Show/Hide This

  Topic: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

  Report Post
  Page 1 of 7 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 131
  1. bibikuku's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th February 2011
   Posts : 818
   Rep Power : 669
   Likes Received
   473
   Likes Given
   334

   Default Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Viongozi wa CCM wazidi kuaibika, baada ya Mkapa sasa ni zamu ya wasira ambapo Kanisa katoliki limekana kuwepo kwa ulaji fedha wakati wa ziara ya Papa na kumtaka Wasira atoe ushahidi............... Sinema zaendelea.

   Kanisa Katoliki Lamshukia Wasira

   LASEMA KAMA ANAO USHAHIDI WA WIZI WA FEDHA ZA PAPA AUTOE, WANASIASA WANAOCHAFUA WENZAO WAMEFILISIKA

   Na Waandishi Wetu

   KANISA Katoliki nchini limemtaka Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano wa Jamii), Stephen Wassira kutoa ushahidi kuthibitisha kama Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alifukuzwa upadre baada ya kuiba fedha za ujio wa Papa John Paul II, alipokuja nchini mwaka 1991.

   Akizungumza kwa simu jana, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Yuda Thadeus Ruwaichi alimtaka Wassira athibitishe tuhuma zake akisema kanisa hilo halijawahi kumtuhumu Dk Slaa kwa tuhuma za wizi.

   Akizungumza katika kampeni za CCM Jimbo la Arumeru Machi 19, mwaka huu, Wassira alimtupia kombora Dk Slaa akidai si mwaminifu kwa kuwa alifukuzwa ukasisi wa kanisa hilo baada ya kufanya ufisadi kwenye fedha za mapokezi ya Papa huyo ambaye sasa ni marehemu.

   Hata hivyo, Wassira jana alipotakiwa kuzungumzia kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi alijibu kwa kifupi: “Mimi nilishazungumza na yakaandikwa kwenye vyombo vya habari, hii leo siyo habari.”

   Ruwaichi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mwanza alisema madai hayo ya Wassira hayana msingi.

   “Kanisa halijawahi kumshutumu Dk Slaa kuhusu madai hayo (ya Wassira). Kama Wassira ameyatoa kwenye mkutano wa hadhara, njia sahihi ya kupata ukweli ni yeye kutupa ushahidi wa vielelezo kuthibitisha madai yake,” alisema Ruwaichi.

   Askofu Ruwaichi amewaonya wanasiasa wanaofanya kampeni za kuchafuana akiwataka waache na waanze kufanya siasa za kistaarabu.

   “Ukiona mwanasiasa anakurupuka na kuanza kumchafua mwenzake ujue amefilisika, vitendo hivyo vinaonyesha udhaifu kwa nchi katika nyanja za siasa,” alisema.

   Askofu Ruwaichi alisema wanasiasa waliokomaa hawapaswi kufanya kampeni za kuchafuana... “Watajishughulisha katika kujadili hoja zinazozingatia mahitaji ya jamii. Kitendo cha wanasiasa wetu kufanya kampeni za kuchafuana kinaonyesha dhahiri kuwa bado tuko dhaifu katika siasa na hatuna vipaumbele.”

   Askofu Ruwaichi aliwataka wanasiasa hao kuachana na kampeni chafu na badala yake wajikite katika kujadili hoja zinazotoa vipaumbele katika matatizo yanayoikabili jamii na namna ya kuyatatua ili kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi bora.

   Kauli hiyo ya Askofu Ruwaichi, imekuja siku chache baada ya Dk Slaa kuzungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru na kusema Wassira ni mwongo na hajui asemalo.

   “Kama tangu mwaka 1991 nipo, basi kitendo cha Serikali kushindwa kunifungulia mashtaka ya wizi wa hizo fedha basi ni Serikali dhaifu na ijiuzulu,” alisema Dk Slaa.

   MY TAKE:
   Ni aina gani ya viongozi wa CCM tulionao kila wakati maneno yao yanakanushwa na kubainika kuwa ni uongo? Alianza Mkapa kudanganya sasa kafuata Wasira. Who is next??

   Last edited by bibikuku; 21st March 2012 at 03:53.
   mizambwa, Kingo, Mwanamayu and 3 others like this.

  2. DSN's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd February 2011
   Location : Home Tanzania
   Posts : 1,614
   Rep Power : 4583
   Likes Received
   813
   Likes Given
   880

   Default re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Yaliyojili ni zawadi ya shukrani kwa kanisa kuwapa nafasi viongozi wa wasio waadilifu na wasio na hofu ya Mungu wanapopewa nafasi kwenye membali za makanisa hatimae hawana aibu kutamka mambo yasiyo na pciha nzuri kwa kanisa yanayolihusu pasipo ushahidi kuhusu ukweli wa matukio hayo tajwa.Nategemea next time wahusika watakuwa ni wageni waalikwa kwenye sherehe za makanisa na misikiti.
   NnyaMbwate and bibikuku like this.

  3. bibikuku's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th February 2011
   Posts : 818
   Rep Power : 669
   Likes Received
   473
   Likes Given
   334

   Default re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Quote By DSN View Post
   Yaliyojili ni zawadi ya shukrani kwa kanisa kuwapa nafasi viongozi wa wasio waadilifu na wasio na hofu ya Mungu wanapopewa nafasi kwenye membali za makanisa hatimae hawana aibu kutamka mambo yasiyo na pciha nzuri kwa kanisa yanayolihusu pasipo ushahidi kuhusu ukweli wa matukio hayo tajwa.Nategemea next time wahusika watakuwa ni wageni waalikwa kwenye sherehe za makanisa na misikiti.
   duh kauli yako hii, let me reserve my comment

  4. timbilimu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd September 2010
   Location : DSM
   Posts : 4,236
   Rep Power : 1377
   Likes Received
   1173
   Likes Given
   426

   Default re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Nashukuru Kanisa langu limekemea uhuni wa Wasira.

  5. bibikuku's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th February 2011
   Posts : 818
   Rep Power : 669
   Likes Received
   473
   Likes Given
   334

   Default re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Quote By timbilimu View Post
   Nashukuru Kanisa langu limekemea uhuni wa Wasira.
   kwa trend ya viongozi wa CCM nilitarajia kabisa hili kutokea. tusubiri who'll be the next kutudanganya tena watanzania kama viongozi wetu walivyozoea
   mizambwa likes this.

  6. UmkhontoweSizwe's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 19th December 2008
   Posts : 2,334
   Rep Power : 1085
   Likes Received
   680
   Likes Given
   398

   Default re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Sikutegemea kama ccm ya Mwalimu inaweza kugeuka na kuwa li-chama la wajinga kiasi hiki! Kama tunatawaliwa na chama cha wajinga Kama Wasira, basi Mungu atuhurumie.

  7. bibikuku's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th February 2011
   Posts : 818
   Rep Power : 669
   Likes Received
   473
   Likes Given
   334

   Default re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Quote By UmkhontoweSizwe View Post
   Sikutegemea kama ccm ya Mwalimu inaweza kugeuka na kuwa li-chama la wajinga kiasi hiki! Kama tunatawaliwa na chama cha wajinga Kama Wasira, basi Mungu atuhurumie.
   mwalimu akifufuka leo atatandika wote hawa six strokes each!

  8. Gang Chomba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th February 2008
   Location : hell
   Posts : 6,724
   Rep Power : 2148
   Likes Received
   1463
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By bibikuku View Post
   mwalimu akifufuka leo atatandika wote hawa six strokes each!
   Ni 12 strokes...
   Wakawaonyeshe na wake zao.

  9. politiki's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd September 2010
   Posts : 2,015
   Rep Power : 1557
   Likes Received
   1069
   Likes Given
   181

   Default re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   jamani hakuna mwana CCM hata mmoja anakipenda chama hiki angalau akasimama na kukemea mambo haya
   mizambwa and bibikuku like this.

  10. Kikarara78's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th November 2010
   Location : Dar es Salaam
   Posts : 417
   Rep Power : 602
   Likes Received
   78
   Likes Given
   648

   Default re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   DSN na Wana JF,
   Mkuu comments yako haiendani na Mada au hoja ya muhusika, ungesoma mada yote ndio u-comments, labda nimekuelewa vingine, kiujumla upo nje ya mada, labda ufafanue una maana gani.
   Nawakilisha

   Quote By DSN View Post
   Yaliyojili ni zawadi ya shukrani kwa kanisa kuwapa nafasi viongozi wa wasio waadilifu na wasio na hofu ya Mungu wanapopewa nafasi kwenye membali za makanisa hatimae hawana aibu kutamka mambo yasiyo na pciha nzuri kwa kanisa yanayolihusu pasipo ushahidi kuhusu ukweli wa matukio hayo tajwa.Nategemea next time wahusika watakuwa ni wageni waalikwa kwenye sherehe za makanisa na misikiti.
   bibikuku likes this.

  11. bibikuku's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 16th February 2011
   Posts : 818
   Rep Power : 669
   Likes Received
   473
   Likes Given
   334

   Default re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Quote By politiki View Post
   jamani hakuna mwana CCM hata mmoja anakipenda chama hiki angalau akasimama na kukemea mambo haya
   sifa ya kwanza ya kuwa mwanaCCM ni kuwa mnafiki
   Yo Yo, Kiduku and Memo like this.

  12. Raia Fulani's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 12th March 2009
   Posts : 9,914
   Rep Power : 2842
   Likes Received
   1509
   Likes Given
   962

   Default Re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   dah! Yalishaandikwa siku za nyuma hivyo si habari tena

  13. Janjaweed's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th January 2010
   Posts : 6,235
   Rep Power : 86701666
   Likes Received
   2885
   Likes Given
   3814

   Default

   Quote By bibikuku View Post
   mwalimu akifufuka leo atatandika wote hawa six strokes each!
   hapana mkuu

   akifufuka leo.... Atakufa tena kwa mshtuko

  14. senzoside's Avatar
   Senior Member Array
   Join Date : 13th March 2012
   Posts : 125
   Rep Power : 476
   Likes Received
   16
   Likes Given
   27

   Default Re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Mnajua wasira anafikiria kwa ********* sasa kama aliiba fedha hizo inabidi kudhibitisha akishidwa kutoa udhibitisho nadhani azomewe kila apitapo kwasababu naona mavuvuzela wamezidi CCM

  15. sanjo's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 29th October 2010
   Posts : 881
   Rep Power : 698
   Likes Received
   239
   Likes Given
   34

   Default

   Quote By Raia Fulani View Post
   dah! Yalishaandikwa siku za nyuma hivyo si habari tena
   Mfa maji haachi kutapatapa. Wewe ulitarajia Wassira alivyo ataongelea issues zipi za maana akiwa ndani ya mazingira kumwombia S. Sumari kura za huruma? This is one of the most useless and inefficient minister in the Cabinet.

  16. Katavi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 31st August 2009
   Location : Lyamba Lya Mfipa
   Posts : 28,562
   Rep Power : 271423474
   Likes Received
   5056
   Likes Given
   3205

   Default Re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Wassira hana hoja tena eti "hii leo sio habari"

  17. Sumba-Wanga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd February 2011
   Location : Gambushi
   Posts : 5,312
   Rep Power : 0
   Likes Received
   1137
   Likes Given
   1388

   Default Re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Quote By UmkhontoweSizwe View Post
   Sikutegemea kama ccm ya Mwalimu inaweza kugeuka na kuwa li-chama la wajinga kiasi hiki! Kama tunatawaliwa na chama cha wajinga Kama Wasira, basi Mungu atuhurumie.
   Mungu alishatusamehe!
   "A man's or woman's best or worst choice in life is his or her spouse"

  18. Mzito Kabwela's Avatar
   JF Bronze Member Array
   Join Date : 28th November 2009
   Location : MPUMBULI
   Posts : 12,403
   Rep Power : 86489592
   Likes Received
   2373
   Likes Given
   20

   Default

   Quote By timbilimu View Post
   Nashukuru Kanisa langu limekemea uhuni wa Wasira.
   Hivi Wassira hakujua kuwa anachoongea ni uongo na unafiki? What was the motive behind uongo wake?

  19. Mungi's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 23rd September 2010
   Location : JF
   Posts : 16,026
   Rep Power : 115513633
   Likes Received
   8436
   Likes Given
   4550

   Default Re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   Point:
   Wameshindwa kujadili hoja zinazozingatia mahitaji ya jamii badala yake wanaeneza siasa za kishenzi!
   Wamefilisika hoja!

  20. tindikalikali's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th January 2011
   Posts : 4,320
   Rep Power : 32373816
   Likes Received
   774
   Likes Given
   118

   Default Re: Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

   “Mimi
   nilishazungumza
   na
   yakaandikwa
   kwenye
   vyombovya
   habari,hii
   leosiyo
   habari.” huyu kweli hakukosewa kuitwa Wassira.
   mizambwa and Kiduku like this.

  Page 1 of 7 123 ... LastLast

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...