Maelezo hapo chini nimeyatoa kwa KICHUGUU kwenye thread yenye kichwa chenye maneno Administrator wa JF ni Mkali.
Nataka TUJUKUMBUSHE ambao hatujachangia (mie pia bado) kuwa mkono mtupu haulambwi. Kazi wanayofanya hawa jamaa si ndogo. Kuna muda nilikuwa na matatizo ya computer, basi Invisible aliichukulia kama ni shida yake. Akawa tayari hata kunitafutia watu waje warekebishe matatizo kwenye computer yangu. Kama CCM wangelijali watu wao walau nusu ya hii basi tungelikuwa mbali. Sasa na yote haya jamaa kujitolea, nafikiri hizi mashine zinahitaji matengenezo ya aina mbalimbali na kuifanya iwe up-to-date. Na kila mtu anajua kuwa kila miezi mitatu, vinatoka vitu vipya na bei yake si znuri sana. Hivyo kama hujasaidia JF basi shime shime tuchangie BANDUGU.
Kwa maana hii mchango na mimi mwaka huu naanza kuchangia.
Invisible nilikuahidi kuwa ntaleta mchango wangu mwenyewe nikiwa Dar ila naona sintaweza au nikaja mwisho wa mwaka. Pesa kidogo tayari zipo Dar na hapo Sister wangu atakuleteeni. Unaweza kunitumia anwani yenu na nani wa kumuona ili akija akupatieni hako kamchango kiduchu!!!Niandikie kwenye PM.
NB:- Mods, baadaye waweza zichanganya na ile ya Kichuguu.
Quote: Napenda kuapa kuwa JF ni forum ambayo inaendeshwa vizuri sana. Admin wa JF ana-respond kwa kila ombi in time. Kukitokea out-of-direction thread, anaishugulikia ipasavyo kabla hijawa kero kwa forum nzima. Ilivyofika wakati wa kipindi cha holidays ali-respond vizuri tukawa na skin ya Chrsimas halafu ikaja skin ya New Year na leo skin yetu ya Tanzania Tanzania Nakupenda kwa Moyo Wote imerudi tena. Nahisi amejenga system nzuri sana kwa kutumia OOP akaweka na objetcs nzuri sana kiasi kuwa haoni ugumu kubadili mambo ikiwa lazima.
Kwa vyovyote vile, ameweka muda wake mwingi ili kuifanya JF iwe sehemu nzuri ya mtu kutumia muda wake hata kama hupendezwi na yanayoongelewa. Mod anastahili pongezi nyingi sana.
__________________ .... hata kama akitambika uchi huyu mwakyembe, ukweli utabaki pale pale kuwa yeye nimiongoni mwa wale wabunge waliokula milioni 5 za rostam wakati wa kampeni (By: Game Theory)
Last edited by Sikonge; 15th February 2010 at 07:02 PM..
Jamani kwa member wote mnao faidi na msio faidi hapa Jamvini naomba kutangaza dau kuwa j3 nita deposit sh.20000/= kama mchango wangu hapa JF naombeni wahusika tukumbushane tu j3 mi nakabidhi kwa Maxelo au nitapeleka BANK kama hakutakuwa na foleni maana vibank vyetu siku ya j3 kuna kuwa na foleni za ajabu.
__________________ Ukiuza utumbo usiogope nzi. Chuda Raha
Jamani kwa member wote mnao faidi na msio faidi hapa Jamvini naomba kutangaza dau kuwa j3 nita deposit sh.20000/= kama mchango wangu hapa JF naombeni wahusika tukumbushane tu j3 mi nakabidhi kwa Maxelo au nitapeleka BANK kama hakutakuwa na foleni maana vibank vyetu siku ya j3 kuna kuwa na foleni za ajabu.
Ishalaah, utakumbushwa!..Bora uwasiliane na Maxelo,kama bank kuna foleni tena jumatatuz umtumie yeye kwa ile huduma ya vodafasta(kama bado ipo)..
__________________ Giving up doesn’t always mean you are weak,sometimes it means that you are strong enough to let go!....
Jamani kwa member wote mnao faidi na msio faidi hapa Jamvini naomba kutangaza dau kuwa j3 nita deposit sh.20000/= kama mchango wangu hapa JF naombeni wahusika tukumbushane tu j3 mi nakabidhi kwa Maxelo au nitapeleka BANK kama hakutakuwa na foleni maana vibank vyetu siku ya j3 kuna kuwa na foleni za ajabu.
Mwaveja sana mwanawane......tutakustua tu kaka!
__________________ “Without leaps of imagination, or dreaming, we lose the excitement of possibilities. Dreaming, after all, is a form of planning - GLORIA STEINEM.
Jamani mie naahidi Tzs 10,000/= ntatuma kwa njia ya sms. Kujiwekea cover vizuri ntanunua sim card ya mia tano mpya ntaandika jina langu la Mzizi kwenye sms hiyo na kuhakikisha Max kishapata pesa hiyo, sinta itumia kwa mtu mwingine yeyote! then ntaivunja hiyo sim card,...UWT wasumbufu sana!
Jamani wakuu nime feel guilty sana kwa kuwa sijachangia my lovely JF hadi leo. Nina moyo wa kuchangia sema najisahau. Ila ningependa kuchangia kwa anonymity. Sasa Maxence na Invisible je ninaweza kutuma kwa kutumia jina bandia? If so then nijulishe mapema ili by next week ni deposit.
Pia wana JF naamini members wote, wawe wa mrengo wa kulia au kushoto, sote tunafaidika na hii forum. Mexence Melo ameamua kuacha kazi rasmi (kuajiriwa) ili aweze kutumia muda wake kwa ajili ya Forum hii. Huu ni uzalendo wa hali ya juu. At the same tima atahitaji fedha kwa ajili ya kendesha maisha yake i.e compensation for his salary forgone. Ninashauri wote tuweze kuchangia michango meaningful ili angalao tuweze kugharamia administrative costs za JF. Kama alivyosema member hapo juu tuko wanachama 5000 na bado wapya wanajinga, hivyo imagine kila member mwenye wezo kifedha akichangia kuanzia 100,0000/= na wenye average income akichangia between 50,0000 - 90,000= na waliobaki wakichangia kuanzia 5,000 -40,000. Pia wale ambao wanaweza kchangia zaidi ya 100,000/= ni vizuri sana na tunawashukuru. Kwa hakika tungepata fedha ya kutosha kiendesha JF bila tabu ya fedha.
Nimechukua Bank account nasubiri Max an Invisible mni PM taratibu za kutuma as anonimous. Then nikishatuma nitawa PM kwa my nick kwa ajili ya records. Thanks.
Jamani wakuu nime feel guilty sana kwa kuwa sijachangia my lovely JF hadi leo. Nina moyo wa kuchangia sema najisahau. Ila ningependa kuchangia kwa anonymity. Sasa Maxence na Invisible je ninaweza kutuma kwa kutumia jina bandia? If so then nijulishe mapema ili by next week ni deposit.
Mkuu Maane, God bless you kwa kuchukua hatua ya kuchangia JF! I know,members wengi wanawasiwasi kujulikana ID zao sio pekee yako!
Mkuu ukisoma post ya Invisible pale mwanzoni utaona Max anasema unaweza kumtuma hata jamaa mwingine tu bank akadeposit hela kwa kutumia hata ID ya say MAANE au other name unayoitaka wewe....then umjulishe MAX kuwa umedeposit kusudi a confirm kwa kuangalia Bank statement yake.....!
So mkuu just go ahead, ofcourse Max na Invisible wanaweza kusaidia zaidi namna ya kudeposit cash mkuu!
Once again tuhamasishane zaidi kuchangia JF ili iendelea kutupatia uhondo huu.......!
Cheers
__________________ “Without leaps of imagination, or dreaming, we lose the excitement of possibilities. Dreaming, after all, is a form of planning - GLORIA STEINEM.
Mkuu kidogo kidogo hujaza kibaba....tuwe na mioyo ya kuchangia si harusi tu wakuu.
Hapo kny bold mkuu, huwa na shangaa sana yaani wabongo kny harusi, sijui send off party etc utaona jamaa wanapledge hadi 1mill but when it comes to issues za maendeleo e.g kumchangia mwanajamii akasome....and the likes humwoni mtu aisee......ivi kwa nini inakuwa hivyo?
__________________ “Without leaps of imagination, or dreaming, we lose the excitement of possibilities. Dreaming, after all, is a form of planning - GLORIA STEINEM.
Ikumbukwe, SI LAZIMA kuandika jina lako la kweli na SI LAZIMA kwenda mwenyewe bank kutuma pesa hizo (kwani unaweza kumpa unayemwamini na kumpa account details na jina lako ambalo ungependa aandike).
Tunaweza kuandika mengi lakini ukweli unabakia pale kuwa JF inahitaji michango yenu kwa sana tu.
Kwa wenye maswali zaidi wanaweza kuwasiliana na Maxence kupitia namba yake ya simu +255713444649.
Asante mkuu,nilikuwa sijui namna ya kuchangia,naomba mnisamehe kwa kutumia huduma hii muhimu bure. Kiasi cha chini ulichoandika wengi wetu tunaweza. Asante,nikifika Dsm nitajitahidi kuchangia kupitia kwa MM (crdb).
Mkuu Junius, kwanza kabisa kumbuka kuwa umeweza kuandika ulichoandika kwa sababu tu kuna watu wamekuwezesha kufanya hivyo hapa JF.....! Sasa kama unataka uendelea kuwezeshwa kufanya hivyo, please tunaomba pledge yako ya hiari kuisaidia JF kuwa hewani!
Pili, ungeweza kutoa dukuduku zako kule kwenye compaints na ungesaidiwa vizuri sana mkuu! Hii thread ni kwa ajili ya fund raising na kutoa maoni ya jinsi ya kuiwezesha JF ijiendeshe mkuu!
Nawatakeni radhi,
Nilikuwa sjaielewa hii thread (I was confused).
am deeply sorry