Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

    Report Post
    Page 8 of 10 FirstFirst ... 678910 LastLast
    Results 141 to 160 of 183
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6154
      Likes Given
      22279

      Default Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Wanabodi,
      Baada ya kujadili mazuri na mafanikio ya rais wetu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kila kwenye mafanikio hapakosi matatizo, mapungufu au changamoto ambazo zikifanyiwa kazi zinabadilisha hali iliyopo sasa na kutupeleka hali bora zaidi.

      Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!.

      Katika kujadili mapungufu, madhaifu, matatizo na changamoto zinazomkabili rais Jakaya Kikwete, nawaombeni tujadili kwa spirit ya constructive criciticism kwa kueleza mapungufu hayo in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa.

      Watanzania tumekuwa ni watu wa kilalamika na kunung'unika wakati wote bila kuchukua hatua zozote positive za kurekebisha!. Naomba hii thread sio thread ya malalamiko au manunguniko dhidi ya JK bali thread ya kutoa ushauri nini cha kufanyika!.

      Kwa kuanzia moja ya mapungufu makubwa ya JK ni mtu wa huruma iliyopitiliza mipaka matokeo yake kutafsiriwa kama ni weakness, yaani "JK ni rais dhaifu", weak!, asiyeweza kufanya maamuzi magumu!.

      Mfano wa kwanza wa udhaifu huu wa huruma uliyopitiliza ni pale alipoyasamehe yale majizi ya EPA kwa kuyaruhusu yarudishe fedha yalizo kwiba kwa exchange ya kusemehewa na kutofikishwa mahakamani!. Hata Spika Sitta pia alimlaumu rais JK kwa upole huu!. Lingekuwa ni bunge makini, imperchment process ingeanzia pale pale right away kwa sababu rais hana mamlaka ya kuizuia sheria kuchukua mkondo wake!, huu ni uvunjaji wa katiba ya JMT!.

      Ni upole huo huo ndio unaopelekea hajamwajibisha Waziri wa Afya na naibu wake kwa sababu anawahurumia!.

      Ushauri ni kwa JK kuwa bold na kufanya maamuzi magumu!. Mfano kwenye huu mgomo wa sasa, siungi mkono JK kuitikia shinikizo la madaktari na wanaharakati kumwajibisha Mponda na naibu wake, hiyo nayo ni weakness. Bold decision ni wahusika watakaosabisha kifo chochote, kupandishwa kizimbani kwa murder!.

      JK anatakiwa kupunguza huruma na upendo wa mshumaa kumulikia wenzake huku yeye kwake kunateketea!. Huruma na upendo alioisha uonyesha sasa unatosha!. JK anatakiwa awe mkali kama alivyokuwa Nyerere watu kujua wamefutwa kazi ni kupitia taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku ya RTD tena ikisomwa na David Wakati!.(RIP).

      Ni huruma na upendo huu uliopitiliza ndio unapelekea kuwahurumia baadhi ya mawaziri na wasaidizi wake ambao hawamsaidii hivyo kuendelea kuwabeba!.

      Kwa vile JK hawezi kufanya kila kitu, piga chini wale wote ambao hawakusaidii hata ikibidi kumpiga chini Pinda, piga chini ili uliokoe taifa katika kipindi hiki chako cha miaka 3 kilichobakia!.

      Nawatakia majadiliano mema.

      Natanguliza shukrani kwa kuzingatia spirit ya constructive criticisim in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa!.

      Wasalaam

      Pasco wa jf.

      NB. Kama hauwezi constructive criticisim unaweza kujisomee tuu na kuishia zako bila kuchangia, kwani sio lazima uchangie kila thread!.
      Last edited by Pasco; 2nd February 2013 at 06:06.

    2. RukaaJuu Final

    3. #141
      Profesa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : Anywhere in Africa
      Posts : 511
      Rep Power : 751
      Likes Received
      219
      Likes Given
      322

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Pasco dah, umenigusa, ninauhakika anajuta kusikiliza uvumi badala ya kusubiri ishara ya ukweli wenyewe. Dah, na unajua principal ya uongozi kwa Tanzania mmoja wapo lazima awe vocal and hypactive ili kumatch mambo, kama Riasi ni mtu anaeendesha mambo kiupole, basi Waziri Mkuu anatakiwa awe hot and Vs Versa.

      Unadhani kwanini Sumaye alisurvive, kwakuwa Mkapa is something hot, na sumaye hakuwa ki hivyo, na ilikuwa rahisi kuendesha mambo. Dah hili ni bonge la kosa. Nahisi akiulizwa kitu atakachokikumbuka, bila shaka atataja kosa hili. Ila anachopaswa kutambua ni kuiwa kwa hali ilivyo, wananchi wanamtaka Lowasa arudi, ila wale walioko Bungeni waliomdhalilisha wanaomba usiku kucha asirudi maana itakuwa balaa.

    4. #142
      Bongolander's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Tandale
      Posts : 4,035
      Rep Power : 1418
      Likes Received
      610
      Likes Given
      44

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By Profesa
      Ila anachopaswa kutambua ni kuiwa kwa hali ilivyo, wananchi wanamtaka Lowasa arudi, ila wale walioko Bungeni waliomdhalilisha wanaomba usiku kucha asirudi maana itakuwa balaa.
      Mkuu wananchi gani wanaomtaka Lowassa arudi? Lowassa alidhalilishwa au alijidhalilishwa mwenyewe?

    5. #143
      Profesa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : Anywhere in Africa
      Posts : 511
      Rep Power : 751
      Likes Received
      219
      Likes Given
      322

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By Bongolander
      Mkuu wananchi gani wanaomtaka Lowassa arudi? Lowassa alidhalilishwa au alijidhalilishwa mwenyewe?
      Bongolander ukiwa mwanasiasa au kiongozi njia pekee ya kukuchafua ni kutumia chombo cha habari ambacho mimi na wewe wote tunatumia hivyo kama jicho la kuchungulia kinachoendelea ndani ya serikali na kwa wanasiasa. Vikikaa kimya hivyo kamwe hatutajua.

      Nataka mtu aniorodheshee tuhuma (kwakuwa hakuhukumiwa ila aliwajibika mwenyewe baada ya kuchukua dhamana kama kingozi) maovu ya Lowasa, halafu mafanikio yake akiwa Waziri Mkuu: Halafu anilinganishie na Mawaziri wakuu wengine kashfa/tuhuma zao na mafanikio yao please. Then Mtaelewa namaanisha nini. Hata wewe ukiwa Kiongozi wa siasa leo, ukigusa maslahi ya watu wenye nguvu, inabidi uwe mzuri wa hoja kupona fitina na majungu na hila za kukuchafua kama kisasi. Lowasa anaweza kuwa alifanya mabaya, ila hayawezi kuzidi maovu ya wengine wote, kwakuwa tunajua mabilioni ya pesa yanayopotea au kukutwa mahali na watuhumiwa tunawajua na tuhuma zao ni zaidi ya moja.

      Siupendi uovu, ila hali ilivyo kwa sasa ya kisiasa, nachelea kuamini kila kinachoonekana kwenye habari kama kina uhakika na ukweli asilimia mia moja.

    6. #144
      Bongolander's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th July 2007
      Location : Tandale
      Posts : 4,035
      Rep Power : 1418
      Likes Received
      610
      Likes Given
      44

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By Profesa
      Bongolander ukiwa mwanasiasa au kiongozi njia pekee ya kukuchafua ni kutumia chombo cha habari ambacho mimi na wewe wote tunatumia hivyo kama jicho la kuchungulia kinachoendelea ndani ya serikali na kwa wanasiasa. Vikikaa kimya hivyo kamwe hatutajua.

      Nataka mtu aniorodheshee tuhuma (kwakuwa hakuhukumiwa ila aliwajibika mwenyewe baada ya kuchukua dhamana kama kingozi) maovu ya Lowasa, halafu mafanikio yake akiwa Waziri Mkuu: Halafu anilinganishie na Mawaziri wakuu wengine kashfa/tuhuma zao na mafanikio yao please. Then Mtaelewa namaanisha nini. Hata wewe ukiwa Kiongozi wa siasa leo, ukigusa maslahi ya watu wenye nguvu, inabidi uwe mzuri wa hoja kupona fitina na majungu na hila za kukuchafua kama kisasi. Lowasa anaweza kuwa alifanya mabaya, ila hayawezi kuzidi maovu ya wengine wote, kwakuwa tunajua mabilioni ya pesa yanayopotea au kukutwa mahali na watuhumiwa tunawajua na tuhuma zao ni zaidi ya moja.

      Siupendi uovu, ila hali ilivyo kwa sasa ya kisiasa, nachelea kuamini kila kinachoonekana kwenye habari kama kina uhakika na ukweli asilimia mia moja.
      Mkuu ukitaka kujua Lowassa ni nani, nenda ukafukue kesi za ardhi utaona jina lake linatokeza mara ngapi, angalia mali zake ujue amezipata vipi, ndio utaona ni kwanini watu waliona toka mwanzo kuwa hafai. Kiutendaji Lowassa ni very effective, ingawa ana udikteta, lakini kwa ufisadi pia ni namba 1, wanaosema kuwa yeye ni kiongozi aliyechafuliwa, hawajui alikuwa mchafu gani alivyoingia kuwa PM, Mawaziri wakuu waliopita ni Nyerere, Kawawa, Sokoine, Msuya, Malecela, Warioba, SUmaye....hao wote kwa ufisadi ni cha mtoto ukilinganishwa na Lowassa, kama ni hatua lowassa yuko mbele hatua 100 wengine wako hatua tatu.

    7. #145
      Profesa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : Anywhere in Africa
      Posts : 511
      Rep Power : 751
      Likes Received
      219
      Likes Given
      322

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By Bongolander
      Mkuu ukitaka kujua Lowassa ni nani, nenda ukafukue kesi za ardhi utaona jina lake linatokeza mara ngapi, angalia mali zake ujue amezipata vipi, ndio utaona ni kwanini watu waliona toka mwanzo kuwa hafai. Kiutendaji Lowassa ni very effective, ingawa ana udikteta, lakini kwa ufisadi pia ni namba 1, wanaosema kuwa yeye ni kiongozi aliyechafuliwa, hawajui alikuwa mchafu gani alivyoingia kuwa PM, Mawaziri wakuu waliopita ni Nyerere, Kawawa, Sokoine, Msuya, Malecela, Warioba, SUmaye....hao wote kwa ufisadi ni cha mtoto ukilinganishwa na Lowassa, kama ni hatua lowassa yuko mbele hatua 100 wengine wako hatua tatu.
      OK nimekuelewa, una hoja, basi tuombe Mungu na tutumie kura zetu vema kupata kiongozi tunaekusudia. Ila natumaini Katiba itatupa uwezo wa kumbadilisha kiongozi pale tunapoona tulikosea, isitugharimu na isitupotezee muda na ukiritimba hasa hii tabia ya sasa viongozi kutokutaka kuwajibika.

    8. Miaka 50

    9. #146
      luvara's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th April 2011
      Posts : 58
      Rep Power : 422
      Likes Received
      10
      Likes Given
      10

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!.

      Quote By Kongosho
      Hivi kushindwa kuwawajibisha wasaidizi wake ni huruma na upendo??

      Huruma na upendo kwa nani?
      Kwa maslah ya nani?

      Mimi naona kama kutojiamini katika maanuzi na kujaribu kuficha uozo wa uteuzi wake wa wasaidizi wake ambao wengi ni washkaji, wengine vilaza ili wasiweze kumchaleni sana.

      Baadhi ya mabosi hasa kama hajiamini hata maofisi anayependa surbodinates waliosmart kuliko yeye.
      Ni vyema tukajitahidi kuelewa baadhi ya mambo kwa makini. Jambo hili la wizi wa EPA lilikuwa ni jambo kubwa sana na lilihusisha wakubwa wengi na hata namna ya kulishughulikiwa haikuwa rahisi kwa hiyo JK alifanya lile ambalo aliona linaweza kufanyika na nchi ikabakia salama. Hata hivyo wezi waliojitokeza baada ya pale wanaendelea kuumbuliwa siku hadi siku. Mimi binafsi napenda sana Rais wetu awe mkali kwa mafisadi, wagomaji na wahujumu wa aina yoyote ile. Ili maendeleo yapatikane na nidhamu iwepo KISASI kina umuhimu wake.

    10. #147
      MNYISANZU's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 6,311
      Rep Power : 0
      Likes Received
      593
      Likes Given
      76

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      JKilaza ana damu chafu/dhaifu ambayo hata nguruwe hainywi.

    11. #148
      MNYISANZU's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 6,311
      Rep Power : 0
      Likes Received
      593
      Likes Given
      76

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      Hivi hili dubwana mlilitoa wapi watanzania jamani?!!

    12. #149
      Shekispia's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th February 2012
      Location : Dar es salaam
      Posts : 201
      Rep Power : 405
      Likes Received
      23
      Likes Given
      0

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      Mbona mnatokwa mapovu mengi,hoja ni nini hasa hapo au mipasho?peleka jukwaa husika hyo mipasho..

    13. #150
      damper's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th February 2011
      Posts : 141
      Rep Power : 445
      Likes Received
      18
      Likes Given
      33

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      Duh! Unaonekana una hasira weye! Sijui ukikutana nae ana kwa ana halafu wawili tu, sijui itakuwaje!
      Utakuwa umekumbwa na jambia kama sio kwenye uwaziri/u dc au jamaa ya karibu wa hao.

    14. #151
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      Mkikosa hoja mnaanza viroja.
      Na ikifika Jumamosi na Jumapili ndio vinazidi.
      Kwi kwi kwi teh teh teh!
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    15. #152
      Mzee wa Rula's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th October 2010
      Posts : 6,383
      Rep Power : 12713
      Likes Received
      2195
      Likes Given
      1820

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      Uzi huu hauna maisha marefu sana!!!
      Pasco likes this.

    16. #153
      Kagalala's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2010
      Posts : 1,237
      Rep Power : 681
      Likes Received
      366
      Likes Given
      147

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      Nina Amani Rohoni kwangu kwani sijawahi kumpenda na kumpigia kura. Dhamira yangu nyeupe. Sorry Kikwete Sijawi kukupenda na sikupendi.
      Our biggest Enemy is not to try what others have done.

    17. #154
      Mwanaharakatihuru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2012
      Posts : 474
      Rep Power : 0
      Likes Received
      114
      Likes Given
      14

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      Kikwete ni chagua la Mungu. Mungu anataka awafundishe somo wa Tanzania.

    18. #155
      afwe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th October 2010
      Posts : 702
      Rep Power : 575
      Likes Received
      81
      Likes Given
      116

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      Ni expression ya kukataa tamaa. Tumekuwa tukisema wakati wote kuwa nchi imepoteza miaka kumi bila kufanya maendeleo hamkuamini.
      Pasco likes this.

    19. #156
      niibada's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 26
      Rep Power : 352
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      Ni sawa lakini wnanchi ndo wanaongoza kwa unafiki wakifuatiwa na wanasiasa kisha wasomi
      Kama si wote wanafiki leo hii tungekuwa mbali
      Unayelalamika mwaka 2015 unaweza ukakuta wewe mwandishi unashabikia upande atakaokuwa Kikwete
      Acha hasira waelimishe wananchi wajue haki zao na waache unafiki ndo wanasiasa nao wataacha unafiki wao
      Pasco likes this.

    20. #157
      Excellent's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th December 2009
      Posts : 5,567
      Rep Power : 2286
      Likes Received
      2356
      Likes Given
      4086

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      Quote By Mzee wa Rula
      Uzi huu hauna maisha marefu sana!!!
      mi natamani ungeachwa tu
      Pasco likes this.
      Mbuzi kafia kwa mwuza supu.

    21. #158
      andrews's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th March 2012
      Posts : 1,683
      Rep Power : 0
      Likes Received
      142
      Likes Given
      76

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      unalia nini mbona ndivyo alivyo
      Pasco likes this.

    22. #159
      Mkereketwa_Huyu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2011
      Location : London | Dar Es Salaam
      Posts : 1,829
      Rep Power : 4590
      Likes Received
      580
      Likes Given
      426

      Default

      Point well taken. For a new Tanzania, we need rais kama Kagame. Hii nchi inabidi itawaliwe kimabavu na Kikwete si mtu anayefaa kuendesha nchi kama yetu maana hana mtazamo zaidi ya kuuza sura.
      Pasco likes this.

    23. #160
      Gwangambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th June 2012
      Location : Mabwepande
      Posts : 1,113
      Rep Power : 570
      Likes Received
      264
      Likes Given
      86

      Default Re: kikwete ni mnafiki no 1

      Nampenda JKilaza wangu, kwanza kwa kukiua CCM, pili kuipa cdm umaarufu, tatu kuhakikisha CCM inatoka 2015. Aaaaaah Mkwereeeeeeh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
      Pasco likes this.

    Page 8 of 10 FirstFirst ... 678910 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...