Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Zitto: Ndio ninautaka urais

    Report Post
    Page 43 of 43 FirstFirst ... 33414243
    Results 841 to 856 of 856
    1. #1
      Mohamedi Mtoi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th December 2010
      Location : Lushoto - Kwemakame.
      Posts : 2,047
      Rep Power : 24548
      Likes Received
      3123
      Likes Given
      354

      Default Zitto: Ndio ninautaka urais

      Mbunge mahiri na machachari kutoka chama makini Zitto Zuberi Kabwe ameweka wazi kuwa anautaka uraisi lakini akiwa atapata ridhaa kutoka kwa chama chake na wananchi kwa ujumla wao,
      NDIO NATAKA KUWA RAIS - Zitto Kabwe


      Kwanza niseme wazi kabisa kabisa kuwa Urais ninautaka.

      Ninaamini ninao uwezo wa kuwa Rais. Ninaamini nina uzalendo wa kutosha na utashi wa kuleta mabadiliko stahili wa namna nchi yetu inavyoongozwa. Ninajua kuwa nchi yetu imesahau maendeleo ya watu na kujikita katika maendeleo ya vitu. Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo (styles) badala ya mambo ya msingi (content). Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika. Ninajua nchi yetu inahitaji Uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa (transformation) badala ya mabadiliko ya juu juu (cosmetic change). Ninajua 'transformation' inahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi na hasa mabwana wakubwa wa nchi za magharibi mfano kuzuia nchi yetu kuuza malighafi tu. Ninajua rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya Umma ni kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi. Ninajua rasilimali kama Madini, Mafuta na Gesi, Ardhi n.k. ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu.


      Hivyo, nchi inahitaji Kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi. Sio kazi rahisi lakini ni kazi ambayo lazima Mtanzania mmoja aifanye. Mimi nataka kuifanya. Nina uwezo wa kuifanya.

      Hata hivyo kazi hii hata kama naitaka ni lazima wenye nchi waamue kunipa kazi hii. Ni lazima kwanza Chama changu kiseme wewe ndio mwanachama unaestahili kuifanya kazi hii. Ni lazima Watanzania wengi waseme wewe ndio mwananchi mwenzetu unayeweza kuchukua jukumu hili. Kuitaka tu haitoshi. Ni lazima wananchi wakuamini na kukupa jukumu hili.



      Sasa kama wananchi watasema huyu Zitto anapaswa kubeba jukumu hili mwaka 2015 tuache iwe. Kama watasema hapana wewe bado mpaka mwaka 2020 au hata 2025 tuache iwe hivyo. Pia Kama hawataki kabisa tuache iwe hivyo.

      Mjadala wa umri wa kugombea Urais imekuwa mjadala mkali sasa. Mjadala huu baadhi ya watu kwa sababu wanazojua wao wameamua kuita ni mjadala wa Zitto na January. Kwamba ni mjadala unaobagua Wazee. Mjadala unaopandikiza chuki na sumu za kibaguzi. Kwamba ni mjadala wa Kitabaka na kuwa Zitto na January sio tabaka stahili la vijana walio wengi. Sitamsemea January, nitajibu baadhi ya hoja za mwandishi wa makala mojawapo kama Zitto. January akitaka atamjibu naye kivyake.

      Mwandishi anasema yeye hapingi hoja ya umri, bali anapinga aina ya watu wanaoshadidia hoja hiyo. Anaipenda hoja ila hapendi watoa hoja. Hoja nzuri lakini Zitto na January wabaya. Amelisema hilo mwanzo kabisa wa makala yake. Kwa hiyo kwake yeye hoja ingeletwa na vijana wengine asingekuwa na shida wala isingekuwa hoja hatari. Kwa kuwa hoja imeletwa na Zitto na January (ingawa sisi sio waanzilishi wa hoja hii) ni hoja ya kibaguzi. Nawashangaa sana wasomi wa siku hizi. Wasomi wanaojadili watu badala ya masuala.

      Mwandishi anasema kwamba vyama vya siasa haviandai vijana kuwa viongozi. Nitamweleza.

      Chama changu kinalea na kukuza vijana kuwa viongozi. Mimi binafsi nimejiunga na chama changu nikiwa na umri wa miaka 16, mtoto. Nimekulia ndani ya chama. Nimepewa majukumu ya kawaida kabisa ya chama kama kusimika miti ya bendera, kupokea viongozi na kuandaa mikutano. Nikiwa Chuo Kikuu Mwenyekiti wa sasa wa Chadema ndugu Mbowe alikuja kuniomba sasa nishiriki kikamilifu kukijenga upya chama. Yeye alikuwa Mbunge wa Hai akitaka chama kiwe imara zaidi, akaambiwa kuna mwanachama wenu kule Mlimani. Wakati huo CHADEMA kilikuwa chama ambacho watu wanakikimbia isipokuwa watu wa Kigoma na Kilimanjaro, Shinyanga, Karatu na Ukerewe. Vijana walikuwa wanajipambanua na CCM zaidi ama CUF au TLP kuliko hiki chama cha mabwanyenye. Huu ni mwaka 2001, muongo mmoja tu uliopita. Mimi na Freeman Mbowe ndio tumefanya mabadiliko yote yanayoonekana CHADEMA. Tumeingiza watu wapya, tumeandika Katiba upya. Ilipofika mwaka 2005 tukasema Freeman Mbowe nenda kwenye Urais, tulijuwa tunashindwa lakini tulitaka kujenga chama chetu. Tukapata Wabunge. Wabunge Wakafanya kazi. Tukaingia mwaka 2010 katika uchaguzi kama chama imara tunachokwenda kuchukua dola.

      Katika mchakato huu tukaingiza vijana kwenye chama na kuwalea. John Mnyika hakuwa CHADEMA, tena alikuwa mgumu sana kuingia kwenye chama chetu. Tukampa moyo. Tukampa majukumu. Leo ni mmoja wa rasilimali watu kubwa sana katika siasa za nchi yetu. Halima Mdee hakuwa mwanasiasa kabisa. Tukampa moyo. Tukampa majukumu. Leo ni Mbunge mahiri kabisa.

      Baadhi ya watu wazima waliingia CHADEMA kufuata vijana. Vijana tulifyeka pori kwanza. Nani anasema hatulei vijana kuwa viongozi wazuri? Nani haoni hazina ya viongozi vijana hivi sasa ndani ya Bunge kutoka vyama vyote? Kuna namna bora ya kulea viongozi zaidi ya kuwapa majukumu?

      Mbowe alikuwa ananifuata pale Hall 1, tunakwenda kufanya kazi za chama usiku kucha, kusoma na kuchambua makabrasha ya kisera na mikakati. Ninarudi chuo usiku wa manane wakati wanafunzi wengine ama wapo wanajisomea au wamelala. Kazi ya kujenga taasisi inayoitwa chama cha siasa.

      Lakini kujengwa kuwa kiongozi sio kazi ya chama pekee. Ni kazi ya jamii kwa ujumla. Wakati wanafunzi wenzangu walikuwa wanaomba kufanya kazi za mafunzo kwenye taasisi kubwa Kama Benki Kuu, nikiwa mwaka wa pili Chuo Kikuu nilikwenda kufanya internship TGNP. Kujifunza Bajeti ya kijinsia na kuipa hoja za kiuchumi. Kina mama wa TGNP wakanijenga na kunipika kiuongozi.

      Chuo Kikuu sikuwa nasoma Sosholojia, lakini rafiki yangu mkubwa alikuwa Chachage. Sikuwa nasoma lugha, lakini mshauri wangu alikuwa Lwaitama. Sikuwa nasoma sheria lakini nilikuwa namwakilisha Shivji na kusoma mada zake alizopasa kuwakilisha kwenye semina kadhaa kuhusu haki za binadamu. Nimefunzwa na makundi ya watu mbalimbali na sio chama changu pekee. Jamii ndio yenye jukumu la kufunda vijana kuwa viongozi. Jamii inafanya kazi hiyo?

      Inasemwa mjadala huu ni hatari kwa namna ulivyopenyezwa. Kupenyezwa? Huu mjadala wa umri umeanza kuzungumzwa mimi nikiwa nipo Chuo Kikuu. Vijana kupitia National Youth Forum Kama Taasisi ya vijana wamekuwa wakisema jambo hili toka miaka ya katikati ya tisini. Jukwaa hili la Vijana chini ya viongozi wake kina Hebron Mwakagenda wamekuwa wakitoa Maazimio na Maazimio kwamba umri wa kugombea Urais upo juu sana toka miaka ya tisini. Taasisi ya TYVA imekuwa ikijenga hoja hii toka miaka ya 2000. Hii sio hoja mpya hata kidogo. Hoja hii haijapenyezwa. Hii ni hoja ya vijana ya miaka mingi sana. Lakini sishangai kuona inaonekana ni hoja mpya kwani watanzania uwezo wetu wa kutunza kumbukumbu ni mdogo sana. Pia tunapenda kujadili mtoa hoja na sio hoja yenyewe. Mfuatiliaji yeyote makini wa siasa za vijana wa Tanzania kupitia makongamano ya vijana anajua hii sio hoja iliyopenyezwa na Zitto au January. Kuijadili kwa kumwangalia Zitto na January ni kuchoka kufikiri.


      Hoja hii haina hatari yeyote inayosemwa na mwandishi. Hoja hii ni hoja kama hoja nyingine yeyote na inaweza kupita au kukataliwa. Hii sio hoja ya watu fulani. Ni hoja ya vijana ya siku nyingi sana. Vijana hawa wanajiona kupitia vijana wengine walio kwenye nafasi mbalimbali kisiasa au hata katika sekta binafsi. Mfano vijana wa Kigoma ninakotoka wakiniangalia wanajiona. Ndio wanaona tuko sawa. Wanaona mimi ni mwenzao. Nimekua miongoni mwao. Nimesoma nao. Nimecheza nao. Nimehangaika nao. Wanaona Ubunge nilionao ni Dhamana tu na hawanizungumzishi kama mtu kutoka tabaka fulani, bali kama mwenzao.

      Ninaishi maisha ninayoishi. Siishi Manzese kwa Mfuga Mbwa. Siishi Masaki pia. Naishi Tabata, kwenye nyumba ya kupanga. Tabata wanaishi vijana wote wale wa tabaka la chini kama asemalo mwandishi na pia tabaka la kati na labda tabaka la juu. Najua na kusikia machungu ya vijana wasio na ajira na ndio maana nahangaika kwa kutumia nafasi ya Ubunge kujaribu kuisukuma Serikali iweke sera zinazotekelezeka za kutatua tatizo la ajira kwa vijana. Ndio maana nahangaika kila siku kujenga hoja kwamba Serikali iingilie kati ukuaji wa uchumi ili pia wanyonge wafaidike. Ninasikia machungu ya vijana wasio na ajira maana ndio walionipigia kura kuwa Mbunge. Zaidi ya hayo nakutana nao sana kuzungumza namna ya kusaidiana.


      Nakutana nao mitaani kwa mijini na vijijini ninakokwenda kila wakati. Nakutana nao kwenye mitandao ya kijamii, wananiandikia na mimi ninawajibu. Nagawana nao kidogo nilichonacho ili nao waweze kijikwamua. Nawasaidia vijana wenye vipaji kukuza vipawa vyao na kupata kipato. Mwandishi anapata wapi haki ya kusema sentensi rahisi rahisi kwamba mimi sisikii machungu ya vijana wenzangu?

      Ninashinda na vijana wa aina zote, ndio kazi kubwa ya Mwakilishi anayefanya kazi yake. Nina marafiki wavuvi, mafundi seremala, waimbaji wa Bongo Flava, machinga na hata wasio na ajira. Nina marafiki wenye makampuni yao, wafanyakazi wa mashirika ya Umma, wasomi wa Vyuo Vikuu na wafanyabiashara wakubwa. Mwakilishi yeyote wa wananchi lazima asikie machungu ya jamii nzima vinginevyo hatoshi.

      Kijana mwenye umri wangu ana mambo mengi anayofanana nami. Ana mambo mengi ya kujifunza kutoka kwangu. Hapa katikati ilikuwa ni kama jambo lisilowezekana kijana wa aina yangu kutoka familia masikini kabisa kuwa Mbunge. Baada ya Zitto kuwa Mbunge na kutokana na kazi niliyofanya Bungeni katika Bunge la Tisa, vijana wengi walihamasika na kusema wanaweza. Leo tuna vijana wadogo kabisa kutoka familia za kawaida kabisa ni Wabunge na wanafanya vizuri. Kina Kafulila, kina Mkosamali, kina Silinde hawa ni watoto wa kimasikinj kabisa ambao ni wa kwanza kupata shahada kwenye familia zao. Hii ni nguvu ya 'inspiration' kutoka kwa rika linalofanana. Sugu ni mkubwa kwangu kiumri, lakini kuingia kwake siasa kumechangiwa sana na kazi zangu pamoja na wenzangu kwenye Bunge.

      Kuna vijana wengi zaidi nchini kwetu wanasema ninataka niwe kama Zitto, kama January, kama Halima Mdee. Tunazungumza nao. Tunaishi nao. Ni ndugu zetu. Ni rafiki zetu. Tunaishi nao mtaani. Tunakwenda nao kwa kinyozi mmoja. Tunakwenda muziki pamoja. Ninajua machungu ya vijana. Ninafanyia kazi machungu ya vijana. Ndio kazi yangu ya kila siku kama Mbunge, kama Mwakilishi wao.

      Mwandishi anasema mjadala unalenga kuleta ubaguzi. Sioni hoja yake. Wanaosema umri wa kugombea Urais ushushwe chini ya miaka 40 hawasemi wazee wasigombee. Wanasema tupanue wigo wa haki hii ya kugombea. Wanaozungumza ubaguzi ndio wenye kupenyeza mbegu za kibaguzi. Kwa kuwa wanawaza kibaguzibaguzi basi kila jambo huliangalia kibaguzi. Kama Katiba inasema yeyote mwenye haki ya kupiga kura ana haki ya kugombea nafasi yeyote ya uongozi, ubaguzi unatoka wapi? Hoja zote zinazotolewa na mtoa hoja kuhusu ubaguzi zinasambaza mbegu ya ubaguzi.

      Mwandishi sasa anawaambia Watanzania waanze kufikiri sasa zamu ya nani. Mimi binafsi sijawahi kusema hii ni zamu ya vijana. Ila nimesema changamoto za sasa za nchi zinahitaji mtu mwenye uwezo wa kuzikabili, ninaamini mtu huyo ni kijana. Ninaamini kuwa kila kizazi kina ajenda zake. Kizazi chetu kina kazi ya kuhakikisha uhuru wa kiuchumi wa nchi yetu. Kizazi cha kina Mwalimu kilikuwa cha ukombozi na kujenga Taifa moja. Mwandishi hamwamini Frantz Fanon?

      Hoja ya kwamba mjadala huu unataka kununua hisia za wanyonge ni hoja isiyo na [mashiko] kabisa. Mimi nimechaguliwa na wanyonge mara mbili kuwa Mbunge wao. Wanyonge wamenipa Ubunge bila kutoa rushwa. Wamenipa Ubunge kwa kuniamini. Sasa kwa nini sasa ninunue hisia zao? Hii hoja ina misingi gani? Hii ni hoja ya kubandika. Hii ni hoja ya kubumba maneno ili mwandishi aonekane kwamba anafanya uchunguzi wa kitabaka. Hakuna dhana ya tabaka katika hoja hii kama ilivyo kuwa hakuna dhana ya tabaka kwa wazee au hata wanawake. Hoja hii haizuii kwa namna yeyote ile wananchi kuhoji chanzo cha ufukara wao. Kwanza wanaosemwa kwenye hoja hii ndio wapo mstari wa mbele kuhakikisha Mali ya Nchi inatumika wa maendeleo ya wananchi. Mimi binafsi nimeanzisha mjadala wa rasilimali Madini nchini mpaka kutungwa kwa sheria mpya inayoweka misingi ya nchi kufaidika na Madini. Mimi binafsi na wenzangu tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha serikali inatekeleza sheria mpya.

      Mwandishi amesahau Buzwagi? Mwandishi amesahau hoja ya Mkonge inayotaka wanyonge wapewe mashamba ya Mkonge na wawezeshwe na Serikali kulima Katani? Mwandishi amesahau hoja ya kusimamia sekta ya nyumba ili wanyonge wasinyonywe na wenye nyumba ambayo imetolewa na mmoja wa wanaotetea hoja ya umri kushushwa? Ama mwandishi ana wanyonge wake anaowasemea? Sio hawa manamba kwenye Mkonge. Sio hawa vijana wachimbaji wadogo. Sio hawa vijana wanaoshindwa kulipa kodi ya nyumba mwaka mzima? Wanyonge wa mwandishi ni wanazuoni wanaoishi kwa fedha za walipa kodi ambao hawana shida ya kujiuliza kama watakula au watalala maana Serikali au wafadhili wa masomo yao wanawalipia malazi na chakula. Kama wanyonge wake ni hawa waliotupigia kura sisi ili kuwawakilisha Bungeni, basi mwandishi hajui asemalo.

      Hoja ya umri wa kugombea Urais, kwa kuweka pa kuanzia ama kuweka kikomo inapaswa kujadiliwa bila kuangalia majina ya wanaotetea hoja hii. Ijadiliwe kwa faida na hasara zake. Kujenga hoja kwa misingi ya kitabaka ni kuchochea ubaguzi na kunyweshea mbegu za kibaguzi. Nani ana uhakika kuwa Zitto atakuwa anaishi ifikapo mwaka 2015? Kwamba tusiandike Katiba yenye kupanua wigo wa kutoa haki ya kugombea Urais kwa sababu ya Zitto?


      Huu woga dhidi ya Zitto unatoka wapi?
      CHANZO: http://udadisi.blogspot.com

    2. FemaTV & Radio

    3. #841
      mkomatembo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th December 2011
      Location : Bweleo
      Posts : 1,018
      Rep Power : 637
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1266

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      NA za yule chacha alopata na aksidenti na Malya je?
      "If the Virgin Mary appears wearing a Veil on all her pictures, how can you ask me to sign on a HIJAB BAN law ?" -Roberto Maroni, Italian Minister.

    4. #842
      Joachim Morgan's Avatar
      Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Posts : 53
      Rep Power : 397
      Likes Received
      13
      Likes Given
      2

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka urais

      Tatizo sio kuutaka urais anamipango gani ya kuyabadilisha maisha ya Mtanzania masikini, kupambana na rushwa, mikataba mibovu na viongozi wasio na uzalendo kwa Taifa letu watachukuliwa hatua gani.

    5. #843
      KENET's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 5th July 2012
      Posts : 242
      Rep Power : 394
      Likes Received
      56
      Likes Given
      75

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Quote By Mohammed Shossi
      Naomba ninukuu maneni ya Ernesto Sheka kwenye maandiko yake ya The Moment Of Truth:

      Can CDM give that a chance to someone from nowhere?
      Wanaweza kumpa mtu yeyote ndani ya CDM kama wanaona anafaa kuongoza.
      Kwa kweli Zito ana mvuto,binafsi nampenda na ni kijana mchapakazi na anakubalika na wengi.Uchaguzi ujao 215 anaweza kuchaguliwa kugombea Urais na anaweza asichaguliwe kugombea vile vile kutokana na makubaliano yao ndani ya chama na si lazima kuhoji ni kwa nini.Katika TEAM ya watu wanaofanya kazi pamoja lazima kuwe na viongozi,viongozi ndiyo wanaojua kama huyu mtu anaweza kufaa kuongoza nchi au hafai.Unaweza kumwona mtu anawakilisha vizuri,msemaji mzuri kwenye jamii lakini viongozi wake ndio wanaojua mapunguifu yake kwa sababu wao ndio wanaokaa naye muda mrefu na kumjua vizuri.Nani alikuwa anajua kwamba Mheshimiwa Ben Mkapa angekuwa Rais wa hii nchi,wengi walikuwa wanamwunga Mkono Mheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema kwa sababu Mrema alikuwa anajua kuzungumza vizuri Bungeni na kuwatetea wananchi wa jimbo lake la Moshi Vijijini wakati huo na alikubalika sana wakati huo.Lakini viongozi wake waliokuwa naye wakati huo walijua mapungufu yake na wala jina lake halikuwepo kwenye waliokuwa wanafikiriwa kugombea Urais.Mrema alihama chama akajiunga na NCCR lakini mwisho wake ulikuwa je?

    6. #844
      Mtanzania1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th December 2010
      Location : Kalenga, Liringa
      Posts : 978
      Rep Power : 620
      Likes Received
      124
      Likes Given
      94

      Default

      Quote By Mr. President
      Weee.... who told u Zitto anachukiwa kisa dini..?? Zitto ana uchu wa madaraka, pili ANACHUNGUZWA KUHUSU KASHFA YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, kuhusu IPTL, each month Tanesco walikuwa wanalipa IPTL FEDHA ZA MAFUTA KUENDESHEA GENS, HUKU MAJI YAPO KUMBE NI MCHEZO WA KUKATA MAJI PURPOSELY, the wana amuru tanesco iwalipe fedha ili kununua mafuta kuwasha generators za IPTL, Zitto alikuwa anapata GAWIO LAKE TENA KUBWA TU, KAMATI YA NISHATI NA MADINI YA BUNGE HADI IMEVUNJWA, ila ZITTO yupo CHC of which anajua inside out ya scandal nzima long time na alikuwa anachukua chake, Zitto mla rushwa mkubwa, HUONI KATULIA AIBU IMEMFIKA ANADECLARE HATAKI ALLOWANCES ZA BUNGE KUMBE ANAKULA RUSHWA KUBWA thru IPTL dili la mafuta, Prof. Muhongo kasema wengi wataaibika.... So stop defending a guy u don't know.....

      Refer ---- BUNGE LILILOPITA -----
      kama ni uchu wa madaraka huu ndiyo msukumo unaowaingiza watu wote kwenye siasa.....ni hulka ya wanasiasa wote......kama tuhuma hizi nzito zikithibitika basi zisiwe kwasababu anataka nafasi ya juu katika nchi yetu......bali nashauri avuliwe nyadhifa zote alizonazo......avuliwe uanachama cdm....afilisiwe mali zake kisha afikishwe mahakamani kwa uhujumu uchumi......bila ya kufanya hivyo basi tutajua ni "siasa za majitaka"

    7. #845
      Vatoi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th August 2011
      Posts : 53
      Rep Power : 402
      Likes Received
      4
      Likes Given
      13

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Quote By Papa D
      The guy is good!! He can make some significant changes!
      How far are you sure? Au ndio campaign yako mmeongae na Zitto? Zitto Acha kutuvuruga, ulishatuambia Katika kikao cha CHADEMA eti wewe peke yako una Dvision ONE, Yaani ndio kutangaza urais? Hata kama ni ONE Ila si una KADEGREE KAMOJA TU? Ndiko unakotambia? wenye elimu zao wamenyamaza , Vipi wewe mtoto wa juzi tu Umeshajitangazia URAIS,? Kumbe wewe unatafuta umaarufu na wala sio kazi ya kupigania wananch! KTK MAPENDEKEZO HUPATI KURA KIJANA !

    8. Miaka 50

    9. #846
      Vatoi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th August 2011
      Posts : 53
      Rep Power : 402
      Likes Received
      4
      Likes Given
      13

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka urais

      Yaan Zitto atakivuruga Chama soon, Mtaniambia, huyu ni SHUSHU,NA NAWEZA KUSEMA AMETUMWA, ILI AMDHOOFISHE SLAA NA MBOWE, TUTASHUUDIA HAYA BAADAYE KWA TAARIFA KAMAILI NILIZO NAZO.

    10. #847
      MARUKENI's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th July 2012
      Posts : 55
      Rep Power : 354
      Likes Received
      5
      Likes Given
      22

      Default

      Quote By Mr. President
      Weee.... who told u Zitto anachukiwa kisa dini..?? Zitto ana uchu wa madaraka, pili ANACHUNGUZWA KUHUSU KASHFA YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, kuhusu IPTL, each month Tanesco walikuwa wanalipa IPTL FEDHA ZA MAFUTA KUENDESHEA GENS, HUKU MAJI YAPO KUMBE NI MCHEZO WA KUKATA MAJI PURPOSELY, the wana amuru tanesco iwalipe fedha ili kununua mafuta kuwasha generators za IPTL, Zitto alikuwa anapata GAWIO LAKE TENA KUBWA TU, KAMATI YA NISHATI NA MADINI YA BUNGE HADI IMEVUNJWA, ila ZITTO yupo CHC of which anajua inside out ya scandal nzima long time na alikuwa anachukua chake, Zitto mla rushwa mkubwa, HUONI KATULIA AIBU IMEMFIKA ANADECLARE HATAKI ALLOWANCES ZA BUNGE KUMBE ANAKULA RUSHWA KUBWA thru IPTL dili la mafuta, Prof. Muhongo kasema wengi wataaibika.... So stop defending a guy u don't know.....

      Refer ---- BUNGE LILILOPITA -----
      Mwaka 2007 Mheshimiwa Zitto alikuwa anamiliki gari aina ya Hammer gari ya KIFAHARI ambayo thamani yake ni karibia milioni mia tano baadae akaona matumizi ya hilo gari ni makubwa sana ikabidi abadilishe na kumiliki gari aina ya Vogue ambalo nalo bei zake ni zilezile na consuption ya mafuta kwa hayo magari ipo juu mno.Zitto kwa maneno yake ni mtu anauchungu sana na vijana wa kitanzania ambao wakiamka asubuhi hawajui waelekee wapi na siku itaishaje.Je hapo bado hajapata nafasi ya kuingia Ikulu anamiliki hayo magari ya kifahari kiasi hicho na anauchungu na walala hoi tukimkabidhi IKULU si atakuwa anatumia ndege kutoka tabata kwenda IKULU?kwani mshahara wa mbunge ni shilingi ngapi?

    11. #848
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14620
      Likes Received
      2841
      Likes Given
      1961

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Quote By Goodrich
      Zitto ni kibaraka wa CCM !
      Lengo lake sio Urais bali kuivuruga Chadema.
      Kabla ya Zitto kuipaisha chadema ilikuwa haijulikani. Zitto ndiye aliyeipaisha chadema, hii mkitaka msitake.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    12. #849
      mfumo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 21st November 2011
      Posts : 129
      Rep Power : 403
      Likes Received
      23
      Likes Given
      159

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka urais

      Namsikitikia sana zito! Ni kijana shupavu na mwenye mvuto kisiasa. Lakini, ni kijana asiyekuwa na dira. Namashangaa kwa kutokujua mwelekeo wa vyama hivi vya kisiasa ( malengo na dhamira zao) masikini zito. Kamwe hutopewa nafasi ya kugombania urais hapo ulipo! Pole sana.

    13. #850
      Kimweri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2008
      Posts : 409
      Rep Power : 652
      Likes Received
      33
      Likes Given
      4

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka urais

      Quote By MARUKENI
      Mwaka 2007 Mheshimiwa Zitto alikuwa anamiliki gari aina ya Hammer gari ya KIFAHARI ambayo thamani yake ni karibia milioni mia tano baadae akaona matumizi ya hilo gari ni makubwa sana ikabidi abadilishe na kumiliki gari aina ya Vogue ambalo nalo bei zake ni zilezile na consuption ya mafuta kwa hayo magari ipo juu mno.Zitto kwa maneno yake ni mtu anauchungu sana na vijana wa kitanzania ambao wakiamka asubuhi hawajui waelekee wapi na siku itaishaje.Je hapo bado hajapata nafasi ya kuingia Ikulu anamiliki hayo magari ya kifahari kiasi hicho na anauchungu na walala hoi tukimkabidhi IKULU si atakuwa anatumia ndege kutoka tabata kwenda IKULU?kwani mshahara wa mbunge ni shilingi ngapi?
      Dude you are so misinformed it hurts my eyes to reply to you.but since i am no politician i will give it to you straight.
      Hammer thamani yake 500M????are you crazy?deluded?insane?there is so much that is wrong with that statement that everything you write afterwards becomes automatically useless.
      Vogue nalo bei zake ni zile zile...,Damn.unakera?from what universe is a vogue costing around 500M?
      while i do not aplaud Zito for using a Hammer,i do not see anything wrong with a vogue,its a normal car for people who can afford it,its now way a prius,but i would not call it a gas gazzler either.you do not expect a four wheel engine to have a 40MPG rating..,Saying consumption ya mafuta iko juu mno is plainly misguided.
      If only God would give me some clear sign! Like making a large deposit in my name in a Swiss bank.
      - Woody Allen

    14. HRM
      #851
      HRM's Avatar
      Member Array
      Join Date : 31st January 2012
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 16
      Rep Power : 371
      Likes Received
      1
      Likes Given
      3

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka urais

      tunamkubali huyu! tushikamane ndugu zangu

    15. #852
      mbogo31's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th November 2008
      Posts : 535
      Rep Power : 641
      Likes Received
      113
      Likes Given
      108

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Quote By Zitto
      Ndugu zangu. Naomba msome makala nzima kabla ya kuchangia. Msichangie kwa kusoma kichwa cha habari tu. Hii ni makala nimeandika kama majibu kwa makala ya mwanazuoni mmoja kuhusu umri wa Urais.

      Nimesema wazi, kuutaka Urais na kuupata ni mambo mawili tofauti. Kwanza lazima chama changu kiniteue. Kama chama kikiona bado lazima nikubaliane na chama. Kama chama kikiona kuna mwanachama mwingine ana uwezo zaidi yangu lazima nimwunge mkono huyo. Hata kama chama kikiniteua lakini wananchi lazima wakubali. Kwa hiyo unaweza kuutaka Urais lakini usiupate!

      Pili nimejibu hoja za ubaguzi, hatari na matabaka za mwanazuoni huyo. Ni vizuri MoD akachukua makala hiyo na kuiweka juu kabisa ili watu wachangie jambo walilolisoma.

      Miye nitaweka makala hiyo kwenye blog yangu zittokabwe.com
      Mh Zitto, nimesoma nakala yako mwanzo mwisho, kwanza nikwambie tu nimeipenda na umeiandika vizuri na kwa lugha ya kiungwana. kunamambo ambayo mimi nimejifunza kutokana na makala yako, kwa hili nakupongeza sana.

      Sasa ombi langu kwako ni kwamba; wewe ni kijana na nikuonavyo bado unayo nafasi ya kuja kuongoza nchi hii kama utapewa ridhaa hiyo na Mungu, Chama chako na wananchi wenyewe, kwa mwaka 2015 achana na hiyo nafasi watu tunataka kufanya mageuzi ya kishindo na kwa upepo ulivyo Dr Slaa bado kwa mtazamo wangu naona atawakilisha vizuri sana kwenye uchaguzi huo na pia akiapishwa kuwa rais atasafisha uchafu uliopo ili baada ya miaka 5 tuchague rais kijana miongoni mwenu atakayeipeleka nchi katika level nyingine ya uchumi. nimezunguka karibu nchi nzima watu wanamkubali Dr Slaa vijijini kwa mijini na ni watu wa rika zote na dini zote.

      ni mawazo yangu tu.
      insanity is keeping doing the same thing, expecting different results"-msigwa

    16. #853
      mujitahid's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th April 2012
      Location : dar
      Posts : 71
      Rep Power : 370
      Likes Received
      4
      Likes Given
      3

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka urais

      kama ni chama imara chenye muongozo na malengo yaliowazi ipi sababu ya slaa kuwa ndio chaguo halisi na zito kuwa bado katika hilo.kama na ajenda ya kukabalika chadema kinakbalika na wote walio ndani yake

    17. #854
      mujitahid's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th April 2012
      Location : dar
      Posts : 71
      Rep Power : 370
      Likes Received
      4
      Likes Given
      3

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka urais

      kama ni chama imara chenye muongozo na malengo yaliowazi ipi sababu ya slaa kuwa ndio chaguo halisi na zito kuwa bado katika hilo.kama na ajenda ya kukabalika chadema kinakbalika na wote walio ndani yake

    18. #855
      kiribo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 26th August 2012
      Posts : 235
      Rep Power : 807
      Likes Received
      38
      Likes Given
      57

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka urais

      kwa timu hii kaka nyakarungu, mwampamba,mchange,ben saanane,shonza mtemelwa,chagulani bila chadema hujajipanga kupata support labda urais wa mitandaoni unaweza kupata maana vijana wako wamejizatiti saana kutukana chama na viongozi kuliko kushughulika na ujenzi wa chama sisi tunaona kuna hoja kubwa nyuma ya pazia

    19. #856
      Musharaf's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st August 2011
      Posts : 137
      Rep Power : 421
      Likes Received
      16
      Likes Given
      0

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka urais

      Bravo Zitto!

    20. Study Abroad
    Page 43 of 43 FirstFirst ... 33414243

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...