Leo nina dukuduku ambalo nataka kulitoa. Sijui kama wenzangu linawatatiza pia. Hivi jamani makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana kazi gani haswa?
Nauliza hivi kutokana na ninayoyaona kwahiyo kama sipo sahihi nitarekebishwa. Kila nikiona kwenye vyombo vya habari namuona makamu wa rais aidha anazindua kitu au ni mgeni rasmi sehemu au anafanya ziara sehemu. Yani amekuwa "mzee wa kukata utepe". Ninachosema ni hivi huyu mtu tunaemuita makamu wa rais tunamlipa na kumhudumia kwa ajili ya kuhudhuria sherehe tu? Kwa nchi masikini kama yetu why do we need a ceremonial leader?
Najua watu wataanza kusema oh ni kwa ajili ya ku-accomodate muungano. Siamini hiyo ni sababu. Kwa maana tunaweza kabisa kufuta nafasi ya makamo wa rais na tukasema rais akitoka upande mmoja wa muungano basi waziri mkuu atoke upande mwingine. Kwanini tupoteze rasilimali za nchi kwa ajili ya kuwa na mtu asiye na shughuli za maana ambazo hata rais na waziri mkuu wanaweza waka gawana na kufanya?
Sina nia ya kumshushia heshima makamu wa raisi wala nafasi ya umakamu wa rais ila ninachosema sasa ifike wakati aidha tumpe makamu wa rais kazi za maana za kufanya au tukifute hiki cheo. Kwa ufahamu wangu, Makamu wa Rais ni msaidizi wa rais kwa maana rais ndiyo anaamua ampe kazi zipi makamu wake. Sasa ni kwamba rais hamuamini makamu wake kumpa kazi zozote za maana?
Makamo wa rais yupo yupo tuu standby just in case anything happens kwa rais!. Ila makamo wa rais anapokuwa mchovu mchovu, hilo nalo neno!
Hilo nalo tatizo. If anything happens to the president siyo bora kuachiwa mtu amabe ana experience ya day to day activities za serikali kuliko kumuachia mtu ambae alikua anakaa kaa tu?
na msafara wake mzito,pkpk magari km 7 hivi,hii nchi ya ajabu sana kwakweli
Yani acha tu. Unnecessary expenditures everywhere. Nakumbuka wakati Bilal ndiyo kwanza anapata umakamu wa raisi JK alimuambia ikiwezekana aendelee kutoa lecture chuo cha UDOM. Sasa kama makamu wa raisi ana muda wa kufundisha na kusafiri mpaka Dodoma kufanya hivyo ina maana ana a lot of free time.
Makamu wa Rais yupo yupo tu na wala hana kazi yoyote tofauti na kula mshahara, kuuza sura na kuzururu huku na huku kwa kutumia kodi za wananchi walalahoi!
Ili kuelewa mkorogo huu wa Makamu wa Rais itakupasa urudi miaka ile siasa za vyama vingi ziliporudishwa katika siasa za Tanzania na Muungano.
Mwanzoni, Rais wa Zanzibar alikuwa automatic anakalia kiti hicho ya Makamu wa Rais na alikuwa anawakilisha maslahi ya Zanzibar katika Muungano.
Tulipofuta utaratibu huo wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ndio tumejikuta na Makamu wa Rais ambaye kama ulivyosema katika kutahadharisha "yupo yupo tu ili kuaccomodate Muungano" lakini hawakilishi Zanzibar au maslahi ya Zanzibar katika Muungano.
Jambo baya ambalo linachochea Zanzibar kulalama na kuutupia madongo Muungano ni ile kumfanya Rais wa Zanzibar kuwa ni (Mjumbe )Waziri asiye na wizara maalum katika Baraza la mawaziri wa muungano.
Ukiangalia kwa undani ,tunaweza kusema kuwa Muungano tuliuvunja siku ile tuliyomfanya mwakilishi mkuu wa upande Zanzibar kuwa hana sauti yoyote katika Muungano.
Neno ulilolitumia "ku-accomodate Muungano" lisomeke funika kombe, au kutia changa la macho ili Muungano uzidi kuonekana kuwa ni kichekesho tu. Ni kweli kama ilivyo leo, Nafasi ya Makamu wa Rais ni ukiritimba tu, cheo ambacho kinafuja fedha za walipa kodi.
Inapotokea watu kuanza kuona Serikali ya Muungano haipaswi kuwa na sura ya Kimuungano basi ujue watu wameanza kufuta tongo, watu wameanza kutoka usingizini na kuona mazingaombwe na ombwe la Muungano usio Muungano.
Hiki cheo kuna haja kufutwa ili iwezeshe kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na serikali ya Zanzibar tayari ipo na kuunda serikali ndogo ya Muungano ambayo, Rais wa Tangayika na Rais wa Zanzibar watatawala kama co-presidency ya Muungano na baraza dogo la wizara za muungano.
Makamu wa Rais ni Gharama tu kwa walipa kodi kwani nafasi hii ipo only to accommodate siasa za muungano. Miaka ya nyuma, nafasi hii ilikuwa more effective kutokana na kuunganishwa kwake na cheo cha Waziri Mkuu na Rais wa Zanzibar ambapo kulikuwa na makamo wa kwanza na makamo wa pili. Kwahiyo cheo cha makamo wa rais kilionekana kina mashiko lakini kumbe kilikuwa kinabebwa zaidi na kofia za waziri mkuu/rais wa znz.
Nyerere alilshauriwa mfumo huu na tume ya Judge Bomani ambae yeye aliiga mfumo wa mgombea mwenza wa Marekani kama njia ya kuondokana na hofu iwapo CUF ingeshinda Uchaguzi ZnZ, kwani chini ya utaratibu wa zamani, rais wa zanzibar alikuwa automatically makamo wa Rais wa muungano. Vilevile mfumo wetu wa muungano nyerere aliiga ule wa UK (Ireland, Wales, Britain). Kwahiyo, with all due respect to baba wa taifa, kuna mambo mengine hayawezi kuwa effective yakiwa to ni 'copy and paste' from another context.
Follow Us Here