Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

    Report Post
    Page 11 of 23 FirstFirst ... 91011121321 ... LastLast
    Results 201 to 220 of 442
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Wanabodi,
      Naangalia TBC Live, Rais Jakaya Kikwete yuko hewani!
      Miongoni wa mazuri ya JK, ni having a good sense of humour, akiongea, huchoki kumsikiliza!.
      Alipokuwa akiongelea kilimo cha ndizi kijijini kwao Msoga, Bagamoyo, akasema wakulima wana bananisha migomba mingi kwenye shina moja, matokeo yake kila mgomba unatoa kichane kimoja au viwili ya vindizi vilivyokondeana!.

      Akasema wanakijiji wale wanalima hivyo kwa sababu hawajui kuwa kama wakiacha mgomba mmoja kwenye shina moja, mgomba huo utatoa mkungu mkubwa wa ndizi, na ndizi zenyewe zitakuwa ni ndizi za shibe kama "Mrisho Mpoto"!. Ukumbi mzima ulizizima kwa vicheko, watu hawana mbavu!.

      Kuwa na 'good sense of humour' ni kipaji na ni miongoni mwa mambo mazuri machache ya rais wetu Jakaya Kikwete, besides good looking!.

      Kwa wale wenye kumbukumbu ya hotuba za Mwalimu, ukiondoa ile hotuba yake ya kutangaza vita, hotuba za Mwalimu, watu walikuwa wanacheka na hutamani amalize kuzungumza!.

      Hii ni thread ya miongoni mwa mazuri ya JK, kama na wewe unalo zuri lolote la JK ambalo unalijua, unaweza kuliweka.

      Kwa vile tunazungumzia mazuri, ningeomba wale ambao hawana zuri lolote la kuzungumzia JK, sio lazima mchangie, wala zuri hili la "good sense of humour", haimaanishi JK sasa ndio rais bora kwa Tanzania, wala haina maana ndio hana mabaya yake!, leo tuzungumzie mazuri yake!

      Angalizo:
      Wanabodi wenzangu, tunajukumu la kujimoderate sisi wenyewe kulinda hadhi ya jukwaa letu, haiwezekana kila siku sisi tukawa ni watu wa kulalamika tuu, au kubonda tuu, mara moja moja kwenye mazuri, pia tutoe sifa pale panapo stahili!.

      Natanguliza Shukrani kwa kunielewa!

      Asanteni!

      Pasco (wa jf)

      Note: Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali ni muumini wa ukweli "seek the truth, and the truth will set you free"!. Kwa wale wanaofikiri Pasco wa jf, ni mshabiki wa CCM, tafuteni thread yangu ya "CCM Imechokwa" !.


      --------------------------------------------
      Hoja Nyingine za Thread ya kibananhukhu iliyounganishwa #148
      Quote By kibananhukhu
      Pamoja na list ya mambo lukuki ambayo wakuu mnamlaumu JK, lakini ni kweli kuwa kuna kitu anafanya siyo kwamba amelele fofofo. Kuna mapungufu pia ni kwa nia njema mnayaainisha kusaidia uboreshaji kazi. Nimefuatilia na kuyaona baadhi ya mazuri ya JK Kama list inavyoainisha, ninaweza kuwa na upungufu kidogo katika takwimu hii itatokana na mimi kutumia kumbukumbu zangu nipo tayari kusahihishwa takwimu. Tupitie mazuri ya JK HAPA CHINI

      1. Mpango wa kuiruhusu bandari (THA) kufanya kazi kwa kuanza na technologia mpya ili dereva tu ndiye awe anakwenda bandarini kupakia mzigo na mengine yote yatamalizwa kwa njia ya mtandao, e-port. Kumbukeni TICTS walikuwa na mkataba mbaya sana kwa miaka 15, na ulirejewa kwa mazingira ya kutatanisha.

      2. Dar tayari nyumba 50 zimeanza kutumia gesi kwa matumizi mbali mbali ya ndani, kama ulaya na kwingineko kwa mara ya kwanza. Mikocheni wameanza jiandaeni kuvuta gesi majumbani kwenu.

      3. Magari yameaanza kutumia gesi japokuwa bado kuna baadhi ya vikwazo kwa wasaidizi wa raisi. Mpango wa JK ilikuwa matuzi ya petroli katika gari yapungue kwa 80%, lkn ukiritimba wetu umesababisha yapungue kwa 55%

      4. Kivuko na daraja kigamboni.

      5. Mradi wa daraja Maragalasi na lami Tabora – Itigi – Kigoma

      6. Ujenzi wa barabara lami kutoka Mombo, Mtibwa turiani, Kilosa, Mikumi na baadaye ifakara, mahenge, Malinyi, Songea. Pia Ifakara, Mlimba hadi Njombe. Usafiri wa songea kupunguza safari kwa masaa 5.

      7. Barabara ya Mafinga, Iringa, Kitonga, Ruaha Mbuyuni, Madaraja mawili mpakani na morogoro imekwishapanuliwa kwa uboro wa hali ya juu. Kipande cha Ipogolo kupandisha kwenda iringa mjini kimepanuliwa sana.

      8. Bara bara ya Iringa Kwenda Dodoma Imekwishaanza

      9. Bara bara ya Tunduma hadi Sumbawanga kuna makandarasi watatu wanashindana kwa ubora wa lami.

      10. Viwanja vya ndege mikoani kuboreshwa.

      11. Karekebisha mkataba wa Songas, ulikuwa hauruhusu mtu meingine yetote awaye kujenga tena bomba la gesi. Sasahivi wakuu mnaruhusiwa kujenga mabomba ya gesi kutoka Kusini.

      12. Mkataba wa wachina na serikali kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi dar ili kuzalisha MG 2900 za umeme dar.

      13. Barabara Dodoma, Manyara lami.

      14. Ujenzi reli kutoka Tanga, Musoma, Uganda.

      15. Ujenzi bandari, Tanga, Mtwara na Babamoyo

      16. Uwanja wa Ndege Terminal two wajengwa.

      17. Maeneo ya Umwagiliaji maji, hekari 20,000 zimejengwa na lengo ni ekari 1milioni.

      18. Kilimo kwanza mashamba darasa na ongezeko la mavuno kwa ekari.

      19. Tanzania ni ya kwanza kwa export afrika masharik na kati

      20. Mradi wa makaa ya Mawe Mchuchuma na katewaka liganga kuzalisha MGW za kutosha nchi nzima

      21. Mradi wa machimbo mgodi wa chuma Liganga, uzalishaji wa Titanium, Vanadium, Fe kwa ajili ya utengenezaji nondo, malighafi ya mabati, vyuma vya kujengea madaraja na maghorofa, kuweka pembezoni mwa mabarabara kuzalishwa nchini. Viwanda vya kutengeneza vifaa vya ujenzi wa meli, ndege, na magari kujengwa nchini.

      22. Machimbo ya makaa yam awe Ngaka Mbinga Ruvuma, uwezo Kuzalisha pia umeme MG 400.

      23. Hospitali upasuaji moyo kwa mara ya kwanza Tanzania.

      24. Hospitali kubwa mingoni mwa zitakazoheshimika kujengwa Tanzania na Appollo ya India. Maradhi yote kutibiwa Tanzania.

      25. Uboreshaji shirika la nyumba NHC, Baadhi ya watanzania kunufaika na mikopo ya nyumba na nyumba kuanza kujengwa kwa spidi kali.

      26. Ujenzi wa barabara nane Dar hadi chalinze.

      27. Ufumuaji na ujenzi wa reli ya kati dar, hadi kigoma, mwanza, mpanda, Rwanda na Burundi.

      28. Ubareshaji maabara shule za kata ($ 90Milioni)

      29. Idadi ya walimu kwaajili ya shule za kata na nyinginezo kuanzia muda mfupi ujao, walimu elfu 40 kuhitimu kila mwaka.

      30. Baadhi ya shule nyingi binafsi zimeanza kudorola au kufungwa kabisha, wengi wamejiunga na shule za kata na ubora unapanda japo kwa spidi ndogo.

      31. Idadi kubwa ya wanafunzi vyuo vikuu, Udom uwezo elfu 40, SAUT elfu 15, UDSM Elfu 15, Ruco elf 2.5, Mkwawa elfu 2.5 Tumaini elfu 2, Open University elfu 20 nk.

      32. Wafanya biashara wamepewa kipau mbele term ya JK, Wengi husafiri na Mheshimiwa Raisi kutafuta na kupata fursa za biashara nje.

      33. Uhuru wa Vyombo vya habari, waandishi wanafanya mambo kwa uhuru ambao wasingelithubutu enzi ya Mwalimu, Mwinyi wala Mkapa. Hata baadhi ya ninyi wakuu, mnaruhusuwa kutoa mawazo yenu japo wengine wanatukana matusi ya nguoni lakini JK anavumilia sana.

      34. Amegundua fitna nyingi sana serikalini, majungu, uongo na sasa hivi anakua mwangalifu sana katika maamuzi na inalazimika kuonekana kana kwamba hana maamuzi ili awe na subira. (Ukiwa na hasiri usifanye maamuzi, ahirisha upate busara)

      35. Makampuni ya madini, yamekupali kuanza kulapa 30% kutoka faida zitakazo patikana kuanzia 2012.

      36. Wapinzani wameanza kumwelewa na kumsifia kwa yale anayoyafanya vizuri.

      37. Mnaweza ongeza list nyingine ili nije baadaye na listi ya faida za kiuchumi kwa taarifa tu, inflation inachangiwa na gharama za chakula kwa 16%.

      Kuna mambo madogo ya kiufundi yakirekebishwa inflation inapashwa iwe 8% single digit. Mfano mahindi yanaoza Ruvuma, Iringa, na Sumbawanga yangeweza kutoa mchango katika kupunguza gharama za chakula na mfumuko wa bei ukashuka.Mengine mengi nitaongeza baadaye. Nadhani kwa faida ya wakuu wangu, nitajitahidi kufuatilia pia ilani yake ili nilinganishe na hayo hapo juu. Hata hivyo, ni ukweli kwamba kwa upanda wa barabara tu, miaka 50 tangu uhuru lami ilifikia km 6000, JK Pekee ameweka mikataba ya lami km 11,000.

      Kuna vitu anafanya JK.
      Last edited by Viwango; 6th March 2012 at 11:52. Reason: Adding points of merged thread

    2. FemaTV & Radio

    3. #201
      Maundumula's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 4,920
      Rep Power : 3095
      Likes Received
      1339
      Likes Given
      5654

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Jk ni kiongozi shupavu, Kwa sababu ameingia madarakani kakutana na ujambazi umeshika kasi, EPA ikabumbulika, Ukame ukafuatiwa na mgao wa umeme,likaja baa la njaa ukame mkali nk kwahiyo miaka 5 ya kwanza ni changamoto nyingi mnoo! Kwakuwa tuli prevail kwenye mengi ktk haya lazima nimpe credit japokuwa swala la umeme bado!

    4. #202
      Marukangasi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th March 2012
      Posts : 13
      Rep Power : 365
      Likes Received
      4
      Likes Given
      1

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Usalama hususani katikati ya majiji makuu Kama Dar es salaam ,Mwanza,Arusha ujambazi umepungua sana,Hilo kwa kweli muheshimiwa anastaili ,pongeze. Lakini yeye Kama mwislamu hajawahi kusikika akisema hata neno alhamdulilah,au sehemu ya mtume (S.A.W) yeye anasema subhanau wataala,lingine analostaili pongezi watu wengi walikuwa wameisha anza kuwa na nyodo na kujifanya wanazo hata za kuhesabia mate(pesa) lakini katika kipindi chake hiki wamerudia Hali zao za zamani a.k.a uchovu waliokuwa nao zamani

    5. #203
      Ulimakafu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2011
      Location : Itabanya Balasi
      Posts : 10,944
      Rep Power : 2602
      Likes Received
      690
      Likes Given
      1615

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Mazuri mengine?

    6. #204
      ipogolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th August 2011
      Posts : 356
      Rep Power : 464
      Likes Received
      48
      Likes Given
      35

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Mh Jakaya mrisho Kikwete ni kiongozi mzuri.Mheshimiwa JK ni shupavu panapobidi, ni jasiri akilazimika kuwa jasiri. . watanzania 80% walimkubali 2005 wakampa kura. Sitaki kusikia lugha ya kuiba kura. mwaka 2010 kura zilipungua lakini zikatosha. Hadi leo hii, Jk akipita sehemu ya watu waungwana wanaotaka kumsalimia wanajitokeza maelfu. Maana yake nini: wengi wanampenda iwe kwa tabasamu ucheshi watu wengi wanampenda. hata ucheshi ni sifa ya uongozi sio. Leaders are born. hiyo ya leaders are made ina nafasi kidogo sana. NABII KWAO HAKUBALIKI.

    7. #205
      FireMan's Avatar
      Member Array
      Join Date : 11th March 2012
      Posts : 15
      Rep Power : 366
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Rais wetu anapenda ngonjera, methali na vijembe!
      Hii sifa inayowafanya watu wampende hata kama nikatka hali ya chukizo!
      Mfano mzuri kipindi kile amewaambia wafanyakazi wawe kama Mbayuwayu.

    8. Miaka 50

    9. #206
      msomi kweli's Avatar
      Member Array
      Join Date : 8th February 2012
      Posts : 25
      Rep Power : 373
      Likes Received
      6
      Likes Given
      33

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      na mimi niseme
      • kukubali kukaa na chama kikuu cha upinzani(CHADEMA) na kuongelea mustakabali wa nchi na kuachana na mambo ya bla! bla! za bunge la CCM
      • kuwa mpole na kukubali watu waondoe misongo kwa kuongea kwa uhuru
      • kushiriki kwenye MISIBA hata midogo kwa jamii


      kwa kweli huyu ni mtu muhimu sana. anafaa kuigwa na viongozi wengine

    10. #207
      mmbangifingi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2011
      Posts : 2,568
      Rep Power : 857
      Likes Received
      452
      Likes Given
      2906

      Default JK Rais na mtu wa watu?

      Hali ya watu kada mbalimbali kutaka kuonana na Mh Rais imeongezeka. Kuna wakati jamaa mmoja aliendesha baiskeli kutoka Shinyanga mpaka Ikulu kwa nia ya kumsalimia. Vyama vya siasa kwa nyakati tofauti vimeonana nae na kuzungumza nae mambo tofauti tofauti ikiwemo suala la Katiba Mpya. Siku c nyingi ujumbe wa wazee kutoka Kyela ilikuwa waende Ikulu kumwona na kuzungumza nae kuhusu hali ya kiafya ya Naibu Waziri na Mbunge wao Dr Mwakyembe. Madaktari nao walipogoma hawakuwa tayari kuonana na yeyote bali JK jambo ambalo lilifanyika.


      Ni kwa sababu JK ni mtu wa watu mwenye utayari wa kukutana/kujadili lolote na yeyote au ni hali ya Wananchi hawa kukosa imani na wawakilishi/Wateule wake katika kutatua shida mbalimbali katika nyanja tofauti zinazowakabili?
      Who Jah bless, No one Curse!

    11. #208
      collezione's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd October 2010
      Posts : 347
      Rep Power : 504
      Likes Received
      132
      Likes Given
      3

      Default Re: JK Rais na mtu wa watu?

      Mwambie awaite na Tanesco waeende IKulu kuongea nae. Nahisi nao wana dukuduku

    12. #209
      LiverpoolFC's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th April 2011
      Posts : 6,676
      Rep Power : 11278
      Likes Received
      1473
      Likes Given
      570

      Default Re: JK Rais na mtu wa watu?

      Ni wanainchi kukosa IMANI nao na ndio mana wanataka kuwaelezeni yalio ktk mioyo ya wanainchi Watanzania wazalendo na wenye uchu na Nchi yao.

      My take:
      Kuna kilometre ngapi toka Mkoani Shinyanga mpk Dar es salaam ambapo yule Mwanainchi alipiga pedo ya baiskeli mpk akafika?

      Tuna hasara na chama tawala sana!
      Na kwa ujumla ni JANGA KUU kwa Nchi yetu yenye Asali na Maziwa lakini imekwamia mikononi mwa watu 20 kt ya watu 42 milioni wanaotegema uhalisia wa Nchi yetu!

      TOO MUCH!

    13. #210
      Young Tanzanian's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2012
      Posts : 564
      Rep Power : 475
      Likes Received
      45
      Likes Given
      49

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Hatutaki muonekano mzuri tuantaka utendaji ata kama unajipendekeza kwake lakini bado yote hiyo ni miradi ya mkapa hakuna kpya ...pascal upo kmaslahi wambie ulishapost watanzania wakakataa
      nawasilisha
      Kaa la Moto likes this.

    14. #211
      Young Tanzanian's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2012
      Posts : 564
      Rep Power : 475
      Likes Received
      45
      Likes Given
      49

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Nazan kusema JK ni mtu wa watu si hoja ya kujadili kwan alijichagua kwenda ikulu mlitegemea awe mtu wa wanyama?jadilini matatzo ya kweli watoto wadogo ni mabilionea bila ata kuwa na ofsi wakati vyuo vkuu wanavyuo hawana mikopo ...maosptalini madaktari bngwa wanavaa ngoz kwenye upasuaji unatuletea habari za kilometa za barabara kama ni kutaja tu ata magufuli ana uwezo wa kuztaja ata usngzin watanzania tusiwe wanafki hakuna kpya kilichofanyika zaid ni kubebana,,
      Kaa la Moto likes this.

    15. #212
      Mamushka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th February 2010
      Posts : 1,613
      Rep Power : 792
      Likes Received
      86
      Likes Given
      141

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Tuna Rais mzuri wa sura he is handsome, ndo ninachokijua, haaa haaaa!
      Not every closed door is locked.

    16. #213
      idawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2012
      Posts : 4,592
      Rep Power : 3332
      Likes Received
      1220
      Likes Given
      461

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      kwanza heshima yake...kwa kuachia demokrasia ya uhuru wa kuongea sasa hivi unaweza kuongea lolote na muda wowote na usifanywe lolote... mtu anaweza kusema watanzania tumeelika ni kweli lakini tujiulize ni nchi ngapi duniani pamoja na kuelimika na kuendelea kiuchumi lakini hazina uhuru wa kuongea kama tz...kuhusu siasa wanasiasa wako huru sana kufanya siasa japo vinatokea vitisho vya hapa na pale na wenye hofu zaidi ni wale wasaidizi wa rais japo rais mwenyewe hana presha na wapinzani. Ndo maana leo ni rahisi kuona wapinzani wakitaja mafisadi bila woga japo ugumu upo kwenye kuwachukulia hatua mafisadi.sasa hivi ni nadra kusikia mpinzani amevunjwa mkono...tumeshuhudia bwana mbowe akibebwa na ndege ya jeshi na ulinzi mkali na wa heshima kupelekwa mahakamani kitu ambacho ni nidra.japo kwenye hili la upinzini nafikiri polisi ndio wanamfanya aonekana mbaya nadhani hii ni kutokana na shinikizo kutoka kwa viongozi wa ccm.tunashukuru kwa kukomesha ujambazi japo saizi majambazi wakubwa ni polis na hii inatokana na viongozi wa juu kufanya ufisadi ni umataduni. kwa wafanyakazi wa kada za chini kupata hasira na kufikia hatua ya kulazimisha rushwa. Mwisho wa yote kila zama na kitabu chake.!!!

    17. #214
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default

      Quote By Young Tanzanian
      Hatutaki muonekano mzuri tuantaka utendaji ata kama unajipendekeza kwake lakini bado yote hiyo ni miradi ya mkapa hakuna kpya ...pascal upo kmaslahi wambie ulishapost watanzania wakakataa
      nawasilisha
      Mkuu Young Tanzanian, kwa hiyo unamaanisha mimi ndio najipendekeza kwa JK?, na niko kimaslahi zaidi?. Fafanua!.

    18. #215
      Kaa la Moto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th April 2008
      Location : Bristol
      Posts : 6,830
      Rep Power : 1945
      Likes Received
      431
      Likes Given
      4213

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Ni rais aliyependa kutalii dunia nzima hata kama wanachi wake wanakufa kwa malaria tu. Nitamkumbuka sana kwa zuri hilo!
      wakati Cuf wanataka kuchukua nchi mwaka 2000 CCM walikuja na single ya kusema Cuf ni waislamu na kwa sasa wanadai sisi Chadema ni chama cha wakristo sasa CCM nacho ni cha watu gani? Watu wakajibu mashetaaaaaniiiiii.!---Wana Kigoma.

      ....Pamoja na kansa ya uongozi wa CCM watu wataendelea kukichagua,au watu wanaweza wakachoka na kusema potelea mbali wakachagua chama KINGINE....Julius. Kambarage. NYERERE"

    19. #216
      Ng'wanangwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th August 2010
      Posts : 5,976
      Rep Power : 1644
      Likes Received
      1133
      Likes Given
      410

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Quote By Pasco
      Kwa vile tunazungumzia mazuri, ningeomba wale ambao hawana zuri lolote la kuzungumzia JK, sio lazima mchangie, wala zuri hili la "good sense of humour", haimaanishi JK sasa ndio rais bora kwa Tanzania, wala haina maana ndio hana mabaya yake!, leo tuzungumzie mazuri yake!
      kusariri marakwa mara bila tija yoyote ni jambo zuri au baya?

      nataka kuchangia.
      CCM HAIKUBALIKI ...TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA...

      REST IN PEACE, DR.D.D. HAULE...Wema hawana Maisha

    20. #217
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default

      [QUO TE=Ng'wanangwa;3514387]kusafiri mara kwa mara bila tija yoyote ni jambo zuri au baya?

      nataka kuchangia.[/QUOTE]
      Ng'wanangwa mwana wane, rekebisha basi post yako, nimekurekebishia, wewe ibilizia!.

      Hakuna safari bila tija, hata kubadili tuu hali ya hewa ni tija iitwayo "refreshing"!. Kitendo tuu cha kunyanyua mguu kukwea pipa ni "adivencha!". Kula na kulala hoteli nzuri inaitwa "rekiriesheno" na kutulia kukodolea majengo, miji, mitaa iliyopendezea unapata kitu inaitwa "sereniti" ambavyo vyote hivi rais wetu anavigitaji ili atawale vyema!.
      Last edited by Pasco; 17th March 2012 at 14:17.

    21. #218
      Eliaona's Avatar
      Member Array
      Join Date : 22nd June 2009
      Posts : 28
      Rep Power : 510
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      May be another good thing about Kikwete is: He is just about to leave the Office of the President. There can't be anything better than that.

    22. #219
      bona's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th November 2009
      Location : tanzania
      Posts : 982
      Rep Power : 681
      Likes Received
      85
      Likes Given
      235

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      Kwa mantiki hiyo kipaji chake cha kuchekacheka kingetumika vizuri kwenye maigizo kuliko kuongelea kipaji kama hicho kwenye nafasi ya mtu aliyepewa dhamana ya kuliongoza taifa maskini kama hili!
      ... if it is a Miracle, any sort of evidence will answer, but if it is a Fact, proof is necessary.

    23. #220
      chumvichumvi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2010
      Location : Kwenye Mapambano
      Posts : 354
      Rep Power : 529
      Likes Received
      42
      Likes Given
      41

      Default re: Miongoni Mwa Mazuri ya Kikwete: "Has Good Sense of Humour"

      JK hamna ki2 .....

    Page 11 of 23 FirstFirst ... 91011121321 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...