Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

    Report Post
    Page 4 of 23 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 442
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,862
      Rep Power : 7377
      Likes Received
      6195
      Likes Given
      22551

      Default Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Wanabodi,
      Naangalia TBC Live, Rais Jakaya Kikwete yuko hewani!
      Miongoni wa mazuri ya JK, ni having a good sense of humour, akiongea, huchoki kumsikiliza!.
      Alipokuwa akiongelea kilimo cha ndizi kijijini kwao Msoga, Bagamoyo, akasema wakulima wana bananisha migomba mingi kwenye shina moja, matokeo yake kila mgomba unatoa kichane kimoja au viwili ya vindizi vilivyokondeana!.

      Akasema wanakijiji wale wanalima hivyo kwa sababu hawajui kuwa kama wakiacha mgomba mmoja kwenye shina moja, mgomba huo utatoa mkungu mkubwa wa ndizi, na ndizi zenyewe zitakuwa ni ndizi za shibe kama "Mrisho Mpoto"!. Ukumbi mzima ulizizima kwa vicheko, watu hawana mbavu!.

      Kuwa na 'good sense of humour' ni kipaji na ni miongoni mwa mambo mazuri machache ya rais wetu Jakaya Kikwete, besides good looking!.

      Kwa wale wenye kumbukumbu ya hotuba za Mwalimu, ukiondoa ile hotuba yake ya kutangaza vita, hotuba za Mwalimu, watu walikuwa wanacheka na hutamani amalize kuzungumza!.

      Hii ni thread ya miongoni mwa mazuri ya JK, kama na wewe unalo zuri lolote la JK ambalo unalijua, unaweza kuliweka.

      Kwa vile tunazungumzia mazuri, ningeomba wale ambao hawana zuri lolote la kuzungumzia JK, sio lazima mchangie, wala zuri hili la "good sense of humour", haimaanishi JK sasa ndio rais bora kwa Tanzania, wala haina maana ndio hana mabaya yake!, leo tuzungumzie mazuri yake!

      Angalizo:
      Wanabodi wenzangu, tunajukumu la kujimoderate sisi wenyewe kulinda hadhi ya jukwaa letu, haiwezekana kila siku sisi tukawa ni watu wa kulalamika tuu, au kubonda tuu, mara moja moja kwenye mazuri, pia tutoe sifa pale panapo stahili!.

      Natanguliza Shukrani kwa kunielewa!

      Asanteni!

      Pasco (wa jf)

      Note: Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali ni muumini wa ukweli "seek the truth, and the truth will set you free"!. Kwa wale wanaofikiri Pasco wa jf, ni mshabiki wa CCM, tafuteni thread yangu ya "CCM Imechokwa" !.


      --------------------------------------------
      Hoja Nyingine za Thread ya kibananhukhu iliyounganishwa #148
      Quote By kibananhukhu View Post
      Pamoja na list ya mambo lukuki ambayo wakuu mnamlaumu JK, lakini ni kweli kuwa kuna kitu anafanya siyo kwamba amelele fofofo. Kuna mapungufu pia ni kwa nia njema mnayaainisha kusaidia uboreshaji kazi. Nimefuatilia na kuyaona baadhi ya mazuri ya JK Kama list inavyoainisha, ninaweza kuwa na upungufu kidogo katika takwimu hii itatokana na mimi kutumia kumbukumbu zangu nipo tayari kusahihishwa takwimu. Tupitie mazuri ya JK HAPA CHINI

      1. Mpango wa kuiruhusu bandari (THA) kufanya kazi kwa kuanza na technologia mpya ili dereva tu ndiye awe anakwenda bandarini kupakia mzigo na mengine yote yatamalizwa kwa njia ya mtandao, e-port. Kumbukeni TICTS walikuwa na mkataba mbaya sana kwa miaka 15, na ulirejewa kwa mazingira ya kutatanisha.

      2. Dar tayari nyumba 50 zimeanza kutumia gesi kwa matumizi mbali mbali ya ndani, kama ulaya na kwingineko kwa mara ya kwanza. Mikocheni wameanza jiandaeni kuvuta gesi majumbani kwenu.

      3. Magari yameaanza kutumia gesi japokuwa bado kuna baadhi ya vikwazo kwa wasaidizi wa raisi. Mpango wa JK ilikuwa matuzi ya petroli katika gari yapungue kwa 80%, lkn ukiritimba wetu umesababisha yapungue kwa 55%

      4. Kivuko na daraja kigamboni.

      5. Mradi wa daraja Maragalasi na lami Tabora – Itigi – Kigoma

      6. Ujenzi wa barabara lami kutoka Mombo, Mtibwa turiani, Kilosa, Mikumi na baadaye ifakara, mahenge, Malinyi, Songea. Pia Ifakara, Mlimba hadi Njombe. Usafiri wa songea kupunguza safari kwa masaa 5.

      7. Barabara ya Mafinga, Iringa, Kitonga, Ruaha Mbuyuni, Madaraja mawili mpakani na morogoro imekwishapanuliwa kwa uboro wa hali ya juu. Kipande cha Ipogolo kupandisha kwenda iringa mjini kimepanuliwa sana.

      8. Bara bara ya Iringa Kwenda Dodoma Imekwishaanza

      9. Bara bara ya Tunduma hadi Sumbawanga kuna makandarasi watatu wanashindana kwa ubora wa lami.

      10. Viwanja vya ndege mikoani kuboreshwa.

      11. Karekebisha mkataba wa Songas, ulikuwa hauruhusu mtu meingine yetote awaye kujenga tena bomba la gesi. Sasahivi wakuu mnaruhusiwa kujenga mabomba ya gesi kutoka Kusini.

      12. Mkataba wa wachina na serikali kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi dar ili kuzalisha MG 2900 za umeme dar.

      13. Barabara Dodoma, Manyara lami.

      14. Ujenzi reli kutoka Tanga, Musoma, Uganda.

      15. Ujenzi bandari, Tanga, Mtwara na Babamoyo

      16. Uwanja wa Ndege Terminal two wajengwa.

      17. Maeneo ya Umwagiliaji maji, hekari 20,000 zimejengwa na lengo ni ekari 1milioni.

      18. Kilimo kwanza mashamba darasa na ongezeko la mavuno kwa ekari.

      19. Tanzania ni ya kwanza kwa export afrika masharik na kati

      20. Mradi wa makaa ya Mawe Mchuchuma na katewaka liganga kuzalisha MGW za kutosha nchi nzima

      21. Mradi wa machimbo mgodi wa chuma Liganga, uzalishaji wa Titanium, Vanadium, Fe kwa ajili ya utengenezaji nondo, malighafi ya mabati, vyuma vya kujengea madaraja na maghorofa, kuweka pembezoni mwa mabarabara kuzalishwa nchini. Viwanda vya kutengeneza vifaa vya ujenzi wa meli, ndege, na magari kujengwa nchini.

      22. Machimbo ya makaa yam awe Ngaka Mbinga Ruvuma, uwezo Kuzalisha pia umeme MG 400.

      23. Hospitali upasuaji moyo kwa mara ya kwanza Tanzania.

      24. Hospitali kubwa mingoni mwa zitakazoheshimika kujengwa Tanzania na Appollo ya India. Maradhi yote kutibiwa Tanzania.

      25. Uboreshaji shirika la nyumba NHC, Baadhi ya watanzania kunufaika na mikopo ya nyumba na nyumba kuanza kujengwa kwa spidi kali.

      26. Ujenzi wa barabara nane Dar hadi chalinze.

      27. Ufumuaji na ujenzi wa reli ya kati dar, hadi kigoma, mwanza, mpanda, Rwanda na Burundi.

      28. Ubareshaji maabara shule za kata ($ 90Milioni)

      29. Idadi ya walimu kwaajili ya shule za kata na nyinginezo kuanzia muda mfupi ujao, walimu elfu 40 kuhitimu kila mwaka.

      30. Baadhi ya shule nyingi binafsi zimeanza kudorola au kufungwa kabisha, wengi wamejiunga na shule za kata na ubora unapanda japo kwa spidi ndogo.

      31. Idadi kubwa ya wanafunzi vyuo vikuu, Udom uwezo elfu 40, SAUT elfu 15, UDSM Elfu 15, Ruco elf 2.5, Mkwawa elfu 2.5 Tumaini elfu 2, Open University elfu 20 nk.

      32. Wafanya biashara wamepewa kipau mbele term ya JK, Wengi husafiri na Mheshimiwa Raisi kutafuta na kupata fursa za biashara nje.

      33. Uhuru wa Vyombo vya habari, waandishi wanafanya mambo kwa uhuru ambao wasingelithubutu enzi ya Mwalimu, Mwinyi wala Mkapa. Hata baadhi ya ninyi wakuu, mnaruhusuwa kutoa mawazo yenu japo wengine wanatukana matusi ya nguoni lakini JK anavumilia sana.

      34. Amegundua fitna nyingi sana serikalini, majungu, uongo na sasa hivi anakua mwangalifu sana katika maamuzi na inalazimika kuonekana kana kwamba hana maamuzi ili awe na subira. (Ukiwa na hasiri usifanye maamuzi, ahirisha upate busara)

      35. Makampuni ya madini, yamekupali kuanza kulapa 30% kutoka faida zitakazo patikana kuanzia 2012.

      36. Wapinzani wameanza kumwelewa na kumsifia kwa yale anayoyafanya vizuri.

      37. Mnaweza ongeza list nyingine ili nije baadaye na listi ya faida za kiuchumi kwa taarifa tu, inflation inachangiwa na gharama za chakula kwa 16%.

      Kuna mambo madogo ya kiufundi yakirekebishwa inflation inapashwa iwe 8% single digit. Mfano mahindi yanaoza Ruvuma, Iringa, na Sumbawanga yangeweza kutoa mchango katika kupunguza gharama za chakula na mfumuko wa bei ukashuka.Mengine mengi nitaongeza baadaye. Nadhani kwa faida ya wakuu wangu, nitajitahidi kufuatilia pia ilani yake ili nilinganishe na hayo hapo juu. Hata hivyo, ni ukweli kwamba kwa upanda wa barabara tu, miaka 50 tangu uhuru lami ilifikia km 6000, JK Pekee ameweka mikataba ya lami km 11,000.

      Kuna vitu anafanya JK.
      Last edited by Viwango; 6th March 2012 at 11:52. Reason: Adding points of merged thread


    2. #61
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,203
      Rep Power : 12279
      Likes Received
      6062
      Likes Given
      6927

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By zomba View Post
      This is exactly what is happening now, tunasikia shule hazina mashimo ya vyoo na hao wanakijiji na mabwana afya wa wilaya wanaruhusu watoto wanakwenda shule bila vyoo. Wakati hao hao watu wana pesa za kuzuia vipindupindu, wanazipeleka wapi? utawakuta wanakwenda kwenye restaurants na kukusanya rushwa badala ya kwenda kuweka mikakati watoto wakapata vyoo.

      Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Kikwete kawawekea mashule, basi hata mashimo ya vyoo mnashindwa? hata madawati? hata nyumba za walimu? mpaka aje Kikwete kuwahamasisha?

      Wabunge kazi yao kutafuta waandishi wa habari na kwenda nao kutoa handouts ili waonekane wanafanya la maana. Sijaona hata mmoja akiwakusanya wananchi na kuwa nao bega kwa bega katika mikakati ya kujitengenezea mashimo ya vyoo wala madawati wala nyumba za walimu, utasikia kapeleka bati alizopewa na barick jimboni kwake. What a way.

      Hakuna hata mbunge mmoja anaekuja na mkakati wa kusema ntazifanya shule zangu ziwe mfano wa kuigwa kwa kuwafanya wanachi wa jimbo langu waziendeshe kwa ufanisi mkubwa kabisa.
      Kamanda you are very right

      ila sasa mimi hili naligeuza kuwa baya la JK....

      wewe ni rais, ukiamua wananchi wote watavaa uniform kwenda kazini na jumamosi watadeki barabara na mataulo!! Unafanya nini na hilo rungu ulilopewa??? unasafiri, unapunzika, unachekacheka, ukishaona pametulia unakuja mbio bila soni unaanza kusema "ile aisee, nilisaini kwa presha tu" au hawa jamaa balaa hawa, wamenichemsha kweli hadi nikaamua kwenda kusherehekea chama kule chini, au naskia kuna stafu kafiwa hapo chini, haijalishi ngoja na mimi niende msibani (bila kujua uwepo wako kwenye misiba mingine ni inconvenience kwa kila mtu, si ajabu hadi maiti yenyewe inapata shida kutokana na ulinzi na protocols

      IF I HAD 24 HOURS, NINGEBEBA BAKORA YANGU NA KUHAKIKISHA WANANCHI, WATENDAJI, WANASIASA NA VIONGOZI WANATIMIZA WAJIBU... KWA SASA KILA MTU ANARELAX KWANI WANAJUA KIKINUKA, MKULU HUWA ANAPISHIA MBALI

      Kwangu mimi mtu anayemchekea nyani na kuyavua mabua siwezi kumuita charming au mtu wa watu, ntasema huyo muuaji na ana lake jambo, killing while smilling!!
      Pasco likes this.
      ....Time is the wisest counselor !!!

    3. #62
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,203
      Rep Power : 12279
      Likes Received
      6062
      Likes Given
      6927

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By zomba View Post
      Kikwete kafanya mazuri mengi sana.

      Ningependa na ningefurahi Kikwete angechaguwa mikoa miwili tu iliyokuwa mwisho kimaendeleo akamleta mzungu mmoja kila mkoa kuwa RC na kila wilaya za huo mkoa Mzungu mmoja kuwa DC na mmoja kuwa DD. na mmoja kuwa DFD, Halafu uone mabadiliko katika hiyo mikoa miwili. Wizi ungekwisha, rushwa ingekwisha na mikoa ingekuwa inatamanika kwa miaka 3 tu na kwa hiyo miaka mitatu hiyo mikoa itaondoka kuwa ya mwisho na kuwa ya kwanza kwa maendeleo.

      Mzungu = wa Mungu

      Afrika (derived from Afri t) = wa shetani.
      hivi kuna mtu kazungumzia race hapa?? umeanza vyema sasa na wewe unahamia kulekule...
      Pasco likes this.
      ....Time is the wisest counselor !!!

    4. #63
      Njowepo's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 26th February 2008
      Location : Santiago
      Posts : 7,779
      Rep Power : 22095
      Likes Received
      1044
      Likes Given
      857

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Nitamkumbuka kwa kuwa kimya hata kunakuwa na burning issue!
      TIMING and Pasco like this.
      WB Tanzania lead economist Jacques Morisset said the GDP doubled in 10 years, but it has failed to produce any significant decline in poverty levels.

    5. #64
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,045
      Rep Power : 14670
      Likes Received
      2954
      Likes Given
      2093

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By paulss View Post
      Zomba nalazimika kukujibu haliyakuwa tupo nje ya topic. kumbe tatizo sio JK tatizo ni sisi kuwa Waafrika, maana hata ukimuweka Slaa bado sio mzungu, is that wahat you means? jitambue mkuu
      That is exactly what I mean. Slaa kafanya nini katika maisha yake ambacho anaweza kutuonesha kuwa hapa nimefanya hiki na hiki na hiki, tuone kuwa ni mfano wa kuigwa, sana sana namsikia akihubiri tu, talkers are never doers, kama nyerere, alikuwa a good talker but never a good doer. Lets be honest, mambo amabayo tulikuwa tuyafanye miaka 50 nyuma ndio anayafanya leo Kikwete. Kilikuwa kinatushinda nini kujenga mashule? kilikuwa knatushinda nini kujenga mabarabara? kilikuwa kinatushinda nini kuruhusu kampuni zenye ujuzi zije kutafuta mafuta? exploration ya mafuta ilianza kufanywa na waingereza 1950s Nyerere alipopata madaraka akasitisha. Why?
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    6. #65
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,203
      Rep Power : 12279
      Likes Received
      6062
      Likes Given
      6927

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By paulss View Post
      Zomba nalazimika kukujibu haliyakuwa tupo nje ya topic. kumbe tatizo sio JK tatizo ni sisi kuwa Waafrika, maana hata ukimuweka Slaa bado sio mzungu, is that wahat you means? jitambue mkuu
      siamini kama slaa atafanya afanyavyo JK, hata mkapa hakufanya hivyo... kiongozi anatakiwa kusimama na kukemea tabia tegemezi, na aponde wabunge wa handouts

      the dude is just enjoying ignorance ya maskini wasio na kitu na umbumbu wao
      Jasusi and Pasco like this.
      ....Time is the wisest counselor !!!


    7. #66
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,045
      Rep Power : 14670
      Likes Received
      2954
      Likes Given
      2093

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By MTM View Post
      hivi kuna mtu kazungumzia race hapa?? umeanza vyema sasa na wewe unahamia kulekule...
      Ukiisoma vizuri post yangu inaonesha wazi kwanini nimebainisha hizo race, sasa unataka tuongee kama majuha, bila kutoa wazo na kuainisha kwanini tumetoa hilo wazo?

      Na hapo nikimaanisha kuwa bila kutumia hawa wa mungu sisi wa afriti hatuwezi kitu, si unaona hata gas na mafuta wanakuja wao kutuonesha iko wapi. Hoteli nzuri za mbugani zinapata tuzo kuwa ni hoteli bora katika dunia ni kwa kuwa zinaendeshwa na hawa wa mungu. Na Kikwete kafanya kazi kubwa sana kuwaomba waje, kila akisafiri anawaaambia waje kuwekeza, na matunda yake tunayaona, gas kedekede, hoteli za kitalii zinapata tuzo za dunia.

      Sasa tunamuomba awalete ma "administrators" wa kizungu awape mikoa miwili, halafu tuone hawa wa mungu na sisi nani zaidi. Bila hivyo mawee. Tutaedelea kuona kampuni za wazungu ndio nzuri na zinalipa vizuri, sasa kwa nini tusihamishie kutoka kampuni kuja serikali zinazoendeshwa na wa mungu.
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    8. #67
      The Boss's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th August 2009
      Location : DARESALAAM
      Posts : 18,507
      Rep Power : 21688
      Likes Received
      13812
      Likes Given
      18061

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      hata mazuri ya Kikwete yamegeuka na kuwa kero na mabaya

      ni sawa na mchezaji mtaalam wa chenga lakini hatoi pasi kwa wenzie
      wala kusikiliza kocha
      mwisho huwa mzigo kwa timu
      pamoja na chenga zake
      Jasusi, TIMING, Ndahani and 1 others like this.
      Watch your thoughts,They become words, Watch your words, They become deeds, Watch your deeds, They become habits, Watch your habits, They become character, Watch your character, It becomes your destiny!

    9. #68
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,045
      Rep Power : 14670
      Likes Received
      2954
      Likes Given
      2093

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Njowepo View Post
      Nitamkumbuka kwa kuwa kimya hata kunakuwa na burning issue!
      Kwi kwi kwi, teh teh teh, sasa burning issue inayoweza kutatuliwa na walio chini yake kwanini ifikie mpaka yeye aingilie? ndio hayo mtamwambia mpaka vyoo vya shue aje kuwachimbia wakati mnaweza kuwafanyia maandaamano madiwani wenu mpaka wahahakikishe vyoo vinapatikana, tenaa vya kisasa. Ni jambo dogo sana. Shule isiyokuwa na choo mnakutana na madiwani, mnawapa muda wakishindwa mnawang'oa. Wataokuja lazima waweke vyoo, sasa nyinyi mnangoja Kikwete aje mumshtakie, Mheshimiwa Rais tumejengewa shule lakini vyoo vilisahauliwa, ns bado mnaacha injinia wa wilaya anadunda mitaani.
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    10. #69
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,045
      Rep Power : 14670
      Likes Received
      2954
      Likes Given
      2093

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By The Boss View Post
      hata mazuri ya Kikwete yamegeuka na kuwa kero na mabaya

      ni sawa na mchezaji mtaalam wa chenga lakini hatoi pasi kwa wenzie
      wala kusikiliza kocha
      mwisho huwa mzigo kwa timu
      pamoja na chenga zake
      Mawazo yako na avatar yako ni vitu tofauti.
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    11. #70
      Gwalihenzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 2,490
      Rep Power : 909
      Likes Received
      648
      Likes Given
      413

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Pasco View Post
      Mkuu MTM, human beings are not static, we are dynamic, we change with time!. Some us changes for the better, some changes for the worse!. Mimi naamini nilijikwaa tuu mahali nikaanguka, nitaamka, nitajifuta vumbi na kusimama tena kuendelea na safari for the better!.
      Ingependeza kama ungeiweka hivi 'some of us change for.................
      TIMING and Pasco like this.

    12. #71
      mama D's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2010
      Posts : 1,524
      Rep Power : 743
      Likes Received
      400
      Likes Given
      1326

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      mwandosya, mwakyembe, babu seya...... mmmh
      Pasco likes this.
      Daily News halisomwi tandale kwa mtogole - MPOKI

    13. #72
      MAMMAMIA's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Location : Near You
      Posts : 3,794
      Rep Power : 3261
      Likes Received
      1496
      Likes Given
      1206

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Pasco View Post
      Kwa hili lazima tumpongeze JK, he is very considerate kwa wenzetu hawa!, na hata kama unaambiwa "asante", kwa nini usiwe ni mtu wa kupokea shukran!.
      Pia sifa nyingine kubwa ya JK ni mtu wa shukrani anayekumbuka fadhila!. Hebu waangalie watu mbalimbali waliomsaidia kufika hapo alipo jinsi alivyowakumbuka!.
      JK ni mwema jamani, na kabla hajamaliza kipindi chake hiki, kuna watu mtasikia wametupwa balozi hizi na zile kabla hajaondoka!. Huu sio wema?.
      Quote By Pasco View Post
      Mtazamo, kitendo cha turning weakness into streghth ni uwezo mkubwa, hivyo JK ana uwezo mkubwa transformation. Nilimsikiliza sana pale alipozungukia mawizara, he had a good vision na good plans ila watendaji wake ndio wamemlet down!. He is so kind, he can't just fire anybody!. Hata akikutana na Mama Nyoni, atamwambia sorry ni Pinda ila tulia kidogo watu wasahau nitakupeleka ubalozini nchi moja nzuri, ukatulie!, nikishakupeleka pia nitakua naitembelea nchi hiyo mara kwa mara!.
      Quote By only83 View Post
      Zuri lingine ni kulinda marafiki wake pale anapohisi kuwa wanafanya madudu..hii ni moja ya sifa nzuri ya mkuu wa kaya,ana uwezo mkubwa wa kukulinda rafiki yake hata kama unafanya madudu.Namkubali kwa hili.
      [Hizo tatu hapo juu nimeziweka pamoja kwa sababu zinahusiana] Hili la kulinda marafiki tunalisema ni zuri kweli au kwa kejeli? Tukumbuke tu kuwa haya mambo ya urafiki, ya udugu na kulipa fadhila binafsi kwa kutumia mali ya umma ndiyo masuala ambayo yamekuwa yakiitafuna TZ miaka nenda miaka rudi. Ni sababu hiyo ya kulipa fadhila kwa waliomfadhili ndio maana akawa amezungukwa na watendaji wabovu na anashindwa kuchukua maamuzi magumu kwa sababu "mfadhiliwa [ni sawa na] mtumwa [wa aliyemfadhili].

      Quote By zomba View Post
      Shule za Sekondari nyingi wakati wa Kikwete, kuliko za wakati wa marais wote waliomtangulia pamoja na za wakoloni, zote ukichanganya hazifikii hata nusu ya shule alizojenga Kikwete kwa miaka 5 tu ya mwanzo.
      Quote By Jasusi View Post
      Kabla hujarudi jiandae kutuambia hizo shule zina waalimu wa hadhi gani. Kujenga shule si kuweka majengo tu bila madawati. Pia usisahau kutupa habari jinsi alivyofanikiwa kumaliza tatizo la umeme.
      Quote By zomba View Post
      Nini ambacho hujakielewa?

      Mashule yanayokosa madawati utakuta yote yapo vijijini na utakuta vijiji hivyo hivyo vinakata miti na kuuza mbao na kuuza kuni badala ya kujitengenezea madawati ya shule zao, wanangoja handouts na au kufanyiwa.

      Kikwete kajenga mashule kwa kuwahamasisha hao hao kwenye kata zao na sasa ilikuwa wakati muafaka hao kwenye kata kuweka mikakati ya kujisaidia kuziendesha kwa ufanisi, kama kukusanyika na kujitengenezea madawati japo mawili au matatu kila wiki. Leo baada ya miaka 6 kungekuwa hakuna shida a madawati. Inabidi watanzania wajuwe kujituma wasingoje kutumikiwa tu.
      [Na hizo hapo juu nimeziweka pamoja kwa sababu tunazungumzia mada moja] Kama kitomeo tu, hapa ninakumbuka riwaya ya Shaaban Robert ya Kusadikika, pale wananchi wa nchi fulani walipotakiwa kujenga barabara pana wakadai zina kazi gani wakati mguu wa binadamu hauzi upana wa inchi 7".

      Tukubali ukweli kuwa rushwa na kukosa uwajibikaji ndio unaotuangusha. Badala ya kutuma rasilimali na juhudi zetu, tunasubiri kila kitu kifanywe na Kikwete (serikali). Hivi leo imekuwa ada, sio kusafisha mtaro wa maji machafu bali tunatupa takataka na mifuko ya plastiki huku tunasubiri serikali kuu ije kutusafishia.

      ANGALIZO KWA WATANZANIA: Tanzania haitaendelea kwa kubadilisha viongozi, hata tupate kiongozi mtendaji mwenye kila sifa ikiwa sisi wenyewe hatukubadilika, tutabaki kupiga kwata la mdundiko au mbwakachoka, hatua kumi mbele, ishirini nyuma.
      zomba, TIMING and Pasco like this.
      "JF - SAUTI YA WASIO NA SAUTI ............ na wapayukaji"

    14. #73
      Rock City's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2012
      Posts : 657
      Rep Power : 582
      Likes Received
      208
      Likes Given
      106

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Binafsi nitamkumbuka kwa,

      • Kuanza kwa vitendo ujenzi wa barabara za magharibi na kuziunganisha tangu uhuru.
      • Barabara ya Nzega-TBR.
      • Urambo-TBR
      • Kuinyenyua kanda ya magharibi hususan kumteua Pinda anayeunyenyua mkoa wa Rukwa/Katavi.
      • Kupendelea wanawake ktk nafasi nyingi (hata kama hawawezi)
      • Hajionyeshi ni nani adui wake, anacheka na wote na anateta na wote.
      • Amenyenyua hali ya mishahara ya askari nchini.
      • Amewasaidia wakazi wa Dar kila wanapokumbwa na dhoruba za mabomu, mafuriko.
      • Anapita mitandaoni na kujumuika nasi.
      • Amezuia ardhi ya Tanzania kutumiwa na EAC kama sehemu ya maridhiano.
      • Ni rais wa kipekee kuhudhuria misiba na mazishi kila apatapo taarifa, na hata awepo nje ya nchi kwa baadhi ya nyakati hurejea.
      • Ndie rais mwenye ulinzi mkali zaidi kulinganisha na waliomtangulia.
      • Amekuwa fair kuzingatia gender na RIKA ktk uteuzi wa nafasi nyingi serikalini/chama.
      TIMING and Pasco like this.

    15. #74
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,203
      Rep Power : 12279
      Likes Received
      6062
      Likes Given
      6927

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By zomba View Post
      Kwi kwi kwi, teh teh teh, sasa burning issue inayoweza kutatuliwa na walio chini yake kwanini ifikie mpaka yeye aingilie? ndio hayo mtamwambia mpaka vyoo vya shue aje kuwachimbia wakati mnaweza kuwafanyia maandaamano madiwani wenu mpaka wahahakikishe vyoo vinapatikana, tenaa vya kisasa. Ni jambo dogo sana. Shule isiyokuwa na choo mnakutana na madiwani, mnawapa muda wakishindwa mnawang'oa. Wataokuja lazima waweke vyoo, sasa nyinyi mnangoja Kikwete aje mumshtakie, Mheshimiwa Rais tumejengewa shule lakini vyoo vilisahauliwa, ns bado mnaacha injinia wa wilaya anadunda mitaani.
      kama hawatatui na yeye anakaa kimya --- inakuaje?
      Pasco likes this.
      ....Time is the wisest counselor !!!

    16. #75
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,045
      Rep Power : 14670
      Likes Received
      2954
      Likes Given
      2093

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By MTM View Post
      Nimekusoma Pasco but i am worried unaposema some of us change for the better, and some change for worse... (knowing if you are better or worse, could be a long term process, requiring external observation as well as a few notable milestones between the timelines) it is difficult to say if you are heading in the right direction without external views, IMO

      But good luck in your endeavor but take it from me; something ahs changed and not to the good for you.... you have lost that neutrality and i even now see how opportunistic your are by tring to use JF views kwenye vipindi vyako unavyotaka ku-air. It is really bad when you think you are smart and can play with people philosophy thinking that it can always go your way

      If you want to succeed, dont be a puppet! but if you want a joyride, then you can be one... My daughter has a toy, it closes its eyes when put asleep and opens the eyes whenever kept in upright position; and she loves it!!!

      I AM SORRY BUT I AM WORRIED NA HIYO JOYRIDE UNAYOTAKA KUENJOY KWA MIGONGO YA JF

      Goodbye and Goodluck
      Hivi huyu MTM ndiye Mike Mckee? ni nje tu ya mada, lakini ningependa kujuwa, maana hii sentensi ya mwisho ina masimango, na masimango hayawezi kutolewa na mlowezi tu, hii ni kujiamini na kuona kuwa amevumbuwa gurudumu na hapendi wenzie waliboreshe na kusafiria.

      Duhh! roho na fikra hizi unazipata Afrika tu (wa afriti kwa wa mungu huzioni hizi).
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    17. #76
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,045
      Rep Power : 14670
      Likes Received
      2954
      Likes Given
      2093

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By MTM View Post
      kama hawatatui na yeye anakaa kimya --- inakuaje?
      Ana chukuwa bomba anakwenda hollywood kutafuta watalii na wawekezaji wataokuja kuweka mahoteli mazuri, kuja kututafutia gas na kuja kutuonesha watu wanavyoishi duniani. Nyie anawaacha kama mlivyo. "mzowea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi".
      Pasco likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    18. #77
      Ngongo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th September 2008
      Location : Mlima Meru
      Posts : 4,965
      Rep Power : 6858
      Likes Received
      2407
      Likes Given
      3170

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Nitamkumbuka Rais Kikwete kama ifuatavyo.

      [1] Ni Rais pekee dunia ambaye amehudhuria misiba mingi ya watanzania wa kawaida.

      [2] Akianzisha jambo lake analisimamia vizuri ingawa anashindwa kuimazia vizuri Kujivua gamba,Taifa Stars,Umeme,shirika la ndege na mikataba ya madini.

      [3] Uhuru wa habari umepanuka sana chini ya uongozi wake.

      [4] Hajaongeza mke baada ya kupata madaraka

      [5] Msimamo wake kuelekea EAC hasa suala la ardhi ya Tanzania ni jambo lingine zuri.

      [6] Mchakato wa katiba hasa baada ya kukubali kukutana na vyama vya siasa na kukubali kuchukua baadhi ya hoja zao ni jambo kubwa kuliko yote.Kikwete anaweza kutuachia katiba bora,kwangu mimi katiba bora yawezakuwa goli kubwa na muhimu kuliko ujenzi wa barabara,machinga Complex,daraja la kigamboni na nk katiba bora ndiyo mambo yote hakuna kilicho baro kuliko katiba nzuri inayozingatia haki za wananchi na kuhakikisha rasilimali za taifa zinalindwa ipasavyo na kulinufaisha tiafa.
      Ndahani and Pasco like this.

    19. #78
      Gwalihenzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 2,490
      Rep Power : 909
      Likes Received
      648
      Likes Given
      413

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Pasco View Post
      Mkuu MTM, thanks for being bold to call a spade a spade!.

      If you were doing something before and you left it for something else which is more paying than what you were getting, yuo simply justfy the move!.

      After a period of time you realise you were a better man before than what you are now, you decide to abandon what you do now and get set to do what you used to be, and plans ahead to do it in a better way!. In a planning stage you just say, channging for the better!.

      The issue of neutrality is a bone of contentions. You are in a jungle struggling for existance, and survival is only for the fittest!. In order to survive one might find himself doing the things he should never have done if that is the one and only way to survive!. I'm survivor!.

      Most preachers who claim to be men if God, are taking a joy ride by playing with peoples mind!. I'll also has to take a joy ride somewhere somehow but I will not play your mind away!. The use of jf mind was not a means but only a way!. As long as I have a means, I can always find my way out not necesarly through jf!. Hivyo don't worry kuwa ninataka kupanda juu kupitia mgongo wa jf!. The plan was to just to scratch my back and I'll scratch yours!. Mission abandoned!. Najipanga upya nitoke kivingine without jf!.

      Hoja ya a puppet or not, the end will justfy the means!.

      Thanks again Mkuu MTM,
      Back to mazuri ya JK!
      Pasco, this is very crude! so you are ready to rape even your own daughter for the sake of selfish survival!
      Pasco likes this.

    20. #79
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,045
      Rep Power : 14670
      Likes Received
      2954
      Likes Given
      2093

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Gwalihenzi View Post
      Pasco, this is very crude! so you are ready to rape even your own daughter for the sake of selfish survival!
      What has survival got to do with raping one's daughter? be realistic. Who is surviving by raping his daughter? what a tinker.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    21. #80
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,203
      Rep Power : 12279
      Likes Received
      6062
      Likes Given
      6927

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By zomba View Post
      Ana chukuwa bomba anakwenda hollywood kutafuta watalii na wawekezaji wataokuja kuweka mahoteli mazuri, kuja kututafutia gas na kuja kutuonesha watu wanavyoishi duniani. Nyie anawaacha kama mlivyo. "mzowea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi".
      NILIKWAMBIA ACHA GANJA ... ONA SASA UMEMTETEA WEEEE MWISHO UNAMMALIZA KABISA... WE AFRI WAHED!!! LOL

      BTW, MIKE MCKEE NDIO NANI??name calling
      Pasco likes this.
      ....Time is the wisest counselor !!!

    Page 4 of 23 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...