TiGo Says
    Show/Hide This

    Topic: Mh Godbless Lema amjibu Tendwa

    Report Post
    Page 1 of 12 12311 ... LastLast
    Results 1 to 30 of 351
    1. #1
      Joblube's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th March 2011
      Posts : 238
      Rep Power : 411
      Likes Received
      85
      Likes Given
      0

      Default Tendwa hili halikubaliki

      Wana JF kitendo cha Msajili wa vyama vya siasa Jonn Tendwa kazungumza na Waandishi wa habari na kusema kuwa katika tathimini yake katika uchaguzi wa Arumeru Wazee wa kimila wamemwambia kuwa wanamwonya Lema asiende kwenye kampeni eti watamuuwa kauli hii imenisikitisha kama si kunishangaza kuwa Tanzania kuna tatizo gani?.

      Hii bila kumumunya maneneo ni makakati wa ndani wa CCM wa kuandaa mazingira ya vurugu ili ikionekena CCM inashindwa waanzishe vurugu katika kampeni ili watu waumizwe waogope kwenda kupiga kura.

      Hili naomba CHADEMA wajiandae mapema . Haingii akilini mtu wa heshima kama msajili wa vyama kuongelea vitu vya vurugu kutoka kwa watu wa kimila waabudu mizimu na wasiomjua Mungu. Nasema hakika haya mnayofanya laana ya Mungu na damu zitakazo mwagika bila hatia itakuwa juu yako na familia yako na vizazi vyako.

      Mimi nadhani wazee hawa ilikuwa ni wakati wa kujenga Tanzania yenye amani zaidi kwa kuweka mazingiza ya watu kushindana kwa hoja na kwa amani ili ichi yetu ambayo imepata heshima kubwa iendelee kuwa nchi ya amani.

      Tuachane na mawazo mgando kuwa ni lazima nyie muendelee kutawala na kutumia mbinu hata zisizofaa jamani tuamke watu wa aina ya Tendwa ni ukoma kwa Taifa.
      August likes this.


    2. #2
      Mwita Maranya's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 1st July 2008
      Location : Ikorongo Le Kurya
      Posts : 4,145
      Rep Power : 1336
      Likes Received
      1964
      Likes Given
      1846

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Quote By Joblube View Post
      Wana JF kitendo cha Msajili wa vyama vya siasa Jonn Tendwa kazungumza na Waandishi wa habari na kusema kuwa katika tathimini yake katika uchaguzi wa Arumeru Wazee wa kimila wamemwambia kuwa wanamwonya Lema asiende kwenye kampeni eti watamuuwa kauli hii imenisikitisha kama si kunishangaza kuwa Tanzania kuna tatizo gani?.Hii bila kumumunya maneneo ni makakati wa ndani wa CCM wa kuandaa mazingira ya vurugu ili ikionekena CCM inashindwa waanzishe vurugu katika kampeni ili watu waumizwe waogope kwenda kupiga kura. Hili naomba CHADEMA wajiandae mapema . Haingii akilini mtu wa heshima kama msajili wa vyama kuongelea vitu vya vurugu kutoka kwa watu wa kimila waabudu mizimu na wasiomjua Mungu. Nasema hakika haya mnayofanya laana ya Mungu na damu zitakazo mwagika bila hatia itakuwa juu yako na familia yako na vizazi vyako. Mimi nadhani wazee hawa ilikuwa ni wakati wa kujenga Tanzania yenye amani zaidi kwa kuweka mazingiza ya watu kushindana kwa hoja na kwa amani ili ichi yetu ambayo imepata heshima kubwa iendelee kuwa nchi ya amani. Tuachane na mawazo mgando kuwa ni lazima nyie muendelee kutawala na kutumia mbinu hata zisizofaa jamani tuamke watu wa aina ya Tendwa ni ukoma kwa Taifa.
      Pamoja na Tendwa kuwa msajili wa vyama vya siasa, na kwa mantiki hiyo yeye ndiye mlezi wa vyama vyote vya siasa nchini kisheria, lakini kiuhalisia Tendwa amekuwa ni mlezi wa ccm na amekuwa akifanya mambo mengi ya kijinga ili kuisaidia ccm.

      Tendwa huyu ndiye alikurupuka na kutaka kuhalalisha raisi kikwete kuzidisha muda wa kampeni mwaka 2010 wakati wagombea wengine wakishushwa na polisi toka majukwaani, ama kuzuiliwa kupanda majukwaani hadi pale NEC ilipokuja kumkana.

      Tendwa huyu ndiye alishiriki kikamilifu kukihujumu chama cha CCJ kisipate usajili wa kudumu ili kuinusuru ccm na hofu ya wanachama wake kadhaa kujimega na kutimkia huko.

      Tendwa huyu ndiye alifumbia macho na ameendelea kufumbia macho matumizi makubwa ya fedha yaliyofanywa na ccm katika kampeni za uchaguzi mkuu mwaka 2010 na katika chaguzi ndogo wakati amepewa uwezo na mamlaka kisheria, kwa mujibu wa sheria ya gharama za uchaguzi ya 2010.

      Mambo ya hovyo yanayofanywa na Tendwa ni mengi sana kuyaeleza, lakini itoshe kusema kwamba kama kuna mtu amekuwa akifikiria kwamba Tendwa hayuko bias basi alikuwa anakosea sana na amtazame Tendwa kwa uangalifu mkubvwa atamuona jinsi anavyotumia ofisi yake kukisaidia chama chake cha ccm.
      August and Cha Moto like this.
      "Last Minutes Method"

    3. #3
      GeniusBrain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Location : CHADEMA Makao Makuu
      Posts : 2,780
      Rep Power : 953
      Likes Received
      119
      Likes Given
      0

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Quote By Joblube View Post
      Wana JF kitendo cha Msajili wa vyama vya siasa Jonn Tendwa kazungumza na Waandishi wa habari na kusema kuwa katika tathimini yake katika uchaguzi wa Arumeru Wazee wa kimila wamemwambia kuwa wanamwonya Lema asiende kwenye kampeni eti watamuuwa kauli hii imenisikitisha kama si kunishangaza kuwa Tanzania kuna tatizo gani?.

      Hii bila kumumunya maneneo ni makakati wa ndani wa CCM wa kuandaa mazingira ya vurugu ili ikionekena CCM inashindwa waanzishe vurugu katika kampeni ili watu waumizwe waogope kwenda kupiga kura.

      Hili naomba CHADEMA wajiandae mapema . Haingii akilini mtu wa heshima kama msajili wa vyama kuongelea vitu vya vurugu kutoka kwa watu wa kimila waabudu mizimu na wasiomjua Mungu. Nasema hakika haya mnayofanya laana ya Mungu na damu zitakazo mwagika bila hatia itakuwa juu yako na familia yako na vizazi vyako.

      Mimi nadhani wazee hawa ilikuwa ni wakati wa kujenga Tanzania yenye amani zaidi kwa kuweka mazingiza ya watu kushindana kwa hoja na kwa amani ili ichi yetu ambayo imepata heshima kubwa iendelee kuwa nchi ya amani.

      Tuachane na mawazo mgando kuwa ni lazima nyie muendelee kutawala na kutumia mbinu hata zisizofaa jamani tuamke watu wa aina ya Tendwa ni ukoma kwa Taifa.
      Napata wasiwasi na uwezo wako wakuchambua mambo, ni mdogo mno kuzidi hata punje ya mchanga !


    4. #4
      Wambandwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd December 2006
      Posts : 1,209
      Rep Power : 831
      Likes Received
      187
      Likes Given
      411

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Huyu Tendwa umri unamtupa mkono, ajabu badala ya kuwa na hekima na busara anakuwa na akili kama ya mtu taahira. Kama kweli wazee wa kimeru walimwambia maneno hayo kweli kwa nini asikae nao na ku resolve tatizo hili?

      Kuzungumza na waandishi wa habari jambo hili ili iweje, Lema asiende kufanya kampeni wakti ukifika? Mh. Lema hawezi kukubali, na huko CCM kazi wanayo ndo watajua kuwa kwa kumweka mkwewe EL wamepotea njia. Ngoja tusubiri tuone, kule si Igunga watu wa Meru wanakula na kushiba wanakunywa maziwa badala ya chai hivyo njaa iliyotengenezwa na CCM kule hakuna, hawaongeki au tuseme hawauzi kura yao.
      August and ral like this.
      For God so loved the world that he gave his one and only Son, that whoever believes in him shall not perish but have eternal life.
      John 3:16


    5. #5
      Bhbm's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2009
      Posts : 505
      Rep Power : 535
      Likes Received
      108
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By GeniusBrain View Post
      Napata wasiwasi na uwezo wako wakuchambua mambo, ni mdogo mno kuzidi hata punje ya mchanga !

      Sasa wewe mwenye brain nyingi si uonyeshe uwezo wako hapa kwa kumwaga point za maana....mtu mzima hovyooooo

    6. #6
      KirilOriginal's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th February 2012
      Posts : 264
      Rep Power : 367
      Likes Received
      60
      Likes Given
      0

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Magamba wameanza, wameru tunawafahamu vzr, sasa hili la Tendwa ni janja ya ccm kujisogeza karibu na watu wa arumeru, magamba ndo zao wanalia kukanyagana wamezoea kuwadanganya watanzania kila kona ya nchi ref Igunga. Mzee Tendwa usiwasaidie magamba kupenya arumeru acha ngoma iwe faire play

    7. #7
      Ileje's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th December 2011
      Posts : 438
      Rep Power : 409
      Likes Received
      135
      Likes Given
      67

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Kilichotakiwa na Tendwa ni kuwaonya wazee wasijiingize katika uvunjifu wa amani na pia kuiomba serikali kuimarisha ulinzi ili kampeni zifanyike kwa haki na amani.
      kweleakwelea and MVUMBUZI like this.

    8. #8
      Bobuk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 824
      Rep Power : 558
      Likes Received
      266
      Likes Given
      0

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Quote By Joblube View Post
      Wana JF kitendo cha Msajili wa vyama vya siasa Jonn Tendwa kazungumza na Waandishi wa habari na kusema kuwa katika tathimini yake katika uchaguzi wa Arumeru Wazee wa kimila wamemwambia kuwa wanamwonya Lema asiende kwenye kampeni eti watamuuwa kauli hii imenisikitisha kama si kunishangaza kuwa Tanzania kuna tatizo gani?.
      I have never ranked Tendwa high! Mimi ninajiuliza hata huo U-JUDGE aliupataje? au ndiyo ainadhirisha ule msemo kwamba CCM is a mental disease? Once you're a CCM zealot your thinking and reasoning capacity approaches ZERO!!.

      Yaani "Wazee" wanapanga kufanya JINAI, tena JINAI ya kutoa ROHO ya mtu, mbele ya Kiongozi Mkubwa, Msajili wa vyama vya SIASA, tena mwenye Cheo cha U-JUDGE (Kama kweli ni judge, maana wajita kila mtu ni JUDGE), badala ya kwenda kutoa report POLICE ili kuzuia hiyo JINAI isitendeke JUDGE mzima na k.o.r.o.n.d.a.n.i zake anakwenda kuropoka kwenye vyombo vya habari? Hivi kweli huyu anayejiita JUDGE alipass hata hiyo LLB 101? Au ndiyo wale ma-JUDGE wa Kijita?! YEGO JAJI
      Kama ma-Judge tulionao nchi hii ni wa aina ya akina Tendwa no wonder mahakama zetu zimeshindwa kutenda HAKI. Huyu Tendwa kama angeletewa kesi yaina I suspect angetoa SUMMARY DISMISSAL kwamba Lema ameuawa kwa KIHEREHERE chake kwasababu alionywa hakusikia.

      Ruling za aina hii is ONLY POSSIBLE IN TANZANIA.
      Wambandwa, August, kiraia and 7 others like this.

    9. #9
      FREDOMFIGHTER's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2010
      Posts : 866
      Rep Power : 556
      Likes Received
      142
      Likes Given
      521

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Kama kuna mtu anastahili kuuwawa basi ni yeye Tendwa,mnafiki mkubwa huyu mzee bishoo wa kubana bana pua.
      tedo likes this.
      NI UTAAHIRA KUIUNGA MKONO CCM.

    10. #10
      only83's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Dodoma-Mjengoni
      Posts : 2,964
      Rep Power : 1074
      Likes Received
      839
      Likes Given
      829

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Msameheni huyu mzee,nadhani anapaswa kuwa ICU akitibiwa matatizo ya kufikiri..na ndio matatizo ya kuendelea kung'ang'ani kwenye ofisi wakati uwezo wa kuongoza umepungua.
      "Tulianza na MUNGU, tunaendelea na MUNGU, tutamaliza na MUNGU"
      Vua GAMBA vaa GWANDA

      Movement For Change(M4C)

    11. #11
      KIROJO's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 7th December 2011
      Posts : 113
      Rep Power : 346
      Likes Received
      15
      Likes Given
      2

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Tendwa Janga la Taifa,sijuwi huyu mzee kwanza anawatoto wanaakili timamu.Mimi ningekua hata ni jirani yangu huko kwetu ningemshauri kitu kimaoja ,aachane na kazi hii ,awe mshauri wa sheria katika kampuni za uwakili siamesoma na Jaji mstaafu,huyu mzee anakokwenda ni kubaya,watu watampinga mimi nakwambieni hayo mambo anayodai ni zamani kwelikweli,wewe na usomi wako huo huwezi kuzungumuzia habari za kishirikiana mbele ya kamera/TV ,aise ndo maana nasikia viongozi wengi wanatembea na mabodyguard wawili,wa kwanza ni ulinzi wa macho ,mwingine wa kiroho,--hiyo ni kubali ni kweli ,ref mwanza wewe angalia tu kiongozi wetu akiwa ameenda sehemu hakubariki,utaona huko nyuma yake kuna walizi wamesimama wawili,wote wanakazi mbili,then kunamutindo siku hizi wa pete ,ref,mtoto wa mkulima mbona zamani alikuwa hana pete leo hii ndo kafanikiwa ndo anavaa pete?
      August likes this.


    12. #12
      Gagurito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2011
      Location : Gangilonga....
      Posts : 5,006
      Rep Power : 1352
      Likes Received
      643
      Likes Given
      671

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Tendwa yupo kikazi zaidi. Anatetea maslahi ya magamba!

    13. #13
      only83's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th October 2010
      Location : Dodoma-Mjengoni
      Posts : 2,964
      Rep Power : 1074
      Likes Received
      839
      Likes Given
      829

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Quote By GeniusBrain View Post
      Napata wasiwasi na uwezo wako wakuchambua mambo, ni mdogo mno kuzidi hata punje ya mchanga !


      Napata wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri na kutoa hoja,inaonekana ubongo wako hauna uwezo wala aibu ya kudandia mambo.Hivi wewe uoni kauli ya Tendwa ni janga kwa Taifa?
      "Tulianza na MUNGU, tunaendelea na MUNGU, tutamaliza na MUNGU"
      Vua GAMBA vaa GWANDA

      Movement For Change(M4C)

    14. #14
      kizazi kipya's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 21st July 2010
      Posts : 226
      Rep Power : 441
      Likes Received
      16
      Likes Given
      8

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Quote By GeniusBrain View Post
      Napata wasiwasi na uwezo wako wakuchambua mambo, ni mdogo mno kuzidi hata punje ya mchanga !

      hata mimi napata waswasi na uwezo wako wa kuchambua mambo ukiwa kama independent person(bila kutumwa)

    15. #15
      Kigogo's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 14th December 2007
      Location : Calabash
      Posts : 5,478
      Rep Power : 1656
      Likes Received
      674
      Likes Given
      183

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      tutamsokomeza vijiti kama gadafi wala hatuna haraka naye ....
      August, Edward Teller and cjilo like this.
      ______________________________ _
      Niko tayari kufa huku nimesimama kuliko kuishi huku nimepiga magoti....

    16. #16
      Kintiku's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2011
      Posts : 329
      Rep Power : 433
      Likes Received
      112
      Likes Given
      60

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      TZ hakuna tofauti kati ya aliyesoma na Ngumbalu linapokuja suala la kuongea. Tendwa aibu hii ni kubwa sana kwa familia yako hasa kama una watoto wa kiume, wanajisikiaje unavyotoa kauli kama hizi za kujitongozesha kwa CCM?
      August likes this.

    17. #17
      Massenberg's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th June 2011
      Posts : 440
      Rep Power : 515
      Likes Received
      249
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By GeniusBrain View Post
      Napata wasiwasi na uwezo wako wakuchambua mambo, ni mdogo mno kuzidi hata punje ya mchanga !

      Wewe mwenye uwezo mkubwa unaandika ID yako GeniusBrain badala ya Genius Brain, wewe una unafuu gani?
      August likes this.

    18. #18
      Ulukolokwitanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th September 2010
      Location : ndzengelendete
      Posts : 1,079
      Rep Power : 596
      Likes Received
      459
      Likes Given
      47

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Hao wazee ni matokeo ya kazi ya kisiri siri ya Edward Lowassa kuweka himaya yake hapa nchini kwa kumtanguliza mkwewe. Nashangaa hata Nape anacheza hiyo hiyo ngoma na Membe yuko kwa David Cameron kuwajadili wasomali na huku Mzee Six yuko busy na Kanumba. Janja ya Lowassa kiboko yake ni CDM tu. Nassary alipata zaidi ya kura 30,000 (Baada ya kuchakachuliwa) 2010 bila hata Lema kwenda kule. CCM wao tishio lao kubwa ni Lema tu wanasahau kuwa CDM sio one man army. Lwaigwanani wenye njaa na waliohongwa na EL wazuie CDM yote kama wanaweza
      R.I.P Chama Cha Magamba.... CCM 1977-2015, Bwana alitoa, Bwana atatwaa.

    19. #19
      Kakulwa P's Avatar
      Member Array
      Join Date : 8th February 2012
      Posts : 90
      Rep Power : 333
      Likes Received
      25
      Likes Given
      7

      Default Re: Tendwa hili halikubaliki

      Kama MZEE TENDWA kama anasema ukweli kuwa wazee wa kimila WASHIRI wamekaa kwenye kikao wakatamka maneno ya kudhamiria KUMUUA GODBLESS LEMA MH basi jeshi la polisi liwakamate wafunguliwe mashtaka ili wachukuliwe hatua za kisheria kwa kuwa tayari shahidi kwenye kesi hiyo yupo.
      Kama Mzee Tendwa katumwa na chama chake kusema maneno hayo na siyo ya wazee wa kimila, afunguliwe mashtaka ya uchochezi na wazee hao wa kimila WASHIRI maana watakuwa mashahidi ktk kesi hiyo kwa kuwa hawakusema maneno hayo.
      Kama hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi ya Mzee Tendwa na Washiri. wananchi wa jimbo la Arumeru Mashariki waamue kuwa na kiongozi makini ambaye hatokani na urithi wa kifamilia ifikapo tarehe 01.04.2012. Kura yao ya kuwakomboa ni muhimu sana.
      Cha Moto and Baba Collins like this.

    20. #20
      KAMANDA HANGA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd September 2011
      Posts : 127
      Rep Power : 360
      Likes Received
      43
      Likes Given
      0

      Default Tendwa umelikoroga lazima ulinywe!!!

      Baada ya msajiri wa vyama vya siasa John Tendwa kuwasemea wale aliowaita wazee wa Arumeru, kundi jipya limeibuka na kudai Tendwa kalisemea kundi la wazee wa CCM nao wanakuja kama wazee wa UPINZANI kusema yafuatayo:-
      1. Neno la kutishia kuua tayari ni kuua na hawakutarajia mtu makini kama Tendwa kuendelea kulisisitiza hadharani kama sio kuchochea vurugu.
      2. Lema hakumtukana mtu hata kama alionyesha vidole viwili kwani yeye mda wote anatetea maslahi ya chama chake. Walitaka atamke kidumu chama cha mapinduzi ndo waridhike?
      3. Wanadai kila mmoja anaweza kuua na wote pande zote mbili ni wakazi na wana Arumeru hawana haja ya kutishana kwani wanatumia siraha sawa na mbinu sawa.
      4. Wanamwambia Lema karibu Arumeru hata leo waone nani anakuwa wa kwanza kumfunga paka kengere.
      5. Mwisho wanamwambia Tendwa awe tayari kujibu mbele za watanzani juu ya madhara yoyote yatakayojitokeza kutokana na vurugu anazozichochea kwa wanameru yeye akishirikiana na CCM.
      Wazee hao nao wanajipanga kuitisha mkuta na waandishi wa habari mda wowote.
      Source: Dr mmoja hospitali ya Tengeru ambaye ni Mmeru mkazi wa Sing'si.

    21. #21
      wasaimon's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th October 2010
      Posts : 171
      Rep Power : 419
      Likes Received
      24
      Likes Given
      104

      Default Re: Tendwa umelikoroga lazima ulinywe!!!

      Kazi kweli kweli!

    22. #22
      Kishongo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2010
      Posts : 933
      Rep Power : 594
      Likes Received
      62
      Likes Given
      47

      Default Re: Tendwa umelikoroga lazima ulinywe!!!

      CDM msituletee umwagaji damu kama mlivyofanya Igunga. Amani mliyoikuta Meru iacheni.

      Inaonekana mmeanza kutapatapa, ... na bado....jimbo la ARUMERU mtalisikia redioni kama ilivyokuwa kwa majimbo mengine ya Igunga na Uzini.

      Ama kweli, CDM ni full shari.
      Jiulize: Umeitendea nini Tanzania katika Miaka 50 ya Uhuru wake!

    23. #23
      Bigirita's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 15th June 2009
      Location : Under a mango tree
      Posts : 8,640
      Rep Power : 2345
      Likes Received
      1583
      Likes Given
      2017

      Default Re: Tendwa umelikoroga lazima ulinywe!!!

      Quote By Kishongo View Post
      CDM msituletee umwagaji damu kama mlivyofanya Igunga. Amani mliyoikuta Meru iacheni.

      Inaonekana mmeanza kutapatapa, ... na bado....jimbo la ARUMERU mtalisikia redioni kama ilivyokuwa kwa majimbo mengine ya Igunga na Uzini.

      Ama kweli, CDM ni full shari.
      Kila mara huwa nafikiri kwamba huwa unapitiwa, kumbe kichwani hakuna ubongo, ni kasha tu!!
      I'm not being rude. You're just insignificant.

    24. #24
      Ulukolokwitanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th September 2010
      Location : ndzengelendete
      Posts : 1,079
      Rep Power : 596
      Likes Received
      459
      Likes Given
      47

      Default Re: Tendwa umelikoroga lazima ulinywe!!!

      Kila chaguzi CCM wanaingia na WRONG tactics ambazo huacha makovu makubwa sana kwa wananchi baada ya uchaguzi. Tendwa katumwa na CCM lakini anajikuta akiwagawa wana Arumeru... Ndio madhara ya kuwa na viongozi legelege
      FJM likes this.
      R.I.P Chama Cha Magamba.... CCM 1977-2015, Bwana alitoa, Bwana atatwaa.

    25. #25
      kichomiz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 2,876
      Rep Power : 945
      Likes Received
      456
      Likes Given
      61

      Default

      Quote By Kishongo View Post
      CDM msituletee umwagaji damu kama mlivyofanya Igunga. Amani mliyoikuta Meru iacheni.

      Inaonekana mmeanza kutapatapa, ... na bado....jimbo la ARUMERU mtalisikia redioni kama ilivyokuwa kwa majimbo mengine ya Igunga na Uzini.

      Ama kweli, CDM ni full shari.
      Acha kutoa coment bila kufikilia,nani kaanza kutoa vitisho kama sio CCM?kila siku nyie ndio mnakuwa wa kwanza kuyaanzisha,alafu baada ya hapo mnawatupia lawama CDM mbinu zenu chafu lazima ziwatokee puani.

    26. #26
      PakaJimmy's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 29th April 2009
      Posts : 11,637
      Rep Power : 3489
      Likes Received
      3166
      Likes Given
      1647

      Default Re: Tendwa umelikoroga lazima ulinywe!!!

      Mzee ameshajichokea huyu, labda ni akili ya kurudi utotoni imeshika kasi!
      "The only thing that walks back from the tomb with the mourners and refuses to be buried is the character of a man.
      What a man is, survives him... it can never be buried"
      (GENEKAI-Jamiiforums, 4th November 2010 07:32PM).
      Pakajimmy@jamiiforums.com

    27. #27
      KirilOriginal's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th February 2012
      Posts : 264
      Rep Power : 367
      Likes Received
      60
      Likes Given
      0

      Default Re: Tendwa umelikoroga lazima ulinywe!!!

      Hapo bado hajaja boiler mchemsaji WASIRA hawa wazee wameifanya hii nchi kama changu doa wanaiinamisha wanavotaka, sasa hapo mgombani hawana bahati wakizidi majabali yanawahusu

    28. #28
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th January 2012
      Posts : 2,315
      Rep Power : 783
      Likes Received
      868
      Likes Given
      169

      Default Tendwa aanza Rasmi kuivuruga CHADEMA Arumeru Mashariki

      MSAJILI wa Vyama vya Siasa, John Tendwa amemshauri Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuwaomba radhi wazee wa kimila wa kabila la Wameru ‘Washiri’ vinginevyo hali ni mbaya kwake na kundi lake.

      Tendwa alisema hayo jana kwa waandishi wa habari wakati akizungumzia mambo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki.

      Alisema utovu wa nidhamu alioonesha Lema siku ya maziko ya aliyekuwa mbunge wa jimbo
      hilo, Jeremiah Sumari, kiliwakera Washiri na kumtaka asikanyage jimbo hilo wakati wa kampeni.

      Alisema yeye alikwenda katika jimbo hilo kuonanana wakuu wa Serikali na taasisi zake kupanga mkakati wa uchaguzi, lakini ghafla alikutana na wazee hao waliosema mbele yake, kuwa Mbunge huyo wa Arusha Mjini, hawataki kumwona katika kampeni, vingivevyo damu inaweza kumwagika juu yake.

      ‘’Washiri wamesema hawataki kumwona Lema katika kipindi cha kampeni kwani alileta dharau kubwa na utovu wa nidhamu siku ya maziko ya Sumari, hatua ambayo iliwakera wazee hao … ni busara tu, Lema kwenda kuwaomba radhi wazee hao kama anataka kufanya kampeni ya mgombea wa chama chake- Chadema,” alisema Tendwa. Pia Tendwa amesema Lema asipowaomba radhi huenda damu ikamwagika.

      Msajili alivitaka vyama vya siasa kuheshimu mila na desturi za makabila, ili kuepuka umwagaji damu na kushauri kuwa ni vema vyama vya siasa katika kampeni kuzingatia hilo.

      Alisema eneo la Arumeru Mashariki ni tete na lenye ushindani mkubwa wa kisiasa na kutokana na hilo, aliwataka wagombea wa vyama vyote na viongozi katika kipindi cha kampeni, kufuata kanuni na sheria za maadili ya uchaguzi tofauti na hapo hali inaweza kuwa mbaya.

      ‘’Hatutaki uvunjifu wa amani uwepo kwa kupindisha demokrasia na maadili ya uchaguzi,
      hivyo kila mgombea anapaswa kuzingatia hilo mara moja na vyama vinapaswa kukubali matokeo na si kuchukua sheria mkononi,” alisema.

      Msajili alisema; ‘’ujambazi wa siasa’’ hautaruhusiwa katika kampeni za jimbo hilo kama vile
      kupigana risasi na kumwagiana tindikali, kwani ofisi yake kwa kushirikiana na Polisi watakuwa mstari wa mbele kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa asilimia 100.

      Tendwa alisema matusi, udini, jinsia na kashfa, ni kauli zinazopaswa kuepukwa katika kampeni hizo, kwani zinaweza kuleta madhara makubwa ya umwagaji damu na ni kinyume na maadili ya uchaguzi, lakini viongozi
      nao wanapaswa kuziepuka.

      Source:Habari Leo


    29. #29
      Tanzaniaist's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 29th November 2011
      Location : arusha
      Posts : 124
      Rep Power : 349
      Likes Received
      117
      Likes Given
      2

      Default CCM kweli ni propaganda tu..! Igunga mashekhe, Arumeru washiri

      Husika na kichwa hapo juu..,Nimeamini kwamba chama cha mapinduzi (CCM) hawana jipya katika kufanya kampeni zao huku wakitumia silaha zao za udini,ukabila,unyanda na siasa za majitaka huku silaha yao ya mwisho ni kuchakachua kura...! kwakuwa hawana mbinu nyingine ya kuishinda CHADEMA baada ya kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi na pia kushindwa kufanikisha maisha bora kwa kila Mtanzania kama ilani yao inavyosema!

      katika kampeni za Igunga mwaka jana..,CCM wakishirikiana na mkuu wa wilaya kutengeneza kesi,waliweza kuwatumia masheikh ambao ni makada wa CCM ili kuishambulia Chadema pamoja na kujenga chuki ya waislamu dhidi ya Chadema mwisho wa siku eti Chadema washindwe kwenye uchaguzi kwa kukosa kura za Waislamu,,.bahati nzuri Waislamu sio wajinga au watu wa kupotoshwa kama walivyodhania CCM,CHADEMA walipata kura nyingi tu hadi kufikia mshindi wa pili..!
      tumeona kwamba CCM ni chama cha kidini

      Vile vile kwenye uchaguzi wa Arumeru ambao utafanyika hivi karibuni,..KAMADA GODBLESS LEMA anawanyima usingizi CCM na ndiyo silaha kubwa ya CHADEMA arumeru yaani (striker), wameanza kutumia UKABILA hasa kwa kuwatumia WASHIRI wazee wa kimeru kumtishia kifo GODBLESS LEMA asikanyanyage meru eti kwa kutoa kauli tata kwenye msiba wa sumari...,huku CCM kwa akili zao za kipuuzi wakiamni watakuwa wamemdhibiti LEMA pamoja na kujenga chuki ya kikabila kwa kuwatumia hao WASHIRI kujenga chuki dhidi ya CHADEMA..,Napenda niwaambie CCM, GODBLESS LEMA hatishiwi kifo hata siku moja ndio maana alikuwa tayari kwenda kulala gerezani na vile vile WAMERU sio wajinga kama mnavyozania kwamba kuwatumia washiri kwenye kampeni zenu chafu dhidi ya CHADEMA..!
      na hii zana nimejidhihirisha CCM ni chama cha kikabila kwa kutumia washiri (wazee wa kimeru ) kuifanyia CCM kampeni na kuishambulia CHADEMA ambao hao WASHIRI..!

    30. #30
      KAMANDA HANGA's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 22nd September 2011
      Posts : 127
      Rep Power : 360
      Likes Received
      43
      Likes Given
      0

      Default Re: Tendwa umelikoroga lazima ulinywe!!!

      Naendelea kufatilia kama hiyo press conference imefanyika niwajuze zaidi wana jamvi. Kama kuna mtu kapata mpya kuhusu swala hilo tafadhari tupe latest. Nipo Tengeru naelekea Meru milimani kudadisi kinchoendelea.
      Muchembe likes this.

    Page 1 of 12 12311 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...