Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

    Report Post
    Page 16 of 23 FirstFirst ... 61415161718 ... LastLast
    Results 301 to 320 of 442
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Wanabodi,
      Naangalia TBC Live, Rais Jakaya Kikwete yuko hewani!
      Miongoni wa mazuri ya JK, ni having a good sense of humour, akiongea, huchoki kumsikiliza!.
      Alipokuwa akiongelea kilimo cha ndizi kijijini kwao Msoga, Bagamoyo, akasema wakulima wana bananisha migomba mingi kwenye shina moja, matokeo yake kila mgomba unatoa kichane kimoja au viwili ya vindizi vilivyokondeana!.

      Akasema wanakijiji wale wanalima hivyo kwa sababu hawajui kuwa kama wakiacha mgomba mmoja kwenye shina moja, mgomba huo utatoa mkungu mkubwa wa ndizi, na ndizi zenyewe zitakuwa ni ndizi za shibe kama "Mrisho Mpoto"!. Ukumbi mzima ulizizima kwa vicheko, watu hawana mbavu!.

      Kuwa na 'good sense of humour' ni kipaji na ni miongoni mwa mambo mazuri machache ya rais wetu Jakaya Kikwete, besides good looking!.

      Kwa wale wenye kumbukumbu ya hotuba za Mwalimu, ukiondoa ile hotuba yake ya kutangaza vita, hotuba za Mwalimu, watu walikuwa wanacheka na hutamani amalize kuzungumza!.

      Hii ni thread ya miongoni mwa mazuri ya JK, kama na wewe unalo zuri lolote la JK ambalo unalijua, unaweza kuliweka.

      Kwa vile tunazungumzia mazuri, ningeomba wale ambao hawana zuri lolote la kuzungumzia JK, sio lazima mchangie, wala zuri hili la "good sense of humour", haimaanishi JK sasa ndio rais bora kwa Tanzania, wala haina maana ndio hana mabaya yake!, leo tuzungumzie mazuri yake!

      Angalizo:
      Wanabodi wenzangu, tunajukumu la kujimoderate sisi wenyewe kulinda hadhi ya jukwaa letu, haiwezekana kila siku sisi tukawa ni watu wa kulalamika tuu, au kubonda tuu, mara moja moja kwenye mazuri, pia tutoe sifa pale panapo stahili!.

      Natanguliza Shukrani kwa kunielewa!

      Asanteni!

      Pasco (wa jf)

      Note: Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali ni muumini wa ukweli "seek the truth, and the truth will set you free"!. Kwa wale wanaofikiri Pasco wa jf, ni mshabiki wa CCM, tafuteni thread yangu ya "CCM Imechokwa" !.


      --------------------------------------------
      Hoja Nyingine za Thread ya kibananhukhu iliyounganishwa #148
      Quote By kibananhukhu
      Pamoja na list ya mambo lukuki ambayo wakuu mnamlaumu JK, lakini ni kweli kuwa kuna kitu anafanya siyo kwamba amelele fofofo. Kuna mapungufu pia ni kwa nia njema mnayaainisha kusaidia uboreshaji kazi. Nimefuatilia na kuyaona baadhi ya mazuri ya JK Kama list inavyoainisha, ninaweza kuwa na upungufu kidogo katika takwimu hii itatokana na mimi kutumia kumbukumbu zangu nipo tayari kusahihishwa takwimu. Tupitie mazuri ya JK HAPA CHINI

      1. Mpango wa kuiruhusu bandari (THA) kufanya kazi kwa kuanza na technologia mpya ili dereva tu ndiye awe anakwenda bandarini kupakia mzigo na mengine yote yatamalizwa kwa njia ya mtandao, e-port. Kumbukeni TICTS walikuwa na mkataba mbaya sana kwa miaka 15, na ulirejewa kwa mazingira ya kutatanisha.

      2. Dar tayari nyumba 50 zimeanza kutumia gesi kwa matumizi mbali mbali ya ndani, kama ulaya na kwingineko kwa mara ya kwanza. Mikocheni wameanza jiandaeni kuvuta gesi majumbani kwenu.

      3. Magari yameaanza kutumia gesi japokuwa bado kuna baadhi ya vikwazo kwa wasaidizi wa raisi. Mpango wa JK ilikuwa matuzi ya petroli katika gari yapungue kwa 80%, lkn ukiritimba wetu umesababisha yapungue kwa 55%

      4. Kivuko na daraja kigamboni.

      5. Mradi wa daraja Maragalasi na lami Tabora – Itigi – Kigoma

      6. Ujenzi wa barabara lami kutoka Mombo, Mtibwa turiani, Kilosa, Mikumi na baadaye ifakara, mahenge, Malinyi, Songea. Pia Ifakara, Mlimba hadi Njombe. Usafiri wa songea kupunguza safari kwa masaa 5.

      7. Barabara ya Mafinga, Iringa, Kitonga, Ruaha Mbuyuni, Madaraja mawili mpakani na morogoro imekwishapanuliwa kwa uboro wa hali ya juu. Kipande cha Ipogolo kupandisha kwenda iringa mjini kimepanuliwa sana.

      8. Bara bara ya Iringa Kwenda Dodoma Imekwishaanza

      9. Bara bara ya Tunduma hadi Sumbawanga kuna makandarasi watatu wanashindana kwa ubora wa lami.

      10. Viwanja vya ndege mikoani kuboreshwa.

      11. Karekebisha mkataba wa Songas, ulikuwa hauruhusu mtu meingine yetote awaye kujenga tena bomba la gesi. Sasahivi wakuu mnaruhusiwa kujenga mabomba ya gesi kutoka Kusini.

      12. Mkataba wa wachina na serikali kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi dar ili kuzalisha MG 2900 za umeme dar.

      13. Barabara Dodoma, Manyara lami.

      14. Ujenzi reli kutoka Tanga, Musoma, Uganda.

      15. Ujenzi bandari, Tanga, Mtwara na Babamoyo

      16. Uwanja wa Ndege Terminal two wajengwa.

      17. Maeneo ya Umwagiliaji maji, hekari 20,000 zimejengwa na lengo ni ekari 1milioni.

      18. Kilimo kwanza mashamba darasa na ongezeko la mavuno kwa ekari.

      19. Tanzania ni ya kwanza kwa export afrika masharik na kati

      20. Mradi wa makaa ya Mawe Mchuchuma na katewaka liganga kuzalisha MGW za kutosha nchi nzima

      21. Mradi wa machimbo mgodi wa chuma Liganga, uzalishaji wa Titanium, Vanadium, Fe kwa ajili ya utengenezaji nondo, malighafi ya mabati, vyuma vya kujengea madaraja na maghorofa, kuweka pembezoni mwa mabarabara kuzalishwa nchini. Viwanda vya kutengeneza vifaa vya ujenzi wa meli, ndege, na magari kujengwa nchini.

      22. Machimbo ya makaa yam awe Ngaka Mbinga Ruvuma, uwezo Kuzalisha pia umeme MG 400.

      23. Hospitali upasuaji moyo kwa mara ya kwanza Tanzania.

      24. Hospitali kubwa mingoni mwa zitakazoheshimika kujengwa Tanzania na Appollo ya India. Maradhi yote kutibiwa Tanzania.

      25. Uboreshaji shirika la nyumba NHC, Baadhi ya watanzania kunufaika na mikopo ya nyumba na nyumba kuanza kujengwa kwa spidi kali.

      26. Ujenzi wa barabara nane Dar hadi chalinze.

      27. Ufumuaji na ujenzi wa reli ya kati dar, hadi kigoma, mwanza, mpanda, Rwanda na Burundi.

      28. Ubareshaji maabara shule za kata ($ 90Milioni)

      29. Idadi ya walimu kwaajili ya shule za kata na nyinginezo kuanzia muda mfupi ujao, walimu elfu 40 kuhitimu kila mwaka.

      30. Baadhi ya shule nyingi binafsi zimeanza kudorola au kufungwa kabisha, wengi wamejiunga na shule za kata na ubora unapanda japo kwa spidi ndogo.

      31. Idadi kubwa ya wanafunzi vyuo vikuu, Udom uwezo elfu 40, SAUT elfu 15, UDSM Elfu 15, Ruco elf 2.5, Mkwawa elfu 2.5 Tumaini elfu 2, Open University elfu 20 nk.

      32. Wafanya biashara wamepewa kipau mbele term ya JK, Wengi husafiri na Mheshimiwa Raisi kutafuta na kupata fursa za biashara nje.

      33. Uhuru wa Vyombo vya habari, waandishi wanafanya mambo kwa uhuru ambao wasingelithubutu enzi ya Mwalimu, Mwinyi wala Mkapa. Hata baadhi ya ninyi wakuu, mnaruhusuwa kutoa mawazo yenu japo wengine wanatukana matusi ya nguoni lakini JK anavumilia sana.

      34. Amegundua fitna nyingi sana serikalini, majungu, uongo na sasa hivi anakua mwangalifu sana katika maamuzi na inalazimika kuonekana kana kwamba hana maamuzi ili awe na subira. (Ukiwa na hasiri usifanye maamuzi, ahirisha upate busara)

      35. Makampuni ya madini, yamekupali kuanza kulapa 30% kutoka faida zitakazo patikana kuanzia 2012.

      36. Wapinzani wameanza kumwelewa na kumsifia kwa yale anayoyafanya vizuri.

      37. Mnaweza ongeza list nyingine ili nije baadaye na listi ya faida za kiuchumi kwa taarifa tu, inflation inachangiwa na gharama za chakula kwa 16%.

      Kuna mambo madogo ya kiufundi yakirekebishwa inflation inapashwa iwe 8% single digit. Mfano mahindi yanaoza Ruvuma, Iringa, na Sumbawanga yangeweza kutoa mchango katika kupunguza gharama za chakula na mfumuko wa bei ukashuka.Mengine mengi nitaongeza baadaye. Nadhani kwa faida ya wakuu wangu, nitajitahidi kufuatilia pia ilani yake ili nilinganishe na hayo hapo juu. Hata hivyo, ni ukweli kwamba kwa upanda wa barabara tu, miaka 50 tangu uhuru lami ilifikia km 6000, JK Pekee ameweka mikataba ya lami km 11,000.

      Kuna vitu anafanya JK.
      Last edited by Viwango; 6th March 2012 at 11:52. Reason: Adding points of merged thread

    2. FemaTV & Radio

    3. #301
      Shardcole's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 15th January 2012
      Posts : 4,393
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1032
      Likes Given
      4

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Pasco, Nape & Jk, these all above guys are MBUMBUMBU people.

    4. #302
      FEELINGS's Avatar
      Member Array
      Join Date : 30th December 2011
      Posts : 42
      Rep Power : 381
      Likes Received
      12
      Likes Given
      15

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Tusisahau kuwa ni mtu wa watu. Huwatembelea wagonjwa hospitalini, huudhuria misiba, huwakumbuka yatima,wajane na wazee hasa katika sikukuu za dini. Pia ameruhusu uhuru mkubwa wa habari mpaka wanamtukana! MAPUNGUFU KWA MWANADAMU NI LAZIMA LAKINI KUNA MENGI MAZURI KAFANYA NA ANASIFA ZAKE NYINGI TU ZA KUTOSHA. Wakati na watu waliomzunguka ndio wanamfanya awe alivyo sasa. SERIKALINI ALIKUWA MIAKA MINGI LAKINI.............
      Maundumula and statila like this.

    5. #303
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Barabara kulilo yeyote yule.

    6. #304
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default

      Quote By Pasco
      Mkuu Jasusi, kiasili Kiafrika hii nayo ni sifa!. Tuache uzungu, wamekuja wametuletea dini zao, Waarabu wakatufunza mwisho wanne, wazungu ndio wakaja na mwisho mmoja!. Tumewakubalia tuu kwa sababu.. ili kiasili hiyo ndio nature yetu!, na kwa hili anastahili pongezi, si unaona hata jinsi ma DC wetu au badhi ya teule watu wanavyopendezea!. Hebu kumbuka Ma DC enzi za Nyerere?!. Iliwezekana kumchukua mtu from no where kwenye diplomatic corridors ukampa key embassy kama ya UK au sasa DC!. Kwa hili lazima tumpongeze JK, he is very considerate kwa wenzetu hawa!, na hata kama unaambiwa "asante", kwa nini usiwe ni mtu wa kupokea shukran!.

      Umenikumbusha jambo jingine jema la JK, japo sometimes anazingiziwa kuwa ni mtu wa visasi with ref. ya kina Babu Seya, Liyumba na Mahalu!, shutuma hizo sii kweli, JK ni mtu wa "forgive and forget!". Wale wa zamani ambao wanajua kulitokea nini pale wizara ya Nishati JK akiwa waziri na Prof. Mwandosya akiwa ni Katibu Mkuu, paliwaka moto!. Prof. Mwandosya akaachia ngazi na kurudi darasani. JK angekuwa mtu wa visasi, baada ya JK kuingia Ikulu ilikuwa Prof atafute pa kukimbilia, lakini its the oposite, ndio kwanza kamuita kwenye cabinet yake!.

      Pia sifa nyingine kubwa ya JK ni mtu wa shukrani anayekumbuka fadhila!. Hebu waangalie watu mbalimbali waliomsaidia kufika hapo alipo jinsi alivyowakumbuka!.

      JK ni mwema jamani, na kabla hajamaliza kipindi chake hiki, kuna watu mtasikia wametupwa balozi hizi na zile kabla hajaondoka!. Huu sio wema?.
      Uteuzi wa wakuu wapya wa wilaya pia umezingatia baadhi ya mazuri ya JK!. Ni mtu wa shukrani anaekumbuka fadhila. Ukimtendea wema utalipwa wema!. Katika list wengi nimewaona ni wanalipwa fadhila!.

    7. #305
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default

      Quote By Shardcole
      Pasco, Nape & Jk, these all above guys are MBUMBUMBU people.
      Ukiitwa mbumbumbu kama kiukweli wewe ni mbumbumbu huna sababu ya kukasirika. Mfano mimi nakubali ni mbumbumbu na sikasiriki kwa sababu ndio ukweli wako!. Lakini kumuita Nape ni mbumbumbu ni kumtukana kwa sababu issue ya hii thread ni mazuri ya JK.

      Lakini kumuita JK ni mbumbumbu sio tuu ni kumtukana rais wetu bali pia unaishushia heshima jf yetu kwa rais kutukanwa na unaachwa hivi hivi.

      Unaweza kumuita JK ni mbumbumbu kama uta justify umbumbumbu wake ni kwenye nini?.

    8. Miaka 50

    9. #306
      Osaka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Location : Morogoro
      Posts : 1,089
      Rep Power : 618
      Likes Received
      266
      Likes Given
      162

      Default

      Quote By Pasco
      Ukiitwa mbumbumbu kama kiukweli wewe ni mbumbumbu huna sababu ya kukasirika. Mfano mimi nakubali ni mbumbumbu na sikasiriki kwa sababu ndio ukweli wako!. Lakini kumuita Nape ni mbumbumbu ni kumtukana kwa sababu issue ya hii thread ni mazuri ya JK.

      Lakini kumuita JK ni mbumbumbu sio tuu ni kumtukana rais wetu bali pia unaishushia heshima jf yetu kwa rais kutukanwa na unaachwa hivi hivi.

      Unaweza kumuita JK ni mbumbumbu kama uta justify umbumbumbu wake ni kwenye nini?.
      Well said Paschal Mayala!
      Pasco likes this.

    10. #307
      Nyakageni's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 1st February 2011
      Posts : 5,248
      Rep Power : 0
      Likes Received
      769
      Likes Given
      52

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Nimekufuatilia Star tv, you have tried to balance ila bado
      Pasco likes this.

    11. #308
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default

      Quote By Osaka
      Well said Paschal Mayala!
      Mkuu Osaka, mimi ni Pasco!. Jf si tuna sheria zetu za name calling?. Hata kama unanidhania mimi ndiye, bado huruhusiwi kunifananisha!. Kwa kukusaidia tuu mimi ni Pasco ila na Pascal Mayalla mwenyewe pia yumo humu!.
      statila likes this.

    12. #309
      MTU POLI's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th May 2012
      Posts : 64
      Rep Power : 367
      Likes Received
      10
      Likes Given
      9

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      No, thanks.
      Pasco likes this.

    13. #310
      RubenM's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 15th April 2009
      Location : MBEYA
      Posts : 104
      Rep Power : 535
      Likes Received
      7
      Likes Given
      8

      Default

      Quote By Pasco
      Wanabodi,
      Naangalia TBC Live, Rais Jakaya Kikwete yuko hewani!
      Miongoni wa mazuri ya JK, ni having a good sense of humour, akiongea, huchoki kumsikiliza!.
      Alipokuwa akiongelea kilimo cha ndizi kijijini kwao Msoga, Bagamoyo, akasema wakulima wana bananisha migomba mingi kwenye shina moja, matokeo yake kila mgomba unatoa kichane kimoja au viwili ya vindizi vilivyokondeana!.

      Akasema wanakijiji wale wanalima hivyo kwa sababu hawajui kuwa kama wakiacha mgomba mmoja kwenye shina moja, mgomba huo utatoa mkungu mkubwa wa ndizi, na ndizi zenyewe zitakuwa ni ndizi za shibe kama "Mrisho Mpoto"!. Ukumbi mzima ulizizima kwa vicheko, watu hawana mbavu!.

      Kuwa na 'good sense of humour' ni kipaji na ni miongoni mwa mambo mazuri machache ya rais wetu Jakaya Kikwete, besides good looking!.

      Kwa wale wenye kumbukumbu ya hotuba za Mwalimu, ukiondoa ile hotuba yake ya kutangaza vita, hotuba za Mwalimu, watu walikuwa wanacheka na hutamani amalize kuzungumza!.

      Hii ni thread ya miongoni mwa mazuri ya JK, kama na wewe unalo zuri lolote la JK ambalo unalijua, unaweza kuliweka.

      Kwa vile tunazungumzia mazuri, ningeomba wale ambao hawana zuri lolote la kuzungumzia JK, sio lazima mchangie, wala zuri hili la "good sense of humour", haimaanishi JK sasa ndio rais bora kwa Tanzania, wala haina maana ndio hana mabaya yake!, leo tuzungumzie mazuri yake!

      Angalizo:
      Wanabodi wenzangu, tunajukumu la kujimoderate sisi wenyewe kulinda hadhi ya jukwaa letu, haiwezekana kila siku sisi tukawa ni watu wa kulalamika tuu, au kubonda tuu, mara moja moja kwenye mazuri, pia tutoe sifa pale panapo stahili!.

      Natanguliza Shukrani kwa kunielewa!

      Asanteni!

      Pasco (wa jf)

      Note: Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali ni muumini wa ukweli "seek the truth, and the truth will set you free"!. Kwa wale wanaofikiri Pasco wa jf, ni mshabiki wa CCM, tafuteni thread yangu ya "CCM Imechokwa" !.


      --------------------------------------------
      Hoja Nyingine za Thread ya kibananhukhu iliyounganishwa #148
      Barabara ya iringa-ruaha mbuyuni imeanza kujengwa 2003 siyo ya Leo hiyo nakumbuka nikiwa nasoma Tosamaganga...
      Hiyo ya kutoka mafinga -iringa yes ndio ya juzi ktk awamu hii... 27 pia mmmh
      Pasco likes this.

    14. #311
      Maundumula's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 4,920
      Rep Power : 3095
      Likes Received
      1340
      Likes Given
      5654

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Reli Tanga Musoma Uganda ishaanza au ndio zile plan za Vision 2050?
      Pasco likes this.

    15. #312
      IWILL's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd June 2011
      Posts : 177
      Rep Power : 438
      Likes Received
      34
      Likes Given
      51

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      hii thread ni endless, nadhani umefika mahali ipelekwe mahali kwake ambapo ni CCM blog iliyofunguliwa hivi majuzi. tuna issue za maana za kuona kuliko jokes za shibe kwa watu walio na njaa kutoka kikwete. anadhani watu wamekosa maalifa ya kilimo kwa sababu wamelogwa? no ni uduni wa maarifa ya kilimo.keep aside that jokers'jokes.
      Pasco likes this.

    16. #313
      bumes's Avatar
      Member Array
      Join Date : 26th May 2012
      Posts : 58
      Rep Power : 363
      Likes Received
      12
      Likes Given
      1

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Thank you for your observation.

      Usually when I sit and think about our president. I can assure you though very few would agree with me that JK Kikwete would have been one of the greatest Presidents Tanzania would have had.

      But I want to say that for every tree to flourish, branches and some leaves must be pruned and weeds removed, the branches, weeds around it will make it bare fruit or not and that demands sacrifices

      There are only two ways, when you stand for the rights of the poor you always become the thorn of the rich who usually are always in control of the destinations of the masses.

      You can only find yourself unknowingly serving one side and leaving others to the mercy of time.

      We shall always thank him for what he has contributed to our country may the almighty GOD help him.
      Pasco and statila like this.

    17. #314
      Blessing's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st April 2009
      Posts : 261
      Rep Power : 566
      Likes Received
      10
      Likes Given
      0

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      kikwete ana wisdom na anamfuto ya urais --- bahati mbaya amenyemelea kwa nguvu urais ili atuibie. Umasikini na uroho imemjaa sana --- analolote infact he does not apeal me kabisa kwa sababu he has no personality. Lastly, hata elimu yake ina question mark.
      Pasco likes this.

    18. #315
      Hatibu Mintanga's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th May 2012
      Posts : 13
      Rep Power : 354
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default

      Wadau Prezida wetu ana mazur meng sana 1-Anasafir sn kwenda nje kutuombea misaada ya maendeleo haijalish kama tanzania kuna madin, maliasili,uvuvi,ufugaj wacha tuwaombe wazungu coz wametutangulia kwenye maendeleo.. 2-Ana huruma sana ndo mana kila msiba anaenda mf:kafa rais wa malawi ,msanii maarufu kanumba na milion 10 katoa ana upendo wa pekee kwa wasanii kafa mzee kipara,isa matona na 5stars alijisahau kuwapa mamilion lkn ni mtu mwema sana alijua watanzania weng hawaend shamba,wanategea kazi,hawaend shul
      Pasco likes this.

    19. #316
      Doreen22's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd June 2012
      Posts : 478
      Rep Power : 604
      Likes Received
      69
      Likes Given
      7

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Mi moja nililoliona ni zuri ni kuboresha baadhi ya ofisi za serikali, kumbuka kwa mfano jengo la Uhamiaji la Zamani na la Sasa, zamani ilikuwa kama stoo ya matoroli na mafagio ya kusafisha barabara za DSm bhana!
      Pasco likes this.

    20. #317
      Doreen22's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd June 2012
      Posts : 478
      Rep Power : 604
      Likes Received
      69
      Likes Given
      7

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Mi moja nililoliona ni zuri ni kuboresha baadhi ya ofisi za serikali, kumbuka kwa mfano jengo la Uhamiaji la Zamani na la Sasa, zamani ilikuwa kama stoo ya kuweka matoroli na mafagio ya kusafisha barabara za DSm bhana!
      Pasco likes this.

    21. #318
      Doreen22's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd June 2012
      Posts : 478
      Rep Power : 604
      Likes Received
      69
      Likes Given
      7

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Najisikia aibu sana ninapopita na mtu ambaye si Mmbongo eneo ambalo kuna ofisi ya serikali, mahakama au kituo cha polisi kilichochakaa mno, wengi wanaonyesha kushangaa, inabidi uzuge na stori nyingine za umbea
      Pasco likes this.

    22. #319
      Doreen22's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd June 2012
      Posts : 478
      Rep Power : 604
      Likes Received
      69
      Likes Given
      7

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Afadhali Mahakama ya Kisutu wameisitiri nje, but vituo vya polisi kama cha Kilwa Road, Oysterbay au Kawe, utafikiri stoo au Magofu fulani, hayavutii wala kupendeza kabisa, majengo na huduma ziboreshwe jamani
      Pasco likes this.

    23. #320
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default

      Quote By Doreen22
      Mi moja nililoliona ni zuri ni kuboresha baadhi ya ofisi za serikali, kumbuka kwa mfano jengo la Uhamiaji la Zamani na la Sasa, zamani ilikuwa kama stoo ya kuweka matoroli na mafagio ya kusafisha barabara za DSm bhana!
      Doreen, its always good to appreciate. Hata Mungu anapenda.

    Page 16 of 23 FirstFirst ... 61415161718 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...