Kampeni ya kummaliza kisiasa JK, Spika na wabunge kadhaa "wakorofi", imeanzishwa rasmi na Karamagi & Co. (Lowassa na Rostam) kupitia magazeti yao maalum ya AHSUBUHI NJEMA, TAZAMA, NYUNDO, TAIFA NA UMMA. Nia ni kuhakikisha JK anakuwa Rais kwa muhula moja tu na Spika Samuel Sitta na wabunge "wakorofi" hawarudi Bungeni mwaka 2010.
Magazeti hayo ambayo huchapishwa kila siku ya kazi kwa mpangilio, toka Jumatatu hadi Ijumaa, yanabeba ujumbe mahsusi wa ushawishi kwa umma kwamba: JK hana shukrani, kawatosa rafiki zake na kuwakumbatia "maadui"; Membe ni msaliti na anampotosha JK; Lowassa ni kiongozi safi na bora ambaye alionewa tu na Kamati ya Dk. Mwakyembe; bila Lowassa, Rostam, Karamagi, Makamba, Kingunge na wanamtandao wengine, JK hashindi uchaguzi wa 2010; Spika Sitta, Naibu Spika Anne Makinda na wabunge "wakorofi" wa CCM akina Anne Kilango, Mwakyembe, Selelii, Manyanya, Ole Sendeka, Kimaro, Zambi, Nkumba, Mpendazoe, Shellukindo (Bw. & Bi.), Mpesya, Ruth Msafiri na Nyalandu, ni wapinzani wa Serikali ya Awamu ya Nne.
Magazeti haya yanahaririwa na waandishi walewale mamluki: Deodatus Balile, Manyerere Jackton, Charles Charles, Muhingo Rweyemamu, Prince Bagenda na Gama wa gazeti la HOJA. Baadhi ya makala huchangiwa na Salva Rweyemamu na Premy Kibanga wa Ikulu na Mbunge wa Kigoma Peter Serukamba ambaye alibubujikwa machozi na kuugua baada ya Lowassa kujiuzulu. Yalianzishwa kwa mtaji wa sh. milioni 300 alizotoa Karamagi kwa niaba ya Lowassa na Rostam, mara baada ya Lowassa kujiuzulu.
Taarifa ndani ya Chama Tawala zinasema magazeti haya yana baraka zote za Makamba. Ndiyo maana baadhi yake yanahaririwa kwenye ofisi za UVCCM na kwa kutumia kompyuta za jumuiya hiyo.
Kwa mujibu wa kikao cha KALOKIRO kilichokaa Morogoro hivi karibuni, magazeti hayo yatasaidiwa baadaye (karibu na uchaguzi mkuu) na magazeti ya RAI, MTANZANIA na THE AFRICAN. Mwakani, mtandao huo wa mafisadi unaanzisha kituo cha redio na televisheni. Lengo kuu ni kuwamaliza wote hao kisiasa na kumwinua Lowassa agombee Urais mwaka 2010.
Matoleo ya wiki mbili zilizopita za magazeti hayo yote yalikuwa na makala za kumsafisha Lowassa na kudai kuwa Sitta anamhujumu JK, Sitta ana lengo la kuhamia CHADEMA, Kimaro kapora shamba la chuo, Mwakyembe ni mkabila, Membe ni mfuasi wa Malecela, JK hana fadhila mfano wa dereva aliyesaidiwa kwa kusukumwa kutoka kwenye matope lakini akakataa kuwabeba waliomsaidia ili wasichafue gari lake n.k. NGOMA IMEANZA, MAKUBWA ZAIDI YAJA!
Mkuu umepiga ndipo! Umelonga kiuelewa. Umenikuna. Hawa watu hawahitaji fedha za mauzo za magazeti yao hayo ya udaku ambayo story zake nyingi ni za ubabaishaji tu. Wao wanauza message na soko lao kubwa ni Dar es Salaam. Fedha ya mauzo ni kwa ajili ya mamluki wao akina Prince Bagenda, Manyerere, Balile, na Muhingo. Magazeti haya yana kazi maalumu. Kwa mfano, gazeti la Nyundo lilipewa kazi moja tu kufanya: kumbomoa huyu kijana Nape kwa kumzulia kila jambo: si mtoto wa Nnauye, mpenda madaraka, mpuuzi, umri mkubwa utadhani Nchimbi ni teenager n.k. Kazi imefanyika, sasa gazeti hilo limesimama kidogo kusubiri assignment nyingine. TAIFA kazi kubwa ni kuwabamiza mastaa wa Mbeya na Kilimanjaro: Kimaro, Mwandosya, Kilango, Mwakyembe n.k. ndiyo maana magazeti mengi ya TAIFA yanauzwa Dar es Salaam, Mbeya na Kilimanjaro. Mkuchika aliingizwa mkenge na Salva na RA kuifungia MwanaHalisi. Walimpa shinikizo kubwa na kumpelekea ujumbe wa siri kuwa kabla ya kuwa Waziri alikuwa mfadhili wa MwanaHalisi. Of course huo ni uongo mkubwa, blackmail tupu. Lakini imefanyakazi.
hahahahahaha! Uzuri JK nae anajua ukizoea kula vya wenzako nawe ukubali kuliwa.........................................., hapo ndipo
...hizi taarifa hapa tunazo kitambo.....na ukweli ni kuwa haya magazeti ,tv,na redio vyote vilikuwa tayari kwenda hewani miezi sita iliyopita...lakini vilikatishwa na moto wa ajabu uliounguza WASHIRIKA BUILDING.....mkurugenzi walikuwa wamempachika PRINCE BAGENDA...tunahisi kuwa moto uliounguza washirika building ulichomwa na personal intelligence wa kikwete ili kupunguza speed ya haya magazeti...........nadhani wamejipanga upya..
kaka wild hawa watu wana pesa hawategemei mauzo ya issues ili waendelee .....siunaona RAI haliuzi lakini hawatetereki......
PM,
Ninaposema hayauziki nina maana pia kwamba hayana wasomaji. Wakianzisha TV na Radio hapo hayo wanayotaka yawafikie watu wengi yatafika. Bahati nzuri ni kuwa wanajulikana kuwa ni watu hatari sio tu kwa ustawi na uchumi wa nchi yetu, bali hata kwa USALAMA na AMANI iliyopo. Walishindwa kumbakiza EL kwenye u-PM, hawataweza na majaribio mengine wanayo/watakayo fanya.
.....................Magazeti haya yanahaririwa na waandishi walewale mamluki: Deodatus Balile, Manyerere Jackton, Charles Charles, Muhingo Rweyemamu, Prince Bagenda na Gama wa gazeti la HOJA. Baadhi ya makala huchangiwa na Salva Rweyemamu na Premy Kibanga wa Ikulu na Mbunge wa Kigoma Peter Serukamba ambaye ...............................
What? Huyu wa Ikulu au mwingine? Mbona inanichanganya. Awe ndumila kuwili kiasi hicho? Naomba kuelemishwa.
Kampeni ya kummaliza kisiasa JK, Spika na wabunge kadhaa "wakorofi", imeanzishwa rasmi na Karamagi & Co. (Lowassa na Rostam) kupitia magazeti yao maalum ya AHSUBUHI NJEMA, TAZAMA, NYUNDO, TAIFA NA UMMA. Nia ni kuhakikisha JK anakuwa Rais kwa muhula moja tu na Spika Samuel Sitta na wabunge "wakorofi" hawarudi Bungeni mwaka 2010.
Magazeti hayo ambayo huchapishwa kila siku ya kazi kwa mpangilio, toka Jumatatu hadi Ijumaa, yanabeba ujumbe mahsusi wa ushawishi kwa umma kwamba: JK hana shukrani, kawatosa rafiki zake na kuwakumbatia "maadui"; Membe ni msaliti na anampotosha JK; Lowassa ni kiongozi safi na bora ambaye alionewa tu na Kamati ya Dk. Mwakyembe; bila Lowassa, Rostam, Karamagi, Makamba, Kingunge na wanamtandao wengine, JK hashindi uchaguzi wa 2010; Spika Sitta, Naibu Spika Anne Makinda na wabunge "wakorofi" wa CCM akina Anne Kilango, Mwakyembe, Selelii, Manyanya, Ole Sendeka, Kimaro, Zambi, Nkumba, Mpendazoe, Shellukindo (Bw. & Bi.), Mpesya, Ruth Msafiri na Nyalandu, ni wapinzani wa Serikali ya Awamu ya Nne.
Magazeti haya yanahaririwa na waandishi walewale mamluki: Deodatus Balile, Manyerere Jackton, Charles Charles, Muhingo Rweyemamu, Prince Bagenda na Gama wa gazeti la HOJA. Baadhi ya makala huchangiwa na Salva Rweyemamu na Premy Kibanga wa Ikulu na Mbunge wa Kigoma Peter Serukamba ambaye alibubujikwa machozi na kuugua baada ya Lowassa kujiuzulu. Yalianzishwa kwa mtaji wa sh. milioni 300 alizotoa Karamagi kwa niaba ya Lowassa na Rostam, mara baada ya Lowassa kujiuzulu.
Taarifa ndani ya Chama Tawala zinasema magazeti haya yana baraka zote za Makamba. Ndiyo maana baadhi yake yanahaririwa kwenye ofisi za UVCCM na kwa kutumia kompyuta za jumuiya hiyo.
Kwa mujibu wa kikao cha KALOKIRO kilichokaa Morogoro hivi karibuni, magazeti hayo yatasaidiwa baadaye (karibu na uchaguzi mkuu) na magazeti ya RAI, MTANZANIA na THE AFRICAN. Mwakani, mtandao huo wa mafisadi unaanzisha kituo cha redio na televisheni. Lengo kuu ni kuwamaliza wote hao kisiasa na kumwinua Lowassa agombee Urais mwaka 2010.
Matoleo ya wiki mbili zilizopita za magazeti hayo yote yalikuwa na makala za kumsafisha Lowassa na kudai kuwa Sitta anamhujumu JK, Sitta ana lengo la kuhamia CHADEMA, Kimaro kapora shamba la chuo, Mwakyembe ni mkabila, Membe ni mfuasi wa Malecela, JK hana fadhila mfano wa dereva aliyesaidiwa kwa kusukumwa kutoka kwenye matope lakini akakataa kuwabeba waliomsaidia ili wasichafue gari lake n.k. NGOMA IMEANZA, MAKUBWA ZAIDI YAJA!
Duh! Magazeti hayo hayapatikani nje ya Dar? Sisi tulio bara tutapataje maana sijawahi kuyaona isipokuwa TAZAMA ambalo kwa kweli limekuwepo kwa miaka hata kabla ya hiyo mitandao ya uchaguzo wa 2005!
Sasa mbona baadhi ya waandishi ni waajiriwa na waandishi wa magazeti ambayo hayajatajwa hapo kama vile Balile (New Habari Coopration-RAI) na Muhingo ambaye ni Mhariri wa Rai? Au Mkuu unataka kutuambia kuwa hayo magazeti uliyoyataja hapo pia ni mali ya New Habari Corporation? Tujuze zaidi Mtindi.
__________________ "Then you will know the truth, and the truth will set you free; I am the way, the truth and the life." Jn 8:32; 14:6
Sioni kitu gani EL anaweza kutufanyia akiwa raisi. Itakuwa ni sherehe (party) ya mbwa mwitu wenye njaa kuwararua mbuzi (WaTz) wasio na hatia (poor naive Tzn)! We should not (by hooks and crooks) let this happen.
Hawa wanajaribu kumsumbua JK na kuifaya kazi yake iwe ngumu, lakini ukweli uko palepale kwamba kelele tunazopiga dhidi ya mafisadi wananchi wanaanza kuelewa, huwezi kuamini kuwa hadi vijijini wananchi wanafahamu ubaradhuli uliofanywa na mafisadi hawa. Hamtaamini nikiwaeleza kuwa baadhi yao mafisadi hawa hawana uhakika na ubunge 2010? ukifika majimboni, pamoja na pesa waliyo nayo, watu wengi wanapanga kuitafuna na kuwakataa vile vile.
Bado najaribu kufikiria hiyo sherehe ya mbwa mwitu itakavyokuwa iwapo watshinda 2010?
Re: Kampeni ya magazeti mapya ya Karamagi & Co. Dhidi ya JK
Habari ina mapungufu mengi ( half baked ) apart from mfano wa Nape hakuna maelezo na mifano halisi ya mateleo ya magazeti hayo kuonyesha hizo "kampeni" za kuwachafua watajwa.
Kuna baadhi ya watajwa haiingii akilini kutokana na nyadhifa zao kushiriki katika jambo kama hilo, one can understand uhusika wa EL, Karamagi et al lakini Premy na Salva give me a break!
__________________
Mkulima kala Mbegu......
Last edited by Masatu; 17th November 2008 at 01:15 PM..
Habari ina mapungufu mengi ( half baked ) apart from mfano wa Nape hakuna maelezo na mifano halisi ya mateleo ya magazeti hayo kuonyesha hizo mengine ya "kampeni" za kuwachafua watajwa.
Kuna baadhi ya watajwa haiingii akilini kutoka na nyadhifa zao kushiriki katika jambo kama hilo, one can understand uhusika wa EL, Karamagi et al lakini Premy na Salva give me a break!
Mkuu we endelea kuwa TOMASO lakini itafika kipindi unaweza ukaja na kauli ya hii habari kuwa breaking news wakati ilisha julikana tayari hapo.
Cha mhimu kama huamini uanze kujifanyia kautafiti kimya kimya.
Lakini ukiangalia vimagazeti hivi vinavyo anzishwa kama uyoga ndo kazi yake hiyo.Kwa mfano kuna kigazeti kimoja hivi nafikiri kinaitwa Vioja kama sijakosea hiki kigazeti kina utamaduni wa kuwaponda ze Orijino Comedi sasa sielewi ni cha hawa jamaa EATV au lah maana kila tokeo chenyewe na akina Masanja,Joti n.k hata hayo aliyo taja mkuu hapo juu nayo hivyo hivyo yanawachamba watu kadhaa.
__________________ Ukiuza utumbo usiogope nzi. Chuda Raha
Habari ina mapungufu mengi ( half baked ) apart from mfano wa Nape hakuna maelezo na mifano halisi ya mateleo ya magazeti hayo kuonyesha hizo mengine ya "kampeni" za kuwachafua watajwa.
Kuna baadhi ya watajwa haiingii akilini kutoka na nyadhifa zao kushiriki katika jambo kama hilo, one can understand uhusika wa EL, Karamagi et al lakini Premy na Salva give me a break!
Wanaweza kuwa wanahusika bila wenyewe kujua, kama mabavyo Lizwan alihusika against baba yake bila kujua