Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

    Report Post
    Page 10 of 10 FirstFirst ... 8910
    Results 181 to 183 of 183
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,862
      Rep Power : 7377
      Likes Received
      6195
      Likes Given
      22551

      Default Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Wanabodi,
      Baada ya kujadili mazuri na mafanikio ya rais wetu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, kila kwenye mafanikio hapakosi matatizo, mapungufu au changamoto ambazo zikifanyiwa kazi zinabadilisha hali iliyopo sasa na kutupeleka hali bora zaidi.

      Katika kujadili mapungufu, nawaombeni sana tujadili kwa nidhamu na staha kwa kuzingatia huyu tunayemjadili ni rais wetu, hivyo sitegemei kuona lugha za kebehi, machukizo, matukano, au maudhi, kwa kifupi lugha zozote ambazo hazina staha!.

      Katika kujadili mapungufu, madhaifu, matatizo na changamoto zinazomkabili rais Jakaya Kikwete, nawaombeni tujadili kwa spirit ya constructive criciticism kwa kueleza mapungufu hayo in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa.

      Watanzania tumekuwa ni watu wa kilalamika na kunung'unika wakati wote bila kuchukua hatua zozote positive za kurekebisha!. Naomba hii thread sio thread ya malalamiko au manunguniko dhidi ya JK bali thread ya kutoa ushauri nini cha kufanyika!.

      Kwa kuanzia moja ya mapungufu makubwa ya JK ni mtu wa huruma iliyopitiliza mipaka matokeo yake kutafsiriwa kama ni weakness, yaani "JK ni rais dhaifu", weak!, asiyeweza kufanya maamuzi magumu!.

      Mfano wa kwanza wa udhaifu huu wa huruma uliyopitiliza ni pale alipoyasamehe yale majizi ya EPA kwa kuyaruhusu yarudishe fedha yalizo kwiba kwa exchange ya kusemehewa na kutofikishwa mahakamani!. Hata Spika Sitta pia alimlaumu rais JK kwa upole huu!. Lingekuwa ni bunge makini, imperchment process ingeanzia pale pale right away kwa sababu rais hana mamlaka ya kuizuia sheria kuchukua mkondo wake!, huu ni uvunjaji wa katiba ya JMT!.

      Ni upole huo huo ndio unaopelekea hajamwajibisha Waziri wa Afya na naibu wake kwa sababu anawahurumia!.

      Ushauri ni kwa JK kuwa bold na kufanya maamuzi magumu!. Mfano kwenye huu mgomo wa sasa, siungi mkono JK kuitikia shinikizo la madaktari na wanaharakati kumwajibisha Mponda na naibu wake, hiyo nayo ni weakness. Bold decision ni wahusika watakaosabisha kifo chochote, kupandishwa kizimbani kwa murder!.

      JK anatakiwa kupunguza huruma na upendo wa mshumaa kumulikia wenzake huku yeye kwake kunateketea!. Huruma na upendo alioisha uonyesha sasa unatosha!. JK anatakiwa awe mkali kama alivyokuwa Nyerere watu kujua wamefutwa kazi ni kupitia taarifa ya habari ya saa 2:00 usiku ya RTD tena ikisomwa na David Wakati!.(RIP).

      Ni huruma na upendo huu uliopitiliza ndio unapelekea kuwahurumia baadhi ya mawaziri na wasaidizi wake ambao hawamsaidii hivyo kuendelea kuwabeba!.

      Kwa vile JK hawezi kufanya kila kitu, piga chini wale wote ambao hawakusaidii hata ikibidi kumpiga chini Pinda, piga chini ili uliokoe taifa katika kipindi hiki chako cha miaka 3 kilichobakia!.

      Nawatakia majadiliano mema.

      Natanguliza shukrani kwa kuzingatia spirit ya constructive criticisim in good faith kwa nia ya kujenga na sio kubomoa!.

      Wasalaam

      Pasco wa jf.

      NB. Kama hauwezi constructive criticisim unaweza kujisomee tuu na kuishia zako bila kuchangia, kwani sio lazima uchangie kila thread!.
      Last edited by Pasco; 2nd February 2013 at 06:06.


    2. #181
      Philipo Kidwanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2012
      Location : kusadikika
      Posts : 2,063
      Rep Power : 983
      Likes Received
      573
      Likes Given
      147

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Lipo jambo moja ambalo watu hawajui na kila siku wanataka kutuongopea kwamba raisi hana matatizo.ambalo hawajui ni kwamba hata uclass monitor jk hauwezi.

    3. #182
      Philipo Kidwanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2012
      Location : kusadikika
      Posts : 2,063
      Rep Power : 983
      Likes Received
      573
      Likes Given
      147

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Quote By pasco View Post
      kazou, kwenye hili la jk kuwa ni msikivu sana na kusikiliza mpaka umbeya na majungu, naomba nimtetee!. Angesikiliza mpaka umbea na majungu, saa hizi angeshasikia watu kibao wana...a debe!. Hata jf ingeshafingwa zamani!.

      Kati ya madhaifu ya jk ni mapuuza!. Naamini kabisa kuna vitu anaambiwa afanye kwa maslahi ya taifa, anasikiliza tuu na hafanyi!. Naamini baada ya ule mgomo wa kwanza, baada ya kamati ya bunge kurudisha majibu, walitoa mapendekezo fulani na kumpigia jk usiku huo huo na kumwambia!. Alisikiliza and he did nothing!. Pinda baada ya kuwatimua mama nyoni na dr. Mtasiwa, alimshauri jk kuwatimua watu fulani, jk did nothing!. Kiukweli jk sio msikivu kabisa!.

      Kwa vile msingi wa thread hii ni constructive criticisim. Jk lazima sio tuu awe msikivu zaidi bali pia awe mtekelezaji promptly baadhi anayotasikia!.

      Tuchukue fursa hii kwa kuwa msikivu kwenye baadhi ya mambo kikiwemo kilio cha katiba mpya na kuwakaribisha wapinzani ikulu kuwasikiliza na kutekeleza ushauri wao!.

      Pia tumpongeze kwa kutosikiliza majungu pale ikulu, kwa nature ya watu wa ukanda pwani. Majungu ni jadi yao!. Tunamshukuru jk anatoka ukanda huo na wapika majungu wamefunga breki!.
      kwa taarifa yako mjungu na umbea ndio vinamuharibu na ndio maana huyu jamaa ana kisasi sana.bila kusikiliza majungu saa hizi angekua mbali sana.we angalia mtu kama nape kapewa cheo kimajungu majungu tu.jk ukigombana na mtu anakupatia cheo,kumbuka sakata la kashfa ya jengo la umoja wa vijana alipogombana lowasa moja kwa moja akampa ukuu wa wilaya na baadae ukatibu mwenezi na hapo ndo tukasikia ishu ya kuvua gamba.kwa majungu anayo kaka.halafu ana tabia ya kutanguliza wenzake wakishaharibikiwa na yeye ndio anajitokeza muulize pinda anajua hili.

    4. #183
      masatujr1985's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th October 2011
      Location : Anumbeye
      Posts : 432
      Rep Power : 472
      Likes Received
      67
      Likes Given
      26

      Default Re: Mapungufu ya JK: Constructive Criticisim!

      Ni kweli kabisa yaweza kuwa watu wanajadili kwa kauli zisizo na staa kwa Rais wa Tanzania. Yote yanatokana na heshima aliyojijengea kwa watanzania wenyewe. Hata baba nyumbani akiwa hatimizi mahitaji ya muhimu kwa wanfamilia wake, alhali watoto wanafahamu fika kuwa anao uwezo wa kufanya hivyo,si shaka kuwa atapoteza heshima na imani kwa watu wake (kama ilivyo kwa Rais wa Tanzania). Anazo sifa na labda malengo ya kuikwamua nchi katika lindi la uozo uliopo kila idara kwa sasa, lakini hana uwezo wa kuset strategy za kufikia malengo yake!!!! Nch hii haina Kiranja thabiti

    Page 10 of 10 FirstFirst ... 8910

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...