Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

    Report Post
    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 113
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,499
      Rep Power : 46709
      Likes Received
      16347
      Likes Given
      8417

      Default Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Kuwalazimisha madaktari kurudi kazini mara moja ama sivyo watajifukuzisha kazi hakubadilishi ukweli wa hali iliyopo. Hata kuwabembeleza warudi kazini mara moja kwa sababu “wagonjwa wanakufa” nako hakubadilishi hali iliyopo. Kwa ufupi, agizo la serikali kutaka madaktari warudi kazini mara moja linapuuzia kabisa madai yao na linatumia ubabe wa madaraka na bila ya shaka nyuma yake kuna tishio la nguvu za dola kulazimisha madaktari. Kwa vile sababu za msingi zilizosababisha mgomo hazijashughulikiwa – hata zile zinazoweza kushughulikiwa mara moja – basi sababu ya uwepo mgomo haijaondolewa au kupunguzwa.

      Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye ametoa tamko la kuwataka madaktari kurudi kazini


      Serikali inaweza kulazimisha madaktari kurudi kazini?
      Serikali ina uwezo wa kulazimisha watu warudi kazini lakini haina uwezo wa kulazimisha watu kufanya kazi. Kwa kutumia tishio au hata nguvu serikali inaweza kuvunja mkutano wa madaktari na kuwakamata viongozi wa mgomo huo na yumkini madaktari wanaweza “kurudi kazini”. Hata hivyo madaktari “kurudi kazini” haina maana wanarudi “kufanya kazi”. Wataweza vipi kufanya kazi yao vizuri kwa uadilifu kama msingi wa malalamiko yao umepuuziwa zaidi ya kuambiwa “madai yenu ni ya msingi na tunayafanyia kazi?”

      Kwa vile serikali haiwezi kulazimisha watu kufanya kazi wazo kuwa madaktari wanalazimishwa kurudi mahospitalini katika mazingira yale yale, yakiwa na vikwazo vile vile ni wazo la hatari. Hivi ni kweli tunaamini kuwa madaktari hawa waliopuuzwa, kudharauliwa na kunyanyaswa wakirudi kuangalia wagonjwa kesho watafanya hivyo vizuri zaidi? Hivi kweli serikali inaamini kuwa maisha ya wagonjwa mikononi mwa madaktari waliopuuzwa yako salama kwa vile madaktari “wamerudi kazini”?

      Mgomo wa madaktari husitishwa kwa makubaliano
      Mgomo wa madaktari hauwezi kuisha kwa kulazimisha au vitisho kwani kwa kufanya hivyo serikali itajikuta inapanda mbegu za mgomo mwingine labda mkubwa zaidi kuliko wa sasa. Huko India mwishoni mwa mwaka jana (kuanzia Disemba 21) madaktari waligoma jimbo la Jaipur. Mgomo wao ulidumu kwa siku 11 na madaktari zaidi ya 10,000 walishiriki. Mwisho serikali ikawaweka ndani madaktari wapatao 500 lakini mwisho wa siku – na baada ya wagonjwa 60 kudaiwa kufa kwa sababu ya mgomo – serikali ilikubali kuwaachilia madaktari wote toka jela, na kuondoa adhabu ya sheria ya kutokugoma na kukubali kuyafanyia kazi madai ya madaktari. Tarehe 1 Januari madaktari wakarudi kazini baada ya makubaliano ya kusitisha mgomo siku moja kabla yake.

      Huko Israeli nako madaktari waligoma mwaka jana kufuatia suala la maslahi vile vile. Mgomo wao ulidumu kwa siku 158 na mwisho wake mwezi Augusti ulikuwa ni makubaliano ambayo serikali ilikubali kuongeza mishahara ya madaktari na kuboresha mazingira yao ya kazi. Badala ya madaktari kusubiri kufukuzwa madaktari walijiuzulu (mass resignations) katika kuonesha kuwa hawakuwa tayari kuburuzwa na serikali. Waziri wa Fedha wa Israeli akitangaza kuishia kwa mgomo huo alikiri kuwa wamefikia makubaliano na madaktari ambayo yamemaliza “mojawapo ya migomo mikubwa zaidi katika historia ya Israeli”. Waziri Mkuu Netanyahu alijikuta akikubali kuwa matokeo ya mgomo ule ilikuwa ni kuboresha maslahi ya madaktari lakini vile vile kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa huduma za afya nchini Israeli.

      Huko Kenya vile vile mgomo wa madaktari wa mwishoni mwa mwaja jana uliishia kwa kufikia makubaliano na serikali ambapo serikali ilikubali kuongeza fedha katika kuboresha miundombinu ya afya, kulipa madeni ya nyuma ya madaktari na kutenga fedha zaidi katika mafunzo n.k Mgomo wao uliodumu kwa siku 10 nao ulimalizwa kwa makubaliano.

      Kwa ufupi, mgomo huu wa kitaifa wa madaktari haupaswi kumalizwa kwa vitisho, kejeli, kupuuzia au dharau. Mgomo unatakiwa kumalizwa kwa makubaliano. Ndio maana ninaamini bila makubaliano mgomo huu unaweza ukazua mgomo mkubwa zaidi kwani mambo ya msingi hayajakubaliwa. Na kwa kweli haupaswi kuisha bila kuweka makubaliano ya msingi ili kuondoa ulazima wa kugoma tena muda si mrefu ujao.

      Kanuni za Makubaliano
      Sasa, kuna msingi wa kusitisha mgomo ambao unategemea kanuni kadhaa. Naamini, makubaliano ya kusitisha mgomo huu lazima yazingatie lau kanuni zifuatazo.

      a. Wagonjwa wapate nafuu – makubaliano yahakikishe kuwa mwisho wa siku ni wagonjwa wanaopata nafuu katika huduma, matibabu na kupona. Utakuwa ni mgomo mbovu kama baada ya makubaliano maisha ya wagonjwa wetu yanarudi pale pale. Hivyo, mambo yote yatakayokubaliwa lazima yazingatie kuwa Wagonjwa wetu wanapatiwa unafuu wa gharama, huduma, na ubora wa hali ya juu wa huduma hiyo. Nje ya hapo mgomo utakuwa umefeli.

      b. Maslahi ya Madaktari ni lazima yaboreshwe na kuinuliwa. Lengo la (a) haliwezi kufikiwa kama madaktari wataendelea kufanya kazi katika miundo mbinu mibovu na hali mbovu ambazo zinawafanya wasiwe makini au waadilifu. Hata mtu anayejitolea anaweza kujitolea zaidi kama kujitolea kwake kunaonekana na kunawezekana. Hivyo, mishahara na posho za madaktari ziongezwe lau kufikia kiasi wanacholipwa Wabunge. Posho za mazingira magumu, on-call, midnight shifts etc ziongezwe mara moja. Kama tunaweza kumpa mbunge shilingi 200,000 kwa kukaa (azungumze au asizungumze) tunaweza kumlipa daktari kiasi hicho kwa zamu ya usiku au mazingira fulani fulani yatakayokubaliwa. Bila ya shaka maslahi ya wafanyakazi wote wa huduma ya afya ni lazima yaangaliwe kwa upana wake. Hili linaweza kuchukua muda mrefu kidogo kukamilika.

      c. Serikali ni lazima itenge fedha za kutosha kuboresha miundo mbinu ya afya ikiwemo suala la nishati, madawa, na vitendea kazi mbalimbali. Hospitali za serikali ni lazima ziwe na kiwango fulani kisichopungua cha vifaa (minimum standard) ili hospitali ifanye kazi. Serikali ni lazima iwekeze vya kutosha kwenye huduma ya afya ili ndani ya miaka angalau mitatu hii kabla hawajaondolewa madarakani- waoneshe kuwa wamebadilisha sekta hii kwa kiasi kikubwa. Siyo kwa kuongeza “idadi” bali kwa kuongeza “ubora”! Katika kuboresha huduma wa sekta ya afya serikali ni lazima iwawabishe viongozi na watendaji ambao wamechangia kufikisha nchi mahali hapa.
      Hivyo, basi kwa kuzingatia kanuni hizo tatu naweza kutoa mapendekezo ya mambo ambayo yanapaswa kukubaliwa na madaktari na serikali ili kusitisha mgomo huu mara moja.

      Serikali:
      1. Kufukuzwa mara moja kwa Waziri wa Afya, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Daktari Mkuu. Hili ni jambo msingi la kwanza kufanywa na serikali kwani hawa watatu walikuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa madaktari hawafikii mahali pa kugoma. Ushahidi wote uliopo wazi hadi hivi sasa umetuonesha kuwa watu hawa watatu wametumia ubabe, dharau na kejeli na kulazimisha mgomo huu. NI LAZIMA WAONDOKE KABLA Mgomo haujasitishwa.

      2. Kutenga fedha za kulipa madeni ya nyuma ya madaktari pamoja na kutenga fedha za kuongeza posho za msingi ambazo zinahusiana na mazingira ya kazi, na usafiri. Kwa vile tayari tunajua serikali inaweza kuongeza posho katikati ya bajeti kwa wabunge tunajua basi inawezekana kufanya hivyo kwa madaktari. Ongezeko la posho hizo liendane na ongezeko la posho walizopewa wabunge. Madaktarii wawe tayari kuahirisha kuongezewa posho hizo endapo posho za wabunge nazo zitafutwa au kupunguzwa.

      3. Serikali itenge fedha sasa hivi kwa ajili ya kufanyia matengenezo vifaa ambavyo havifanyi kazi kwenye mahospitali yetu ikiwemo uagizwaji wa wa vifaa vya kisasa vya kutolea huduma. Kama serikali inaweza kuagiza magari mapya kwa watendaji mbalimbali wa serikali kila mwaka wakati umefika kwa serikali hiyo hiyo kukubali kuagiza vifaa vipya. Kwa kuanzia hospitali zote za mkoa zipatiwe CT Scan kabla ya mwisho wa mwaka huu pamoja na wataalamu wa vifaa hivyo. Hii inazingiatia kanuni ya (a). Vile vile hili linaweza kupatiwa motisha wa kodi (tax incentive). Kama kuna kodi kwenye vifaa vya afya wakati umefika kufuta kodi hizo ili kurahisisha uingizwaje wake nchini.

      4. Serikali ijiwekee viwango (standard) za huduma za afya ambavyo wananchi watarajie kuona kwenye hospitali zao za umma. Hospitali za Umma lazima zionekane zina ubora wa kuweza kushindana na zile za binafsi.

      5. Serikali ifanyie mabadiliko ya sheria inayowapa viongozi haki ya kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa gharama za wananchi. Kwa kadiri ya kwamba viongozi wanahaki hiyo hawawezi kuboresha sekta ya afya kwani mahospitali yetu yatakuwa ni mahali pa kupata rufaa tu za kwenda nje. Kiongozi anayetaka kwenda nje ajipeleke kwa fedha zake mwenyewe au jamaa zake au ndugu zake. Kuendelea kuruhusu hilo ni kuendelea kuruhusu kuvuja kwa fedha zetu kwenda nje ya nchi. Endapo viongozi watajua kuwa wao na watoto wao watatabiwa hapa hapa nchini wataona umuhimu na uharaka wa kuboresha hospitali zetu. Kinyume chake wao wanafikiria kuboresha “hospitali zetu” wakati wenyewe wako tayari kwenda kutibiwa kwenye “hospitali za wenzetu”.

      Kama serikali haitofanya hivi ni matumaini yetu wabunge wa upinzani (ambao nao ni wanufaika wa mfumo huu) wataandaa mswada binafsi wa kuondoa hivi vipengele. Viongozi pekee ambao kwa muda wanaweza kuruhusiwa kuendelea kuangaliwa nje ni wale waliokwisha staafu na wao watapewa nafasi hiyo kwa mwaka mmoja ujao tu baada ya hapo na wao lwao!

      6. Serikali iwe tayari kwa kushirikiana na madaktari kuunda a Special Task Force ambayo itapitia sera na mfumo wetu wa afya na kutoa mapendekezo ndani ya miaka mitatu ya mabadiliko makubwa ya sekta ya afya. STF hiyo iundwe na madaktari na wataalamu wa afya, wa fedha, na wanasheria ili hatimaye ije na mapendekezo ambayo yataanza kuingizwa kwenye bajeti ya mwaka huu ili kufanyia mabadiliko makubwa mfumo wetu wa huduma za afya (major healthcare reform). Waangalie, tatizo liko wapi, fedha zinapotea wapi, nini kibadilishwe na vipi na mwananchi atanufaika vipi katika mabadiliko hayo. Mfumo wa sasa siyo endelevu ni mzigo mkubwa kwa wananchi.

      Madaktari

      1. Kama sehemu ya kuonesha wanajali madaktari watangaze kurudi kazini mara baada ya uongozi wa sasa wa Wizara ya Afya kujiuzulu. Mgomo huu kwa kiasi kikubwa umesababishwa na hawa viongozi kwa hiyo kuumaliza ni lazima hawa waguswe. Wafanyakazi wa afya hawawezi kufanya kazi na hawa watu tena – wamepoteza moral legitimacy kuongoza wizara hiyo hasa baada ya kuachilia vifaa vibovu vya kupima HIV kuendelea kutumika nchini na pia kudharau madai ya madaktari hadi mgomo umetokea. Ni lazima waondoke kama sharti la kwanza la madaktari kurudi kazini na kuzuia wauguzi na wataalamu wengine kujiunga kwenye mgomo huu.

      2. Madaktari wawe tayari kupata ongezeko dogo katika mishahara na mafao mbalimbali wakisubiri STF ije na mapendekezo yake na bajeti mpya. Kiasi gani wakubali inategemea na ofa itakayotolewa na serikali.

      3. Madaktari wawe tayari kurudi kazini mara moja endapo serikali itatenga fedha za dharura kununulia vifaa vya msingi vya huduma ya afya kwa mahospitali yote ya umma. Vitu kama maglovu, sindano, nk ni vitu ambavyo ni lazima viwepo hospitalini. Serikali ikubaliane na madaktari kuwa ndani ya miezi mitatu hospititali zote za umma na za binafsi zitatakiwa kuwa na vifaa vya msingi vya kutolea huduma ya afya. Hii ni pamoja na kutenga fedha za kuhakikisha kuwa hakuna mgonjw anayelala chini kwenye wodi yoyote ile au hospitali yoyote ile. Hii ni mojawapo ya kashfa kubwa za huduma ya afya nchini ni lazima tuondokane nayo.

      4. Madaktari kwa kutumia hiyo STF waandae mapendekezo ya kuboresha elimu na ujuzi wa madaktari ili hatimaye tuweze kupata madaktari wengi zaidi kwa muda mfupi zaidi. Je, nini kinaweza kufanyika kuharakisha mafunzo ya madaktari yenye ubora wa hali ya juu? Hatuwezi kutumia mfumo wetu wa zamani wa kuandaa madaktari kwani itatuchukua muda mrefu sana kuweza kuziba pengo. Lazima tutumie uwezo wetu kubuni mfumo mzuri wa kufundisha madaktari ili kwa haraka – ikiwezekana ndani ya miaka mitano hivi tuweze kuongeza idadi ya madaktari kwa kiasi kikubwa.

      Hayo ni baadhi ya mambo tu yanayoweza kukubaliwa na pande mbili ambayo matokeo yake yatakuwa ni manufaa kwa wananchi. La msingi ni kuwa hatuwezi na hatupaswi kuahirisha huu mgomo kwa vitisho isipokuwa kwa makubaliano. Kuwapa amri madaktari kurudi kazini mara moja ati kwa kufikiria kwamba wasiporudi basi wanafukuzwa kazi na Tanzania italeta madaktari kutoka nje ni kujaribu kukwepa tatizo. Kwanini?

      a. Madaktari wa kigeni hawatakuja kwa kujitolea nao bado watahitaji kulipwa kwani na wenyewe wanatakiwa kuishi maisha ya utu na kufanya kazi mazingira mazuri.

      b. Madaktari mbadala nao wataenda kufanya kazi kwenye mazingira yale yale. Kitakachokuwa kimebadilishwa ni madaktari tu na siyo mazingira ya kazi. Hivyo, wataweza kufanya kazi kwa siku, wiki au mwezi lakini baada ya muda na wao wenyewe watakufanya na yale yale ambayo yametufikisha hapa. Kuleta madaktari wa nje, kutazuia kuvuja kwa damu tu lakini hakutakuwa kumetoa tiba ya kidonda!

      c. Madaktari wetu wenyewe ni madaktari wetu kuwafukuza kazi au kuwaweka nje kwa sababu wamekataa kurudi kazini hakutaondoa
      ukweli kuwa mfumo wetu wa afya ni mbovu na watu wanakufa pasipo ulazima – bila haja ya mgomo! Madaktari wetu wanagombania kitu kikubwa zaidi hao madaktari mbadala watakuja kutibu tu lakini hawatokuja kupigania kuboresha mfumo wetu wa afya.

      d. Wakileta madaktari wengine halafu wauguzi, madaktari wa meno, madaktari wa dawa ya usingizi nao wakagoma kuunga mkono madaktari wao serikali italeta wauguzi kutoka India, Misri na Israeli? Au mwisho italeta hadi wafagizi kugoka nje?
      Kwa ufupi, agizo la Waziri Mkuu kuwa madaktari warudi kazini mara moja bila kufanya nayo makubaliano ni sawasawa na kujaribu kumaliza vita bila kufanya mapatano ya kumaliza mgogoro. Vita havimalizwi kwa truce bali kwa kufanya mapatano ya kumaliza vita (cessation of hostilities). Hili linaweza kufanywa ama kwa kusalimu amri (surrender agreement) ambapo mshindi anatoa terms of surrender (ndivyo inaonekana serikali inafanya) au kwa pande mbili kuona kuwa vita havilipi na hivyo wanaamua kupatana. Ninaamini, serikali inataka kulazimisha surrender bila kupatana.

      Hii ni hatari kwa huduma ya afya. Ni makubaliano tu yatamaliza mgogoro, makubaliano ambayo yatazingatia madai ya madaktari, yatakubali na kuanza kutekeleza sehemu ya madai hayo kama hatua za kujenga imani na vile vile kuweka utaratibu wa kuona mambo mengine yaliyokubaliwa yanatimizwa bila kuchelewa na katika muda muafaka.

      Nje ya hapo, mgomo huu utaduma na hautakoma kwa haraka au kwa vitisho kwani hata madaktari wakikubali kurudi kazini, hakuna mtu anayeweza kuwalazimisha kufanya kazi, na hata wakilazimika kufanya kazi watakuwa wamepewa sababu nyingine ya kufanya mgomo mwingine huko mbeleni. Ndugu zangu, ni bora ujue madaktari wamegoma na wamegoma kuliko kutokujua kuwa daktari anayekuhudumia amegoma moyoni.

      Lakini hakuna kibaya zaidi kama kumshambulia mtu badala ya hoja. Katika vitu vya kushangaza sana Waziri Mkuu ameamua kufanya mashambulizi ya mtu – ad hominem – kwa Dr. Ulimboka katika kuonesha kuwa hoja za madaktari hazina msingi. Hivi, ni kweli kuwa Dr. Ulimboka akiacha kushiriki kwenye mgomo huu manake ni kuwa madai ya madaktari yanafutika? Serikali inaweza kabisa kushambulia watu au mtu yeyote katika kujaribu kuonesha kuwa inawajua watu hao na inaweza kuwasema vibaya vyovyote vile lakini ukweli wa hoja zao utasimama ulivyo.

      Ukiona watu wanamshambulia mtu badala ya hoja zake, manake ni kuwa tayari wameshindwa hoja sasa wanataka kutumia nguvu! Kama watu wengine wanavyouliza mbona hatujaambiwa mambo ya wabunge ambao wamesimama kutetea posho? Au na yeye watu waanze kuulizia kwanini anatetea wafanyabiashara wakubwa kuchukua maeneo makubwa ya ardhi nchini? Hoja zijibiwa kwe hoja siyo viroja!

      Ni hatari kwa wagonjwa.
      kwa wagonjwa.
      Last edited by Mzee Mwanakijiji; 30th January 2012 at 03:53.

    2. Miaka 50

    3. #21
      Mzalendo80's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2010
      Location : Magogoni, Tanganyika
      Posts : 2,270
      Rep Power : 958
      Likes Received
      815
      Likes Given
      1589

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Hizo Hospital zingekuwa zinatibu viongozi wangesikilizwa lakini ni za walalahoi, they don't care.
      The CCM is a crime syndicate, Most members and MPs of CCM are corrupt. No conceince, No brains no nothing, just bunches of criminal and theft. Corruption cost mlalahoi in de street.

    4. #22
      Mzalendo80's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th October 2010
      Location : Magogoni, Tanganyika
      Posts : 2,270
      Rep Power : 958
      Likes Received
      815
      Likes Given
      1589

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Quote By Mikael P Aweda
      Serikali inachezea shilingi Chooni - itajuta muda si mrefu.
      Ubora wa Kiongozi hupimwa nyakati kama hizi -Pinda ameonesha kuwa yeye ni failure.


      Pinda na Kikwete ni sawa na Kiziwi na Kipofu, sijui nani atamuongoza mwezake, two hopeless people
      The CCM is a crime syndicate, Most members and MPs of CCM are corrupt. No conceince, No brains no nothing, just bunches of criminal and theft. Corruption cost mlalahoi in de street.

    5. #23
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6152
      Likes Given
      22273

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Tusipoangalia mgomo huu utakuwa ni Richmond ya Pinda - utaondoka naye.
      Mkuu Mzee Mwanakijiji, kama unafikiri aliyoyasema Pinda ni ya kwake, you are wrong!. Unless things get off hand na Pinda nae aendoke kumnusuru mtutu yule yule ambaye Lowassa aliondoka kumnusuru kwenye Richmond!.
      Sikonge, Zion Train, polly and 1 others like this.

    6. #24
      Tiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2008
      Posts : 1,660
      Rep Power : 886
      Likes Received
      365
      Likes Given
      470

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Mwanakijiji,

      Tuko pamoja hapa. Tatizo serikali yetu inafikiria kufanya ubabe tu badala ya kutumia busara. Kama ulivyosema, mwaka jana pale Kenya madakatari waliamua kuweka manyanga chini kwa siku kadhaa. Serikali iliwaomba wapeleke ujumbe wao kukutana na serikali na kuangalia ni njinsi gani matatizo yao yanaweza kutatuliwa. At the end of the day, muafaka ulifikiwa na madaktari walikubaliana na serikali na hivyo kurudi kazini. Vitisho havikutumika hata kidogo. Inakuwaje huyo anayejiita mtoto wa mkulima atumie ubabe kuwarudisha madakatari kazini?

      Anajidanganya!!!!!

      Tiba
      Mzalendo80 likes this.

    7. #25
      Josephine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th September 2010
      Posts : 695
      Rep Power : 730
      Likes Received
      753
      Likes Given
      134

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Baada ya kusikiliza maneno ya Pinda jana,niliwaza na kukosa usingizi usiku kucha.Nimekubaliana na wengi wanaosema hivi sasa upeo wa viongozi wetu umeshuka kwa kiwango cha kasi sana.

      MM nakubaliana na yote uliyosema,bado natamani Watanzania walio wengi walitambue hili ili tuweze kuungana nao.

      Vitisho na Dola haviwezi kuendelea kutawala katikati yetu bila kutafuta suluhisho.

      Ni wakati muafaka sasa kujua ni nini cha kufanya.

      Pinda ameonyesha ni jinsi gani serikali yake imefika mwisho wa kufikiri.kwani matatizo hupimwa kwa kiwango cha kuyatatua.kwa maanaa hiyo Nchi yetu itaendelea kuwa na matatizo makubwa zaidi ya hayo.
      Mzalendo80 likes this.

    8. FemaTV & Radio

    9. #26
      andrewk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th April 2010
      Posts : 2,224
      Rep Power : 906
      Likes Received
      283
      Likes Given
      59

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Quote By jigoku
      Mwanakijiji M.M naomba ushauri huu au mawazo yako yaandikwe gazetini,maana nimesikiliza tamko la PM nimesoma bandiko lako nimeona mawazo yako ndio yalitakiwa ayatoe PM wakati akijadiliana na M-dr,na Tamko la PM ni kama tamko la mtu ambaye alikuwa anapiga porojo wala hakuwa amejiandaa ku-address issue kubwa kama hii,sijui tatizo liko wapi kwa viongozi wetu,sijui ni kweli kwamba wao wanaamini kila migomo inayotokea hapa nchi inakuwa backed up na Chadema?
      Please mwanakijiji naomba mawazo haya yawe published soon kwenye moja ya print media.
      subiri baada ya siku mbili tu utayana magazetini

    10. #27
      WATANABE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th April 2011
      Posts : 783
      Rep Power : 570
      Likes Received
      272
      Likes Given
      83

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Quote By Kimbunga
      Makubaliano ni muhimu sana. Lakini mbona madaktari hawakutaka kukutana na PM? Hayo makubaliano bila mazungumzo yatapatikanaje kwa njia ya kuandikiana barua?
      Utawezaje kuka meza moja na watu ambao ndio channzao cha mgomo huo, kama kweli serikali ingekuwa makini inewaondoa kwanza waziri, katibu mkuu na mganga mkuu (huyu alikuwa mganga wa Manispaa, Jiji ndipo kwa uswahiba akwa Chief Medical Doctor) ndipo mazungumzo yafanyike

    11. #28
      Nyangomboli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2010
      Location : Mwisenge
      Posts : 886
      Rep Power : 607
      Likes Received
      121
      Likes Given
      4

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Sikuamini kama ilikuwa speech ya PM jana. Ni kitu kimenikosesha usingizi. Hao madaktari wa Jeshi na wengineo alowataja hawataweza acha pengo huko watokako?

    12. #29
      Zion Train's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2008
      Posts : 506
      Rep Power : 660
      Likes Received
      72
      Likes Given
      155

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      mkuu Pasco nakubaliana na wewe kabisa, Pinda kama Pinda hawezi kabisa kusema vile, mkuu kamchoka na anamtafutia sababu ya kumuondoa na jamaa haoni mbali , sema ndiyo hivyo still atakuwa anapata 75% ya mshahara wake na miradi miradi yake na madeal ya ardhi maisha yatakuwa yanaendelea kama kawaida, watu wanaumwa na wanaotegemewa kuwatibu ni hao wanaogoma, kiongozi makini alipaswa anyenyekee haswa,lakini sasa anafawafanya wagome zaidi, kweli tuna viongozi

      Quote By Pasco
      Mkuu Mzee Mwanakijiji, kama unafikiri aliyoyasema Pinda ni ya kwake, you are wrong!. Unless things get off hand na Pinda nae aendoke kumnusuru mtutu yule yule ambaye Lowassa aliondoka kumnusuru kwenye Richmond!.
      Love is my Religion

    13. #30
      Ntemi Kazwile's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2010
      Location : Bongo salidalam
      Posts : 1,873
      Rep Power : 832
      Likes Received
      135
      Likes Given
      446

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Tamko la Pinda kwa Madaktari ni la enzi zile za mwalimu ambapo chama kilikuwa kimeshika hatamu. Katika wakati huu wa dot.com inahitajika busara zaidi.
      Lazima kwanza Waziri Mkuu akiri kuwa watendaji wa Wizara hawakutumia hekima katika hatua za mwanzo za mzozo huu kwa kutumia maneno ya kejeli na dharau bila kusikiliza hoja za madaktari, kwa hiyo inatakiwa hawa wawajibike kwanza ama kwa kuomba radhi kwa madaktari na watanzania ama kwa kuachia ngazi ili watanzania wengine wanaoweza kuzitatua changamoto za wizara ya afya wapewe nafasi hiyo, kuwaamrisha madaktari warudi kazini bila kwanza ya kuwawajibisha waliosababisha mgomo huu ni kuendeleza "impunity" ambazo wanasiasa na wateule wa wanasiasa wamekuwa wakizionyesha (mfano mtakula majani lakini ndege ya rais itanunuliwa, rada ni yetu kwa hiyo tutanunua hata waseme namna gani, na mengine mengi)
      “If people are not laughing at your dreams at least once a week, you are aiming too low.” Robin Sharma.

    14. #31
      Ntemi Kazwile's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2010
      Location : Bongo salidalam
      Posts : 1,873
      Rep Power : 832
      Likes Received
      135
      Likes Given
      446

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Kama imeuzwa na sisi watupatie mgao wetu!
      “If people are not laughing at your dreams at least once a week, you are aiming too low.” Robin Sharma.

    15. DSN
      #32
      DSN's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2011
      Location : Home Tanzania
      Posts : 1,443
      Rep Power : 4452
      Likes Received
      690
      Likes Given
      576

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Uzoefu unaonyesha kila madaktari walipotishwa wakatishika basi mazoea hayo yaligeuka kuwa tabia.Endapo madaktari hawa kwa mara ya kwanza watakuwa wameenda kinyume na matakwa ya mazoea na utamaduni wa kutishika basi ni kweli Taifa litakuwa limesonga mbele kwa namna yake.Kwa kuwa kwa mara ya kwanza Wananchi wa Tanzania kupitia taaluma ya udaktari watakuwa wameipa fundisho Serikali kujifunza na kuangalia njia sahihi za kuondoa kero zinazotokana na kutofautina na kada za kitaaluma Tanzania.

      Kwa hakika madaktairi wakiafiki na kuludi kukubaliana na matakwa yaliyotamkwa na Pinda, basi tukili kuwa bado tuna safari ndefu sana ya ukombozi wa kifikra kwa Watanzania hasa kada ya wasomi kitaaluma.Na cha ubaya sana ni hatari kwa kada ya kitaaluma kushindwa kusimamia haki zake za msingi ambazo wao kwa udhahiri wanaona zinapokwa pasipo sababu.

      Kama kada ya wanataluuma watashindwa kusimamia haki zao, watu wasio na upeo wa kuchambua hoja na matukio kwa upeo wa juu watakwamuka vipi na kwa msaada wa nani kama si wasomi.

      Natumaini madakati walio wengi ni vijana wa miaka ya sabini,themanini na tisini basi watende kwa kufuata mioyo yao wasiige mioyo ya kizazi cha miaka ya sitini,na hamsini, ambayo utii ulipotiliza kwa wakuu umelifikisha Taifa hapo tulipo kwa mfumo wa OBEY YOUR SUPERIOR, hata kama hao Superior wako chaka kiupeo, wewe obey tu kwa kuwa wanamamlaka.Noooooooooo way HAIWEZEKANI AMKENI JAPO WATANZANIA WATAUMIA LAKINI DAMU YA KUJIBU YA WATAKAO ATHIRIKA NA MAAMUZI YENU WAKATI WA HATUA ZA KUPIGANIA MASLAHI YENU ZITAENDA KWA WATAWALA WA TAIFA HILI.

      HAKI UINUA TAIFA.

    16. #33
      Mzee Wa Rubisi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th November 2010
      Location : Chini ya mgomba
      Posts : 1,276
      Rep Power : 688
      Likes Received
      205
      Likes Given
      264

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Quote By Mikael P Aweda
      Serikali inachezea shilingi Chooni - itajuta muda si mrefu.
      Ubora wa Kiongozi hupimwa nyakati kama hizi -Pinda ameonesha kuwa yeye ni failure.

      Kweli kwani kashindwa kutatua tatizo anakimbilia Sitting allowance Dodoma

    17. #34
      siarrah's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 27th January 2012
      Posts : 7
      Rep Power : 370
      Likes Received
      2
      Likes Given
      2

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      nani kakwambia walikataa kukutana nae...embu soma hapo juu..si walienda jaman..na wakaishia kutukanwa...jumapili wakakubaliana kabisa jumatatu..

    18. #35
      WildCard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2008
      Posts : 6,453
      Rep Power : 1979
      Likes Received
      1797
      Likes Given
      59

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      MaDaktari, WanaSheria( Mwakili, Mahakimu) wanaponiambia wanagoma kwa ajili ya maslahi duni moyo unanikataza kuamini kabisa. Wanafanya madudu mengi mno kwa kutumia fani zao hizi kwa migongo ya uelewa wetu mdogo na kutokuwa na pa kwenda.
      Ninawaelewa MaDaktari wakilalamikia vifaa na mzingira duni ya kazi. Hili lisingesababisha WAGONJWA duni kukosa huduma hata ile ya msingi kabisa.

    19. #36
      Zemu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2008
      Posts : 425
      Rep Power : 644
      Likes Received
      45
      Likes Given
      18

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Quote By Kimbunga
      Makubaliano ni muhimu sana. Lakini mbona madaktari hawakutaka kukutana na PM? Hayo makubaliano bila mazungumzo yatapatikanaje kwa njia ya kuandikiana barua?
      Mi nawaunga mkono kwa kuto taka kukutana na PM, Mi naamini PM ni bendera fuata upepo, ni mangapi ameshindwa kuyatatua mpaka amngoje JK? Kumbuka ya Jairo na lile la kuongeza posho, ameshindwa kabisa kuact km PM na kuacha watu wamburuze km toroli, mi ningeshauri waseme kuwa wao wanataka kumuona JK mwenyewe sio PM cha uoga.Jana kaongea lakini ukimcheck tu utaona confidence hana sema tu kaamua kusema.Kingine mi madaktari bila kukamalia yule katibu mkuu wa wizara ua afya kuondolewa pale na kuletewa mtu makini basi hakuna kitakacho endelea. Mi nawaunga mkono madaktari waendelee na mgomo wao ili sekta ya afya ipate ukombozi, kila kwenye kutafuta mabadiliko lazima vifo vitokee, kwa hio kwa hili sioni tatizo.

    20. #37
      Nyumbu-'s Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th May 2009
      Posts : 666
      Rep Power : 642
      Likes Received
      65
      Likes Given
      204

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Pinda ana damu ya kutetewa kila wakati , ati maneno yake atakuwa kaelekezwa na Mkuu wa nchi....Huu ni uongo kabisa, Pinda mwenyewe is a problem. Consider maamuzi yake toka ameingia Uwaziri Mkuu wa JMT :
      1.Alipobanwa kuhusu kero ya mauaji ya Albino aliishia kulia lia tu, mpaka leo hatuoni kama hilo swala amelimaliza kivipi. Maana wanunuzi wa viungo vya ndugu zetu Albino hakuna hata mmoja aliyekamatwa au kutangazwa kakamatwa . Unataka kusema wale vijana waliokamatwa kwa kosa la mauaji hawajawataja hao wanunuzi wa vioungo vya Albino? Mbona Pinda hili kalifumbia macho, na bado watu wanamung'unya maneno kumweleza ukweli Pinda kwamba yeye si Mtoto wa Mkulima kama anavyojiita: Ni mtu anayekuchekea huku akikumaliza na watu wanamwamini
      2. Puinda alitoka wizara ya TAMISEMI kabla hajawa Waziri Mkuu. Yeye mwenyewe amewahi kuongea kwamba fedha nyingi zinafujwa kule kwenye Halmashauri. Wizara ya TAMISEMI iko chini ya ofisi ya Waziri Mkuu. Amefanya nini kuondo tatizo la ufujaji wa fedha hizo huko TAMISEMI wakati anajua kila linaloendelea huko? Au umesikia wapi Pinda amemwondo Mkurugenzi kwa utendaji mbovu pamoja na CAG kuanika madudu mengi ya halmashauri zetu? Sana sana alimwondoa Mkurugenzi wa wilaya ya HAI kwa sababu za kisiasa tu ambazo watu wote walizishitukia wakati ule wa uchaguzi 2010i. Pinda hawezi kutetewa kwamba ni mzuri, eti anashindwa kwa ajili ya JK, NO ! Tuliona akina Sokoine wakifanya kazi hata kumzidi Mwalimu Nyerere, haiwezekani waziri Mkuu ashindwe kufanya kazi eti kwa ajili ya kumwogopa Boss wake, kama kweli ni mwadilifu si angejiuzuru kuliko kuonekana kituko? Ni wazi kwamba yeye ndio failure ns si JK kama watu wanavyotaka kutuaminisha.
      3.Swala la posho za wabunge CHADEMA walivyozigomea , wote tulimsikia huyu huyu mnaemwita mtoto wa Mkulima akiwakejeli wapinzani kwa kusema " WANAMEZEA" mate posho zile. Hii ni wazi kwamba haguswi ghata kidogo na matatizo ya wananchi, bali yeye anaangalia faida yake , chama chake na mtandao wake basi..
      4. Pinda huyu huyu anatetea uporaji wa ardhi tena nyumbani kwao kwa be ya $0.25 /HA per year huku wanakijiji wakihamishwa kupisha wawekezaji. Kama kweli nia yake ni kusaidia hao wakulima, ameshindwa nini kuwalazimisha wawekeza hao waingie ubia na wenyeji , badala ya kuwafukuzi sehemu zuisizo na rutuba? Pinda ni mnyonyaji tu kama wote aliozungukwa nao....asitetewe kabisa ati ni mwadilifu...No!
      5.Pinda ndiye aliyeshindwa kutimiza mapendekezo ya Richmond. Haiwezekani aaminiwe huyu, kama angekuwa na uchungu na nchi hii, basi baada ya kushindwa hili asingekubali kuwa PM tena , maana ni aibu sana kwake na watoto wake.
      6. Huyu Pinda anayewatishia madaktari, ndo huyo huyo aliyegwaya kuwashitaki watuhumiwa wa ufisadi. Tena bila aibu alitamka kwamba kushitaki hao watu ni kama kujitia kitanzai, na mpaka kesho hataiki mijadala ya Meremeta nk. Whata do you expect from this failed man? Anawatetea wezi, anapandisha gharama za umeme kwa haop Watnzania ambao Mishahara yao ipo chini. Maisha yanapaa kwa ugumu, bado huyu mtu tunamwona anaweza kuitoa TZ hapa ilipo? Huyu ni katili tu, na anapenda madaraka. Haiwezekani useme unaleta madaktari wa jeshi hospitali zote za TZ, hivi hao wanajeshi wapo wangapi? Na je wao ndo wanastahili kulipwa posho kidogo kwa sababu tu ya utii wao? Ana uhakika gani kwamba hao madaktari wa jeshi wana furaha ni mapato au na miundo mbinu ya hospitali watokako?
      Pinda aache kulewa madaraka, ni wakati sasa wa kumweleza ukweli na si kumfichaficha....
      Last edited by Nyumbu-; 30th January 2012 at 12:46. Reason: Change wordinng
      Mzee Mwanakijiji likes this.

    21. #38
      Kimbunga's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Kisiwani Juma
      Posts : 7,477
      Rep Power : 6168
      Likes Received
      3044
      Likes Given
      1017

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Quote By WATANABE
      Utawezaje kuka meza moja na watu ambao ndio channzao cha mgomo huo, kama kweli serikali ingekuwa makini inewaondoa kwanza waziri, katibu mkuu na mganga mkuu (huyu alikuwa mganga wa Manispaa, Jiji ndipo kwa uswahiba akwa Chief Medical Doctor) ndipo mazungumzo yafanyike
      Mkuu serikali inayoweza kufanya hivyo labda ni serikali ya kijiji cha ujamaa. Waondolewe kwa kosa gani? Wao ndio wanatoa posho? Kwa jinsi PM alivyosema inaonekana mambo haya yalikuwa yakiongelewa na serikali kwa ujumla. Pia PM hajatoa tamko lake ametoa tamko la Serikali.
      CCM na CDM vyote ni vyama vya siasa vinavyoongozwa na wanasiasa; tofauti yao kubwa ni moja kwamba kimoja kina dola kingine kinataka kushika dola.

    22. #39
      Ngambo Ngali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th April 2009
      Posts : 2,569
      Rep Power : 1027
      Likes Received
      530
      Likes Given
      398

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      Hebu tujiuleze, je serikali ilkuwa tayari kuongea na kuwasikiliza madaktari?

      Kinacho nishangaza ni speech ya saa moja iliyosomwa na PM mara baada ya kuingia na kuelezwa position na waziri wa afya, moja kwa moja akaanza kusoma kwenye statement iliyotayarishwa ambayo ilikuwa na hitimisho kama tulivyosikia jana.

      Walijuaje kama madaktari hawatatokea?

      walijuaje kama madaktari watakataa upuuzi wa serikali?

      Hebu tujadili hili ili tuone kama kulikuwa na utayari wa kumaliza mgogoro huu kwa upande wa serikali.
      Injustice anywhere is a threat to justice everywhere.

    23. #40
      Ngisibara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd January 2009
      Posts : 1,154
      Rep Power : 759
      Likes Received
      134
      Likes Given
      129

      Default Re: Mgomo wa Madaktari hautaisha kwa vitisho na Dola; ni kwa Makubaliano tu!

      RichardBrunwick
      26 January 2012 2:33PM
      Tanzania's Kikwete is one of the most pathetic African leaders of our times. He is a peacetime leader for a country known to be one of the richest in the world in terms of natural resources, yet he leades the world with begging. Foreign companies have known Tanzania to be a free land in which you can go in and take all you can without being asked a question. I really don't get the mind set of its leaders especially their prsident Mr. Kikwete, a Muzungu worshiper. Having worked with the UNDP in that country for 8 years, I realized how inneficient and corrupt the country's leadership is. His ministers that requested bribes from BAE have never been tried despite the damning evidence against them. British TAX payers must stop funding this man's corruptin and foreign trips. His human rights record is horrible. Mr. Kikwete had no business of going to Davos to ask for foreign aid. Already his country is the world third leading foreign Aid dependant nation. He should be embarassed to say to the world that people are poor. His people living "hand to mouth " is his own is own ignorance and stupidity.That is hiw own problem, Brits are having their own problems he must realize that. We cant bankroll his foreign trips. He should make good use of his country's wealth. Instead of letting his corrupt officials and foreigners loot his country, he needs to think before letting himself be a global loughing stock. I read in one of the regional (kenyan) publication the mockery nature related to his frequent foreign trips. Palestinian, Haiti, Lebanon, Somalia and even Rwanda economies are more robust that of Tanzania. We must question the nations that welcomes this "Joker's" request for AID. He needs to be on a "no-fly" list so he can be serious. Hopefully the billionaires questions what he has done with the Money he has received for decades. The Arab spring should turn into the African summer and get rid of the Kikwete likes
      (http://www.guardian.co.uk/discussion...alink/14344505)
      SEMINA ELEKEZI, Mie ntakula mpaka kulee, wewe palee na nyie paleee, Mawaziri wangu angalieni msiingiliane mpaka tutakapokutana 2015


    Page 2 of 6 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Tags for this Topic

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...