Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Zitto: Ndio ninautaka urais

    Report Post
    Page 4 of 43 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 856
    1. #1
      Mohamedi Mtoi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th December 2010
      Location : Lushoto - Kwemakame.
      Posts : 2,062
      Rep Power : 24551
      Likes Received
      3149
      Likes Given
      357

      Default Zitto: Ndio ninautaka urais

      Mbunge mahiri na machachari kutoka chama makini Zitto Zuberi Kabwe ameweka wazi kuwa anautaka uraisi lakini akiwa atapata ridhaa kutoka kwa chama chake na wananchi kwa ujumla wao,
      NDIO NATAKA KUWA RAIS - Zitto Kabwe


      Kwanza niseme wazi kabisa kabisa kuwa Urais ninautaka.

      Ninaamini ninao uwezo wa kuwa Rais. Ninaamini nina uzalendo wa kutosha na utashi wa kuleta mabadiliko stahili wa namna nchi yetu inavyoongozwa. Ninajua kuwa nchi yetu imesahau maendeleo ya watu na kujikita katika maendeleo ya vitu. Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo (styles) badala ya mambo ya msingi (content). Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika. Ninajua nchi yetu inahitaji Uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa (transformation) badala ya mabadiliko ya juu juu (cosmetic change). Ninajua 'transformation' inahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi na hasa mabwana wakubwa wa nchi za magharibi mfano kuzuia nchi yetu kuuza malighafi tu. Ninajua rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya Umma ni kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi. Ninajua rasilimali kama Madini, Mafuta na Gesi, Ardhi n.k. ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu.


      Hivyo, nchi inahitaji Kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi. Sio kazi rahisi lakini ni kazi ambayo lazima Mtanzania mmoja aifanye. Mimi nataka kuifanya. Nina uwezo wa kuifanya.

      Hata hivyo kazi hii hata kama naitaka ni lazima wenye nchi waamue kunipa kazi hii. Ni lazima kwanza Chama changu kiseme wewe ndio mwanachama unaestahili kuifanya kazi hii. Ni lazima Watanzania wengi waseme wewe ndio mwananchi mwenzetu unayeweza kuchukua jukumu hili. Kuitaka tu haitoshi. Ni lazima wananchi wakuamini na kukupa jukumu hili.



      Sasa kama wananchi watasema huyu Zitto anapaswa kubeba jukumu hili mwaka 2015 tuache iwe. Kama watasema hapana wewe bado mpaka mwaka 2020 au hata 2025 tuache iwe hivyo. Pia Kama hawataki kabisa tuache iwe hivyo.

      Mjadala wa umri wa kugombea Urais imekuwa mjadala mkali sasa. Mjadala huu baadhi ya watu kwa sababu wanazojua wao wameamua kuita ni mjadala wa Zitto na January. Kwamba ni mjadala unaobagua Wazee. Mjadala unaopandikiza chuki na sumu za kibaguzi. Kwamba ni mjadala wa Kitabaka na kuwa Zitto na January sio tabaka stahili la vijana walio wengi. Sitamsemea January, nitajibu baadhi ya hoja za mwandishi wa makala mojawapo kama Zitto. January akitaka atamjibu naye kivyake.

      Mwandishi anasema yeye hapingi hoja ya umri, bali anapinga aina ya watu wanaoshadidia hoja hiyo. Anaipenda hoja ila hapendi watoa hoja. Hoja nzuri lakini Zitto na January wabaya. Amelisema hilo mwanzo kabisa wa makala yake. Kwa hiyo kwake yeye hoja ingeletwa na vijana wengine asingekuwa na shida wala isingekuwa hoja hatari. Kwa kuwa hoja imeletwa na Zitto na January (ingawa sisi sio waanzilishi wa hoja hii) ni hoja ya kibaguzi. Nawashangaa sana wasomi wa siku hizi. Wasomi wanaojadili watu badala ya masuala.

      Mwandishi anasema kwamba vyama vya siasa haviandai vijana kuwa viongozi. Nitamweleza.

      Chama changu kinalea na kukuza vijana kuwa viongozi. Mimi binafsi nimejiunga na chama changu nikiwa na umri wa miaka 16, mtoto. Nimekulia ndani ya chama. Nimepewa majukumu ya kawaida kabisa ya chama kama kusimika miti ya bendera, kupokea viongozi na kuandaa mikutano. Nikiwa Chuo Kikuu Mwenyekiti wa sasa wa Chadema ndugu Mbowe alikuja kuniomba sasa nishiriki kikamilifu kukijenga upya chama. Yeye alikuwa Mbunge wa Hai akitaka chama kiwe imara zaidi, akaambiwa kuna mwanachama wenu kule Mlimani. Wakati huo CHADEMA kilikuwa chama ambacho watu wanakikimbia isipokuwa watu wa Kigoma na Kilimanjaro, Shinyanga, Karatu na Ukerewe. Vijana walikuwa wanajipambanua na CCM zaidi ama CUF au TLP kuliko hiki chama cha mabwanyenye. Huu ni mwaka 2001, muongo mmoja tu uliopita. Mimi na Freeman Mbowe ndio tumefanya mabadiliko yote yanayoonekana CHADEMA. Tumeingiza watu wapya, tumeandika Katiba upya. Ilipofika mwaka 2005 tukasema Freeman Mbowe nenda kwenye Urais, tulijuwa tunashindwa lakini tulitaka kujenga chama chetu. Tukapata Wabunge. Wabunge Wakafanya kazi. Tukaingia mwaka 2010 katika uchaguzi kama chama imara tunachokwenda kuchukua dola.

      Katika mchakato huu tukaingiza vijana kwenye chama na kuwalea. John Mnyika hakuwa CHADEMA, tena alikuwa mgumu sana kuingia kwenye chama chetu. Tukampa moyo. Tukampa majukumu. Leo ni mmoja wa rasilimali watu kubwa sana katika siasa za nchi yetu. Halima Mdee hakuwa mwanasiasa kabisa. Tukampa moyo. Tukampa majukumu. Leo ni Mbunge mahiri kabisa.

      Baadhi ya watu wazima waliingia CHADEMA kufuata vijana. Vijana tulifyeka pori kwanza. Nani anasema hatulei vijana kuwa viongozi wazuri? Nani haoni hazina ya viongozi vijana hivi sasa ndani ya Bunge kutoka vyama vyote? Kuna namna bora ya kulea viongozi zaidi ya kuwapa majukumu?

      Mbowe alikuwa ananifuata pale Hall 1, tunakwenda kufanya kazi za chama usiku kucha, kusoma na kuchambua makabrasha ya kisera na mikakati. Ninarudi chuo usiku wa manane wakati wanafunzi wengine ama wapo wanajisomea au wamelala. Kazi ya kujenga taasisi inayoitwa chama cha siasa.

      Lakini kujengwa kuwa kiongozi sio kazi ya chama pekee. Ni kazi ya jamii kwa ujumla. Wakati wanafunzi wenzangu walikuwa wanaomba kufanya kazi za mafunzo kwenye taasisi kubwa Kama Benki Kuu, nikiwa mwaka wa pili Chuo Kikuu nilikwenda kufanya internship TGNP. Kujifunza Bajeti ya kijinsia na kuipa hoja za kiuchumi. Kina mama wa TGNP wakanijenga na kunipika kiuongozi.

      Chuo Kikuu sikuwa nasoma Sosholojia, lakini rafiki yangu mkubwa alikuwa Chachage. Sikuwa nasoma lugha, lakini mshauri wangu alikuwa Lwaitama. Sikuwa nasoma sheria lakini nilikuwa namwakilisha Shivji na kusoma mada zake alizopasa kuwakilisha kwenye semina kadhaa kuhusu haki za binadamu. Nimefunzwa na makundi ya watu mbalimbali na sio chama changu pekee. Jamii ndio yenye jukumu la kufunda vijana kuwa viongozi. Jamii inafanya kazi hiyo?

      Inasemwa mjadala huu ni hatari kwa namna ulivyopenyezwa. Kupenyezwa? Huu mjadala wa umri umeanza kuzungumzwa mimi nikiwa nipo Chuo Kikuu. Vijana kupitia National Youth Forum Kama Taasisi ya vijana wamekuwa wakisema jambo hili toka miaka ya katikati ya tisini. Jukwaa hili la Vijana chini ya viongozi wake kina Hebron Mwakagenda wamekuwa wakitoa Maazimio na Maazimio kwamba umri wa kugombea Urais upo juu sana toka miaka ya tisini. Taasisi ya TYVA imekuwa ikijenga hoja hii toka miaka ya 2000. Hii sio hoja mpya hata kidogo. Hoja hii haijapenyezwa. Hii ni hoja ya vijana ya miaka mingi sana. Lakini sishangai kuona inaonekana ni hoja mpya kwani watanzania uwezo wetu wa kutunza kumbukumbu ni mdogo sana. Pia tunapenda kujadili mtoa hoja na sio hoja yenyewe. Mfuatiliaji yeyote makini wa siasa za vijana wa Tanzania kupitia makongamano ya vijana anajua hii sio hoja iliyopenyezwa na Zitto au January. Kuijadili kwa kumwangalia Zitto na January ni kuchoka kufikiri.


      Hoja hii haina hatari yeyote inayosemwa na mwandishi. Hoja hii ni hoja kama hoja nyingine yeyote na inaweza kupita au kukataliwa. Hii sio hoja ya watu fulani. Ni hoja ya vijana ya siku nyingi sana. Vijana hawa wanajiona kupitia vijana wengine walio kwenye nafasi mbalimbali kisiasa au hata katika sekta binafsi. Mfano vijana wa Kigoma ninakotoka wakiniangalia wanajiona. Ndio wanaona tuko sawa. Wanaona mimi ni mwenzao. Nimekua miongoni mwao. Nimesoma nao. Nimecheza nao. Nimehangaika nao. Wanaona Ubunge nilionao ni Dhamana tu na hawanizungumzishi kama mtu kutoka tabaka fulani, bali kama mwenzao.

      Ninaishi maisha ninayoishi. Siishi Manzese kwa Mfuga Mbwa. Siishi Masaki pia. Naishi Tabata, kwenye nyumba ya kupanga. Tabata wanaishi vijana wote wale wa tabaka la chini kama asemalo mwandishi na pia tabaka la kati na labda tabaka la juu. Najua na kusikia machungu ya vijana wasio na ajira na ndio maana nahangaika kwa kutumia nafasi ya Ubunge kujaribu kuisukuma Serikali iweke sera zinazotekelezeka za kutatua tatizo la ajira kwa vijana. Ndio maana nahangaika kila siku kujenga hoja kwamba Serikali iingilie kati ukuaji wa uchumi ili pia wanyonge wafaidike. Ninasikia machungu ya vijana wasio na ajira maana ndio walionipigia kura kuwa Mbunge. Zaidi ya hayo nakutana nao sana kuzungumza namna ya kusaidiana.


      Nakutana nao mitaani kwa mijini na vijijini ninakokwenda kila wakati. Nakutana nao kwenye mitandao ya kijamii, wananiandikia na mimi ninawajibu. Nagawana nao kidogo nilichonacho ili nao waweze kijikwamua. Nawasaidia vijana wenye vipaji kukuza vipawa vyao na kupata kipato. Mwandishi anapata wapi haki ya kusema sentensi rahisi rahisi kwamba mimi sisikii machungu ya vijana wenzangu?

      Ninashinda na vijana wa aina zote, ndio kazi kubwa ya Mwakilishi anayefanya kazi yake. Nina marafiki wavuvi, mafundi seremala, waimbaji wa Bongo Flava, machinga na hata wasio na ajira. Nina marafiki wenye makampuni yao, wafanyakazi wa mashirika ya Umma, wasomi wa Vyuo Vikuu na wafanyabiashara wakubwa. Mwakilishi yeyote wa wananchi lazima asikie machungu ya jamii nzima vinginevyo hatoshi.

      Kijana mwenye umri wangu ana mambo mengi anayofanana nami. Ana mambo mengi ya kujifunza kutoka kwangu. Hapa katikati ilikuwa ni kama jambo lisilowezekana kijana wa aina yangu kutoka familia masikini kabisa kuwa Mbunge. Baada ya Zitto kuwa Mbunge na kutokana na kazi niliyofanya Bungeni katika Bunge la Tisa, vijana wengi walihamasika na kusema wanaweza. Leo tuna vijana wadogo kabisa kutoka familia za kawaida kabisa ni Wabunge na wanafanya vizuri. Kina Kafulila, kina Mkosamali, kina Silinde hawa ni watoto wa kimasikinj kabisa ambao ni wa kwanza kupata shahada kwenye familia zao. Hii ni nguvu ya 'inspiration' kutoka kwa rika linalofanana. Sugu ni mkubwa kwangu kiumri, lakini kuingia kwake siasa kumechangiwa sana na kazi zangu pamoja na wenzangu kwenye Bunge.

      Kuna vijana wengi zaidi nchini kwetu wanasema ninataka niwe kama Zitto, kama January, kama Halima Mdee. Tunazungumza nao. Tunaishi nao. Ni ndugu zetu. Ni rafiki zetu. Tunaishi nao mtaani. Tunakwenda nao kwa kinyozi mmoja. Tunakwenda muziki pamoja. Ninajua machungu ya vijana. Ninafanyia kazi machungu ya vijana. Ndio kazi yangu ya kila siku kama Mbunge, kama Mwakilishi wao.

      Mwandishi anasema mjadala unalenga kuleta ubaguzi. Sioni hoja yake. Wanaosema umri wa kugombea Urais ushushwe chini ya miaka 40 hawasemi wazee wasigombee. Wanasema tupanue wigo wa haki hii ya kugombea. Wanaozungumza ubaguzi ndio wenye kupenyeza mbegu za kibaguzi. Kwa kuwa wanawaza kibaguzibaguzi basi kila jambo huliangalia kibaguzi. Kama Katiba inasema yeyote mwenye haki ya kupiga kura ana haki ya kugombea nafasi yeyote ya uongozi, ubaguzi unatoka wapi? Hoja zote zinazotolewa na mtoa hoja kuhusu ubaguzi zinasambaza mbegu ya ubaguzi.

      Mwandishi sasa anawaambia Watanzania waanze kufikiri sasa zamu ya nani. Mimi binafsi sijawahi kusema hii ni zamu ya vijana. Ila nimesema changamoto za sasa za nchi zinahitaji mtu mwenye uwezo wa kuzikabili, ninaamini mtu huyo ni kijana. Ninaamini kuwa kila kizazi kina ajenda zake. Kizazi chetu kina kazi ya kuhakikisha uhuru wa kiuchumi wa nchi yetu. Kizazi cha kina Mwalimu kilikuwa cha ukombozi na kujenga Taifa moja. Mwandishi hamwamini Frantz Fanon?

      Hoja ya kwamba mjadala huu unataka kununua hisia za wanyonge ni hoja isiyo na [mashiko] kabisa. Mimi nimechaguliwa na wanyonge mara mbili kuwa Mbunge wao. Wanyonge wamenipa Ubunge bila kutoa rushwa. Wamenipa Ubunge kwa kuniamini. Sasa kwa nini sasa ninunue hisia zao? Hii hoja ina misingi gani? Hii ni hoja ya kubandika. Hii ni hoja ya kubumba maneno ili mwandishi aonekane kwamba anafanya uchunguzi wa kitabaka. Hakuna dhana ya tabaka katika hoja hii kama ilivyo kuwa hakuna dhana ya tabaka kwa wazee au hata wanawake. Hoja hii haizuii kwa namna yeyote ile wananchi kuhoji chanzo cha ufukara wao. Kwanza wanaosemwa kwenye hoja hii ndio wapo mstari wa mbele kuhakikisha Mali ya Nchi inatumika wa maendeleo ya wananchi. Mimi binafsi nimeanzisha mjadala wa rasilimali Madini nchini mpaka kutungwa kwa sheria mpya inayoweka misingi ya nchi kufaidika na Madini. Mimi binafsi na wenzangu tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha serikali inatekeleza sheria mpya.

      Mwandishi amesahau Buzwagi? Mwandishi amesahau hoja ya Mkonge inayotaka wanyonge wapewe mashamba ya Mkonge na wawezeshwe na Serikali kulima Katani? Mwandishi amesahau hoja ya kusimamia sekta ya nyumba ili wanyonge wasinyonywe na wenye nyumba ambayo imetolewa na mmoja wa wanaotetea hoja ya umri kushushwa? Ama mwandishi ana wanyonge wake anaowasemea? Sio hawa manamba kwenye Mkonge. Sio hawa vijana wachimbaji wadogo. Sio hawa vijana wanaoshindwa kulipa kodi ya nyumba mwaka mzima? Wanyonge wa mwandishi ni wanazuoni wanaoishi kwa fedha za walipa kodi ambao hawana shida ya kujiuliza kama watakula au watalala maana Serikali au wafadhili wa masomo yao wanawalipia malazi na chakula. Kama wanyonge wake ni hawa waliotupigia kura sisi ili kuwawakilisha Bungeni, basi mwandishi hajui asemalo.

      Hoja ya umri wa kugombea Urais, kwa kuweka pa kuanzia ama kuweka kikomo inapaswa kujadiliwa bila kuangalia majina ya wanaotetea hoja hii. Ijadiliwe kwa faida na hasara zake. Kujenga hoja kwa misingi ya kitabaka ni kuchochea ubaguzi na kunyweshea mbegu za kibaguzi. Nani ana uhakika kuwa Zitto atakuwa anaishi ifikapo mwaka 2015? Kwamba tusiandike Katiba yenye kupanua wigo wa kutoa haki ya kugombea Urais kwa sababu ya Zitto?


      Huu woga dhidi ya Zitto unatoka wapi?
      CHANZO: http://udadisi.blogspot.com

    2. Miaka 50

    3. #61
      Mohammed Shossi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th January 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 3,801
      Rep Power : 1192
      Likes Received
      853
      Likes Given
      250

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi

      Namuona mheshimiwa yumo ndani ya nyumba

      1.eti mhe yasemwayo yana ukweli?
      2.je ni kweli kwenye chama hakuna mtu mwingine ila slaa peke yake?
      3.je Dr akisema hagombei hamtaweka mgombea urais 2015? kumbuka kila kitu kinawezekana as we are human beings and not machines/angels.
      Siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale uwongo utakapojitenga - Zitto Z. Kabwe

    4. #62
      Wingu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2011
      Posts : 3,974
      Rep Power : 1217
      Likes Received
      247
      Likes Given
      41

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi

      Haya bwana minyukano ndani ya chama itakapo anza hapo amini usiamini.Wako watu ndani ya chama ambao hawataki kabisa kumsikia huyu jamaa na kundi lake

    5. #63
      Fredrick Sanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2011
      Location : Kijitonyama
      Posts : 2,982
      Rep Power : 2589
      Likes Received
      637
      Likes Given
      776

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi

      Kwa nini mnanchukia Zitto, Atafaa muda muafaka kama yeye alivyosema.
      mawazotu likes this.
      We shall overcome, righteousness shall always prevail.

    6. #64
      Angel Msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Posts : 6,266
      Rep Power : 1826
      Likes Received
      1397
      Likes Given
      0

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi

      yakwenu yamewashinda hamjui mumsimamishe nani, mmehamia kuchokonoa kwa jirani zenu.

    7. #65
      1800's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th December 2010
      Posts : 1,657
      Rep Power : 891
      Likes Received
      415
      Likes Given
      21

      Default

      Quote By Molemo
      Mkuu nimeachana naye nadhani huyu G.Brain hakumaliza drs la saba.
      Afadhali mkuu,dawa ya mjinga ni kumpuuzia ajione ujinga wake hakuna mwingine anaye uchangia,maana ukianza ku argue nae,pia na yeye atajiona kumbe ana + ideas!

    8. FemaTV & Radio

    9. #66
      Mzito Kabwela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th November 2009
      Location : MPUMBULI
      Posts : 6,424
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1086
      Likes Given
      7

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi

      Kama ni vijana wafaao kugombea urais ,
      Komredi Martine Shigella anafaa zaidi kuliko wote

    10. #67
      idawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2012
      Posts : 4,587
      Rep Power : 3331
      Likes Received
      1220
      Likes Given
      460

      Default

      Quote By Angel Msoffe
      we ni gamba na km ni mwanachadema basi hauko makini.
      niko makini na ndio maana sio muumini wa zidumu fikra za mwenyekiti.

    11. #68
      Rufiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2006
      Posts : 1,574
      Rep Power : 976
      Likes Received
      281
      Likes Given
      49

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi

      Kuchangia kuhusu Zitto na mwenzake January kugombea urais 2015 ni kupoteza muda kwani katiba haitawaruhusu kufanya hivyo kutokana na umri wao. Kinachotakiwa kufanyika ni kubadili katiba kwanza, kitu ambacho itakuwa ni vigumu kufanyika.

      Hawa vijana inawezekana wana dhamira lakini bado hawajajua jinsi ya kufanikisha malengo yao ya kisiasa. Ili waweze kubadili umri wa kugombea ni lazima wapitie bungeni, ambapo majority ya wabunge wana umri zaidi ya miaka 40. Sasa kitendo cha kusema ni kijana hatakayeweza kukabili challenge za urais, kiasi fulani kitawaudhi wabunge ambao sio vijana na hawataupigia kura huo mswada ukiwasilishwa.

      Hawa watu wangetafuta njia itakayofanya hoja yao iwe na mshiko bila ya kudharau upande mwingine. Na kwa kiasi fulani hii inaonyesha ni jinsi gani ambavyo bado hawajaiva katika siasa...

    12. #69
      Angel Msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Posts : 6,266
      Rep Power : 1826
      Likes Received
      1397
      Likes Given
      0

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi

      habari za kuaminika kutoka ndani ya vikao vya ccm zinadai kuwa CCM INATARAJIA KUMSIMAMISHA WASSIRA a.k.a TYSON kugombea urais kutokana na kuwa na mvuto wa kisiasa hasa katika kampeni za Arumeru mashariki. Souce: Tingatinga

    13. #70
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,422
      Rep Power : 10874
      Likes Received
      3800
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By Fredrick Sanga
      Kwa nini mnanchukia Zitto, Atafaa muda muafaka kama yeye alivyosema.
      Ni makosa makubwa kumchukia Zitto kama Zitto.Huyu na vijana wengine ni hazina kubwa ndani ya chama miaka ijayo.Anachopaswa kufanya Zitto ni kuwa mtiifu kwa viongozi wake na kukijenga chama kuanzia vijijini. Zitto anapaswa kujiweka mbali na makundi ya wapuuzi wanaochochea migawanyiko ndani ya chama na kujaribu kuwachafua viongozi kupitia mitandao ya kijamii.Binafsi ninaamini nguvu ya CDM kwa sasa pia Zitto ana mchango mkubwa.Zitto anafaa lakini bado anahitaji kupikwa zaidi ndani ya chama.

    14. #71
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,502
      Rep Power : 46710
      Likes Received
      16361
      Likes Given
      8419

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi

      Ooh boy!!
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    15. #72
      Angel Msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Posts : 6,266
      Rep Power : 1826
      Likes Received
      1397
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By idawa
      niko makini na ndio maana sio muumini wa zidumu fikra za mwenyekiti.
      huko kwenu ndo kuna hizo fikra.

    16. #73
      peter tumaini's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2012
      Location : DSM
      Posts : 575
      Rep Power : 483
      Likes Received
      86
      Likes Given
      54

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Quote By Zitto
      Ndugu zangu. Naomba msome makala nzima kabla ya kuchangia. Msichangie kwa kusoma kichwa cha habari tu. Hii ni makala nimeandika kama majibu kwa makala ya mwanazuoni mmoja kuhusu umri wa Urais.

      Nimesema wazi, kuutaka Urais na kuupata ni mambo mawili tofauti. Kwanza lazima chama changu kiniteue. Kama chama kikiona bado lazima nikubaliane na chama. Kama chama kikiona kuna mwanachama mwingine ana uwezo zaidi yangu lazima nimwunge mkono huyo. Hata kama chama kikiniteua lakini wananchi lazima wakubali. Kwa hiyo unaweza kuutaka Urais lakini usiupate!

      Pili nimejibu hoja za ubaguzi, hatari na matabaka za mwanazuoni huyo. Ni vizuri MoD akachukua makala hiyo na kuiweka juu kabisa ili watu wachangie jambo walilolisoma.

      Miye nitaweka makala hiyo kwenye blog yangu zittokabwe.com
      Shukrani kwa ufafanuzi huo, nimesoma makala yako kwa usahihi sana na nimeielewa.

      Fanya kazi kwa bidii kwani taifa letu lina changamoto nyingi sana fanyia kazi hizo changamoto kwa nguvu zako zote, naamini tumeshaona bidii yako na tunahitaji ufanye zaidi; wakati ukifika hutakuwa na mpinzani mkuu.

      Kuhusu hili swala la ajira kwa vijana naomba uandae forum ya kulijadili na uishauri serikali iliweza kutenga maeneo kwa ajili ya EPZ kwa kila wilaya, itenge tena maeneo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi kwa vijana kila wilaya kulingana na mahitaji na eneo kama maeneo ya kilimo, holticulture, matunda, mkonge, korosho, viwanda vidogo vidogo. Anza kwa kuondoa changamoto hii.
      Ben Saanane and mshikachuma like this.

    17. #74
      Nyalotsi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th July 2011
      Posts : 2,653
      Rep Power : 926
      Likes Received
      587
      Likes Given
      83

      Default

      Quote By FJM
      Labda Zitto wa 2007, lakini Zitto wa 2012 - siungi mkono.
      nimepoteza imani na zito ambayo nilikuwa kabla. Huyu na mwenzake wamekaa na mwenzake wanaplani kuwaminya watu waliojenga nyumba na kupangisha,eti itaongeza mapato! Wafanyabiashara kibao wanakwepa kodi,madini yetu, samaki wetu, ardhi yetu wanaacha vinabebwa na wazungu. Wanyama wetu,magogo yetu vyote vinaibiwa, kwa nini umuumize mpangaji? Hawajui kwamba ni kutuumiza sie wapangaji? No matter why walikuwa wanadai umri upunguzwe.

    18. #75
      Mzito Kabwela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th November 2009
      Location : MPUMBULI
      Posts : 6,424
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1086
      Likes Given
      7

      Default

      Quote By Angel Msoffe
      habari za kuaminika kutoka ndani ya vikao vya ccm zinadai kuwa CCM INATARAJIA KUMSIMAMISHA WASSIRA a.k.a TYSON kugombea urais kutokana na kuwa na mvuto wa kisiasa hasa katika kampeni za Arumeru mashariki. Souce: Tingatinga
      na pia sura yake inauzika, na kwamba ccm wanampango kutumia wingi wao bungeni kuishinikiza serikali ichapishe sura ya rais kwenye noti zetu. Jambo hili litafanya SURA YA WASSIRA ITOKEE KWENYE NOTI PINDI ATAKAPOKUWA RAIS
      Kimox Kimokole likes this.

    19. #76
      Ngongo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th September 2008
      Location : Mlima Meru
      Posts : 4,869
      Rep Power : 1976
      Likes Received
      2340
      Likes Given
      3022

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi.

      Heshima kwako Zitto,

      Nimesoma makala yako kwa kweli imetulia sana na imenivutia kiasi nakosa neno sahihi la kuelezea jinsi nilivyovutiwa na hoja zako.Kuna jambo moja nashindwa kukuamini/kukuelewa ni msimamo wako kuelekea shirikisho la EAC, nakumbuka michango yako ndani bunge letu ulishindwa kutetea maslahi ya Tanzania huku wabunge wengi wakipinga suala la ardhi na ajira kuingizwa katika mkataba wa EAC. Naomba unijuze bado msimamo wako ni uleule na kwanini au umebadilika kwanini ?
      Quote By Zitto
      Ndugu zangu. Naomba msome makala nzima kabla ya kuchangia. Msichangie kwa kusoma kichwa cha habari tu. Hii ni makala nimeandika kama majibu kwa makala ya mwanazuoni mmoja kuhusu umri wa Urais.

      Nimesema wazi, kuutaka Urais na kuupata ni mambo mawili tofauti. Kwanza lazima chama changu kiniteue. Kama chama kikiona bado lazima nikubaliane na chama. Kama chama kikiona kuna mwanachama mwingine ana uwezo zaidi yangu lazima nimwunge mkono huyo. Hata kama chama kikiniteua lakini wananchi lazima wakubali. Kwa hiyo unaweza kuutaka Urais lakini usiupate!

      Pili nimejibu hoja za ubaguzi, hatari na matabaka za mwanazuoni huyo. Ni vizuri MoD akachukua makala hiyo na kuiweka juu kabisa ili watu wachangie jambo walilolisoma.

      Miye nitaweka makala hiyo kwenye blog yangu zittokabwe.com

    20. #77
      Fredrick Sanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2011
      Location : Kijitonyama
      Posts : 2,982
      Rep Power : 2589
      Likes Received
      637
      Likes Given
      776

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi

      Quote By Angel Msoffe
      habari za kuaminika kutoka ndani ya vikao vya ccm zinadai kuwa CCM INATARAJIA KUMSIMAMISHA WASSIRA a.k.a TYSON kugombea urais kutokana na kuwa na mvuto wa kisiasa hasa katika kampeni za Arumeru mashariki. Souce: Tingatinga
      Kwa kweli watakuwa wamefanya la maana sana, maana yeye ni taswira ya CCM kabisa.
      We shall overcome, righteousness shall always prevail.

    21. #78
      mgomba101's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 1,548
      Rep Power : 779
      Likes Received
      541
      Likes Given
      249

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi

      Nashangaa hapa Tz kila mtu anataka kuwa RAIS!! mpaka mzito kabwela nae anautaka urais!! anashinikiza umri wa urais uwe miaka 35!! Bado naaamini Dr slaa au Dr salim Ahmed Salim wanaweza kutuongoza vizuri.
      Nawakiulisha.
      MR.SILVER likes this.
      You can fool all the people some of the time, and some of the people all the time, but you cannot fool all the people all the time.

    22. #79
      Angel Msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Posts : 6,266
      Rep Power : 1826
      Likes Received
      1397
      Likes Given
      0

      Default Re: Zitto: Ndio ninautaka uraisi

      zitto ni kijana mpambanaji na jasiri lakini kuna tatizo alilonalo linalomkosesha imani mbele za Watanzania, pamoja na umaarufu wake wote alionao lakini kwa sasa hafai kuwa rais wa Tz,
      MR.SILVER likes this.

    23. #80
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,422
      Rep Power : 10874
      Likes Received
      3800
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By Nyalotsi
      nimepoteza imani na zito ambayo nilikuwa kabla. Huyu na mwenzake wamekaa na mwenzake wanaplani kuwaminya watu waliojenga nyumba na kupangisha,eti itaongeza mapato! Wafanyabiashara kibao wanakwepa kodi,madini yetu, samaki wetu, ardhi yetu wanaacha vinabebwa na wazungu. Wanyama wetu,magogo yetu vyote vinaibiwa, kwa nini umuumize mpangaji? Hawajui kwamba ni kutuumiza sie wapangaji? No matter why walikuwa wanadai umri upunguzwe.
      Mkuu wangu huu upuuzi wa kuweka sheria ya kodi kwa wenye nyumba ni hoja hovyo kabisa ya January Makamba.Hakika hiki ni kitanzi kwa vijana wote mijini wanaoishi nyumba za kupanga.Hivi ni mwenye nyumba gani ataacha kupandisha kodi kufidia hasara atakayopata? Ninaomba CDM waongoze maandamano ya kulaani sheria hii haramu.CDM fahamuni nguzo kuu yenu ni Vijana na sisi ndio tutaumia kwa sheria hii ya hovyo isiyojali umasikini wetu.Nimuulize swali January hivi haoni kila serikali inapopandisha kodi vitu vinapanda bei? Sasa anadhani kodi ya kwenye nyumba atabeba mwenye nyumba au mpangaji? Nitalia na Mungu na hii sheria ya hovyo ya kuwaangamiza vijana mpaka siku Mungu atakapojibu maombi yangu.
      Rufiji and Ngongo like this.

    Page 4 of 43 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...