
      Likes Received
      1397
      Likes Given
      0

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      sitampa kura yangu na wala hatutampitisha.
      Matola likes this.

    9. #7
      Goodrich's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2012
      Posts : 610
      Rep Power : 621
      Likes Received
      217
      Likes Given
      29

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Zitto ni kibaraka wa CCM !
      Lengo lake sio Urais bali kuivuruga Chadema.
      Last edited by Goodrich; 27th March 2012 at 23:09.
      Ongeauchoke likes this.
      ... our Conflict has never been about the establishment of a Palestinian state, it's always been about the existence of the Jewish state. - Benjamin Netanyahu.

    10. #8
      Andy1's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th June 2011
      Posts : 64
      Rep Power : 414
      Likes Received
      7
      Likes Given
      1

      Default

      Rais wa familia yako

    11. #9
      GeniusBrain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Location : CHADEMA Makao Makuu
      Posts : 3,806
      Rep Power : 1143
      Likes Received
      187
      Likes Given
      0

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Quote By Ulukolokwitanga
      Kinachokusumbua wewe ni udini tu. Jaribu kuangalia habari imetoka wapi sio kukurupuka. Labda anaongelea urais 2025 Dr Slaa akishamaliza vipindi vyake, which kila mwana CDM atamuunga mkono. Lakini kwa sasa Zitto HAJAKWIVA kuwa rais na hata katiba haimruhusu
      Ndio tatizo lenu watu wa kaskazini mnalazimisha Slaa 2015 agombee urais ili hali atakuwa mzee na hatufai tena. Na isitoshe mzee hana jipya kwa sasa, awaachie vijana wakina Zitto. Kuhusu umri katiba ijayo tunalirekebisha hilo na Zitto ambae ni chaguo la CDM wengi ata qualify.
      RUTARE and mathematics like this.

    12. #10
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,291
      Rep Power : 1195
      Likes Received
      1179
      Likes Given
      1551

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Muambieni ZITTO akazitafute vizuri habari za atiku abubakari wa Nigeria

    13. #11
      Mohammed Shossi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th January 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 3,801
      Rep Power : 1191
      Likes Received
      852
      Likes Given
      250

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Naomba ninukuu maneni ya Ernesto Sheka kwenye maandiko yake ya The Moment Of Truth:
      Je,ilikuwaje Mbowe akashinda uenyekiti na si Zitto Kabwe?
      Edwin Mtei namnukuu akisema,"we can't give this position to a man from nowhere" akimaanisha Zitto Kabwe,Zitto alitaka kuondoka ila alibaki kwa sababu zake.Tafakari hiyo kauli ya Mtei.Who's a man from nowhere and who's a man from somewhere??
      Can CDM give that a chance to someone from nowhere?
      Siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale uwongo utakapojitenga - Zitto Z. Kabwe

    14. FJM
      #12
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,168
      Rep Power : 2566
      Likes Received
      5318
      Likes Given
      4585

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Labda Zitto wa 2007, lakini Zitto wa 2012 - siungi mkono.

    15. #13
      idawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2012
      Posts : 4,527
      Rep Power : 3319
      Likes Received
      1206
      Likes Given
      457

      Default

      Quote By Angel Msoffe
      sitampa kura yangu na wala hatutampitisha.
      hamtampa kura wala hamtampitisha wewe na nani.?
      mgt software and ITEGAMATWI like this.

    16. #14
      Angel Msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Posts : 6,266
      Rep Power : 1825
      Likes Received
      1397
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By idawa
      hamtampa kura wala hamtampitisha wewe na nani.?
      kwani we nani mpaka unihoji?
      Kifimbo Cheza likes this.

    17. #15
      Mohammed Shossi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th January 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 3,801
      Rep Power : 1191
      Likes Received
      852
      Likes Given
      250

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Quote By Sangarara
      Muambieni ZITTO akazitafute vizuri habari za atiku abubakari wa Nigeria
      Au za Ernesto Sheka
      Siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale uwongo utakapojitenga - Zitto Z. Kabwe

    18. #16
      idawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2012
      Posts : 4,527
      Rep Power : 3319
      Likes Received
      1206
      Likes Given
      457

      Default

      Quote By Angel Msoffe
      kwani we nani mpaka unihoji?
      mwanachadema!

    19. #17
      Mohammed Shossi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th January 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 3,801
      Rep Power : 1191
      Likes Received
      852
      Likes Given
      250

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Quote By Angel Msoffe
      kwani we nani mpaka unihoji?
      Si ndio hapo! hajui cdm ina wenyewe?
      chama likes this.
      Siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale uwongo utakapojitenga - Zitto Z. Kabwe

    20. #18
      Eng. Y. Bihagaze's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 8th September 2011
      Location : Czech(but now in DAR)
      Posts : 764
      Rep Power : 5115
      Likes Received
      579
      Likes Given
      111

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      My take:
      Kwa katiba la Tz la kuwa Rais on 10 years bases.. Mtu mwenye miaka 35 akiukwaa urais given kwenye 45 atalazimika kuwekwa kando Kama sio 40. Na Kwa umri huu ndio Wa ujana Lakini unapachikwa Jina la mstaafu..

      Ni wazi sehemu ya maisha yako itakuwa kula kulala. Mara nyingi kwenye nchi ambazo hawana democracy hata mtoto anaweza kuwa mtawala but he/she will be there hadi anazeeka.. Na ikitokea nchi ya kidokrasia yenye mafungu ya kuongaza Kwa miaka kadhaa Na ikatokea kiongozi kijana.. Lazima atafanya jitihada za kuchakachua katiba ili ajinemeshee miaka zaidi.

      Vijana wengi wa kwetu ni wakirupukaji, waninafsi Na wasaliti. Hang'ang'ania vyeo Na nafasi za juu sana za uongozi bila kufikiria after uongozi kuisha itakuwaje.. Mtu hata familia Hana, hajajua house management and children care ikovipi

    21. #19
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,403
      Rep Power : 10870
      Likes Received
      3780
      Likes Given
      426

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Zitto anafaa walau kuanzia 2025 atakuwa amepikwa na kukomaa vizuri.Kwa hivi sasa ni nafasi ya Dr Slaa.Dr Slaa kwa sasa hana mbadala ndani ya CDM.Ni kujilisha upepo kudhani kuna mtu mwingine atapitishwa kugombea Urais zaidi ya Dr wa ukweli walau kwa sasa.CDM ina vijana wengi na hakika huko Mbeleni kina Zitto na Mnyika na wengine ni hazina kubwa ya chama
      MpendaTz likes this.

    22. #20
      Mohamedi Mtoi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th December 2010
      Location : Lushoto - Kwemakame.
      Posts : 2,048
      Rep Power : 24548
      Likes Received
      3125
      Likes Given
      354

      Default

      Quote By Pendael laizer
      Mleta thread ni mmagamba tu na katumwa na mafsadi wa ccm kuja kuleta ugomvi huku cdm kama walionao magamba
      Acha fikira za hovyo hovyo! Jadili kilicho kwenye mada usimjadili mleta mada, na kama ukigundua kuwa mleta mada ni m-chadema utafanya nini?! Bofya hapa upate uhakika www.facebook.com/mouddymtoi

    23. Miaka 50
    Page 1 of 43 12311 ... LastLast

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...