Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

    Report Post
    Page 3 of 6 FirstFirst 12345 ... LastLast
    Results 41 to 60 of 113
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,518
      Rep Power : 46714
      Likes Received
      16434
      Likes Given
      8471

      Default Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Kuwalazimisha madaktari kurudi kazini mara moja ama sivyo watajifukuzisha kazi hakubadilishi ukweli wa hali iliyopo. Hata kuwabembeleza warudi kazini mara moja kwa sababu “wagonjwa wanakufa” nako hakubadilishi hali iliyopo. Kwa ufupi, agizo la serikali kutaka madaktari warudi kazini mara moja linapuuzia kabisa madai yao na linatumia ubabe wa madaraka na bila ya shaka nyuma yake kuna tishio la nguvu za dola kulazimisha madaktari. Kwa vile sababu za msingi zilizosababisha mgomo hazijashughulikiwa – hata zile zinazoweza kushughulikiwa mara moja – basi sababu ya uwepo mgomo haijaondolewa au kupunguzwa.

      Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye ametoa tamko la kuwataka madaktari kurudi kazini


      Serikali inaweza kulazimisha madaktari kurudi kazini?
      Serikali ina uwezo wa kulazimisha watu warudi kazini lakini haina uwezo wa kulazimisha watu kufanya kazi. Kwa kutumia tishio au hata nguvu serikali inaweza kuvunja mkutano wa madaktari na kuwakamata viongozi wa mgomo huo na yumkini madaktari wanaweza “kurudi kazini”. Hata hivyo madaktari “kurudi kazini” haina maana wanarudi “kufanya kazi”. Wataweza vipi kufanya kazi yao vizuri kwa uadilifu kama msingi wa malalamiko yao umepuuziwa zaidi ya kuambiwa “madai yenu ni ya msingi na tunayafanyia kazi?”

      Kwa vile serikali haiwezi kulazimisha watu kufanya kazi wazo kuwa madaktari wanalazimishwa kurudi mahospitalini katika mazingira yale yale, yakiwa na vikwazo vile vile ni wazo la hatari. Hivi ni kweli tunaamini kuwa madaktari hawa waliopuuzwa, kudharauliwa na kunyanyaswa wakirudi kuangalia wagonjwa kesho watafanya hivyo vizuri zaidi? Hivi kweli serikali inaamini kuwa maisha ya wagonjwa mikononi mwa madaktari waliopuuzwa yako salama kwa vile madaktari “wamerudi kazini”?

      Mgomo wa madaktari husitishwa kwa makubaliano
      Mgomo wa madaktari hauwezi kuisha kwa kulazimisha au vitisho kwani kwa kufanya hivyo serikali itajikuta inapanda mbegu za mgomo mwingine labda mkubwa zaidi kuliko wa sasa. Huko India mwishoni mwa mwaka jana (kuanzia Disemba 21) madaktari waligoma jimbo la Jaipur. Mgomo wao ulidumu kwa siku 11 na madaktari zaidi ya 10,000 walishiriki. Mwisho serikali ikawaweka ndani madaktari wapatao 500 lakini mwisho wa siku – na baada ya wagonjwa 60 kudaiwa kufa kwa sababu ya mgomo – serikali ilikubali kuwaachilia madaktari wote toka jela, na kuondoa adhabu ya sheria ya kutokugoma na kukubali kuyafanyia kazi madai ya madaktari. Tarehe 1 Januari madaktari wakarudi kazini baada ya makubaliano ya kusitisha mgomo siku moja kabla yake.

      Huko Israeli nako madaktari waligoma mwaka jana kufuatia suala la maslahi vile vile. Mgomo wao ulidumu kwa siku 158 na mwisho wake mwezi Augusti ulikuwa ni makubaliano ambayo serikali ilikubali kuongeza mishahara ya madaktari na kuboresha mazingira yao ya kazi. Badala ya madaktari kusubiri kufukuzwa madaktari walijiuzulu (mass resignations) katika kuonesha kuwa hawakuwa tayari kuburuzwa na serikali. Waziri wa Fedha wa Israeli akitangaza kuishia kwa mgomo huo alikiri kuwa wamefikia makubaliano na madaktari ambayo yamemaliza “mojawapo ya migomo mikubwa zaidi katika historia ya Israeli”. Waziri Mkuu Netanyahu alijikuta akikubali kuwa matokeo ya mgomo ule ilikuwa ni kuboresha maslahi ya madaktari lakini vile vile kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa huduma za afya nchini Israeli.

      Huko Kenya vile vile mgomo wa madaktari wa mwishoni mwa mwaja jana uliishia kwa kufikia makubaliano na serikali ambapo serikali ilikubali kuongeza fedha katika kuboresha miundombinu ya afya, kulipa madeni ya nyuma ya madaktari na kutenga fedha zaidi katika mafunzo n.k Mgomo wao uliodumu kwa siku 10 nao ulimalizwa kwa makubaliano.

      Kwa ufupi, mgomo huu wa kitaifa wa madaktari haupaswi kumalizwa kwa vitisho, kejeli, kupuuzia au dharau. Mgomo unatakiwa kumalizwa kwa makubaliano. Ndio maana ninaamini bila makubaliano mgomo huu unaweza ukazua mgomo mkubwa zaidi kwani mambo ya msingi hayajakubaliwa. Na kwa kweli haupaswi kuisha bila kuweka makubaliano ya msingi ili kuondoa ulazima wa kugoma tena muda si mrefu ujao.

      Kanuni za Makubaliano
      Sasa, kuna msingi wa kusitisha mgomo ambao unategemea kanuni kadhaa. Naamini, makubaliano ya kusitisha mgomo huu lazima yazingatie lau kanuni zifuatazo.

      a. Wagonjwa wapate nafuu – makubaliano yahakikishe kuwa mwisho wa siku ni wagonjwa wanaopata nafuu katika huduma, matibabu na kupona. Utakuwa ni mgomo mbovu kama baada ya makubaliano maisha ya wagonjwa wetu yanarudi pale pale. Hivyo, mambo yote yatakayokubaliwa lazima yazingatie kuwa Wagonjwa wetu wanapatiwa unafuu wa gharama, huduma, na ubora wa hali ya juu wa huduma hiyo. Nje ya hapo mgomo utakuwa umefeli.

      b. Maslahi ya Madaktari ni lazima yaboreshwe na kuinuliwa. Lengo la (a) haliwezi kufikiwa kama madaktari wataendelea kufanya kazi katika miundo mbinu mibovu na hali mbovu ambazo zinawafanya wasiwe makini au waadilifu. Hata mtu anayejitolea anaweza kujitolea zaidi kama kujitolea kwake kunaonekana na kunawezekana. Hivyo, mishahara na posho za madaktari ziongezwe lau kufikia kiasi wanacholipwa Wabunge. Posho za mazingira magumu, on-call, midnight shifts etc ziongezwe mara moja. Kama tunaweza kumpa mbunge shilingi 200,000 kwa kukaa (azungumze au asizungumze) tunaweza kumlipa daktari kiasi hicho kwa zamu ya usiku au mazingira fulani fulani yatakayokubaliwa. Bila ya shaka maslahi ya wafanyakazi wote wa huduma ya afya ni lazima yaangaliwe kwa upana wake. Hili linaweza kuchukua muda mrefu kidogo kukamilika.

      c. Serikali ni lazima itenge fedha za kutosha kuboresha miundo mbinu ya afya ikiwemo suala la nishati, madawa, na vitendea kazi mbalimbali. Hospitali za serikali ni lazima ziwe na kiwango fulani kisichopungua cha vifaa (minimum standard) ili hospitali ifanye kazi. Serikali ni lazima iwekeze vya kutosha kwenye huduma ya afya ili ndani ya miaka angalau mitatu hii kabla hawajaondolewa madarakani- waoneshe kuwa wamebadilisha sekta hii kwa kiasi kikubwa. Siyo kwa kuongeza “idadi” bali kwa kuongeza “ubora”! Katika kuboresha huduma wa sekta ya afya serikali ni lazima iwawabishe viongozi na watendaji ambao wamechangia kufikisha nchi mahali hapa.
      Hivyo, basi kwa kuzingatia kanuni hizo tatu naweza kutoa mapendekezo ya mambo ambayo yanapaswa kukubaliwa na madaktari na serikali ili kusitisha mgomo huu mara moja.

      Serikali:
      1. Kufukuzwa mara moja kwa Waziri wa Afya, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Daktari Mkuu. Hili ni jambo msingi la kwanza kufanywa na serikali kwani hawa watatu walikuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa madaktari hawafikii mahali pa kugoma. Ushahidi wote uliopo wazi hadi hivi sasa umetuonesha kuwa watu hawa watatu wametumia ubabe, dharau na kejeli na kulazimisha mgomo huu. NI LAZIMA WAONDOKE KABLA Mgomo haujasitishwa.

      2. Kutenga fedha za kulipa madeni ya nyuma ya madaktari pamoja na kutenga fedha za kuongeza posho za msingi ambazo zinahusiana na mazingira ya kazi, na usafiri. Kwa vile tayari tunajua serikali inaweza kuongeza posho katikati ya bajeti kwa wabunge tunajua basi inawezekana kufanya hivyo kwa madaktari. Ongezeko la posho hizo liendane na ongezeko la posho walizopewa wabunge. Madaktarii wawe tayari kuahirisha kuongezewa posho hizo endapo posho za wabunge nazo zitafutwa au kupunguzwa.

      3. Serikali itenge fedha sasa hivi kwa ajili ya kufanyia matengenezo vifaa ambavyo havifanyi kazi kwenye mahospitali yetu ikiwemo uagizwaji wa wa vifaa vya kisasa vya kutolea huduma. Kama serikali inaweza kuagiza magari mapya kwa watendaji mbalimbali wa serikali kila mwaka wakati umefika kwa serikali hiyo hiyo kukubali kuagiza vifaa vipya. Kwa kuanzia hospitali zote za mkoa zipatiwe CT Scan kabla ya mwisho wa mwaka huu pamoja na wataalamu wa vifaa hivyo. Hii inazingiatia kanuni ya (a). Vile vile hili linaweza kupatiwa motisha wa kodi (tax incentive). Kama kuna kodi kwenye vifaa vya afya wakati umefika kufuta kodi hizo ili kurahisisha uingizwaje wake nchini.

      4. Serikali ijiwekee viwango (standard) za huduma za afya ambavyo wananchi watarajie kuona kwenye hospitali zao za umma. Hospitali za Umma lazima zionekane zina ubora wa kuweza kushindana na zile za binafsi.

      5. Serikali ifanyie mabadiliko ya sheria inayowapa viongozi haki ya kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa gharama za wananchi. Kwa kadiri ya kwamba viongozi wanahaki hiyo hawawezi kuboresha sekta ya afya kwani mahospitali yetu yatakuwa ni mahali pa kupata rufaa tu za kwenda nje. Kiongozi anayetaka kwenda nje ajipeleke kwa fedha zake mwenyewe au jamaa zake au ndugu zake. Kuendelea kuruhusu hilo ni kuendelea kuruhusu kuvuja kwa fedha zetu kwenda nje ya nchi. Endapo viongozi watajua kuwa wao na watoto wao watatabiwa hapa hapa nchini wataona umuhimu na uharaka wa kuboresha hospitali zetu. Kinyume chake wao wanafikiria kuboresha “hospitali zetu” wakati wenyewe wako tayari kwenda kutibiwa kwenye “hospitali za wenzetu”.

      Kama serikali haitofanya hivi ni matumaini yetu wabunge wa upinzani (ambao nao ni wanufaika wa mfumo huu) wataandaa mswada binafsi wa kuondoa hivi vipengele. Viongozi pekee ambao kwa muda wanaweza kuruhusiwa kuendelea kuangaliwa nje ni wale waliokwisha staafu na wao watapewa nafasi hiyo kwa mwaka mmoja ujao tu baada ya hapo na wao lwao!

      6. Serikali iwe tayari kwa kushirikiana na madaktari kuunda a Special Task Force ambayo itapitia sera na mfumo wetu wa afya na kutoa mapendekezo ndani ya miaka mitatu ya mabadiliko makubwa ya sekta ya afya. STF hiyo iundwe na madaktari na wataalamu wa afya, wa fedha, na wanasheria ili hatimaye ije na mapendekezo ambayo yataanza kuingizwa kwenye bajeti ya mwaka huu ili kufanyia mabadiliko makubwa mfumo wetu wa huduma za afya (major healthcare reform). Waangalie, tatizo liko wapi, fedha zinapotea wapi, nini kibadilishwe na vipi na mwananchi atanufaika vipi katika mabadiliko hayo. Mfumo wa sasa siyo endelevu ni mzigo mkubwa kwa wananchi.

      Madaktari

      1. Kama sehemu ya kuonesha wanajali madaktari watangaze kurudi kazini mara baada ya uongozi wa sasa wa Wizara ya Afya kujiuzulu. Mgomo huu kwa kiasi kikubwa umesababishwa na hawa viongozi kwa hiyo kuumaliza ni lazima hawa waguswe. Wafanyakazi wa afya hawawezi kufanya kazi na hawa watu tena – wamepoteza moral legitimacy kuongoza wizara hiyo hasa baada ya kuachilia vifaa vibovu vya kupima HIV kuendelea kutumika nchini na pia kudharau madai ya madaktari hadi mgomo umetokea. Ni lazima waondoke kama sharti la kwanza la madaktari kurudi kazini na kuzuia wauguzi na wataalamu wengine kujiunga kwenye mgomo huu.

      2. Madaktari wawe tayari kupata ongezeko dogo katika mishahara na mafao mbalimbali wakisubiri STF ije na mapendekezo yake na bajeti mpya. Kiasi gani wakubali inategemea na ofa itakayotolewa na serikali.

      3. Madaktari wawe tayari kurudi kazini mara moja endapo serikali itatenga fedha za dharura kununulia vifaa vya msingi vya huduma ya afya kwa mahospitali yote ya umma. Vitu kama maglovu, sindano, nk ni vitu ambavyo ni lazima viwepo hospitalini. Serikali ikubaliane na madaktari kuwa ndani ya miezi mitatu hospititali zote za umma na za binafsi zitatakiwa kuwa na vifaa vya msingi vya kutolea huduma ya afya. Hii ni pamoja na kutenga fedha za kuhakikisha kuwa hakuna mgonjw anayelala chini kwenye wodi yoyote ile au hospitali yoyote ile. Hii ni mojawapo ya kashfa kubwa za huduma ya afya nchini ni lazima tuondokane nayo.

      4. Madaktari kwa kutumia hiyo STF waandae mapendekezo ya kuboresha elimu na ujuzi wa madaktari ili hatimaye tuweze kupata madaktari wengi zaidi kwa muda mfupi zaidi. Je, nini kinaweza kufanyika kuharakisha mafunzo ya madaktari yenye ubora wa hali ya juu? Hatuwezi kutumia mfumo wetu wa zamani wa kuandaa madaktari kwani itatuchukua muda mrefu sana kuweza kuziba pengo. Lazima tutumie uwezo wetu kubuni mfumo mzuri wa kufundisha madaktari ili kwa haraka – ikiwezekana ndani ya miaka mitano hivi tuweze kuongeza idadi ya madaktari kwa kiasi kikubwa.

      Hayo ni baadhi ya mambo tu yanayoweza kukubaliwa na pande mbili ambayo matokeo yake yatakuwa ni manufaa kwa wananchi. La msingi ni kuwa hatuwezi na hatupaswi kuahirisha huu mgomo kwa vitisho isipokuwa kwa makubaliano. Kuwapa amri madaktari kurudi kazini mara moja ati kwa kufikiria kwamba wasiporudi basi wanafukuzwa kazi na Tanzania italeta madaktari kutoka nje ni kujaribu kukwepa tatizo. Kwanini?

      a. Madaktari wa kigeni hawatakuja kwa kujitolea nao bado watahitaji kulipwa kwani na wenyewe wanatakiwa kuishi maisha ya utu na kufanya kazi mazingira mazuri.

      b. Madaktari mbadala nao wataenda kufanya kazi kwenye mazingira yale yale. Kitakachokuwa kimebadilishwa ni madaktari tu na siyo mazingira ya kazi. Hivyo, wataweza kufanya kazi kwa siku, wiki au mwezi lakini baada ya muda na wao wenyewe watakufanya na yale yale ambayo yametufikisha hapa. Kuleta madaktari wa nje, kutazuia kuvuja kwa damu tu lakini hakutakuwa kumetoa tiba ya kidonda!

      c. Madaktari wetu wenyewe ni madaktari wetu kuwafukuza kazi au kuwaweka nje kwa sababu wamekataa kurudi kazini hakutaondoa
      ukweli kuwa mfumo wetu wa afya ni mbovu na watu wanakufa pasipo ulazima – bila haja ya mgomo! Madaktari wetu wanagombania kitu kikubwa zaidi hao madaktari mbadala watakuja kutibu tu lakini hawatokuja kupigania kuboresha mfumo wetu wa afya.

      d. Wakileta madaktari wengine halafu wauguzi, madaktari wa meno, madaktari wa dawa ya usingizi nao wakagoma kuunga mkono madaktari wao serikali italeta wauguzi kutoka India, Misri na Israeli? Au mwisho italeta hadi wafagizi kugoka nje?
      Kwa ufupi, agizo la Waziri Mkuu kuwa madaktari warudi kazini mara moja bila kufanya nayo makubaliano ni sawasawa na kujaribu kumaliza vita bila kufanya mapatano ya kumaliza mgogoro. Vita havimalizwi kwa truce bali kwa kufanya mapatano ya kumaliza vita (cessation of hostilities). Hili linaweza kufanywa ama kwa kusalimu amri (surrender agreement) ambapo mshindi anatoa terms of surrender (ndivyo inaonekana serikali inafanya) au kwa pande mbili kuona kuwa vita havilipi na hivyo wanaamua kupatana. Ninaamini, serikali inataka kulazimisha surrender bila kupatana.

      Hii ni hatari kwa huduma ya afya. Ni makubaliano tu yatamaliza mgogoro, makubaliano ambayo yatazingatia madai ya madaktari, yatakubali na kuanza kutekeleza sehemu ya madai hayo kama hatua za kujenga imani na vile vile kuweka utaratibu wa kuona mambo mengine yaliyokubaliwa yanatimizwa bila kuchelewa na katika muda muafaka.

      Nje ya hapo, mgomo huu utaduma na hautakoma kwa haraka au kwa vitisho kwani hata madaktari wakikubali kurudi kazini, hakuna mtu anayeweza kuwalazimisha kufanya kazi, na hata wakilazimika kufanya kazi watakuwa wamepewa sababu nyingine ya kufanya mgomo mwingine huko mbeleni. Ndugu zangu, ni bora ujue madaktari wamegoma na wamegoma kuliko kutokujua kuwa daktari anayekuhudumia amegoma moyoni.

      Lakini hakuna kibaya zaidi kama kumshambulia mtu badala ya hoja. Katika vitu vya kushangaza sana Waziri Mkuu ameamua kufanya mashambulizi ya mtu – ad hominem – kwa Dr. Ulimboka katika kuonesha kuwa hoja za madaktari hazina msingi. Hivi, ni kweli kuwa Dr. Ulimboka akiacha kushiriki kwenye mgomo huu manake ni kuwa madai ya madaktari yanafutika? Serikali inaweza kabisa kushambulia watu au mtu yeyote katika kujaribu kuonesha kuwa inawajua watu hao na inaweza kuwasema vibaya vyovyote vile lakini ukweli wa hoja zao utasimama ulivyo.

      Ukiona watu wanamshambulia mtu badala ya hoja zake, manake ni kuwa tayari wameshindwa hoja sasa wanataka kutumia nguvu! Kama watu wengine wanavyouliza mbona hatujaambiwa mambo ya wabunge ambao wamesimama kutetea posho? Au na yeye watu waanze kuulizia kwanini anatetea wafanyabiashara wakubwa kuchukua maeneo makubwa ya ardhi nchini? Hoja zijibiwa kwe hoja siyo viroja!

      Ni hatari kwa wagonjwa.
      kwa wagonjwa.
      Last edited by Mzee Mwanakijiji; 30th January 2012 at 03:53.

    2. RukaaJuu Final

    3. #41
      gogomoka's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th June 2008
      Posts : 69
      Rep Power : 572
      Likes Received
      49
      Likes Given
      240

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Kwanza huu n mgomo ambao ungeweza kuepukika mapema kweli lakini hapa ulipofikia si pazuri kabisa.
      Mwanakijiji,

      Tupo ukurasa mmoja. Mie naona mgomo ulipofikia ndio pazuri kwani tunakaribia apex ya ukombozi wa kifikra kwa watanzania wote. Come 2015 (kama watafika maana wengine wanaweza kuwa Hague kama Gbagbo) kila kura italindwa kwa hali na mali. Kwenye kampeni inakuwa ni kuwakumbusha kuhusu ndugu zetu waliokufa kutokana na uzembe wa viongozi wao waliowaamini kwa miaka 50+.

    4. #42
      Kombo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th October 2010
      Posts : 1,825
      Rep Power : 800
      Likes Received
      455
      Likes Given
      40

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Quote By Ngisibara
      RichardBrunwick
      26 January 2012 2:33PM
      Tanzania's Kikwete is one of the most pathetic African leaders of our times. He is a peacetime leader for a country known to be one of the richest in the world in terms of natural resources, yet he leades the world with begging. Foreign companies have known Tanzania to be a free land in which you can go in and take all you can without being asked a question. I really don't get the mind set of its leaders especially their prsident Mr. Kikwete, a Muzungu worshiper. Having worked with the UNDP in that country for 8 years, I realized how inneficient and corrupt the country's leadership is. His ministers that requested bribes from BAE have never been tried despite the damning evidence against them. British TAX payers must stop funding this man's corruptin and foreign trips. His human rights record is horrible. Mr. Kikwete had no business of going to Davos to ask for foreign aid. Already his country is the world third leading foreign Aid dependant nation. He should be embarassed to say to the world that people are poor. His people living "hand to mouth " is his own is own ignorance and stupidity.That is hiw own problem, Brits are having their own problems he must realize that. We cant bankroll his foreign trips. He should make good use of his country's wealth. Instead of letting his corrupt officials and foreigners loot his country, he needs to think before letting himself be a global loughing stock. I read in one of the regional (kenyan) publication the mockery nature related to his frequent foreign trips. Palestinian, Haiti, Lebanon, Somalia and even Rwanda economies are more robust that of Tanzania. We must question the nations that welcomes this "Joker's" request for AID. He needs to be on a "no-fly" list so he can be serious. Hopefully the billionaires questions what he has done with the Money he has received for decades. The Arab spring should turn into the African summer and get rid of the Kikwete. likes
      (http://www.guardian.co.uk/discussion...alink/14344505)
      Daaah..!! Haya matusi sasa!

    5. #43
      zumbemkuu's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 11th September 2010
      Location : street dweller
      Posts : 5,345
      Rep Power : 2004
      Likes Received
      2124
      Likes Given
      7828

      Default Mgogoro wa madaktari

      Nimeisikiliza hotuba ya waziri mkuu kuhusu mgomo wa madaktari kama mtiririko wa matukio ni ule aliyoeleza waziri mkuu, waziri mkuu ame’missimage mgogoro huo.

      Kasoro ya 1: yalikuwa ni makosa makubwa kukubali kuongea na madaktari zaidi ya mia nne (400) kwa sababu sio rahisi kupata suluhu ya mvutano katika mkusanyiko wa watu mia nne, yeye angekubali kuongea na wawakilishi.

      Kasoro ya 2: ni kutoa majibu ya mkato tuu kuwa madai ya nyongeza ya tshs3,000,000/= hayawezekani. Nakubaliana na madai ya nyongeza ya mshahara toka tshs.900,000/= hadi tshs.3,000,000/= ni unrealistic lakini angewauliza hao madaktari wametumia vigezo vipi kufikia ongezeko la madai ya zaidi ya 300%, inawezekana madaktari walijiropokea tu, angewauliza vigezo wangejiona hawana hoja. Pia angewaeleza financial implications za madai yao kitaifa , madaktari ni watu wenye vipaji vya akili ya juu na ni waelewa wangemwelewa. Majibu yaliyotelewa ya mkato hayakuwa ya kutafuta mwanzo wa mazungumzo ya kutafuta mwafaka. Hapa pia ni upungufu wa kutafuta mwafaka.

      Kasoro ya 3: madaktari pia walitaka walipwe risk allowance, hili lingeweza kutolewa ufumbuzi, wangeambiwa wa classify hizo risks kwa sababu siyo wote wana risk zinazofanana, kukubali hili lingewapa muda wa kutafakari na pia lingeweza kuwagawa na kupunguza makali, hapa sielewi ilipataje kigugumizi . madaktari pia walitaka walipwe hardship allowance hili pia halina utata, mbona wafanyakazi wengine wanaopelekwa mfano kasulu, kibondo n.k wanalipwa kwanini isiwe madaktari? Hapo waziri mkuu amewapotosha wananchi.

      Kasoro 4: madaktari walitaka wapewe au wakopeshwe magari, hapa sioni utata. Serikali ingewakopesha kwa awamu na wengine wangelipwa transport allowance, kuna mashirika ya Umma karibu yote hapa nchini yanatoa transport allowance kwa wafanyakazi wao kufuatana na vigezo mbali mbali.

      Kasoro ya 5: waziri mkuu ameshindwa kutoa majibu ya madai ya nyumba kwa madaktari. Naamini madaktari sio vichaa, siamini wangetegemea wapewe nyumba siku ya pili yake. Wangepewa housing allowance ambazo mashirika mengi ya umma hapa nchini wanatoa kwa wafanyakazi wao. Sidhani km ingekuwa mgogoro.

      Kasoro ya 6. Kwamba madaktari walitaka madai yao yatekelezwe mara moja. Hii tafsiri kwa waziri mkuu ni kama AMRI au DHARAU, madaktari walitaka makubaliano sio utekelezaji ufanyike siku hiyohiyo moja, au wajenge nyumba siku hiyo hiyo, hili lingeweza kuongelewa bila viongozi kujiona wamedhalilishwa.

      Kasoro ya 7: waziri mkuu kugusia maslahi binafsi ya madktari kama yalivyoainishwa kwenye madai yao bila hata kugusa mazingira ya kazi na vitendea kazi kama walivyoainisha kwenye madai yao, hapo waziri mkuu alikuwa na lengo la kuwagombanisha madaktari na wananchi.

      Mwisho kabisa ni kuwapiga marufuku wasikutane popote. Serikali imewafukuza kazi hii inatosha, wasikutane popote hii inatoka wapi na kwenye katiba ipi, huu ni ufashist.
      "watakaotubeza na kututukana wasameheni wanahitaji ukombozi wa fikra" Mh.G.Lema

    6. #44
      zumbemkuu's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 11th September 2010
      Location : street dweller
      Posts : 5,345
      Rep Power : 2004
      Likes Received
      2124
      Likes Given
      7828

      Default Re: Mgogoro wa madaktari

      kwenye heading nilitaka niweke MGOGORO WA MADAKTARI-WAZIRI MKUU AMETELEZA, mods mnaweza mkanisaidia.
      Last edited by zumbemkuu; 30th January 2012 at 20:53.
      "watakaotubeza na kututukana wasameheni wanahitaji ukombozi wa fikra" Mh.G.Lema

    7. #45
      We know next's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2010
      Posts : 574
      Rep Power : 556
      Likes Received
      151
      Likes Given
      119

      Default Re: Mgogoro wa madaktari

      Nadhani ingesomeka vizuri. " Mgogoro wa Madaktari Waziri Mkuu Amekurupuka"

    8. Miaka 50

    9. #46
      zumbemkuu's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 11th September 2010
      Location : street dweller
      Posts : 5,345
      Rep Power : 2004
      Likes Received
      2124
      Likes Given
      7828

      Default Re: Mgogoro wa madaktari

      Quote By We know next
      Nadhani ingesomeka vizuri. " Mgogoro wa Madaktari Waziri Mkuu Amekurupuka"
      hili ndo sahihi kabisa, maana serikali nzima kuanzia raisi ni watu wakukurupuka tu, sijui wana ugonjwa gani? serikali ya kukurupuka.
      Last edited by zumbemkuu; 30th January 2012 at 16:21.
      "watakaotubeza na kututukana wasameheni wanahitaji ukombozi wa fikra" Mh.G.Lema

    10. #47
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,352
      Rep Power : 12596
      Likes Received
      5870
      Likes Given
      781

      Default Re: Mgogoro wa madaktari

      Mods unganisha hii thread ya madaktari na zingine zimeishakuwa nyingi.

    11. #48
      Gek.com's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 21st January 2012
      Posts : 9
      Rep Power : 371
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Mgogoro wa madaktari

      Jamii, Mbuge ni mtu yeyote ambaye hana hanafani yeyote, ila kwa swala la madaktari hawa sio watu wa ovyo ovyo lazima awe na UJUZI,So ina kuaje wabunge waongezewe mshahara na watu wanaoshika vinyes,mikojo ,damu na hata wanao jali afya zetu,hawaongezewi risk allawance na mambo mengne kama hayo.

    12. #49
      zumbemkuu's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 11th September 2010
      Location : street dweller
      Posts : 5,345
      Rep Power : 2004
      Likes Received
      2124
      Likes Given
      7828

      Default Re: Mgogoro wa madaktari

      Quote By Gek.com
      Jamii, Mbuge ni mtu yeyote ambaye hana hanafani yeyote, ila kwa swala la madaktari hawa sio watu wa ovyo ovyo lazima awe na UJUZI,So ina kuaje wabunge waongezewe mshahara na watu wanaoshika vinyes,mikojo ,damu na hata wanao jali afya zetu,hawaongezewi risk allawance na mambo mengne kama hayo.
      kinachokosekana kwa viongozi wetu ni busara, wao kila kitu wanaingiza siasa, wanakurupuka kutoa majibu mepesi kwenye maswala mazito yanayohusu uhai wa mtanzania.
      "watakaotubeza na kututukana wasameheni wanahitaji ukombozi wa fikra" Mh.G.Lema

    13. #50
      Edward Teller's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2010
      Location : Area 51
      Posts : 3,431
      Rep Power : 1120
      Likes Received
      570
      Likes Given
      612

      Default Re: Mgogoro wa madaktari

      Quote By zumbemkuu
      Nimeisikiliza hotuba ya waziri mkuu kuhusu mgomo wa madaktari kama mtiririko wa matukio ni ule aliyoeleza waziri mkuu, waziri mkuu ame’missimage mgogoro huo.

      Kasoro ya 1: yalikuwa ni makosa makubwa kukubali kuongea na madaktari zaidi ya mia nne (400) kwa sababu sio rahisi kupata suluhu ya mvutano katika mkusanyiko wa watu mia nne, yeye angekubali kuongea na wawakilishi.

      Kasoro ya 2: ni kutoa majibu ya mkato tuu kuwa madai ya nyongeza ya tshs3,000,000/= hayawezekani. Nakubaliana na madai ya nyongeza ya mshahara toka tshs.900,000/= hadi tshs.3,000,000/= ni unrealistic lakini angewauliza hao madaktari wametumia vigezo vipi kufikia ongezeko la madai ya zaidi ya 300%, inawezekana madaktari walijiropokea tu, angewauliza vigezo wangejiona hawana hoja. Pia angewaeleza financial implications za madai yao kitaifa , madaktari ni watu wenye vipaji vya akili ya juu na ni waelewa wangemwelewa. Majibu yaliyotelewa ya mkato hayakuwa ya kutafuta mwanzo wa mazungumzo ya kutafuta mwafaka. Hapa pia ni upungufu wa kutafuta mwafaka.

      Kasoro ya 3: madaktari pia walitaka walipwe risk allowance, hili lingeweza kutolewa ufumbuzi, wangeambiwa wa classify hizo risks kwa sababu siyo wote wana risk zinazofanana, kukubali hili lingewapa muda wa kutafakari na pia lingeweza kuwagawa na kupunguza makali, hapa sielewi ilipataje kigugumizi . madaktari pia walitaka walipwe hardship allowance hili pia halina utata, mbona wafanyakazi wengine wanaopelekwa mfano kasulu, kibondo n.k wanalipwa kwanini isiwe madaktari? Hapo waziri mkuu amewapotosha wananchi.

      Kasoro 4: madaktari walitaka wapewe au wakopeshwe magari, hapa sioni utata. Serikali ingewakopesha kwa awamu na wengine wangelipwa transport allowance, kuna mashirika ya Umma karibu yote hapa nchini yanatoa transport allowance kwa wafanyakazi wao kufuatana na vigezo mbali mbali.

      Kasoro ya 5: waziri mkuu ameshindwa kutoa majibu ya madai ya nyumba kwa madaktari. Naamini madaktari sio vichaa, siamini wangetegemea wapewe nyumba siku ya pili yake. Wangepewa housing allowance ambazo mashirika mengi ya umma hapa nchini wanatoa kwa wafanyakazi wao. Sidhani km ingekuwa mgogoro.

      Kasoro ya 6. Kwamba madaktari walitaka madai yao yatekelezwe mara moja. Hii tafsiri kwa waziri mkuu ni kama AMRI au DHARAU, madaktari walitaka makubaliano sio utekelezaji ufanyike siku hiyohiyo moja, au wajenge nyumba siku hiyo hiyo, hili lingeweza kuongelewa bila viongozi kujiona wamedhalilishwa.

      Kasoro ya 7: waziri mkuu kugusia maslahi binafsi ya madktari kama yalivyoainishwa kwenye madai yao bila hata kugusa mazingira ya kazi na vitendea kazi kama walivyoainisha kwenye madai yao, hapo waziri mkuu alikuwa na lengo la kuwagombanisha madaktari na wananchi.

      Mwisho kabisa ni kuwapiga marufuku wasikutane popote. Serikali imewafukuza kazi hii inatosha, wasikutane popote hii inatoka wapi na kwenye katiba ipi, huu ni ufashist.
      yaani PM hataki kujua kitu inaitwa freedom of assembly,ambapo kwa kufanya hivyo anapingana kabisa na human rights
      zumbemkuu likes this.
      “Talk slowly but think quickly”

    14. #51
      Mr. Zero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2007
      Posts : 4,076
      Rep Power : 1436
      Likes Received
      481
      Likes Given
      72

      Default Re: Mgogoro wa madaktari

      Hii thread ikiunganishwa na nyingine watu watashindwa kupata huu uchambuzi mzuri!!!

      Ukweli ni kuwa madaktari wameanza na 3,000, 000 ili wakienda kwenye bagaining walau wanaweza kupata 1.5 m. Sasa serikali inaanza kupoliticise huu mgomo kwa vile wanajuwa ukuiendelea sana unaweza ukabadilika na kuwa wa kisiasa. Kumbuka Tunisia revolution ilianzishwa na machinga moja tu.

      Twist nyingine inakuja, serikali inajua kuwa kama itakubali madai yote ya madaktari ............ next watakuwa nurses.................... then Lecturers na baada ya hapo makunguru (Waalimu). Kwa hiyo serikali itakomaa na kujaribu kuwamaliza nguvu taratibu. Nafikiri by the end of next week Rais atakuwa ameshawaita wazee wa CCM kupiga propaganda.

      All in all posho ya wabunge imezua mambo!! Pamoja na madai ya madaktari kuwa ya msingi.... Je serikali ina pesa za kumudu hivyo viwango??
      zumbemkuu likes this.
      "The Only Necessary for the Triumph of Evil is for Good Men to do Nothing" Edmund Burke (1729 - 97)

    15. #52
      Uwezo Tunao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 6,916
      Rep Power : 2298
      Likes Received
      1155
      Likes Given
      1500

      Default Re: Mgogoro wa madaktari

      Mkuu, you are a gret thinker nimekukubali uchambuzi wako.

    16. #53
      Mokerema's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th November 2011
      Posts : 236
      Rep Power : 427
      Likes Received
      117
      Likes Given
      84

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Mzee MMNakushukuru kwa ulivyojitahidi kuweka mpangilio Mzuri wa hii mada. Nakuomba iwekwe kwa Mwanahalisi kama hajafunga. Nilishasema. Pinda is a govt boy. For all his life amezoea kutoa amri kwa Askari wa chini yake. Umefika muda wa kuondoka hata Kenya wamevumilia mgomo wa Madaktari for almost 2weeks na hawakuwafukuza. Hatuna Madaktari sasa ukifukuza hata hao 200 interns ni wengi. Nashauri mazungumzo! Hao wanajeshi wanalipwa shillingi ngapi?

    17. #54
      Jeremiah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th February 2009
      Location : Geita
      Posts : 334
      Rep Power : 589
      Likes Received
      41
      Likes Given
      25

      Default Re: Mgogoro wa madaktari

      I agree with your points. You are a real great thinker . You are over Jk and Tha son of the farmer.

    18. #55
      Izack Mwanahapa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st April 2011
      Location : Mwanza
      Posts : 314
      Rep Power : 472
      Likes Received
      129
      Likes Given
      94

      Default Athari za Tamko la Pinda dhidi ya mgomo wa Madaktari

      Nianze kwa kusema: Ninaogopa sana kama kweli madactari watarudi kazini kwa vitisho kwa necha ya taaluma yao na kazi wanayoifanya kwa sababu moja tu ya “hofu ya kupoteza kazi” Hili likitokea Madactari hawa watakuwepo kazini lakini morali yao ya kufanya kazi itakuwa imepotea kabisa na hili linaweza kupelekea “Mgomo baridi” ambao kwangu nauona ni hatari zaidi kuliko mgomo unaoendelea sasa.


      Athali za matumizi ya ubabe katika mambo ya msingi Tumeona mfano mara baada ya kuzuwia kwa vitisho kwa mgomo wa waalimu hapa nchini, matokeo yake ni kwamba walimu wanakwenda shuleni kama wajibu lakini hawatekelezi kazi ipasavyo na kimsingi huu ni mgomo baridi ambao bado unaendelea matokeo yake wanafunzi wanamaliza elimu ya msingi lakini hawajui kusoma, kuandika wala kuhesabu. Wapo wanafunzi wa darasa la tano lakini hawawezi kujibu mtihani wa darasa la pili. Utafiti uliofanywa na Uwezo Tanzania Uwezo.net


      Serikali imechukua hatua gani juu ya tatizo la kufeli kwa wanafunzi? Naamini wote hapa ni wafuatiliaji wazuri wa habari, zifuatazo ni baadhi ya hatua ambazo serikali imezichukua ambazo si kati ya kelo zinazolalamikiwa na walimu:


      1. 1. Matumizi ya simu za mkononi kwa wanafunzi yamepigwa marufuku
      2. 2. Waziri wa elimu anasema wanafunzi waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza watapimwa tena kabla hawajaanza sekondari na atakayefeli mkuu wake wa shule atawajibishwa
      3. 3. Mtihani wa kidato cha pili umerejeshwa
      4. 4. Michango ya masomo ya ziada imepigwa marufuku

      NOTE:

      Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2010 kati ya wanafunzi 353840 waliofanya mtihani huo ni wanafunzi 40,388 tu ndio waliofaulu kwa daraja la kwanza hadi la tatu.


      Kwa upande wa Madactari Sasa tujiulize, kama madactari nao watarudi kazini na kuendesha mgomo baridi watanzania tutakuwa kwenye wakati gani? Ni bora ya sasa kila mtu anajua wamegoma hivyo anakwenda kwenye hospitali binafsi lakini katika mgomo baridi hatutajua madactari wanaweza wakawepo na wakatupa matibabu tofauti yatakayopelekea athari mbaya kwa wananchi. Lakini pia Tanzania haina madactari mbadala wa kujaza nafasi za madactari hawa ikiwa wataondolewa kazini kama inavyosemwa. Siamini kama matumizi ya mabavu yatalete suluhu katika jambo hili na mwisho wa siku wanaokuja kuumia ni masikini waliopewa jina “WATANZANIA WA KAWAIDA”

    19. #56
      NG'OMBE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th March 2011
      Posts : 291
      Rep Power : 438
      Likes Received
      60
      Likes Given
      125

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Serikali inakwenda kuiua kabisa sekta ya afya kama walivyoiua sekta ya elimu, Elimu ya Tanzania ilishakufa na sababu ni hizi hizi za kutoa vitisho kwa watumishi. Matokeo yake ni wanafunzi kumaliza la saba hajui hata kusoma na kuandika. Sasa janga hilo linaenea hadi sekta ya afya, watakuja kugundua baadae. Hapa ni wananchi kubadiri fikra zao wakati wa kuchagua viongozi, wasifanye kwa mazoea, lasivyo wataendelea kuteseka huku viongozi wao wakistarehe.

    20. #57
      Bill's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2007
      Posts : 1,663
      Rep Power : 927
      Likes Received
      300
      Likes Given
      203

      Default Re: Athari za Tamko la Pinda dhidi ya mgomo wa Madaktari

      Pinda angetumia mabavu kupambana na ufisadi ama Jairo ningemwelewa. Mbona ni kwa madaktari tu na Chadema.
      "Wanafunzi wanaopata Mimba ni kwa sababu ya kiherehere chao" JK 2010.

    21. #58
      Jackbauer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : CTU
      Posts : 4,876
      Rep Power : 1692
      Likes Received
      1348
      Likes Given
      277

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      sasa nimeanza kuamini.the only way foward ni kwa serikali kushuka na wala haitamaanisha imeogopa,maana yake itatafsrika kuwa serikali inasikiliza wananchi wake.
      You may succeed in silencing me but that silence comes at a price-Alex litvinenko

    22. #59
      LATTICE BOND's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 30th May 2011
      Posts : 219
      Rep Power : 447
      Likes Received
      48
      Likes Given
      17

      Default Re: Mgogoro wa madaktari

      Madaktari nanyi tuambieni mmetumia vigezo gani kufikia hiyo 3,000,000 plus other fringe benefits ambazo mwisho wa siku sitafikia karibu 5,000,000/=
      1. Hamuoni kuwa Polisi nao wanastahili kupata mshahara kama huo maana wao wanahatarisha maisha yao binafsi na maisha ya wale wanaolindwa na hao askari?
      2. Hamuoni askari magereza nao wanahitaji mshahara kama huo maana kazi wanayofanya kulinda wahalifu ni hatari na inawafanya wafanane na hao wafungwa?
      3. Hamuoni walimu nao wanahitaji mshahara kama huo maana uhuru wao wa kuomba rikizo muda wanaotaka kama ninyi mfanyavyo wamenyang'anywa kwa kigezo kwamba wakienda kipindi cha madarasa wanafunzi hawatapata elimu?
      4. Hamuoni kuwa uhamiaji nao wanahitaji mshahara kama wenu maana wanafanya kazi hatari ya kuhakikisha nchi hii haipati wageni wasio rasmi hivyo kukulinda wewe na wenzako dhidi ya wageni wa aina hiyo?
      .
      .
      .
      .
      .
      Kitendo walichofanyiwa interns si cha kiungwani. Ingekuwa vema kama mngeendelea na hoja zenu za kushinikiza Mponda, Nkya, Nyoni na Mtasiwa wafukuzwe. kwa kufanya hivo mngeonyesha usomi na weledi!! ila mambo mnayodai ni ubinafsi ambao hauna tofauti na ule ubinafsi wa Wabunge!!!
      Kwanza mnaposema kazi na kutibu mgonjwa ni hatari kwa afya yako nami ntasema kazi wa kuwasha mtambo wa kahansi au kulinda majambazi gerezani ni hatari. Lakini hatari hizo zoote nlizozitaja zinaondolewa na mafunzo nyote mlopata kwa kazi husika kwa hiyo msije na visingizio vya hatari!!!
      BADALISHENI MAUDHUI YA MGOMO WENU AU RUDINI KAZINI!!!!!!!!!!!!

    23. #60
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7663
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Mzee Mwanakijiji,
      Niseme mathlan unakubaliana na madai ya madaktari..mimi siyajui vizuri zaidi ya yale yaliyowekwa hapa JF..nakuomba wewe kama serikali au waziri mkuu ni yapi utakubaliana nayo na yapi hutakubaliana nayo na kwa kufanya nini?. Ili madaktari warudi kazini ni mazingira gani ya kazi utayabadilisha kulingana na madai yao.
      Exploration of reality

    Page 3 of 6 FirstFirst 12345 ... LastLast

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...