Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

    Report Post
    Page 5 of 23 FirstFirst ... 3456715 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 442
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Wanabodi,
      Naangalia TBC Live, Rais Jakaya Kikwete yuko hewani!
      Miongoni wa mazuri ya JK, ni having a good sense of humour, akiongea, huchoki kumsikiliza!.
      Alipokuwa akiongelea kilimo cha ndizi kijijini kwao Msoga, Bagamoyo, akasema wakulima wana bananisha migomba mingi kwenye shina moja, matokeo yake kila mgomba unatoa kichane kimoja au viwili ya vindizi vilivyokondeana!.

      Akasema wanakijiji wale wanalima hivyo kwa sababu hawajui kuwa kama wakiacha mgomba mmoja kwenye shina moja, mgomba huo utatoa mkungu mkubwa wa ndizi, na ndizi zenyewe zitakuwa ni ndizi za shibe kama "Mrisho Mpoto"!. Ukumbi mzima ulizizima kwa vicheko, watu hawana mbavu!.

      Kuwa na 'good sense of humour' ni kipaji na ni miongoni mwa mambo mazuri machache ya rais wetu Jakaya Kikwete, besides good looking!.

      Kwa wale wenye kumbukumbu ya hotuba za Mwalimu, ukiondoa ile hotuba yake ya kutangaza vita, hotuba za Mwalimu, watu walikuwa wanacheka na hutamani amalize kuzungumza!.

      Hii ni thread ya miongoni mwa mazuri ya JK, kama na wewe unalo zuri lolote la JK ambalo unalijua, unaweza kuliweka.

      Kwa vile tunazungumzia mazuri, ningeomba wale ambao hawana zuri lolote la kuzungumzia JK, sio lazima mchangie, wala zuri hili la "good sense of humour", haimaanishi JK sasa ndio rais bora kwa Tanzania, wala haina maana ndio hana mabaya yake!, leo tuzungumzie mazuri yake!

      Angalizo:
      Wanabodi wenzangu, tunajukumu la kujimoderate sisi wenyewe kulinda hadhi ya jukwaa letu, haiwezekana kila siku sisi tukawa ni watu wa kulalamika tuu, au kubonda tuu, mara moja moja kwenye mazuri, pia tutoe sifa pale panapo stahili!.

      Natanguliza Shukrani kwa kunielewa!

      Asanteni!

      Pasco (wa jf)

      Note: Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali ni muumini wa ukweli "seek the truth, and the truth will set you free"!. Kwa wale wanaofikiri Pasco wa jf, ni mshabiki wa CCM, tafuteni thread yangu ya "CCM Imechokwa" !.


      --------------------------------------------
      Hoja Nyingine za Thread ya kibananhukhu iliyounganishwa #148
      Quote By kibananhukhu
      Pamoja na list ya mambo lukuki ambayo wakuu mnamlaumu JK, lakini ni kweli kuwa kuna kitu anafanya siyo kwamba amelele fofofo. Kuna mapungufu pia ni kwa nia njema mnayaainisha kusaidia uboreshaji kazi. Nimefuatilia na kuyaona baadhi ya mazuri ya JK Kama list inavyoainisha, ninaweza kuwa na upungufu kidogo katika takwimu hii itatokana na mimi kutumia kumbukumbu zangu nipo tayari kusahihishwa takwimu. Tupitie mazuri ya JK HAPA CHINI

      1. Mpango wa kuiruhusu bandari (THA) kufanya kazi kwa kuanza na technologia mpya ili dereva tu ndiye awe anakwenda bandarini kupakia mzigo na mengine yote yatamalizwa kwa njia ya mtandao, e-port. Kumbukeni TICTS walikuwa na mkataba mbaya sana kwa miaka 15, na ulirejewa kwa mazingira ya kutatanisha.

      2. Dar tayari nyumba 50 zimeanza kutumia gesi kwa matumizi mbali mbali ya ndani, kama ulaya na kwingineko kwa mara ya kwanza. Mikocheni wameanza jiandaeni kuvuta gesi majumbani kwenu.

      3. Magari yameaanza kutumia gesi japokuwa bado kuna baadhi ya vikwazo kwa wasaidizi wa raisi. Mpango wa JK ilikuwa matuzi ya petroli katika gari yapungue kwa 80%, lkn ukiritimba wetu umesababisha yapungue kwa 55%

      4. Kivuko na daraja kigamboni.

      5. Mradi wa daraja Maragalasi na lami Tabora – Itigi – Kigoma

      6. Ujenzi wa barabara lami kutoka Mombo, Mtibwa turiani, Kilosa, Mikumi na baadaye ifakara, mahenge, Malinyi, Songea. Pia Ifakara, Mlimba hadi Njombe. Usafiri wa songea kupunguza safari kwa masaa 5.

      7. Barabara ya Mafinga, Iringa, Kitonga, Ruaha Mbuyuni, Madaraja mawili mpakani na morogoro imekwishapanuliwa kwa uboro wa hali ya juu. Kipande cha Ipogolo kupandisha kwenda iringa mjini kimepanuliwa sana.

      8. Bara bara ya Iringa Kwenda Dodoma Imekwishaanza

      9. Bara bara ya Tunduma hadi Sumbawanga kuna makandarasi watatu wanashindana kwa ubora wa lami.

      10. Viwanja vya ndege mikoani kuboreshwa.

      11. Karekebisha mkataba wa Songas, ulikuwa hauruhusu mtu meingine yetote awaye kujenga tena bomba la gesi. Sasahivi wakuu mnaruhusiwa kujenga mabomba ya gesi kutoka Kusini.

      12. Mkataba wa wachina na serikali kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi dar ili kuzalisha MG 2900 za umeme dar.

      13. Barabara Dodoma, Manyara lami.

      14. Ujenzi reli kutoka Tanga, Musoma, Uganda.

      15. Ujenzi bandari, Tanga, Mtwara na Babamoyo

      16. Uwanja wa Ndege Terminal two wajengwa.

      17. Maeneo ya Umwagiliaji maji, hekari 20,000 zimejengwa na lengo ni ekari 1milioni.

      18. Kilimo kwanza mashamba darasa na ongezeko la mavuno kwa ekari.

      19. Tanzania ni ya kwanza kwa export afrika masharik na kati

      20. Mradi wa makaa ya Mawe Mchuchuma na katewaka liganga kuzalisha MGW za kutosha nchi nzima

      21. Mradi wa machimbo mgodi wa chuma Liganga, uzalishaji wa Titanium, Vanadium, Fe kwa ajili ya utengenezaji nondo, malighafi ya mabati, vyuma vya kujengea madaraja na maghorofa, kuweka pembezoni mwa mabarabara kuzalishwa nchini. Viwanda vya kutengeneza vifaa vya ujenzi wa meli, ndege, na magari kujengwa nchini.

      22. Machimbo ya makaa yam awe Ngaka Mbinga Ruvuma, uwezo Kuzalisha pia umeme MG 400.

      23. Hospitali upasuaji moyo kwa mara ya kwanza Tanzania.

      24. Hospitali kubwa mingoni mwa zitakazoheshimika kujengwa Tanzania na Appollo ya India. Maradhi yote kutibiwa Tanzania.

      25. Uboreshaji shirika la nyumba NHC, Baadhi ya watanzania kunufaika na mikopo ya nyumba na nyumba kuanza kujengwa kwa spidi kali.

      26. Ujenzi wa barabara nane Dar hadi chalinze.

      27. Ufumuaji na ujenzi wa reli ya kati dar, hadi kigoma, mwanza, mpanda, Rwanda na Burundi.

      28. Ubareshaji maabara shule za kata ($ 90Milioni)

      29. Idadi ya walimu kwaajili ya shule za kata na nyinginezo kuanzia muda mfupi ujao, walimu elfu 40 kuhitimu kila mwaka.

      30. Baadhi ya shule nyingi binafsi zimeanza kudorola au kufungwa kabisha, wengi wamejiunga na shule za kata na ubora unapanda japo kwa spidi ndogo.

      31. Idadi kubwa ya wanafunzi vyuo vikuu, Udom uwezo elfu 40, SAUT elfu 15, UDSM Elfu 15, Ruco elf 2.5, Mkwawa elfu 2.5 Tumaini elfu 2, Open University elfu 20 nk.

      32. Wafanya biashara wamepewa kipau mbele term ya JK, Wengi husafiri na Mheshimiwa Raisi kutafuta na kupata fursa za biashara nje.

      33. Uhuru wa Vyombo vya habari, waandishi wanafanya mambo kwa uhuru ambao wasingelithubutu enzi ya Mwalimu, Mwinyi wala Mkapa. Hata baadhi ya ninyi wakuu, mnaruhusuwa kutoa mawazo yenu japo wengine wanatukana matusi ya nguoni lakini JK anavumilia sana.

      34. Amegundua fitna nyingi sana serikalini, majungu, uongo na sasa hivi anakua mwangalifu sana katika maamuzi na inalazimika kuonekana kana kwamba hana maamuzi ili awe na subira. (Ukiwa na hasiri usifanye maamuzi, ahirisha upate busara)

      35. Makampuni ya madini, yamekupali kuanza kulapa 30% kutoka faida zitakazo patikana kuanzia 2012.

      36. Wapinzani wameanza kumwelewa na kumsifia kwa yale anayoyafanya vizuri.

      37. Mnaweza ongeza list nyingine ili nije baadaye na listi ya faida za kiuchumi kwa taarifa tu, inflation inachangiwa na gharama za chakula kwa 16%.

      Kuna mambo madogo ya kiufundi yakirekebishwa inflation inapashwa iwe 8% single digit. Mfano mahindi yanaoza Ruvuma, Iringa, na Sumbawanga yangeweza kutoa mchango katika kupunguza gharama za chakula na mfumuko wa bei ukashuka.Mengine mengi nitaongeza baadaye. Nadhani kwa faida ya wakuu wangu, nitajitahidi kufuatilia pia ilani yake ili nilinganishe na hayo hapo juu. Hata hivyo, ni ukweli kwamba kwa upanda wa barabara tu, miaka 50 tangu uhuru lami ilifikia km 6000, JK Pekee ameweka mikataba ya lami km 11,000.

      Kuna vitu anafanya JK.
      Last edited by Viwango; 6th March 2012 at 11:52. Reason: Adding points of merged thread

    2. FemaTV & Radio

    3. #81
      Magane's Avatar
      Member Array
      Join Date : 18th July 2011
      Posts : 61
      Rep Power : 409
      Likes Received
      17
      Likes Given
      0

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Ni baba wa democracia katika taifa letu la Tanzania hapajatokea kiongozi yeyote tangu uhuru kuwahi kuruhusu demokrasia ichukue mkondo wake katika hali hii tunayoishuhudia pia ni kiongozi mvumilivu na msikivu asiyekurupukia maamuzi.Tazama anavyowachukua watanzania wote bila ya ubaguzi. Mungu ambariki na kumjalia afya njema. Amen
      zomba and Pasco like this.

    4. #82
      manuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2009
      Posts : 711
      Rep Power : 655
      Likes Received
      263
      Likes Given
      185

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Wapi Pasco wa JF.?
      Pasco likes this.
      TO BE HURT ITS YOUR OWN WILLING

    5. #83
      Kipeperushi's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th August 2011
      Location : DAR ES SALAAM
      Posts : 168
      Rep Power : 430
      Likes Received
      29
      Likes Given
      9

      Default

      Quote By ngwini
      Nitamkumbuka kwa kupata CPA na faida za kuwa m2mishi wa Umma nikiwa kijana na kupewa u-chief accountant..maana bila CPA hauwez kuwa chief
      Daah..! Kumbe JK huwa anatoa CPA...!?, haya bwana hongera..
      Pasco likes this.

    6. #84
      John Kangethe's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th October 2008
      Posts : 75
      Rep Power : 556
      Likes Received
      19
      Likes Given
      166

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By The Boss
      JK angekuwa the best ever president kama tu
      'angebahatika' kuwa na the best and the brightest around him
      na angekubali kuwa 'hajui'
      na anahitaji kusaidiwa......kwa sababu ana sifa nyiingi mno za kiongozi wa kuwa kiongozi bora...

      1.kwanza anapenda sifa ya kuonekana anaweza
      2.pili ni msikivu na mvumilivu na hana papara
      3.ana personality ya a 'movie star'
      watu wanampenda tu hata kama wanajua hawezi
      4.anapenda watu.....haoni tabu kuchanganyika na watu
      5.anapenda anasa,hii angeweza kuitumia kwa faida.mfano anapenda kuvaa suti za gharama
      basi angehakikisha tuna viwanda vya nguo za quality anayotaka

      but too bad mshauri wake mkuu ni Yussuph Makamba
      Hatuna rais, bora Mzee wetu Mkapa.
      Kikwete ni tatizo, ni tatizo kubwa, ni mbabaishaji, hana kipaji cha uongozi, siasa hajui.

      Wananchi walionekana kumpenda sana kwa kusema tumepata rais kijana, rais amabye ataleta mabadiliko. Lakini hii haikuwa kweli.

      Rushwa tupu kwenye mikataba ya madini. Hakuna tunachofaidi kwenye madini zaidi ya kuijenga Europe na America. Ni aibu kuona utajiri wa Tanzania unajenga nchi za Ulaya na Amerika.
      Jasusi and Pasco like this.

    7. #85
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By John Kangethe
      Hatuna rais, bora Mzee wetu Mkapa.
      Kikwete ni tatizo, ni tatizo kubwa, ni mbabaishaji, hana kipaji cha uongozi, siasa hajui.

      Wananchi walionekana kumpenda sana kwa kusema tumepata rais kijana, rais amabye ataleta mabadiliko. Lakini hii haikuwa kweli.

      Rushwa tupu kwenye mikataba ya madini. Hakuna tunachofaidi kwenye madini zaidi ya kuijenga Europe na America. Ni aibu kuona utajiri wa Tanzania unajenga nchi za Ulaya na Amerika.
      Mikataba ya madini Kikwete kaikuta na aakiundia tume ya kurekebishwa mikataba na Kikwete akamchagua mwakilishi wa upinzani Zitto kabwe. Umashajiuliza hiyo mikataba ilandikwa wakati wa nani? Mkapa. usimsukumie Kikwete madudu ya Nkapa.
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    8. Miaka 50

    9. #86
      Mikael P Aweda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th December 2010
      Posts : 1,840
      Rep Power : 6549
      Likes Received
      2443
      Likes Given
      2223

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      JK anapenda sana watu wake, mimi nilikutana naye ktk msiba wa Regia Mtema nyumbani kwa REGIA. Hiyo nayo ni moja ya uzuri wake, kuhudhuria misiba ya watu hata kama si wenye vyeo vya juu serikalini AU siyo mbunge. Watu wa kawaida kabisa. Si kila Rais anaweza kufanya hivyo.
      Ndahani, Pasco and Rock City like this.
      Mikael P Aweda 0784 583 330
      Elimu kwanza

    10. #87
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Moja ya mambo mabaya sana na yanayofanya Kikwete achukiwe ni kuongeza mashule, kuongeza vyuo vya walimu, kuongeza intake ya wanafunzi vyuo vikuu, kuongeza vyuo vya ufundi. Kwa ufupi, kupanua wigo wa elimu kuliko marais wote waliopita pamoja na mkoloni, ni kitu kibaya sana alichokifanya Kikwete. Asingefanya hicho, mpaka leo angekuwa ni mzuri sana na anae-kubalika na Watanzania wote.
      TIMING and Pasco like this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    11. #88
      ANKOJEI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th November 2010
      Posts : 404
      Rep Power : 512
      Likes Received
      98
      Likes Given
      89

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      barabara wakubwa hatakama akisemwaje, linapokuja swala la barabara namkubali....doi, senkenke wakuu palikuwa panatisha
      iyo ya uvumilivu nalo n neno, kumbuka cku ile pale mwembe yanga jamaa mmoja alipo mchana live uch wa mnyama kama vile hana wazazi. it was terrible, jamaa kamsamehe kiroho safi tu!
      Pasco likes this.

    12. #89
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default

      Quote By zomba
      What has survival got to do with raping one's daughter? be realistic. Who is surviving by raping his daughter? what a tinker.
      I still have conscious!
      TIMING likes this.

    13. #90
      Lokissa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Location : Goba
      Posts : 4,092
      Rep Power : 5807
      Likes Received
      1025
      Likes Given
      2876

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      hivi daraja la kigamboni linajengwa na CCM au ni michango ya wanachama wa NSSF ambao ni wafanyakazi wa nyanja tofuati bila kujali itikadi zao
      sidhani kama chama kinahusika hapa?
      mazuri ya JK ni ever smilling president anaewaonea aibu mawaziri wake wenye kashfa lukuki bila thubutu ya kuwawajibisha.



      Quote By Raia Mwema
      Pasco



      leo umeleta thread ya maana hebu tujaribu kuzungumzia japo mazuri machache ya Jk. Hakuna binadamu asiye na zuri hata moja

      Mimi nitamkumbuka kwa kutununulia Panton la magogoni - Kigamboni. kabla ya hapo ilikuwa ni mateso.

      Panton kubwa Afrika Mashariki na kati hadi Mwai kibaki alikuwa kuliona alipotembelea Tanzania na akaahidi kuwanunulia wakenya

      Linabeba magari 60 na abiria 2000

      Na sasa ujenzi wa daraja la Kigamboni umeanza
      Pasco likes this.
      You may know me but you have no Idea who I am !

    14. #91
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Lokissa
      hivi daraja la kigamboni linajengwa na CCM au ni michango ya wanachama wa NSSF ambao ni wafanyakazi wa nyanja tofuati bila kujali itikadi zao
      sidhani kama chama kinahusika hapa?
      mazuri ya JK ni ever smilling president anaewaonea aibu mawaziri wake wenye kashfa lukuki bila thubutu ya kuwawajibisha.
      Kwani Kikwete ni Rais wa wana CCM tu? tuiona hata magwanda walipokuwa na matatizo na bunge waliomba kumuona Ikulu ili awatatulie tatizo lao, wakapewa Juisi na kashata na pilau na akawatatulia tatizo lao wakatoka huko kimyaaaaaaaa, mpaka leo, hatujasikia maandamano wala kususa. Hiyo ni sifa moja kubwa sana ya Kikwete, anatatua matatizo yaliyowashinda wengine.

      Katika sifa za Kikwete ni pamoja na:

      Kuwapatanisha Wakenya.
      Kuwapatanisha Wazanzibari.
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    15. #92
      Gwalihenzi's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 2,379
      Rep Power : 0
      Likes Received
      615
      Likes Given
      377

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By zomba
      What has survival got to do with raping one's daughter? be realistic. Who is surviving by raping his daughter? what a tinker.
      Zomba, which school did you attend?
      Pasco and Lokissa like this.

    16. #93
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Gwalihenzi
      Zomba, which school did you attend?
      Who the hell are you to question my education? I am simply better educated than you by 100 folds.
      Ndahani and Pasco like this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    17. #94
      Rock City's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2012
      Posts : 626
      Rep Power : 572
      Likes Received
      193
      Likes Given
      106

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Nyongeza:
      Wakenya wanamuheshimu sana JK , tena saana. Anakumbukwa na atakumbukwa na Wakenya katika upatanishi wa PNU/ODM na hata KANU.
      Pasco likes this.

    18. #95
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By zomba
      Who the hell are you to question my education? I am simply better educated than you by 100 folds.
      Haahaaaa! Mkuu umenichekesha sana..calm down...don't take it personal!
      zomba and Pasco like this.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    19. #96
      MZEE WA ROCK's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd October 2011
      Posts : 145
      Rep Power : 415
      Likes Received
      17
      Likes Given
      99

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By ngwini
      Nitamkumbuka kwa kupata CPA na faida za kuwa m2mishi wa Umma nikiwa kijana na kupewa u-chief accountant..maana bila CPA hauwez kuwa chief
      kweri hiyo CPA umepewa coz wewe unaonekana ni full kilaza, (elewa mada na ujadili mada kwa usahihi) usidhni kila unachofikilia unatupia tu
      Pasco likes this.

    20. #97
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,623
      Rep Power : 2892
      Likes Received
      3840
      Likes Given
      12234

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By zomba
      Mikataba ya madini Kikwete kaikuta na aakiundia tume ya kurekebishwa mikataba na Kikwete akamchagua mwakilishi wa upinzani Zitto kabwe. Umashajiuliza hiyo mikataba ilandikwa wakati wa nani? Mkapa. usimsukumie Kikwete madudu ya Nkapa.
      Hapana. Huu ni uwongo mtupu. Mikataba ya madini ameisani Kikwete mwenyewe akiwa waziri wa nishati na madini. Sikiliza hotuba yake ya March 2007 Afrika kusini anavyojisifia jinsi alivyokata mbuga kuwatafuta wawekezaji katika madini. Huyu jamaa ni janga la taifa. Hata pale alipoahidi kuipitia upya ali exempt kampuni kubwa ya rafiki yake, Barrick. Tunavuna uoza aliotupandia Kikwete na Mkapa wake.
      Pasco and John Kangethe like this.

    21. #98
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Jasusi
      Hapana. Huu ni uwongo mtupu. Misaada ya madini ameisani Kikwete mwenyewe akiwa waziri wa nishati na madini. Sikiliza hotuba yake ya March 2007 Afrika kusini anavyojisifia jinsi alivyokata mbuga kuwatafuta wawekezaji katika madini. Huyu jamaa ni janga la taifa. Hata pale alipoahidi kuipitia upya ali exempt kampuni kubwa ya rafiki yake, Barrick. Tunavuna uoza aliotupandia Kikwete na Mkapa wake.
      Ukiwa waziri wa madini ndio nini? utapingana na waziri mkuu wako na Rais wa nchi? usituletee fikira za kitoto hapa.

      Usitake kudanganya watu, huyo rafiki yake "Barrick" ni wa kampuni ipi?

      Board of Directors


      Howard L. Beck, Q.C.

      Toronto, Ontario
      Corporate Director
      Mr. Beck has been a Director of Barrick since 1984.
      C. William D. Birchall

      Toronto, Ontario
      Vice Chairman and Director, Barrick Gold Corporation
      Mr. Birchall has been a Director of Barrick since 1984.
      Donald J. Carty, O.C.

      Dallas, Texas
      Chairman, Porter Airlines Inc. and Virgin America Airlines
      Mr. Carty has been a Director of Barrick since 2006.
      Gustavo A. Cisneros

      Santo Domingo, Dominican Republic
      Chairman, Cisneros Group of Companies
      Mr. Cisneros has been a Director of Barrick since 2003.
      Peter A. Crossgrove, O.C.

      Toronto, Ontario
      Corporate Director
      Mr. Crossgrove has been a Director of Barrick since 1993.
      Robert M. Franklin

      Toronto, Ontario
      President, Signalta Capital Corporation
      Mr. Franklin has been a Director of Barrick since 2006.
      J. Brett Harvey

      Canonsburg, Pennsylvania
      Chairman, President and Chief Executive Officer, CONSOL Energy Inc.
      Mr. Harvey has been a Director of Barrick since 2005.
      Dambisa Moyo

      London, United Kingdom
      International economist and commentator on the global economy
      Elected to the Board of Directors at the 2011 Annual General Meeting.
      The Right Honourable Brian Mulroney, P.C.

      Montreal, Quebec
      Chairman of Barrick’s International Advisory Board
      Senior Partner, Norton Rose OR LLP
      Mr. Mulroney has been a Director of Barrick since 1993.
      Anthony Munk

      Toronto, Ontario
      Managing Director, Onex Corporation
      Mr. Munk has been a Director of Barrick since 1996.
      Peter Munk, C.C.

      Toronto, Ontario
      Founder and Chairman, Barrick Gold Corporation
      Prior to September 2006, Mr. Munk was also the Chairman of Trizec Properties, Inc.
      Aaron W. Regent

      Toronto, Ontario
      President and CEO, Barrick Gold Corporation
      Mr. Regent has been a Director of Barrick since February 2009.
      The Honourable Nathaniel P. Rothschild

      Klosters, Switzerland
      Corporate Director
      Founder and Co-Chairman, Vallar PLC, Co-Chairman, EN+ Group Limited
      Mr. Rothschild has been a Director of Barrick since 2010.
      Steven J. Shapiro

      Houston, Texas
      Corporate Director
      Mr. Shapiro has been a Director of Barrick since 2004.
      Audit Committee

      S.J. Shapiro, Chairman
      D.J. Carty
      P.A. Crossgrove
      R.M. Franklin

      Compensation Committee

      D.J. Carty, O.C.,Chairman
      G.A. Cisneros
      J.B. Harvey
      S.J. Shapiro

      Corporate Governance and Nominating Committee

      R.M. Franklin, Chairman
      H.L. Beck
      D. Moyo

      Corporate Responsibility Committee

      P.A. Crossgrove, O.C., Chairman
      C.W.D. Birchall
      J.B. Harvey
      D. Moyo
      A.W. Regent

      Finance Committee

      C.W.D. Birchall, Chairman
      H.L. Beck
      A. Munk
      N. Rothschild

      Number of Registered Shareholders

      18,547
      Last edited by zomba; 4th March 2012 at 21:26.
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    22. #99
      georgeallen's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd June 2011
      Location : Seattle, WA, USA
      Posts : 2,052
      Rep Power : 0
      Likes Received
      516
      Likes Given
      260

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Mimi namkubali JK na hasa pale aliposema kuwa President Bush alimwambia yeye ni "good man." aliongeza na kusema: unajua hawa watu weupe wakikuambia wewe ni good man basi ujue mambo yataanza kunyooka. misaada kede kede.
      Pasco likes this.

    23. #100
      Mwanajamii's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th March 2008
      Posts : 7,085
      Rep Power : 1810
      Likes Received
      24
      Likes Given
      13

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Raia Mwema
      Pasco

      leo umeleta thread ya maana hebu tujaribu kuzungumzia japo mazuri machache ya Jk. Hakuna binadamu asiye na zuri hata moja

      Mimi nitamkumbuka kwa kutununulia Panton la magogoni - Kigamboni. kabla ya hapo ilikuwa ni mateso.

      Panton kubwa Afrika Mashariki na kati hadi Mwai kibaki alikuwa kuliona alipotembelea Tanzania na akaahidi kuwanunulia wakenya

      Linabeba magari 60 na abiria 2000

      Na sasa ujenzi wa daraja la Kigamboni umeanza
      mkuu umesema maneno mazito sana..

      mimi namshukuru na nitamkumbuka kwa kutujengea chuo kikuu cha Dodoma UDOM na sasa mimi pamoja na bijana wengi ambao sasa tungekuwa machoko raa tunapata degree zetu kwa utulivu kabisa
      Pasco likes this.

    Page 5 of 23 FirstFirst ... 3456715 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...