Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

    Report Post
    Page 7 of 14 FirstFirst ... 56789 ... LastLast
    Results 121 to 140 of 273
    1. #1
      EasyFit's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2011
      Posts : 832
      Rep Power : 565
      Likes Received
      572
      Likes Given
      196

      Default Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      Quote By Mchaga 25
      Amini usiamini wale walioko ndani na system wamelitambua, mkuu wa kaya akiri kabisa mambo hayaendi, kufuatia mfumuko wa bei, kuporomoka shilling kwa mara ya pili, kupanda kwa bei ya mafuta tunapo kutarajia hivi karibuni, migomo inayojiri na ambayo usalama wa taifa wa wamesha tahadharisha kuwa iko likely kutokea mwanzoni mwa mwezi wa pili.

      Busara za wadau wengine zinaanza kutafutwa, hakika tuko pabaya.

      KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini na kuchukua hatua za haraka kurejesha amani kabla Watanzania hawajaishiwa uvumilivu na utawala wa serikali yake.

      Dk. Slaa amesema kuongezeka kwa matukio ya matumizi ya nguvu ya dola katika kulinda uhalali wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kufikia hatua ya kuua watu wasiokuwa na hatia, yanadhihirisha kuwa muda si mrefu ujao nchi itakuwa haitawaliki tena ikiwa Kikwete ataendelea kufumbia macho mauaji hayo.

      Akifungua Ofisi ya Baraza la Vijana wa chama hicho (Bavicha) Mtaa wa Togo, Dar es Salaam jana, Dk. Slaa alisema kuwa mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola chini ya serikali ya CCM kupitia kwa viongozi wake hususan Jeshi la Polisi, hayawezi kuvumilika tena na yanawasukuma wananchi kufikia mwisho wa uvumilivu.

      Alisema sasa kuna dalili zote za wazi zinazotishia amani na mustakabali wa nchi na watu wake, zikiifanya nchi isitawalike, na wala serikali haiwezi tena kukwepa lawama za kuhusika na mauaji ya wananchi, na kutolea mfano wa tukio la kutwangwa risasi kwa watu wanne wasiokuwa na hatia waliokuwa wakiandamana kudai haki ya kulindwa na serikali yao mkoani Ruvuma mapema wiki hii.

      Dk. Slaa akizungumza kwa uchungu alisema mauaji ya Songea yalitokana na uzembe wa hali ya juu wa viongozi wa serikali na vyombo vya dola ngazi ya wilaya na Mkoa wa Ruvuma.

      “Napenda kutoa kauli juu ya mauaji dhidi ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi huko Songea. Kwa taarifa nilizonazo, mauaji yale yametokea kwa sababu ya uzembe wa hali ya juu na ufinyu tu wa akili ya viongozi, akiwamo mkuu wa Mkoa na polisi wale. Hivi unawaambiaje raia wenye uchungu na vifo vya wananchi wenzao, waliojikusanya na kuamua kuandamana kudai haki, eti wachague kiongozi wa kuonana na mkuu wa mkoa,” alisema.

      Aliitaka serikali kuunda tume huru ya kuchunguza mauaji hayo ya Songea na kudai kuwa hakuna uhalali wowote wa viongozi wa serikali wa mkoa ambao ni watuhumiwa wa mauaji hayo kuunda chombo cha kuchunguza.

      “Tunawapongeza wananchi na hasa vijana wa Songea kwa kuandamana kudai haki. Tunataka ufanyike uchunguzi huru juu ya mauaji hayo, yatakayoihusisha mahakama (Korona) na mkuu wa mkoa na polisi hawana uhalali wa kuunda tume za kuchunguza kwani wao pia ni watuhumiwa katika tukio hilo,” alisema.

      Katibu mkuu huyo wa CHADEMA alilaani tukio la juzi usiku, ambapo polisi katika mji wa Tunduma wanadaiwa kushusha bendera za chama hicho katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

      Alisema kitendo hicho ni uchokozi tosha kwa CHADEMA na kimelenga kuleta fujo nyingine zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani.

      “Niliwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, pia mkuu wa mkoa, niliwaambia mimi sipendi kugombana nao kwa masuala ya hovyo kama hayo, tupo kwa mujibu wa sheria, bendera zetu zinatokana na kodi za Watanzania, wakasema eti zingine ziko sokoni, nikawauliza za CCM huwa zinawekwa wapi?

      “Watu hawana maji, hawana zahanati, elimu inashuka, mkuu wa wilaya hajawahi kuamuka usiku, lakini kwenye kushusha bendera za CHADEMA wanaamka usiku wa manane,” alisema.

      Alitumia wasaa huo kuwataka vijana wa CHADEMA wasimamie haki na kupinga dhuluma na uonevu popote pale wanapofanyiwa Watanzania na wahakikishe wanajua kinachoendelea katika maeneo ya Songea na Tunduma ili chama hicho kijue hatua za kuchukua.

      Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche, mbali ya kumshukuru Dk. Slaa na makao makuu ya chama hicho kwa kuwawezesha kuwa na ofisi yao, alisema kuwa watakuwa mstari wa mbele kusimamia malengo ya chama hicho hasa katika kutetea haki za Watanzania, kudai uwajibikaji wa viongozi na serikali kwa wananchi, pia kulinda rasilimali za taifa.

      Alisema kuwa vijana watakuwa mstari wa mbele katika vuguvugu la mageuzi yanayoendelea nchini, akisema kuwa ofisi hiyo itakuwa sehemu sahihi ya kuendeshea mipango ya ukombozi wa taifa ambalo pamoja na utajiri wa rasilimali za kila aina, bado wananchi wake wanaishi katika umaskini wa kupindukia.
      DEUS NSHANGE and kygrykos like this.

    2. Miaka 50

    3. #121
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,484
      Rep Power : 6170
      Likes Received
      3058
      Likes Given
      1020

      Default

      Quote By Mag3
      Historia inatakiwa itufundishe lakini mmm! wengi wetu ni viziwi. Hebu tujikumbushe kidogo tarehe 25 December, 1989 wananchi wa Romania walipomchoka aliyekuwa Kiongozi wao Nikolai Ceusesku pamoja na mkewe Elena.



      Iko siku!

      Nakumbuk alikuwa tu ametoka ziarani nchini Tanzania. Nakumbuka kumpungia mkono pale msimbazi roundabout. Mkuu watu wake walikuwa wamezichoka siasa za kikomunist na walichochewa na kuanguka kwa USSR; sijui kama ina uhusiano na huu uzi.

    4. #122
      Mag3's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 31st May 2008
      Posts : 3,540
      Rep Power : 1805
      Likes Received
      2464
      Likes Given
      2504

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      Quote By Kimbunga
      Nakumbuk alikuwa tu ametoka ziarani nchini Tanzania. Nakumbuka kumpungia mkono pale msimbazi roundabout. Mkuu watu wake walikuwa wamezichoka siasa za kikomunist na walichochewa na kuanguka kwa USSR; sijui kama ina uhusiano na huu uzi.
      Hapana Mkuu, Soviet union ilianguka miaka miwili baada ya mapinduzi ya Romania. Somo nililotaka kulitoa ni kuwa ilifika wakati ambapo hata jeshi lake alilolitumia kukandamiza watu wake waliweka silaha chini na kusalimu amri kwa Umma. Huko ndiko tunakoelekea kwa hivi sasa - hata mbwa iko siku anaweza kumgeuka bwanake na kumng'ata!
      Jasusi likes this.
      The true sign of intelligence is not knowledge but imagination.
      Education is what remains after one has forgotten what one has learned in School
      -Albert Einstein.


    5. #123
      Ronal Reagan's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 2,636
      Rep Power : 961
      Likes Received
      615
      Likes Given
      256

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      [QUOTE=EasyFit;3389202]Dk. Slaa akizungumza kwa uchungu alisema mauaji ya Songea yalitokana na uzembe wa hali ya juu wa viongozi wa serikali na vyombo vya dola ngazi ya wilaya na Mkoa wa Ruvuma.

      “Napenda kutoa kauli juu ya mauaji dhidi ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi huko Songea. Kwa taarifa nilizonazo, mauaji yale yametokea kwa sababu ya uzembe wa hali ya juu na ufinyu tu wa akili ya viongozi, akiwamo mkuu wa Mkoa na polisi wale. Hivi unawaambiaje raia wenye uchungu na vifo vya wananchi wenzao, waliojikusanya na kuamua kuandamana kudai haki, eti wachague kiongozi wa kuonana na mkuu wa mkoa,” alisema.

      Aliitaka serikali kuunda tume huru ya kuchunguza mauaji hayo ya Songea na kudai kuwa hakuna uhalali wowote wa viongozi wa serikali wa mkoa ambao ni watuhumiwa wa mauaji hayo kuunda chombo cha kuchunguza.

      “Tunawapongeza wananchi na hasa vijana wa Songea kwa kuandamana kudai haki. Tunataka ufanyike uchunguzi huru juu ya mauaji hayo, yatakayoihusisha mahakama (Korona) na mkuu wa mkoa na polisi hawana uhalali wa kuunda tume za kuchunguza kwani wao pia ni watuhumiwa katika tukio hilo,” alisema.

      Katibu mkuu huyo wa CHADEMA alilaani tukio la juzi usiku, ambapo polisi katika mji wa Tunduma wanadaiwa kushusha bendera za chama hicho katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

      Alisema kitendo hicho ni uchokozi tosha kwa CHADEMA na kimelenga kuleta fujo nyingine zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani.

      “Niliwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, pia mkuu wa mkoa, niliwaambia mimi sipendi kugombana nao kwa masuala ya hovyo kama hayo, tupo kwa mujibu wa sheria, bendera zetu zinatokana na kodi za Watanzania, wakasema eti zingine ziko sokoni, nikawauliza za CCM huwa zinawekwa wapi?

      “Watu hawana maji, hawana zahanati, elimu inashuka, mkuu wa wilaya hajawahi kuamuka usiku, lakini kwenye kushusha bendera za CHADEMA wanaamka usiku wa manane,” alisema.


      DR. SLAA ni zaidi ya Rais kwa kazi azitendazo. I'm very impressed with his bolded quotes.

    6. #124
      MNYISANZU's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 6,311
      Rep Power : 0
      Likes Received
      592
      Likes Given
      76

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      Heko Dr Slaa. JK ni robot ambalo halijitambui hata kidogo.

    7. #125
      KASHOROBANA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th July 2011
      Posts : 1,463
      Rep Power : 687
      Likes Received
      233
      Likes Given
      86

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      Jk ni mtu wa ajabu, hii nchi ilisha mshinda kitambo, na ndo kaamua kuwa mzululaji na mbaya zaidi anatumia kodi zetu, nasikitika kwa walompigia kura na kumchagua na wanaoendelea kushabikia ccm magamba laana hii wanayo kwani shida, maisha magumu, ufisadi na wizi unaolitafuna taifa ni wazi wao wamechangia pakubwa katika hili, so wajijue kwa kuchangia aya madhira, laana pia dhambi lazima nao wanapata

    8. RukaaJuu Final

    9. #126
      cjilo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th September 2011
      Location : Behind you
      Posts : 391
      Rep Power : 468
      Likes Received
      119
      Likes Given
      157

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      dr sijui huwa anaandaliwa yakuongea kwa watu, da maana hakuna siku aliyoshindwa kunikosha nafsi kwa kukemea ujinga wa jk
      liwalo na liwe

    10. #127
      Hakikwanza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th December 2010
      Posts : 1,107
      Rep Power : 2653
      Likes Received
      147
      Likes Given
      18

      Default

      Quote By ENGINE CONTROL
      Tanzania ni nyepesi sana na wananchi wake tupo tupo tu ndiyo mana ccm inafanya lolote wawezalo wakijua na kuamin kuwa hatuna lolote la kuwafanya.
      Hii ni kweli kabisa

    11. #128
      1800's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th December 2010
      Posts : 1,657
      Rep Power : 891
      Likes Received
      416
      Likes Given
      21

      Default

      Quote By ENGINE CONTROL
      Tanzania ni nyepesi sana na wananchi wake tupo tupo tu ndiyo mana ccm inafanya lolote wawezalo wakijua na kuamin kuwa hatuna lolote la kuwafanya.
      Ni kweli mkuu,ila kile kizazi chetu cha wepesi wepesi ndio kinaelekea ukingoni,kizazi chenye akili timamu na msimamo thabiti ndio kinachochipukia
      RedDevil likes this.

    12. #129
      1800's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th December 2010
      Posts : 1,657
      Rep Power : 891
      Likes Received
      416
      Likes Given
      21

      Default

      Quote By cjilo
      dr sijui huwa anaandaliwa yakuongea kwa watu, da maana hakuna siku aliyoshindwa kunikosha nafsi kwa kukemea ujinga wa jk
      Uliangalia speech aliyoitoa katika matembezi ya ihari waliyoshiriki yeye na Dr Kikwete?kila mtu alitoa speech yake,ila ambae yuko good upstairs hajifichi,Dr Slaa sijui ni elimu au ni zawadi ya Mungu tu!ni ngumu kuelewa kwa kweli

    13. #130
      1800's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th December 2010
      Posts : 1,657
      Rep Power : 891
      Likes Received
      416
      Likes Given
      21

      Default

      Quote By Mtindo1
      Chadema siwapendi hata robo secnd.
      Njoo na hoja,usifikiri siasa ni kama ushabiki wa simba na yanga au mipasho mliyozoea,hauna hoja nenda kwy jukwaa la porojo!empty brain wewe

    14. #131
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,484
      Rep Power : 6170
      Likes Received
      3058
      Likes Given
      1020

      Default

      Quote By Mag3
      Hapana Mkuu, Soviet union ilianguka miaka miwili baada ya mapinduzi ya Romania. Somo nililotaka kulitoa ni kuwa ilifika wakati ambapo hata jeshi lake alilolitumia kukandamiza watu wake waliweka silaha chini na kusalimu amri kwa Umma. Huko ndiko tunakoelekea kwa hivi sasa - hata mbwa iko siku anaweza kumgeuka bwanake na kumng'ata!
      Umenikumbusha mkuu. Nilifuafilia sana hayo matukio. Nakumbuka vyombo vya usalama viliwapiga waandamanaji ila baads ya muda wakageuka ghafla wakamkamata Cescescu na mkewe na kuwatupa korokoroni kabla ya kuwapeleka kuzimu.

    15. #132
      Anheuser's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2011
      Posts : 1,296
      Rep Power : 673
      Likes Received
      335
      Likes Given
      135

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      Quote By jmushi1
      Mapinduzi ya Libya yalianzishwa na mpigania haki aliyekuwa akitetea haki za ndugu wa wale waliouwawa kwenye maandamano ya waislam, yale ya kupinga ile katuni ya udhalilishaji wa mtume wao.

      Serikali ni kweli kuwa lazima iwe makini.

      Gaddafi alidhani west wangemsapoti kwasababu wale walikuwa ni mujahedeen, na yeye alisema walikuwa alkaeda, hakusikilizwa licha ya kwamba kuna ukweli kwenye madai yake.

      Cha msingi hapa ni haki ya raia, unauwa raia wenye kuandamana?
      Chanzo cha mapinduzi ya Libya had nothing to do na Uislam na 'kupinga katuni ya udhalilishaji wa mtume.'

      Beginnings of protests

      Between 13 and 16 January, upset at delays in the building of housing units and over political corruption, protesters in Bayda, Derna, Benghazi, Bani Walid and other cities broke into, and occupied, housing that the government had been building. Protesters also clashed with police in Bayda and attacked government offices. By 27 January, the government had responded to the housing unrest with a €20 billion investment fund to provide housing and development.

      "In late January, Jamal al-Hajji, a writer, political commentator and accountant, "call[ed] on the Internet for demonstrations to be held in support of greater freedoms in Libya" inspired by the Tunisia and Egytian revolutions. He was arrested on 1 February by plain-clothes police officers, and charged on 3 February with injuring someone with his car. Amnesty International claimed that because al-Hajji had previously been imprisoned for his non-violent political opinions, the real reason for the present arrest appeared to be his call for demonstrations. In early February, Gaddafi, on behalf of the Jamahiriya, met with political activists, journalists and media figures and warned them that they would be held responsible if they disturbed the peace or created chaos in Libya."
      Wikipedia.

      Kwa hiyo usituambie eti walikuwa wanapinga katuni ya Mtume, wamedhalilishwa, wanapinga katuni ya Mtume kwani Libyan government ndio ilichora katuni ya Mtume?

    16. #133
      only83's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Dodoma-Mjengoni
      Posts : 4,157
      Rep Power : 1846
      Likes Received
      1431
      Likes Given
      1539

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      Alisema kitendo hicho ni uchokozi tosha kwa CHADEMA na kimelenga kuleta fujo nyingine zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani.

      “Niliwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, pia mkuu wa mkoa, niliwaambia mimi sipendi kugombana nao kwa masuala ya hovyo kama hayo, tupo kwa mujibu wa sheria, bendera zetu zinatokana na kodi za Watanzania, wakasema eti zingine ziko sokoni, nikawauliza za CCM huwa zinawekwa wapi?

      “Watu hawana maji, hawana zahanati, elimu inashuka, mkuu wa wilaya hajawahi kuamuka usiku, lakini kwenye kushusha bendera za CHADEMA wanaamka usiku wa manane,” alisema.
      Kwa kauli hii ya dokta utagundua kuwa ni mtu makini na asiyependa ubabaishaji...alikuwa na uwezo wa kuwaambia wananchi,washabiki na wanachama wake kule Tunduma waingie mtaani au watumie nguvu...ila kwa kauli hii,sipendi ugomvi wa hovyo hovyo imenifurahisha sana...Na ndio maana anatofautiana na huyu Dr Dr Dr Dr Dr Dr.....
      "Problems can not be solved by the same level of thinking that created them"
      "Matatizo hayawezi kutatuliwa na uwezo ule ule mdogo wa watawala wa CCM walioyasababisha"




    17. #134
      MziziMkavu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2009
      Location : European Union
      Posts : 22,189
      Rep Power : 19210
      Likes Received
      8155
      Likes Given
      26620

      Exclamation Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      Dk Slaa aionya Serikali

      *ASEMA YANAYOFANYWA NA POLISI YATASABABISHA NCHI ISITAWALIKE
      Geofrey Nyang’oro KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa ameionya Serikali ya Jakaya Kikwete kuwa mambo mbalimbali yanayoendelea kutokea nchini, likiwemo tukio la hivi karibuni la polisi kuua raia wanne kwa risasi mjini Songea, yanaweza kuifanya nchi isitawalike.


      Akizungumza katika uzinduzi wa jengo la vijana wa chama hicho (Bavicha) lililopo Kinondoni jijini Dar es Salaam jana, Dk Slaa alisema kamwe wananchi hawawezi kuvumilia kitendo cha polisi kuua raia wasio na hatia.


      “Nimewahi kutoa kauli kuwa nchi haitatawalika, sikuwa na maana kuwa Chadema itaongoza harakati za kupinga nchi isitawalike, bali vitendo vya viongozi na watendaji wa Serikali kukiuka sheria wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ndio kunaweza kuifanya nchi isitawalike,” Dk Slaa alisema mauaji ya Songea ni matokeo ya viongozi wa mkoa huo kushindwa kusoma saikolojia ya wananchi

      walipoandamana wakipinga wenzao kuuliwa katika mazingira ya kutatanisha.

      Alisema kitendo cha viongozi hao kushindwa kusoma saikolojia ya wananchi hao na kukataa kuwasikiliza huku wakiamuru polisi

      kuwatawanya ndio kilichosababisha watu wasio na hatia kupoteza maisha. Alisema katika mazingira hayo, Serikali inapoteza uhalali wa kuwatumikia wananchi kwa sababu polisi wanaotakiwa kulinda usalama wa raia, wanafanya mauaji huku viongozi waliopewa

      jukumu la kuwalinda, wakibariki vitendo hivyo. Dk Slaa alimtaka Rais Kikwete kuwavua nyadhifa viongozi wakuu wa mkoa huo na kuunda tume huru ya kuchunguza chanzo cha mauaji hayo.


      “Tukio la Songea linasikitisha sana, namshauri Rais Kikwete awaondoe kwenye nyadhifa zao Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kupisha uchunguzi wa mauaji hayo, pia tume zilizoundwa na viongozi hao wa mkoa, zivunjwe sababu hazina tija, tunahitaji tume huru Songea,” alisisitiza Dk Slaa. Dk Slaa alisema chama chake hakiwezi kukubali kuona haki za binadamu zikikiukwa na kwamba,

      kitashughulikia tukio la Songea kuhakikisha kuwa ukweli unapatikana na wahusika wanachukuliwa hatua. Katika kutekeleza hilo, Dk Slaa ametoa wiki mbili kwa Bavicha kufuatilia na kukabidhi ripoti ndani ya wiki mbili, ili chama hicho kiweze kuchukua hatua.

      Kushushwa bendera za Chadema

      Akizungumza suala la madai ya kushushwa bendera za chama hicho alilodai liliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tunduma, Dk Slaa alisema kuwa vitendo hivyo vinachochea vurugu nchini. “Juzi nilipigiwa simu na kuambia Mkuu wa Wilaya akiongozana na Kamanda wa Polisi, wameshusha bendera za Chadema…, inapofikia hatua Mkuu wa Wilaya anaongoza harakati za kushusha bendera ili

      Makamu wa Rais aweze kufanya ziara eneo husika, ni kuchochea vurugu,” alisema Dk Slaa Alisema baada ya kupata taarifa hizo alimpigia simu Mkuu huyo wa Wilaya kumuuliza na baadaye akamuuliza Mkuu wa Mkoa huo, Abass Kandoro aliyetaka amueleze kama katika katiba ya nchi Chadema haitakiwi kuwa katika mkoa wa Mbeya.


      Amvaa Tendwa Dk Slaa pia alimvaa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa kuwa kitendo chake cha kudai Mbunge wa Arusha Mjini Godles Lema hatakiwi kufika katika Jimbo la Arumeru Mashariki, ni sawa na kufanya kampeni za kisiasa za kukitafutia ushindi CCM. Awasihi vijana Mara baada ya kuzindua jengo hilo la vijana, aliutaka uongozi wa vijana hao ukiongozwa na Mwenyekiti wake, John Heche kutumia fursa ya kuwa na jengo lao kuunganisha makundi ya vijana wa aina mbalimbali ili kuleta ukombozi katika Taifa.


      Alisema kwa sasa vijana wamegawanyika katika makundi mbalimbali kwa misingi ya itikadi za kisiasa, lakini akawataka viongozi hao kuwaunganisha kwa pamoja. Kwa upande wake, Heche alisema wao kama vijana watalitumia jengo hilo kuongoza harakati za kuleta mageuzi nchini ili kuwezesha Watanzania kujikomboa. MWIS

      chanzo.Dk Slaa aionya Serikali
      Only Do What Your Heart Tells You




      Allah
      Has Not Revealed A Disease without Treatment....
      (Prevention is Better Than Cure) Email Address yangu hii [email protected]

    18. #135
      Uwezo Tunao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 6,892
      Rep Power : 2293
      Likes Received
      1153
      Likes Given
      1492

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      KAMA VIONGOZI WETO WOTE WAMEAMUA KWA DHATI KUSALITI 'HAKI YA KUISHI NA USALAMA WA MALI ZETU' KIASI HIKI SASA SERIKALI YENYEWE INAKUA NA MAANA KWA VIONGOZI WENYEWE AU SISI WANANCHI WALIPA KODI???????

      Kijana umeongea kwa uchungu wa hali ya juu sana na yote ulioyataja humu ni ROBO TU ya jinsi gani tunavyowaona zaidi ya asilimia 98 % ya mbegu ya viongozi tulionao hivi sasa katika nchi yetu.

      Mpaka hapa hakika mjue ya kwamba pindi mnapoendelea hata kwa robo hatua kwa kutuambia eti mchote tena kodi zetu ziwe posho zaidi kwenu, eti maisha Tanzania hii sasa ni magumu tu kwa hawa viongozi wanaofilisi taifa letu ...,

      ... nasema tunapoendelea kusikia eti hata MAFISADI waliokubuhu nao bado wanaendelea kuonekana wakirandaranda mitaani kutaka wakatuongoze tena badala ya kujivua gamba ...,

      ... kwa uhakika pindi vijana wa taifa hili tunapoendelea kushuhudia eti wengine wakiagiza polisi watuue raia na kutubandika nembo za WAHUNI pindi tunapoandamana kudai HAKI YA KI-KATIBA NA JUKUMU NAMBA MOJA YA serikali kutulinda na mali zetu ...

      Mpaka hapo wenzetu ni kama vile akili zinataka kuturuka vile, ni kama vile wengine tunatamani kwenda kuondoa kabisa uozo wa aina hii kwa mikono yetu bila kuendelea kuhesabu vifo zaidi nchini; mkoa baada ya mkoa. Rai Kikwete kwa uhakika, kachukuwe hatua za dharura KUKOMESHA hii hulka mpya ya DOLA kuwaua raia kinyama kiasi hiki.

      Mpaka hapa ni kwamba tungependa ieleweke kwamba HATUTOPENDEZEWA kuona vifo zaidi ya raia hata mmoja wakati kodi zetu polisi na jeshi letu wakiendelea kulipwa kila mwezi.

      Nasema kwamba wala haitusaidii kitu kuendelea kuwa na viongozi sanamu sawa na picha tu ukutani kwa jina la Vuai Nahodha, Saed Mwema, Mkuu wa Mkoa, Wilaya na RPC huko Ruvuma wakati raia tukiendelea kuchinjwa na waajiriwa wetu wenyewe kwa mtaji wa kodi zetu!!

      a.
      Wanaharakati mko wapi au mnasubiri tu kuja kuandika mi-ripoti ndefu mara baada ya familia kadhaa nchini kupoteza zaidi y nusu ya ukoo wao?

      b.
      UDASA huu ukimya wenu tafsiri yake ni kujiunga na mdhulumishi au tuwaelewe vipi?

      c.
      Tangnyika Law Society ndio tuseme mpaka O'Campo awe ametoa neno ndio mtiririko wote huu wa mauaji katika mkoa mmoja baada ya nyingine ipate kuwagusa?

      d.
      Akina Mama kwenye taasisi zenu zote kama vile UWT inamaana uchungu wa mtoto wa mke mwenzio wala haukuhusu kitu isipokua ni jukumu la Mama Nkya na Kijo Bisimba peke yao sio?

      e.
      Enyi wanafunzi wa vyo vikuu nchini mliopata kua VIWAKILISHI VYA SAUTI YA HAKI KATIKA JAMII, mnaona ni vema hadi afe mtu wa ngapi tangu Mauaji ya raia Mwembechai, Pemba, Arusha, Igunga, Musoma, Uyole-Mbeya, na sasa Songea, ndio mpate hata kuguna tu juu ya mwenendo wote huu wa mambo?

      f.
      Kamisheni na taasisi zote za haki za binadamu nchini, inamaana hata kukemea tu muaji haya yote ni mpaka kupatikane mfadhili kutoka nje ya nchi ndio akawape fedha ndio mpate kutekeleza majukumu yenu?

      g.
      Vyombo vya maamuzi ya Juu nchini kama vile NEC-CHADEMA, NEC-CCM, Baraza la Mawaziri na Taasisi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivi kweli vikao vya dharura mtaweza kuviitisha tu pindi mambo ya kisiasa yanapowaendeeni vibaya kwa njia moja au nyingine na wala si kule KUTOLEWA ROHO Mtanzania mwenzetu??

      h. Hivi kweli Tanzania tumefika mahala ambapo uhai wa raia ni sawa tu na uhai wa inzi na wala halichukuliwi kwa uzito wake kama ambavyo tumewahi kusikia enzi hizo Mzee Mwinyi alipokua Waziri wa Mambo ya Ndani?

      i.
      Wazee wetu tunaowaheshimu saaana katika taifa hili; Joseph Sinde Warioba, Salim Ahmed Salim, Benjamin Mkapa, Edwin Mtei, Bob Makani, Mufti Mkuu Sheikh Simba, Mwashamu Askofu Polycarp Pengo, Jenerali Ulimwengu, Rejnald Mengi, Mzee Bahresa ...

      ... je ukimya wenu wote huu wakati Dola ikiendelea kuua mkoa hadi mkoa ndio tuseme ni usaliti au usahihi wa msimamo wenu kutetea jukumu mama kikatiba kulinda uhai wa kila Mtanzania na mali zake au mpaka vurugu zije zitukumbe ndio mje kuanza kukatisha kushoto kulia.

      Kamati ya kutumu ya Bunge kuhusu ulinzi na usalama, tunaomba maelezo kuhusu mauaji yote haya huku Rais Kikwete yeye akiendelea tu na safari zake za huko na kule kama vile hakuna cha ajabu kinachotokea ndani ya nchi yetu.

      Kwa kweli kwa jinsi mambo yanavyoeneda hivi sasa na kwa usahihi ambao huyu Ndugu KweleaKwelea wa JF ameweza kubainisha kero za ndani kabisa wa kila kijana ndani ya nchi hii, napenda kusema kwamba NAUNGA MKONO karipio kali kwenye hotuba ya Mhe Dr Slaa, alioitoa hapo jana jijini Dar es Salaam, neno kwa neno na nukta kwa nukta bila ajizi!!


      Quote By kweleakwelea
      Well, simlaumu sana mama yetu lakini anawakilisha mawazo ya kizazi kilichopita chenye uvivu wa kujituma na kumtumikia kafiri bora mkono uende kinywani....

      Ni kizazi ambacho hakina matumizi makubwa ya kichwa.... hakiwezi hata kuset priorities za taifa..... ni kizazi cha hunters and gatherers...... hakijafikia hata stage kuitwa horticultural societies.........

      1. Kizazi hiki huona bora kiue kiwanda cha kiatu ili kinunue viatu vya ulaya.....
      2. kizazi hiki huona bora kiue ginerry na vyama vya ushirika ili products zikawe processed ulaya.....

      3. Kizazi hiki hudhani kuwa kutembelea 4 wd za gharama kutainua uchumi kuliko kujenga barabara bora....
      4. Kizazi hiki hupenda kwenda kupumzika ulaya na si kuendeleza mambo mazuri ili kipimzikie nyumbani....

      5. Kizazi hiki hupenda sana dili za muda mfupi mfupi hata kama zina gharama kwa taifa...
      6. Kizazi hiki hakioni umuhimu wa huduma ya reli kuwa bora na umuhimu wa huduma hii kuwa chini ya state.....

      7. Kizazi hiki ni hopeless.... ni hopeless kuliko kile cha chifu mwangunga kwani kimeenda shule lakini mambo yao kama kinavuta bangi mbichi......

      NOTE: it is high time tulijipanga kwenye forum zetu kuwa tupigane mshahara wa mbunge uwe as high as the university professor....ili ONLY COMMITED PEOPLE TO GET IN PALE MJENGONI.........

      Kwa heshima na taadhima NINAWAOMBA WABUNGE WOTE WAZEE WAFUNGASHE NA WAIGE MFANO WA MAMA MAKINDA (ambaye kwa kauli hii nimemuheshimu sana)....

      Pia nawaomba wale wabunge vijana wanaofikiri kwa kutumia masaburi pia waunge bogi.....
      lets leave the brilliant DOT COMs produce the new cadre to save our sunking Tanzania....
      such that hakutakuwa na KULOGANA tena kwa ajili ya hii position......

      kiasi kwamba B**** letu limekuwa kambi la wachawi.....

      mAMA YETU KASOMA ALAMA ZA NYAKATI...she is brilliant!

      Mungu mbariki Makinda...

      Mungu ibariki Tanzania...
      Quote By EasyFit
      KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini na kuchukua hatua za haraka kurejesha amani kabla Watanzania hawajaishiwa uvumilivu na utawala wa serikali yake ...

    19. #136
      only83's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Dodoma-Mjengoni
      Posts : 4,157
      Rep Power : 1846
      Likes Received
      1431
      Likes Given
      1539

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      Hivi unawaambiaje raia wenye uchungu na vifo vya wananchi wenzao, waliojikusanya na kuamua kuandamana kudai haki, eti wachague kiongozi wa kuonana na mkuu wa mkoa,” alisema.

      Kwenye hii kauli hasa hapo kwenye red haiingii akilini kabisa...hawa jamaa ni watu wa ajabu sana,wanataka wachague kiongozi wa namna gani? Kama sio kuwatega ili kuvunja nguvu yao,huyo kiongozi angekuwa ni mwanachama wa CDM wangesema unaona,ni CDM hawa...kama angekuwa wa CCM wangemuonga hela hili awasaliti wenzake.Viongozi wanapaswa kujua wakati mwingine kukiwa na hoja zilizowazi watu wanaweza kufanya kazi hata bila kiongozi....na hii ndio imeonekana huko Songea na Mbeya wakati wa wamachinga...tuache siasa majitaka kwenye mambo ya msingi.
      "Problems can not be solved by the same level of thinking that created them"
      "Matatizo hayawezi kutatuliwa na uwezo ule ule mdogo wa watawala wa CCM walioyasababisha"




    20. #137
      Mdutch's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th November 2011
      Posts : 107
      Rep Power : 401
      Likes Received
      49
      Likes Given
      2

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      Nadhani kauli ya DR Slaa ilipaswa kuwa hivi " Nchi itaendelea kutokutawalika kama JK akiendelea kupuuza". Nchi hii mbona haitawaliki tena chini ya Kikwete na CCM yake iliyokufa tangu january tano 2011!

      Nchi itatawalikaje wakati tuna rais mzururaji?
      Nchi itatawalikaje wakati tuna Rais mwoga asiyeweza kufanya maamuzi?
      Nchi itatawalikaje wakati tuna Raisi asiyejua kwa nini nchi yake ni masikini?
      Nchi itatawalikaje wakati tuna Rais omba omba?
      Nchi itatawalikaje wakati tuna Rais anayeendekeza ushikaji ndani ya serikalo yake?

      Acheni bana, Inakera ni vipi!

    21. Omr
      #138
      Omr's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th November 2008
      Location : maswa
      Posts : 1,162
      Rep Power : 768
      Likes Received
      89
      Likes Given
      51

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      Quote By only83
      Kwa kauli hii ya dokta utagundua kuwa ni mtu makini na asiyependa ubabaishaji...alikuwa na uwezo wa kuwaambia wananchi,washabiki na wanachama wake kule Tunduma waingie mtaani au watumie nguvu...ila kwa kauli hii,sipendi ugomvi wa hovyo hovyo imenifurahisha sana...Na ndio maana anatofautiana na huyu Dr Dr Dr Dr Dr Dr.....
      Wewe lazima utasifia kila jambo lakini ukweli ni kuwa Slaa ni mnafiki tu, hawezi uwaambia wananchi waingie mtaani kwasababu alishaonywa alipokwenda Ikulu.

    22. #139
      1800's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th December 2010
      Posts : 1,657
      Rep Power : 891
      Likes Received
      416
      Likes Given
      21

      Default

      Quote By Omr
      Wewe lazima utasifia kila jambo lakini ukweli ni kuwa Slaa ni mnafiki tu, hawezi uwaambia wananchi waingie mtaani kwasababu alishaonywa alipokwenda Ikulu.
      Jamaha uwaga una hoja nyepesi wewe!sijawahi ona!kila hoja unayochangia uwa ni kama vile,unaokota mawazo yako kwy vijiwe vya shoe shiners vile

    23. #140
      Songoro's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th May 2009
      Posts : 2,222
      Rep Power : 0
      Likes Received
      487
      Likes Given
      21

      Default Re: Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

      Nchi itatawalika mpende msipende,si mliwatumia akina kijo kisimba kuanzisha maandamano ya kwenda ikulu?! Watu walojitokeza hawajai hata kwenye Hiace moja,watanzzania wengi hawana imani na jk but bado wana imani na chama chao cha Ccm so wanasubir 2015 kufanya kweli,wapinzani hawaaminiki hata kidogo ndo maana wapo walopitia misikitini na makanisani komba kura wakamwagwa na wananchi.

    Page 7 of 14 FirstFirst ... 56789 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...