Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

    Report Post
    Page 5 of 10 FirstFirst ... 34567 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 183
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7367
      Likes Received
      6151
      Likes Given
      22265

      Default Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Wanabodi,
      Baada ya kujadili mazuri na mafanikio ya rais wetu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kila kwenye mafanikio hapakosi matatizo, mapungufu au changamoto ambazo zikifanyiwa kazi zinabadilisha hali iliyopo sasa na kutupeleka hali bora zaidi.

      Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!.

      Katika kujadili mapungufu, madhaifu, matatizo na changamoto zinazomkabili rais Jakaya Kikwete, nawaombeni tujadili kwa spirit ya constructive criciticism kwa kueleza mapungufu hayo in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa.

      Watanzania tumekuwa ni watu wa kilalamika na kunung'unika wakati wote bila kuchukua hatua zozote positive za kurekebisha!. Naomba hii thread sio thread ya malalamiko au manunguniko dhidi ya JK bali thread ya kutoa ushauri nini cha kufanyika!.

      Kwa kuanzia moja ya mapungufu makubwa ya JK ni mtu wa huruma iliyopitiliza mipaka matokeo yake kutafsiriwa kama ni weakness, yaani "JK ni rais dhaifu", weak!, asiyeweza kufanya maamuzi magumu!.

      Mfano wa kwanza wa udhaifu huu wa huruma uliyopitiliza ni pale alipoyasamehe yale majizi ya EPA kwa kuyaruhusu yarudishe fedha yalizo kwiba kwa exchange ya kusemehewa na kutofikishwa mahakamani!. Hata Spika Sitta pia alimlaumu rais JK kwa upole huu!. Lingekuwa ni bunge makini, imperchment process ingeanzia pale pale right away kwa sababu rais hana mamlaka ya kuizuia sheria kuchukua mkondo wake!, huu ni uvunjaji wa katiba ya JMT!.

      Ni upole huo huo ndio unaopelekea hajamwajibisha Waziri wa Afya na naibu wake kwa sababu anawahurumia!.

      Ushauri ni kwa JK kuwa bold na kufanya maamuzi magumu!. Mfano kwenye huu mgomo wa sasa, siungi mkono JK kuitikia shinikizo la madaktari na wanaharakati kumwajibisha Mponda na naibu wake, hiyo nayo ni weakness. Bold decision ni wahusika watakaosabisha kifo chochote, kupandishwa kizimbani kwa murder!.

      JK anatakiwa kupunguza huruma na upendo wa mshumaa kumulikia wenzake huku yeye kwake kunateketea!. Huruma na upendo alioisha uonyesha sasa unatosha!. JK anatakiwa awe mkali kama alivyokuwa Nyerere watu kujua wamefutwa kazi ni kupitia taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku ya RTD tena ikisomwa na David Wakati!.(RIP).

      Ni huruma na upendo huu uliopitiliza ndio unapelekea kuwahurumia baadhi ya mawaziri na wasaidizi wake ambao hawamsaidii hivyo kuendelea kuwabeba!.

      Kwa vile JK hawezi kufanya kila kitu, piga chini wale wote ambao hawakusaidii hata ikibidi kumpiga chini Pinda, piga chini ili uliokoe taifa katika kipindi hiki chako cha miaka 3 kilichobakia!.

      Nawatakia majadiliano mema.

      Natanguliza shukrani kwa kuzingatia spirit ya constructive criticisim in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa!.

      Wasalaam

      Pasco wa jf.

      NB. Kama hauwezi constructive criticisim unaweza kujisomee tuu na kuishia zako bila kuchangia, kwani sio lazima uchangie kila thread!.
      Last edited by Pasco; 2nd February 2013 at 06:06.

    2. FemaTV & Radio

    3. #81
      Joss's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th May 2009
      Posts : 715
      Rep Power : 651
      Likes Received
      126
      Likes Given
      121

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Yaani kutowawajibisha wezi wa EPA ni huruma? kama anahuruma kwanini asiwasamehe na wengine pia kama akina babu seya? JK ni msanii, ndani ya usanii huo kuna ufisadi, ushikaji, kutaka kupendwa na kila mtu, kuchukulia kila jambo ni kama mzaha, vyote hivyo naviweka ndani ya usanii.

      Hakuna upole wala huruma hapo. Sheria ni sheria haina cha mkubwa wala mdogo, tusijifanye hatujui kwanini aliwasamehe wezi wa EPA, au hakuchukua hatua dhidi ya Ufisadi wa rada, Richmond n.k maana huwezi kumuepusha JK na kashifa hizi.

      Labda niseme hayo yote yanasababishwa na udhaifu mmoja mkubwa sana, JK ni mtu wa hila, hulka yake ni kupata jambo fulani kwa njia yeyote hata kama ni kwa hila. sasa watu kama akina RA ambao ni ma king maker huwa wanatumia nafasi hiyo kuifanikisha hiyo hila, ili baadaye waje kuwa na nguvu katika maamuzi, ambapo matokeo yake ndo kiongozi kama JK anakuwa hawezi kufanya maamuzi yake mwenyewe.

    4. #82
      KAPONGO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th May 2009
      Location : Madongo kuinama
      Posts : 598
      Rep Power : 627
      Likes Received
      69
      Likes Given
      216

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!.

      Baniani mbaya, kiatu chake ni dawa!

      JK atakumbukwa kwa hulka yake ya kutoa uhuru wa kila mtu kusema ama kubwabwaja atakavyo kwa kupitia kinywa chake ama vyombo vya habari ilimradi azingatie kuwa 'unapoishia uhuru wake ndio unapoanzia uhuru wa mwingine'. Na kwa sababu hiyo jamii imenufaika kwa kupata mawazo na fikra mbadala, hata km ni mwiba kwa serikali na chama tawala.

      Kubuni mradi wa ujenzi wa UDOM ni credit nyingine kwake...na kuruhusu ufisadi uliotendeka wakati wa awamu ya tatu kuwekwa hadhani ni ujasiri mwingine...

    5. #83
      kilolambwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd December 2010
      Posts : 370
      Rep Power : 570
      Likes Received
      65
      Likes Given
      65

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By JeanPrierre
      Jamani msitafute mchawi, mkulu ndo tatizo. haiwezekani umepangwa kupiga penati halafu na ww unatoa pasi!!!. Sina haja ya kutaja mambo ambayo yy kama yy alikuwa anatakiwa kutoa kauli ya mwisho, anamwachia Pinda.
      Mbaya zaidi huyo pinda akifanya maamuzi anamshushua.

    6. #84
      WildCard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2008
      Posts : 6,453
      Rep Power : 1978
      Likes Received
      1797
      Likes Given
      59

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Nchi inasonga mbele.

      Watu tunatoka Dar kwa Bajaj hadi Mwanza. Tuna mabenki zaidi ya 50 sasa nchi hii. Tuna mashule mengi tu. Tuna vyuo na vyuo vikuu vingi tu. Tunafufua reli iliyofia mikononi mwa Mkapa. Watanzania wanamiliki majumba, magari ya kisasa kwelikweli. Chaguzi zinazidi kuwa huru zaidi. JMK ataacha KATIBA MPYA kabisa. Tuna vyombo vingi vya habari kuliko wakati mwingine wowote tangu uhuru. Tunaandika na kusema mengi juu ya JMK na wengine wote. Harusi na misiba sasa ni ya mamilioni.

      Baadhi ya mapungufu yake ni kujenga watu wenye nguvu ndani ya chama chake kuliko chama chenyewe. Hili kwa sehemu kubwa limechangiwa na namna alivyoupata URAIS. Pungufu jingine ni kuteua watu wa kumsaidia kwa USWAHIBA, UDINI.

      Jingine ni usimamizi hafifu wa KATIBA ya JMT. Zanzibar ni NCHI sasa. Pungufu jingine ni kutotumia kikamilifu na kisheria vyombo vya DOLA hasa UwT, PCCB, POLICE,..

      Jingine kutoipa umuhimu MAHAKAMA kama afanyavyo kwa BUNGE. Pungufu jingine ni kuigawa mno CCM. Ndani ya CCM watu wanachukiana kwa viwango vya kutisha. Hili nalo lina mizizi yake tangu alipoanza kuusaka URAIS.

      Pungufu jingine ni ile nguvu ya URAIS inapotakiwa kutumika, kuonekana, kuhitajika, kusimama kama TAASISI inakuwa tatizo.

      Rais wetu pia ameelemewa mno na familia na marafiki zake. Wamekuwa WABIA wake kwenye URAIS.

    7. #85
      kanyanga's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th July 2011
      Posts : 45
      Rep Power : 406
      Likes Received
      15
      Likes Given
      1

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By Pasco
      Wanabodi,
      Baada ya kujadili mazuri na mafanikio ya rais wetu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kila kwenye mafanikio hapa kosi mapungufu, matatizo au changamoto ambazo zikifanyiwa kazi zinabadilisha hali iliyopo na kutupeleka mahali bora zaidi.

      Nawaombeni sana katika kujadili mapungufu, nawaombeni tujadili kwa nidhamu na staha ya hali ya juu haswa kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukana ua lugha zozote ambazo hazina staha!.

      Katika kujadili mapungufu, madhaifu, matatizo na changamoto zinazomkabili rais Jakaya Kikwete, nawaombeni tujadili kwa spirit ya constructive criciticism kwa kueleza mapungufu hayo in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa.

      Watanzania tumekuwa ni watu wa kilalamika na kunungunika wakati wote bila kuchukua hatua zozote positive. Naomba hii thread sio thread ya malalamiko au manunguniko dhidi ya JK bali shaurini nini cha kufanyika!.

      Naomba ukosoaji ufanyike kwa nia njema ukiambatana na ushauri wa nini cha kufanyika kurekebisha mapungufu hayo!.

      Kwa kuanzia moja ya mapungufu makubwa ya JK ni mtu wa huruma iliyopitiliza mipaka matokeo yake kutafsiriwa kama ni weakness, yaani JK ni rais weak asiyeweza kuchukua maamuzi magumu!.

      Mfano wa kwanza wa udhaifu huu wa huruma uliyopitiliza ni pale alipowasamehe majizi ya EPA na kutaruhusu yarudishe fedha yalizo kwiba na kusemehewa kutofikishwa mahakamani!. Spika Sitta pia alimlaumu rais JK kwa upole huu!. Lingekuwa ni bunge makini, imperchment process ingeanza right away!.

      Ni upole huo huo ndio unaopelekea hajamwajibisha Waziri wa Afya na naibu wake kwa sababu anawahurumia!.

      Ushauri ni kwa JK kuwa bold na kufanya maamuzi magumu!. Mfano kwenye huu mgomo wa sasa, siungi mkono JK kuitikia shinikizo la madaktari na wanaharakati kumwajibisha Mponda na naibu wake, hiyo nayo ni weakness. Bold decision ni wahusika watakaosabisha kifo chochote, kupandishwa kizimbani kwa murder!.

      JK anatakiwa kupunguza huruma na upendo wa mshumaa kumulikia wenzake huku yeye anateketea!. Huruma na upendo aliountesha sasa unatosha!. Awe mkali kama alivyokuwa Nyerere watu kujua wamefutwa kazi ni kupitia taarifa ya habari ya RTD tena ikizimwa na David Wakati!.(RIP).

      Ni huruma na upendo huu uliopitiliza ndio unapelekea kuwahurumia baadhi ya mawaziri na wasaidizi wake ambao hawamsaidii hivyo kuendelea kuwabeba!. Kwa vile JK hawezi kufanya kila kitu, piga chini wale wote ambao hawakusaidii hata ikibidi kumpiga chini Pinda, piga chini uliokoe taifa hiki kipindi chako cha miaka 3 kilichobakia!.

      Nawatakia majadiliano mema.

      Natanguliza shukrani kwa kuzingatia spirit ya constructive criticisim in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa!.

      Wasalaam

      Pasco wa jf.

      NB. Kama hauwezi constructive criticisim naomba usichangie, jisomee tuu na kuishia zako, sio lazima uchangie kila thread!.
      Mkuu Pasco, hapo kwenye nyekundu ndo balaa na usitake kupata uhakika kwa kutumia njia hiyo.Nina hakika utakuwa na tetesi fulanifulani sasa u just want to prove beyond any reasonable doubt.Kwa taarifa yako (isiyokuwa na chembe ya uongo) JK aliingia madarakani kwa pesa za EPA na usijaribu kupata wazo kwamba kuna siku atakuja kuwafunga hao MAJIZI.

      Picha yenyewe ilikuwa hivi, baada ya jina la JK kupitishwa kuwa mgombea wa CCM 2005 Mh.B.W.Mkapa alifuatwa na wanamtandao wakiongozwa na Rostam Aziz ili kupanga mkakati wa kupata pesa kwa ajili ya Kampeni.Mkapa akamwita Mzee Apson Mwang'onda na kumweleza afanye anavyojua ili pesa ya Kampeni ipatikane.Sababu kubwa ya kumtumia Apson aliyekuwa DG wa TISS ni kutokana na ukweli kwamba TISS wanakula pesa sana na hakuna maelezo zaidi ya kutoa taarifa tu kwamba ni kwa shughuli za Usalama na Ulinzi wa nchi. Mzee Apson akamvaa Daudi Balali aliyekuwa Governor wa BOT.

      Huyo ndiye aliyewashtua kwamba kuna michuzi ya EPA, katika hatua kama hiyo Rostam hafanyi kosa hata siku moja.Hadi kufikia hatua hiyo nataka kukuhakikishia kwamba JK alikuwa anafuatilia sana suala la pesa za Kampeni kwa kuwa jamaa alikuwa na usongo na U-Presidaa kuliko tamaa ya fisi kwenye mkono wa binadamu unaoning'inia.Baada ya wizi huo na JK kuukwaa u-presidaa, Kumbuka kuwa Auditors waliokuwa BOT wakagundua mchezo, Balali akaona ishakuwa noma akawawakia kwamba hiyo haikuwa sehemu ya kazi waliyotakiwa kuifanya.

      Balali akawatoa nduki, lakini tayari watu wa World Bank walishapata habari na walishajua Account zote zilizojazwa pesa chafu za EPA wakatuma taarifa ya kumtaka Presidaa apitishe haraka sheria ya biashara chafu ya pesa MONEY LAUNDERING,Presidaa alipotaka ushauri kwa Apson akaambiwa hiyo inaweza kuwa hatari kwa kuwa Presidaa hajui inaweza kuja kumgusa nani, so yawezekana ikajamgusa hata mtoto wake, kwa hiyo jamaa akaitolea nje na World Bank wakajulishwa kwamba transactions walizoona wale Auditors zinahusu masuala ya Usalama.

      Rejea Statement ya Zakia Meghji akiwa Finance Minister.Wabia/Washirika wa maendeleo walipokuja juu na Serikali ikaona itapigwa chini kuhusu misaada ndo bomu likaiva.Pasco hadi kufikia hapo hiyo huruma kupita kiasi ya JK iko wapi ? Huyo ni mwizi kama wezi wengine tu Rostam, Lowasa na wengineo wengi.Hawezi kuthubutu kumtupa mwizi yeyote Selo kwa kuwa naye ni sehemu ya wizi huo na ndio wizi uliotumika kumfikisha hapo alipo.

      JK alipokuwa akiwania kuteuliwa aliwatumia watu wengi sana kuwapanda migongoni mwao, leo amewapa asante ya kumwezesha kuwa hapo.Nakuhakikishia JK mwenyewe kwa upeo mdogo wa kuchambua mambo alionao hajui kama jamaa hawamsaidii, achilia mbali hao mawaziri wenyewe kutojijua kwamba si msaada wowote kwenye serikali.Hii si huruma ni Serikali ya Ki-ushikaji tu na kisanii.Pendekezo langu nadhani ingefaa kuitwa KAOLE GOVERNMENT na si THE GOVERNMENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA,kwani tangu 2005 hiyo serikali haipo.
      John Kangethe and Henge like this.

    8. Miaka 50

    9. #86
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Jamani jamani, Ikiwa JK aliiingia Ikulu kwa pesa za EPA (ufisadi), itakuwaje awe na mapungufu anapofanya Ufisadi.. mapungufu yake yangekuwa kama angefanya kinyume cha Ufisadi..JK anawalinda mafisadi inavyopaswa kulindwa, anawaweka watu wake wanaoweza kumlinda yeye na utawala huu iweje yawe mapungufu ili hali nyie wenyewe mlimchagua kwa sifa za kulinda Ufisadi?..Mapungufu mnayo nyie wenyewe wananchi na ndio maana mlimchagua YEYE..na he is doing what you deserve ikiwa leo hii mfano mbora kwenu kwa kiongozi ni Mkapa na Lowassa...Na ndio maana nasema mapungufu hupimwa kutokana na ujazo mnaoutaka na sifa zake. Kama JK ni robo chupa, Mkapa kafika nusu halafu Lowassa robo tatu ya Ufisadi itakuwaje mseme JK ana mapungufu kwa kutumia kipimo tofauti kabisa wakati sifa zinakwenda kwa kina Mkapa?

      Sasa ikiwa yeye ana mapungufu hivi kweli hamkuona mapungufu wakati wa Mwinyi na Mkapa ambao wote wameyafanya sawa au zaidi ya JK ila kwa nyakati tofauti?. IPTL, Loliondo, Rada, City water, Meremeta, Green bank yaani kashifa juu ya kashifa toka enzi za kina Ami mpungwe na Idd Simba.. Ilikuwaje Elimu nchini imepiga mbizi baada ya Mwinyi kuingia madarakani, Mahospital yetu pamoja na kuwa mengi (quantity) lakini quality ya huduma zake zilipungua toka wakati wa Mwinyi tukavaa mitumba na ikawa sifa kubwa za Mh. Mwinyi na Ruksa - kipindupindu, Ukoma na maradhi ambayo yaliisha wekwa ktk koba la karantini yakarudi kwa kasi kubwa. Hamtaki kuzungumzia maswala ya Elimu na Afya, viwanda na miundombinu ilivyokufa kwa sababu mnazo interest zenu japokuwa kuna vitu wazi kabisa.

      Makanisa wamerudishiwa mashule na Hospital mbona Aghakhan yule mdosi hakurudishiwa shule zake kama vile Mwanza sekondary, Tambaza na kadhalika. halafu tujiulize hivi kweli kurudisha zile shule ilikuwa maamuzi ya busara. Mtasema NDIO japokuwa ni ktk maamuzi kama hayo JK hana uwezo wa kuwaambia chochote akihofia kiti chake, leo taasisi za dini wanaepa kodi, tax exemption zimetupotezea mabillioni ya fedha na tuna NGOs mia kidogo zote hizi zikiepa kodi. JK aseme jamanin haifai tayari anaitwa mdini..Machinga, Chokoraa, MaChangudoa wamejaa mabarabarani kila kona ya miji yetu wakizuiwa kidogo, Vurugu nchi nzima na wanaungwa mkono na wanasiasa wetu wenyewe.

      Magufuli na Mama Tibaijuka wakajaribu mangapi, na mwisho wa siku huonekana wao ndio watu wabaya sana wenye wivu na mtajaribu kila njia kuonyesha wao sii saints. Heee jamani tazameni reli ya kati, bandari, tumeua viwanda na hata kilimo na mazao yote ya biashara tukitegemea kuuza nyumba na viwanja kwa mafisadi ndio ajira kubwa leo ya Mtanzania, bado tu hamuoni tunakoelekea!.Jk anafanya exactly what he is supposed to do! kwa sababu akifanya inavyotakiwa haswa kupambana na ufisadi nchini na katika mazingira ambayo almost 50% ya wananchi wake ni unemployed, hatuzalishi kitu ila kuiba fedha za WB na Bank ya Afrika mtamchukia vibaya na pengine hataweza kumaliza miaka yake ya utawala.

      Hee! wameondoka wangapi walijaribu kutetea maslahi ya wananchi na hakuna Mtanzania hata mmoja anayewakumbuka kwa mazuri. Toka Kolimba hadi huyu Mwakyembe mguu nje ndani hawapewi msaada wowote zaidi ya watu kudai atoe ushahidi laa sivyo afe huko huko India. Kuna mpiganaji gani alosifika kwa kupambana na ufisadi zaidi ya Dr.Slaa na vijana kama Zitto ambao leo hawapendwi na wameundiwa chuki kubwa. Wao sii wajinga hata kidogo wanapenda kuishi, maisha matamu jamani watafika mahala watachoka vile vile.

      Madaktari wamegoma lakini hamtaki kuzungumzia fedha wanazopewa asasi zinazohusika na huduma za Afya wao wanazitumia vipi, JK anaogopa kugusia swala la CSSC na hatkuna kiongozi hata mmoja wa Upinzani anayethubutu kuzungumzia hili - Hakuna na kama yupo asimame hata mmoja kukemea mfumo wa misamaha ya Tax, Elimu na Afya nchini!.. wote hawa wana waogopa nyie wananchi kutokana na nguvu ya Udini iliyopo nchini, kinyume watapoteza unga wao. Leo mnamtuaka Mponda na Nkya wajiuzuru bila kujua wamekosa nini hasa kupitia sheria..Mapungufu tunayo sisi wananchi na kibaya zaidi sisi ni wanafiki hakuna mfano!
      Last edited by Mkandara; 8th March 2012 at 17:38.
      John Kangethe and Mike McKee like this.
      Exploration of reality

    10. #87
      OLESAIDIMU's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd December 2011
      Posts : 1,241
      Rep Power : 732
      Likes Received
      494
      Likes Given
      468

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By Mkandara

      Appreciated mkuu....deep insights and thoughts

      Say now you are in the committee to advice on how to get out of this mess. It is like we are in the enmeshed pile of contradictions. What are we supposed to do on our way forward stepwise???
      Hegemony is unlikely ever to be complete (A. Gramsci)

    11. #88
      BUBE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2010
      Location : KIMANZICHANA
      Posts : 629
      Rep Power : 557
      Likes Received
      170
      Likes Given
      174

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Pasco hujafahamu kuwa dunia imebadilika sana! Enzi za mwalimu kutoa amri ilikuwa kawaida na raisi akisema haulizwi swali....pengine hivyo silka/hulka ndiyo imetufikisha hapa, ila napenda kusema enzi za kutoa amri katika maslahi na haki za binadamu hazina nafasi tena. Serikali za siku hizi zinaendeshwa kwa hoja, majadiliano na maridhiano. Japokuwa siungi mkono mgomo wa madaktari, sioni wapi raisi anaweza kuwalazimisha hao kuingia kazini. Maana linalohitajika hapa sio presence but ufanyaji kazi. Watu wamesema waweza kumlazimisha ng'ombe kwenda mtoni....lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji. Bahati mbaya wenye kuumia ni sisi ambao hosptali za umma ndo kimbilio. Kama huo ndo ushauri wako kwa mh raisi wa kuwafungulia mashtaka madaktari nadhani wewe hapo sio mshauri mzuri hata kidogo....that proposal will never work
      Quote By pasco
      wanabodi,
      baada ya kujadili mazuri na mafanikio ya rais wetu, mhe. Jakaya mrisho kikwete, kila kwenye mafanikio hapa kosi mapungufu, matatizo au changamoto ambazo zikifanyiwa kazi zinabadilisha hali iliyopo na kutupeleka mahali bora zaidi.

      Nawaombeni sana katika kujadili mapungufu, nawaombeni tujadili kwa nidhamu na staha ya hali ya juu haswa kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukana ua lugha zozote ambazo hazina staha!.

      Katika kujadili mapungufu, madhaifu, matatizo na changamoto zinazomkabili rais jakaya kikwete, nawaombeni tujadili kwa spirit ya constructive criciticism kwa kueleza mapungufu hayo in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa.

      Watanzania tumekuwa ni watu wa kilalamika na kunungunika wakati wote bila kuchukua hatua zozote positive. Naomba hii thread sio thread ya malalamiko au manunguniko dhidi ya jk bali shaurini nini cha kufanyika!.

      Naomba ukosoaji ufanyike kwa nia njema ukiambatana na ushauri wa nini cha kufanyika kurekebisha mapungufu hayo!.

      Kwa kuanzia moja ya mapungufu makubwa ya jk ni mtu wa huruma iliyopitiliza mipaka matokeo yake kutafsiriwa kama ni weakness, yaani jk ni rais weak asiyeweza kuchukua maamuzi magumu!.

      Mfano wa kwanza wa udhaifu huu wa huruma uliyopitiliza ni pale alipowasamehe majizi ya epa na kutaruhusu yarudishe fedha yalizo kwiba na kusemehewa kutofikishwa mahakamani!. Spika sitta pia alimlaumu rais jk kwa upole huu!. Lingekuwa ni bunge makini, imperchment process ingeanza right away!.

      Ni upole huo huo ndio unaopelekea hajamwajibisha waziri wa afya na naibu wake kwa sababu anawahurumia!.

      Ushauri ni kwa jk kuwa bold na kufanya maamuzi magumu!. Mfano kwenye huu mgomo wa sasa, siungi mkono jk kuitikia shinikizo la madaktari na wanaharakati kumwajibisha mponda na naibu wake, hiyo nayo ni weakness. Bold decision ni wahusika watakaosabisha kifo chochote, kupandishwa kizimbani kwa murder!.

      Jk anatakiwa kupunguza huruma na upendo wa mshumaa kumulikia wenzake huku yeye anateketea!. Huruma na upendo aliountesha sasa unatosha!. Awe mkali kama alivyokuwa nyerere watu kujua wamefutwa kazi ni kupitia taarifa ya habari ya rtd tena ikizimwa na david wakati!.(rip).

      Ni huruma na upendo huu uliopitiliza ndio unapelekea kuwahurumia baadhi ya mawaziri na wasaidizi wake ambao hawamsaidii hivyo kuendelea kuwabeba!. Kwa vile jk hawezi kufanya kila kitu, piga chini wale wote ambao hawakusaidii hata ikibidi kumpiga chini pinda, piga chini uliokoe taifa hiki kipindi chako cha miaka 3 kilichobakia!.

      Nawatakia majadiliano mema.

      Natanguliza shukrani kwa kuzingatia spirit ya constructive criticisim in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa!.

      Wasalaam

      pasco wa jf.

      Nb. Kama hauwezi constructive criticisim naomba usichangie, jisomee tuu na kuishia zako, sio lazima uchangie kila thread!.

    12. #89
      Mabwepande's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th February 2012
      Posts : 230
      Rep Power : 412
      Likes Received
      34
      Likes Given
      0

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Mapungufu ya Jk ni mengi mno! Kwanza ni mtu wa Visasi.
      John Kangethe likes this.

    13. #90
      Mindi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th April 2008
      Posts : 254
      Rep Power : 618
      Likes Received
      48
      Likes Given
      108

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By WildCard
      Nchi inasonga mbele.

      Watu tunatoka Dar kwa Bajaj hadi Mwanza. Tuna mabenki zaidi ya 50 sasa nchi hii.
      Idadi ya mabenki kuwa kubwa haina maana kwamba nchi inasonga mbele. cha msingi ni kwamba mabenki hayo yanamsaidia mtanzania? ama ni mirija tu ya ku-siphon mali za mtanzania? kuna uwekezaji wa akili na wa faida na kuna ule wa hasara. wetu ni wa hasara zaidi.

      Quote By WildCard
      Tuna mashule mengi tu. Tuna vyuo na vyuo vikuu vingi tu.
      Mashule mengi? sema tuna "vituo" vingi wanapokusanyika wanafunzi. kama wamekaa chini, kama wana maabara au hawana, kama hawana waalimu au hawana, hiyo ni ishu nyingine. "shule" ni ukamilifu wa mahitaji ya shule, kitu ambacho kitaifa hakipo. tunatengeneza taifa lenye matabaka kielimu. na hata huko mashuleni na vyuoni, kuna quality education? kutoka wapi? ni usanii juu ya usanii.

      Quote By WildCard
      Watanzania wanamiliki majumba, magari ya kisasa kwelikweli.
      Hii ni maendeleo kwa wale wanaotengeneza magari hayo na kutuuzia, siyo sisi tunaoyanunua kama mazuzu, magari ya gharama kubwa ambayo hayatumiki kuinua uchumi, bali kutambiana kwa ufahari wa kijinga. yanaongeza foleni na kuchelewesha hata wale ambao wako serious na nchi hii, washindwe kutoa mchango wao vizuri. wenye akili wala hawahangaiki nayo, ila sisi tu hapa. nenda Rwanda ukaone.

      Hayo uliyoita maendeleo na kupiga hatua, kwa kweli yanaingia kwenye matatizo tu ya nchi hii

    14. #91
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7367
      Likes Received
      6151
      Likes Given
      22265

      Default

      Quote By Pasco
      Wanabodi,
      Baada ya kujadili mazuri na mafanikio ya rais wetu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kila kwenye mafanikio hapakosi matatizo, mapungufu au changamoto ambazo zikifanyiwa kazi zinabadilisha hali iliyopo sasa na kutupeleka hali bora zaidi.

      Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!.

      Katika kujadili mapungufu, madhaifu, matatizo na changamoto zinazomkabili rais Jakaya Kikwete, nawaombeni tujadili kwa spirit ya constructive criciticism kwa kueleza mapungufu hayo in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa.

      Watanzania tumekuwa ni watu wa kilalamika na kunung'unika wakati wote bila kuchukua hatua zozote positive za kurekebisha!. Naomba hii thread sio thread ya malalamiko au manunguniko dhidi ya JK bali thread ya kutoa ushauri nini cha kufanyika!.

      Kwa kuanzia moja ya mapungufu makubwa ya JK ni mtu wa huruma iliyopitiliza mipaka matokeo yake kutafsiriwa kama ni weakness, yaani "JK ni rais weak"!,: asiyeweza kuchukua maamuzi magumu!.

      Mfano wa kwanza wa udhaifu huu wa huruma uliyopitiliza ni pale alipoyasamehe yale majizi ya EPA kwa kuyaruhusu yarudishe fedha yalizo kwiba kwa exchange ya kusemehewa na kutofikishwa mahakamani!. Hata Spika Sitta pia alimlaumu rais JK kwa upole huu!. Lingekuwa ni bunge makini, imperchment process ingeanzia pale pale right away kwa sababu rais hana mamlaka ya kuizuia sheria kuchukua mkondo wake!, huu ni uvunjaji wa katiba ya JMT!.

      Ni upole huo huo ndio unaopelekea hajamwajibisha Waziri wa Afya na naibu wake kwa sababu anawahurumia!.

      Ushauri ni kwa JK kuwa bold na kufanya maamuzi magumu!. Mfano kwenye huu mgomo wa sasa, siungi mkono JK kuitikia shinikizo la madaktari na wanaharakati kumwajibisha Mponda na naibu wake, hiyo nayo ni weakness. Bold decision ni wahusika watakaosabisha kifo chochote, kupandishwa kizimbani kwa murder!.

      JK anatakiwa kupunguza huruma na upendo wa mshumaa kumulikia wenzake huku yeye kwake kunateketea!. Huruma na upendo alioisha uonyesha sasa unatosha!. JK anatakiwa awe mkali kama alivyokuwa Nyerere watu kujua wamefutwa kazi ni kupitia taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku ya RTD tena ikisomwa na David Wakati!.(RIP).

      Ni huruma na upendo huu uliopitiliza ndio unapelekea kuwahurumia baadhi ya mawaziri na wasaidizi wake ambao hawamsaidii hivyo kuendelea kuwabeba!.

      Kwa vile JK hawezi kufanya kila kitu, piga chini wale wote ambao hawakusaidii hata ikibidi kumpiga chini Pinda, piga chini ili uliokoe taifa katika kipindi hiki chako cha miaka 3 kilichobakia!.

      Nawatakia majadiliano mema.

      Natanguliza shukrani kwa kuzingatia spirit ya constructive criticisim in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa!.

      Wasalaam

      Pasco wa jf.

      NB. Kama hauwezi constructive criticisim unaweza kujisomee tuu na kuishia zako bila kuchangia, kwani sio lazima uchangie kila thread!.
      Mode, nakuomba na hii thread ifanye sticky ili tunapoendelea kusoma yale mazuri ya JK, na mabaya pia tuyaone!.

    15. #92
      IKHOIKHOI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th January 2012
      Location : Bustani ya Eden
      Posts : 344
      Rep Power : 436
      Likes Received
      34
      Likes Given
      34

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Tanzania ni nchi pekee iliyopo ktk likizo ya uongozi kw nafasi ya rais tangu 2005
      Pasco and John Kangethe like this.
      ora et labora

    16. #93
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7367
      Likes Received
      6151
      Likes Given
      22265

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By Pasco
      Wanabodi,
      Baada ya kujadili mazuri na mafanikio ya rais wetu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kila kwenye mafanikio hapakosi matatizo, mapungufu au changamoto ambazo zikifanyiwa kazi zinabadilisha hali iliyopo sasa na kutupeleka hali bora zaidi.

      Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!.

      Katika kujadili mapungufu, madhaifu, matatizo na changamoto zinazomkabili rais Jakaya Kikwete, nawaombeni tujadili kwa spirit ya constructive criciticism kwa kueleza mapungufu hayo in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa.

      Watanzania tumekuwa ni watu wa kilalamika na kunung'unika wakati wote bila kuchukua hatua zozote positive za kurekebisha!. Naomba hii thread sio thread ya malalamiko au manunguniko dhidi ya JK bali thread ya kutoa ushauri nini cha kufanyika!.

      Kwa kuanzia moja ya mapungufu makubwa ya JK ni mtu wa huruma iliyopitiliza mipaka matokeo yake kutafsiriwa kama ni weakness, yaani "JK ni rais weak"!,: asiyeweza kuchukua maamuzi magumu!.

      Mfano wa kwanza wa udhaifu huu wa huruma uliyopitiliza ni pale alipoyasamehe yale majizi ya EPA kwa kuyaruhusu yarudishe fedha yalizo kwiba kwa exchange ya kusemehewa na kutofikishwa mahakamani!. Hata Spika Sitta pia alimlaumu rais JK kwa upole huu!. Lingekuwa ni bunge makini, imperchment process ingeanzia pale pale right away kwa sababu rais hana mamlaka ya kuizuia sheria kuchukua mkondo wake!, huu ni uvunjaji wa katiba ya JMT!.

      Ni upole huo huo ndio unaopelekea hajamwajibisha Waziri wa Afya na naibu wake kwa sababu anawahurumia!.

      Ushauri ni kwa JK kuwa bold na kufanya maamuzi magumu!. Mfano kwenye huu mgomo wa sasa, siungi mkono JK kuitikia shinikizo la madaktari na wanaharakati kumwajibisha Mponda na naibu wake, hiyo nayo ni weakness. Bold decision ni wahusika watakaosabisha kifo chochote, kupandishwa kizimbani kwa murder!.

      JK anatakiwa kupunguza huruma na upendo wa mshumaa kumulikia wenzake huku yeye kwake kunateketea!. Huruma na upendo alioisha uonyesha sasa unatosha!. JK anatakiwa awe mkali kama alivyokuwa Nyerere watu kujua wamefutwa kazi ni kupitia taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku ya RTD tena ikisomwa na David Wakati!.(RIP).

      Ni huruma na upendo huu uliopitiliza ndio unapelekea kuwahurumia baadhi ya mawaziri na wasaidizi wake ambao hawamsaidii hivyo kuendelea kuwabeba!.

      Kwa vile JK hawezi kufanya kila kitu, piga chini wale wote ambao hawakusaidii hata ikibidi kumpiga chini Pinda, piga chini ili uliokoe taifa katika kipindi hiki chako cha miaka 3 kilichobakia!.

      Nawatakia majadiliano mema.

      Natanguliza shukrani kwa kuzingatia spirit ya constructive criticisim in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa!.

      Wasalaam

      Pasco wa jf.

      NB. Kama hauwezi constructive criticisim unaweza kujisomee tuu na kuishia zako bila kuchangia, kwani sio lazima uchangie kila thread!.
      Baada ya kilichomkuta Mhe. JJ. Mnyika, nimepitia hii thread nikagundua kumbe kosa la Mnyika ni kuwa too bold to call a spade, a spade!.

      Katika kumzungumzia JK, nilitoa angalizo lifuatalo "Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!." Inawezekana kabisa, Mhe. Ndungai amemtoa nje Mnyika kwa kuyaona matamshi yale siyo ya staha!, that being the case, Naibu Spika was Right!

    17. #94
      Sr. Magdalena's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th August 2011
      Posts : 301
      Rep Power : 523
      Likes Received
      117
      Likes Given
      36

      Default

      Quote By Pasco

      Baada ya kilichomkuta Mhe. JJ. Mnyika, nimepitia hii thread nikagundua kumbe kosa la Mnyika ni kuwa too bold to call a spade, a spade!.
      Kaka Pasco bado nataka kuendelea kukuheshimu, personally na michango yako hapa jukwaani, convince me please.

      Quote By Pasco

      Inawezekana kabisa, Mhe. Ndungai amemtoa nje Mnyika kwa kuyaona matamshi yale siyo ya staha!, that being the case, Naibu Spika was Right!
      Aisee!
      Pasco likes this.

    18. #95
      Sr. Magdalena's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th August 2011
      Posts : 301
      Rep Power : 523
      Likes Received
      117
      Likes Given
      36

      Default

      Quote By Pasco
      Wanabodi,

      Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!.

      "JK ni rais weak"!,: asiyeweza kuchukua maamuzi magumu!.

      .
      Fafanua pleasa, kuanzia hapo juu kwenye warning hadi hapo chini..je wewe unatofauti gani na JJ na mamlaka ya kuja hapa na kumhukumu JJ unayatoa wapi huku na wewe umefanya vilevile.
      Pasco and John Kangethe like this.

    19. #96
      Moony's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2011
      Location : Oshakati, Namibia
      Posts : 1,103
      Rep Power : 630
      Likes Received
      260
      Likes Given
      279

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By Pasco
      Mkuu Kongosho, mission na vission ni ile ilani ya uchaguzi aliyoinadi na kuchaguliwa. He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.

      vision
      Pasco and Communist like this.

    20. #97
      Moony's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th April 2011
      Location : Oshakati, Namibia
      Posts : 1,103
      Rep Power : 630
      Likes Received
      260
      Likes Given
      279

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By Pasco

      Baada ya kilichomkuta Mhe. JJ. Mnyika, nimepitia hii thread nikagundua kumbe kosa la Mnyika ni kuwa too bold to call a spade, a spade!.

      Katika kumzungumzia JK, nilitoa angalizo lifuatalo "Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!." Inawezekana kabisa, Mhe. Ndungai amemtoa nje Mnyika kwa kuyaona matamshi yale siyo ya staha!, that being the case, Naibu Spika was Right!
      right?, May be he had a good reason to but how he handled the issue... mmmhh....alitumia JAZBA.
      busara haijatumika katu.
      Pasco and Communist like this.

    21. #98
      Las Mas Bobos's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2012
      Posts : 890
      Rep Power : 527
      Likes Received
      292
      Likes Given
      82

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By Pasco
      Mkuu Kongosho, mission na vission ni ile ilani ya uchaguzi aliyoinadi na kuchaguliwa. He had a mission ya maisha bora kwa kila Mtanzania na vision Tanzania yenye neema inawezekana kupitia ari mpya, kasi mpya, na nguvu mpya!. Watendaji aliowategemea ndio wamemwangusha!.
      Mijadala ya namna hii na wabunge wa CCM tofauti iko wapi? Huu ndio upuuzi aliousema Mnyika. Eti watendaji wamemwangusha, kwani nani alimchagulia watendaji?

      Wewe nafahamu kuwa una akili zote, mashaka yangu umetumwa kubadili mada hapa jamvini. Mtu unaweza kuacha wezi wachukue billions halafu unawaambia warudishe halafu mtu mwingine JUHA anasema hiyo ni huruma! Angekuwa na huruma angewahurumia wamama wanaojifungulia sakafuni huko vijijini.

      Njoo na mada nyingine ya maana, hii imekaa ki-CCM (according to Ho.Mnyika MP)
      Pasco, Ngigana and Communist like this.
      By the time a man comes to realize that his father was right, he usually has a son who think he is wrong.

    22. #99
      Midavudavu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd January 2012
      Posts : 199
      Rep Power : 408
      Likes Received
      38
      Likes Given
      0

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Tabia ya mtoto huwa inarandana na wazazi wake.

      Akiwa mtukukutu ujue kuna shida katika malezi aliyopata kutoka kwa walezi au wazazi . Akiwa mvivu si ajabu anajifunza toka kwa wazazi/walezi wake.

      Naamini hatuwezi kuzungumzia udhaifu wa viongozi tuliowachagua bila kuzungumzia udhaifu wetu sisi tunaowachagua.

      Tunapaswa kujilaumu kwa udhaifu miongoni mwa wale tuliowachagua kuwa viongozi wetu.
      Pasco and Communist like this.

    23. #100
      Communist's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st June 2012
      Location : Ubungo
      Posts : 2,714
      Rep Power : 2263
      Likes Received
      599
      Likes Given
      783

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By zumbemkuu
      1, hasimamii kile anachokisema (kwa ufupi ni muongo)
      2, ni mtu kigeugeu
      3, anajifanya msikivu sana kumbe mnafiki.
      4, ni mdini mkubwa.
      5. hajui ni kwanini yupo ikulu na wala hajui majukumu ya mtu anayefika ikulu ni yapi. (anafikiri ikulu ni dangulo au soko la maharamia)
      Huyu Ndugu yangu hajui maana ya Ikulu ni mahala patakatifu. Tangu alipofundishwa kuweka maslahi binafsi mbele na kumtumia Rtzi kuchota, amepoteze dira. Amejaa mgongano wa kimaslahi, na sasa amekuwa ni dhaifu saanaa kwa nafasi hiyo. Good charisma but bad character.
      Pasco likes this.
      Simple life is healthier than egoism.

    24. Study Abroad
    Page 5 of 10 FirstFirst ... 34567 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...