Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

    Report Post
    Page 2 of 23 FirstFirst 123412 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 442
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Wanabodi,
      Naangalia TBC Live, Rais Jakaya Kikwete yuko hewani!
      Miongoni wa mazuri ya JK, ni having a good sense of humour, akiongea, huchoki kumsikiliza!.
      Alipokuwa akiongelea kilimo cha ndizi kijijini kwao Msoga, Bagamoyo, akasema wakulima wana bananisha migomba mingi kwenye shina moja, matokeo yake kila mgomba unatoa kichane kimoja au viwili ya vindizi vilivyokondeana!.

      Akasema wanakijiji wale wanalima hivyo kwa sababu hawajui kuwa kama wakiacha mgomba mmoja kwenye shina moja, mgomba huo utatoa mkungu mkubwa wa ndizi, na ndizi zenyewe zitakuwa ni ndizi za shibe kama "Mrisho Mpoto"!. Ukumbi mzima ulizizima kwa vicheko, watu hawana mbavu!.

      Kuwa na 'good sense of humour' ni kipaji na ni miongoni mwa mambo mazuri machache ya rais wetu Jakaya Kikwete, besides good looking!.

      Kwa wale wenye kumbukumbu ya hotuba za Mwalimu, ukiondoa ile hotuba yake ya kutangaza vita, hotuba za Mwalimu, watu walikuwa wanacheka na hutamani amalize kuzungumza!.

      Hii ni thread ya miongoni mwa mazuri ya JK, kama na wewe unalo zuri lolote la JK ambalo unalijua, unaweza kuliweka.

      Kwa vile tunazungumzia mazuri, ningeomba wale ambao hawana zuri lolote la kuzungumzia JK, sio lazima mchangie, wala zuri hili la "good sense of humour", haimaanishi JK sasa ndio rais bora kwa Tanzania, wala haina maana ndio hana mabaya yake!, leo tuzungumzie mazuri yake!

      Angalizo:
      Wanabodi wenzangu, tunajukumu la kujimoderate sisi wenyewe kulinda hadhi ya jukwaa letu, haiwezekana kila siku sisi tukawa ni watu wa kulalamika tuu, au kubonda tuu, mara moja moja kwenye mazuri, pia tutoe sifa pale panapo stahili!.

      Natanguliza Shukrani kwa kunielewa!

      Asanteni!

      Pasco (wa jf)

      Note: Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali ni muumini wa ukweli "seek the truth, and the truth will set you free"!. Kwa wale wanaofikiri Pasco wa jf, ni mshabiki wa CCM, tafuteni thread yangu ya "CCM Imechokwa" !.

      --------------------------------------------
      Hoja Nyingine za Thread ya kibananhukhu iliyounganishwa #148
      Quote By kibananhukhu
      Pamoja na list ya mambo lukuki ambayo wakuu mnamlaumu JK, lakini ni kweli kuwa kuna kitu anafanya siyo kwamba amelele fofofo. Kuna mapungufu pia ni kwa nia njema mnayaainisha kusaidia uboreshaji kazi. Nimefuatilia na kuyaona baadhi ya mazuri ya JK Kama list inavyoainisha, ninaweza kuwa na upungufu kidogo katika takwimu hii itatokana na mimi kutumia kumbukumbu zangu nipo tayari kusahihishwa takwimu. Tupitie mazuri ya JK HAPA CHINI

      1. Mpango wa kuiruhusu bandari (THA) kufanya kazi kwa kuanza na technologia mpya ili dereva tu ndiye awe anakwenda bandarini kupakia mzigo na mengine yote yatamalizwa kwa njia ya mtandao, e-port. Kumbukeni TICTS walikuwa na mkataba mbaya sana kwa miaka 15, na ulirejewa kwa mazingira ya kutatanisha.

      2. Dar tayari nyumba 50 zimeanza kutumia gesi kwa matumizi mbali mbali ya ndani, kama ulaya na kwingineko kwa mara ya kwanza. Mikocheni wameanza jiandaeni kuvuta gesi majumbani kwenu.

      3. Magari yameaanza kutumia gesi japokuwa bado kuna baadhi ya vikwazo kwa wasaidizi wa raisi. Mpango wa JK ilikuwa matuzi ya petroli katika gari yapungue kwa 80%, lkn ukiritimba wetu umesababisha yapungue kwa 55%

      4. Kivuko na daraja kigamboni.

      5. Mradi wa daraja Maragalasi na lami Tabora – Itigi – Kigoma

      6. Ujenzi wa barabara lami kutoka Mombo, Mtibwa turiani, Kilosa, Mikumi na baadaye ifakara, mahenge, Malinyi, Songea. Pia Ifakara, Mlimba hadi Njombe. Usafiri wa songea kupunguza safari kwa masaa 5.

      7. Barabara ya Mafinga, Iringa, Kitonga, Ruaha Mbuyuni, Madaraja mawili mpakani na morogoro imekwishapanuliwa kwa uboro wa hali ya juu. Kipande cha Ipogolo kupandisha kwenda iringa mjini kimepanuliwa sana.

      8. Bara bara ya Iringa Kwenda Dodoma Imekwishaanza

      9. Bara bara ya Tunduma hadi Sumbawanga kuna makandarasi watatu wanashindana kwa ubora wa lami.

      10. Viwanja vya ndege mikoani kuboreshwa.

      11. Karekebisha mkataba wa Songas, ulikuwa hauruhusu mtu meingine yetote awaye kujenga tena bomba la gesi. Sasahivi wakuu mnaruhusiwa kujenga mabomba ya gesi kutoka Kusini.

      12. Mkataba wa wachina na serikali kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi dar ili kuzalisha MG 2900 za umeme dar.

      13. Barabara Dodoma, Manyara lami.

      14. Ujenzi reli kutoka Tanga, Musoma, Uganda.

      15. Ujenzi bandari, Tanga, Mtwara na Babamoyo

      16. Uwanja wa Ndege Terminal two wajengwa.

      17. Maeneo ya Umwagiliaji maji, hekari 20,000 zimejengwa na lengo ni ekari 1milioni.

      18. Kilimo kwanza mashamba darasa na ongezeko la mavuno kwa ekari.

      19. Tanzania ni ya kwanza kwa export afrika masharik na kati

      20. Mradi wa makaa ya Mawe Mchuchuma na katewaka liganga kuzalisha MGW za kutosha nchi nzima

      21. Mradi wa machimbo mgodi wa chuma Liganga, uzalishaji wa Titanium, Vanadium, Fe kwa ajili ya utengenezaji nondo, malighafi ya mabati, vyuma vya kujengea madaraja na maghorofa, kuweka pembezoni mwa mabarabara kuzalishwa nchini. Viwanda vya kutengeneza vifaa vya ujenzi wa meli, ndege, na magari kujengwa nchini.

      22. Machimbo ya makaa yam awe Ngaka Mbinga Ruvuma, uwezo Kuzalisha pia umeme MG 400.

      23. Hospitali upasuaji moyo kwa mara ya kwanza Tanzania.

      24. Hospitali kubwa mingoni mwa zitakazoheshimika kujengwa Tanzania na Appollo ya India. Maradhi yote kutibiwa Tanzania.

      25. Uboreshaji shirika la nyumba NHC, Baadhi ya watanzania kunufaika na mikopo ya nyumba na nyumba kuanza kujengwa kwa spidi kali.

      26. Ujenzi wa barabara nane Dar hadi chalinze.

      27. Ufumuaji na ujenzi wa reli ya kati dar, hadi kigoma, mwanza, mpanda, Rwanda na Burundi.

      28. Ubareshaji maabara shule za kata ($ 90Milioni)

      29. Idadi ya walimu kwaajili ya shule za kata na nyinginezo kuanzia muda mfupi ujao, walimu elfu 40 kuhitimu kila mwaka.

      30. Baadhi ya shule nyingi binafsi zimeanza kudorola au kufungwa kabisha, wengi wamejiunga na shule za kata na ubora unapanda japo kwa spidi ndogo.

      31. Idadi kubwa ya wanafunzi vyuo vikuu, Udom uwezo elfu 40, SAUT elfu 15, UDSM Elfu 15, Ruco elf 2.5, Mkwawa elfu 2.5 Tumaini elfu 2, Open University elfu 20 nk.

      32. Wafanya biashara wamepewa kipau mbele term ya JK, Wengi husafiri na Mheshimiwa Raisi kutafuta na kupata fursa za biashara nje.

      33. Uhuru wa Vyombo vya habari, waandishi wanafanya mambo kwa uhuru ambao wasingelithubutu enzi ya Mwalimu, Mwinyi wala Mkapa. Hata baadhi ya ninyi wakuu, mnaruhusuwa kutoa mawazo yenu japo wengine wanatukana matusi ya nguoni lakini JK anavumilia sana.

      34. Amegundua fitna nyingi sana serikalini, majungu, uongo na sasa hivi anakua mwangalifu sana katika maamuzi na inalazimika kuonekana kana kwamba hana maamuzi ili awe na subira. (Ukiwa na hasiri usifanye maamuzi, ahirisha upate busara)

      35. Makampuni ya madini, yamekupali kuanza kulapa 30% kutoka faida zitakazo patikana kuanzia 2012.

      36. Wapinzani wameanza kumwelewa na kumsifia kwa yale anayoyafanya vizuri.

      37. Mnaweza ongeza list nyingine ili nije baadaye na listi ya faida za kiuchumi kwa taarifa tu, inflation inachangiwa na gharama za chakula kwa 16%.

      Kuna mambo madogo ya kiufundi yakirekebishwa inflation inapashwa iwe 8% single digit. Mfano mahindi yanaoza Ruvuma, Iringa, na Sumbawanga yangeweza kutoa mchango katika kupunguza gharama za chakula na mfumuko wa bei ukashuka.Mengine mengi nitaongeza baadaye. Nadhani kwa faida ya wakuu wangu, nitajitahidi kufuatilia pia ilani yake ili nilinganishe na hayo hapo juu. Hata hivyo, ni ukweli kwamba kwa upanda wa barabara tu, miaka 50 tangu uhuru lami ilifikia km 6000, JK Pekee ameweka mikataba ya lami km 11,000.

      Kuna vitu anafanya JK.
      Last edited by Viwango; 6th March 2012 at 11:52. Reason: Adding points of merged thread

    2. FemaTV & Radio

    3. #21
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,478
      Rep Power : 6168
      Likes Received
      3051
      Likes Given
      1017

      Default

      Quote By Songoro
      Jk ana moyo wa subira sana hata kwa yale anayozushiwa ana uvumilivu wa kukaa kimya bila kuwatisha wazushi,uhuru wa kujieleza sasa upo juu kuliko kipindi chochote tangu mungu kaumba dunia hii!!,mgogoro wa Znz kaumaliza bila ya watu kutegemea,wanafunzi hata wa div 3 sasa wana uhakika wa kupata shahada, kaikumbuka sana mikoa ya magharibi kuliko Rais yoyote wa Tz kabla yake.
      Mkuu kwa binadamu wa kawaida uvumilivu na subira aliyoionyesha JK sijui kama itakuja kutokea kwa kuwa haijawahi kutokea. JK ameruhusu watu waseme kila kitu hadi wanapitiliza lakini ndio uhuru huo. Ila tujue pia kwamba kuna nchi za hapa jirani zina demokrasia lakini hazina uhuru wa kunena kama huu tunaoushuhudia hapa TZ. Wenzetu Kenya pamoja na katiba mpya na bill of rights mpya lakini hawana uhuru kama huu. Big up JK. Na hilo lingine la Zanzibar JK kaliweza. Tetesi zinasema kuwa mzee Ben Mkapa angweza kujinyakulia yale madola ($) ya Mo Ibrahim lakini timbwili la Zanzibar la tarehe 27 January lilimchafua; JK amepata dawa ya Zanzibar. Tukumbuke kuwa hili la Zanzibar ni la tangia miaka ya 60 hata Mwalimu Mwenyewe alitumia nguvu kulituliza ila JK ametumia busara tu. Bila shaka na hilo linampa sifa juu ya utatuzi wa migogoro. Akina Chief Anyauku walinyoosha mikono; majaribio ya miafaka zaidi ya mitano yote hakuna kitu.
      Pasco amesema tusema mazuri tu basi.
      Waberoya and Pasco like this.

    4. #22
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Shule za Sekondari nyingi wakati wa Kikwete, kuliko za wakati wa marais wote waliomtangulia pamoja na za wakoloni, zote ukichanganya hazifikii hata nusu ya shule alizojenga Kikwete kwa miaka 5 tu ya mwanzo.

      Ntakuja na sifa zake moja moja kila baada ya muda, sifa ambazo ni record kwa Kikwete ya amma kuwapita marais wote wa kabla yake amma kwa kuwa wa kabla yake hawajayafanya hayo kabisa.
      MAMMAMIA, Pasco and statila like this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    5. #23
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,478
      Rep Power : 6168
      Likes Received
      3051
      Likes Given
      1017

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Tusisahau pia ujenzi wa Barabara hapa nchini. Nina hakika kila mkoa unashuhudia mradi mkubwa wa barabara. Daraja la malagalasi nasikia linajengwa, nasikia Sumbawanga inaunganishwa na Tunduma, nasikia.Tabora inaunganishwa na Nzega, nasikia Tabora inaunganishwa na Kigoma, nasikia Iringa inaunganishwa na Dodoma, nasikia Singida, Arusha na Manyara zinaunganishwa, nasikia Dodoma na Manyara zinaunganishwa, nasikia Mtwara na Ruvuma zinaunganishwa kupitia Tunduru, nasikia Tanga, Handeni, Korogwe na Morogoro zinaunganishwa pia nasikia Bukoba na Biharamulo zinaunganishwa. Zooooote hizo ni kwa lami siyo changarawe. Penye sifa na apewe sifa.

      Pasco amesema tuongelee mazuri tu hapa. Huenda akaja na nyingine itakayoongelea aliposhindwa.
      Ndahani, Pasco and statila like this.

    6. #24
      jouneGwalu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Location : Studio
      Posts : 2,341
      Rep Power : 969
      Likes Received
      1314
      Likes Given
      1755

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Pasco
      Mkuu Jasusi, kwa Watanzania huwa wanaandaliwa kuchagua nini?. Kama kuwa karibu na watu, ku smile nao, na kuwachekesha kunakufanya upendeke na kuchagulika, then why not?. Hii inamaana hiki ndicho Watanzania tulichotaka!.

      Mimi nilitanguliza fani ya habari ndipo baadae nikaenda UDSM, nikiwa mtaani niliona jinsi magazeti ya udaku, yanavyonunuliwa kwa wingi!. Nilijiaminisha kuwa magazeti hayo ya udaku yanafasi kubwa mitaani nikijifariji washabiki wakubwa ndio hao walioishia darasa la saba!. Nilipofika UDSM, sikuamini nilipokuta ni magazeti hayo hayo ya udaku ndio yanayoongoza kwa mauzo pale UDSM!. Nimeishi Mabobo hostel miaka 4, ikifika saa mbili usiku TV zinahamishiwa Channel Ten kuangalia "muziki"!.

      Ninahudhuria sana mikutano ya kampeni, burudani na Ze Comedy ndio wanaochukua muda mrefu zaidi na burudani zikiisha, ukifika muda wa kumwaga sera, makundi makubwa ya watu, hujiondoke!. Hii inamaanisha hicho ndicho Watanzania wanachotaka!.

      Kwa mfano msomi mzuri mwenye Ph.D ya kuondoa umasikini akigombea ubunge wa Temeke na Juma Nature, unajua nani atachaguliwa?!. Lets appreciate baadhi ya mazuri ya rais wetu na tuache kubeza kila kitu!.
      Nimeipenda hii thread yako Mkuu wangu Pasco....

      Ila kabla sijaeleza "zuri" langu juu ya JK, naomba nipingane na wewe kwa jinsi ulivyofafanua maana ya "zuri" au "uzuri"...
      Kwamba kitu chochote,ilimradi tu ndio kinapendwa na watu wengi eti ndio kinakuwa kizuri!

      Hii inaweza isiwe tafsiri sahihi sana ya neno husika "zuri"...
      kwa mtu mwenye kuelewa marketing kama wewe unaweza kuelewa zaidi nini kipo nyuma ya msukumo huo...
      Kwamba kuna vichocheo vingine kabisa vinavyowasukuma watu kuingia kwenye kushabikia au kutumia vitu flani,
      nje ya mapenzi yao au ubora au uzuri wa kitu husika.

      Hivyo, si kweli kuwa kila chenye ushabiki wa wengi ni kizuri...

      Ndio maana nimeziwekea red bold hayo maeneo ya msisitizo kwenye jibu lako kwa Jasusi.

      Kwa maana hiyo, sio sahihi kuita hizo sifa za JK kuwa "Mazuri" eti kwasababu tu tunaamini kwayo ndio watz walimchagua, sababu tukiacha hivyo kwa eti "Mazuri" itabidi mjadala uwe mpana sana kuhusisha vipimo mbalimbali vya "uzuri" wa jambo husika, ndio maana nadhani wadau kama Jasusi akatoa post # 7.

      Nadhani tuviite vibweka, visifa ama vituko ambavyo vinaongeza mvuto wa kiongozi wetu, kwamba pamoja na kuvurunda kwake ila hivyo bado vinabaki na vinatakiwa vitukumbushe kuwa kuna siku tulivitumia kama ndio nguvu zake za ziada kuwazidi wapinzani wake kisiasa....

      Kisifa ninachomkubali sana JK ni Suti zake na mavazi yake kwa ujumla... yupo smart sana kwenye kuvaa!
      Jasusi, Ndahani and Pasco like this.
      Music affect the lives!!

    7. #25
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,619
      Rep Power : 2891
      Likes Received
      3837
      Likes Given
      12224

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By zomba
      Shule za Sekondari nyingi wakati wa Kikwete, kuliko za wakati wa marais wote waliomtangulia pamoja na za wakoloni, zote ukichanganya hazifikii hata nusu ya shule alizojenga Kikwete kwa miaka 5 tu ya mwanzo.

      Ntakuja na sifa zake moja moja kila baada ya muda, sifa ambazo ni record kwa Kikwete ya amma kuwapita marais wote wa kabla yake amma kwa kuwa wa kabla yake hawajayafanya hayo kabisa.
      Kabla hujarudi jiandae kutuambia hizo shule zina waalimu wa hadhi gani. Kujenga shule si kuweka majengo tu bila madawati. Pia usisahau kutupa habari jinsi alivyofanikiwa kumaliza tatizo la umeme.
      MAMMAMIA, Ndahani, Ngongo and 1 others like this.

    8. Miaka 50

    9. #26
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Jasusi
      Sawasawa. Ngoja na mimi nichangie ninayoyajua kwa nini Kikwete alipata 80% supposedly katika uchaguzi wa 2005.

      Ukiangalia tulikotokea tangu mfumo wa vyama vingi vya siasa (1992) ni CCM peke yake ndiyo iliyokuwa na ujuzi na uwezo wa kucheza mchezo wa uchaguzi wa kura. Mwaka 1995 Mrema alikuwa maarufu sana lakini alichezewa rafu na CCM kwa sababu upinzani haukujua mchezo wa kushinda kura.

      Come 2005 Kikwete aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania lakini nina hakika Watanzania hawakujua Kikwete ni mtu wa aina gani, personality wise and leadershipwise. Kwa sababu kama Kikwete angekuwa mtu anayejiamini hakuwa na sababu ya kununua waandishi wa habari kumpamba kwamba ni mwanasiasa mkomavu wakati ukomavu wake hata haujathibitika. Kikwete hakudebate na mgombea yeyote kwa hiyo uwezo wake wa kujenga hoja na kujieleza haukuwa challenged. Ni kama vile alipata free pass.

      By 2005 Watanzania wengi waliamini kuwa CCM peke yake ndiyo inayoweza kutoa kiongozi makini kwa sababu baada ya kufifia kwa Mrema upinzani haukuwa na mtu yeyote ambaye angeweza ku challenge CCM. Hiyo ndiyo sababu Kikwete alishinda kwa kishindo.

      Sasa miaka mitano baadaye Watanzania walishagundua ubabaishaji wa Kikwete, kwamba si mtu mwenye uwezo wa kushughulikia matatizo ya nchi, ni mbabaishaji, na anapenda kuzungumza tu bila kuchukua hatua. Na kadri ninavyoona, ni huo huo ubabaishaji wa Kikwete ambao umesababisha/utasababisha kupungua kwa umaarufu wa CCM come next election.
      Mkuu Jasusi, come 2015, tutaletewa mwingine anaechagulika na Watanzania, watamchagua!. Kama hakuna civic education ya kuwaeleza Watanzania wachague nini, then chochote tutakacholetewa tutachagua!

      Mimi chaguo langu kwa mgombea wa CCM ni EL, jamaa hajichekeshi, ni no nonsense man mwenye kutaka delivery, wengi humu hamumpendi kwa sababu ya mizigo aliyowabebea watu!. Kwa vile JK ni diplomat, alitoka foreign, na moja ya sifa za good diplomat ni kujua kujichanganya na watu na kusmile, ambazo JK anazo, basi jiandaeni kuletewa aliyeko foreign sasa, Mhe, Membe, he is good looking, he smiles good, na pia ni mtu wa watu, mkifuatilia baadhi ya hotuba zake, pia atakuwa na 'good sense of humour' ambazo ndizo sifa Watanzania wanazotaka kwa rais ajaye!, na tutamchagua kwa kishindo kuliko kile cha JK 2005 kwa sababu wapiga kura wengi zaidi ni wale wasomi zaidi, na wasomi wengi zaidi ni watu wa dini fulani zaidi, hivyo zitaongezeka japo kidogo, haswa kutegeeana na waraka wa wakati huo pia!
      Ndahani, Profesa and statila like this.

    10. #27
      Mtazamaji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th February 2008
      Location : global village
      Posts : 5,979
      Rep Power : 1775
      Likes Received
      1323
      Likes Given
      2661

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Uzuri wa JK ni weakness zake zimewezesha mazuri . Sometime udhaifu unaweza kuwa silaha. Kuna mambo yanaoyendelea CCM . Na maamuzi yake ya kuchelewa au kusburi kusiiklizia umma na kugeuka geuka yamesaidia sana. Mfano Isue ya Jairo, Nyogeza wa posho za wabunge nk. Mkapa aliongoza kwa style ya udiketa fulani hivi . hakukuw aa nafasi ya kurudi nyuma no.

      Na huko CCM uzuri wake JK wa kuuma na kupuliza nadhani hata Lowasa anajiuliza kama walikutana bararaani

      Yaani kuna sifa fulani za JK angekuwa nazo Mkapa na na sifa fulani za Mkapa angekuwa nazo JK may be tungekuwa hatua tano mbele zaidi ya tulipo sasa
      Jasusi and jessetz like this.
      Tazama michezo live katika gym nayotumia kukuzia misuli ya IT- http://teknohama.x10.mx/live-sports/

    11. #28
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Kimbunga
      Tusisahau pia ujenzi wa Barabara hapa nchini. Nina hakika kila mkoa unashuhudia mradi mkubwa wa barabara. Daraja la malagalasi nasikia linajengwa, nasikia Sumbawanga inaunganishwa na Tunduma, nasikia.Tabora inaunganishwa na Nzega, nasikia Tabora inaunganishwa na Kigoma, nasikia Iringa inaunganishwa na Dodoma, nasikia Singida, Arusha na Manyara zinaunganishwa, nasikia Dodoma na Manyara zinaunganishwa, nasikia Mtwara na Ruvuma zinaunganishwa kupitia Tunduru, nasikia Tanga, Handeni, Korogwe na Morogoro zinaunganishwa pia nasikia Bukoba na Biharamulo zinaunganishwa. Zooooote hizo ni kwa lami siyo changarawe. Penye sifa na apewe sifa.

      Pasco amesema tuongelee mazuri tu hapa. Huenda akaja na nyingine itakayoongelea aliposhindwa.
      Kwa kuongezea tu, Tanzania kwa sasa ina miradi ya barabara mingi kuliko nchi yoyote ya Afrika chini ya sahara, na pia miradi ya barabar iliyoanza, kumalizika amma kusainiwa wakati wa Kikwete, ni record kwa uwingi kifedha, ki kilomita, na kwa kuunganisha mikoa kuliko miradi yote ya barabara za lami ukijumlisha pamoja ya marais wote pamoja na mkoloni.

      Hongera Kikwete
      Kimbunga and statila like this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    12. #29
      Taso's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2010
      Posts : 1,174
      Rep Power : 794
      Likes Received
      308
      Likes Given
      121

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      kama na wewe unalo zuri lolote la JK ambalo unalijua, unaweza kuliweka.
      His moral rectitude in the public square.

      Toka awe Rais, sijasikia Jakaya Kikwete kafumaniwa na kimada Ikulu au kwenye vichochoro vya panya, au kaoa wake wengi wengi (kama Mwinyi na Billal), au kalewa hadharani (kama Mkapa), au kamfungulia mkewe biashara Ikulu (kama Mama Anna, au Mama Sitti au Mama Maria na mabanda ya kuku Ikulu ya Nyerere) au hata kuvuta sigara tu (kama Nyerere siku za mwanzo za uhuru).

      Maswaiba wengi wa duara lake la ndani wanasema kabla hajawa Rais watu walikuwa wanapishana nae kwenye mabanda ya mashangazi na mashangingi uswahilini. Ushahidi ni idadi ya wanawake aliowazalisha kabla hajawa Rais.

      Baada ya Urais shutuma kama hizo hazijatamkwa asilani juu ya jina la Rais Jakaya Khalfani Mrisho Kikwete.

    13. #30
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Jasusi
      Kabla hujarudi jiandae kutuambia hizo shule zina waalimu wa hadhi gani. Kujenga shule si kuweka majengo tu bila madawati. Pia usisahau kutupa habari jinsi alivyofanikiwa kumaliza tatizo la umeme.
      Utaweka wapi madawati kama huna jengo? utaweka wapi walimu kama huna jengo? hata wewe na mimi tulivyozaliwa tulianza kukuwa kwa kujiharia, kujikojolea mpaka tulipoweza kuwa na akili ya kuwa sasa nimeshikwa na tumbo. Kila kitu kinakwenda kwa mpangilio wake, huwezi kuanza kununuwa fanicha kabla hujawa na pa kuiweka.

      Leo tunashuhudia rekodi nyingine ya Kikwete, vyuo vya walimu vingi kuliko awamu yoyote ya kabla yake.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    14. #31
      Saint Ivuga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2008
      Posts : 20,692
      Rep Power : 10170
      Likes Received
      5660
      Likes Given
      12666

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By zomba
      Utaweka wapi madawati kama huna jengo? utaweka wapi walimu kama huna jengo? hata wewe na mimi tulivyozaliwa tulianza kukuwa kwa kujiharia, kujikojolea mpaka tulipoweza kuwa na akili ya kuwa sasa nimeshikwa na tumbo. Kila kitu kinakwenda kwa mpangilio wake, huwezi kuanza kununuwa fanicha kabla hujawa na pa kuiweka.

      Leo tunashuhudia rekodi nyingine ya Kikwete, vyuo vya walimu vingi kuliko awamu yoyote ya kabla yake.
      yaani wewe hueleweki unarahisha mambo sana..
      JF the best place to be. and the POWER of God be with us all the time.

    15. #32
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,619
      Rep Power : 2891
      Likes Received
      3837
      Likes Given
      12224

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Taso
      His moral rectitude in the public square.

      Toka awe Rais, sijasikia Jakaya Kikwete kafumaniwa na kimada Ikulu au kwenye vichochoro vya panya, au kaoa wake wengi wengi (kama Mwinyi na Billal), au kalewa hadharani (kama Mkapa), au kamfungulia mkewe biashara Ikulu (kama Mama Anna, au Mama Sitti au Mama Maria na mabanda ya kuku Ikulu ya Nyerere) au hata kuvuta sigara tu (kama Nyerere siku za mwanzo za uhuru).

      Maswaiba wengi wa duara lake la ndani wanasema kabla hajawa Rais watu walikuwa wanapishana nae kwenye mabanda ya mashangazi na mashangingi uswahilini. Ushahidi ni idadi ya wanawake aliowazalisha kabla hajawa Rais.

      Baada ya Urais shutuma kama hizo hazijatamkwa asilani juu ya jina la Rais Jakaya Khalfani Mrisho Kikwete.
      Naona hujasafiri nje ya nchi ndugu yangu. Nenda London kaulize nani pale alikuwa anamliwaza. Nenda Marekani kaulize ni akina nani waliolipiwa nauli kwenda kuweka joto kwenye viota vya mahaba. Don't even go there.
      TIMING, Ndahani and samora10 like this.

    16. #33
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,619
      Rep Power : 2891
      Likes Received
      3837
      Likes Given
      12224

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By zomba
      Utaweka wapi madawati kama huna jengo? utaweka wapi walimu kama huna jengo? hata wewe na mimi tulivyozaliwa tulianza kukuwa kwa kujiharia, kujikojolea mpaka tulipoweza kuwa na akili ya kuwa sasa nimeshikwa na tumbo. Kila kitu kinakwenda kwa mpangilio wake, huwezi kuanza kununuwa fanicha kabla hujawa na pa kuiweka.

      Leo tunashuhudia rekodi nyingine ya Kikwete, vyuo vya walimu vingi kuliko awamu yoyote ya kabla yake.
      Kumbe hujasikia vilio vya waalimu waliopo? Kumbe hujaona matokeo ya mitihani shule za kata? Unapojenga majengo ya shule 20 ishirini unahakikisha unao waalimu 60 tayari si kujenga jengo kwanza halafu ndio uanze kuandaa waalimu. Kwa mtaji huu Watanzania hata hawawezi kushindana na wenzao katika jumuiya ya Afrika mashariki. Na zile kompyuta alizoahidi kwa kila mwanafunzi nchini kote zimeishia wapi? Au utasema kwanza anashughulikia tatizo la umeme wa uhakika? System at work kweli kweli.
      TIMING likes this.

    17. #34
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,084
      Rep Power : 12251
      Likes Received
      6014
      Likes Given
      6851

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Kweli JF sasa nayo ni shamba la bibi... hata hii mada ni sticky!!! hebu tuwekeeni na ya mabaya ya JK kama sticky basi watu wamwage ukweli i.e mada nzuri lakini sio sticky... asilani!!!

      Halafu Pasco naona vile vikao vimeanza kumsaidia kimaisha, wamefika dau... anabadilika, bahati mbaya anabadilika kila kitu, mwisho wa siku asije kubadili na jinsia tu!!!
      Last edited by TIMING; 4th March 2012 at 03:12.
      .....Ana sifa zote, nzuri na mbaya!!!

    18. #35
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default

      Quote By MTM
      Kweli JF sasa nayo ni shamba la bibi... hata hii mada ni sticky!!! hebu tuwekeeni na ya mabaya ya JK kama sticky basi watu wamwage ukweli i.e mada nzuri lakini sio sticky... asilani!!!

      Halafu Pasco naona vile vikao vimeanza kumsaidia kimaisha, wamefika dau... anabadilika, bahati mbaya anabadilika kila kitu, mwisho wa siku asije kubadili na jinsia tu!!!
      Asante MTM, nadhani hapa jf, hakuna copy right ya thred starter!. Hivyo nashauri anzisha tuu tutachangia!.

      Kwa upande mimi Pasco ni yule yule juzi, jana na leo na ndio kwanza najipanga kusimama tena ili nihesabiwe!.

      You have to learn to "fear the Greeks, especially when when they bring gifts!"
      Last edited by Pasco; 4th March 2012 at 05:48.
      TIMING likes this.

    19. #36
      King'asti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2009
      Location : The Jungle
      Posts : 17,189
      Rep Power : 28902
      Likes Received
      11663
      Likes Given
      4819

      Default

      Lol! Muambie zipu haziwekwi komeo!
      Quote By Jasusi
      Naona hujasafiri nje ya nchi ndugu yangu. Nenda London kaulize nani pale alikuwa anamliwaza. Nenda Marekani kaulize ni akina nani waliolipiwa nauli kwenda kuweka joto kwenye viota vya mahaba. Don't even go there.
      Jasusi likes this.

    20. #37
      mchemsho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th June 2011
      Posts : 2,015
      Rep Power : 809
      Likes Received
      269
      Likes Given
      20

      Default

      Quote By Songoro
      Jk ana moyo wa subira sana hata kwa yale anayozushiwa ana uvumilivu wa kukaa kimya bila kuwatisha wazushi,uhuru wa kujieleza sasa upo juu kuliko kipindi chochote tangu mungu kaumba dunia hii!!,mgogoro wa Znz kaumaliza bila ya watu kutegemea,wanafunzi hata wa div 3 sasa wana uhakika wa kupata shahada, kaikumbuka sana mikoa ya magharibi kuliko Rais yoyote wa Tz kabla yake.
      hana subira yoyote.! Ni mwoga wa kufanya maamuzi, uzushi ukiachwa bila kukemewa huwa ukweli, anaogopa kufanya maamuzi kwa kuwa anagopa outcome ya maamuzi

    21. #38
      TIMING's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2008
      Location : Roaming...
      Posts : 20,084
      Rep Power : 12251
      Likes Received
      6014
      Likes Given
      6851

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Pasco
      Asante MTM, nadhani hapa jf, hakuna copy right ya thred starter!. Hivyo nashauri anzisha tuu tutachangia!. Kwa upande mimi niko ok, you have to learn to "fear the Greeks, especially when when they bring gifts!"
      Thanks MY BRO... I KNOW!!! as always it depends on the school of thoughts and mentors in life

      One thing for sure my friend, if you try to analyse yourself, you will realise that you have almost eaten your very own self. My advice mkuu.... practice what you preach!! and BTW, I learned to Fear the COPTIC, especially when they bring ornaments
      .....Ana sifa zote, nzuri na mbaya!!!

    22. #39
      King'asti's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th November 2009
      Location : The Jungle
      Posts : 17,189
      Rep Power : 28902
      Likes Received
      11663
      Likes Given
      4819

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Anavaa lipete lizuri kama la marehemu sheikh yahya
      mama D likes this.

    23. #40
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default

      Quote By Jasusi
      Naona hujasafiri nje ya nchi ndugu yangu. Nenda London kaulize nani pale alikuwa anamliwaza. Nenda Marekani kaulize ni akina nani waliolipiwa nauli kwenda kuweka joto kwenye viota vya mahaba. Don't even go there.
      Mkuu Jasusi, kiasili Kiafrika hii nayo ni sifa!. Tuache uzungu, wamekuja wametuletea dini zao, Waarabu wakatufunza mwisho wanne, wazungu ndio wakaja na mwisho mmoja!. Tumewakubalia tuu kwa sababu.. ili kiasili hiyo ndio nature yetu!, na kwa hili anastahili pongezi, si unaona hata jinsi ma DC wetu au badhi ya teule watu wanavyopendezea!. Hebu kumbuka Ma DC enzi za Nyerere?!. Iliwezekana kumchukua mtu from no where kwenye diplomatic corridors ukampa key embassy kama ya UK au sasa DC!. Kwa hili lazima tumpongeze JK, he is very considerate kwa wenzetu hawa!, na hata kama unaambiwa "asante", kwa nini usiwe ni mtu wa kupokea shukran!.

      Umenikumbusha jambo jingine jema la JK, japo sometimes anazingiziwa kuwa ni mtu wa visasi with ref. ya kina Babu Seya, Liyumba na Mahalu!, shutuma hizo sii kweli, JK ni mtu wa "forgive and forget!". Wale wa zamani ambao wanajua kulitokea nini pale wizara ya Nishati JK akiwa waziri na Prof. Mwandosya akiwa ni Katibu Mkuu, paliwaka moto!. Prof. Mwandosya akaachia ngazi na kurudi darasani. JK angekuwa mtu wa visasi, baada ya JK kuingia Ikulu ilikuwa Prof atafute pa kukimbilia, lakini its the oposite, ndio kwanza kamuita kwenye cabinet yake!.

      Pia sifa nyingine kubwa ya JK ni mtu wa shukrani anayekumbuka fadhila!. Hebu waangalie watu mbalimbali waliomsaidia kufika hapo alipo jinsi alivyowakumbuka!.

      JK ni mwema jamani, na kabla hajamaliza kipindi chake hiki, kuna watu mtasikia wametupwa balozi hizi na zile kabla hajaondoka!. Huu sio wema?.
      Jasusi, MAMMAMIA and Rock City like this.

    Page 2 of 23 FirstFirst 123412 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...