| Find/Invite Friends | Register | Calendar | Search | Today's Posts | Mark Forums Read |
| FAQ | Members List | Bongo Flava | Zilipendwa | Taarab | Injili |
|
|
#1 | |||||||||||
|
||||||||||||
|
Views: 5247
|
||||||||||||
|
#2
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Kila muhula wa miaka mitano unapoisha kwa Rais ni sahihi kwa wananchi wanaoamini kuwa wana uwezo na malengo mazuri ya kuongoza nchi kuwaomba wanachi kupewa fursa hiyo. Hakuna sababu yoyote ya nchi kuyumba kwa sababu ukweli ni kwamba wako watanzania wengi wenye uwezo wa kusimamia utawala wa nchi yetu iwapo watapata fursa hiyo toka wananchi. Kumzui JK kugombea ni mawazo ya wasioelewa maana ya demokrasia, JK ana haki zote za kugombea - sasa kwa nini azuiliwe???na je ni nani mwenye mamlaka hayo??? Sanasana kama mtu ana sababu za msingi anaweza AKAMSHAURI asigombee, lakini sio kumzuia.
__________________
"To whom much is given, much is expected" |
|
#3
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Kichwa cha habari cha thread kina-syntax error..
__________________
Nakuona ulivo na wahka na shauku ya kugombana na keyboard, lakini swali ni .. Je una jipya?? |
|
#4
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Yeye sio Mungu na Tanzania sio mali yake! Tanzania ilikuwepo kabla yake na itakuwepo baada yake. Tanzania sio ya mtu mmoja. Tanzania ni ya watu milioni 38-40. Hii dhana ya kumtegemea mtu mmoja na bila yeye hatuwezi ku survive ni dhana ya kichovu. Mimi sijali kama chama chake kitamteua kugombea tena au vipi. Kwanza sijui hata utaratibu wao wa kuchagua wagombea ukoje. Ninachojali mimi ni kupata mgombea mbadala ndani au nje ya CCM mwenye sifa za uongozi na aliye na rekodi ya utendaji wa kazi wenye matokeo mazuri. Hii sio guarantee kwamba mtu huyo atakuwa raisi bora (kuliko Kikwete) lakini angalau tutakuwa na matumaini halisia kuwa anaweza kuja kufanya kazi nzuri.
Narudia tena. Tanzania sio mali ya mtu mmoja na haitegemei mtu mmoja kuiongoza. Kikwete na CCM ni binadamu kama sisi wengine na wala sio wateule wa Mungu walioletwa kuja kuongoza Tanzania (kuna baadhi ya watu wanaamini hivyo). Waondoke tu na sisi tutakuwa just fine.
__________________
Miafrika Ndivyo Tulivyo!! |
|
#5
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Kipindi cha kwanza (1985 - 1990) cha Mhe. ally Hassan Mwinyi aliongoza nchi vizuri ndiyo maana alipewa kipindi kingine. Hata hivyo aliharibu sana, uchumi wa nchi ulidorora kabisa, migomo ilitapakaa, hali ya kisiasa ilikuwa mbovu kabisa ndani ya CCM. Hali kadhalika Mhe. Ben Mkapa, alifanya vizuri sana katika kipindi cha kwanza. uchumi ulipanda, miundominu ilianza kujengwa hasa barabara. hali ya kisiasa ndani ya CCM ilikuwa tulivu kabisa. Kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, alipewa awamu nyingine ambayo aliboronga sana. Hali ya uchumi ikaanza kuyumba tena, kero zikaongezeka, migomo ikaanza tena kwa kasi, ujambazi ukaongezeka mara dufu. Pia hali ya kisiasa ndani ya CCM ikawa mbaya kabisa huku Wanamtandao wakiwa vinara katika kuendesha propoganda na siasa chafu.
Mhe. JK ameharibu toka awamu yake ya kwanza; uchumi umekuwa ovyo, migomo, hali ya kisiasa ndani ya CCM ni mbovu than anytime before. Watanzania wamekata tamaa, hakuna falsafa hasa baada ya kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya kuzikwa na richmond. Sasa kunasababu gani ya kumpa Kikwete awamu ya pili? Kikwete alipoingia madarakani alisema kuwa watangulizi wake wamejenga msingi imara, kazi yake ni kujenga ukuta tu. Je! huo ukuta uko wapi? misingi anayosimamia ya waliopita iko wapi? aibu kwa Mtawala kushindwa kuficha udhaifu wake. Pia historia ya watawala waliotangulia inatuonyesha kwamba kipindi cha pili huwa ni kuharibu na siyo kujenga. Je, huyu Kikwete, aliyeshinda kipindi cha kwanza, cha pili si itakuwa balaa? Somo la Mwinyi na Mkapa linatutosha kwamba Rais anapaswa kuwa wa kipindi kimoja tu. namshauri mhe. kikwete asigombee 2010. nchi itakuwa shwari tu. Kunawatu wenye uwezo na moyo wa utumishi na uzalendo, watakaokuwa tayari kuiongoza nchi. |
|
#6
|
|||||||||||
|
|||||||||||
|
Mimi nadhani hiyo itakuwa ni mwanzo wa kukua kwa demokrasia na uwajibikaji ndani ya taifa letu maana hata hao viongozi watakaokuja thereafter they will have that in mind kwamba usipodeliver hata hiyo tano ya mwanzo unaweza usifikishe.
Cha msingi JK from now should prove to us Tanzanians and not CCM kwamba ni kwa nini tumpe tena the last 5 yrs. Akishindwa hata hao CCM wakimpitisha tumpige chini. Can we do it????????????? YES WE CAN!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! !!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! |
|
#7
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
__________________
Miafrika Ndivyo Tulivyo!! |
|
#8
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
Kwa mantiki hiyo basi CCM kama kweli wana demokrasi iliyokomaa ndani ya chama chao basi hawastahili kumpa Kikwete nafasi hiyo bali wamtafute mtu mwingine atakayeweza kukisafisha chama hicho na kuiongoza Tanzania vizuri ili ipate maendeleo yanayostahili na pia kupambana na mafisadi bila woga. Kuna sababu chungu nzima za kuwa na Rais mpya baada ya uchaguzi wa 2010.
__________________
~*~Life is Good~*~ |
|
#9
|
||||||||||||
|
||||||||||||
|
|
|
#10
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
«
Previous Thread
|
Next Thread
»
Tuma Ukurasa huu kwa rafiki yako! All times are GMT +3. The time now is 01:35 AM.
Powered by JamiiForums.com
Copyrights reserved to JamiiForums.com | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||